Jinsi Ya Kupima Thamani Ya Utajiri Ulionao


Kama una ndoto kubwa na za kufika mbali basi ni muhimu kwako kujua utajiri ulionao kwa sasa. Hii itakupa nguvu ya wewe kuendelea kupambana zaidi ili uweze kufika mbali.

Muda wa wewe kupima Utajiri wako.

Kutokana na shughuli kuwa nyingi, huwezi kuwa unapima Utajiri wako kila siku. Ila unaweza kuwa unapima Utajiri wako walau mara moja kila baada ya miezi mitatu. Au hata mara moja kila mwezi. Hapa utaangalia namna ulivyoweza kukuza utajiri wako kulinganisha na siku za nyuma na lakini pia kuweka mpango wa kukuza Utajiri wako kwa siku zijazo.

Sasa napimaje thamani ya Utajiri wangu?

Kupima thamani ya Utajiri wako, fanya hivi; chukua thamani ya mali zote unazomiliki toa madeni yote.

UTAJIRI= THAMANI YA RASILIMALI-MADENI YOTE.

Utakachopata ndio utajiri wako kwa wakati husika. Sasa je, wewe una kiwango gani kwa sasa.
Ni mamilioni
Ni malaki
Ni maelfu?

Kwa kiwango chochote ulichonacho sasa hivi, kazana kukikuza zaidi. Inawezekana

SOMA ZAIDI: Bilionea Ni Mtu Wa Aina Gani?Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X