Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Tofauti Kati Ya Kazi na Ajira

    Kazi ni kitu ambacho kinampa mtu heshima. Na hata maandiko mbalimbali yamethibitisha na kusisitiza hili la kufanya kazi kwa namna tofauti tofauti, huku maandiko maarufu yakiwa yale yanayosema kwamba asiyefanya kazi basi asile. Rafiki yangu, kazi ni moja ya kipimo cha utu.

    Kwa hiyo, kama unataka kuheshimika kwenye jamii, basi fanya kazi.

    Kwa watu wengi unapoongelea kazi, basi kinachokuja kwenye kichwa chao au kwenye akili zao ni kuwa ajira.  Yaani, kazi fulani hivi ya kukaa ofisini huku kukiwa na kiyoyozi, huku wenyewe wakiwa wananesa kwenye kiti fulani hivi amazing! Rafiki yangu, kuna tofauti kubwa sana kati ya kazi na ajira.

    Kamusi ya Kiswahili sanifu inasema kazi ni shughuli anayofanya mtu kama vilekulima, kuandika au kufundisha.

    Huku ikisema kuwa ajira ni kazi izitolewazo au zifanywazo kwa malipo katika kampuni serikalini au kwa mtu binafsi.

    Kumbe kwa mantiki hiyo ndiyo kusema kwamba, kazi zipo nyingi. Kufanya kazi siyo lazima uwe umeajiriwa chini ya mtu, unaweza kufanya kazi hata kama hujaajiriwa. Unaweza kujishughulisha wewe mwenyewe. Kwa mfano unaweza kuanza kutengeneza vitumbua na kusambaza kwa kuanzia mtaani kwako. hivi kweli kitu kama hiki nacho kinaweza kukushinda?

    Kitumbua kimoja kinauzwa shilingi 100. Kila siku ukijiwekea lengo la kutengeneza vitumbua na kuuza vitumbua 500, maana yake kila siku utakuwa unaingiza kiasi cha shilingi  elfu hamsini.  ili uweze kufanikisha lengo lako hili la kuuza vitumbua 500 kila siku unahitaji walau uwe na kijana mmoja ambaye anajituma na anafanya kazi kwelikweli. Mmoja wenu, anaweza kuwa yeye au wewe anakaa chini na kutengeneza vitumbua, huku mwingine akizunguka mtaani na kusambaza vitumbua kwa watu wenye uhitaji, ikiwa ni pamoja na kwenda kwenye maeneo yenye mkusanyko mkubwa watu kama stendi na sokoni.

    Rafiki yangu, kwa jinsi hii unakuwa umejitengenezea kazi lakini wakati huohuo unakuwa tayari umetengenza ajira. Kwenye hiyo shilingi elfu hamsiini uliyouza ndani ya siku husika, ukitoa gharama au mtaji wa biashara yako. Huwezi kukosa kubaki na hela ya kwako, tena hela ya maana tu. ebu tuchukulie baada ya kutoa gharama zote ukabaki na elfu ishirini tu. Hii siyo hela kidogo, ukiwa unaingiza kiasi hiki cha hela kwa mwezi ni sawa na laki sita!

    Wewe unakuwa siyo mtu wa viwango vya kawaida. Mpaka hapo unakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja, ukiendelea kukaza unashangaa baada ya miaka mwiili una kiwanda chako cha kutengeneza vitumbua. Usicheke, ujue hapa naongea vitu siriazi!

    Kwa hiyo, rafiki yangu, achana na dhana ya kulia kuwa hauna kazi kuanzia leo hii. tafuta kazi na anza kufanya kazi.

    • Inaweza kuwa ni kutengeneza vitumbua kama nilivyokwambia
    • Inaweza kuwa ni vitu vingine kama kuuza karanga, kulima mboga, na vitu vingine vingi
    • Nadhani kuna mawazo mengi ambayo unaweza kuanza kufanyia kazi leo hii, tena ambayo yanahitaji mtaji mdogo tu!

    Tatizo kubwa linalowakumba vijana wengi ni kudharau kazi wakati hawana kazi. Na hii zaidi ni kwa wasomi ambao wamehitimu vyuo na ngazi nyingine, wanaona kwamba baadhi yakazi siyo kazi za viwango vya, hivyo, kitu pekee ambacho wao wanaamua kufanya ni kukaa bila kufanya kazi.

    Rafiki yangu, kama hauna kazi na haujui kitu gani unaswa kufanya, basi usidharau. Chagua kazi yoyote ile kisha anza kuweka juhudi kwenye hiyo kazi. Ifanye ili iweze kukuingizia kipato.

    Siyo eti kwa sababu umesoma basi muda wote unabaki kusuka nywele huku ukihofia kwenda shambani kufuga na kulima, huku ukiendelea kulalamika kuw ahuna kazi.

    Kuuza vitu vya mia mia

    Hapo juu nimetolea mfano wa mtu ambaye ameamua kujiajiri kwa kufanya kuuza vitumbua. Tena nikatolea mfano kuwa kitumbua kimoja kinauzwa shilingi mia moja! (japo vipo vitumbua ambavyo vinauzwa zaidi ya hapo). sasa hapa ninachotaka kukwambia ni kuwa vitu vya mia mia vinawapa hela kuliko unavyoweza kufikiria.

    Ndio maana unaona mpaka mabilionea wanazidi kutegeneza vitu vya mia mia! Hivi kiberiti, kinauzwa shilingi ngapi vile… Huku mtaani kwetu kinauzwa shilingi mia moja sijajua huko kwenu. Mo Dewji ni bilionea mkubwa hapa Tanzania, ila huku mtaani kuna viberiti ambavyo ametengeneza yeye.

    Hivi, pipi zinauzwa shilingi ngapi vile…najua utaniambia bei tofauti zikiwemo za mia moja na mia mbili au hata zaidi..

    Kuna watu wenye hela zao, wamewekeza mabilioni ya hela wanatengeneza pipi eti. Tena pipi zingine zinauzwa shilingi hamsini tu za Kitanzania.

    Ninachotaka kukwambia ni nini? ninataka kukwambia kwamba usidharau vitu vidogo, maana hivi vitu vidogo mwisho wa siku huwa vinakuwa na matokeo makubwa kuliko unavyoweza kufikiri.

  • Vitu Viwili Kuhusu Kipaji Ambavyo Hakuna Mtu Amewahi Kukwambia

    Jana nilikuwa naangalia mahojiano kati ya mtengenezaji wa maudhui kutoka Ghana maarufu sana kama Wode Maya na msanii wa Zimbabwe Jah Prayzah.

    Kuna mengi waliyongea ila mimi binafsi niliondoka na mawili ambayo yamenigusa na ambayo nimeona nikushirikishe na wewe.

    Kitu  cha kwanza kabisa Jah Prayzah alisema hivi, mimi sikuchagua kuwa msanii ila nilichaguliwa kuwa msanii. Hii maana yake nini, maana yake ni kwamba kuimba kupo ndani yake. Hiki ni kipaji chake cha kuzaliwa nacho kabisa.

    Nimekuwa nakushauri mara kwa mara rafiki yangu kuwa na wewe uhakikishe unajifanyia tathimini ili uweze kugundua na kutumia kipaji chako.  Ukigundua kipaji chako rafiki yangu na ukakitumia, mara zote utakuwa ukifanya kazi yako na majukumu yako kwa furaha. Kwa sababu unafurahia kazi au kile unachofanya.

    Kuna siku Arnorld Schwarzenegeer aliwahi kuulizwa, kwa nini, unakuwa na furaha sana muda wote mbali na kuwa unakuwa unanyanyua vyuma kwa muda wa saa tano kila siku. Watu walimuuuliza hivi kwa sababu waliona wengine waliokuwa wananyanyua vyuma hawakuwa na furaha hata kidogo kwenye maisha yao. Kwa kujibu hili Arnorld Swacherzenegger alisema kwamba, ninapenda ninachofanya. Rafiki yangu, kipaji chako ni kitu ambacho kinapaswa kitu kinachotoka moyoni. Kitu ambacho huoni kama umelzimishwa au umesukumwa kukifanya, badala yake unahisi kama kuna msukumo wa ndani kabisa ambao unakusukuma wewe kukifanyia kazi kipaji chako na kukifanikisha kwa viwango vikubwa

    Kitu cha pili Jah Prayzah alisema kwamba, mimi mpaka leo bado nafanya kazi kwa bidii kama msanii mchanga. Yaani, bado najituma kwa nguvu zangu zote kama msanii ambaye hajatoboa, na sasa ndio anatafuta namna ya kuweza kutoboa na kwenda hatua ya ziada kwenye maisha.

    Hiki kitu rafiki yangu na wewe kitumie kwenye kazi zako na kwenye kitu chochote kile ambacho unafanya. mara zote fanya kazi kama vile wewe bado ni mchanga kwenye sekta ambayo unafanyia kazi, hata pale unapokuwa umekua na umeweza kufika viwango vya juu. Kwa nini?

