Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Nguvu Ya Vitu Vidogo Kuelekea Mafanikio Makubwa katika Vitendo…

    Huwa kuna kichekesho mtandaoni ambacho huwa kinasema ibada ilianza hivi, mpaka inaisha ilikuwa hivi..

    Au ibada ilianza vizuri, ila mambo yalibadilila pale mchungaji aliposema atakayeimba vizuri ataondoka na sadaka…

    Vichekesho vya aina hii huwa vinakuja kwa mfumo tofauti, ila lengo la hivi vichekesho huwa ni kitu kimoja tu, kusisitiza nguvu ya KUCHUKUA HATUA YA KWANZA ambayo ikiunganishwa na VITU VODOGO huwa inaleta matokeo makubwa.

    Na hiki ndicho ninataka kukwambia leo. Mwanzo wako hauwezi kuwa sawa na mwisho wako kana utaamua kufanya kile ulichochagua kweli bila kurudi NYUMA.

    Kumbuka, unahitaji ufanyie kazi ulichoamua kwa nguvu na kwa juhudi zako bila kurudi nyuma, mwisho wa siku, zile juhudi kidogo, zitaleta matokeo makubwa.

    Mambo yatakuwa mazuri kama utaendeleea kukomaa. Yatakuwa magumu pale uakapoishia njiani. Na mimi sitaki wewe uishie njiani…

    Endelea kupambana hata kama leo itaonekana ngumu..

    Jack Ma anasema leo itakuwa ngumu, kesho itakuwa ngumu zaidi, lakini siku baada ya kesho mambo yatakuwa marahisi ila ukweli mchungu ni kuwa watu wengi huwa wanakufa kesho jioni.

    Wewe usife kesho jioni…
    Unajua kufa kesho jioni maana yake ni nini?
    Maana yake ni kuacha kufanyia kazi ndoto zako.
    Maana yake ni kurudi nyuma baada ya kuwa umeanza
    Maana yake ni kuacha kufanyia kazi malengo yako kabla riba mkusanyiko haijaanza kuleta mabadiliko.

    Endelea mbele, hata kama leo mambo ni magumu, kesho mambo yatakuwa mazuri zaidi.

    Vitabu vitatu unavyopaswa kusoma leo ni

    1. NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA
    2. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
    3. NYUMA YA USHINDI: Kuna Kushindwa, Kushindwa, Kushindwa,….

    Kupata nakala zako wasiliana na 0684408755

    Asante sana

  • Vitu viwili vinavyokufanya ushindwe kufikia ndoto zao

    Ukiingia kwenye mitandao ya kijamii utakuta vijana mbalimbali wameandika kwenye mitandao yao mambo kadha wa kadha, unaweza kukuta mtu ameandika mfanyabiashsra, CEO, mjasiriamali na vungine vingi.

    Kati ya hayo matamanio mengi wanayokuwa nayo, ni wachache sana sana ambao huwa wanafikia na ndoto hizo. Kwa nini?

    Ninaenda kutoa sababu kuu mbili lakini kwanza, angalia video hiyo hapo juu👆🏿

    Sababu ya kwanza kwa Nini vijana wengi hawafikii ndoto zao kuwa na mambo mengi.

    Naam, huu ndiyo sababu ya kwanza kwa nini wengi hawafikii ndoto zao. Tena utakuta mtu anasema kuwa mambo ni mengi muda ni mchache. Ukweli ni kuwa unapokuwa na ndoto, akili yako na muda wako mwingi unapaswa kuuweka kwenye ndoto yako, sahau mambo mengine yasiyohusiana na ndoto zako na weka umakini wako wote kwenye ndoto zako.

    Ukiweza kuachana na mambo mengi unayopambana nayo na kuweka nguvu zaidi kwenye ndoto zako, ni wazi kuwa hii ndoto yako kubwa lazima tu utaifikia. Sasa swali ambalo unapaswa kujiuliza ni mambo gani ambayo umekuwa unafanya nje ya ndoto yako kuu? Je, ni vijitabia gani hasa ambavyo vinakupotezea muda ambao ungeweza kuuweka kwenye ndoto yako kubwa? Hivi vijitabia unapaswa kuachana navyo ili ujenge ndoto yako kubwa au la achana na ndoto yako kubwa ili ujenge vijitabia…..

