-
Kama kila mtu angekuwa ni…
Hivi kaa chini ufikirie kama kila mtu angekuwa ni mzembe kama wewe.
Kama kila mtu angekuwa na visingizio kama wewe
Kama kila mtu angekuwa ni mwoga kama wewe
Kama kila mtu angekuwa ni mlalamikaji kama wewe.
Kama kila mtu angeona aibu kuitumia akili yake?
Kama kila mtu angesema ni acha nile maisha leo kesho itajijua yenyewe
Hivi unadhani nani angethubutu kufanya vitu vya tofauti. Ni nani angethubutu kutengeneza nguo unazovaa? Ni nani angethubutu kuanzisha biashara ambazo zinakusaidia wewe kuweza kufanya kazi zako.
Bila shaka asingekuwepo. Kila unapoona kitu kizuri basi ujue kwamba kuna watu waeamua kuachana na uoga, ulalamikaji, uzembe, kutupia watu lawama na wamekuwa tayari kubeba majukumu ya maisha yao.
Hivyo basi, kitu ambacho unapaswa kufanya kuanzia leo basi ni kuchukua hatua, kuacha kulalamika, uzembe, kutupia watu lawama na uwe tayari kubeba majukumu yanayokuhusu.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.
Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA
-
Kuwa Imara
Tunaishi katika dunia ambayo haipendi vitu ambavyo siyo imara. Na hili jambo la KUWA imara halijaanza leo. Limekuwepo kwa siku nyingi sana.
Vitu ambavyo vimekuwa imara kwa miaka mingi ya nyuma, ndivyo ambavyo viliendelea kuishi, huku vile ambavyo siyo imara vikidhoofu na kufa.
Watu wanyonge, mimea minyonge, wanyama wanyonge havina nafasi kubwa ya kuishi Kama vile vitu ambavyo ni imara. Hivyo, na wewe unapaswa KUWA imara.
Najua hiki kitu kinaweza kuonekana cha ajabu sana hasa kwa upande wako ukizingatia kwamba umezoea kuambiwa KUWA wewe Ni MNYONGE. Na hivyo kuna watu wanakutetea wewe na unyonge wako.
Ninachotaka kukwambia ni kuwa, usikubali kuwa MNYONGE. Unyonge ni hali ya chini ambayo MTU yeyote hapaswi kuibeba.
Unapaswa KUBEBA ujasiri, uthubutu, na sifa nyingine za aina hii.Unyonge haukai meza moja na ujasiri. Unyonge hauwezi kukaa meza moja na uthubutu. Unyonge hauwezi kukaa meza moja na utawala.
Ukiwa MNYONGE unanyongwa na haki yako hupewi. Huo ndio ukweli.Hivyo, nataka ujiondoe kwenye hali ya unyonge kuanzia Leo hii na uanze kuwa jasiri, uwe imara.
Kama kuna rafiki unayemfahamu anayepaswa kuwa imara mtumie ujumbe huu hapa kupitia hapa chini
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.
Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA
-
Fanya hiki kitu unapokuwa na watu mara zote
Utagundua kwamba wiki hii nimekuletea makala za namna ya kuhusiana na watu, kuanzia juzi, jana na hata leo. Lengo ni moja tu. Uweze kujifunza saikolojia ya binadamu kwa undani na ikusaidie kuwa mtu mwenye ushawishi zaidi kuliko mtu mwingine ambaye amekuzunguka.
Nakumbuka wakati nipo chuoni, nilipata kusoma kitabu cha Dale Carnergie kinachoitwa How to Win Friends And Influence People.
Hiki ni kitabu, kama jina lake linavyosema, kipo hivyo hivyo kwelikweli. Nilikisoma kwa umakini mkubwa sana, nikatumia mbinu zilizokuwe kwenye hiki kitab. Muda si mrefu, nikaanza kuwa mtu mwenye ushawihi miongoni mwa watu niliokutana nao.
Kitabu cha Dale Carnigie ni kitabu ambacho nashauri na wewe uweze kukisoma pia. Tena kwa kulifahamu hilo nimeshakuandalia mpaka uchambuzi wake ambao unaweza kuusoma hapa
Moja ya kitu ambacho mwandishi anaongelea sana kwenye hiki kitabu na kitu muhimu sana ni kujenga utamaduni wa kujali na kuthamini vitu na maisha ya watu wengine. Yaani, kuwaonesha watu wengine kuwa unawajali na unawathamini sana.
Kwenye hili la kuwajali wengine kuna mengi ambayo unaweza kufanya.
- Unaweza kuwajali kwa kukumbuka majina yao
- Unaweza kuwajali wengine kwa kukumbuka tarehe zao za kuzaliwa
- Unaweza kuwajali na kufuatilia vitu wanavyopendelea
- Kuwasifia n.k.
Rafiki yangu, kuanzia leo hii, hatakama ulikuwa hujali sana kuhusu maisha ya watu. anza kuonesha kwamba unawajali hao watu. Onesha hilo kwa vitendo, hata kama unaongea na hao watu kwa simu,
Na ubora vitu unavyohitaji kuonesha kwa watu kuwa unawajali siyo vitu vya gharama. Ni vitu vya ambavyo unaweza kufanya tena bure kabisa.
Kwa hiyo basi, kuanzia leo hii, jenga utaratibu wa kuonesha kuwa unajali wengine. Hiki kitu kitakuweka mbele kuliko watu wengine wote ambao umewahi kukutana nao kwenye maisha yako.