    Ili niweze kujibu kwa nini yako kwa undani zaidi, naomba nikutolee mfano mzuri kwenye biashara, mwanzoni mtu anapoanzisha biashara anakuwa anajituma na kuweka nguvu kubwa sana kuhakikisha kwamba biashara yake inakua. Anatafuta wateja, anawapigia simu na mambo mengine mengi. Yote haya anayafanya kwa lengo moja tu, la kuhakikisha kwamba anafanya mauzo zaidi kwenye biasahra yake. Lakini kadiri biashara hiyo inavyokuwa inazidi kukua, inafikia hatua ambapo yule mtu anasahua ile misingi iliyomwinua na hivyo, kujikuta kwamba anaanza kufanya kazi kwa mazoea.

    Na hapo ndipo anguko la biashara nyingi huwa linatokea.

    Hiki kitu huwa hakitokei tu kwenye biashara peke yake, bali pia kwenye kwa watu wenye vipaji vyao. Unakuta mtu ana kipaji kizuri, anakifanyia kazi, anakua na kufikia viwango vya juu, ila sasa baada ya muda anasajisahau, anarelax na kuanza kuishi maisha ya kawaida sana. kitu ambacho huwa kinamepekea kwenye anguko. Hapa ndipo huwa unasikia habari za kwamba

    Msanii fulani ameshuka kiwango

    Au mchezaji ameshuka kiwango

    Kinachomfanya ashuke kiwango siyo kitu kingine bali ni kwamba zile juhudi alizokuwa anaweka mwanzoni kwenye kazi, sasa haweki juhudi hizohizo, kitu hiki kinamfanya aanze kushuka kidogo kidogo na baadaye anashuka kabisa.

    Kwa hiyo rafiki, mara zote fanya kazi kama vile ndio kwanza unatafuta maisha.

    KIPAJI NI DHAHABU
    Rafiki yangu, nimeandika kitabu. Kinaitwa KIPAJI NI DHAHABU. Ili kupata kitabu hiki, wasialiana na mi kwa 0755848391 sasa

    Rafiki yangu, ili kukurahisishia safari yako ya kukifanyia kazi kipaji chako. Nimekuandalia kitabu maalumu kabisa, kinaitwa Kipaji ni Dhahabu. Nashauri sana uweze kusoma kitabu hiki cha kipekee kwa shilingi elfu kumi tu.

    Kupata nakala yako, wasiliana nami kwa 0755848391

  • Kitu hiki kimoja kitakutofautisha wewe na watu wengine wenye kipaji kama cha kwako

    KIPAJI NI DHAHABU
    Rafiki yangu, nimeandika kitabu. Kinaitwa KIPAJI NI DHAHABU. Ili kupata kitabu hiki, wasialiana na mi kwa 0755848391 sasa

    Kama kuna kitu ambacho kinaweza kukutofautisha wewe na watu wengine wenye kipaji kama cha kwako basi kitu hiki siyo kingine bali ni kujifunza na kulielewa eneo ambalo unafanyia kazi kwa undani zaidi kuliko mtu mweingine yeyote. Yaani, unahakikisha kuwa taarifa zote za  muhimu kuhusana na kipaji chako unakuwa nazo na unazitumia kwa manufaa kuhakikisha kwamba unaweza kufika kule uhnaptaka kufika kwenye maisha yako.

    Ukiwa na taarifa sahihi ni rahisi pia kufanya maamuzi bora (sound choice). Kwa hiyo, jitahidi kuhakikisha kwaba unalifanyia kazi. na njia ya wewe kulifanyia hili kazi ni kuhakikisha kwamba unajifunza kila mara kwa kusoma vitabu na kupitia majarida mbalimbali.

    Kamwe usikifikie hatua ambapo utajiona kama vile umefika au umekamilika. Badala yake infanye kila dakika ambayo upo hapa duniani kuwa ni dakika yako ya kujifunza na kukielewa vizuri kipaji chako nje ndani, hili jambo hili rafiki yangu. ukilifanyia kazi baada ya siku nyingi sana ni wazi kuwa hili jambo moja tu litakufikisha mbali.

    Kama huamini lijaribu kwa kuliweka kwenye vitendo ili uweze kuona maajabu yake na namna ambavyo litafanya kazi kwako. kumbuka kwamb alinafanya kazi kwa wengine, na litafanya kazi kwako pia.

  • Hiki kitu Kimoja Tu, Kitakufanya Utumie Kipaji Chako Kwa Viwango Vikubwa

    KIPAJI NI DHAHABU
    Rafiki yangu, nimeandika kitabu. Kinaitwa KIPAJI NI DHAHABU. Ili kupata kitabu hiki, wasialiana na mi kwa 0755848391 sasa

    Leo asubuhi nimeamka na kuangalia video moja ambayo Kobe Braynat alikuwa akihojiwa na Patrick Bet-David. Moja ya swali ambalo Kobe Brayant aliulizwa ni kuwa ni msukumo gani ambao umekuwa ukimsukuma kujituma na kuhakikisha anakuwa jinsi anakuwa mchezaji bora. Kati ya mengi ambayo ameongea, kitu kikubwa amesema sitaki siku moja nije nianze kujuta kuwa ningeweza kuwa zaidi ya hapo. nataka nihakikishe kamba natumia uwezo wangu kwa viwango vya juu  kiasi kwamba hakuna siku hata moja ambayo nitakaa na kuanza kujuta kwa nini sikuweza kukamilisha jambo fulani ambao nilipaswa kuwa niweza kufanikisha.

    Kobe Brayant

    Rafiki yangu, sijui wewe upo kwenye hali gani kwenye maisha, na wala hata siui kipaji wala uwezo wako ni upi. Ila kitu kimoja cha kuhakika ni kuwa kama na wewe utayatumia haya maneno ya kobe Brayant kwenye maisha yako ni wazi kuwa unaenda kufika mbali na kufanya makubwa. Hii ndio kusema kwamba utajituma zaidi ya unavyofanya sasa hivi, siyo ilimradi tu umejituma, bali ukiwa unajua kuwa sitaki hata siku moja kuja kujutia.

    Rafiki yangu, kama una nafasi ya kufanya makubwa leo hii, usiwe mzembe. Yafanye haoyo  makubwa.

    Kama unaweza kufanya mazoezi leo, fanya hivyo.

    Kama kuna wateja ambao unaweza kuwapigia simu leo hii ili waje kununua kwako, wapigie simu.

    Kama kuna kitu unaweza kufanya, kifanye. Kwa vyovyote vile rafiki yangu, hakikisha kwamba, mara zote unajisukuma kuwa bora zaidi ya vile ulivyo sasa hivi.

    Rafiki yangu kama kila mtu kwenye hii dunia akifanya kile anachopaswa kufanya kwa namna anavyopaswa kukifanya, ni wazi kuwa hii dunia itakuwa sehemu nzuri sana.

    Nzuri kwelikweli!

    Lakini ukweli ni kuwa hatuwezi kusubiri kila mtu afanye ndio na sisi tuanze…

    Mimi na wewe tuanze. Tufanye kile tunachopaswa kufanya, wengine wataona na wataiga kutoka kwetu…

    Timiza wajibu wako kama unavyopaswa kuutimiza.

    Kama wajibu wako ni kupika chakula…kipike vizuri sana.

    Kama wajibu wako ni kucheza..cheza

    Kama wajibu wako ni kufundisha fanya hivyo

    Fanya hivyo kiasi kwamba hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kufanya kazi unayofanya kwa viwanvgo unavyofanya. Kwa jinsi hiyo utakuwa umejitofautisha…

  • Sababu Sita Zisizopingwa Kwa Nini Unapaswa Kuendeleza Kiapaji Chako

    KIPAJI NI DHAHABU
    Ili kupata kitabu hiki, wasialiana na mi kwa 0755848391 sasa

    Kwenye kitabu cha Acres of Diamond, mwandishi ameeleza historia ya jamaa ambaye aliambiwa kuwa ukiwa na almasi yenye ukubwa kidole unaweza kuimiliki dunia. Huyu jamaa kusikia hivyo, aliamua kusafiri kwenda kuitafuta dhahabu ambayo mwisho wa siku hakuipata!

    Siku hizi bado watu wanatafuta dhahabu! Utasikia watu wanapeana stori kuwa ukienda kwenye machimbo ya Geita au Mererani basi wewe kutoka kimaisha ni njenje tu! lakini ukiachana na hayo ni ukweli kuwa  mbali na hayo madini na hizo dhahabu ambazo unaweza kupata kutoka kwenye hayo maeneo, kuna dhahabu  ambazo watu wanazo ila wanaonekana kutozitumia vizuri na dhahabu hizi siyo nyingine bali ni uwezo na vipaji tulivyonavyo. Ukifahamu thamani ya kipaji, utajihidi kuhakikisha kwamba unatumia kipaji chako kwa nguvu zako zote bila kuacha. KIPAJI NI DHAHABU. Na unapaswa kukinoa vizuri rafiki yangu.

    Kwa leo nataka niingie kwa undani na kukueleza sababu sita kwa nini hasa unapaswa kunoa kipaji chako, ili kiweze kuwa chenye manufaa kwako wewe mwenyewe.

    Sababu ya kwanza ni Umezaliwa Nacho Wewe Ila Siyo Chako

    Huwa napenda kuwaambia watu kuwa unapewa kipaji sio kwa manufaa yako, bali kwa manufaa ya jamii nzima. Na kuthibitisha hili hapa huwa napenda kutolea mfano wa mwanamziki.

