Habari ya leo rafiki yangu wa ukweli. Hongera sana kwa siku nyingine njema sana rafiki yangu. Siku ya leo nikwambie moja ya sababu kubwa kwa nini watu wengi huwa hawaweki malengo.
Unajua kwa nini watu wengi huwa hawaweki malengo? Kuna sababu nyingi sana ila hizi ndizo zinawafanya watu wengi wasiweke malengo.
Ya kwanza ni kwa sababu ya uoga; wengi wana uoga linapokuja suala zima la kuweka malengo. Mtu anaanza kufikiria kwamba nikiwe malengo, na nisipoyatimiza itakuwaje? Hiki kitu kinamfanya mtu aogope.
SOMA ZAIDI: Uoga wako ndio umasikini wako
Sasababu ya pili inayowafanya watu washindwe kuweka malengo ni kwa sababu hawajui namna ya kuweka malengo. Hiki ni kitiu kingine kikubwa kinachowakwamisha watu na hivyo kujikuta kuwa wanaishi maisha yao yote bila ya kuwa na malengo.
sababu ya ta tatu ni kwa sababu wanajiona hawastahili kupata hivyo vitu vizuri. Ukijiona kwamba hustahili kuwa na hiyo nyumba nzuri. Husatahil kuwa na hilo gari zuri. Hustahili kuwa na huyo mchumba n.k. huwezi kuwa naye. Kitu chochote kile ambacho wewe mwenyewe unaona kwamba huwezi kufanikisha kwenye maisha yako, ni ukweli kuwa hutakaa ukifanikishe
SOMA ZAIDI: Unafunga Sehemu Gani?
Kwa hiyo, kinachotakiwa sasa hivi ni wewe kubadili mtazamo wako kwanza kwa kuhakikishakwamba unaondoa uoga, pili kaa chini ujifunze namna ya kuweka malengo. Kisha weka malengo hayo. Na mwishao jua kuwa unastahili kupata mazuri ambayo dunia inatoa. Unastahili kuwa na afya bora, hiyo nyumba nzuri ni stahiki yako, watoto wazuri, wenye tabia yako ni haki yako.
sasa kwa kuwa unastahili kupata hivi vitu anza kuvifanyia kazi. Anza kuvifanyia kazi ili uweze kuvifikia.
Hizo ndizo sababu tatu ambazo zinawafanya watu wengi wasiweke malengo. Nimeona nikushirikishe hizi sababu, ni imani yangu kuwa unaenda kuzifanyia kazi na kuepuka zisikukwamishe. kama kuna watu wawili ambao unawafahamu wanaoweza kunufakika na hii makala, tafadhali watumia hii makala ili nao waweze kuisoma. Kama una makundi mawili ya whatsap ambapo unaweza kutuma hii makala, itume, nina uhakika kuna watu wawili ambao watanufaika..
Uwe na wakati mwema.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza. Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza wasiliana naye kwa kupiga simu +25568408755