Jijengee Utaratibu Wa Kusema Kidogo Na Kuwa Na Matendo Makubwa


Kuna usemi kuwa ni rahisi kusema ila vigumu kutenda. Na katika ulimwengu huu ambao tunaishi sasa hivi wasemaji ni wengi. au watu wenye maneno ni wengi. unaweza kukuta watu kwenye mitandao yao ya kijamii wameandika kwamba wao ni wakurugenzi wa makampuni, wakiwa hawaweki juhudi za kuanzisha hayo makapuni.

 

Kitu pekee ambacho ninaweza kusema kwako ni kuwa jijengee utaratibu wa kusema kidogo na kuwa na matendo makubwa. yape kipaumbele matendo yako.

Kama hakuna ulazima wa wewe kuongea basi usifanye hivyo.

Muda mwingine unapaswa kukaa chini na kusikiliza watu wengine wanasemaje.

Unapokuwa muongeaji sana unashindwa hata kusikililza mambo ya maana ambayo yanasemwa kwako, ambayo kama ungeyafanyia kazi yangekufanya wewe kuwa bora zaidi. Hivyo basi, kuanzia siku ya leo anza kujijengea utaratibu wa kusema kidogo na kuweka matendo makubwa.

 

Rafiki yangu, nakutakia siku njema sana.

Umekuwa nami,

GODIUS RWEYONGEZA

0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X