Home


  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

     

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Njia za Kweli za Kuwathibiti Wakatisha Tamaa

    Kuna watu wengi wanaokatisha tamaa kwenye maisha yetu ya kila siku. Hata hivyo, ni muhimu sana, kuwa kujua njia ya kujikinga na wakatisha tamaa. kama ambavyo kuna mavazi ambayo ni bullet proof, hivyohivyo kuna njia ambazo ukizitumia naweza kuthubutu kuziita, kukatishwa tamaa proof, yaani njia hizi zitakufanya uzidi kusongambele hata katikati ya wakatisha tamaa. Utakuwa hushikiki, na mara zote utakuwa na malengo na ndoto kubwa ambazo unazipambania

    Ngoja kwanza nikuchane ukweli, 

    Ukweli wa kwanza ni kwamba kama unakata tamaa kwa sababu ya watu wanaokukatisha tamaa, basi wewe hutakuja kufanikiwa. Maana tunavyoyaendea mafanikio makubwa ni kwamba kuna watu watatishika na mafanikio yetu ambayo tunayafanyia kazi. Na wengine watakukatisha tamaa kwa sababu tu wanaogopa zile hatua kubwa ambazo unachukua, kitu pekee watakachoona wanaweza kufanya ni kukukatisha tamaa.

    Ukweli namba mbili ni kwamba kama unatakatishwa tamaa na watu, maana yake hauko bize kiasi cha kutosha, na hasa kama maneno na kauli ambazo watu wanatoa juu yako.

    Ukweli ni kuwa unapaswa kuwa bize mara zote kuliko hata ubize wenyewe. Hakuna kitu kingine nje ya kazi zako na majukumu yako ambacho kinapaswa kukukwamisha wewe wala kukurudisha nyuma

    Ukweli nambari tatu, kuna watu wamejipa kazi ya kukatisha tamaa wengine. Hivyo, waache wafanye kazi zao, na wewe kazi yako iwe ni kupambania malengo na ndoto zako kubwa.

    Ukweli nambari nne, mti unaopigwa mawe ni mti wenye matunda.

    Kiufupi ujumbe wangu ninaotaka kukwambia wewe ni kwamba haupaswi kuwa mtu wa kurudi nyuma na wala haupaswi kukatishwa na kitu chochote. kile kwenye maisha yako.

    sasa ili usikate tamaa kuna silaha muhimu ambazo unapaswa kuwa nazo ambazo zitakusaidia sana kuhakikisha kwamba unasongambele.

    SILAHA YA KWANZA: Kuwa na ndoto kubwa kama vile utaishi milele. rafiki yangu unapaswa kuwa na ndoto kubwa ambazo unazifanyia kazi, na zifanyie kazi mara zote bila ya kurudi nyuma, zifanyie kazi ndoto zako leo kama vile unaenda kufa kesho.

    SILAHA YA PILI: Mara zote kuwa kwenye ratiba ya kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa. Kamwe usirudi na usikubali kurudishwa nyuma na mtu au kitu chochote kile. Usipokuwa bize na ndoto zako, hakuna mtu hata mmoja ambaye atakuwa bize na ndoto zako. Kumbuka ile nukuu ya madebe tupu huvuma

    SILAHA YA TATU: Hakikisha mara zote umepangilia ratiba zako kwa umakini kiasi kwamba unakuwa hauna muda wa kupoteza.  Hii ni silaha kubwa sana kwa sababu, itakufanya uwe biza na maisha yako na uachane na mambo ya wengine.

    na ukweli ni kuwa una mambo mengi ya kufuatilia juu ya maisha yako kuliko kufuatilia maisha ya watu wengine

    SOMA ZAIDI: 

    Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

    Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

    SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

    Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

    Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

    Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

    Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

    For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

  • Iko hivyo. Vitu ambavyo watu wanakwambia kinyume chake na nini chakufanya kuanzia leo hii

    Nakumbuka kwenye hesabu za kidato cha tatu kulikuwa na hesabu fulani za maumbo, ambapo ulikuwa unatafuta ukubwa wa pembe fulani au urefu fulani.

    Sehemu ya kwanza kabisa ulipokuwa unaanzia ilikuwa ni kutumia zile pembe ambazo zinafanana.

