Home


  • Ufanye nini Unapojihisi kama kukata tamaa kwenye kuandika

    Kama unahisi kama kukata tamaa kwenye kuandika kitabu chako, basi kitu kikubwa sana ambacho unatakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba unakaa chini na kujiuliza kwa nini ulianza kuandika kitabu hiki?

    Ni manufaa gani ambayo watu watapata kutokana na kusoma kitabu chako?

    Ni hasara gani ambazo watu watapata kwa kusoma kitabu chako?

    Je, unakubali kweli kwamba usiache urithi kudumu kupitia maandishi kwa siku nyingi zinazokuja.

    Hayo ni mswasli ya muhimu sana ambayo unapaswa kujiuliza, kama kweli umedhamiria kuandika kitabu chako na unaona kwmaba unakata tamaa?

  • Vitu vidogo ambavyo watu wanapuuza, ila vinawanyima mafanikio makubwa

    Rafiki yangu wa ukweli, salaam. Hongera sana kwa siku hii nyingine ya kipekee sana. Leo ikiwa ni tarehe 30/7/2024, ni siku nyingine ambayo unapaswa kwenda kupambana.

    Siku ya leo, nimeona nikwambie vitu vidogo ambavyo watu wanapuuza, ila mwisho wa siku vinakuwa na madhara makubwa.Ndiyo, ni vitu vidogo, lakini ukivipuuza, madhara yake yanakuwa ni makubwa sana.

    Kitu cha kwanza ni muda. Sote tayari tunajua umuhimu wa muda kwenye maisha ya kila siku. Lakini ni wachache sana ambao huwa wanaheshimu muda. Muda ni rasilimali ambayo ukiipoteza hutaipata tena.

    Kitu cha pili. Ni kutokuwa na msimamo kwenye vitu wanavyofanya. Kukosa msimamo kwenye kazi unazofanya, au kufanya leo na kesho ukaacha, kitu hiki kinapelekea wewe kukosa mwendelezo kwenye kile unachofanya.

    Tatu ni kutaka mafanikio ya haraka, hiki ni kitu kingine ambacho kinawaangusha wengi. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unakuwa kwenye mchakato kwa muda mrefu. Ukikaa kwenye mchakato, bila kuhitaji kupata mafanikio ya haraka, basi hili litakusaidia wewe kuweza kufika mbali.

    Nakutakia kila la kheri.

    Karibu sana

  • Njia Rahisi Ya kuandika Kitabu Hata Kama Uko Bize

    Habari rafiki yangu,

    Watu wengi wana malengo ya kuandika vitabu lakini hukosa muda wa kuandika kutokana na majukumu mengi yanayowabana. Mara nyingi wanapanga kuandika jioni baada ya kazi, lakini wanajikuta wamechoka na hawawezi kuandika tena.

    Je, kuna njia rahisi ya kuandika hata kama uko bize? Ukweli ni kuwa njia hiyo ipo. Amka asubuhi na mapema, kabla ya kuanza majukumu yako ya siku, na utapata muda wa kutosha wa kuandika bila usumbufu. Muda wa asubuhi ni mzuri kwani akili yako ni freshi, hakuna kelele nyingi, na familia haijakuanza kuhitaji.

    Ukikosa muda asubuhi, ni nadra sana kuja kuandika jioni kwa sababu akili itakuwa imechoka, kelele za familia na mazingira, changamoto za siku nzima, na mambo mengine kama kutazama filamu. Muunganiko wa haya yote hukufanya usiweze kuandika vizuri jioni.

    Kwa hivyo, muda bora kabisa wa kuandika ni asubuhi na mapema. Ukiweza kutenga dakika chache tu asubuhi na mapema kwa ajili ya kuandika, baada ya muda utakuwa umeweza kuandika kitabu kikubwa kabisa.

    Je, ungependa kuandika kitabu chako na kuwa mbobevu kwenye uandishi? Basi sikiliza vizuri. Anza kwa kujipatia nakala ya kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. Kitabu hiki kimeeleza kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi wa vitabu.

