Kwa Nini Nashindwa Kutimiza Malengo Yangu?


Habari ya leo rafiki yangu

Kwenye makala ya leo ningependa kutoa ushauri kwa rafiki yetu mmoja ambaye ameuomba kutoka kwangu. Rafiki yetu anasema kwamba kwa nini hafikii malengo ilihali ana uwezo wa kufanya hivyo?

Kujibu swali lake ningependa kuja moja kwa moja kwenye pointi ya msingi kueleza kwa nini hafikii malengo yake. Hiki ni kitu ambacho kinawakumba watu wengi. Maana unaweeza kukuta mtu ana malengo na mipango ambayo anatamani kuifanyia kazi mwaka hadi mwaka, ila mipango hiyo haifanyii kazi.

Kuna mtu mmoja alikuwa na lengo la kupanda miti, ila kila mwaka huwa anasema anataka kupanda miti, ila kiuhalisia hajawahi kupanda miti. Siyo kwamba hana uwezo wa kupanda miti, siyo kwamba kipato hakitoshi. Sasa katika mazingira kama haya, tatizo ni nini?

Kwenye hii makala tunaenda kuona hili na namna ya kuliepuka ili kuweza kufikia makubwa.

1. Hujui unachotaka. Huu ni ukweli mchungu na mgumu sana kumeza ila ukweli muhimu sana.

Hiki kitu kinaweza kuonekana cha kushangaza,ila siyo kwamba uko peke yako. Asilimia kubwa ya watu pia wako hivyo. Hili limehibitishwa na tafiti mbalimbali ambazo zimekuwa zinafanyika na kila zinapofanyika imegundulika kwamba watu kwa hakika hawajui wanachotaka. Tafiti zimeonesha waziwazi kuwa ukichukua watu 100 kati ya hao watu 100 ni watu watatu tu ndio utakuta kwamba wanajua wanachotaka.

Kitu hiki kinaweza kukushangaza zaidi hasa pale ambapo mtu unakuwa mzima halafu, unaambiwa eti hujui unachotaka. Hili linawezekanaje?

Ili tuthibitishe kama hili ni kweli wacha naomba ujibu hili swali. Je, malengo ambayo hufikii ni yapi? Jiulize tu hili swali. Hivi haya malengo ambayo ninasema kwamba siyafikii ni yapi? Unaweza kujishangaza kwa kukuta hata hujui malengo yenyewe.

Unayajua kwa undani haya malengo? Umeweka uwe umeyafikia baada ya muda gani? Umeayaandika wapi haya malengo?

Majibu ya haya maswali naomba usiniambie, ila jijibu mwenyewe. Wewe mwenyewe unajua kama majibu ya maswali hayo ni sawa au siyo sawa.

Cha kufanya sasa unapaswa kujinasua kwenye huu mtego. Yaani, badala ya kuishi maisha ambayo hayana mwelekeo na ambayo hujui wapi unataka kufika kwenye maisha yako, anza kwa kuhakikisha kwamba unajua malengo na ndoto zako. kisha haya malengo na ndoto zako zifanyie kazi.

2. Una malengo lakini hujaweka hatua unazokwenda kuchukua

Hiki kitu inawezekana hukijui. Ila ngoja nikushirikishe namna ambavyo huwa nafanya nikiweka malengo. Kwa kawaida huwa nikiweka malengo, huwa siishii tu kuweka malengo. Bali huwa naweka hatua kwa hatua vitu ambavyo naenda kufanya.

Huwa naandika chini, kuwa ili niweze kufikia lengo langu kubwa, sharti nifanye kitu fulani, nikifanya kitu fulani kitanipelekea kwenye kitu fulani, na kitu hicho ndicho mwisho wa siku kitanfanya nifikie lengo.

Na wewe unapaswa kufanya hivi. Inawezekana plan yako ya kwanza kama hii isiwe sahihi kwa asilimia 100, ila unapokuwa na plan ambayo unaifanyia kazi, unakuwa kwenye hali nzuri zaidi ya kufanikisha malengo yako kuliko mtu ambaye anakuwa hana plan kabisa.

Hivyo, kuanzia leo hii usiishie tu kuweka malengo, bali baada ya kuwa umeweka malengo, weka na hatua ambazo unaenda kuchukua ili kuweza kufikia malengo yako.

3. Weka ratiba

Baada ya kupanga mikakati yako, andika ratiba ya kila hatua utakayochukua na uhakikishe kuwa unafanya kazi kwa kuzingatia ratiba hiyo. Kwa mfano, kama mkakati wako ni kuanza kufanya mazoezi, andika ratiba ya muda wa kufanya mazoezi na kuzingatia ratiba hiyo. Ratiba itakusaidia kudhibiti muda wako na kuhakikisha kuwa unafanya kazi kwa ufanisi.

Mara zote fuata ratiba yako kama katiba, usikubali watu waivuruge hovyohovyo.

4. Huchukui hatua

Huwezi kuweka malengo na kukaa huku ukisubiri siku moja ambapo malengo yako hayo makubwa yatatimia. Ni lazima unapoweka malengo uchukue na hatua pia.

Mfano lengo la kuweka akiba ya milioni 100 linapaswa kuchukukuliwa hatua. Siyo tu kwamba unaishia kuweka lengo na kutulia,bali unaweka lengo na kuchukua hatua. Kama ni kuweka akiba, weka akiba. Kama ni kuandika, andika. Kama ni

5. Unachukua ambazo hazitoshi

Inawezekana unachukua hatua, ila siyo hatua ambazo zinatosha.

