-
Shhh! Sikiliza Vizuri; pesa ya akiba siyo pesa ya kula

Ukikosa pesa ya kula, pambana kadiri unavyoweza kuhakikisha kwamba unaipata sehemu nyingine ila siyo kwenye akiba Yako
Akiba iwekwe kwa lengo maalum. Ni muhimu zaidi kama akiba itawekwa sehemu ambayo huwezi kufikia kwa haraka.
Hii itakusaidia kutokuwa unaifikiria mara kwa mara, kitu kitakachokupelekea wewe kuitoa.
Kama Bado hujajipatia nakala ya kitabu Cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA pamoja na kitabu NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.
Muda wa wewe kuhakikisha unafanya hivyo ni Sasa.
Pata nakala Yako Leo. Tumia namba ya simu 0684408755 karibu sana.
-
Kuandika kunahitaji Nidhamu. Unakuwa na vitu Gani vingi vinavyokufanya usiandike?
Unakuwa na vitu Gani vingi vinavyokunya ukose hata dakika 15 za Kuandika kila siku?
Kuandika kunahitaji nidhamu. Kama ambavyo kusoma darasani kunahitaji nidhamu ili ufaulu, Kuandika pia kunahitaji nidhamu. Nidhamu ya Kuandika. Ukiona mtu ameandika na kitabu chake kimekamilika, ujue Moja ya gharama aliyoilipa ni nidhamu ya kukaa chini na Kuandika.
Kuandika hata pale alipokuwa hajisikii Kuandika.
Kuandika hata pale alipoona kama vile kaishiwa na mawazo ya Kuandika.
Kuandika hata pale alipokuwa amezungukwa na vishawishi vingi vya kumfanya asiandike.Unapaswa kuwa na hii nidhamu, la sivyo unaweza kukuchukua Miaka mingi unaendelea tu kutamani Kuandika ila hujawahi Kuandika.
Siku ya leo, sahau yote, Tenga dakika 15 tu. Kaa chini andika
Ukikwama uliza. Nitakusaidia.
Kila la kheri
-
Vitu Vinavyofanya Wengi Washindwe Kufikia Malengo Na Ndoto Zao

Kwanza ni kuiga watu wengine. Mwandishi wa vitabu John Mason, anasema kwamba imitation is limitatiom, akimaanisha kwamba kuiga ni kikwazo kikubwa sana ambacho kinawazuia watu wengi kuweza kufanyia kazi malengo na ndoto zao na hata kuweza kuzifikia. Ukweli ni kuwa, kama una malengo na ndoto kubwa, kamwe usiige wengine wanafanyaje. Badala yake amua kufanya vitu kwa staili yako mwenyewe.
Kuiga wengine ni kuamua kujiibia uwezomkubwa uliolala ndani yako.
Pili ni ni kukosa vipaumbele.
Unapokosa vipaumbele hata kama una majukumumengi unaweza kujikukuta kwamba hufanyii chochote. Kwa nini?
Kwa sababu huna vipaumbele. Muda ambao unatakiwa kuwa unafanya kazi, unaingia instagram kuchati na huoni shida kwa sababu huna kipaumbele.
Muda ambao unapaswa kuwa unafanya kazi, anakuja mtu anakwambia kwamba mwende kuangalia mpira, kwa sababu huna vipaumbele, kwa muda huo kwako hicho ndiyo kinakuwa kipaumbele chako! Kwa hiyo mwisho wa siku unaweza kujikuta unaimaliza siku yako ukiwa umechoka. Lakini ni kitu gani cha maana ambacho umeweza kufanya ndani ya siku yako, kikiangaliwa kitu hicho, bado huwezi kukiona vizuri kwa sababu tu HUNA VIPAUMBELE
Sikiliza maisha bila vipaumbele, siyo maisha ambayo unapasawa kuwa unaishi wewe.
Na vipaumbele vyako vinapaswa kuanzia kwenye ndoto zako. Unazijua ndoto zako?
Inashauriwa asilimia 80 ya muda wako uutumie kwenye kufanyia kazi malengo na ndoto zako.
Kama umeajiriwa zaidi ya asilimia 80 ya muda wako unapaswa kuitumia kwenye kufanya kazi za ofisi.
Kama umejiajiri zaidi ya asilimia 80 ya muda wako unapaswa kuutumia kwenye biashara yako.
Yaani, kufanya kazi kunapaswa kuchukua sehemu kubwa ya muda wako kuliko kitu kingine chochote.
Kama kuna wakati utajikuta umekosa kipaumbele. Jiulize ni kitu gani nafanya sasa hivi kuelekea malengo yangu makubwa?
Kama hakuna kitu unafanya, basi huo utakuwa muda mzuri wa wewe kuhakikisha kwamba unafanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa zilizo mbele yako.
Imeandikwa na Godius Rweyongeza
Kupta vitabu vya Godius Rweyongeza wasiliana naye kwa 0684408755 sasa
-
Ufanye nini Unapojihisi kama kukata tamaa kwenye kuandika

