Mambo Saba (07)Ambayo Watu Waliofanikiwa Huwa Wanaepuka Kufanya


Nikiongea na rafiki zangu, wengi huonekana wamekata tamaa na wanahisi hawajabahatika kufikia malengo yao.

Wengine wanahisi wamerogwa au kuna watu wanawachezea. Wanahisi wamekwama kiasi kwamba hawajui wafanye nini.

Mimi kitu cha kwanza ambacho hufanya ni kuangalia vitu ambavyo hupoteza muda wao na kuwafanya wakwame. Vitu ambavyo huingia katika njia yao ya mafanikio.

SOMA ZAIDI: Kupe Hawa Wanne (04) Wananyonya Muda Wako Kila Siku.

Nafikri sote hufanya mambo ambayo hupoteza mda wetu. Kuna kipindi nilikuwa nafanya hivyo kwa sana lakini nilibadilika baada ya kusoma kitabu kimoja kilichobadilisha mwelekeo wa maisha yangu.

Ni vizuri kuangalia ni kwa namna gani tunautumia muda saa kwa saa kwa kuondoa vikwazo ambavyo hututatiza njiani. Na njia bora ya sisi kutumia muda wetu vizuri ni kwa kuangalia watu waliofanikiwa wanavyotumia muda wao. Kama hawa watu wamefanikiwa kwa viwango vikubwa, ni wazi kuwa moja ya kitu ambacho wanatumia vizuri ni muda wao.

Sasa unaanza hapa kama ifuatavyo.

1. Watu waliofikia mafanikio huwa hawaanzi siku bila mpango
Watu waliofanikiwa wana mpango, wanajua siku hiyo watafanya nini mpaka siku inaisha.

Rafiki yangu mmoja huwa ana imani sana katika kusoma vitabu na huwa haipiti siku bila yeye kusoma kitabu. Kila siku mpya yeye huipangia atasoma nini na kwa muda gani.

Utaratibu wake aliojiwekea ni kwamba kila siku anahakikisha anafanya mambo makubwa matatu, ambayo huyavunja katika malengo mengine madogo madogo na hivyo hujikuta akifurahia maisha kila siku na akitamani aweze kukamilisha kila kitu.

Jiwekee utaratibu wa kufanya mambo matatu kila siku na yavunje katika mambo madogo madogo kadiri ya vipaumbele vyako vilivyo. Anza kwa kufanya  vipaumbele vikubwa. Utajikuta unafurahia kila hatua unayopiga.

SOMA ZAIDI: SITAKI UNAFIKI; Mambo Saba Ya Kufanya Unapokuwa Na Ndoto Kubwa

2. Watu waliofikia mafanikio hawafanyi mambo ya kuwarudisha nyuma. 
Watu waliofanikiwa hawajihusishi kabisa na mambo ambayo husababisha warudi nyuma kimaendeleo. Mfano; huwa hawajihusishi na kuvuta bangi au madawa ya kulevya ya aina yoyote.

Kwa hiyo kabla ya kufanya kitu, jiulize kile kitu kinaongeza thamani gani kwako?
Kama unafikiri hakiwezi, achana nacho. Na unapoulizwa swali, sio lazima utoe jibu la kitu fulani,  punde tu unapoulizwa. Jijengee utaratibu wa kufikiri kabla hujasema NDIO au HAPANA.

SOMA ZAIDI: WANAVYOKAMATA NGEDERE NCHINI INDIA (Jifunze Kutoka Kwa Viumbe Hawa)

3. Watu wazalishaji na waliofikia mafanikio hawamezwi na mitandao.

Mitandao ya kijamii imekuwa ni jambo la kawaida sana kwa watu kutembelea.  Kuangalia picha instagram, mambo mapya facebook, kutuma picha na video wasap. Yaani imekuwa ni sehemu ya kawaida ya maisha yetu.

Kiufupi kama hujajiwekea utaratibu ni muda gani utaingia mtandaoni na utafanya nini. Masaa yatapaa na  utashangaa masaa 24 yameisha na hujafanya chochote.
Jiwekee kikomo cha muda cha kuwa mtandaoni na lazima kiwe kidogo sana. Kama huwezi kujizuia weka hata alarm ili ikukumbushe ni mda gani sasa inabidi uzime data na kufanya mambo mengine kama ratiba yako ilivyo.

SOMA ZAIDI: Nijibu SMS 1000 Au Nisome Kurasa 1000? Ipi Bora? Nifanye Ipi?

4. Watu waliofanikiwa huwa wanasoma vitabu.
Mara nyingi mtu akihitimu masomo basi anajiona kamaliza kila kitu. Kwa hiyo kumwambia asome vitabu kwake anaona ajabu.

Habari njema ni kwamba kusoma na kutafuta maarifa hakuna mwisho. Ni muhimu sana wewe kusoma na kujua mambo gani yanaendelea.
Mabadiliko gani yanatokea na jinsi ya kukabliana nayo.

Kusoma , kujifunza na kutafuta maarifa hakuna mwisho.

PATA ZAWADI YA KITABU: BONYEZA HAPA UPATE Zawadi YAKO

5. Watu waliofanikiwa hawana wasiwasi na mambo ambayo hawawezi kuyazuia.

Watu waliofanikiwa wanajua kuogopa hakuwezi kukupeleka kokote. Hasa pale unapokuwa huna uwezo wa kuzuia jambo.

Kwa hiyo badilisha mawazo yako, ili kushughulika na mambo ambayo utaweza kuzuia.

6. Watu waliofanikiwa  hawafanyi kile ambacho kila mtu anafanya.

Ni vizuri mtu kuvutiwa na mtu fulani kwa kile anachofanya. Lakini haupaswi kujifananisha na yeye. Watu waliofanikiwa huwa hawendelei na ratiba zilezile walizokuwa nazo zamani. Bali hubadili ratiba zao na kufanya jambo kwa kuliongezea thamani.

Ukifanya kile kitu ambacho kila mtu anafanya haiwezi kukupa utaofauti na hivyo itawapelekea watu kuona ni mambo yaleyale tu waliyozoea kutoka kwa watu wengine. Ebu jitofautishe na watu wengine kwa kufanya kile ambacho hawafanyi.

SOMA ZAIDI:

7. Watu waliofanikiwa hawawazii makosa ya zamani.
Watu waliofanikiwa hufanya makosa sana. Moja ya mbinu ambazo huzitumia watu waliofanikiwa ni kutorudia kosa lilelile kila siku. Huwa wanafanya mabadiliko makubwa kutokana na makosa yao na hivyo kupiga hatua kimaendeleo.

SOMA ZAIDI: Makosa Ambayo Watu Hufanya Kwenye Fedha Zao

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Ni mimi ndugu yako,
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X