    Kupata nakala ya kitabu hiki, wasiliana nami sasa kwa kutumia namba ya simu 0684 408 755.


    Natumai mabadiliko haya yataboresha ujumbe wako. Je, kuna jambo lolote ungetaka kuongeza au kubadili?

  • Kanuni Ya Imani Ya PESA

    Ni kutafufa PESA ili ifike hatua hata kama watu hawakuheshimu basi waheshimu PESA zako.

    PESA ni kitu ambacho unapaswa kukipambania kila kukicha, asubuhi mchana na jioni.

    Zipende PESA kwa sababu bila ya kuzipenda hazitakupenda.

    Maana fedha Ina tabia ya kwenda kwa watu wanaoipenda. Kwa hiyo kuanzia leo, ipende fedha nayo itakupenda.

  • Hiki Kitu Ambacho Kinaua Ndoto Zako Kwa Ukubwa

    Nitaifanya kesho anajua ndoto za watu wengi. Ukweli ni kuwa huwezi kuendelea kusema kwamba nitaifanya kesho badala ya kuchukua hatua na kufanya kitu Leo. 

    Muda mzuri wa kufanya jambo lako na kulifanikisha ni Leo.

    Chukua hatua Sasa. 

    Utajishukuru kesho kuwa Leo uliweza kuchukua hatua kuliko ambavyo utajilaumu.

    Uwe na siku njema

    Godius Rweyongeza 

    0755848391

    Morogoro; Mafiga Tenki Bovu

  • Kitu Muhimu Ambacho Kila mwandishi anapaswa kuwa anafanya

    moja ya kazi muhimu sana ambayo kama mwandishi unapaswa kuhakikisha kwamba umeifanya ni kuandika.

    hauwi mwandishi kwa kujiita tu mwandishi, bali unakuwa mwandishi kwa kuandika. Mwandishi anaandika.

    Hivyo wito wangu mkubwa kwako wewe mwandishi ni kwamba ukae chini na uandike kitabu chako au makala ambayo unafikiria kuandika bila ya kurudi nyuma.

    Naomba unisikilize vizuri.
    Kwa kawaida
    Daktari anatibu
    Mwalimu anafundisha
    Mwandishi pia anapaswa kuandika

    kaa chini na uandike kitabu chako kuanzia leo.

    Kupata mwongozo wenye hatua kwa hatua kuhusu uandishi wa vitabu, tuwasiliane kwa namba ya simu 0755848391

    tuwasiliane sasa uweze kupata mwongozo huu

  • Unahitaji kuwa mtu wa pekee ili kuandika kitabu?

    Watu wengi huwa wakifikiria kuhusu kuandika kitabu, basi kitu cha kwanza ambacho huwa kinakuja kwenye akili yao ni kwamba unapaswa kuwa mtu wa pekee kabisa.

    Nakubaliana na watu hawa kwamba ili kuandika kitabu chako unapaswa kuwa wa pekee. Na upekee mkubwa ambao unauhitaji wewe ili kuandika kitabu chako na kukikamilisha ni NIDHAMU YA KUKAA CHINI NA KUANDIKA.

    Ukweli ni kuwa bila ya kuwa na nidhamu hii, hata kama utautaka uandishi kiasi gani, huu uandishi hautakuja kwenye uhalisia, hata kama utakuw ana wazo zuri kiasi gani la kuandika. Wazo hili halitakuja kwenye uhalisia kwa sababu hujakaa chini na kuandika. Hivyo, kama unataka unataka kuandika vitabu KAA CHINI ANDIKA.

    Hiki ni kitu pekee unachohitaji.

  • Mambo 16 unayopaswa kuanza kuyafanyia kazi kuanzia Leo hii

    1. Weka akili Yako pale unapotaka kuwa. Fanya kile unachojiita.
    Mimi ni mwalimu, muda mwingi fundisha. Mwekezaji, wekeza.
    Mfanyabiashara,

    2. Ambatana na watu ambao ungependa kujifunza kwao. Kama Hawa watu hawako karibu Yako, Toka eneo Hilo na uende sehemu nyingine.