Kama unahisi kama kukata tamaa kwenye kuandika kitabu chako, basi kitu kikubwa sana ambacho unatakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba unakaa chini na kujiuliza kwa nini ulianza kuandika kitabu hiki?
Ni manufaa gani ambayo watu watapata kutokana na kusoma kitabu chako?
Ni hasara gani ambazo watu watapata kwa kusoma kitabu chako?
Je, unakubali kweli kwamba usiache urithi kudumu kupitia maandishi kwa siku nyingi zinazokuja.
Hayo ni mswasli ya muhimu sana ambayo unapaswa kujiuliza, kama kweli umedhamiria kuandika kitabu chako na unaona kwmaba unakata tamaa?
-
Vitu vidogo ambavyo watu wanapuuza, ila vinawanyima mafanikio makubwa

Rafiki yangu wa ukweli, salaam. Hongera sana kwa siku hii nyingine ya kipekee sana. Leo ikiwa ni tarehe 30/7/2024, ni siku nyingine ambayo unapaswa kwenda kupambana.
Siku ya leo, nimeona nikwambie vitu vidogo ambavyo watu wanapuuza, ila mwisho wa siku vinakuwa na madhara makubwa.Ndiyo, ni vitu vidogo, lakini ukivipuuza, madhara yake yanakuwa ni makubwa sana.
Kitu cha kwanza ni muda. Sote tayari tunajua umuhimu wa muda kwenye maisha ya kila siku. Lakini ni wachache sana ambao huwa wanaheshimu muda. Muda ni rasilimali ambayo ukiipoteza hutaipata tena.
Kitu cha pili. Ni kutokuwa na msimamo kwenye vitu wanavyofanya. Kukosa msimamo kwenye kazi unazofanya, au kufanya leo na kesho ukaacha, kitu hiki kinapelekea wewe kukosa mwendelezo kwenye kile unachofanya.
Tatu ni kutaka mafanikio ya haraka, hiki ni kitu kingine ambacho kinawaangusha wengi. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unakuwa kwenye mchakato kwa muda mrefu. Ukikaa kwenye mchakato, bila kuhitaji kupata mafanikio ya haraka, basi hili litakusaidia wewe kuweza kufika mbali.
Nakutakia kila la kheri.
Karibu sana
-
Njia Rahisi Ya kuandika Kitabu Hata Kama Uko Bize
Habari rafiki yangu,
Watu wengi wana malengo ya kuandika vitabu lakini hukosa muda wa kuandika kutokana na majukumu mengi yanayowabana. Mara nyingi wanapanga kuandika jioni baada ya kazi, lakini wanajikuta wamechoka na hawawezi kuandika tena.
Je, kuna njia rahisi ya kuandika hata kama uko bize? Ukweli ni kuwa njia hiyo ipo. Amka asubuhi na mapema, kabla ya kuanza majukumu yako ya siku, na utapata muda wa kutosha wa kuandika bila usumbufu. Muda wa asubuhi ni mzuri kwani akili yako ni freshi, hakuna kelele nyingi, na familia haijakuanza kuhitaji.
Ukikosa muda asubuhi, ni nadra sana kuja kuandika jioni kwa sababu akili itakuwa imechoka, kelele za familia na mazingira, changamoto za siku nzima, na mambo mengine kama kutazama filamu. Muunganiko wa haya yote hukufanya usiweze kuandika vizuri jioni.
Kwa hivyo, muda bora kabisa wa kuandika ni asubuhi na mapema. Ukiweza kutenga dakika chache tu asubuhi na mapema kwa ajili ya kuandika, baada ya muda utakuwa umeweza kuandika kitabu kikubwa kabisa.
Je, ungependa kuandika kitabu chako na kuwa mbobevu kwenye uandishi? Basi sikiliza vizuri. Anza kwa kujipatia nakala ya kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. Kitabu hiki kimeeleza kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi wa vitabu.
Kupata nakala ya kitabu hiki, wasiliana nami sasa kwa kutumia namba ya simu 0684 408 755.
Natumai mabadiliko haya yataboresha ujumbe wako. Je, kuna jambo lolote ungetaka kuongeza au kubadili?
-
Kanuni Ya Imani Ya PESA
Ni kutafufa PESA ili ifike hatua hata kama watu hawakuheshimu basi waheshimu PESA zako.
PESA ni kitu ambacho unapaswa kukipambania kila kukicha, asubuhi mchana na jioni.
Zipende PESA kwa sababu bila ya kuzipenda hazitakupenda.
Maana fedha Ina tabia ya kwenda kwa watu wanaoipenda. Kwa hiyo kuanzia leo, ipende fedha nayo itakupenda.
-
Hiki Kitu Ambacho Kinaua Ndoto Zako Kwa Ukubwa