Na kujali kunaanzia hapahapa. Kama umeipenda hii makala au ambazo umesoma siku za nyuma, washirikishe wengine unaowajali ili waisome. Watumie link hapa chini
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.
Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA
SEMINA YA MWEZI WA SITA
ITAFANYIKA JUNI 24, MOROGORO
- Itakuwa ni siku ya Jumamosi
- Itaanza asubuhi saa moja na kumalizika jioni saa 12
- Itakuwa ni siku ya jumamosi
SEMINA YA MWEZI WA SITA
MADA ZITAKAZOFUNDISHWA
- Jinsi ya kufanikisha malengo makubwa ndani ya muda mfupi
- Safari ya kuelekea uhuru wa kifedha
- Namna ya kugundua na kutumia uwezo mkubwa uliolala ndani yako
- Jinsi ya kutawala hofu inayokuzuia kuanza na kufanyia kazi malengo na ndoto zako
SEMINA YA MWEZI WA SITA
KUJIANDIKISHA KWA AJILI YA SEMINA
- Tuma taarifa zako kamili kwenye whatsap 0755848391
- Mwambie na mwenza wako ushiriki naye
- Njoo Morogoro, tujifunze, tukutane na watu, tutengeneze konekisheni
-
Kosa kubwa unalofanya unapokuwa unaongea na watu
Kwenye makala ya jana rafiki yangu, niliandika sana juu ya umuhimu wa wewe kukumbuka majina ya watu, na kwa nini mara zote unapaswa kuhakikisha kwamba unakumbuka majina ya watu. sikuishia hapo, nilikupa mbinu za kutumia ili kukumbuka majina ya watu bado nikakueleza umuhiu wa majina ya watu.
Sasa tukiwa bado hapo kwenye kuongea na kuzungumza na watu, siku ya leo ningependa tu kukwambia makosa ambayo watu huwa wanafanya wakiwa na watu, na jinsi ya kuyaepuka haya makosa ili uweze kuwa mtu mwenye ushawishi zaidi.
Kosa la kwanza kabisa ambalo watu huwa wanafanya ni kutumia simu wanapokutana na watu. Rafiki yangu katika ulimwengu wa leo, simu ni dhana muhimu sana ambayo tunaitumia. Nadhani na wewe utakuwa unaitumia sana, sana simu. Pamoja na raha nyingi za kuwa na simu, pamoja na mambo mengi ambayo simu inaweza kutusaidia kufanya, kuna kitu kimoja ambacho naona bado watu hawajaweza kukitambua. Na kitu hiki ni kwamba unapokutana na mtu kwa ajili ya mazungumzo, tafadhali usitumie simu.
Simu unayo muda wote. Yaani, wewe unashinda na simu na ulala nayo na pengine kitu uachoangalia kikiwa cha kwanza asubuhi ni simu.
Sasa pamoja na kuwa unakuwa na muda mwingi wa kutumia simu kiasi hicho ni kuwa unapokutana na mtu bado unataka kutumia simu tu. hivi hili ni kweli? Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu, watu wanapenda sana kuonekana wanathaminiwa, na njia ya watu kuonekana kwamba wanathaminiwa ni wewe kuwapa umakini wote pale unapokuwa unaongea hao watu. Hivyo basi, unapokutana na mtu yeyote, hakikisha kwamba hautumii simu.
Weka umakini na nguvu zako zote kwenye mazungumzo yako na huyo mtu. Achana na vitu vyote au kitu kingine ambacho hakiendani na mazungumzo.
Utakuwa na muda wa kutosha wa kutumia simu yako hapo baadaye, hivyo, kwa sasa achana kabisa na simu yako. Weka nguvu zako zote kwenye mazungumzo. Hiki kitu kitakusaidia kutogawa umakini wako. Hiki kitakusaidia kumsikiliza mtu kwa umakini. Hiki kitu kitakusaidia wewe kupata ushawishi zaidi wa watu.
Inashangaza sana kuona kwamba watu wanaalikana ili wapige stori halafu badala ya kupiga stori, wanaanza kuongea na simu, wanaanza kuchati na kutuma jumbe.
Ukiamua kwamba unaenda kukutana na mtu, usitumie simu.Na kama kutakuwa na ulazima wa wewe kutumia simu. Basi mwombe huyo mtu ambaye umekutana naye kwamba ungependa kuongea na mtu fulani mara moja au ungependa kumtumia mtu fulani ujumbe mara moja kisha unaendela na mazungumzo.
Siyo unaongea na mtu halafu unatumia simu yako, hiyo ni dharau. Yaani, mtu ameacha majukumu yake yote, amekuja kukutana na wewe. Halafu, wewe unatumia simu muda wote. Huo ni ukosefu wa nidhamu aisee.
Achana nao.
Unaweza pia kusoma zaidi makala hii KITABU: JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO: Njia Za Uhakika Zitakazokufanya Ulipwe Mara Kumi Zaidi ya Unavyolipwa Sasa
Kosa la pili amablo watu wanafanya ni kutoangalia watu kwenye uso. Naam, unapooongea na watu unapaswa kuwaangalia watu kwenye uso. Hiki kitu kitaonesha kwamba uko makini kwenye mazungumzo ambayo yanaendela, lakini pia kitakusaidia wewe kuweza kumfuatilia mhusika kwa ukaribu na kuona namna anavyowasilisha mada kwako. Sambamba na hilo kumwangalia mtu usoni kunaonesha kwamba uko makini sana na unajali.
