
Rafiki yangu, kuna maswali mawili mazuri sana ambayo unapaswa kuwa unajiuliza kila siku. Haya maswali yatakufanya utafakari juu ya mambo mengi ambayo unafanya kila siku na namna gani unaweza kuendelea kuifanya hii dunia kuwa sehemu bora kabisa kuwahi kutokea.
Maswali haya tunayapata kutoka kwa Benjamin Franklin ambaye alikuwa ni mmoja wa wanasiasa, mvumbuzi na mwanadipolomasia wa Marekani. Ni masawli ambayo alikuw anajiuliza miaka hiyo, na aleo hii bado tunaweza kujiuliza hayo maswali na tukapata matokeo mazuri pia kwenye maisha yetu.
Swali la kwanza kabisa ambalo Benjamin Franklina alikuwa anajiuliza lilikuwa ni ni je, ni kitu gani ambacho ninaenda kufanya leo kikawa msaada kwa watu wengine leo?
Tunapojiuliza swali hili tunaondoka kwenye dhana ya kujifikiria sisi wenyewe kwanza. Badala yak e tunaanza kuwafikiria wengine kwanza. Mpaka hapo unaweza kuwa unajiuliza, hivi kwa nini napaswa kuwafikiria wengine badala ya kuanza kujifikiria mimi mwenyewe. Ukweli wa hili tunaweza kuupata kwa kuisikiliza nukuu ya Zig Ziglar inayosema kwamba, unaweza kupata chochote unachotaka kama utawasaidia wengine kupata wanachotaka. HiI NDIYO Kusema kwamba kuwafikria wengine ni namna moja ya kujififikiria wewe kwanza. Maana unaweza kupata chochote unachotaka, ila kikubwa unapaswa kuwa tayari kuwasaidia wengine kwanza.
Ebu tuone mfano wa mtu ambaye anafungua duka mtaani kwako. Huyu mtu anapofungua duka maana yake kuna kitu choa tofauti ambacho anakuwa tayari ameshaona, hakipo au kinalegalega. Inawezekana unapoenda dukani kwenye duka zilizopo kununua bidhaa huzipati zote sehemu moja, unalazimika kununua bidhaa moja hapa na nyingine pale. Sasa huyu jamaa anaweza kuwa amaeona hilo gepu na hivyo, akaamua kulitumia vizuri sana. Badala ya wewe kwenda duka fulani, ukanunua bidhaa moja, kisha ukalazimia kwenda duka jingine ili kununua bidhaa nyingine, yeye anakuunganishia bidhaa zote kwa pamoja. Ukienda kwake unaweza kununua kila bidhaa unayotaka. Hii maana yake nini? Hii maana yake ni kwamba amekusaidia wewe kupata unachotaka. Ni kitu gani unataka, unataka bidhaa za nyumbani, lakini hutaki uchovu wa kuzunguka zunguka huku na kule ukinunua bidhaa moja hapa na nyingine pale. Unataka ukitoka nyumbani na hela yako uende sehemu moja ununue bidhaa zako kisha uondoke.
Lakini pia inawezekana huyu ameshaona fursa, ya huduma bora. Inawezekana watu waliopo wanatoa huduma, ila siyo huduma bora na yakuaminika. Mteja anaweza kwenda kununua kitu, wanaanza kukufokea na wanakuona kama mtu mwenye shida. Huyu akafungua duka, akaamua kwamba wewe mteja ndiye mfalme. Wewe ndiye mwanzo na mwisho. Akaanza kuwahudumia vizuri wateja wake.
Kumbe rafiki yangu swali hili moja tu la kujiuliza kila siku, linakufungulia fursa kibao. Ni swali muhimu sana ambalo unapaswa kuwa unajiuliza kila siku bila ya kuacha. Naamini utaanza kulifanyia kazi moja bila ya kurudi nyuma.
Soma zaidi:
- Maswali Manne Muhimu Unayopaswa Kujiuliza Baada Ya Kusoma Kitabu
- NJE YA KUMI NA NANE: fikiri, Hoji Na Uliza Maswali Katika Ulimwengu Ambao Hautaki Uwe Hivyo.
- Iambie dunia kile unachotaka kufanya, ila kwanza kioneshe hicho kitu
Swali la pili ambalo unapaswa kujiuliza ni swali Ni kitu gani bora nimeweza kufanya siku ya leo kwa ajili yaw engine?
Unapaswa kujiuliza hili swali jioni kabla ya kulala. Usilale kabla hujajiuliza hili swali, na ikitokea kwenye kujiuliza hili swali umegundua kwamba siku hiyo hujafanya kitu, basi itumie nafasi hiyo kufanya kitu hata kama ni kidogo.
Kuna siku moja nilijiuliza hili swali, nikagundua kwamba mbali na kwamba siku hiyo nilikuwa bize tokea asubuhi mpaka jioni, lakini sikuweza kufanya kazi ya yoyote ya kuwasaidia watu wengine. Nilichofanya japo nilikuwa tayari nimechoka, nilichukua muda kidogo na kuandika makala fupi nzuri sana ambayo watu wengine wangeweza kusoma na kupata kitu cha kufanyia kazi. Na hivyo kwa namna hiyo nikawa nimeweza kufanya kitu chenye mchango kwenye hii dunia.
Rafiki yangu, kamwe usiache kujiuliza haya maswaili mawili kila siku. Isipite siku ambayo hujajiuliza haya maswlai, utagunduakwamba unazidi kuwa bora zaidi kwenye kazi zako na unaimarika.
SOMA ZAIDI:
- Kitabu cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA ni kitabu ambacho kila mtu anapaswa kusoma
- Vita Ya Maisha Anashinda Mtu Anayefikiri Anaweza
- Kitu Kimoja Ambacho Hakuna Mtu anaweza Kukifanya Kwa Niaba Yako
Nikutakie kila la kherii kwenye kufanyia kazi haya ambayo tunajifunza
Makala hii imendikwa na Godius Rweyongeza
Unaaweza kuwasiliana na mwandishi kupitia namna ya simu 0755848391
Mwandishi yuko Morogoro, nchini Tanzania