Mambo 15 ambayo Godius Rweyongeza anashauri Uanze Kuyafanyia kazi Mara Moja


Habari ya Leo. Hongera sana Kwa siku hii nyingine njema sana

1. Tuitumie Leo kufanya makubwa. Kila mmoja Kwa jukumu lake analopaswa kufanya, alifanye Kwa weredi mkubwa

2. Mabadiliko Unayotaka kuyaona Anza kuyasababisha mwenyewe siku ya Leo Kwa kufanya jambo lolote hata kama ni Dogo.

3. Ukitimiza wajibu wako na Kila mmoja akatimiza wajibu wake, hii dunia Itakuwa sehemu nzuri sana kuishia.

4. Vitu vingi ambavyo vitakupa MAFANIKIO MAKUBWA vinahitaji uvifanye Kwa kurudia rudia mara Kwa mara. Uwekeze mara Kwa mara, ujifinze mara Kwa mara, uongeze kipato chako mara Kwa mara n.k

5. Usiischoke safari ya KUELEKEA malengo na ndoto zako kubwa. Endelea kupambania Kila siku.

6. Ukweli ni kuwa usipofanyia kazi NDOTO ZAKO hakuna mtu atazifanyia kazi Kwa niaba Yako

7. Muda Mzuri Wa kupanda mti ulikuwa ni miaka 20 iliyopita, ila muda mwingine Mzuri zaidi ni Sasa

8. Kama Kuna jambo linakukwamisha, jifunze Hilo jambo kupitia usomaji wa vitabu.

9. Mara zote kuwa unasoma kitabu.

10. Kama hauna ndoto kubwa sahau kuishia maisha yenye mafanikio makubwa

11. Fikiri Kwa ukubwa

12. Jihusishe na watu chanya

13. Pangilia siku Yako Kila siku

14. Anzisha biashara 2024.

15. Shukuru Kwa mambo mazuri mengi uliyonayo. Familia, wazazi, watoto, mwenza, afya njema kuiona siku ya Leo ……

SOMA ZAIDI: 

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.

Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X