Home


  • Vitabu Viwili Unavyopaswa Kuhakikisha umesoma mwezi huu wa tisa

    Habari ya leo rafiki yangu, siku ya leo ningependa kwa ufupi nikwambie vitabu vitano ambavyo unapaswa kusoma ndani ya mwezi huu wa tisa.

    Bila kupoteza muda, vitabu vyenyewe ni

    1. The school of money

    Hiki ni moja ya kitabu muimu sana ambacho unapaswa kusoma hasa kuhusiana na suala zima la fedha. Kitabu hiki ndani yake kimeeleza mbinu na kanuni za kukusaidia wewe kuweza kupiga hatua na kusongambele kwenye suala zima la fedha. Kama kuna kitabu kimoja cha fedha utapaswa kusoma ndani ya mwezi huu wa tisa, basi soma kitabu hiki cha The school of money. Kama utahitaji kupata softcopy ya hiki kitabu, basi unaweza kunitumia ujumbe kwa namba ya 0755848391 ili nikueleze namna ya kuipata.

    2 NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

    Najua kuwa una malengo na ndoto kubwa za kufanyia kazi na hata kufikia mwaka huu, ila unajua nini. Malengo yako haya, unahitaji kuyafanyia kazi hata kwa udogo. Hii ndio dhana nzima ya kitabu cha nguvu ya vitu vidogo kuelekea mafanikio makubwa. kwenye hiki kitabu unaenda kujifunza mbinu na kanuni za kukusaidia wewe kuweza kufanyia kazi na kufikia lengo au ndoto yoyote ile kwa kuanza kidogo. Hatua ndogondogo mwisho wa siku zinaleta matokeo makubwa.

    Kitabu hiki kinapatikana kwa mfumo wahardcopy na audiobook

    Gharama ya hardcopy (nakala ngumu) ni 20,000/- unatumiwa kitabu hiki popote pale ulipo duniani.

    Gharama ya audiobook ni 10,000/- tu. na hii utaipata bila kujali upo wapi hapa duniani, ndani ya dakika chache tu baada ya kulipia.

    kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO

    Hivi ni vitabu viwili ambavyo unapaswa kusoma ndani ya mwezi hu wa nane rafiki yangu.

    Ubora ni kuwa kitabu kimojawapo kimesomwa kwa sauti na unaweza kukisikiliza kwa sauti, hivyo unakuwa huna shida ya kukaa chini na kuanza kukisoma moja kwa moja. Hiki kitu kinakufanya uweze kwa hakika kusoma vitabu viwili kwa mwezi huu na kuvimaliza. Kama utapata vitabu hivi viwili, kimoja unaweza kukisiliza kwa njia ya sauti, huku kingine ukiwa unakisoma kwa njia ya kawaida. Hiki kitu kitakusaidia sana kuweza kupata maarifa sehemu mbili na kunufaika kwa ukubwa sana.

    Rafiki yangu, soma vitabu hivi viwili, nina hakika utanishukuru sana kwa miezi ijayo na miaka inayofuata.

    Sina cha kukusaidia zaidi ya kusema wasiliana na mimi sasa ili uweze kupata hivi vitabu vyote viwili kwa wakati mmoja.

    Mimi hapa sina la ziada

    Akhsante

  • JINSI UBUNIFU UNAVYOWEZA KUKUINUA KWENYE BIASHARA

    Siku moja nilikuwa naongea na rafiki yangu Edius Katamugora, akawa ameaniambia juu ya kinyozi aliyekuwa anatengeneza app ya kuwakumbusha wateja kurudi kunyolewa. Yaani, app yenyewe ingekuwa inafanya kazi hivi,

    Pale Ambapo ungekuwa unaenda kunyoa kwa yule fundi kinyozi, angekuwa anachukua namba yako, saa chache baada ya kuwa umenyoa app ingekutumia ujumbe kukushukuru kwa kuja konyoa. Wakati app hiyohiyo ikikutumia ujumbe wiki mbili mbeleni ikikumbusha kunyoa kwa mara nyingine. Maana kwa kawaida Ndani ya wiki mbili nywele zinakuwa zimeshaota, kiasi cha kuhitaji kunyoa tena. Huu ni ubunifu.

    Siku nyingine nilikutana na jamaa ambaye alikuwa anatunza namba Simu za wateja wanaofanya miamala kwake, siku nyingine ulipokuwa unaenda kufanya muamala kwake badala ya kuanza kukuuliza namba yako ni ipi, alikuwa anakuuliza unatuma kwenye namba ileile au tofauti. Ukisema ileile basi hapohapo alikuwa anaendelea na muamala bila kukuuliza namba yako.Huu pia ni ubunifu mwingine.

    Ubunifu kwenye biasharani moja ya kitu muhimu Sana ambacho Unahitaji kulifanyia kazi. Ubunifu unawapa sababu ya wateja kuja kwenye BIASHARA yako badala ya biashara za watu wengine.

    • Unaweza Kuwa ubunifu wa KUWEKA benchi za watu kukaa.
    • Unaweza pia kuwa ubunifu wa kukumbuka kitu alichonunua mteja mara mwisho au mbacho anapendelea kununua mara kwa mara.
    • Unaweza Kuwa ubunifu wa kuwapa watoto pipi moja ya shilingi 50 kila wanapokuja kununua dukani kwako. Si unajua watoto huwa wanatumwa sana na wazazi, ukibuni kitu Cha kuwapa motisha, unashangaa kila wanapotumwa wanakuja dukani kwako kununua.
    • Unaweza kuwa mbunifu kwa kuwapa wataje wako ofa, hata ya  kitu kidogo pale wanaponunua kwako mara kwa mara.
    • Kwa vyovyote vile ubunifu Ni moja ya kitu muhimu sana unachohitaji.