Sasa kuanzia leo hii usiongee tu na watu. ukiongea na mtu yeyote yule hakikisha kwamba unaongea na ukiwa umemwangalia usoni. Mara zote, mwangalie huyo mtu usoni. Hiki kitu kitakupa maksi kubwa sana.
Juzi juzi wakati napita mtandaoni nilikutana na nukuu ya

Anasema kwamba kama unaangalia simu kuliko unavyoangalia watu usoni, jua kwamba kuna kitu kikubwa unakosea.
Kumbuka hii ni nukuu ya mkurugenzi wa kampuni kubwa ya APPLE inayozalisha simu. Lakini bado anasisitiza wewe kuwaangaliwa watu usoni kuliko unavyoangalia simu yako. Na leo hii kwenye hii makala, bado naendelea kukusisitiza wewe kuendelea kuwaangalia watu usoni hasa pale unapokuwa unaongea nao.
FANYA HIVYO MARA ZOTE,
Kwa upande mwingine inawezekana hiki kitu hujakizoea. Kama hujazoea hiki kitu, kuna kitu kimoja tu unaweza kufanya kuanzia sasa hivi. Na kitu hiki siyo kingine bali ni kuhakikisha kwamba unaanza kujenga utaratibu wa kuangaia watu usoni pale unapokuwa aunaongea nao. Fanya hivyo kuanzia siku ya leo.
Nakutakia kila la kheri
-
Jinsi Ya Kupata Ushawishi Mkubwa Miongoni Mwa Watu
Rafiki yangu mpendwa salaam,
Umeshawahi kuona hili, unakutana na mtu, anakwambia au unamwambia kwamba nakukumbuka sura yako, ila sikumbuki jina lako. Sijawahi kukutana na mtu ambaye anakumbuka jina la mtu ila amesahau sura yake. Kwenye makala ya leo tunaenda kuangazia sula zima la MAJINA YA WATU. Tutaona njia rahisi utakayoitumia kupata majina ya watu, kukumbuka majina ya watu.
Hivi umeshawahi kujiuliza ni kitu gani ukikifanya, kwa watu watu watapenda sana kuendelea kuwa karibu na wewe na watavutiwa kuonana na wewe mara kwa mara. Naam, kitu cha aina hiyo kipo.
Kitu hiki ni kukumbuka majina ya watu. Hakuna mtu hata mmoja ambaye huwa anachukia kuitwa jina lake. Kila mmoja huwa anapenda sana kusikia akiitwa kwa jina lake.
Hivyo kama kuna kitu cha maana sana ambacho unaweza kufanya, basi kitu hicho ni kuhakikisha kwamba mara zote unakumbuka majina ya watu. Majina ya watu ni silaha kubwa sana ambayo unapaswa kuitumia kwenye maisha yako.
Nadhani imewahi kukutokea ukawa kwenye kusanyiko la watu na kukawa na mzungumzo ambayo yanaendelea. Mara ghafla ukasikia kwamba kuna kikundi cha watu wanataja jina lako. Linaweza kuwa ni eneo lenye kelele nyingi sana, ila kile kitendo cha wewe kusikia jina lako likitajwa na wale watu, kinakufanya wewe uanze kufuatilia yale mazungumzo yao hata kama wale watu mwanzoni ulikuwa hufuatilii mazungumzo yao.
Hiki ni kiashiria tosha kuonesha ni kwa namna gani huwa tunaweka nguvu kubwa kwenye kufuatilia majina yetu na kutaka kujau ni kwa na mna gani watu wanaongea juu yetu.
Hivyo, basi kuanzia leo hii nakupa jukumu moja tu. Jukumu la kuhakikisha kwambna kila mtu ambaye wewe unakutana naye unakumbuka jina lake. na hili litawezekana kama utafuata mambo yafuatayo.
Kwanza, kama utahakikisha kwamba kila mtu ambaye unakutana naye unamsikiliza vizuri pale anapokutajia jina lake. MARA NYINGI WATU huwa wanasahau majina ya watu, ila kitu kikubwa sana ambacho uwa kinawafanya hao watu wasahau majina ya watu ni kwa sababu huwa hawako makini kwenye kusikiliza hayo majina mara ya kwanza kabisa. unakuta kwamba mtu anataja jina lake lakini anayetajiwa jina hilo, hayuko makini kusikiliza.
Sasa kama wewe unataka kuhakikish kwamba unakumbuka jina la kila metu ambaye unakutana naye, kitu cha kwanza kabisa, ni kuhakikisha kwamba unamsikiliza kwa umakini mtu huyo anapokuwa anakutajia jina lake.
Lakini siyo tu kumskiliza kwa umakini, baada ya huyo mtu kukutajia jina lake hakikisha kwamba unatumia jina la huyo mtu kwenye mazungumzo. Litumie mara kwa mara kwenye mazungumzo na kwenye maeneo ambapo unaona kwamba linafaa kutumiwa. Mtu asiishie tu kujitambulisha kwako, halafu wewe ukawa hujatumia jina lake kwenye maongezi naye.
Pili, kama mtu amekutajia jina lake na wewe hujalisikia. Basi hakikisha kwamba unamwuliza vizuri ili arudie kukutajia jina lake kwa usahihi. Usiishie tu kusema kwamba ahaa, ok sawasawa.
Tatu, mara zote hakikisha kwamba unajua namna jina la mtu linavyotamkwa na linavyoandikwa. Kuna mtu anaweza kukutajia jina lake ukawa unajiuliza hivi hili jina linaandikwaje, au linatamkwaje, kuwa makini kwenye hilo. Mara zote hakikisha kwamba unajua jina la mtu linavyoandikwa na linavyotamkwa pia.
