Kama unajua Kuna wenzako wanakuzidi, elimu, kipaji, ujuzi, konekisheni n.k. unapaswa kupiga kazi kwa bidii.
Yaani, wewe huna maarifa, ujuzi, kipaji halafu unabweteka. Inakuwa siyo poa hata kidogo.
Moja ya kitabu ambacho nimewahi Kusoma kikanifungua sana ni kitabu cha 50CENT na cha Kobe Bryant.
50CENT anasema hivi, unaweza kumzidi akili, unaweza kumzidi konekisheni, unaweza kumzidi kipaji na vitu vingine vyote, ila huwezi kumzidi kuchapa kazi kwa bidii.
Jamaa anasema anachapa kazi kwa bidii. Na kuchapa kazi kwa bidii kumemfanya kuwa alivyo. Ameeleza haya kwenye kitabu chake cha HUSTLE HARDER, HUSTLE SMARTER
Kobe Bryant mwenyewe kwenye kitabu chake cha THE MAMBA MENTALITY anasema alikuwa anaamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kufanya mazoezi. Hapa alikuwa anaamka asubuhi na mapema kabla ya mchezaji mwingine yeyote.
Na alikuwa anafanya mazoezi usiku wakati wenzake wote wanaenda kulala.
Hii nayo naweza kuihusisha na Ile ya 50CENT ya kuchapa kazi kwa bidii.
Niliwahi kusikia eti Mohammed Ali alikuwa hana utaratibu wa kuhesabu pushap anazopiga mpaka pale anapojisikia kuanza kuchoka.
Kama kweli unajijua kuna wenzako wamekuzidi kipaji, akili, konekisheni, uwezo, n.k chapa kazi kwa bidii. Mambo nengine yatajipanga
Naomba kuishia hapo.
Uchambuzi wa kitabu cha 50 CENT huu hapa
Ukitaka pia kujua uchambuzi wa kitabu cha Kobe Bryant basi utabonyeza hapa.
SOMA ZAIDI:
- Ufanyeje pale bidii yako inapotumika kama mtaji kwa watu wengine
- USIONGEE SANA, ACHA KAZI ZAKO ZIONGEE
- FANYA KAZI KWA BIDII
Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.
Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.
SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea
Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com
Asante.
Kila la kheri
Umekuwa nami .
Rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz
3 responses to “Cha Kufanya Pale Wenzako Wanapokuzidi Elimu, Kipaji, Ujuzi, Konekisheni n.k”
Nimependa sana kitabu hiki na nimependa zaidi maneno ya 50CENT
[…] Cha kufanya pale wenzako wanapokuzidi elimu, kipaji, ujuzi konekisheni n.k. […]
[…] Cha kufanya pale wenzako wanapokuzidi elimu, kipaji, ujuzi konekisheni n.k. […]