    Mwanamziki akiimba wimbo wake sio tu kuwa unamnufaisha yeye peke yake, bali wimbo huo unakufaisha hata wewe ambaye unausikiliza. Tena unakuta kwamba wewe msikilizaji ndiye unasikiliza ule wimbo kuliko hata mwanamziki mwenyewe. Kwa hiyo, wewe unapokuwa na kipaji unapaswa kukifanyia kazi sio tu kwa ajili ya manufaa yako bali kwa manufaa ya watu wengine pia.

    Kuna watu wengine ili waweze kufanikisha vipaji vyao wanahitaji wewe ufanyie kazi kipaji chako kwanza. Ebu chukulia mfano wa mtu kama Albert Einstein. Huyu ni mtu ambaye alikuwa na kipaji cha hesabu mpaka akaweza kuja mlinganyo maarufa sana kwenye fikizia wa E=Mc2. Lakini Einstein sio baba wa fikizia!

    Inawezekana kama akina Newton na Galileo wasingeweka njia, basi kipaji cha Einstein kisingeonekana. Kwa hiyo hakikisha unatumia kipaji chako, kwa ajili ya manufaa yako, kwa ajili ya manufaa ya jamii, na kwa ajili pia ya kuhamasisha watu wengine.

    Mwaka 2007 ulikuwa ni wa kipekee kwenye ulimwengu wa kidigitali. Ni mwaka ambao kwa mara ya kwanza simu janja (smartphones) zilivumbuliwa na kuletwa kwenye umma wa watu. hata hivyo, cha kushangaza ni kwamba, aliyegundua simu hizi, alishalala zamani ila simu hizi zimeendelea kuwa zenye faida na manufaa kwa watu wengine zaidi yake. Hiki kitu kikuoneshe na wewe kuwa kipaji au huo uwezo ulio nao ndani yako siyo tu kwamba ni wa kwako peke yako, bali upo pia kwa ajili ya manufaa ya watu wengine.

    Leo hii watu wengi wananufaika kwa kutumia simu janje pengine kuliko hata aliyetengeneza simu hizo. Simu zinawaingizia watu fedha, simu zimetumika kuwaunganisha watu walio mbali, simu zimewezesha kuwatumia fedha ndugu zetu walio mbali…

    Kuna watu wameweza kugundua vitu vingine kwa sababu tu walikuwa na simu au walikuwa wanajua kuna simujanja. Kwa mfano, hizi app za simu zimetengenezwa mara tu baada ya kuwepo kwa simu. Kuna watu maisha yao yanategemea app za simu tu.

    Sasa ebu jiulize kama aliyetengeneza simujanja angeamua kufa na uwezo wake, leo hii hawa watu ambao maisha yao yanategemea app za simu peke yake wangekuwa wapi?

    Kumbe muda mwingine kipaji chako kinaweza kuwa kimebeba ajira za watu wengine ila wewe hujui tu. Ebu kifanyie kazi siyo tu kwa ajili ya manufaa yako, bali kwa ajili ya manufaa ya watu wengine pia.

    Sababu ya pili ni kuwa kuna watu wanaweza kubadlil maisha kwa sababu ya kipaji chako. Endapo utafanyia kazi kipaji chako na kukifanikisha kuna watu ambao watajifunza kwako na watataka kunoa vipaji vyao ili wawe kama wewe.

    Hujawahi kusikia mtu anasema nikikua nataka niwe kama mtu fulani. Sasa kuendeleza kipaji chako kunawafanya  watu watamani sana  kuwa na maisha kama ya kwako.

    Kuna watu wengine watanoa na kufanyia kazi vipaji vyao kwa sababu wanajifunza kwako.

    Ngoja ni kwambie kitu rafiki yangu. ujue kitu kimoja kwenye maisha ni kuwa kwa vyovyote vile, popote pale ulipo kuna watu ambao wanajifunza kitu kutoka kwako. Inawezekana nyuma yako kuna watu wawili au mmoja ambao ni mashabiki wako, sasa hawa watu wakikuona wewe unafanyia kazi kipaji chako, ni wazi kuwa wenyewe watatamani sana kuweza kunoa kipaji chao na kukifanikisha,

    Kuna watu wamekuwa wanamziki baada ya kuwa wamemwona mtu wa mtaani kwao kwenye runinga au kumsikia kwenye redio. Hiki kitu kimewapa hamasa kubwa na hivyo wao wakapambana ili na wao waweze siku moja kuonekana kwenye redio na runinga.

    Na mimi nina uhakika leo hii ukifanyia kazi kipaji chako, kuna watu nyuma yako watapenda na watakuwa tayari kutaka kufuata nyayo zako. usiwaangushe, noa kipaji chako. Kiendeleze mpaka kiimarike.

    Sababu ya tatu ni kuwa utaishi maisha ambayo unayapenda. Utafiti maarufu ni kuwa watu wengi huwa wanakufa jumatatu asubuhi. Kwenye utafiti huu wanaonesha kuwa wengi wa wale ambao huwa wanakufa siku ya jumatatu ni wale ambao huwa hawapendi kazi zao. Yaani, mtu anaenda kazini lakini kazi yenyewe anayoifanya siyo ile ambayo anapenda.

    Hivyo akishakula bata siku za wikendi, halafu akaamka jumatatu akiwa anafahamu kuwa anaenda kufanya kazi ambayo hapendi, anakata tamaa na kupoteza maisha.

    Rafiki yangu, kipaji chako ni kitu ambacho unakipenda. Unapofanyia kazi kipaji chako, maana yake unakuwa unafanyia kazi kile ambacho wewe mwenyewe unapenda. Sijui umenielewa mpaka hapo.

    Hiki kitakufanya uishi miaka mingi na kheri duniani! Watu wanaofanya kile wanachopenda wana furaha, wana amani ya mwili na roho, wanajiamini kwenye kazi zao na hawana msongo

    Ila kama unafanya kazi ambayo huipendi matokeo yake yanakuwa ni tofauti. Na utafiti mwingine unaonesha kwamba watu wanaotumia uwezo na vipaji vyao wanafanya vizuri zaidi kwenye kazi kuliko wale ambao hawatumii vipaji na uwezo wao.

    Sababu ya nne ni kuwa utatengeneza fedha kutoka kwenye kipaji chako

    Kadiri utakavyokuwa unakitumia kipaji kuna watu wataona kwamba wanaweza kunufaika na kipaji chako, na hivyo kuwa tayari kulipia ili wapate vitu vingi zaidi kutoka kwako

    Sababu ya tano ni kuwa utaacha alama inayodumu milele. Kwa kazi ambazo utazifanya kutokana na kipaji chako, mwisho wa siku unaenda kuacha alama ambayo itadumu kwa siku nyingi hata baada ya wewe kuwa umeaga dunia.

    Sababu ya sita kujiondolea majuto. Usipofanyia kazi kipaji chako, kuna siku utaanza kujuta kwa nini hukufanyia kazi kipaji chako. Kwanza, utasikia kwenye vyombo vya habari kwamba vijana machachari sehemu fulani, wameweza kufanya mambo makubwa. Wakati nawe, ulipaswa kuwa kijana machahari kama hao wanaotajwa. Hiki kitu  kitakuumiza na kukukatisha tamaa.

    Pili, utaanzisha usemi utakaokuwa unautoa kama hadithi kwa watoto mpaka kwa wajukuu wako. Utaanza kuwaambia, bwana mnamwona fulani, nilisoma naye ila sasa hivi hashikiki. Kama si hivyo huenda ukasema kwamba, nilikuwa ninakaa naye darasa moja ila sasa hivi amefanikiwa sana. Utasema, kuna kipindi huyu mtu alikuwa na maisha mabaya ila sasa hivi maisha yake yamebadilika sana. Au pengine utasema, mimi ndiye nilikuwa kinara darasani na huyu jamaa hakuwahi hata kuonekana kwenye zile kumi bora. Binafsi, nimekuwa ninawavumilia sana wazee ambao wanasema hivi. Ila wewe, sitakuvumilia hata kidogo.

    Nitakuuliza, wakati hawa wanapambana wewe ulikuwa wapi? Ni kitu gani kilikuzuia wewe kufanya makubwa? Je, hawa watu walikufunga kwenye mti wakaanza kuchapa kazi, sasa ndiyo wamekuja kukufungua? Kiukweli sitakuvumilia.

    Rafiki yangu, hizo ni sababu zangu sita kwa nini wewe unapaswa kufanyia kazi kipaji chako tena, kuanzia leo hii. rafiki kama kuna zawadi unapaswa kujipa wewe mwenyewe kwenye maisha, basi ni zawadi ya kufanyia kazi kiapji chako. Halafu ujue kwamba nina zawadi ya kitabu ya kitabu. Kipokee kitabu chenyewe kwa kujaza taarifa zako hapa chini

    kitabu cha maajabu ya kuweka akiba

  • Jinsi Ya Kutangaza Kipaji Chako

    Moja kati ya kitu ambacho nimekuwa nikiwaambia watu wengi ni kuwa tuna bahati ya kuishi kwenye ulimwengu wa leo tunaoishi. Mababu zetu wangekuwa wanarudi leo hii na kuona fursa kibao zilizotuzunguka, ni wazi kuwa wenyewe wangetuonea gere.