    Mfano ungeweza kusema kwamba pembe ABC ni sawa na pembe EFG kwa sababu iko hivyo (its given). Kama yangekuwa maandiko matakatifu basi tungesema imeandikwa.

    Sasa leo, nataka nikwambie vitu ambavyo vipo hivyo (given). Havibadiliki, hata ufanyeje.

    Lengo la makala hii ni kukwambia ukweli na kukufungua ili uweze kupambania malengo na ndoto zako, bila kurudi nyuma.

    Lengo la makala hii ni kukupa hasira, nakwambia bila hasira hii, hutatoboa.

    kitu cha kwanza ni ambacho kiko hivyo, ni kwamba wanyonge wanayongwa na haki yao hawapewi.

    kama hili ulikuwa hulijui ndiyo nataka ulijue. Kama wewe unaendelea kujiita mnyonge mpaka leo hii, utanyongwa kweli mpaka ufe. Na hapa usije ukaanza kusema kwamba mbona huyu anaandika vitu ambavyo sio kweli na havipo.

    Hivi vitu siyo kwamba hata nimevigundua mimi, bali vimekuwepo kwa miaka mingi. Miaka mingi iliyopita Darwin aliwahi kusema kwamba, vitu vinyonge ndiyo vinatoweka kwanza kabla ya vyenye nguvu.

    Vinyonge vinakosa chakula.

    Vinyonge vinakosa ushawishi

    Vinyonge vinakosa hoja

    Vinyonge vinakanywagwa.

    Ni vivyonge. Na vinanyongwa kwelikweli.

    Unachotakiwa kufanya ni kubadili mtazamo. Toka kwenye mtazamo wa kuwa mnyonge, badala yake kuwa mpambanaji. Nimeandaa kabisa Mwongozo Wa Wapambanaji ambao na wewe unaweza kuupata. Mwongozo huu unapatikana kirahisi tu, wasiliana na 0684 408 755 sasa kupata mwongozo wako.

    Kamwe usikubali kuwa mnyonge. Kuwa mpambanaji na mara zote pambania melengo na ndoto zako kubwa.

    Kitu cha pili ambacho kiko hivyo ni kwamba, watu wote siyo sawa.

    Ninavyoandika makala hii siyo kwamba nataka kuwa mbaguzi. hapana, ila nataka nikwambie tu ukweli.

    Na hapa nitaeleza hasa kwenye eneo moja ambalo nalifahamu vizuri

    Mfano kazini. Au ofisini, siyo wote ni sawa.

    Ndiyo maana unakuta bosi anamlipa mtu fulani kiasi kikubwa cha fedha na mwingine kiasi cha kawaida, japo wote wanafanya kazi muda uleule. Kungekuwepo na usawa basi watu wote wangefanya kazi na kulipwa kwa usawa.

    Kwenye timu ya mpira wa miguu kuna wachezaji kumi na moja, lakini malipo yao ni tofauti. Japo wote wanacheza dakika 90, ila kuna wanaolipwa zaidi na wale ambao wanalipwa kidogo. Hii ni kwa sababu hakuna usawa na usawa huu hauwezi kulazimishwa kuwepo, isipokuwa tu wewe unaweza kubadili mtazamo wako na kujiweka kwenye nafasi ya wale wanaopokea kikubwa badala ya wale wanyonge wanaongwa na kupokea kidogo.

    wale wenye vipaji na upekee kwenye kucheza mpira wanalipwa zaidi.

    Hivyo hivyo kwenye kazi

    Mnaweza kuanza kazi sehemu mkiwa wawili. Mmoja baada ya muda akaongezewa mshahara, na pengine akapandishwa hata cheo, wakati mwingine akiwa bado anabung’aa. au pengine hata mwingine akafukuzwa.

    Ukweli ni kuwa hakuna meneja ambaye huwa anafukuza mtu anayefanya vizuri. Meneja atafanya chochote kile anachoweza kuhakikisha kwamba mtu anayefanya vizuri anaendelea kubaki naye. Kama ni mshahara atamwongezea, kama ni bonus zaidi atamongezea.

