-
Mtag ambaye ungependa ujumbe huu umfikie

Kwenye vipindi mbalimbali vya redio huwa kuna kipindi cha kutuma salamu na ujumbe.
Kama kuna mtu ambaye leo hii ungependa ujumbe huu umfikie mtag hapa ili aje auone.
UWE NA SIKU NJEMA
-
Hiki Ndiyo Kiwango cha mafanikio ambayo unapaswa kuyapigania

/
Rafiki yangu aliwahi kuniambia kwamba kuna wakati aliangalia tamthiliya. Kwenye tamthilya hii kuna jamaa aliachwa na mke wake. Mke alimwacha kwa sababu jamaa hakuwa na hela.
Badala ya kukimbilia kuingia kwenye mahusiano mengine ili amuoneshe ex wake kwamba hajamkomoa kwa kuachwa. Jamaa aliamua kuanza kupambana ili kujenga biashara na kuzisaka hela.
Akapambana kwelikweli kiasi kwamba ikafikia hatu aambapo ex wake alikuwa ni shabiki wake kwenye vitu alivyokuwaanafanya.
Na siyo tu ex wake bali ex wake na mme wake wote kwa pamoja walianza kumshabikia jamaa.
Hiki ni kiwango cha mafanikio ambayo unapaswa kukipigani hasa unapoachwa kwa sababu huna hela. Badala ya kukimbili kufanya yale ambayo siyo ya muhimu. amua kwamba unaenda kuwekeza nguvu zako zote kwenye kutafuta pesa.
Badalaya kutafuta mchumba mwingine ili utambe kwa ex wako kuwa amekuacha kwa bahati mbaya, amua kwamba unaenda kuwekeza muda wako na nguvu zako kwenye kipaji, kujenga ujuzi au kitu ambacho kitakufanya kuwa mtu wa pekee.
Amua kuachana na kitu kingine chochote ambacho kitakuwa kinyume na hapo.
Ni kwa namna hiyo utaweza kujiondoa kwenye hali ya kuwa unaachwa kila wakati kwa ajili ya pesa rafiki yangu. Pambania malengo na ndoto zako kubwa kuanzia sasa.
Nakutakia kila la kheri.
-
Kitu Hiki Unapaswa Kukibadili Mara Moja

Moja ya siku ambayo watu huwa wanaadhimisha ni siku ya kuzaliwa. Ukiachana na sikukuu ya kuzaliwa kuna sikukuu maarufu sana ambazo huwa tunaadhimisha, ikiwa ni pamoja na Eid, Pasaka, Krismasi, Mwaka mpya na nyingine..
Ukiziangalia hizi sikukuu zote zina kitu kimoja ambacho kinaziunganisha. Hizi sikukuu zote huwa zinatokea kwa sababu ya kalenda. Ni sikukuu za kikalenda.
Hii nbdiyo kusema kwamba furaha yote ambayo huwa unakuwa nayo siku ya sikukuu hizi inatokana na kalenda. wewe hakuna juhudi zozote ambazo unaweka kuhakikisha sikukuu hizi zinatokea.
Utake usitake lazima tu sikukuu hizi zitakuwepo.
Hivyo, kufurahia kwenye sikukuu hizi ni jambo zuri lakini usisahau kuwa kitu unachoshangilia kwamba kimetokea hujakisababisha wewe.
Ninachotaka uanze kufanyia kazi baada ya hapa ni wewe kuhakikisha unaanza kupambania malengo yako makubwa. Mwaka huu usiishie tu kushereheakea sikukuu ya kuzaliwa na sikukuu nyingine ambazo ziko nje ya uwezo wako. Yaani, sikukuu ambazo hujazisababisha wewe kutokea., Bali sambamba na mafanikio mengine ambayo utasherehekee mwaka huu basi uweze kusherehekea na mafaniko ambayo umeweza kusababisha mwenyewe.
Kuna kitu kimoja ambacho kama utakipambania unaweza kukileta kwenye uhalisia. Ni kitu gani hicho kimoja? hiki ndicho kitu pekee ambacho unapaswa kukipambania usiku na mchana na bila kukwama wala kuyumbishwa na mtu yeyote.
Kama utaanza kupambania malengo na ndoto zako leo, nakuhakikishia kuwa wanaoonak kama huwezi kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa, kuna siku hawahawa watakuwa wanakushangilia kuwa umeweza kuzifanyia kazi ndoto zako mpaka zikaja kwenye uhalisia.
-
Anza na kile ulichonacho