Lakini pia katika ulimwngu wa leo, unaweza kupata jina la mtu kupitia intaneti, bado ukiongea na huyo mtu utapaswa kumwuliza namna sahihi ya kutamka hilo jina ili huyo mtu aweze kujitambulisha kwako kwa usahihi na wewe uweze kutambua jina lake.
Nne, kama mtu huyo anatambulishwa kwako na mtu mwingine, hakikisha aliyemtambulisha kwako amelitamka vizuri jina la mhusika na wewe umelisikia. Kama hilo jina hujalisikia vizuri, usikubali yapite. Maana mara nyingi watu huwa wanaona kama hawatakuja kuonana na mhusika ambaye wameongea naye, ila ukweli ni kuwa unapaswa kulikumbuka vizuri jina la mtu, hata kama unahisi huyo mtu hutaonana naye tena maishani mwako.
Njia nzuri ya kupata majina ya watu
Njia nzuri ya kupata majina ya watu ni wewe kujitambilisha kwa hao watu na kuwaambia kwamba wewe unaitwa…. Na kuwauliza wao wanaitwa akina nani? Hakikisha kwamba unajitambulisha kwa watu unaokutana nao punde baada ya kuwa umekutana nao.
Ukiacha kujitambulisha kwa hao watu na ukaacha muda ukapita, nakuhakikishaia kwamba, baada ya muda wa kukaa na huyo mtu, utajikuta kwamba umezoea kukaa naye ila humjuui jina lake, na itakuwa ni vigumu kwako kuweza kumuuliza tena, maana utaogopa kuonekana kama mtu ambaye hajali muda wote huo hujauliza jina lake na sasa hivi ndio unataka kuuliza jina lake.
Kwa hiyo, unapouktana na mtu, jitambulishe, na muulize yeye jina lake.
Kisha litumie hilo jina kwenye mazungumzo yako na yeye bila kurudi nyuma.
Kwa mfano, mimi naitwa Godius Rweyongeza, na wewe ni……(EBU JAZA JINA LAKO KAMILI, BARUA PEPE NA NAMBA YAKO YA SIMU HAPO CHINI). Nitakupigia simu kukupongeza kwa kusoma makala hii.
Sasa ukijua majina itakusaidia nini
Kwanza itakusaidia kuteka umakini wa mtu. Ngoja nikupe mbinu ambayo utaitumia siku ya leo. Unapotaka hapa fanya kitu kimoja tu, nenda uulize jina la mtu ambaye hujawahi kukutana naye na wala hajui jina lako. Ukishajua jina lake, nenda uonane naye. Kisha ukionana na huyo mtu, mchangamkie. Mtaje jina lake kisha msalimie. Kwa kufanya kitu hicho kidogo tu, utaona ni kwa namna gani huyo mtu ataanza kukuuliza hivi jina langu umelifahamuje. Na utaona namna ambavyo huyu mtu atakuwa tayari kukusikiliza kwa umakini zaidi kwenye kile unachoongea.
Ukijilijua jina la mtu na ukalitumia jina hilo kwenye mazungumzo, basi nakuhakikishia kuwa huyo mtu utamvuta umakini wake. na hata kama huyo mtu alikuwa na mambo mengi ambayo anayafanyia kazi, nakuhakikishia kuwa huyo mtu ataacha kila kitu na kukusikiliza wewe kwanguvu zako zote.
Pia kujifunza zaidi, hakikisha unasoma: INALIPA KUKUMBUKA MAJINA YA WATU
Pili, majina utayatumia kwenye mahusiano ya kawaida ya kila siku. Pata picha leo hii mtu amejitambulisha kwako, halafu kesho, ukakutana tena na huyo mtu. Ukamwita jina lake na ukaendelea kuongea naye kwa ustadi wa hali ya juu kuhusuaiana na kitu fulani. Ni wazi kuwa huyo mtu atapenda sana, kuwa karibu na wewe na hivyo, itakusaidia wewe kujenga mahusiano makubwa zaidi pamoja na yeye.
Tatu, Kwenye biashara. Kama mfanyabiashara, unakutana na watu wengi, na kama mfanyabiashara unafanya kazi na watu wengi, ambao wanaweza kuwa ni wafanyakazi, wahisani, wapambe, wawekezaji, washirika n.k.. Rafiki yangu, unahitaji kuhakikisha kwamba unakumbuka majina yao.
Pia soma zaidi: Njia Ya Uhakika Ya Kutoboa Kwenye Biashara
Tatu kwenye mauzo, utatumia majina ya watu kwenye mazungumzo na watu ili kuweza kuwauzia. Mara zote. unapokuwa unafanya mazungumzo ya mauzo hakikisha kwamba unatumia majina ya watu kwenye mazungumzo nao.
Nne, kwenye kampeni. Kama wewe ni mwanasiasa na unataka kupata ushawishi mkubwa wa watu, basi kumbuka majina ya hao watu.
Kwenye matangazo, ulimwengu wa sasa hivi umerahisha sana. Unaweza kufanya matangazo kwa njia mbalimbali, na kwa kutumia hizi njia unaweza kutumia majina ya watu na kuyataja. Mfano, utangazaji wa kutumia baruapepe…au kwa kutumia njia ya simu. Bado unaweza kutaja jina la mhusika na hivyo kuendelea kuvuta umakini wake kwenye kukusikiliza.