    Ukweli ndio huo …
    Hakikisha umepata kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO utanishukuru kwa kukisoma, hiki mtandaoni hapa

    Au piga 0684408755 sasa uletewe nakala yako

    Sababu ya pili ni kuiga maisha ya watu wengine

    Kwenye clip fupi ambayo nimekushirikisha hapo juu nimekuonesha mhusika ambaye kila anapotembea kidogo anawaona wengine wanavyotembea anaanza kuiga mwenenedo wao wa kutembea. Sasa naomba unisikilize vizuri ili tuweze kuelewana; kuna vijana wengi wanapokuwa wanafanyia kazi ndoto zao wanakuwa hivi.

    Wanakuwa kama bebdera na kila wakati wanafuata upepo. Ukivuma kwa kasi kutoka kaskazini kuelekea kusini, wanaanza kuelekea kusini, baadaye ukibadili mwelekeo na wao wanabadili mwelekeo. Sikiliza, ukishajua ndoto yako kubwa ni ipi, kinachofuata ni wewe kukomaa nayo, haijalishi upepo unatokea wapi kuelekea wapi. Wewe komaa kwanza na ndoto yako moja mpaka kieleweke

    Usiwe mtu wa kuiga rafiki zako wanafanya nini. Ukweli ni kuwa ukienda kwa staili hiyo huwezi kufanikisha ndoto zako. Kwa sababu kila mara utakuta kuna mtu ambaye anafanya kitu fulani au ambaye amekuzidi.

    Lakini ukweli mwingine mchungu ni kuwa kadiri unavyobadili mwelekeo wako, ndivyo ambavyo utakosa kutumia UBUNIFU mkubwa ulionao. Nimeandika kitabu kizima kinachozungumzia namna unavyoweza kuibua ubunifu ulio ndani yako, unaweza kukipata mtandaoni ndani dakika mbili tu hapa.

    Kwa kumalizia Ningependa kusema kuwa ndoto uliyonayo, inawezekana kabisa kuitimiza. Unaweza kuitimiza kwa asilimia 100. Ila inahitaji ujitoe, ufanye kazi kwa bidii na ujitume mpaka kieleweke.

    Nakukumbusha kuhakikisha umepata kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO utanishukuru kwa kukisoma, hiki mtandaoni hapa

    Au piga 0684408755 sasa uletewe nakala yako

    Kuwa wewe mwenyewe.

    Makala hii imeqndikwa na Godius Rweyongeza
    Kujifunza zaidi kutoka Kwa Godius Rweyongeza tembelea www.songambele.co.tz
    Wasiliana naye Kwa 0755848391
    Morogoro-Tz

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza wasiliana na 0684408755

    Kujifunza UANDISHI na kupata usimamizi wa Moja Kwa Moja kutoka Kwa Godius Rweyongeza wasiliana na 0678848396

    Karibu sana

  • Unachohitaji wewe siyo hamasa zaidi bali ni matendo zaidi

    Mara kwa mara watu wamekuwa wanatafuta hamasa ya kufanya kitu. Ukweli ni kuwa huhitaji hamasa pekee ili kufanikisha lengo na ndoto yako kubwa. Bali unahitaji matendo ili uweze kufanyia kazi malengo na ndoto zako ziweze kufanikiwa.

    Nakwambia hivi kwa sababu hamasa huwa haidumu, hamasa ni kitu cha muda mfupi ambacho kinapotea. Hivyo ili ufanikishe malengo na ndoto zako kubwa ulizonazo unahitaji zaidi ya hamasa. Unahitaji matendo

    Wakati mwingine hujisikii kama kufanya kitu chochote kile. Lakini unapaswa kujisukuma kwa sababu ukisubiri hamasa pekee ili ufanyie kazi ndoto zako, ukweli ni kuwa hamasa hiyo itachelewa sana.

    Leo hujisikii kama una hamasa. Sikiliza, fanya kitu kimoja tu. Fanya kile kitu unachopaswa kufanya hata kama huna hamasa. Hamasa itakuja njiani, na hata kama hamasa haitakuja, utakuwa umeweza kukifanya hicho kitu.

    Kwa leo nadhani ujumbe umetosha sana.

    Kikubwa ni wewe kuufanyia kazi

    Kupata nakala za vitabu vyangu, basi wasiliana na 0684408755 karibu sana.

