Ngoja nikwambie kitu, hakuna namna ambavyo wewe unaweza Kuepuka kazi katika suala zima la kufanikiwa. Kama unataka kufanikiwa sharti uwe tayari kuweka kazi itakayokufikisha kule unapotaka kufika.
Usije unategemea kwamba MTU yeyote atafanya kazi kwa ajili yako.
Nakumbuka siku za nyuma niliwahi kuandika Makala hapa nikasema kwamba hakuna MTU ambaye anaweza kupiga Push-Up kwa ajili yako.
Hii ndio kusema kwamba, Kama unataka afya njema, fanya vitu vitakavyokupa afya njema. Hakuna mtu anaweza kufanya hivyo vitu kwa ajili yako.
Kama unataka kufikia utajiri wa kifedha, sharti ukubali kufanya vitu vitakavyokufikusha kwenye mafanikio ya kifedha. Hakuna mtu atakusaidia wewe kufikia huko.
Sasa kazi ni kwako rafiki yangu. Ebu jiulize unataka kufikia kitu gani maishani mwako, halafu jiulize je, upo tayari kulipa gharama ya kukufikisha huko?
Kama haupo tayari kulipa gharama sahau kuhusu kufikia mafanikio unayotaka….
Hakikisha umejiunga na mfumo wetu wa kupokea Makala maalumu kwa watu maalumu. Jaza taarifa zako hapo chini.