Rafiki yangu siku ya leo ningependa kikufundishe njia Saba Bora za KUTANGAZA UJUZI WAKO KWA watu, kiasi Cha kuweza kuwashawishi watu waweze kutoa hela zao mfukoni na kukulipa.
Naomba ifahamike hapa kuwa ninapoongelea Aina za ujuzi namaanisha, kile kitu ambacho tayari unacho na unaweza kukipangilia vizuri kikaanza kuleta mafanikio.
Kuna watu wanaposikia ujuzi Basi wanadhani kinapaswa kuwa ni kitu cha kipekee sana kitu ambacho hakijawahi kufanyika au kuonekana ssehemu yoyote.
Ujuzi unaweza kuwa elimu au taaluma yako.
Ujuzi unaweza kuwa kitu ambacho umefanya kwa muda mrefu na Sasa umebobea.
Kwenye hicho kitu kiasi kwamba unaweza kuwafundisha wengine wakanufaika nacho.
Ujuzi unaweza kuwa wa kujifunza pia mtandaoni
SOMA ZAIDI: AINA TATU ZA UJUZI UNAOHITAJI ILI KUONGEZA THAMANI YAKO NA KULA MEMA YA NCHI
Kwenye makala ya leo ningependa nikuoneshe njia Saba za kutangaza ujuzi wako
Kwanza unaweza kutangaza ujuzi wako mtandaoni
Pili unaweza kuwatumia watu wanaokujua kutangaza ujuzi wako
Tatu ni kuandaa na kuonesha kazi zako
Nne Ni kuomba rufaa
Tano nii kuwa na data za wateja walionunua na wale wanaonesha nia ya kufanya.
Sita ni kuwatembelea watu walipo na saba
na saba ni kupitia kufanya kazi ambayo ni bora kabisa kiasi kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kukupuuza.
Rafiki yangu hizo ndiyo njia saba za kutangaza ujuzi wako kwa watu, na habari njema ni kwamba, unaweza kuchagua njia moja ambayo unaweza kuanza kutumia sasa hivi.
kisha ukaanza kuitumia.
Kama kuna njia kati ya hizo utaitumia halafu ikaleta matokeo, usiache kuitumia hiyo njia. Endelea kuitumia zaidi na zaidi hku ukiboresha ili uweze kuwafikia watu kwa wingi zaidi.
SOMA ZAIDI:
- Cha kufanya pale wenzako wanapokuzidi elimu, kipaji, ujuzi konekisheni n.k.
- NIMEZALIWA MSHINDI; Huu Ndio Ujuzi Ambao Hauuzwi Sokoni
- Jifunze Ujuzi Huu Mmoja Tu, Utakufaa Maisha Yako Yote
Kwa leo naomba niishie hapo rafiki yangu.
Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.
Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.
Kwa mazungumzo ya ana kwa ana utalipia LAKI MBILI NA NUSU kwa saa
Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea
Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com
One response to “Njia Saba (07) Bora Za Kutangaza Ujuzi Wako Kwa Watu”
Asante sana kwa mafunzo yanaleta hamasa na nguvu ya kusonga mbele