  • Jinsi ya kupunguza najuto yako utakapokuwa umezeeka

    Moja ya changamoto kubwa ammbayo huwa inawakuta watu ambao wanakuwa hawafanyii kazi malengo na ndoto zao ni kwamba wanapofikia mwisho wa maisha yao basi wanakuwa na majuto mengi ambayo yanawaandama kutokana nay ale ambayo hawakuweza kufanyia kazi. Sasa wali kubwa ambalo unaweza kuwa unajiuliza ni kuwa je, kuna namna ambavyo naweza kupunguza haya majuto kwenye maisha yangu? Je, kuna namna ambavyo naweza nisije kuwa na majuto kabisa?

    Ili kujibu haya maswali ni lazima kwanza tujue ni kitu gani ambacho huwa kinasababisha watu kuwa na majuto

    Kwanza ni kufanya yale ambayo hawapendi.

    Pili ni kutotumia uwezo wao

    Tatu ni kutosimamia ukweli

    Nne, ni kutochukua hatua na kujituma zaidi hasa  wanapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

    Sasa kujua vitu ambavyo huwa vinasabahisha majuto miongoni mwa watu ni hatua moja kuwa, ila sasa baada ya kuijua hii hatua, kinachofuata ni kuchukua uamuzi wa  wa kuahikisha kuwa mwisho wa siku unakuwa hauna majuto kwenye maisha yako. Fanya kinyume na hivyo vitu yaani

    Fanya yale unayopenda kufanya

    Fanya yale unayoona ni sahihi

    Simamia ukweli

    Tumia uwezo wako bila kuubana

    Ukiweza kufanya hivyo, ni ukweli ulio wazi na usiopingika kuwa mwisho wa maisha yako hautakuwa na majuto, bali utakuwe umeweza kufanikisha makubwa pia

    Kwa leo inatosha, nikutakie siku njema sana.

  • Kishiria kuwa umechelewa kufanya maamuzi

    Rafiki yangu, kila siku kuna maamuzi ambayo tunatakiwa tufanye, yanaweza kuwa ni maamuzi ya nani uwe naye kwenye mahusiano, maamuzi ya biashara gani ufanye, maamuzi ya sehemu gani uende kutembelea. Maamuzi ya aina gani ya matangazo ufanye. Maamuzi ya nani umwajiri, nani umwondoe kazini au nani umpandishe cheo. Maamuzi ya shule gani mwanao asome au gari gani ununue na mengine mengi.

    Kwa kuwa kuna maeneo mengi ya kufanyia maamuzi, siku ya leo ningependa tu kukwambia kuwa kama unafanya maamuzi hasa kwenye biashara ukiwa na uhakika wa asilimia 100 basi ni wazi kuwa unakuwa umechelewa. Yaani, umesubiri kila kitu kiwe sawa sawia.

  • Kuanguka ni kiashiria kuwa kuna kitu unafanya

    Kuanguka siyo tatizo, kuanguka ni kishiria kwamba kuna kitu unafanya na ndiyo maana unakutana na vikwazo. Kumbe kuanguka kwako usikuone kama kigezo cha wewe kutoendelea mbele. Bali kuone kama sehemu ya wewe kuendelea kusonga mbele ili kuja kufanya makubwa zaidi.

    Kadiri unavyokua, maanguko yako yanakuwa makubwa zaidi. Na yanajulikana kwa watu wengi zaidi kuliko pale unapokuwa chini, lakini hili lisikurudishe nyuma wala kukufanya ushindwe uweze kufanyia kazi malengo na ndoto zako. Bali hili liwe ni kama chachu ya wewe kuweza kufanya makubwa zaidi

    Kwa sababu ukiendelea kubaki hapohapo ulipo, itakuwa ni vigumu kwako kuweza kufanya makubwa zaidi.

    Wengine wanaogopa kuchukua hatua kwa sababu wanalinda heshima, labda ameajiriwa na anaogopa kwamba akianzisha biashara itafeli. Ukweli ni kuwa kulinda heshima ni sawa na timu inayolinda goli wakati wa mechi. Kama wachezaji hawatatoka kwenda kushambulia. Tena kushambilia kwa kiingereza kuna gumu kidogo  to make an offense, . Kama wachezaji hawatatoka kwenda kushambulia, ujue wazi kuwa timu hiyo haitafunga.

    Lakini uwezekano wa timu hiyo kufungwa ni mkubwa sana.

    Kama huchukui hatua yoyote ile kwa kuogopa kushindwa, unakuwa huna tofauti na mtu ambaye analinda lango. Kazi yako, siyo kulinda lango, bali kushambulia mara kwa mara kadiri unavyoweza. Kadiri unavyoshambulia ndivyo ambavyo unaongeza uwezekano wa wewe kuweza kufunga zaidi.