    Mambo ambayo miaka hiyo yalikuwa hayawezekani, leo hii yanawezekana, tena siyo kwamba yanawezekana kidogo, yanawezekana sana tu.

    Ebu chukulia kwa mfano jinsi ilivyokuwa kazi ngumu kunoa kipaji chako miaka ya nyuma. Tusiende mbali sana, tuongelee miaka michache hii baada ya uhuru. Kiukweli, kunoa na kuendeleza kipaji chako ilikuwa ni moja ya kazi ngumu kitu hiki kilifanya watu wengi washindwe kunoa na kuendeleza vipaji vyao. Na hata wengine kwa kukosa maarifa sahihi kama ambayo nimeandika kwenye kitabu cha KIPAJI NI DHAHABU, walishindwa kabisa kujua vipaji vyao.

    KIPAJI NI DHAHABU
    Ili kupata kitabu hiki, wasialiana na mi kwa 0755848391 sasa

    Ebu tuchukulie mfano kuwa ulikuwa na kipaji cha kuimba, miaka hiyo na labda ulikuwa mkoa wa Mtwara. Kwanza ili kurekodi wimbo ulipaswa kwenda studio na kuwasilisha wazo lako, ambapo studio wazo lako lingeweza kukubaliwa au kukataliwa, lakini pia ulipaswa kuwa na hela kubwa ya kukusaidia kurekodi wimbo wako.

    Baada ya kuwa umerekodi huo wimbo ulipaswa kuwa na mtu wa kusambaza hizo nyimbo zako na hata wafadhili wa kukupiga tafu kwenye kazi zako.

    Siyo hilo tu, kama miaka hiyo ulitaka kutangaza wimbo wako, njia za kipekee na za uhakika za kutangaza wimbo huo, zilikuwa ni kupitia vyombo vya habari. Kwa kuwa vyombo vingi vya habari vilikuwa Dar, wewe uliyekuwa Mtwara, ulilazimika kusafiri mpaka Dar ili ukutane na watu hawa wa vyombo vya habari au la kutangaza kipaji chako kwenye hivi vyombo vya habari ilikuwa ni ngumu sana.

    Na hata baada ya kukutana nao kutokana na mfumo uliokuwepo wangeweza kukukubali au kukukatalia au hata kutaka uwape rushwa kubwa ili wakufanyie tangazo.

    Sasa chukulia hiyo hali na jinsi mambo yalivyo sasa hivi, kwa sasa hivi mambo yamebadilika kwa asilimia 100. Huo mchakato wote umevunjwa kiasi kwamba unaweza kufanya hayo yote bila kizuizi kikubwa.

    Kama una wimbo au kipaji cha kuimba na ukatunga wimbo wako. Unaweza kwenda studio na kurekodi wimbo wako

    • kwa gharama nafuu sana na
    • bila vikwazo

    Pengine unaweza ukawa hauna hela ya kurekodi, ukaamua tu kuanza kutumia simu yako kurekodi wimbo wako na hata baadaye ukautoa.

    Kama nakuona vile unavyoguna kuwa haiwezekani kurekodi wimbo kwa kutumia simu!

    Ila kabla hujakataa kabisa hilo wazo kuna vitu viwili ambavyo ningependa kukwambia.

    Kama unatumia simu janja (smartphone), simu yako ina uwezo mkubwa kuliko kompyuta iliyopeleka mtu mwezini. Huo ni ukweli nambari moja. Sasa ebu fikiria kompyuta iliyopeleka mtu mwezini ilikuwa na uwezo mdogo kuliko simu yako janja, je,unadhani kompyuta zilizokuwa zinatumika kurekodi nyimbo miaka hiyo zilikuwa zinafananaje? Ni wazi kuwa uwezo wake ulikuwa ni mdogo zaidi. Kumbe simu yako hiyo ni mgodi mkubwa sana ambao umeulalia, jitahidi sana ili uweze kuutumia mgodi huu.

    Niendelee au nisiendelee!

    Ukweli nambari mbili ambao utakufungua macho zaidi ni juu ya vijana wa Nigeria waliorekodi movie kwa kutumia simu. Vijana hawa kutoka Nigeria Kaskazini, walikuwa na simu moja hivi ambayo imekwaruzwakwaruzwa kwenye kioo. Ila waliitumia hiyo hiyo kama kamera kuhakikisha kwamba wanarekodi tamthiliya.

    Kumbe kama una simu kubwa, maarufu kama simu janja au smartphone basi jua wazi kuwa umelalia hazina kubwa sana ambayo haupaswi kuichezea rafiki yangu. Ni hazina ambayo mababu zetu hawakuwa nayo, ila wewe una bahati ya kuwa nayo. Usiitumie ktu kuchati, bali itumie kwa manufaa.

    Kuna watu wamerekodi video na kuziweka kwenye mitandao kama youtube na tiktoka na hatimaye kunufaika na kupata fedha. Kuna watu wametengeneza kazi mbalimbali za sanaa kwa kutumia simu zao. Mimi nimeitumia simu yangu kuandika vitabu na kuendesha mitandao ya blogu yangu ya songambele (www.songambele.co.tz). Rafiki yangu badala ya kusubiri siku ambayo utakuwa na rasilimali kubwa na za kipekee hakikisha  kwamba unaanza kuzitumia hizi rasilimali za kawaida ulizonazo. Ukiweza kuzitumia vizuri hizi rasilimali kidogo ulizonazo, ukipata rasilimali kubwa ni uhakika kuwa utaweza kufanya makubwa zaidi ya hapo.

    vijana wa Nigeria wakirekodi Movie kwa kutumia simu yao

    Bado unafikiri haiwezekani kurekodi muziki wako kwa kutumia simu? Kama unafikiri kitu hiki  hakiwezekani basi fikiri tena!

    Kwenye mtadao wa Tiktok kuna kijana mmoja maarufu sana ambaye ana wafuasi wengi kuliko watu wote kwenye mtandao huo. Kijana huyu si mwingine bali ni kijana Kaby Lame. Huyu kijana ni raia wa Senegali anayeishi Italia. Mpaka mwaka 2020 alikuwa ni mmoja wa wafanyakazi kwenye kiwanda kimojawapo pale nchini ITALIA, wakati wa kipindi cha Corona kampuni aliyokuwa nafanyia kazi ilipunguza wafanyakazi. Akiwa haelewi ni kitu gani ambacho angeweza kufanya katika kipindi kama hiki, aliamua kuchukua simu yake na kuanza kurekodi video fupifupi alizokuwa akifanya kama uchambuzi fulani hivi wa tamthiliya.

    Alianza kidogo kidogo, na mara punde hizi video zake zilianza kushika kasi. Leo hii ni mmoja wa vijana wenye ushawishi mkubwa sana kwenye mtandao wa TIKTOK, lakini kitu kikubwa ambacho  alianza nacho ni simu yake aliyokuwa nayo.

    Khaby Lame

    Leo hii najua vijana ambao wana ndoto na vipaji vikubwa, ila wanasubiri kupata mfadhili kutoka maeneo ambayo wenyewe hawajui kama atatokea.

    Miaka kadhaa nyuma kabla hata sijajua kama kuna watu waliweza kurekodi movie kwa kutumia simu na kabla sijajua kuwa kuna akina Khaby Lame ambao wanarekodi video fupifupi kwa kutumia simu, nilikuwa nikiongea na mmoja wa ndugu zangu wa karibu ambaye moyoni mwake alikuwa akipenda kuigiza.

    Nilimweleza namna ambavyo angeweza kuanza kufanyia kazi kipaji chake cha kuigiza huku akijirekodi kwa kutumia simu yake. Nilipomwambia wazo huyu ndugu alilikataa kabisa, huku akisema kwamba haiwezekani kufanya kitu kama hico. Leo hii kile alichokuwa anasema kwamba hakiwezekani kuna watu wameweza kukifanya kwa manufaa na kujulikana duniani.

    Pengine yeye leo hii asingekuwa maarufu kama hawa, lakini angekuwa anafanya kitu anachopenda. Lakini mpaka ninavyoandika hapa, bado amesubiri muujiza fulani wa kumnyanyua na kumfanya aigize. Anasubiri awe na kamera za kisasa na timu ya kumrekodi.

    Hiki kitu kinanikumbusha usemi wa kuwa, pale unaposema kwamba haiwezekani, anatokea mtu mbele yako ambaye anakifanya. Wewe ukiendelea kusema kwamba haiwezekani, basi jua kwamba muda si mrefu kuna watu mbele yako ambao watatokea na kufanya kile kitu ambacho wewe mwenyewe ulikuwa unasema kwamba hakiwezekani.

    Baada ya kuwa umeanza kufanyia kazi kipaji chako, hakikisha kwamba hauishii tu kwenye kuanza kukifanyia kazi. lakini kuwa na mwendelezo wa kile unachofanya. Hiki ni kitu ambacho huwa kinawaangusha watu wengi. kuna watu kadha wa kadha ambao huwa wanaanza kufanyia kazi vitu ila huwa wanaishia njiani. Rafiki yangu, usifanyie kazi kipaji chako mara moja kisha ukatulia. Kuwa na mwendelezo kwenye kufanyia kazi kipaji chako. Usifanyie kazi kipaji chako mara moja, kifanyie kazi mara kwa mara.