Endapo utatumia vizuri hizi mbinu ambazo nimezianinisha hapa, ni wazi kuwa baada ya muda utakuwa superstar kwenye kukumbuka majina ya watu. Utaachana na dhana ya kwamba nakukumbuka sura ila sikumbuki jina lako.
Jina la mtu ni muhimu sana, ndio maana leo nimezama ndani zaidi kueleza hiki kitu.
Makala nyingine inayoendana na hii: Kitabu: How to Win Friends and Influence People
Unaweza kuwashirikisha wengine makala hii pia kwenye mitandao ya kijamii
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.
Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA
-
Sehemu Wanapokosea Wajasiriamali
Watu wengi wamekuwa wakifahamu kuwa ujasiriamali ndiyo njia ya uhakika ya kutoboa na kufanya makubwa. Hata hivyo, wengi wamekuwa wanakosea kwa namna wanavyofanya ujasirimali na biashara zao kiasi kwamba, kutoboa kwao imekuwa ni ngumu sana.
Kinachowakwamisha watu wengi ni kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Unakuta mtu ameanzisha biashara, wakati huohuo ana kitu kingine anachofanya sehemu nyingine. wakati huoho anapoteza muda mwingi sana kwenye mitandao. Biashara yake ikiwa bado haijatengamaa anasikia kwamba kuna fursa ya kuwekeza pesa zake sehemu akapata mara mbili ndani ya muda mfupi, anakimblia kuwekeza huko.
Maabo yake yakiwa bado hayajakaa sawa anakimbilia kucheza vikoba ili siku moja aje apate mkopo.Na hapa ndipo wanapokosea wajasirimali wengi. Yaani, wanafanya vitu vingi sana, kwa wakati mmoja. ukifanya vitu vingi kwa wakati mmoja rafiki yangu, ni wazi kuwa huwezi kuona matokeo unayotegemea. Maana utakuwa unatawanya nguvu zako badala ya kuziweka sehemu moja. Nguvu zako ukiziweka sehemu moja, utapata matokeo makubwa kuliko ukitawanya nguvu zako kwenye maeneo mengi.
Kitu Kimoja Ambacho Unakihitaji Ili Kuweza Kufaulu Katika Kazi Zako
Ni kama mwanga wa jua. Huu mwanga huwa una nguvu kubwa sana, ila huwa umetawanyika. ila ukikusanywa sehemu moja, huwa unawasha moto. sasa na wewe kama unataka kuwasha moto, kama unataka biashara yako iende kwenye ngazi za kimataifa, basi washa moto na weka nguvu zako sehemu moja. Sehemu ambapo utaweza kupata matokeo makubwa.
Nakuhakikishia kuwa hiki ni kitu ambacho watu wengi hawapo tayari kukifanya, ukiweza kukifanya, kitakupa matokeo makubwa sana.
Kila la kheri.Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.
Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA
-
Njia Ya Uhakika Ya Kutoboa Kwenye Biashara
Rafiki yangu, siku ya leo ningependa kukwambia njia ya uhakika ya wewe kutoboa kwenye biashara yako, unajua njia hii ni ipi?
Ngoja kwanza nikwambie kitu. Tafiti nyingi kwenye biashara zimeonesha kwamba asilimia 90 ya biashara ambazo huwa zinaanzishwa kila mwaka, huwa zinakufa. hii ndio kusema kwamba kati ya biashara 100 ambazo huwa zinaanzishwa kila mwaka ni biashara kumi tu ambazo huwa zinauvuka mwaka wa kwanza.
Na kati ya hizo biashara kumi ambazo huwa zinauvuka mwaka wa kwanza, bado ni biashara chache sana ambazo huwa zinaweza kuvuka mpaka kufikia miaka mitano.Hili wewe mwenyewe unaweza kulishuhudia kwenye maneneo yako unayoishi. Ni wazi kuwa kuna watu wengi ambao huwa wanajitahidi kila mwaka kuhakikisha kwabna wanaanzisha biashara mpya, ila ni wachache sana ambao huwa wanaweza kuendeleza biashara hizo kabla hawajafunga.
Unadhani shida hapa ni nini?
Kuna vitu kadha wa kadha ambavyo watu wanaoanzisha bishara kila mwaka wanakosa. Ukiwa na hivi vitu, ni wazi kuwa utaweza kufanya makubwa, naam, utaweza kufanya makubwa sana.Kwanza unapaswa kufanya biashara ambayo unapenda. Haupaswi kufanya biashara au kitu ambacho hupendi. Kwa sababu unaenda kuwa unaamka kila siku kwenye hii biashara maisha yako au kwa miaka mingi ijayo. Sasa haifai hata kidogo kwako kufanya biashara ambayo wewe mwenyewe hupendi, au hujisikii kufanya.
sasa kosa kubwa ambalo watu huwa wanafanya ni kufanya biashara kwa mkumbo. Kisa eti kasikia watu wanasema kwamba biashara fulani inalipa, basi na yeye anakimbilia kwenye kufanya biashara hiyo. Rafiki yangu, naomba unielewe kitu kimoja na cha uhakika. Fanya biashara unayopenda, tena biashara unayopenda kutoka moyoni, ila siyo biashara ambayo umesikia watu wanasema kwamba inalipa.