    Nakumbuka kuna siku nilisoma wasifu wa Strive Masiyiwa akawa anasema kwamba, aliwahi kumwachia mfanyakazi ambaye alikuwa anamfukuzia gari. Na yeye akatembea kwa mguu, hii ni kwa sababu alikuwa anamhitaji afanye kazi. Lakini tunaposema kwamba huyu mfanyakazi alimwachia gari, kuna watu ambao baada ya kuongea nao, alitamani asionane nao tena kwa sababu walikuwa hawafai.

    Mtu ambaye hafanyi vizuri (mnyonge) ananyongwa haraka (kama ni kazini anaondolewa haraka) na ndiyo maana nilikwambia mapema kabisa kwamba kamwe kwenye maisha yako usikubali kuwa mnyonge maana watakunyonga na haki yako hutapewa.

    Unachotakiw kuafanya ni kuhakikisha kwamba unakuwa mtu mwenye thamani kubwa. Ongeza thamani yako zaidi, na ukiwa mtu mwenye thamani, hakuna mtu atakayekupuuza. Kila mtu atahitaji kukaa karibu na wewe.

    Unakuwa kama moto. Tunaupenda, kukiwa na baridi, tuna uhakika wa kupata joto. kukiwa chakula tuna uhakika wa kupika chakula chetu kwa wakati

    Kwa kumalizia makala ya leo nipende kukusisitiza vitu viwili ambavyo nimeongelea siku ya leo. Kitu cha kwanz ani kwamba usikubali kuwa mnyonge la sivyo utanyongwa na haki yako hutapewa. Kitu cha pili ni kwamba usikubali kuwa mtu kawaida kwa kisingizio kwamba watu wote ni sawa. Huo usawa upo kwenye karatasi tu, ila kwenye uhalisia usawa haupo. Jitofautishe, kuwa mtu mwenye thamani kubwa, ni uhakika kwamba ukifikia hivi viwango watu hawataweza kukupuuza hata kidogo.

    Utaweza kulipwa kwa namna unavyotaka. Na utaweza kupata chochote unachotaka hata hao wanaotoa hicho kitu watakuwa tayari kuwakosesha wengine.

    watakuwa tayari kuwapunguzia wengine mishahara ili usiache kazi.

    watakuwa tayari kukulipa mara mbili mpaka mara tatu zaidi ya wengine kwa sababu upekee wako.

    watakuwa tayari kufanya lolote kwa niba yako

    Utakula na wafalme.

    mimi nakupenda

  • Ushauri Kwa ambaye Hajaanzisha Biashara Na Jambo Moja Ambalo aliyeanzisha Biashara Anapaswa Kufanya

  • Njia pekee ya kuongeza mshahara wako mara mbili

    Biashara ndiyo njia pekee ya kuongeza kipato chako mara mbili kadiri muda unavyokwenda. Ni tofauti na njia nyingine zozote. Uongezwaji wa kipato kwenye ajira una kikomo, na mshahara kwenye ajira hauwezi kuongezeka mara mbili kila mwaka, lakini kwenye biashara, kama kweli utajifunza biashara kwa kina na kufanyia kazi yale unayotakiwa kufanyia kazi. Inawezekana.

  • Anza tu

    Wewe anza, kisha endelea mbele. wanaokubeza leo, wanaoona kwamba huwezi leo, kuna siku watakushangilia huku wakisema kwamba nilijua tu mwamba lazima atafanikiwa

    ✅

  • Njia Bora Na Ya Uhakika Ya Kunufaika Elimu Na Elimu Yako Ya Chuo

    Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana ambao wanahitimu chuo huku wakiwa bado wakiwa hawana mwelekeo. na ambacho kimekuwa kinatokea ni kwamba hawa vijana ambao wamesoma  chuo na kufaulu vizuri, baadaye wanaingia mtaani, wanakutana na maisha ya huku kitaani, yanawapiga, wanaishia kufanya kazi ambazo hata wao wenyewe walikuwa hawapendi.

    SIKU YA LEO nipo hapa kukuonesha namna unavyoweza kunufaika na elimu yako ya chuoni.

    KAMA BADO UKO CHUONI: Fuatilia masomo yako vizuri. Hudhuria masomo yale ambayo ni ya lazima uwepo na usipokuwepo hutaweza kuelewa vizuri.

    Usipoelewa uliza.

    Kama kuna mazoezi yakufanya yafanye.