    Hii ni njia bora ya kujitangaza bila kutumia gharama kubwa. kuna watu wanaweza kupuuza kazi zako kadhaa za kwanza, ila wakiona unaendelea kuweka juhudi kubwa kwenye kile unachofanya inafikia hatua wanaanza kufuatilia kazi zako, na hivyo unakuwa umewateka na kuwaleta kwako.

    Kuna watu watafuatilia kazi zako na kuwaambia watu wengine juu yako. Kwa jinsi hii,kazi zako zinakuwa zinakutangaza zaidi kwenye maeneo mbalimbali

    Wekeza kwenye kipaji chako. Pale unapokuwa unapata hela, usitumie zote kwa pamoja. Badala yake toa kiasi fulani ambacho utakirudisha kwenye kipaji chako. Utakirudisha kwenye kipaji kwa kununua vifaa vya kisasa zaidi ambavyo zitakusaidia kutoa kazi ambazo ni bora kadiri siku zinavyoenda. Utawekeza tena kwenye kipaji chako kwa kukitangza ili kiweze kwenda mbali kuliko ilivyokuwa mwanzoni. Na kujifunza vitu mbalimbali ili uzidi kubobea zaidi.

    Na kwenye ulimwengu wa leo kuna njia lukuki za kutangza kipaji chako.

    Unawezakutengaza kipaji chako kwenye mtandao wa intaneti . Google wana mfumo wao wa kutengeneza matangazo ambapo hayo matangazo unayaonesha mbele ya watu wanaoendana na tangazo lako. Lakini pia kuna mitandao kama youtube ambapo unaweza kutangaza kipaji chako huku.

    Mtandao kama instagram pia ni mtandao mzuri kwa ajili ya kutangaza kipaji chako, ambapo kwa gharama kidogo tu unaweza kuwafikia melfu kwa maelfu ya watu. Hiki kitu kilikuwa hakiwezekani miaka ya nyuma. Ebu chukukulia miaka ya nyuma kama ungependa kujitangaza kwenye gazeti. Gharama tu kuchukua nusu ukurasa kwenye gazeti, ni kubwa sana. na hii siyo kwa miaka ya nyuma tu, bali mpaka leo hii. Bado ukitaka kutangaza kipaji chako kwa njia magazeti au redio na runinga, gharama yao ya kutangaza kazi yako au kipaji chako ni kubwa ukilinganisha na mitandao kama facebook, twitter na instagram. Ambapo kwa gharama kidogo tu unaweza kufanya matangazo ambayo yatawafikia watu wengi

    Kwa leo naishia hapa.

    Kesho nitaendeea

    Mimi ni rafiki yako Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

    Kupata ebook ya MAAJABU YA KUWEKA AKIBA utalipia elfu tano tu. Namba ya simu ni 0755848391

  • Jinsi Ya Kushughulika Na Fedha Unazopata Kutokana Na Kipaji Chako

    Limekuwa ni kama jambo la kawaida kusikia watu waliokuwa na vipaji na watu ambao wakati fulani walikuwa wakiingiza fedha nzuri kupitia vipaji vyao wakiwa hawana fedha. Vyombo vya habari, vimekuwa vikiripoti kuwa hawa watu hawana fedha na muda mwingine kupitisha mchango ili hawa watu waweze kupata mahitaji yao ya muhimu au hata kupata sehemu ya kukaa. Wengine huwa wanafukuzwa nyumba walipopanga na hivyo kuwaletea fedheha na kujenga picha mbaya kwa watu wenye vipaji. Kitu hiki kinafanya vyombo vya habari ndio visaidie kupitisha mchango ili watu hao waweze kuchangiwa.

    Japo vyombo vya habari vimekuwa vikifanya hivi kwa mazoea, na vimekuwa vikifanya vizuri, ila hili siyo jambo ambalo tunapaswa kulifumbia macho na kuacha kulifundisha ili yeyote atayesikia la mkuu, asije akavunjika guu, halafu eti mkuu mwenyewe ni mimi, hahaha. Kama mtu ana kipaji chake na kipaji chake kinamwingizia fedha nzuri sasa hivi, basi hata miaka mingine mbeleni baada ya kustaafu, hapaswi kuendelea kulalamika wala kupungukiwa na kitu, ndio maana hii sura nimeiandaa maalumu kwa ajili ya hili jambo.

    Kuna tatizo kubwa

    Kuna sehemu kuna tatizo kubwa na hili tatizo tunapaswa kuhakikisha tunalifanyia kazi ili kuliondoa. Maana, ukiachana na watu wenye vipaji na ujuzi wao, hata wafanyakazi na watu ambao wamekuwa wanaingiza kipato kizuri kwa miaka yao yote ambayo wamekuwa wakifanya kazi, mara tu baada ya kustaafu unakuta kwamba wanakuwa na ukata mkubwa sana wa fedha. Sasa kumbe hili jambo tunapaswa kulipigia kelele, ili watu waweze kujua namna sahihi ya kuishi na hela zao, kuzitumia kwa manufaa, kuziwekeza ili hata baadaye watakapostaafu, waweze kustaafu kwa raha mustarehe, wakiwa na uhakika wa mzigo mkubwa wa hela nyuma yao.

    Watoto wanaorithi mali

    Wengi wamekuwa wakifananisha watu wenye vipaji (wakimbiaji wa mbio za marathoni, wanamziki, wanamichezo na wengineo) na watoto ambao wanarithi mali…

    Yaani, kwamba wote hawa wana vitu viwili ambavyo vinafanana, kwanza ni kupata mali nyingi kwa wakati mmoja na pili ni kuzitapanya au kuzitumia hizo mali zote na baadaye kubaki bila ya fedha

    Tafiti nyingi zimerudiwa mara kwa mara na kuonesha kuwa watoto ambao huwa wanarithi mali, asilimia kubwa sana ya watoto hawa wanaishia kupoteza hizo mali ndani ya muda kidogo na baadaye kuishia kwenye umasikini mkubwa sana. Kitu hiki pia kimekuwa kikitokea kwa watu wenye vipaji vyao. Mtu anakuwa ana kipaji anafanya vizuri, anapata fedha, na halafu hizo fedha anazitapanya na mwisho wa siku anabaki bila ya fedha yoyote ile. Hiki kitu baadaye kinamfanya aishiwe na hata kufikia hatua ya kuombaomba kwa watu na kwenye vyombo vya habari. Swali linabaki je, mzunguko kwa watu wote vipaji unapaswa kuwa hivi?

    Yaani, ina maana kwamba kila mtu mwenye kipaji anapaswa kufikia hatua ambapo ataishiwa fedha na kuanza kuomba msaada li kujikimu na maisha yake?

    Usiilalamikie serikali

    Kuna wamekuwa wakiilalamikia serikali kuwa haiwajali baada ya kuwa wamestaafu kufanya kazi. sasa kabla hatujafika huko kote, ebu ngoja tuweke msingi wakati ukiwa unapokea fedha. Ili uweze kuitumia vizuri hii miaka yako ambayo uko kazini kwa ajili ya kuhakikisha kuwa hii miaka inakuwa yenye manufaa makubwa kwako, kiasi kwamba utakapostaafu au likitokea jambo lolote la kukufanya usiendelee na kazi basi uwe na chanzo cha uhakika cha kukuingizia fedha.

    Na kitu kingine na muhimu cha kufahamu ni kuwa maisha ni wajibu wako, hivyo kama maisha ni wajibu wako, unapaswakuubeba huu wajibu wa maisha yako kwa asilimia 100.

    Usisishindane kufanya starehe unapopata fedha

    Wengi wanapokuwa na nguvu na wanapopata fedha basi kitu cha kwanza wanachofanya ni kuonesha kwamba wanazo hizo fedha. Utasikia watu wanasema kwamba tumia fedha zikuzoee. Au ponda mali kufa kwaja. Utasikia mwingine anasema kwamba hapa duniani tunaishi mara moja. ni kweli tunaishi mara moja hapa duniani, na unapaswa kufurahia maisha yako na uwepo wako hapa duniani, ila sasa usitumie fedha kiasi cha kupitiliza wakati hujajenga misingi ya kukuingizia fedha hata kama umelala.

    Kama umewahi kufuatilia watu wenye fedha siyo watu ambao huwa wanatumia fedha zao hovyohovyo, badala yake ni watu ambao huwa wanaitumia fedha zao kwa manufaa kabisa.

    Wanawekeza na wanajenga vyanzo vya kipato katika kuhakikisha kwamba wanakuwa na fedha zaidi. Na wewe fuata nyayo zao. Na hapa chini ninaenda kukuonesha ni kwa namna gani unaweza kufuata nyayo za hawa watu ili uweze kufanya makubwa.

    Anza kufuata misingi ya fedha

    Kila kitu kwenye maisha kina sheria na misingi yake. Daktari anayefanya matibabu kuna misingi na sheria ambazo anapaswa kuzifuata kwenye matibabu, hivyo hivyo kwa mwanasheria, kuna misingi na kanuni ambayo anaifuata kwenye kazi yake.

