Kwa Nini Unapaswa Kuwa na Fikra za Kuwa Bilionea


Rafiki yangu mpendwa, salaam.
Leo nataka Nikwambie sababu kuu Kwa Nini Wewe unahitaji kuwa na fikra za kuwa bilionea.

Wengi wakifikiria juu ya hili Huwa wanaogopa sana na kuona kama kitu ambacho haiwezekani, ila ukweli ni kuwa kile anachofikiria mtu ndiyo anakuwa.

Kama Leo hii unaingiza KIPATO chochote, hata kama ni kidogo, una nafasi kubwa ya kutengeneza mabilioni ya PESA hapo baadaye.

  • Ukweli ni kuwa mabilioni ya PESA yanaanza na PESA kidogo TU hizi ambazo unaingiza Leo hii. Hiki kitu unaweza kukiona kama Cha kipumbavu hivi
  • Ila ngoja nianze Kwa KUELEZA hiki kitu Kwa namna ya kawaida TU.
  • kama unaingiza Elfu kumi Kwa siku, mfano, kiasi hiki kidogo kama kilivyo, kinaweza kuwa tiketi ya wewe kuingiza mamilioni zaidi. Ni wazi kuwa ukipambana hii Elfu kumi Kwa siku, baada ya muda inaweza kuwa laki Moja Kwa siku. Au na hapo unataka kunikatalia😁😁.

Ukishagundua namna ya kuingiza laki moja kwa siku, unaweza pia kuingiza milioni Moja Kwa siku.

Hivyohivyo kuendelea mpaka milioni kumi, mpaka milioni 100 ma zaidi ..

Na hiyo ndiyo inaweza kuwa tiketi yako ya kufikia ukuu na ubilionea unaoutaka.

RAI yangu Usifikirie kiudogo rafiki yangu Mara zote fikiria Kwa ukubwa.

Ni Bora uwe na fikra za kuwa na mabilioni ya PESA, Ili ikiotokea hujafikia, walau uwe sehemu nzuri zaidi. Kuliko kuwa fikra ndogo ambazo ikitokea hujafikia kabisa utafeli vibaya sana.

Sasa baada ya kusema hayo wacha nikupe sababu yangu Kwa Nini unapaswa kufikiri katika mabilioni. Na kumbuka hapa ninaposema ubilionea simaanishi Kwa PESA za Tanzania. Namaanisha ubilionea Kwa Dola.

  • Siku za nyuma niliwahi KUELEZA hapa kuwa ubilionea haupimwi Kwa shilingi, Bali Kwa Dola Marekani. Ndiyo kipimo kinachotumika kupima utajiri Kwa Sasa
  •  SOMA ZAIDI HAPA Bilionea Ni Mtu Wa Aina Gani?
  • Hapa kuna sababu kumi kwa nini unapaswa kuwa bilionea: SABABU YA KUMI NA KUMI NA MOJA NI NZURI ZAIDI

1. Uwezo wa Kubadilisha Maisha: Kama bilionea, utakuwa na uwezo wa kubadilisha maisha ya watu wengi kwa kutoa fursa za kazi, elimu, na huduma za kijamii.

2. Uhuru wa Kifedha: Kuwa bilionea kutakupa uhuru wa kifedha ambao utakuruhusu kufanya chochote unachotaka bila wasiwasi mkubwa wa fedha.

3. Nguvu ya Kufanya Mabadiliko: Kwa kuwa na utajiri mkubwa, utakuwa na uwezo wa kushawishi sera na kufanya mabadiliko makubwa kijamii na kiuchumi.

4. Fursa za Uwekezaji: Kama bilionea, utakuwa na fursa za kuwekeza katika miradi mbalimbali na hivyo kuongeza utajiri wako na kusaidia katika maendeleo ya jamii.

5. Kuwa Na Athari ya Muda Mrefu: Kwa kuwa bilionea, unaweza kujenga athari ya muda mrefu ambayo itaendelea kuathiri vizazi vijavyo kupitia miradi na taasisi za kijamii utakazozianzisha.

6. Kuboresha Ubunifu na Teknolojia: Utajiri wako unaweza kuwekezwa katika kuboresha ubunifu na teknolojia, kusaidia katika kuleta maendeleo makubwa kwa binadamu.

7. Kuwa Mfano wa Kuigwa: Kama bilionea, utakuwa mfano wa kuigwa kwa vijana na watu wengine, kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii na kufikia malengo yao.

8. Kupata Fursa za Kusafiri na Kujifunza: Utajiri wako utakuruhusu kusafiri na kujifunza mambo mbalimbali duniani kote, kuongeza ufahamu wako na mtandao wa kijamii.

9. Kufurahia Maisha: ubilionea utakuruhusu kufurahia maisha na kutimiza ndoto zako bila kikwazo cha kifedha.

10. Ubilionea itaonesha ni Kwa namna gani umeweza kutoa THAMANI kubwa Kwa watu. Ni Kwa namna gani umeweza kuleta mchango chanya Kwa jamii kiasi kwamba jamii umekuwa tayari kutoa Fedha na kupata huduma au bidhaa zako ambazo zimekufikishabkwenye ubilionea

11. Ni kwa sababu wewe umeubwa Kwa mabilioni.

  • Kama wewe ni mwanaume, wanasanyansi wananiambia kwamba mwili wako una seli bilioni 36.Seli trilioni 36 ni sawa na seli bilioni 36 mara Elfu Moja
  •  Kama wewe ni mwanamke wanasayansi wananiambia kuwa mwili wako una Trilioni 28. Seli trilioni 28 ni sawa na seli bilioni 28 mara Elfu Moja.

Huo ndiyo mwili wako. Hauna mamia ya seli, Wala siyo Malaki au mamilioni, ni mabilioni.

Anza kufikiri Kwa mabilioni wewe!

Ukiachana na seli hizo ambazo unazo Kwa maelfu ya mabilioni.

Wanasanyansi wananiambia Kuna hiki kitu kinaitwa Neurons. Hizi wanasema unazo bilioni 100 na zimeunganishwa zenyewe Kwa zenyewe bilioni 100 mara 1000.

Na hii ndiyo sababu kwa nini unapaswa kufikiri Kwa mabilioni.

Enewei Kwa Leo inatosha au unasemaje? Tukutane Dar Es Salaam Ubungo; Landmark hotel tarehe 29 JUNI

Soma tarehe vizuri👆🏿

Tutaanza mapema saa 1 mpaka jioni saa 1 jioni. Itakuwa ni siku yetu Moja ya kukaa pembeni, kujifunza Kwa kina, Kisha tutachukua kubwa zaidi baada ya hapo.

Kundi la wahudhuriaji wa semina hili hapa

https://chat.whatsapp.com/CAdCnW82i8N0clD2fDvn7v

SOMA ZAIDI: 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X