
Tunaishi kwenye dunia ya kipekee sana. Mara paap, headphones hizo hapo tunazo na tunatamba nazo. Unaweza kuzivaa kwenye daladala
Kwenye usafiri wowote wa umma au wa binafsi
Ukiwa unatembea
Na hata ukiwa ofisini au nyumbani.
Leo nataka tujadiliane kwa pamoja kwamba uvaaji huu wa hizi headphones ni wa faida au hasara
Ni jambo la wazi kuwa uvaaji wa headphones una faifda zake lakini pia umeambatana na hasara kadhaa.Haya yote nataka tuyaangalie kwa jicho la tai aliye juu angani na angalia vitu kama vilivyo bila ya kupepesa macho.
IKo wazi kwa mfano kwamba ukiwa kwenye mazingira yenye kelele nyingi, ukiwa na headphone zinakusaidia sana kundelea na majukumu yako. Nakumbuka wakati nipo chuoni, NILIKUW NA UWEZO WA KUENDELEA NA MAJUKUMU YANGU HATA KAMA NILIKUWA NIMEZUNGUYKWA NA WATU WENYE MAKELELE kwa sababu tu nilikuwa nimevaa headphone.
Kuna kipindi fulani unahitaji usikilize jambo au taarifa ambazo hutaki upande wa pili usikie. na hapa ndipo headphone zinafanya kazi nzuri sana.
Aidha kwenye suala zima la kujifunza kwangu, huwa napenda kuzivaa na kusikilza vitabu vya sauti. Yaani audioooks kama hizi ambazo unaweza kuzipata hapa. Kila ninapopita na headphone zangu, ninakuwa ninapata maarifa bila shida yoyote ile.
Wengine pia wanapenda kuzivaa wakati wa kufanya mazoezi, kitu hiki kinawafanya wanaua ndege wawili kwa jiwe moja.
Hata hivyo kuna mazingira tunazivaa kupitiliza. Mfano, unakuta mtu anapanda kwenye usafiri. muda wote wa safari (labda kutoka Morogoro kwenda Dar) amevaa headphone tu.! je, hii ni faida au hasara?
Ukiniuliza mimi nitakwambia hii ni hasara. unajua kwa nini? Umekaa kwenye treni au gari au ndege, hujasalimiana na mtu wa karibu yako. HUjajua ni nani n.k.
- Halafu wewe huyohuyo kila siku unaomba uweze kukutana na watu wazito, unadhani utakutana nao kivipi? watashuka kutoka mbinguni? Hapana, inawezekana konekisheni unazozitafuta umeshapishana nazo mara nyongi tu kwa sababu ya kutozitumia. au kwa kuwa bize muda wote.
USHAURI WANGU: Ukipanda usafiri au ukiwa kwenye mazingira ya watu, weka pembeni headphone hata kwa muda kwa ajili ya kusalimiana na watu. Usisafiri na mtu kwa saa mbili, bila kumjua vizuri. Unaweza kukuta huyo ni mteja mzuri wa bidhaa zako, unaweza kukuta anakuja kuwa msambazaji wa bidhaa zako, unaweza kukuta anakuwa mshirika wako muhimu na pengine anaweza asiwe chochote. Lkini haya yote yatawezekana kwa wewe kuhakikisha unakuwa na mazungumzo na huyu mtu
SOMA ZAIDII: JINSI YA KUANZISHA MAZUNGUMZO NA MTU YEYOTE
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza
Jipatie vitabu vya Godius Rweyongeza kwa kuchagua HAPA.
Hakikisha umepata kitabu cha RASILIMALI ZA WATU WENGINE, ni kitabu kizuri kwa ajili yako. wasiliana na 0755848391 au 0745848395 sasa
Makala ya kesho itawekwa kwenye blogu ya SONGAMBELE ambayo unaweza kuifikia kupitia www.songambele.co.tz na itawekwa kwenye channel ya telegram pia ambayo unaweza kuifikia kwa KUBONYEZA HAPA