    Kitu hiki mara nyingine huwa kinaitwa miiko ya kazi. hizi ndizo kwa kiingereza zinaitwa dos and donts. Yaani, vitu vya kufanya na vitu ambavyo siyo vya kufanya.

    Sasa kuna misingi ya kukuza kipaji chako ambayo, kiuhalisia nimeielezea kwenye kitabu cha KIPAJI NI DHAHBU, nashauri sana uweze kupata kitabu hiki cha kipekee ila kwa leo tutaongelea upande wa fedha, upande ambao umekuwa ukiwasumbua watu wengi. ili pale utakapokuwa umeanza kupata fedha kutokana na kipaji chako basi, usije ukayumba wala kutetereka sehemu.

    KIPAJI NI DHAHABU
    Ili kupata kitabu hiki, wasialiana nami kwa 0755848391 sasa

    Kwanza kifanye kipaji chako kama biashara

    Unajua kwa nini nasisitiza hili la kukifanya kipaji chako kuwa kama biashara

    Kwanza ni kwa sababu watu wengi wamekuwa wakifanyia kazi vipaji vyao kama hobby. Hobby ni kitu unafanya tu ilimradi umefanya kwa ajili ya kujifurahisha.

    Siku moja nilikuwa naongea na rafiki yangu mmoja kuhusiana na huduma nyingi ambazo tulikuwa tunapata kwa rafiki zetu wakati tuko chuoni, mtaani huduma hizohizo zinalipiwa gharama kubwa ila pale chuoni tulikuwa tunazipata bure kabisa. Kumbe hata hawa ndugu zetu wangeweza kuweka vipaji vyao katika mfumo wa kibiashara na hivyo kuweza kupokea fedha na hata kujenga biashara zaidi ambayo ingewafikia wengi.

    Kwa kusema hili sIyo kwamba nakataza watu kutoa msaada au kusaidia. Ila msaada usipitilize kiasi cha mtu kujisahau.

    Mfano wa huduma mojawapo ambayo tulikuwa tunapatabure pale chuoni ni huduma ya kutengenezewa simu na marafiki wa karibu pale inapoharibika. Unakuta mtu ana ujuzi wa kutosha kwenye hili kiasi kwamba simu yako ikiharibika anaitengeneza na kuirudisha kwenye uimara wake, anaitengeneza vizuri bure. Kitu ambacho ni kizuri. lakini walau angeweza kuchaji kiasi kidogo kwa ajili ya kuifanya hiyo huduma yake iweze kusongambele zaidi. Huduma hizihizi huku mtaani, tunazilipia, kwa mwanachuo pia unaweza kuweka kiasi kidogo tu cha watu kukulipa na hivyo kupata fedha za hapa na pale za kuendesha maisha chuoni na kujenga ukiwa chuoni au baada ya chuo.

    Kitu kingine cha kuongezea hapa ni kuwa, mtu akikosa huduma ya kwako ya bure ataenda mtaani kwa mtu ambaye anatoza hela na ataitoa hela. Mfano simu yake ikiharibika na wewe kipindi hicho ukawa umesafiri, au unaumwa na huwezi kuitengeneza, kwa sababu anaihitaji kwa haraka ataenda kwa mwingine na atamlipa hela ili simu yake itengenezwe kwa haraka, sasa kwa nini na wewe usiwachaji watu kiasi kidogo ili wakulipe kwa hiyo huduma unayotoa. Fikiri kibiashara.

    Lakini pia nasisitiza kwamba ufikiri kibiashara zaidi kwa sababu, ukishaweka mfumo kwenye biashara yako, ni wazi kuwa kipaji chako kitendelezwa baada hata ya wewe kuwa umezeeka au hata baada ya kufa. Kuna watu wengi wana vipaji vizuri vya kupika, ila wachache wameweza kufanya vipaji vyao kuwa biashara. Ebu chukulia mfano rahisi tu wa kupika maandazi. Kuna watu wengi wanapika mandazi, ila ni wangapi wameweza kusambaza mandazi yao kama Bakhresa? Sidhani hata kama Bakhresa ana kipaji cha kupika mandazi, hahaha. Ila tofauti kubwa kati ya Bakhresa na watu wengine wanaopika maandazi ni kuwa Bahkhersa yeye anafikiri kibiashara zaidi.

    Hivyo, yeye ameweka mfumo wa kibiashara kwenye mandazi yake. Mfumo huu upo kuanzia kwenye kupika mandazi, kuyapaki, kuyasambaza mpaka kuyauza sokoni. Hiki kitu kinafanya maandazi yake yaweze kuuzika siyo kwenye eneo alipo yeye, bali yanauzika karibia nchi nzima. Wakati hapo mtaani kwenu kuna mama ambaye anapika maandazi na hayo maandazi hata hayajasambaa mtaa mzima mnapoishi.

    Sijui  unanielewa hapo. kumbe na wewe anza kufikiri kibiashara, anza kufikiri Bakhresa, Bakhresa ili na wewe kipaji chako uweze kukiwekea mifumo ya kibishara na kukifanya kweze kwenda mbali zaidi hata kama hautakuwepo.

    Mfumo wa biashara utafanya kipaji chako kiweze kusogea. Unaanzaje sasa kuweka mfumo wa biashara kwenye kipaji chako,

    Hivi hapa ndivyo unaweza kuanza

    Kwanza anza wewe kufanyia kazi kipaji chako. Hiki sihitaji kukieleza zaidi, maana tayari nimeshakieleza kwa kin kwenye kitabu cha KIPAJI NI DHAHABU. Nakala ya kitabu hiki ni elfu tano tu. kupata nakala hii, tuma fedha kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Pili, angalia majukumu yote ambayo unafanya kwenye biasahra yako. Kisha yagawe hayo majukumu, angalia yale majukumu ambayo ni ya  muhimu sana na yanahitaji uwepo wako, wewe yafanye hayo. Majukumu mengine wape watu wakusaidie kuyafanya.

    Tafuta watu kukusaidia kwenye hayo majukum ili nao waweze kufanya hayo majukumu huku wewe ukiweka nguvu kubwa zaidi kwenye yale majukuu ya muhimu sana kwako.

    Nne, weka mfumo wa namna vitu vinavyofanyika. Kwa  mfano kwamba wakati wa kutengenza mandazi,  haya ndiyo mambo ambayo kila mtu anapaswa kuzigantia. Hii itakusaidia kiasi kwamba hata kama hautakuwepo, majukumu yako yataweza kuendelea mbele zaidi bila ya kurudi nyuma. Lakini pia hii itasaidia kwamba hata kama yule uliyemwajiri akitoka, bado utakuwa na uhakika kuwa shughuli zako zinaendelea bila ya kurudi nyuma tena kwa ubora ule ule.

    Umeshawahi kuona watu wanakataa kununua chakula kwa sababu mhudumu fulani hayupo siku hiyo. Changamoto inakuwa pale ambapo mhusika mmojawapo kwenye biashara anaondoka, ubora unapungua, au kama ni huduma kwa wateja ndio siku hiyo inakuwa sifuri.

    Sasa mfumo ni mwongozo. Unapaswa kufuatwa bila kujali wewe upo au haupo. Unapaswa kufuatwa bila kujali mtu fulani uliyemwajiri yupo au hayupo. Rafiki yangu lifanyie kazi hili kwenye kipaji chako pia.

    Nne, simamia mfumo. Hapa hakikisha kwamba kila kitu kwenye mfumo kinaenda sawa kama inavyostahili.

    Tano weka mtu wa kusimamia mfumo, hapa unaweka mtu wa kusimamia mfumo, huyu anasimamia kiasi kwamba hata kama haupo kila kitu kinaendelea. Ukiwa na mfumo mzuri hata ukifa, kila kitu kinaendelea. Ndio maana leo hii unaona kampuni kama cocacola zinazidi kusongambele. Unajua Cocacola ilianzishwa mwaka gani? Utakuwa sahihi, ni mwaka 1892. Ni zaidi y a miaka 100. Mwanzilishi wake alishakufa miaka mingi sana iliyopita, ila kitu kimoja kilicho nyuma yah ii kampuni na kinachoifanya iendelee kusonga mbele ni mfumo unaosimamia uzalishaji wa bidhaa zake. Hakuna hata siku moja  utakunywa cocacola ukuta kuwa ile ladha imebadilishwa, ladha ni ileile kila siku. Ladha ni ileile ukiwa Tanzania, Uganda, Afrika kusini au kazikazini! Kwa nini? kwa sababu ya mfumo ulio nyuma ya utengenezaji wa soda hii. kuna vitu ambavyo unapaswa kuzingatia. Na ukizingatia hivyo tu, basi umemaliza. Na wewe unapaswa kufanya hivyo, tengeneza mfumo kwa ila kitu.