Tuanze na kile tulichonacho. Tufanye kinachowezekana sasa hivi kabla ya kuja kufanya yasiyowezekana.
Rafiki yangu mpendwa salaam, umekuwa unajiuliza ni kwa namna gani unaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako. Njia bora ya wewe kufanya makibwa ni kwa wewe kuanza na yale ambayo unaweza sas hivi. Kufanya kinachowezekana sasa hivi kabla ya kuja kufanya yasiyowezekana. Wengi wanafikiri kufanya makubwa kabla hawajaanza kufanya madogo ambayo wanaweza sasa hivi. Ukweli ni kuwa, unaweza kufanya makubwa, ila tu unapaswa kuanza na madogo kwanza, kabla ya kuja kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Anza leo hii kwa kufanya madogo ambayo unaweza sasa hivi, kisha baadaye nakuhakikishia kuwa utaweza kufanya makubwa.
-
Watu 60 Walioshindwa Karibia Kwenye Kila Kitu Na Bado Wakashinda Kwa Kishindo
Watu 60 Walioshindwa Karibia Kwenye Kila Kitu Na Bado Wakashinda Kwa Kishindo
Katika maisha, kila mmoja wetu anakutana na changamoto, vikwazo, na kushindwa mara kwa mara. Lakini je, unajua kuwa watu wengi maarufu na wenye mafanikio makubwa walipitia hali ngumu zaidi, kushindwa tena na kabla ya kufanikiwa kwa kishindo? Kitabu hiki “Watu 60 Walioshindwa Karibia Kwenye Kila Kitu Na Bado Wakashinda Kwa Kishindo” kinaleta hadithi za kusisimua na zenye msukumo wa watu ambao walishindwa katika nyanja nyingi, lakini hawakukata tamaa, na hatimaye walifikia mafanikio makubwa.
Kwa Nini Usome Kitabu Hiki?
Kitabu hiki kinakufundisha kwamba kushindwa si mwisho wa safari yako ya maisha. Hivi ni vikwazo vya muda tu ambavyo vinaweza kukupa funzo kubwa na kukuandaa kwa mafanikio makubwa zaidi. Kupitia hadithi za watu kama Nelson Mandela, Abraham Lincoln, Richard Branson, Vera Rubin, Eminem, Jay-Z na wengine wengi, utapata nguvu ya kuendelea mbele licha ya changamoto na kushindwa unazokutana nazo.
Hakikisha unapata nakala yako leo
Kitabu hiki kina hadithi ambazo zitakuhamasisha kuchukua hatua leo. Hakuna wakati bora wa kujifunza kutoka kwa mafanikio ya wengine kuliko sasa. Unapopata hadithi hizi, utagundua kwamba kushindwa si jambo la ajabu, bali ni sehemu ya safari ya kila mtu anayetaka kufanikiwa. Jifunze kutoka kwa waliopitia hali kama zako na wakapita upande wa pili wakiwa washindi.
Bei Nafuu ya Softcopy: Tsh 10,000/-
Kwa bei ya kipekee ya Tsh 10,000 tu, unaweza kupata nakala ya softcopy ya kitabu hiki. Ni fursa adimu ya kupata maarifa haya ya thamani kwa gharama nafuu sana! Hii ni zawadi ya kipekee kwako au kwa mtu unayempenda ili kupata msukumo wa kubadilisha maisha.
Jinsi ya Kupata Kitabu Hiki
Kitabu hiki kinapatikana kwa shilingi elfu kumi tu. Tuma malipo ya Tsh 10,000 kupitia namba 0684 408 755 kwa jina GODIUS RWEYONGEZA, kisha utapokea nakala yako ya kitabu kwenye email au whatsap yako. Hakikisha unapata kitabu hiki leo na uanze safari yako ya kufanikiwa!
Usisubiri Kesho, Chukua Hatua Leo!
Kushindwa si mwisho, ni sehemu tu ya safari yako. Chukua hatua leo, nunua kitabu hiki na uanze kujiandaa kwa mafanikio makubwa. Muda wa kubadilisha maisha yako ni sasa!
Kummbuka, kama utalipia leo, utapewa bure kitabu cha NYUMA YA USHINDI: KUNA KUSHINDWA, KUSHINDWA, KUSHINDWA.
Chukua hatua sasa.
-
Penye Changamoto Pana Fursa.

