Mshangao! Jinsi Muda Ulivyo wa Dhahabu Kwa Mfanyabiahsara na Mtu yeyote makini


Leo nakuruhusu ufanye kitu kimoja tu, uzunguke popote pale hapa duniani, halafu  uje kuniambia ni wapi umekuta wanaweza kuongeza kiwango cha muda ndani ya siku.

Ni wapi ambapo mtu anaweza kuwa na saa moja, lakini akaomba kuuongezewa saa jingine zaidi na akaongezewa? Ni wapi ambapo mtu anaweza kukopesha muda wake wa leo ili aje alipwe kwa riba kesho yake?

Ukweli, ni kuwa hakuna sehemu ambapo muda unaweza kuongezwa, muda ni rasilimali muhimu sana ambayo haiwezi kuongezwa au kupunguzwa.

Hivyo kama wewe ni mfanyabiashara, moja ya kitu muhimu sana ambacho unatakiwa kuhakikisha kwamba umefanya ni kutumia muda wako vizuri. Unaweza kupoteza vitu vingine vyote ukavipata, ila huwezi kupoteza muda ukaupata. Muda ni zaidi ya mali. 

Hivyo moja ya jambo ambalo unaweza kulifanya likawa kama favor kwako ni kutumia vizuri muda wako. Na hili unaweza kulifanya kuanzia sasa.

njia bora ya kuanza kwenye hili ni kuhakikikisha kwamba unaanz akupangilia ratiba yako ya kila siku vizuri. Yaani, kila siku unapoamka asubuhi, hakikisha kwamba unapangilia ratiba yako vizuri. Ipangilie ratiba yako, kisha anza kufanya na kutimiza majukumu yako kulingana na majukumu ambayo yako mbele yako.

Kitu kimoja kikubwa ambacho nigependa kujua kutoka kwako ni kwa namna gani unaenda kuupangilia muda wako kuanzia leo hii

kama bado hujajua njia ya kukusaidia wewe kuupangilia muda wako ni hivi, 

Anza kwa kupangilia kila saa la siku yako kuanzia unapoamka mpaka jioni.

Kila sasa lipa mamjukum,u ambayo utakuw aunafanya na kukamiliusha ndani ya huo muda.

Kisha endelea mbele kwa kuhakikisha kwamba unautumia vizuri muda wako.

Kumbuka Muda Ni Dhahabu

 

SOMA ZAIDI: Kitabu Cha KIPAJI NI DHAHABU

Hii Ni Sentensi Iliyonichekesha

UWEKEZAJI NI NINI?

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X