    Halafu angalia kati ya hayo yote unayojifunza, ni kitu gani ambacho unapenda zaidi. Ukifuatilia kozi zako vizuri kuanzia mwaka wa kwanza mpaka unapomaliza mwaka wa tatu, wa nne au wa tano. Utagundua kwamba kuna kozi moja au mbili ambazo unazipenda zaidi na unaweza kuzitumia kwenye maisha yako ya kila siku.

    Amua kuzichagua hizi kozi na kuzitumia kwenye maisha yako ya kila siku. Angalia ni kwa namna gani unaweza kupata pesa kutokana na hizo kozi ambazo umejifunza.

    Angalia ni mambo gani ambayo watu wana uhitaji nayo na namna ambavyo wewe unaweza kutatua hayo mahitaji. Kisha tatua hizo changamoto kwa kuwaletea suluhisho.

    Kwa namna hiyo, utajikuta kwamba unawasaidia watu huku wewe mwenyewe ukiwa unazidi kufnaya kitu unachopenda na unapata pesa.

    KAMA UMESHAHITIMU: Najua unaijua hiyo kozi ambayo uliilewa sna, kozi ambayo ulikuwa unaipensa sana wakati ukiwa chuoni.

    Hiyo kozi moja ambayo leo hii, hata ukiamshwa tu usingizini unaweza kuileza hata kwa bibi yako akakuelewa vyema kabisa.

    ANZA kuangalia ni kwa namna gani ambavyo hii kozi sasa unaweza kuileta kwenye uhalisia wa maisha yako ya kila siku. Anza kuangalia ni kwa namna gani unaweza kuifanyia kazi hiyo kozi na watu wakawa tayari kutoa pesa zao mfukoni na kukulipa.

    Kisha fanyia kazi kile utakachokuwa umepata.

    Ukweli ni kuwa kwa fikra hizi sitegemi kwamba baada ya hapa uendelee tu kukaa nyumbani ukiwa unasema kwamba hauna kitu cha kufanya.

    BADALA yake unapaswa kuanza kupambania lengo lako kubwa na ndoto zako kubwa za sasa hivi ambazo ni kuwasaidia kupiti kile unachojua.

    Nimeandika kitabu kizuri sana, kinaitwa, TENGENEZA FEDHA KWA KUUZA KILE UNACHOJUA. Ni moja ya kitabu bora sana kabisa ambacho kila mwanachuo anapaswa kuhakikisha kwamba amesoma. Kimeeleza kwa undani kuhusu dhana nzima ya kutumia unachojua (ujuzi, maarifa, konekisheni, au chochote unachojua).

    Kupata nakala ya kitabu hiki ni rahisi sana.

    Wasiliana nasi kwa +255 684 408 755 sasa ili uweze kupata nakala yako. Utaletewa popote pale ulipo duniani.

    SOMA ZAIDI:

    Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.

    Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

    Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

    SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.

    Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

    Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

    Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

    Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

    For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

  • Utajiri ni asili ya mwanadamu yeyote. Ni kitu muhimu kwake kuwa nacho

  • Unakwepa Hatari Zipi?

    Moja ya kitu ambacho huwa kinawakwamisha walio wengi ni kuogopa hatari. Wengi wanaogopa kuchukua hatua katika baadhi ya vitu kwa kuogopa hatari ambazo zinaweza kuwatokea kwenye maisha yao ya kila siku.

    Huwa napenda kuwaambia watu kuwa hatari kwenye maisha tunatembea nazo kila sehemu. Hatari tunazo kila wakati na hatari ni kama sehemu ya maisha yetu.

    Kutembea tu hatari.

    Kuongea na watu ni hatari.

    Na hata kulala ni hatari.

    Hakuna sehemu ambayo haina hatari.

    Linapokuja suala zima la hatari, watu wengi huwa wanakwepa hatari na hasa kwenye uwekezaji. Mtu anaogopa kuwekeza kwa sababu anaogopa, atapoteza

    Ila ninachoweza kukwambia siku ya leo ni kwamba, chagua kwa usahihi. Pata elimu sahihi ya uwekezaji, kisha wekeza kwa nguvu zako zako zote.

    rafiki yangu, kwenye maisha, hatari zipo kila sehemu. Hivyo, usiogope hatari. maana unaweza kukutana nazo popote utakapokuwa.