Nitaifanya kesho anajua ndoto za watu wengi. Ukweli ni kuwa huwezi kuendelea kusema kwamba nitaifanya kesho badala ya kuchukua hatua na kufanya kitu Leo.
Muda mzuri wa kufanya jambo lako na kulifanikisha ni Leo.
Chukua hatua Sasa.
Utajishukuru kesho kuwa Leo uliweza kuchukua hatua kuliko ambavyo utajilaumu.
Uwe na siku njema
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro; Mafiga Tenki Bovu
-
Kitu Muhimu Ambacho Kila mwandishi anapaswa kuwa anafanya

moja ya kazi muhimu sana ambayo kama mwandishi unapaswa kuhakikisha kwamba umeifanya ni kuandika.
hauwi mwandishi kwa kujiita tu mwandishi, bali unakuwa mwandishi kwa kuandika. Mwandishi anaandika.
Hivyo wito wangu mkubwa kwako wewe mwandishi ni kwamba ukae chini na uandike kitabu chako au makala ambayo unafikiria kuandika bila ya kurudi nyuma.
Naomba unisikilize vizuri.
Kwa kawaida
Daktari anatibu
Mwalimu anafundisha
Mwandishi pia anapaswa kuandikakaa chini na uandike kitabu chako kuanzia leo.
Kupata mwongozo wenye hatua kwa hatua kuhusu uandishi wa vitabu, tuwasiliane kwa namba ya simu 0755848391
tuwasiliane sasa uweze kupata mwongozo huu
-
Unahitaji kuwa mtu wa pekee ili kuandika kitabu?
Watu wengi huwa wakifikiria kuhusu kuandika kitabu, basi kitu cha kwanza ambacho huwa kinakuja kwenye akili yao ni kwamba unapaswa kuwa mtu wa pekee kabisa.
Nakubaliana na watu hawa kwamba ili kuandika kitabu chako unapaswa kuwa wa pekee. Na upekee mkubwa ambao unauhitaji wewe ili kuandika kitabu chako na kukikamilisha ni NIDHAMU YA KUKAA CHINI NA KUANDIKA.
Ukweli ni kuwa bila ya kuwa na nidhamu hii, hata kama utautaka uandishi kiasi gani, huu uandishi hautakuja kwenye uhalisia, hata kama utakuw ana wazo zuri kiasi gani la kuandika. Wazo hili halitakuja kwenye uhalisia kwa sababu hujakaa chini na kuandika. Hivyo, kama unataka unataka kuandika vitabu KAA CHINI ANDIKA.
Hiki ni kitu pekee unachohitaji.