Ndiyo maana tunapaswa kupambana. Maisha muda mwingine yanabadilila kwa sababu Kuna changamoto, Bila ya hizi changamoto mambo MAKUBWA tunayoona Leo tusingekuwa tunayaona.
Leo ngoja nikupe Mifano ya vitu vilivyogunduliwa baada ya kuwepo kwa changamoto
1. Penicillin: Alexander Fleming aligundua penicillin, dawa ya kwanza ya antibiotic, baada ya kukutana na changamoto ya kutafuta njia ya kuzuia bakteria hatari. Ugunduzi huu umeokoa maisha ya mamilioni ya watu.
2. Internet: Mtandao wa internet ulitokana na changamoto ya mawasiliano ya haraka na rahisi kati ya wanasayansi na watafiti. Changamoto hii iliwahamasisha kuunda mfumo wa mawasiliano wa ARPANET, ambao ulizaa internet tunayojua leo.
3. Airplanes: Ndege zilivumbuliwa baada ya changamoto ya usafiri wa haraka kati ya sehemu tofauti za dunia. Ndugu wawili wanaojulikana kama Wright Brothers, walikabiliana na changamoto ya kuunda chombo kinachoweza kuruka na kudhibitiwa, na hatimaye walifaulu kutengeneza ndege ya kwanza inayofanya kazi.
4. Vaccines: Chanjo nyingi zimegunduliwa kutokana na changamoto ya kuzuia magonjwa hatari kama vile polio, ndui, na surua. Hii imekuwa moja ya njia kuu za kudhibiti na kutokomeza magonjwa mbalimbali duniani.
5. Electric Light Bulb. Thomas Edison alikabiliwa na changamoto ya kuleta mwanga wa kudumu na salama kwa watu baada ya giza kuingia. Hii ilimpelekea kugundua taa ya umeme, ambayo imebadilisha jinsi tunavyoishi na kufanya kazi. Kwa Nini naandika haya yote? Jibu ni Moja tu?
Changamoto, matatzizo, shida za Dunia hazitakaa ziishe. Badala yake Mimi na wewe tunapaswa kuwa na jicho la ujasiriamali mara zote.
Maana penye changamoto Pana fursa. Naomba niweke kituo ili niwahi kazini

-
Maisha ni wajibu wako, ukishinda ni juu yako, ukishindwa ni juu yako pia

Usije ukafanya kosa la kutaka kuwaachia wengine jukumu la maisha yako. Hakuna mtu anayeweza kujali kuhusu maisha yako kama wewe mwenyewe. Wewe ndiye mtu wa kwanza unayepaswa kujali kuhusu maisha yako kabla ya mtu mwingine yeyote.
Na unapaswa kulifanyia kazi kwa uhakika bila ya kurudi nyuma wala kukubali kukwamishwa na mtu au kitu chochote.
Kuwa na ndoto kubwa. Lakini ndoto hizi usiishie tu, kuwa nazo bila kuzifanyia kazi. Ukweli ni kuwa hakuna mjomba, shangazi au mama mdogo ambaye atafanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa ulizonazo. Ni au uzifanyie kazi wewe mwenyewe au la uachane nazo kabisa.
Hilo ni jukumu lako, ndiyo maana nasema kwamba maisha ni wajibu wako, ukishinda ni juu yako mwenyewe na ukishindwa ni juu yako mwenyewe.Kwa kuwa wewe umeamua kubeba jukumu la maisha yako, leo hii. Hakikisha Unasoma kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Kitabu hiki kinakueleza ukweli mmoja tu kuwa, usipofanyia kazi malengo nandoto zako, kuna mtu atakuajiri, kufanyia kazi malengo na ndoto zake.
Umeipata hiyo. Chukua hatua sasa upate nakala yako kwa kuwasiliana na 0655848392 sasa
Nakala moja ni 25,000/- tu.Ijumaa Kareem
-
Kwa Nini KUWEKA akiba ni Muhimu Hata Kama Hujui Lini Utakufa