Hii siyo ngoma ya kuingia ili ubahatishe tu. Unapaswa kuchagua kitu ambacho kuwa tayari kukifanya kwa muda mrefuPili, unapaswa kufanya kwa muda mrefu. Siyo unaingia leo hii kwenye biashara halafu kesho unategemea kuwa umetoboa na kupata mafanikio makubwa. Kitu kama hiki hakipo rafiki yangu. inahitaji muda. ndio maana hata serikali huwa zinapewa muda. Unakuta kwamba muda wa uongozi wa serikali tangu wanapoingia madarakani mpaka uchaguzi mwingine unapofanyika ni miaka mitano. Hiki ni kipindi ambacho inatarajiwa kama jambo au mambo fulani yatafanyiwa kazi kwa mwendelezo kila siku na bila kuacha yatakuwa yameweza kuonesha matokeo.
Lakini siyo suala la kulala leo na kuamka kesho.Sasa nikuulize wewe kitu chako umeshakifanya mfululizo, tena kila siku kwa miaka mitano mfululizo. Kama bado hujakifanya kwa miaka mitano ujue wazi kuwa bado unahitaji kuweka nguvu na juhudi kubwa kwenye kukifanya hiki kitu.
SOMA ZAIDI: Kitu kimoja ambacho hupaswi kuacha kufanya hata kama una nguvu ya pesa
Tatu, unapaswa kujituma kwenye kazi na kuwa tayari kufanya kazi kwa viwango vya juu kuliko watu wengine. Hiki ni kitu muhimu sana rafiki yangu, na hakikisha kwamba unakifuatilia kwa umakini mkubwa sana na bila ya kuchoka.
SOMA ZAIDI: Fanya kazi kwanza, tutaongea

Nne, jali afya yako. kwa kuwa hii ngoma siyo ya muda mfupi, basi hakikisha kwamba unajali afya yako. Yaani, hakikisha kwamba afya yako imekuwa ni kipaumbele chako nambari moja. Mara zote na siku zote, ipambanie afya yako. Hakikisha kwamba afya yako ndiyo kipaumbele chako nambari moja kila siku. Kula vizuri, pata muda wa kulala pia na fuata taratibu zote za kitalaamu kwenye afya. Hili jambo litakufanya uwe na afya njema, mara zote uwe kwenye mapambano.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.
Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA
-
Ukifanya Hiki Kitu Kimoja Tu Utafanikiwa Sana
Rafiki yangu wa ukweli, kuna kitu kimoja ambacho endapo utakifanyia kazi, ni wazi kuwa utafanikiwa, tena siyo kwa viwango vya chini, bali utafanikiwa kwa viwango vya juu sana.Unaweza kuwa unajiuliza hili linawezekanaje maana kila siku najifunza kuhusu mambo mengi ya kufanya ili kufanikiwa.
Kitu kikubwa unachohitaji wewe siyo kufanya mambo mengi ili ufanikiwe, bali unahitaji kujithibiti wewe mwenyewe na kuhakikisha kwamba umekuwa na nidhamu kwenye yale unayotakiwa kuyafanya na kuyafanya bila ya kukosa. Ukiweza kufanya hili, ujue utafika mbali sana/
Hii ni kutokana na ukweli kuwa asilimia kubwa ya vile vitu vya msingi unavyotakiwa kufanya kwa ajili ya mfanikio yako, tayar unavijua.
Najua unajua kwamba unahitaji kuweka akiba. Kwa hiyo wewe unachohitaji sasa hivi siyo kuambiwa kwamba weka akiba. Unajua vizuri tu. unachohitaji ni nidhamu ya kuweka akiba bila ya kuacha.
Tayari unajua kwamba unapaswa kufanya kazi kwa bidii. Unachihitaji wewe siyo kuambiwa tena kwamba fanya kazi kwa bidii. Bali ile nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii.
Tayari unajua kwamba mafanikio makubwa hayaji ndani ya siku moja. bali ni matokeo ya vile vitu vodogovidogo unavyokuwa unafanya kila siku na unavifanya kwa mwendelezo bila ya kuacha.

Kwa hiyo, unachihitaji wewe siyo kusubiri uwe na mabilioni ya fedha kwenye akaunti yako ili uwe bilionea, bal unajua wazi kuwa kuweka akiba hata kama ni kidogokidogo kwenye akaunti yako kila siku, kutekupeleka wewe kwenye ubilionea huo
Kumbe basi rafiki yangu, unachohitaji wewe siyo vitu vingi sana ili ufanikiwe. Unahitaji kitu kimoja tu. na kitu hiki ni nidhamu ya kuamua kufanya jambo na ukahakikisha kwamba hilo jambo unalifanya kwelikweli.
Sasa ninachotaka kutoka kwako siku ya leo ni kitu kimoja tu. Nataka uniambie ni kitu gani kimoja ambacho utakuwa unafanya na utakufanya kwa msimamo kila siku bila ya kuacha. Halafu, mimi nikusaidie kukufuatilie kwenye hilo, ukifanye hicho kitu mpaka uifanikishe.
Hilo ndilo jambo kubwa sana ambalo nilitaka kukwambia siku ya leo. Naomba nikutakie kila la kheri.
Kitu kimoja cha ziada, ningependa tu kukumbusha kuwa semina yetu ya ana kwa ana ambayo itafanyika Morogoro mwezi wa sita, ndio hiyo hapooo inakaribia.
Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye semina hii ya kipekee sana.
Kitu kimoja cha kufanya ni wewe kuhakikisha kwamba unajiandikisha kwa ajili lya kuhudhuria semina hii. Fanya hivi. TUMA UJUMBE unaothibisha kwamba utashiriki kwenye hii semina kwa whatsap Namba 0755848391.
Ada ya semina ni 50,000/-
-
Tumezindua audiobook mpya, haya hapa ni mambo ya msingi ambayo unahitaji kuyajua.