    Siku ya leo nataka uondoke na vitu viwili vikubwa

    Kwanza fahamu kuwa kushindwa siyo tatizo, bali kushindwa kuchukua hatua na kuogopa kushindwa ni kikwazo na tatizo pia.

    Pili, nataka ufahamu kuwa  mara zote unapaswa kuwa kwenye mwendo wa kushambulia. Usilinde lango, usilinde heshima. Wewe shambulia tu hata kama utashindwa, utapata heshima zaidi kwa kushambulia kuliko kulinda lango

    Mpaka siku nyingine, uwe na siku njema sana.

    By the way nimeandika vitabu  viwili ambavyo kwa siku ya leo ni muhimu sana kwako uvipate. Kitabu cha kwanza ni kitabu cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA, na kitabu kingine ni kitaub cha NYUMA YA USHINDI: Kuna kushindwa, kushindwa, kushindwa. Kuapata nakala za vitabu hivi tuwasiliane kwa 0684408755 sasa

    Mpaka kesho, mimi nakutakia siku njema kwako

  • TAARIFA KWA UMMA

    Siku za karibuni whatsap zimepatwa na changamoto na changamoto ya kufungiwa, kitu ambacho kimenifanya nikawa siwezi kupata jumbe zenu moja kwa moja. Nimejaribu kufungua akaunti nyingine za whatsap ambazo nazo pia zimefungiwa pia.

    Hivyo, kwa sasa nimeamua kuwa nitatulia kutumia whatsap kwanza. ila nitakuwa natumia telegram. Unaweza kunifikia kwa haraka telegram kwa namba hii ya +255755848391

    Hata hivyo ifahamike kuwa namba hii hii ya +255755848391 bado inapatikana vizuri kwa simu ya kawaida ya kupiga na SMS.

    Aidha, namba ya ofisi ambayo ni +255684408755 inafanya kazi vizuri whatsap, na unaweza kuitumia bila wasiwasi wowote.

    Natumaini utakuwa umeweza kunielewa na asante kwa kuelewa mabadiliko haya.

    Asanteni,
    [Jina lako]

  • Wewe unafahamika Kwa kitu Gani ?

    Moja ya uamuzi unaohitaji kufanya ni Uamuzi wa namna unavyotaka ufahamike kwenye maisha Yako. Nimekuwa nikisisitiza hiki kitu mara Kwa mara, lakini cha kushangaza ni kuwa Watu wengi wamekuwa Bado wanarudia kufanya makosa yaleyale Kila mara.

    Ngoja nikwambie KITU, watu wengi unaowafahamu, huwafahamu Kwa sababu wanafanya Kila kitu au walikuwa wanafanya Kila kitu, bali unawafahamu Kwa sababu walibobea sehemu Moja.

    1. Iwe ni viongozi wa kiroho kama Budha, Yesu na Mtume Muhammad
    2. Au wanasiasa kama Nyerere.
    3. Au wanamuziki
    4. Wanamichezo na hata waandishi

    Nyerere anafahamika kama mwalimu, lakini impact yake haukuwa kwenye kufundisha, kwake ualimu umebaki kuwa cheo Cha heshima tu, ila impact yake ilikuwa kwenye siasa.

    Ndiyo maana mwaka 1955 aliachana na ualimu Ili aingie kwenye siasa Kwa sababu huko ndiko alitaka kuacha alama.

    Ualimu ulikuwa unamlipa. Kwa lugha ya Leo tunaweza kusema alikuwa anapata maokoto mazuri tu Kwa ajili ya kuendesha maisha yake, Tena kipindi hicho ambacho Ajira zilikuwa ni adimu.

    Lakini aliamua kuachana na Ajira Ili na kuingia kwenye siasa, Kwa sababu aliona alama yake kubwa ataiacha kama atakuwa kwenye siasa kuliko akiwa mwalimu.

    Wakati mwingine inaonekana vigumu kuweka nguvu sehemu moja hasa pale ambapo vitu vyako vidogo vidogo unavyofanya vinapokuwa vinakuingizia maokoto kidogokidogo. Ila ukweli ni kuwa hiki kitu ndicho kitakupoteza pia. Maana haya maokoto kidogo ndiyo yatakunyina pesa za maana laiti kama ungewekeza muda na nguvu zako sehemu Moja na kuikuza. Ni ukweli kuwa ungeweza kupata matokeo makubwa zaidi.

