Home


  • Kama unaandika kitabu chako Kwa ajili ya faida za kiuchumi TU. Nina Habari Njema Na Mbaya Kwa ajili kwako

    Siku za nyuma nimewahi kuandika nakala inayoeleza sababu 18 Kwa Nini tunaandika vitabu na Kwa Nini wewe unapaswa kuandika Cha kwako.

    Unaweza kupata na KUSOMA makala hii hapa

    Au unaweza kuisikiliza pia Kwa sauti hapa

    Sasa mbali na hizo sababu hapo juu. Kuna ndugu anataka kujua sababu za kiuchumi TU ambazo ndizo ziwe chachu ya kumsukuma kuandika.

    Mara Kwa mara nimekuwa nikiwaambia watu kuwa kama sababu pekee ya wewe kuandika Kitabu Chako ni PESA. Bora usiandike kitabu chako

    Kwa sababu utakata Tamaa. Na hiki kitu kimewatokea waandishi Wengi sana.

    Unakuta mtu anaandika kitabu, lakini kuuza hata nakala 50 TU ni changamoto.

    Kwa nini
    Naomba unisikilize vizuri Sasa
    Kwa sababu usomaji wa vitabu nchini Tanzania Bado upo chini ukilinganisha na nchi nyingine na hasa nchi za Ulaya. Kwa hiyo, kuuza vitabu kunahitaji usiwe TU mtu ambaye anataka PESA pekee Bali mtu ambaye upo tayari kuona watu wanapata mabadiliko kupitia maandishi Yako.

    Kutakuhitaji kujitoa.
    Kutoa elimu Kwa watu.

    Hivyo Unapoandika Kitabu unapaswa kuwa na msukumo zaidi ya kutengeneza Fedha. Na hasa msukumo wa kuwasaidia watu waweze kuboresha maisha Yao.

    Hili kitakupa NGUVU zaidi na hata ikitokea mauzo ya vitabu hayaendi vizuri Bado utakuwa una msukumo mkubwa Kwa sababu unajua ujumbe wako ulio kitabu ni, ukileta matokeo chanya Kwa mtu mmoja, unakuwa umeweza kufanya mchango mkubwa Kwa jamii.

    Ni Nini msukumo wako wa kuandika Kitabu?

    Karibu SONGAMBELE CONSULTANTS

    ✅ Tunakuandikia kitabu chako (ghostwriting) 
    ✅ Tunatoa mwongozo wa kuandika kitabu chako 
    ✅ Kuhariri vitabu 
    ✅ Tunatoa usimamizi wa karibu kwenye uandishi wa kitabu chako 
    ✅ Tuna vitabu bora vyenye hatua muhimu za kufuata katika uandishi 
    ✅Na hata kuchapa kitabu chako

    Mawasiliano:
    Simu/WhatsApp: +255755848391
    Email: jifunzeuandishi@gmail.com 

    Eneo: Morogoro mjini; Mafiga, Tenki Bovu

    Telegram: https://t.me/jifunzeuandishi

  • Kama una changamoto ya kuandika Kitabu Chako Na Kufuta, Kuna Kitu Hiki Hapa Unapaswa KUZINGATIA

    Unaandika unafuta Nini?

    Andika kwanza kitabu chako chote bila kufuta.Utafuta wakati unahariri.

    Kupata msaada wa kuandikiwa

    Karibu SONGAMBELE CONSULTANTS

    ✅ Tunakuandikia kitabu chako (ghostwriting) 

    ✅ Tunatoa mwongozo wa kuandika kitabu chako 

    ✅ Kuhariri vitabu 

    ✅ Tunatoa usimamizi wa karibu kwenye uandishi wa kitabu chako 

    ✅ Tuna vitabu bora vyenye hatua muhimu za kufuata katika uandishi 

    Mawasiliano:Simu/WhatsApp: +255 684 408 755  au +255 655 848 392 au +255 678 848 396Email: jifunzeuandishi@gmail.com 

    Eneo: Mafiga, Tenki Bovu

  • Kama Unataka Kuandika Kitabu Njoo Nikusaidie Kufanikisha Haya Haraka

    Wewe niletee kitabu chako TU, nami nitakusaidia

    1. Aidha kukiandika
    2. Kukupa mwongozo wa namna ya kukiandika vizuri na Kwa weredi.
    3. Kukihariri
    4. Kukichapa n.k

    Kwa masuala yote yanayohusiana na uandishi wa vitabu. Nicheki Sasa Kwa namba ya simu 0755848391 Ili tumalize mchezo.

  • Ushawahi kuona kitabu, halafu ukasema na Mimi ningeweza kuandika hicho?

    Ushawahi kuona kitabu, halafu ukasema na Mimi ningeweza kuandika hicho?

    Suala kubwa kubwa siyo kwamba na wewe unaweza kuandika hicho .

    Suala kubwa hapa ni kwamba unajua na HUANDIKI.

    Unadhani Kuna watu wangapi wanajua vitu na hawafanyi?

    Kuna wanaohua kuwa ulevi ni NOMA, ila Bado wanalewa TU. Wengine uvitajiq wa sigara ni mbaya Kwa afya, ila Bado wanavuta TU.

    Kumbe kujua kwamba unaweza kuandika Kitabu Fulani bila kukiandika, hakusaidii chochote.

    Kikubwa JUA-Fanyia kazi-SONGAMBELE

    Kama umenielewa umenielewa tu

  • Kiashiria Kwamba Umeshindwa Kuandika Kitabu Chako

    Rafiki yangu mpendwa, kitabu ambacho hujachukua hatua ya kukiandika kinakushinda.

    Ni mpaka pale utakapokuwa umeamua kuchukua HATUA na kuandika Kitabu Chako ndiyo kitabu chako kitafanikiwa

    HATUA za kuchukua Leo.
    1. Jua wazo lako ni lipi hasa kwenye kuandika Kitabu Chako.

    2. Anza kukiandika Kitabu Chako

    3. Jiunge na kundi letu la telegram hapa
    https://t.me/jifunzeuandishi

    Godius Rweyongeza
    0755 848 391

  • Kitabu kitakachokusaidia Kuandika Kitabu

    Siku ya Leo hakikisha unapata kitabu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU MBOBEVU.

    Kitakusaidia sana kuandika Kitabu Chako Kwa miezi sita hii ijayo. Safari ndiyo kwanza imeanza.
    Piga 0655 848 392 kupata nakala Yako.

  • Sikiliza, USIKATE TAMAA kwenye kuandika Kitabu Chako

    Kuanzia Leo tuna miezi sita Kamili. Isiyo na chenga KABLA ya mwaka huu kuisha.  

    Kama upo siriazi ndani ya hii miezi sita hutashindwa kuandika kitabu chako. Nakuhakikishia. 

    Unaweza kujiuliza kivipi? Beep 0755 848 391 nikupigie tuongee Ili uweke plan Yako vizuri ya kuandika.

  • Weka lengo la kuandika kitabu

    https://t.me/jifunzeuandishi

    Weka lengo la kuandika Kila siku, hata kama ni kurasa mbili au hata Aya moja au sentensi moja tu. Kikubwa uwe kwenye mwendo muda

    wote.www.songambele.co.tz

    Telegram: https://t.me/jifunzeuandishi

  • jukumu la kufanikisha Malengo Yako ni kwako

    Nakukumbusha tu kuwa jukumu la kufanikisha Malengo Yako ni kwako siku zote. 

    Wala siyo la 

    Mjomba

    Shangazi au mtu mwingine awaye yeyote.

    Ukishindwa ni juu yako, ukishinda pia ni juu yako.

  • Upo tayari kubadili mtazamo wako?

    Upo tayari kubadili mtazamo wako?



    Mtazamo wako ni mmoja ya kitu MUHIMU unachopaswa kubadili. Usispobadili mtazamo wako, hutabadili MAISHA Yako

    1. Badili mtazamo wako kwenye jukumu la MAISHA Yako.

    Fahamu wazi kuwa MAISHA ni Wajibu wako, ukishindwa ni juu Yako, ukishinda ni juu Yako.

    Usisubiri watu wengine watimize Wajibu ambao unakuhusu wewe 

    2. Badili mtazamo wako kwa kufanyia kazi Yale ambayo wewe umekuwa unapanga kufanya kazi, badala tu ya kukaa ukitakani kufanyia kazi vitu Fulani, ingia ulingoni kabisa na ufanyie kazi Yale ambayo unapaswa kuyafanyia kazi.

    3. Badili mtazamo wa kuanza kuweka akiba na KUWEKEZA. Kiasi unachoweka kama AKIBA Leo, hata kama ni kidogo, kitakupeleka oakubwa hapo baadaye. 

    4. Badili mtazamo wako kwa kuanza kujifunza kwa watu waliojenga utajiri. Ni kwa namna hiyo, utaweza kujenga utajiri pia.

    Salaam, 

X