Rafiki yangu mpedwa kwa mara ya kwanza kabisa mwaka jana tulizindua audiobook ya kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. ilikuwa ni audiobook ya kwanza ya kiswhili, Tanzania kama siyo Afrika Mashariki nzima. Watu wengi waliichangamkia hii audiobook, kitu kilichonifanya nione kwamba kuna uhitaji mkubwa wa hizi audiobook, kutokea hapo tumeendelea kutengeneza audiobooks za vitabu tofautitofauti. Ambapo mpaka sasa hivi tumetengeneza audiobooks zifuatazo.
1. JINSI YA KUFIKIA NZOTO ZAKO ina urefu wa saa 2 dakika 57 (sample ya audiobook hii iko hapa chini)
Hii ni sample ya audiobook, audiobook kamili ipo na ina urefu wa saa 2 dak 57. TUwasiline kwa 0687408755 2. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKA MAFANIKIO MAKUBWA (ina urefu wa saa 3 dakika 37) pamoja (sample ya audiobook hii iko hapa chini)
3. MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE ina urefu wa saa 5 dakika 06 (sample ya audiobook hii iko hapa chini)
Audiobook ya kitabu cha maisha ni fursa, tuliizindua mwishoni mwa mwaka jana.
Kitu kimoja ambacho nimekuja kugundua kwenye utengenezaji wa audiobooks ni kwamba watu ambao wanaonja utamu wa kusikiliza vitabu kwa sauti, hawataki kuacha hata kidogo. Hili nimeliona mwenyewe, maana wale waliopata kusikiliza audiobook hizo tatu hapo juu, wamekuwa wakinipigia au kunitumia jumbe kila mara kutaka kupata audiobooks nyingine zaidi.
Na kitu hiki kimenisukuma kuandaa audiobook nyingine mpya na hivyo leo nina furaha kubwa sana kukutangazia kuwa tumezindua audiobook ya kitabu cha JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO.

Audiobook hii ni ya kipeke sana na ambayo nashauri uhakikishe kwamba umeipata, tena sasa hivi.
Ina urefu wa saa 4
Imesomwa na Fadhil Kirundwa ambaye amekuwa anasoma audiobooks zetu za siku za nyuma.
Unaipata kwa telegram
Na gharama yake ni 15,000/-.ila habari njema ni kwamba endapo utafanya malipo siku ya leo. Basi hii audiobook utaweza kuipata kwa ofa ya shilingi 10,000/- tu. Malipo yote yafanyike kupitia namba ya simu ya 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Ukishafanya malipo. Tuma ujumbe kwa namba hiyohiyo ili uweze kutumiwa audioboook yako.
Utapokea audiobook yako ndani ya dakika tano tu baada ya kuwa umefanya malipo. Karibu sana.
-
Mabilioni yayeyuka upatu mpya
Hiki kichwa wala hata siyo mimi niliyekitunga, kilikuwa ni kichwa kwenye gazeti la mwananchi juzi. Ni moja ya habari ambayo imetikisa kwenye vyombo vya habari, na kwenye mitandao ya kijamii. Swali ambalo unaweza kuwa unajiuliza ni kuwa inawezekanaje watu wanalizwa kila mara kwa kutapeliwa na bado wanazidi kutapeliwa?
Utapeli hautaisha hapa duniani.
Moja kati ya matapeli wakubwa sana ambao waliwahi kuishi hapa duniani, ni bwana mmoja ambaye anajulikana kwa jina la Ponzi. Huyu jamaa alifanya utapeli wake miaka ya 1920
Huu ulikuwa ni mradi ambao ulikusanya pesa nyingi za watu na baadaye jamaa akawa ameyeyuka na pesa za watu.
Mpaka leo hii michezo ya upatu mingi imekuwa inajulikana kwa jina la PONZI SCHEME. Ikichukua jina la tapeli mkubwa sana kuwahi kutokea hapa duniani. Kabla ya huyu jamaa utapeli ulikuwa ukifanyika na hata baada ya utapeli huo mkubwa alioufanya, bado utapeli umekuwa unafanyika. Kwani mwaka 2008, tapeli mwingine mkubwa kwa jina la Bernoff alikuwa ametapeli watu zaidi ya dola bilioni 64.
Huu nao ulikuwa ni utapeli mkubwa sana.
Naweza kuonekana naongelea utapeli unaoendelea kwenye nchi za watu wengine, halafu ikaonekana kama vile hapa kwetu hakuna uutapeli unaonendelea. Hapa kwetu pia utapeli umekuwa unaendelea kwa wingi sana.
Nadhani, mara ka mara umekuwa unasikia watu wanavyotapeliwa.
Juzijuzi tu hapa kulikuwa na watu wanaitwa Kaylinda, hawa waliyeyuka na pesa nyingi za watu pia. Sasa juzi tena gazeti la mwananchi lililipoti taarifa ya mabilioni ya watu kulizwa kwa mabilioni yao kupelekwa.
Unachopaswa kufahamu mpaka hapa ni kwamba utapeli upo na utaendelea kuwepo kwa miaka yote ambayo binadamu atakuwa hapa duniani.
Hii hapa ni sababu kwa nini utapeli utaendelea kuwepo hapa duniani.
Kwanza unajua kwa nini watu huwa wanatapeliwa?
Watu huwa wanatapeliwa kwa sababu wanapenda kupata faida kubwa ndani ya muda mfupi, au huwa wanataka kupata fedha nyingi ndani ya muda mfupi na bila ya kufanya kazi. Hiki ndicho chanzo cha watu kutapeliwa. Na ndio maana watu wataendelea kutapeliwa.