    SOMA ZAIDI:

    Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

    Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

    SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

    Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

    Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

    Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

    Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

    For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

  • Misingi Sahihi Ya Kujenga Urafiki Kwenye Biashara

    Uache urafiki ubaki kwa ajili ya urafiki na wewe

    1.  Fanya kazi na watu wanaojua kufanya kazi
    2. Fanya biashara na watu wanaojua misingi ya biashara na amba watakukwa tayari kuisimamia mara zote.

    Kwenye biashara, urafiki mzuri ni ule unaotengenezwa na biasahara. Ila siyo mtu mlikuwa rafiki halafu eti mnaanzisha biashara, mara nyingi mtajikuta mnaweka urafiki kwenye biashara na hivyo kuharibu biashara

     

    Hivyo kama unafikiri kuanzisha biashara, kwa kiwango kikubwa utakuta kwamba rafiki yako wa sasa hivi anaweza asiwe mtu ambaye atakufaa sana kwenye biashara. 

    Najua utakuwa umesikia stori nyingi sana za watu walioanzisha biashara na marafiki zao.

    Ila wengi ukifuatilia, urafiki ulikuwa umejengwa kwenye misingi ya biashara.

    Siyo wewe unaanzisha biashara na rafiki yako ambaye msingi mkubwa wa urafiki wenu mmeujenga kwenye kubeti, kushangilia mpira, kuangalia movie na vitu kama hivyo.

    Baadaye unafika wakati ambapo mnapata pesa kidogo tu, kila mmoja anafikiri juu ya kupata pesa asepe.

    Angalia urafiki wa watu maarufu kama Steve Jobs na mweza Stephen Wozniak, hawa watu walikuwa marafiki, ila urafiki wao ulikuwa umeunganishwa kwenye ubunifu. Wote walikuwa wanapenda ubunifu na kubuni vifaa kama kompyuta, na ndiyo maana waliweza kufanya makubwa kwa pamoja.

    Au chukulia mfano wa urafiki kama Bill Gates na Allen Paul, hawa pia urafiki wao ulikuwa umejengwa kwenye kupenda kompyuta na ubunifu.

    Urafiki mzuri ni ule ambao utatokana na kazi, au biashara

    Kama urafiki wa Bill Gates na Warren Buffet au urafiki wa 

    kWA KUMALIZIA: Leo ningependa tu kukwambia kwamba urafiki wako wa kweli ujengwe kwenye misingi ya biashara, ila siyo urafiki ambao utabomoa biashara.

    SOMA ZAIDI:

  • Mtu Pekee Atakayekusaidia Kufanikisha Makubwa, Cha Kushangaza Ni Kwamba Humtumii. Mfahamu Sasa

    Ngoja nikwmabie kitu rafiki yangu.

    Kuna vitu ambavyo unapaswa kufanya mwenyewe. Siku za nyuma nimewahi kuandika hapa kwamba hakuna mtu anayeweza kupiga pushup kwa ajili yako.

    Makala hiyo bado ina nguvu kubwa sana kama ambavyo niliiandika miaka hiyo. Kama ulivyo ukweli usiopingika kuwa hakuna mtu anayeweza kupiga pushup kwa ajili yako. Hivyohivyo ni ukweli usiopingika kuwa kuna vitu ambavyo hata ukiwa na watu bora kuliko wote duniani hawawezi kuvifanya kwa niaba yako.

    • Hakuna Daktari ambaye atakufanya wewe kuwa mwenye afya bora
    • Hakuna mtalaamu yeyote atakufanya uwe na mwili wa kawaida
    • Hakuna mwalimu ambaye atakufanya wewe kuwa mwenye akili
    • hakuna Guru yeyote ambate atakufanya uwe na utulivu
    • Hakuna mshauri yeyote atakayekufanya uwe tajirii

    Mtu pekee anayeweza kukupa hayo yote ni wewe mwenyewe.

    Ni wewe mwenyewe ambaye unapaswa kubeba hayo majukumu yako bila ya kurudi nyuma. Lakini kama utasubiri watu wakufanyie kazi, nakuhakikishia kwamba utasubiri sana.

    SOMA ZAIDI: 

    Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

    Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

    SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

    Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

    Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

    Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

    Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

    For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

X