    3. Kuwa eneo ambalo linasapoti juhudi zako, kwa rasilimali, mamenta n.k.

    4. Kujitoa. Unatumia kila fursa unayoipata ili kufanikiwa. Hiki ndiyo kitu pekee unachopaswa kuwa unafikiria.

    5. Fanya hata kama mambo ni magumu. Wengi hufanya mambo yakiwa rahisi, ila yakiwa magumu hukata tamaa.

    6. Usihame kwenye kufanya kazi na zako. Chagua kitu kimoja Cha kupambana nacho na kipambanie kwelikweli.

    7. Mambo yakiwa rahisi Fanya, mambo yakiwa magumu Fanya.

    8. Unapokutana na magumu, Dunia inakuwa inakupima. Usikate tamaa.

    9. Jua unachotakiwa kufanya, kifanye kwa nguvu zako zote.

    10. Haijalishi jambo linachukua muda mwingi kiasi Gani. Lifanye.

    10. Una vitu vingi vya kufanya. Kama ni mwandishi una maktaba nzima ndani Yako.

    11. Uwe na eneo la kufanyia kazi zako. Na eneo hili liwe kama madhabahu Yako.

    12. Usihangaike na kuingia mtandaoni muda ambao unapaswa kuwa kazini.

    13. Matamanio MAKUBWA, na yapambanie muda wote. Tuwe na lengo mara mbili.

    14. Usiwe na mpango mbadala.

    15. Usiahirishe mambo. Hakikisha ulichopanga kufanya, unakifanya kweli.

    16. Kile unachokipambania,

    17. Wengi wanaoajiriwa hawataki kazi, japo mwanzoni wanaonekana wanapambania kazi. Wakishapata kazi, wanazembea. Hawazingatii mambo n.k.

    Imeandikwa na Godius Rweyongeza

    Kupata vitabu vya mafanikio. Tumia namna ya simu 0655848392

  • Njia rahisi sana ya kuandika kitabu ndani ya mwaka mmoja?

    Tupige hesabu kidogo

    Ukiandika maneno 100 Kila siku, Kwa mwaka ni maneno 36,500. Hiki ni kitabu tosha.

    Unadhani maneno 100 ni mengi. Ujumbe wa leo una maneno 48 TU!

    Unadhani unashindwa maneno 100 Kila siku.
    Fikiria sms unazotuma
    Comment unazoweka Whatsapp,
    Facebook n.k

    Bado unadhani huwezi?

    Njoo tukusaidie kuandika na tukupe mwongozo wa kuandika Kitabu Chako.
    Tuwasiliane Kwa 0755848391

    Karibu

  • Raha ya kuandika Kitabu ni pale unapokimaliza. Unajua Kwa Nini?

    Kuanza ni kazi kubwa. Wengi Huwa hawaanzi. 

    Ila kuendelea ulichoanza ni kazi kubwa zaidi, Wengi ambao hujitahidi kuanza, huishia njiani.

    Usiwe mmoja wao linapokuja suala la kuandika Kitabu. 

    Anza kuandika Kitabu na kimalize.

    Karibu sana SONGAMBELE CONSULTANTS

    ✅ Tunakuandikia kitabu chako (ghostwriting)  

    ✅ Tunatoa mwongozo wa kuandika kitabu chako  

    ✅ Kuhariri vitabu  

    ✅ Tunatoa usimamizi wa karibu kwenye uandishi wa kitabu chako  

    ✅ Tuna vitabu bora vyenye hatua muhimu za kufuata katika uandishi  

    Mawasiliano:

    Simu/WhatsApp: +255 684 408 755  au +255 655 848 392 au +255 678 848 396

    Email: jifunzeuandishi@gmail.com  

    Eneo: Sabasaba, Tenki Bovu

X