    Jipe muda wa kuwekeza kwenye ndoto Yako kuu na kuachana na vitu vingine vyote unavyofanya Kwa Sasa.

    Inaweza isikulipe Kwa Sasa ila itakulipa baadaye.

    Makala ya Leo imeandikwa na Godius Rweyongeza
    Whatsap: 0687848391
    Calls & SMS: 0755848391

    Jifunze zaidi Kwa Godius Rweyongeza Kwa kutembelea www.songambele.co.tz

    Mpaka wakati mwingine. Tchao.

  • Kufa Leo, uishi milele

    Ikiwa inamaanisha pambana Leo Ili juhudi zako ziendelee kukusaidia Mpaka kesho. WEKEZA Leo ule vinono kesho.

    Kubali kupoteza Leo, Ili kesho kesho kutwa upate Kila kitu.

    Ukweli ni kuwa maisha Yana trade off. Huwezi kupata Kila kitu unapokihitaji. Kuna baadhi ya vitu unahitaji uvipoteze Leo, Ili ufanye vingine lakini ukiwa Unajua kesho Utapata zaidi.

    Na hili litawezekana kama tu utakuwa na ndoto kubwa. Kitu kinachonishangaza ni kuwa Watu wengi wanafanya vitu wakiwa hawana ndoto kubwa.

    MTU anafanya BIASHARA, lakini hajui anataka BIASHARA hiyo impeleke wapi miaka mitano au Kumi ijayo.

    MTU anafanya KAZI, au anaajiriwa lakini ukimuuliza, Nini malengo Yako na hii ajira Yako, Hana malengo Wala ndoto zozote.

    Sasa haishangazi kuona MTU huyu anaanza Kufanya KAZI bila Kuweka juhudi Wala kujituma Kwa sababu hajui wapi hasa anaelekea.

    Haishangazi kuona kwamba MTU anapopata mafanikio ya muda mfupi anaridhika na kuona kuwa amekwishafika, kumbe Bado sana.

    Je, wewe ndoto zako kubwa ni zipi?

    Kama Bado Hauna ndoto kubwa, kinachofuata hapa ni wewe kuhakikisha kwamba unapata kitabu Cha jinsi ya kufikia ndoto zako. Hiki Kitabu kina MWONGOZO mzuri WA kukusaidia wewe kufanikisha makubwa ambayo umekuwa unatamani kufanikisha Kwenye maisha Yako.

    Watu wengi waliosona kitabu Hiki, nawaona wakipiga hatua kiasi kwamba ninaendelea kuwa na uhakika zaidi kuwa na wewe ukipata nakala Yako utaweza kupata matokeo makubwa kama haya na zaidi.

    Kama Hawa wameweza, wewe unaweza pia.

    Sasa, sikiliza kupata nakala Yako ni rahisi sana.

    Lipia 20,000/- kwenda Airtel money 0684408755 Jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Ukishalipia, utanitumia ujumbe nikutumie Kitabu chako. Nauli ni juu Yako.

    Asante sana

    Makala hii imeqndikwa na Godius Rweyongeza
    Whatsapp: 0687848391
    Calls & SMS: 0755848391
    MOROGORO-TZ

    Tembelea:www.songambele.co.tz

    Kujifunza zaidi kutoka Kwa Godius Rweyongeza

  • Wiki Hii Nipo Nasoma Kitabu Cha Elon Musk. Kitu Kimoja Unachopaswa Kufahamu Kwanza

    Wiki hii nipo nasoma kitabu kizuri sana Cha ELON MUSK: Kilichoandikwa na Walter Isaacson mtalaam wa kuandika vitabu vya wasifu (biographies).

    Kwa Kuwa Bado naendelea kukisoma Kwa Sasa sitasema mengi zaidi ya kusema kuwa bila kujali unezaliwa wapi, Bado unaweza kuweka alama kwenye hii Dunia

    Huhitaji ruhusa ya watu wengine zaidi ya ruhusa Yako tu kufanya hivyo.

    Labda siku ya Leo Ningependa kuuliza swali Moja tu. Ndoto Yako kubwa ni ipi?
    Iandike chini, Kisha chukua Hatua Ili uanze kuifanyia KAZI

    Kupata kitabu Cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Bonyeza hapa

    Je, na wewe ungependa kupata Kitabu hiki Cha Elon Musk kilichoandikwa na Walter Isaacson. Utalipia vocha tu, tukutumie kitabu chako. Lipia Kwa 0684408755

    Karibu sana

X