Vipi usipokufa na huna akiba na ukaishi mpaka miaka 80 au 90?
Ni kweli kwamba kifo ni jambo lisilotarajiwa, lakini pia ni kweli kwamba unaweza kuishi maisha marefu. Bila akiba, maisha hayo marefu yanaweza kuwa magumu na yenye changamoto nyingi za kifedha. Hapa kuna sababu za kwa nini kuweka akiba ni muhimu hata kama hatujui lini tutakufa:
- Usalama wa Baadaye: Ikiwa utaishi kwa muda mrefu, akiba inakusaidia kuhakikisha kuwa una rasilimali za kutosha kuishi maisha ya heshima bila kutegemea wengine kwa msaada wa kifedha. Inaweza kukusaidia kugharamia matibabu, gharama za maisha, na mahitaji mengine ya kimsingi unapokuwa mzee.
- Kujitegemea: Bila akiba, unaweza kujikuta ukitegemea msaada wa kifedha kutoka kwa familia, marafiki, au hata misaada ya kijamii unapokuwa mzee. Kuweka akiba kunakupa uhuru na heshima ya kujitegemea, bila kulazimika kumtegemea mtu mwingine.
- Kutoa Urithi: Akiba inaweza kuwa urithi mzuri kwa watoto wako au wapendwa wako. Hata kama hautaifaidika mwenyewe, unaweza kuwaacha wengine katika nafasi bora ya kifedha kwa sababu ya maamuzi yako ya kuweka akiba.
- Kukabiliana na Matukio Yasiyotarajiwa Maisha yanaweza kuleta changamoto nyingi, kama ugonjwa, kupoteza kazi, au gharama nyingine zisizotarajiwa. Akiba inakupa kinga dhidi ya hali hizi, ikikupa uhakika wa kifedha hata katika nyakati ngumu.
- Kujenga Maisha Bora Kuweka akiba siyo tu kwa ajili ya dharura; pia ni kwa ajili ya kufikia malengo yako ya maisha kama kununua nyumba, kuanzisha biashara, au kuwekeza katika elimu. Haya yote yanahitaji mpango wa kifedha ambao akiba ni sehemu muhimu.
Kuweka akiba ni kama kujenga bima ya maisha yako ya baadaye. Kama utaishi maisha marefu, akiba itakusaidia kuishi kwa heshima na bila wasiwasi. Na hata kama maisha yatakuwa mafupi, akiba yako inaweza kuacha urithi wa maana kwa wale unaowapenda.
NB: Hakikisha Umepata kitabu Cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA.
Kinapatikana kwa 10,000/- tu softcopy
Hardcopy ni 20,000/-. Lipia Sasa kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZADaniel Katunzi Emmanuel Msemakweli Emmanuel Akyoo Edius Katamugora
-
MAMBO MUHIMU KUHUSU KUWEKA AKIBA
Kwenye somo la leo ninakueleza kwa undani mambo ya msingi na ya muhimu sana ambayo unahitaji kuzingatia linapokuja suala zima la kuweka akiba.
Kuna makosa ambayo umekuwa unayafanya, lakini habari njema ni kwamba haya makosa unaweza kuyaepuka.
Haya yote yameelzwa kwa kina kwenye somo la leo. Hakikisha umelfuatilia somo hilimpaka mwisho.
Kujipatia nakala za vitabu ambavyo nimezungumzia kwenye somo la leo, basi wasiliana nami kwa namba ya simu 0755 848 391 sasa
-
Kitu Aambacho Kimekuwa Kikikwamisha Watu Wengi. Kinakukwamisha Na WEWE pia?

Kama kuna mtu ambaye unaona kwamba ameweza kufikia mafanikio makubwa, basi ujue kwamba kuna gharama ambazo ameliipa na wewe hujalipa hizo gharama, unapaswa kuwa tayari kulipa gharama ambazo mtu huyu amelipa ili uweze kufikia kwenye ngazi ambazo yeye amefikia.
Kama unataka kujenga biashara kubwa ambayo itakufikisha kwenye ngazi ya ubilionea unapaswa kuwa tayari kulipa gharama ambayo itakufikisha kwenye hicho unachotaka kufanya.
Upo tayari kulipa gharama. Kama haupo tayari kulipa gharamam usitegemee kupata matokeo makubwa.
Wahenga wanasema kwamba ukitaka cha uvunguni ni sharti ukubali kuinama kwanza.
Hii ndiyo kusema kwamba ukitaka kula vinono, unapaswa kuwa tayari kuumia kidogo. Unapaswa kuwa tayari kulipa gharama ya kupata hivyo vinono ndiyo uje kuvipata.
Nakutakia siku njema rafiki yangu.
Kwenye kitabu cha JINSI YA KUFIKIAI NDOTO ZAKO; Nimeeleza gharama tano ambazo unapaswa kulipa. Na gharama hizi ni….au basi, pata nakala ya kitabu hiki ili uweze kusoma na kuzijua gharama hizi. Kupata nakala yako, tuwasiliane kwa 0684408755 sasa ili uweze kujipatia nakala yako.