    Tengeneza mfumo kwenye uzalishaji, watu wajue mchakato wote wanaofuata kwenye kutengeneza bidhaa au kutoa kitu. Mama anayepika maandazi mtaani kwako, anapika mandazi matamu sana, ila siku asipokuwepo kutengeneza mandazi yale, akaja mwanae ujue siku hiyo yanatengenezwa maandazi ya hovyo. Kwa nini? kwa sababu mama anajua mchakato wote wa kutengeneza mandazi, ia sasa ule mfumo haufahamiki kwa mtoto. Hakuna sehemu umeandikwa. Kwa hiyo uandike huo mfumo wako, ili kila anayefanya kazi kwenye kitengo husika akae akiujua huo mchakato wa kufuata.

    Sita wakabe hao watu uliowaweka kusimamia mfumo

    Saba ongeza juhudi zaidi kwenye kusimamia mfumo na kwend ambali zaidi.

    Sambamba na kuweka mfumo sahihi wa kibishara kwenye kipaji chako unachofanya unahitaji pia kuweka mfumo sahihi wa kifedha kwenye kipaji chako. Na kwa kuanzia, anza na vitu rahisi tu. anza na kuhakikisha unajua mapato na matumizi. Yaani, fedha yote inayoingia ijulikane na fedha yote inayotoka ijulikane. Hiki kitu ni kidogo sana ile chenye nguvu kubwa sana.

    Halafu hao watu hao ambao unawaita ili kukusaidia kazi za hapa na pale hakikisha kwamba unawaliipa. Niwazi kuwa na wao wana ndoto na malengo ambayo wanegependa kutimiza, hivyo kwa  kile kiasi utakachowalipa, watakuwa na uwezo wa kuanza kufanyia kazi malengo na ndoto zao huku wakiendelea kukusaidia wewe. hivyo, walipe. Kazi yako kubwa itakuwa ni kuhakikisha kuwa unaajiri pale ambapo mtu atakuwa anahitajika kwenye biashara ili aweze kusaidia majukumu fulani, kitu ambacho kitakusaidia wewe na timu yako kuweka nguvu kwenye kukuza mauzo zaidi na hivyo kuweza kuwalipa.

    Kwa hiyo utatoa kiasi utawalipa. Na wewe mwenyewe utajilipa mshahara wa kawaida.

    Kisha faida itakayobaki iwekeze.

    Na kwa kuwa nataka nikupe mwongozo kamili, sikiliza nenda kawekeze fedha yako kwenye mifuko ya uwekezaji ya pamoja, iliyo chini ya UTT.

    Najua watu wengi watakushawishi kuhusu kuwekeza kwenye maeneo mengi mengi kama kilimo, bitcoin, na mengine mengi. Lakini kwa kuwa wewe nguvu yako kubwa unaiweka kwenye kipaji chako, huhitaji kuwekeza nguvu kubwa kwenye maeneo mengine, nguvu yako yote iwekeze kwenye kipaji chako na hata unapoongea na timu yako, wasukume wafanye vizuri zaidi ili kipaji chako kama bishara kiweze kufika mbali, ila kwa vyovyote vile hakikisha kuwa hautawanyi nguvu zako kwa kuziweka kwenyea maneo mengine ambayo huyafahamu, badala yake wekeza nguvu zako zote kwenye kipaji  mpaka kifikie ngazi kubwa za kimataifa.

    Kwa hiyo, uwekezaji wako wote ufanyie kupitia mifuko ya uwekezaji wa pamoja ya UTTt

    Najua utakuwa unajiuliza UTT ni kitu gani na hii mifuko ya pamoja inafanyaje kazi, hiki kitu sitaweza kukieleza kwa kina kwenye makala hii. Ila nimeandika kitabu kinaitwa maajabu ya kuwekeza kwenye hisa, hatifungani na vipande. Nashauri sana uweze kupata kitabu hiki cha kipekee, kwa kuwasiliana nami kwa 0755848391

    Ngoja nikwambie kitu, unapowekeza kwenye hii mifuko unakuwa unaifanya fedha ikufanyie kazi hata kama wewe haupo, kitu ambacho kinakutengenezea maisha mazuri ya hapo baadaye. Lakini pia ni sehemu ya wewe kuweka akiba na kuteng eneza kesho yako bora.

    Umeshapata kitabu hiki Cha Maajabu ya Kusoma Vitabu? Gharama yake Ni 5,000

    Asante sana,

    Nakutakia kila la kheri

    Godius Rweyongeza (SONGAMBELE)

    0755848391

    Morogoro-Tz

    SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA CHINI

  • Jinsi Kizazi Kinachostaafu Kinavyoweza Kuandaa Kizazi Kijacho

    Mara kwa mara nimekuwa nakutana na watu wazima wenye umri wa miaka 50 na zaidi au niseme watu walio kwenye umri wa miaka ya kustaafu, kila ambapo nimekuwa nikiongea na watu hawa kuhusiana na vipaji basi wenyewe moja kwa moja wamekuwa wakiniambia kuwa umri wao umeshaenda, hivyo kwao huu sio muda tena wa wao kunoa au kuendeleza vipaji.

    Kitu kimoja ambacho nimekuwa nikiongea nao ni kuwa wao wanaweza kuwa sehemu ya kuwasaidia kizazi kijacho (, watoto wao, wajukuu wao na vijana wengine) kugundua vipaji vyao, kuvinoa na kuviendeleza. Hiki ni kitu ambacho naamini kinawezekana kabisa kufanyika na mzee yeyote yule anaweza kusaidia kutengeneza taifa bora kwa siku za mbeleni.

    Jack Ma aliwahi kusema kwamba unapofikisha umri wa miaka 60 na zaidi ni muda wa wewe kuhakikisha unaandaa kizazi kjacho. Nadhani, wazee wote ambao wanasema kwamba kwa sasa hawawezi kugundua wala kuendeleza vipaji vyao, basi walau hata hawawezi kushindwa kushiriki kwenye kuandaa kiazazi kijacho.

    Tukiwa na kizazi kizuri kinachojitambua, kizazi ambacho kila kijana anajua uwezo wake na kwa nini yuko hapa duniani. Kizazi ambacho kila kijana anatumia uwezo alio nao ndani yake, ni wazi kuwa tutatengeneza taifa zuri na bora sana kuwahi kutengeneza hapa duniani.

    Na hiki ni kitu ambacho tunapaswa kupigania.

    Kama wewe una watoto au wajukuu ambao unakaa nao, kwa nini usitoe sehemu ya muda wako katika kufuatilia na kuangalia uwezo wao walio nao na huku ukiwasaidia kuutumia huo uwezo kwa manufaa ya sasa hivi na siku zijazo.

    Wewe una uwezo mkubwa sana

    Kuna kitabu nilikuwa nasoma, ila sikumbuki mwandishi ni nani. Kwenye hiki kitabu mwandishi akawa anaeleza kuwa alikuwa anakaa bibi yake,  pale kwa bibi yake walikuwa wanakaa watoto kama kumi hivi na zaidi. Sasa siku moja bibi yake alimwita pembeni huyu mjukuu wake kwa ajili ya maongezi binafsi ambapo watoto wengine hawakuwepo. Kijana alimsikiliza bibi yake kwa umakini mkubwa sana, bibi yake alimwambia kwamba, nimeangalia kati ya vijana wote wanaokaa hapa, nimeona kwamba wewe una uwezo mkubwa sana na ninakuhakikishia kwamba siku moja wewe unaenda kufanikiwa sana.

    Bibi yake akamsisitiza kuwa aende autumie huo uwezo wake vizuri kuhakikisha anafanya makubwa kwenye maisha, na mwisho kabisa akamwabia asimwambie mtu hayo aliyomwambia.

    Mwandishi alisema hiki kitu 5 kilimpa nguvu kubwa sana kwenye maisha.

    Baadaye alikuja kugundua kuwa bibi yake alikuwa na utaratibu wa kumwita kila kijana wake mmoja mmoja na kumwambia maneno hayohayo, kumbe siyo yeye tu alikuwa ameambiwa hayo maneno. bali watoto wengine walikuwa wameambiwa hayo maneno, lakini bado kujua hilo halikumkatisha tamaa. Alichukua kile alichoambiwa na bibi yake moyoni na kuamua kukifanyia kazi ili kuhakikisha anafanya makubwa kwenye maisha.

    Wewe pia kama mzazi unaweza kuwatia moyo watoto na wajukuu kwa kuwaambia maneno mazuri ambayo yatawasukuma kufanya kitu cha tofauti kwenye maisha yao. Na muda mzuri ni sasa.

    Muda mzuri wa kupanda miti

    Kuna msemo mmoja wa kiafrika unaosema kwamba muda mzuri wa kupanda mti ulikuw ani miaka ishirini iliyopita, ila muda mzuri zaidi ni sasa. Unajiuliza hivi kupanda miti na kunoa vipaji sasa vinaendanaje? Ninachotaka nikwambie hapa ni kuwa kama wewe hukuweza kugundua kipaji chako ukiwa kijana, basi wewe unaweza kusaidia vijana na watoto kugundua vipaji vyao pia.

    Na wakishagundua vipaji vyao, wafuatilie kwenye kuvifanyia kazi mazoezi na kuhakikisha vipaji hivyo vinakuwa vyenye manufaa kwao pia.

    Nimewahi kusikia stori, kuwa baba yake Mbwana Samatta alikuwa anamfuatilia nyuma kuhakikisha anafanya vizuri kwenye mchezo, na hata alikuwa na mfumo wa kutoa zawadi au adhabu kama Samatta angefunga.

