Hii ndiyo njia rahisi ya wewe kujipoteza


Rafiki yangu, kama kuna njia rahisi ya wewe kujipoteza ni kufanya vitu kama ambavyo kila mtu anafanya. sote tunajua kwamba vitu ambavyo watu wengi huwa wanafanya huwa siyo sahihi. Na njia ya pekee ya wewe kuishi maisha ya kawaida, ni wewe kufanya vitu kama ambavyo kila mtu anafanya.

Hii ni njia ambayo haifanyi kazi, na laiti kama hii njia ingekuwa inafanya kazi maana yake watu wengi wa kawaida wangekuwa matajiri wakubwa sana au la wangekuwa na mafanikio ambayo siyo ya kawaida. Lakini hali siyo hivyo.

Kumbe vitu ambavyo watu wengi wafanya siyo sahihi. Na kitu kufanywa na watu wengi hakikifanyi kuwa sahihi.

EBU KWA MFANO tuchukulie tu maisha ya kawaida ambayo mtu anaishi. Anaambiwa kwamba nenda shule usome kwa bidii, na kweli anaenda shule anasoma kwa bidii, kisha baada ya shule anatafuta kazi. tuchukulie huyu mtu amepata kazi, baada ya hapo anaenda kazini. Akifika kazini, anaambiwa kwa kuwa sasa una mshahara, wewe unaweza kupata mkopo ambao utakufaa.

Anachukua mkopo.

Wakati huohuo, anakuta kwamba kuna sheria ambayo inamtaka kujiunga na mashirika ya MAFAO, hivyo anaanza kuaminishwa kwamba ukiweka hela yako, hutahitaji kushughulika na pesa zako tena. Na wala hutahitaji kujiandaa kwa ajili ya kuja kustaafu, badala yake sisi, tutakufanyia kila kitu.

Anaanza kuishi maisha yake kihivyo, mpaka anafikia miaka ya kustaafu ambapo anakuja kupewa MAFAO yake, hapo ndio anagundua kwamba hayatoshi. Muda huu sasa ndio anaanza kufunguka ili aweze kutafuta ajira na kazi nyingine.

Habari njema ni kwamba unaweza kujiondoa kwenye huu mnyororo wa watu wengi, na kujiweka kwenye mnyororo wa watu uwachache.

Kwenye jamii yoyote ile huwa kuna wachache waliofanikiwa. Na hawa watu ukiwafuatilia, utagundua kitu kimoja kutoka kwao. Kitu hiki ni kufanya vitu kwa namna ya upekee, tofauti na watu wengine

Hawa ndio wale ambao utakuta wanajilipa wenyewe kila baada ya kuwa wamepata kipato chao.

Hawa ndio wale ambao utakuta kwamba wanawekeza na kuchukua kiasi cha fedha na kukifanya kiwafanyie kazi.

Hawa ndio wale ambao huwa hawanunui vitu kuwaridhisha watu wengine. Badala yake huwa wananunua kutokana na uhitaji wao kwa wakati husika.

Rafiki yangu, ninachotaka kukusisitiza siku ya leo ni kwamba wewe unaweza kujiingiza kwenye kundi la watu wachache sana ambao wanafanya makubwa. Na hili linawezekana vizuri sana. Ila utahitaji kuzingatia yafuatayo.

Kwanza, utahitaji kujisukuma kwenye kila kitu unachofanya. Na kuhakikish kwamba hicho kitu unakifanya kwa namna ya utofauti ukilinganisha na watu wengine. Jisukume kwenye kitu chochote unachofanya na hakikisha kwamba kila unachofanya, unakifanya kwa viwanvo vikubwa sana. Naam, unakifanya kwa viwango vikubwa sana kuliko ambavyo umewahi kukifanya.

Kiasi kwamba mtu yeyote atayeona kazi yako, aseme kweli hii kazi imefanywa na mtu fulani.

Pili, utahitaji ujiepushe na mambo mengine yote ambayo hayachangii kwenye kufikia ndoto zako. na hapa namaanisha mambo mengine yote. Kama umekuwa unaangalia runinga kila siku. Kuanzia sasa hivi, anza kujiuliza, hivi runinga inasaidiaje kwangu kwenye kufikia ndoto zangu. Ukifuatilia kwa umakini utagundua kwamba, runinga haina manufaa yoyote yale kwako. Hivyo, unaweza kuiweka pembeni ili uweze kufanyia kazi majukumu yale machache ambayo yatakuwa na manufaa kwako.

Kama umekuwa unafuatilia maisha ya watu wengine, jiulize ni kwa namna gani kufuatilia maisha ya watu wengine kumekuwa na manufaa kwangu? Utagundua kwamba kufuatilia maisha ya watu wengine hakuna manufaa yoyote yale kwako. Hivyo, badala ya wewe kuanza kufuatilia maisha ya watu wengine, weka nguvu sasa kwenye kujifuatilia wewe mwenyewe. Weka nguvu kwenye kufuatilia mipango yako na mambo mengine ambayo yanakuhusu wewe mwenyewe.

Tatu, usiige maisha. Uwepo wa mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii. Uwepo wa runinga na vitu vingine umewafanya vijana wengi waishi maisha ya kuigiza kwa wingi kuliko uhalisia. Wengi watanunua vitu hata kama hawahivitaji. Wanasahau kwamba Warren Buffet anasema sheria kuu mbili unazopaswa kuziangatia ni moja, kutokupoteza fedha. Na mbili ni kutosahau sheria ya kwanza.

Rafiki yangu, kwa leo ningependa niishie hapo. Naamini kuna kitu utakuwa umepata kutoka kwenye hii makala ya leo. Kama wewe umeweza kunufaika hata kwa kupata kitu kimoja tu unachoweza kufanyia kazi. basi kuna wengine wanaweza kunufaika pia. Ebu washirikishe rafiki zako wawili tu hii makala ili na wao waweze kuisoma na kunufaika nayo.

Chagua kimoja, kisha nicheki kwa 0755848391 ili uweze kupata nakala ya kitabu chako.

Bila kuongeza kitu cha ziada. Nikutakie siku njema sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X