Kiwango cha chini cha kuchukua hatua kinapaswa kuwa ni mara kumi zaidi ya kawaida. Na hiki kinapaswa kuanzia kwenya malengo ambayo unaweka.

Yaani, kama lengo lako ni kufanya mauzo ya elfu kumi zidisha mara kumi zaidi. kama unapaswa kukutana na mteja mmoja, kutana nao kumi. Kama unataka utume jumbe kwa watu, badala ya kutuma kwa watu watano tu, tuma kwa hamsini. mara zote fanya mara kumi zaidiii ya vile ambavyo watu wa kawaida wanafanya.

Naomba unisikilize na unielewe vizuri, wanaofikia malengo yao, siyo kwamba wanakuwa na akili kubwa sana kuliko wewe. Wanaofikia malengo makubwa siyo kwamba wana konekisheni kubwa kuliko wewe. Na wala wanaofikia malengo siyo kwamba wana kitu chochote cha tofauti zaidi yaw ewe.

Kitu pekee walichonacho ni kwamba wanapoweka malengo wanahakikisha wameyafanyia kazi haya malengo kwa kujitoa na bila ya kurudi nyuma. Wanayafanyia kazi malengo hayo hata kama ni kwa kuchukua hatua kidogokidogo.

Hiki kitu ni tofauti na watu wengi ambao huwa wanaweka malengo. Maana asilimia kubwa ya wale ambao huwa wanaweka malengo, huwa hawachukui hatua, badala yake huwa wanaendelea kusub iri siku fulani hivi ambapo kila kitu kitakuwa sawa kwa upande wao.

Rafiki yangu, nakuomba kitu kimoja ukifanyie kazi kuanzia leo hii. Kitu hiki ni kwamba, weka malengo na chukua hatua kuyafanyia kazi hata kama ni kidogo.

Lengo lako kubwa usiishie tu kuliona kwa ukubwa wake. Lengo la kuweka akiba ya milioni kumi, linaweza kuonekana kubwa, ila unahitaji uchukue hatua, hata kama ni kidogo

6. Uzembe

Moja ya dhambi kubwa sana ambayo unapaswa kuepuka ni dhambi ya uzembe. Sikiliza uzembe hauwezi kukufikisha popote kwenye maisha yako.

Unapoteza muda kwenye mambo ambayo siyo ya muhimu

Kama una malengo, muda wako wote unapaswa kuwekwa kwenye malengo. Kitu kikubwa. Mambo mengine ambayo yako nje ya malengo yako unapaswa kuachana nayo.

Usifuatilia maisha ya watu wengine kabla hujafuatilia maisha yako mwenyewe.

Usifanye kitu kingine kile kabla hujafanya mambo ya msingi sana kuhusu maisha yako

Hayo ndiyo mambo ya msingi ambayo unahitaji kufanyia kazi ili uweze kufanikisha maengo yako.

Kabla sijamalizia kuandika makala hii ningependa kukushikirisha stori moja fupi ya Zig Ziglar, siku moja Zig Ziglar alikuwa anatoa mafunzo. Mtu mmoja alimwuliza kwa nini hamasa huwa hazidumu. Zig Ziglar alimwambia hamasa ni kama kuoga, huogi mara moja na kuacha. badala yake unaoga kila siku.

Hivyo, hivyo, kwenye kufanyia kazi malengo yako. Inawezekana mwanzoni unakuwa na hamasa na unajituma kweli, ila baada ya muda hamasa yako inapotea na unaanza kuishi maisha ambayo ulikuwa nayo mwanzoni.

Sikiliza, hamasa haiwezi kudumu na kuendelea kuwepo kwa ajili yako mara zote. Ila inapotokea kwamba hamasa yako imepotea, haupaswi kukata tamaa wala kurudi nyuma. Badala yake unapaswa kuendelea mbele na muda mwingine kujilazimisha kufanyia kazi malengo yako hata kama hauna hamasa.

Lakini pia unapaswa kuendelea kujihamasisha mwenyewe hasa kwa kujifunza na kusoma vitabu na kusikiliza masomo ambayo yatakuinua kama vitabu ambavyo vimesomwa kwa sauti.

Kwa kumalizia kabisa, kuna RASILIMALI muhimu ambazo zitakusaidia wewe kwenye kufanikisha malengo yako. Na rasilimali hizi ni vitabu ambavyo unapaswa kusoma ili kuweza kufanyia kazi malengo na ndoto zako.

MOJA: KITABU CHA: NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZANa Kwa Nini UNAHITAJI KUMALIZA KILE ULICHOANZA.

Hiki ni kitabu muhimu sana kwako. na hakikisha unakipata, ili uweze kuchukua hatua ya kwanza kwenye kufanyia kazi malengo yako. na siyo tu kufanyia kazi malengo yako, bali kuyafanyia kazi kwa msimamo bila kuacha mpaka pale malengo yanapoonekana kwenye uhalisia.

Pili ni kitabu cha NGUVU YA VITUV VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA: Hiki ni kitabu kingine muhimu sana ambacho unapaswa kuhakikisha kwamba umepata. Kitakusaidia wewe kuweza kufanikisha lengo lako kubwa lolote hatua kwa hatua

Na mwisho ni kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI: Hiki ndicho kina mwongozo wa kukusaidia wewe kuweka malengo ambayo utayafanyia kazi na kuweza kufanikisha makubwa.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X