    Yaani kwamba walikuwa wameweka mkataba kwamba kama Samatta atafunga goli, basi baba yake atamzawadia shilingi elfu mbili, na kama atafungwa basi yeye anapaswa kulipa faini ya elfu mbili.

    Japo sina uhakika na hili kwa asilimia mia moja. lakini hiki kitu kinaweza kuwa kitu chenye manufaa kwa wazazi, kukitumia kwa watoto. Unaweza kutumia mfumo wa zawadi na adhabu kumsaidia mwanao, mjukuu au mtoto yeyote kwenye kunoa na kuendeleza kipaji chake.

    Mfano unaweza kununua zawadi na kuja nazo  pale nyumbani, hizo zawadi ukaziwekea sharti ya kuzipata.

    Mfano unaweza kumwambia kuwa utapata zawadi hii endapo utafanya hiki na kile, utapata zawadi hii endapo utakamilisha hesabu zako za darasani.

    Utapata zawadi hii endapo utafanya homework na kuimaliza. Hiki kitu kikampa motisha mtoto kufanyia kazi kipaji chake cha hesabu au kusoma, na hivyo kumsaidia kuboresha zaidi kile kilicho ndani yake,

    Lakini pia ni motisha kwa mtoto maana anakuwa anajua kwamba endapo hatafanya mazoezi au hatakamilisha jambo fulani basi hatapata zawadi yake uliyomwandalia ambayo kwake ni adhabu.

    Hiki kitu kina nguvu kubwa sana, maana mtoto anapokuwa anajua kuwa nyuma yake mara zote kuna wazazi ambao wanafuatilia kile anachofanya, basi ni hakika kuwa huyu mtoto atajitahidi kuhakikisha kwamba anafanya vizuri. Pale mzazi anapokuwa ni shabiki namba moja wa mwanae, ni wazi kuwa mtoto anakuwa hataki kumwangusha mtoto wake kwenye kile anachofanya

    Tujenge utaratibu wa kufuatilia. Kazi za wanetu

    Kama mzazi na mtu ambaye anaanda kizazi kijacho cha vijana, basi ni muhimu sana ukajenga utaratibu wa kufuatilia vitu ambavyo mwanao anakuwa anafanya. hata michezo ya kawaida, vinampa nguvu kubwa sana, lakini wakati huo vinamwepusha kufanya mambo ambayo siyo maana anakuwa anajua kuna mtu nyuma yangu ambaye anafuatilia kila ninachofanya.

    Kwenye kitabu chake cha Think Big, mwandishi Ben Carson anaeleza namna ambavyo mama yake alikuwa akifuatilia kazi zake anazofanya na hat kumpa kazi ya kusoma vitabu viwili kila wiki. Hiki kitu tu, kilimfanya kijana huyu ajenge utaratibu wa kusoma vitabu, kitu ambacho baadaye maishani mwake kilikuja kuwa chenye manufaa makubwa sana kwake. Katika harakati za kuandaa kizazi kijacho, tunaweza kujifunza hapa pia.

    Siku moja kwenye kundi mojawapo la whatsap kulikuwa na mjadala wa namna ya kuandaa kizazi kijacho, ila walikuwa wakizungumzia zaidi kwa upande wa fedha na uwekezaji. Kutoka kwenye huu mjadala nimeona nikushirikishe kipande kimoja muhimu sana ambacho na unaweza kunufaika nacho.

    …..kufundisha watoto ni raha sana

    …take it easy as a game play

    Mfano:

    Unawapa Task eg.MAKING MONEY

    1) Mwambie somo lolote akipata above 90%… ana jishindia Tzs10,000.Hivyo more 90% means more money..getting rich

    2) Na hizi pesa ….yeye ndio ana keep recprds kwenye note book yake.Humpi cash.Akitaka kuspend kwenye toys anapunguza kwenye balance yake.

    3) Mshindanishe na nduguze.They will all improve the grades….enjoy the proces,stay motivated….while learning about Money, practically….with adrenalin pump

    5)Pia mpe vitabu kuhusu Money ,Investments na Self Development…….. kila kitabu akimaliza aandae presentation…..anakuhadithia, [akifanya vizuri] mzawadie Tzs15,000 [kwa] kila presentation…..utashangaa walivyo smart na idadi ya vitabu atakavyosoma

    6) Akifika 18yrs, akapata NIDA, immediately …mpe balance yake…anaanza trading and investment….on his own…..tena kwa pesa yake aliyoitengeneza mwenywewe.

    *Money Runs The world…..kids enjoy earning it too*

    …i have tested it…several times…. it works very well….. kids are lovely learning partners.Utajikuta na wewe unajifunza mengi ili kumlainishia…akuelewe..same time mna tengeneza bonge la parent-child relationship

    …also gets you to learn human behaviour arround money & investments via little beings

    …ukija baadae kumfundisha technical and fundamental approaches…..hashangai chochote….kuhusu patterns,candlestics,risk management,money psychology,sentiments etc….kwani ulianzia kwenye DNA of money….yaani X & Y chromosomes of money , to be specific

    Maisha yanapokupa limau unatengeneza juisi

    Mzee mmoja baada ya kuona kwamba umri wake umeenda na hawezi tena kuingia uwanjani na kuanza kujifunza mpira, aliona atatumia kipaji chake kufundisha watoto na vijana  mpira wa miguu, hivyo alijifunza ukocha wa mpira wa miguu na kuanza kutoa mafunzo kwa kizazi kijacho. Baada ya hapo alienda mbali zaidi na kuwa na shule maalumu ya kuwafundisha vijana na kuandaa kizazi kijacho. Kwa jinsi hiyo hakuruhusu kipaji na uwezo wake ufe bila ya yeye kuutumia kama ambavyo alikuwa anatakiwa kuutumia.

    Wewe pia pengine umri wako umeenda na unaona kwamba huwezi kurudi nyuma na kuanza kunoa kipaji chako upya, ila kitu kimoja cha uhakika ni kuwa kuna namna unavyoweza kusaidia kizazi kingine huku wewe ukinufaika pia.

    Pengine unaweza hata kuandka kitabu na kutoa mafunzo kwa vijana na kuwaasa wasifanye makosa kama ya kwako uliyofanya kwenye kunoa na kuendeleza kipaji chako.

  • Ukipenda pesa, lazima upende na kazi

    Rafiki yangu mpendwa, vitu vingi vilivyo hapa duniani huwa vinaenda viwili viwili.
    Mfano ukiongelea juu, lazima kuwepo chini.
    Ukisema mbele lazima kuna nyuma
    Ukizungumzia kulia sharti kuwepo kushoto pia

    Sasa hiki kitu kina funzo kubwa sana kwetu na hasa kwenye kutafuta fedha na mafanikio.
    Na ujumbe ni kuwa ukipenda fedha lazima upende kazi.

    Ni wazi kuwa huwezi kupata fedha bila ya KUWEKA kazi kwanza. Lakini pia ili upate fedha zaidi Unapaswa kuijua misingi ya fedha kwenye uwekezaji, na kuifanya fedha ukifanyie kazi zaidi. Komaa humohumo.

    Fanya kazi kwa bidii
    Pata pesa.
    Weka akiba
    Wekeza
    Rudia tena hayo.

    Kila la kheri
    Godius Rweyongeza

  • KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kukigundua, Kukinoa Na Kukitumia Kipaji Chako Kwa Manufaa

    Kwenye kurasa za kitabu hiki nimeeleza kipaji kwa kina kiasi kwamba kama kitabu hiki anakisoma mtoto wa miaka sita aweze kunielewa.

    Kwenye sura ya kwanza nimeanza kwa kueleza kwamba kipaji ni kitu gani? Ambapo nimeeleza dhana nzima ya kipaji na jinsi kinavyofanya kazi.

    Kwenye sura ya pili nimeeleza namna ambavyo unaweza kugundua kipaji chako. Je, unajiuliza ni kwa namna gani ambavyo unaweza kugundua hicho kipaji chako? Basi nenda moja kwa moja kwenye sura ya pili.

    Kwenye sura ya tatu nimeonesha mbinu unazoweza kutumia kwenye kunoa na kuendeleza kipaji chako. Hapa utakutana na mbinu za kukusaidia wewe kuweza kupeleka kipaji chako mbali. Na kwenye sura ya nne tutaona kwa nini watu hawathamini vipaji vyao.

    Kwenye sura ya tano tutaona mbinu zitakusaidia wewe kutengeneza fedha kwa kutumia kipaji chako.

    Tunaishi kwenye ulimwengu wa intaneti. Na hapa tutaingia kwenye sura ya sita ambapo tutaona namna ambavyo unaweza kupeleka kipaji chako kwenye mtandao na kunufaika na intaneti.

    Kwenye sura ya saba  tutaona kipaji na elimu. Kwa nini elimu inapewa kipaumbele zaidi kuliko kipaji na je, kuna ulazima wowote wa kuendeleza kipaji chako au ukomae tu na elimu?

    Uko tayari kwa ajili ya safari hii ya kipekee? Basi wacha tuianze kama ifuatavyo.

X