Nguvu Ya Mtazamo (Ninalipwa laki mbili ndiyo maana mimi ni maskini vs Ninalipwa laki mbili ndiyo maana mimi ni tajiri)


Rafiki yangu, mtazamo ni moja ya kitu muhimu sana hasa linapokuja suala la mafanikio. Mtu afikirivyo ndivyo anavyokuwa.

Hivyo, kama unataka kufanikiwa, unapaswa kubadili mtazamo wako kutoka kuwa mtazamo hasi na kuw amtazamo chanya. Unapaswa kubadili mtazamo wako na kuanza kuona uchanya kwenye kile unachofanya.

Hali na matukio mbalimbali yanayotokea kwenye maisha yako, badala ya kuona katika namna ya uhasi, uone uchanya.

Tukichukua watu wawili, ambao wanaishi maisha sawa, ila wanatofautiana tu mtazamo. Hawa watu wawili, baada ya  muda watakuja kuwa na maisha tofauti, huku mmoja akiwa amefanikiwa na mwingine akiwa na maisha yaleyale ya kulalamika.

Kwa nini,

Kwa sababu ya mtazamo.

Tuchukulie hawa watu wawili wanalipwa laki mbili kila mwezi. Mmoja akawa na mtazamo kwamba sitaweza kutengeneza utajiri kwa sababu tu ya kipato ambacho naingiza. Na mwingine akasema kwamba nitatengeneza utajiri kutokana na kipato ninachoingiza.

Unadhani ni nani atatengenenza utajiri? Ukweli ni kuwa, yule ambaye ana mtazamo chanya. Mtazamo wa kuona kwamba kile kiwango cha fedha alichonacho ni sehemu ya kuanzia. Huyu ndiye atakayetengeneza utajiri ukilinganisha na mtu ambaye ana mtazamo hasi.

Ujumbe muhimu ambao nataka uondoke nao siku ya leo ni kuhakikisha unakuw ana mtazamo chanya. Fikra chanya zitakupelekea mbali kuliko utakapokuwa na mtazamo hasi.

SOMA ZAIDI:

  1. Kauli Yenye Nguvu: Ni bora Ufe Ukiwa unafanya unachopenda…
  2. Athari Ya Mtazamo Wako Kwa Vitu Vinavyokutokea
  3. 2024 badili mifumo yako ya kufikiri

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X