Kuna watu wengi wanaokatisha tamaa kwenye maisha yetu ya kila siku. Hata hivyo, ni muhimu sana, kuwa kujua njia ya kujikinga na wakatisha tamaa. kama ambavyo kuna mavazi ambayo ni bullet proof, hivyohivyo kuna njia ambazo ukizitumia naweza kuthubutu kuziita, kukatishwa tamaa proof, yaani njia hizi zitakufanya uzidi kusongambele hata katikati ya wakatisha tamaa. Utakuwa hushikiki, na mara zote utakuwa na malengo na ndoto kubwa ambazo unazipambania
Ngoja kwanza nikuchane ukweli,
Ukweli wa kwanza ni kwamba kama unakata tamaa kwa sababu ya watu wanaokukatisha tamaa, basi wewe hutakuja kufanikiwa. Maana tunavyoyaendea mafanikio makubwa ni kwamba kuna watu watatishika na mafanikio yetu ambayo tunayafanyia kazi. Na wengine watakukatisha tamaa kwa sababu tu wanaogopa zile hatua kubwa ambazo unachukua, kitu pekee watakachoona wanaweza kufanya ni kukukatisha tamaa.
Ukweli namba mbili ni kwamba kama unatakatishwa tamaa na watu, maana yake hauko bize kiasi cha kutosha, na hasa kama maneno na kauli ambazo watu wanatoa juu yako.
Ukweli ni kuwa unapaswa kuwa bize mara zote kuliko hata ubize wenyewe. Hakuna kitu kingine nje ya kazi zako na majukumu yako ambacho kinapaswa kukukwamisha wewe wala kukurudisha nyuma
Ukweli nambari tatu, kuna watu wamejipa kazi ya kukatisha tamaa wengine. Hivyo, waache wafanye kazi zao, na wewe kazi yako iwe ni kupambania malengo na ndoto zako kubwa.
Ukweli nambari nne, mti unaopigwa mawe ni mti wenye matunda.
Kiufupi ujumbe wangu ninaotaka kukwambia wewe ni kwamba haupaswi kuwa mtu wa kurudi nyuma na wala haupaswi kukatishwa na kitu chochote. kile kwenye maisha yako.
sasa ili usikate tamaa kuna silaha muhimu ambazo unapaswa kuwa nazo ambazo zitakusaidia sana kuhakikisha kwamba unasongambele.
SILAHA YA KWANZA: Kuwa na ndoto kubwa kama vile utaishi milele. rafiki yangu unapaswa kuwa na ndoto kubwa ambazo unazifanyia kazi, na zifanyie kazi mara zote bila ya kurudi nyuma, zifanyie kazi ndoto zako leo kama vile unaenda kufa kesho.
SILAHA YA PILI: Mara zote kuwa kwenye ratiba ya kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa. Kamwe usirudi na usikubali kurudishwa nyuma na mtu au kitu chochote kile. Usipokuwa bize na ndoto zako, hakuna mtu hata mmoja ambaye atakuwa bize na ndoto zako. Kumbuka ile nukuu ya madebe tupu huvuma
SILAHA YA TATU: Hakikisha mara zote umepangilia ratiba zako kwa umakini kiasi kwamba unakuwa hauna muda wa kupoteza. Hii ni silaha kubwa sana kwa sababu, itakufanya uwe biza na maisha yako na uachane na mambo ya wengine.
na ukweli ni kuwa una mambo mengi ya kufuatilia juu ya maisha yako kuliko kufuatilia maisha ya watu wengine
SOMA ZAIDI:
- Inawezekana Kama Hautangalia Nyuma
- Maisha Ni Fursa: Zitumie ZIKUBEBE
- Utatimiza Ndoto Yako Kama Utafanya Hivi
Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.
Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.
SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea
Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com