Watu wataendelea kutapeliwa kwa sababu wanapenda hivyo vitu viwili nilivyoanisha hapo juu. Faida kubwa kutokana na uwekezaji wao, tena ndani ya muda mfupi pamoja na pesa nyingi tena bila ya kutoa jasho.
Sasa kwa kuwa matapeli wanayajua hayo mambo mawili, wakija kukutapeli wanaanzia hapo.
Wanakuahidi kukupa fedha nyingi ndani ya muda mfupi, tena bila ya kufanya kazi au kutoa jasho.
Kwa kuwa watu wanataka kuwekeza na kupata mrejesho mkubwa, hapo ndipo wanaanza kuchutapeliwa.
Viashiria kwamba hapa uwekezaji fulani ni upatu
1. Unaambiwa kwamba ufanye uwekezaji na hakuna hatari yoyote ile kwenye uwekezaji huo.
Kila uwekezaji una hatari zake, ukiona mtu anaanza kukwambia uwekezaji fulani hauna hatari yoyote, basi ujue kwamba hicho ni kiashiria cha kuwepo cha mchezo wa upatu.
2. wanatoa mrejesho mkubwa kwa watu wawekezaji wa kwanza ili kuwavutia watu kuwekeza zaidi. unachoopaswa kujua wewe kama mwekezaji ni kwamba hakuna uwekezaji ambao huwa unatoa mrejesho mkubwa tu mara zote. kuna wakati mrejesho unaweza kuwa ni mkubwa na muda mwingine ukapungua. Ila ukiona unaambiwa ukiwekeza utapata mrejesho mkubwa tu, au ukiona watu wanapewa mrejesho mkubwa tu kila mara. Basi hapo ujue kuwa kiashiria cha utapeli.
3. shughuli zinazoleta kipato hazijulikani. Yaani, wewe unaambiwa weka laki moja leo na kesho tutakupa laki mbili, lakini ukiwauliza ni shughuli gani ambazo zinawapa hicho kipato kwa haraka hivyo, wanakuwa hawako tayari kuziweka wazi. Ila wewe unaambiwa, wewe wekeza tu uone….
Ukiona hivyo, ukiwekeza tu ujue utaona kwelikweli…
Sasa ufanyeje ili kuepukana na kutapeliwa?
Rafiki yangu, hivi nilikwambia kwamba watu wamekuwa wanatapeliwa na wataendelea kutapeliwa kwa siku zote ambazo binadamu anaendelea kuishi. Ndio, sijakosea kwenye hili, na kuthibitisha hili wewe mwenyewe unaweza kujaribu kuorodhesha utapeli ambao umewahi kusikia au kuona kwa macho yako tangu umekuwa na akili timamu. Tuachane na tangu umekuwa na akili timamu, tuchukue tu hata miaka mitano iliyopita. ni mara ngapi umesikia watu wametapeliwa. Ni mara nyingi sana. na hao ni wale ambao walitangazwa kwenye vyombo vya habari, kuna wale amba habari zao hazisikiki kwenye vyombo vya habari, na hao ni wengi pia.
Ssa ufanyeje ili kuepukana na kutapeliwa?
Yafuatayo ni mabo ya kuzingatia.
Kwanza usikurupuke kuwekeza. Kisa unaona watu wengi wanakimbia kuwekeza na wewe unakimbia tu kuwekeza.

Pili, wekeza kwenye uwekezaji unaoeleweka. Kama kitu hukielewi, usiweke hela yako hata kama wanakuahidi kukupa hela mara elfu moja ya ile uliyoweka. Warren Buffet ni mmoja wa matajiri wakubwa sana hapa duniani, na anafanya uwekezaji. Lakini kitu kikubwa sana kuhusu gwiji wa uwekezaji ni kwamba huwa hawekezi kwenye vitu ambavyo havielewi. Yeye huwa anawekeza tu kule anapokuelewa.Hiki kitu kimefanya watu wengi wamseme sana, ila yeye kwa upande wake ameendelea kusimamia msimamo wake huo bila kuteteleka. Mfano, moja ya msimamo wake ni msimamo wake wa kutowekeza kwenye makampuni ya mitandao ya intaneti. Ni aina ya biashara ambayo alikuwa haielewi, na hivyo hajawekeza huko. Ndio kuna watu wamewekeza na wanapata faida nzuri, ila yeye haelewi, hivyo, hata haweki nguvu kwenye hayo makampuni.
WEWE pia kwa upande wako unapaswa kuwa hivyo, usiwekeze kwenye kitu ambacho hukijui.
Tatu, Wekeza kwenye uwekezaji uliorasimishwa na serikali kama uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE unmerasimishwa na unaendeshwa chini ya soko la HISA LA DAR ES SALAAM. Kuelewa zaidi kuhusu hisa, hatifungani na vipande basi soma kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Hiki ni kitabu ambacho kimewasaidia watu wengi, na wewe kitakusaidia pia. Kipate hiki kitabu kwa manufaa yako.

Pata hiki kitabu kwa 20,000 hardcopy na 10,000 softcopy Sambamba na hicho kitabu, kuna kitabu kingine muhimu sana ambacho unapaswa kuchukua. na kitabu hiki siyo kingine bali ni hiki hapa

Kipate kitabu hiki kwa manufaa yako Kupata vitabu hivi, wasiliana na 0755848391. Au bonyeza hapa kutuma ujumbe kwa whatsap. BONYEZA HAPA
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.
Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA