Uache urafiki ubaki kwa ajili ya urafiki na wewe
- Fanya kazi na watu wanaojua kufanya kazi
- Fanya biashara na watu wanaojua misingi ya biashara na amba watakukwa tayari kuisimamia mara zote.
Kwenye biashara, urafiki mzuri ni ule unaotengenezwa na biasahara. Ila siyo mtu mlikuwa rafiki halafu eti mnaanzisha biashara, mara nyingi mtajikuta mnaweka urafiki kwenye biashara na hivyo kuharibu biashara
Hivyo kama unafikiri kuanzisha biashara, kwa kiwango kikubwa utakuta kwamba rafiki yako wa sasa hivi anaweza asiwe mtu ambaye atakufaa sana kwenye biashara.
Najua utakuwa umesikia stori nyingi sana za watu walioanzisha biashara na marafiki zao.
Ila wengi ukifuatilia, urafiki ulikuwa umejengwa kwenye misingi ya biashara.
Siyo wewe unaanzisha biashara na rafiki yako ambaye msingi mkubwa wa urafiki wenu mmeujenga kwenye kubeti, kushangilia mpira, kuangalia movie na vitu kama hivyo.
Baadaye unafika wakati ambapo mnapata pesa kidogo tu, kila mmoja anafikiri juu ya kupata pesa asepe.
Angalia urafiki wa watu maarufu kama Steve Jobs na mweza Stephen Wozniak, hawa watu walikuwa marafiki, ila urafiki wao ulikuwa umeunganishwa kwenye ubunifu. Wote walikuwa wanapenda ubunifu na kubuni vifaa kama kompyuta, na ndiyo maana waliweza kufanya makubwa kwa pamoja.
Au chukulia mfano wa urafiki kama Bill Gates na Allen Paul, hawa pia urafiki wao ulikuwa umejengwa kwenye kupenda kompyuta na ubunifu.
Urafiki mzuri ni ule ambao utatokana na kazi, au biashara
Kama urafiki wa Bill Gates na Warren Buffet au urafiki wa
kWA KUMALIZIA: Leo ningependa tu kukwambia kwamba urafiki wako wa kweli ujengwe kwenye misingi ya biashara, ila siyo urafiki ambao utabomoa biashara.
SOMA ZAIDI: