Home


  • NAMNA YA KUKUZA BIASHARA YAKO

    NAMNA YA KUKUZA BIASHARA YAKO
    -kitu kimojawapo kinachoweza kukusaidia KUKUZA BIASHARA YAKO kwa haraka zaidi

    *Watu wengi wamedumaa kwenye biashara kwa kuangalia lengo Moja tu la mauzo.Hatakama utafanya mauzo sana utajikuta unaanza kupoteza

    1) HUMAN RESOURCES
    -Biashara pamoja na BIDHAA na HUDUMA unayotoa kitu Cha MUHIMU pia katika biashara ni watu na ni MUHIMU sana kuchagua watu sahihi katika biashara
    Watu wanaweza kuharibu JINA la biashara na ubora wa BIDHAA

    👉.Hata wewe Kuna sehemu unaweza ukaenda sio sababu ya HUDUMA unayoipata pale sana ni sababu ya mtu ambae anatoa hiyo HUDUMA mahali pale.

    👉Kwa hivyo ni MUHIMU sana kuchagua watu sahihi wa kufanya kitu ambacho unataka kukifanya kama biashara
    -Ni Bora utumie gharama nzuri na kubwa kupata mtu sahihi kwenye kufanya biashara yako kuliko KUTAFUTA cheap labour ambae ataharibu biashara na pengine ataharibu uhusiano ulionao na wateja.

    Makala hii imeandaliwa nami,
    Faith Mark Mrema
    0742 825 286
    Morogoro_Tanzania

  • Ukiandika Kitabu hata baada ya kuaga Dunia unaendelea kuishi kupitia kitabu chako

    Unaweza kuaga Dunia kimwili, ila ukaendelea kuishi kupitia kitabu chako. Kama hujaandika kitabu chako, Fanya hivyo Leo.

    Hakikisha umepata kitabu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU Leo.

    Kupata nakala, nicheki Kwa 0684 408 755

    Wasap: 0745 848 395

  • MAMBO 6 YA KUACHA ILI UFANIKIWE

    MAMBO 6 YA KUACHA ILI UFANIKIWE
    Ili uweze kufikia Malengo na MAFANIKIO unayotaka lazima ukubali kuacha baadhi ya mambo
    🤷MAFANIKIO kwako yanaweza kuwa na maana tofauti ,Kila mmoja wetu na wengi wetu hutafsiri MAFANIKIO ni kama Pesa,umaarufu,majumba,magari,.Wengine hutafsiri kama MAFANIKIO kwako ni furaha,Amani,uhuru,inategemea ni JINSI Gani unaweza kutafsiri MAFANIKIO kwako wewe mwenyewe

    👉Ukijua maana ya MAFANIKIO kwako basi ni MUHIMU sana kujua mambo ambayo yanaweza kukuzuia wewe KUFIKIA MAFANIKIO katika MAISHA
    👇👇
    1)ACHA KUTAFUTA NJIA FUPI ILI KUFANIKIWA
    -Itakuwa mbaya sana kama utafanya hivyo MAFANIKIO ya kweli katika chochote unachotaka utafanikiwa kwa kufanya kazi kwa bidii


    2)ACHA KUWA NA MAWAZO MGANDO
    -Uwezo au ujuzi wa mtu unatakiwa uwe na MAWAZO ya kukua na aina hii ya MAWAZO utafanya kazi kuwa vizuri zaidi na kupata uzoefu zaidi
    3)ACHA KULAUMU WENGINE
    -Utakapofeli katika jambo lako acha KULAUMU wengine siku zote kubaki kuwa wewe mwenyewe ndie unaehusika kwa kiasi kikubwa


    4)ACHA KUSEMA SINA MUDA
    _Anza kuanza kutumia muda wako vizuri na uache kusema huna Muda mwingine wa kufanya jambo la ziada
    Tuna muda wa kiwango sawa kama wengine kwa siku ni kuamua ni njia gani utakavyo tumia Muda wako

    5)ACHA KUTEGEMEA KUPATA ZAIDI BILA YA KUFANYA ZAIDI
    -Unatakiwa kufanya kazi kwa bidii Ili kupata promotion au mshahara mkubwa kazini biashara zilizofanikiwa kupata mapato mengi kwa kutoa THAMANI kwanza kwa WATEJA wao na kupata MAFANIKIO. Acha kusubiri Mpaka mambo yakae sawa ndio uanze kufanya kazi kwa bidii

    6)Acha kusubiri
    -Usikubali uoga wako ukurudishe nyuma chochote ulichokuwa unapanga, unaota,unawaza kama ulipanga kuanzisha biashara chukua hatua hiyo sasa weka uoga pembeni na Anza kufanya kitu

    Makala hii imeandaliwa nami,
    Faith Mark Mrema
    0742 825 286
    Tanzania_Morogoro

  • MAMBO 6 YA KUACHA ILI UFANIKIWE 😊

    MAMBO 6 YA KUACHA ILI UFANIKIWE
    Ili uweze kufikia Malengo na MAFANIKIO unayotaka lazima ukubali kuacha baadhi ya mambo
    …MAFANIKIO kwako yanaweza kuwa na maana tofauti ,Kila mmoja wetu na wengi wetu hutafsiri MAFANIKIO ni kama Pesa,umaarufu,majumba,magari,.Wengine hutafsiri kama MAFANIKIO kwako ni furaha,Amani,uhuru,inategemea ni JINSI Gani unaweza kutafsiri MAFANIKIO kwako wewe mwenyewe

    👉Ukijua maana ya MAFANIKIO kwako basi ni MUHIMU sana kujua mambo ambayo yanaweza kukuzuia wewe KUFIKIA MAFANIKIO katika MAISHA
    👇👇
    1)ACHA KUTAFUTA NJIA FUPI ILI KUFANIKIWA
    -Itakuwa mbaya sana kama utafanya hivyo MAFANIKIO ya kweli katika chochote unachotaka utafanikiwa kwa kufanya kazi kwa bidii


    2)ACHA KUWA NA MAWAZO MGANDO
    -Uwezo au ujuzi wa mtu unatakiwa uwe na MAWAZO ya kukua na aina hii ya MAWAZO utafanya kazi kuwa vizuri zaidi na kupata uzoefu zaidi


    3)ACHA KULAUMU WENGINE
    -Utakapofeli katika jambo lako acha KULAUMU wengine siku zote kubaki kuwa wewe mwenyewe ndie unaehusika kwa kiasi kikubwa


    4)ACHA KUSEMA SINA MUDA
    _Anza kuanza kutumia muda wako vizuri na uache kusema huna Muda mwingine wa kufanya jambo la ziada
    Tuna muda wa kiwango sawa kama wengine kwa siku ni kuamua ni njia gani utakavyo tumia Muda wako

    5)ACHA KUTEGEMEA KUPATA ZAIDI BILA YA KUFANYA ZAIDI
    -Unatakiwa kufanya kazi kwa bidii Ili kupata promotion au mshahara mkubwa kazini biashara zilizofanikiwa kupata mapato mengi kwa kutoa THAMANI kwanza kwa WATEJA wao na kupata MAFANIKIO. Acha kusubiri Mpaka mambo yakae sawa ndio uanze kufanya kazi kwa bidii

    6)Acha kusubiri
    -Usikubali uoga wako ukurudishe nyuma chochote ulichokuwa unapanga, unaota,unawaza kama ulipanga kuanzisha biashara chukua hatua hiyo sasa weka uoga pembeni na Anza kufanya kitu

    Makala hii imeandaliwa nami,
    Faith Mark Mrema
    0742 825 286
    Tanzania_Morogoro

  • Kitabu Siyo Ubwabwa

    Mwanzoni utatumia gharama kubwa
    . Kuandika
    . Kuhariri
    . Kupata ISBN na Barcode
    . Kuchapa

    Huu ni uwekezaji, Kwa sababu kitabu siyo kama ubwabwa kwamba kikiiva unakula unananawa na kusubiri kuandaa kingine.

    Kitabu kikiiva, kimeiva, watu wanaendelea kula maarifa maisha yote, hata baada ya wewe kufa.

    www.songambele.co.tz

  • Usitafute ukamilifu mwanzoni mwa kuandika Kitabu Chako, tafuta kuanza

    Lakini ninachoandika mbona siyo kizuri, anajiuliza mmoja wa waandishi. Ukweli ni kuwa wewe mwanzoni Anza kuandika TU, andika hata kama mwanzoni huoni huo uzuri. Baadaye utaboresha

  • Usisubiri Uwe na Muvi Kichwani Ili uandike kitabu chako. Una mengi ya kuandika leo

    Anayekwambia kwamba usubiri mpaka uwe na muviq kichwani Ili uandike kitabu chako anakudanganya. Wewe hapo ulipoq na ninavyokuona wewe una mengi ya kuandika

    • elimu Yako
    • uzoefu wako
    • utalaam wako
    • kitu unachopenda kufuatilia
    • changamoto zinazoikumba jamii Yako
    • Kitu unachopenda kufuatilia
    • changamoto zinazoikumba jamii
    • na mengine mengi

    haya yote yanaweza kuwa chanzo Cha wewe kuandika na kukamilisha kitabu chako.

    Kila la kheri

    kupata usimamizi au msaada wa kuandika Kitabu Chako tumia 0678 848 396

  • Aina Tano Za Uwekezaji Ambazo Unaweza Kufanya Leo Hii, Zikakupa Faida Hapa Duniani Na Hata Pale Uakapokuwa Umetangulia Ahera

    Kuna aina za uwekezaji ambazo unaweza kufanya leo hii, zikaweza kukuletea faida ukiwa hapa duniani, hata itakapofika hatua ukatangulia mbele ya haki, bado utakuwa unaengeneza faida hapa duniani. Unajua aina hizi za uwekezaji ni zipi?

     

    Aina ya kwanza ni uwekezaji kwenye hisa

    Kama utachagua aina nzuri ya uwekezaji na ukaufanya kwa msimamo, nakuhakikishia kuwa utatengeneza faida ukiwa hapa duniani, na uaengeneza faida ukiwa ahera. Kiufupi ni kwamba wale watu utakaokuwa umewaacha, wataendelea kupata gawio kwa siku nyingi sana hata baada yaw ewe kuwa umetoka hapa duniani.

    Uwekezaji kwenye hisa ni njia nzuri ya kutengeneza faida ukiwa hapa duniani. Unapowekeza katika hisa za kampuni ambazo zina faida, unaweza kupata gawio la faida na pia thamani ya hisa zako inaweza kuongezeka kwa muda. Hata baada ya wewe kufariki, wale walioachiwa urithi wako wanaweza kuendelea kupata gawio na faida kutokana na uwekezaji huu.

     

     

    Aina ya pili ni uwekezaji kwenye vipande.

    Vipande au mutual funds ni njia nyingine bora ya uwekezaji. Kwa kuwekeza kwenye vipande, unakuwa unachangia kwenye mfuko ambao unawekeza kwenye hisa na dhamana mbalimbali. Hii ni njia nzuri ya kupunguza hatari na kuongeza faida. Faida zinazopatikana zinaweza kuendelea hata baada ya kifo chako, na hivyo kuwanufaisha warithi wako.

    Kama ulivyo uwekezaji kwenye hisa. Uwekezaji kwenye vipande na hasa utt amis, ni sehemu nzuri sana ambayo itakuwezesha kuengeneza faida hapa duniani. Na haa baada ya  ya wewe kuwa umeaga dunia, wau utakaowaacha hapa duniani, wataendelea kuengeneza faida kwa siku nyingi zitakazofuata.

     

    Aina ya tatu ni uwekezaji kwenye hatifungani.

    Na hasa hatifungani za serikali. UNAJUA KWA NINI? KWA sababu ni ukweli kuwa serikali haiwezi kuffilisika na hata kuacha kuwalipa wananchi wake. Hivyo, ukiwekeza kwenye hatifungani za serikali maana yake utaweza kupata  faida ukiwa bado hapa duniani, lakini habari njema zaidi ni kwamba, kama utaaga dunia, basi uwekezaji wako bado utaendelea kuwanufaisha wale autakaokuwa umewaacha.

    Aina ya nne ni ya uwekezaji ni uandishi wa kitabu. Kitabu ni kitu kingine ambacho kama utakifanya, kitakufanya upate faida hapa duniani, lakini pia hata baada ya kuwa umetoka hapa duniani, bado utaendelea kuengeneza faida zaidi.

    Kuandika na kuchapisha vitabu ni uwekezaji wa kipekee. Vitabu vinaweza kuuza kwa muda mrefu na kuleta mapato kupitia mauzo na mirabaha. Ikiwa kitabu chako kitakuwa maarufu, kitaleta faida kwa muda mrefu, hata baada ya wewe kufariki, na faida hizi zinaweza kuendeleza familia yako au mirathi yako.

     

    Aina ya tano ni uwekekezaji kwenye katika Mali Isiyohamishika

    Kununua ardhi au majengo ni uwekezaji thabiti ambao una faida ya muda mrefu. Thamani ya mali isiyohamishika kawaida huongezeka kwa muda, na unaweza kupata mapato ya kodi kama ukiamua kupangisha. Hata baada ya wewe kuondoka duniani, mali hizi zinaweza kuendelea kuleta faida kwa warithi wako.

    Aina ya sita ni Uwekezaji katika Biashara

    Kuanzisha na kuendesha biashara yenye faida ni njia nzuri ya kutengeneza kipato kikubwa. Biashara inaweza kuendelea kuendeshwa na warithi wako na kuleta faida kwa muda mrefu hata baada ya wewe kufariki. Kumbuka hapa biashara ninayoongelea siyo hizi biashara nyingi ambazo zimekuwa zinafanywa kwa mazoea na watanzania walio wengi. Bali ni biashara ambazo zinajiendesha zenyewe kwa faida kubwa.

    Aina ya saba ni uwekezaji kwenye elimu ya watoto.

    Kwa kuwa watoto wako ndiyo watakuwa wanaendesha hivi vitu na wanapaswa kuendelea kuviendesha kwa siku nyingi zinazokuja, basi unapaswa unapaswa kuwajengea msingi mzuri wa kujifunza  na kuwap elimu sahihi. Ili kazi yako kubwa isiishie tu kwenye kuanzisha hivi vitu, bali watoto wako waweze kuendelea kuendesha hivi vitu kwa siku nyingi zinazokuja.  Hivyo wajengee sehemu sahihi.

     

    Hizi aina za uwekezaji ni uhakika, zitakupa faida ukiwa hapa duniani na hata baada ya kuwa umeaga dunia. Kwa kuchagua uwekezaji mzuri na kwa kufanya maamuzi ya busara, unaweza kuhakikisha kuwa una faida hapa duniani na pia baada ya kuondoka duniani, wale unaowaacha wanaweza kufaidika kwa muda mrefu pia.

    Makala hii imeandikwa n Godius Rweyongeza

    Kujifunza zaidi kuhusiana na aina hizi mada ambazo nimeeleza hapa. Hakikisha unapata nakala mbil za vitabu. Kwanza ni kitabu cha maajabu ya kuwekeza kwenye hisa, hatifungani na vipande pamoja na kitabu cha Jinsi ya kuw amwandishi mbobevu.

    Kupata nakala yako ni rahisi sana. Lipia 25,000 ambayo ni gharama ya kila nakala. Tuma kwa 0684 408 755 ili uweze kutumiwa nakala yako. Baada ya kufanya malipo, tafadhali wasiliana na namba hiyo hiyo kwa ajili kufanya utaratibu wa kutumiwa vitabu vyako.

     

     

  • Gharama ya uandishi wa kitabu ni uwekezaji. Hii hapa ni sababu Kwa Nini?

    Gharama unayotumia mwanzoni kwenye kuandika Kitabu Chako, ni uwekezaji.

    Kitabu kikishakamlika.
    Kitaendelea kuwepo maisha yako yote na hata baada ya wewe kuaga Dunia.

    Uandishi wa kitabu ni kazi unayofanya mara Moja ila unalipwa maisha yako yote.

    Hata baada ya kufa, kitabu kinakutengenezea faida ukiwa duniani na hata ukiwa ahera.

    Godius Rweyongeza 

    +255755848391

  • Muda wa kuandika Kitabu unausubiri utoke wapi?

    Utasikia mtu anakwambia nasubiri siku niwe na muda wa kutosha Ili niandike.

    Sikiliza. Tena sikiliza vizuri. Muda wa kutosha haupo.
    Hakuna mwandishi mwenye muda wa kutosha.
    Kila mwandishi yuko bize.

    Ila muda mchache TU anaopata anaandika. Hata wewe Fanya hivyo.

    Kusubiri muda wa kutosha Ili uandike kitabu chako ni uongo. Hatusubiri tuwe na muda wa kutosha Ili tule, hatusubiri tuwe na muda wa kutosha Ili tuonge. Hata kama tuko bize, tutatafuta muda TU Ili tule na kuoga

    Sasa inakuwaje tunasubiri muda wa kutosha Ili TUANDIKE? Tunasubiri muda huu utoke wapi?

    www.songambele.co.tz

X