    Ubunifu unakutofautisha wewe na watu wengine ambao wanakuwa wanafanya kitu Cha kwako. Ubunifu unawapa watu sababu ya kuja kununua kwenye biashara yako badala ya kwenda kununua kwingine [MSISITIZO].

    Na ubunifu siyo tu kwenye biashara,ubunifu unaweza kuutumia kwenye Kipaji chako, elimu yako, mahusiano, n.k. Ndio maana nimeandika kitabu Cha akili ya Diamond Kitabu kinachoeleza mambo 50 ya kujifunza kutoka kwa Dimond Platnumz Kuhusu Ubunifu, Kipaji Na Mafanikio. Unaweza kukipata kwa kuwasiliana na 0755848391

    Ubunifu kwenye biashara.

    Hivi ninapoandika HAPA, naendelea kusoma kitabu cha THE SCHOOL OF MONEY. Juzi wakati nakisoma nilikutana na kitu ambacho kilinifurahisha sana. Ilikuwa Ni hadithi fupi ya dereva teksi ambaye aliongeza ubunifu kwenye Kazi yake na kuanza kulipwa mara mbili mpaka mara kumi zaidi ya alivyokuwa analipwa mwanzoni.

    Mwandishi anaieleza siku alivyoshuka uwanja wa mdege (airport) na kukutana na dereva huyo. Dereva yule alivyosimamisha teksi tu, wakati anaingiza mizigo ya abiria wake kwenye gari alimpa abiria wake karatasi. Kwenye karatasi hiyo kulikuwa na maono makubwa ambayo dereva huyo anayafanyia kazi na msimamo ambao dereva anausimamia kwenye uendeshaji teksi.

    Kitu hiki kilimshangaza kidogo mwandishi maana hakuwahi kuona dereva wa aina hii popote pale duniani. Mwandishi wa kitabu hicho aliposoma kwenye Ile karatasi mojawapo wa kauli, ilisema lengo langu ni kusafirisha na kuwafikisha abiria kwa usalama wa hali ya juu.

    Wakati mwandishi akiwa anaendelea kutafakari Hilo, dereva alikuwa amemaliza kupakia mizigo yake, na hivyo muda huohuo aliingia kwenye teksi yake.

    Alivyokaa tu kabla ya kuwasha teksi kuondoka, alimwambia abiria wake huwa ana utaratibu wa kuwapa abiria wake kahawa, hivyo alimkaribisha aweze kupata kahawa.

    Abiria alikataa kwa kusema hapendi kahawa Bali anapenda kinywaji Baridi. Palepale dereva akamtolea soda nzuri na kumpa yule mteja wake. Hiki kitu kilimshangaza abiria kiasi akawa anakuuliza mbona napata huduma za viwango vya kifalme?

    Baadaye abiria alifunguka na kumwuliza dereva teksi, huwa unafanya hivi kwa abiria wako wote? Hapo ndipo dereva yule alijieleza kwa kusema kuwa KWELI huwa anafanya hivyo kwa kila abiria. Akaendelea kwa kueleza historia yake ya siku za nyuma.

    Ambapo hapo zamani alikuwa kama madereva teksi wengine. Alikuwa analalamila kuwa maisha Ni magumu. Sasa siku moja alikaa na kutafakari kuona utofauti gani yeye anao ambao watu wengine hawana. Alichokuja Kugundua Ni kuwa yeye na madereva wengine walikuwa wanafanya kazi yao kwa mazoea.

    Teksi zao wote zilikuwa chafu. Walikuwa hawachukui mawasiliano ya wateja wao baada ya kuwabeba ili waendelee kuwasiliana na endapo siku nyingine hao abiria wana safari wawasiliane nao waweze kuwasafirisha kwa mara nyingine.

    Dereva huyo anasema tangu siku hiyo hakuwahi kurudi nyuma na Wala hakuwahi kufanya kazi yake kama ambavyo mtu mwingine alikuwa akifanya. Alijitofautisha.

    Kitu hiki kilimfanya kwanza asiwe tu anakaaa kwenye vijiwe bila mwelekeo, maana watu wengi walikuwa wkintafute huyo dereva, na hata mwandishi kukutana na yule dereva ilikuwa ni kama bahati, siku hiyo. Maana dereva huyo yuko bize muda wote akisafirisha abiria wanaompigia na abiria wengine wapo tayari kulipia fedha yao mapema ili tu waweze kusafirishwa na yule dereva.

    Huo pia ni ubunifu.
    Na wewe Unahitaji kufanya ubunifu kwenye biashara yako au kitu chochote unachofanya. Wape watu sababu ya kuja kununua kwako badala ya kwenda kununua kwa mwingine.

    Wape watu sababu ya kufanya biashara na wewe na siyo mwingine. kuwa mbunifu.

    Ubunifu wa KUONGEZA teknolojia.

    Moja ya kitu ambacho nimekuwa nikiwaambia watu wengi ni kuwa kwenye Biashara yoyote Ile unayofanya unapaswa kuangalia namna gani unaweza KUONGEZA teknolojia. Ukifuatilia Biashara nyingi zinazofanyika kwenye kipindi Cha leo, utagundua kuwa kitu kikubwa ambacho Biashara hizi zimefanya Ni KUONGEZA teknolojia au intaneti kwenye biashara ambazo zikikuwepo kwa siku nyingi zilizopita.

    Watu wamekuwa wanauza na kununua vitabu Vitabu kwa siku nyingi kabla ya amazon. Walichofanya Amazon Ni KUONGEZA teknolojia au intaneti kwenye uuzaji wa vitabu. Badala ya mtu kuhangaika kurafuta vitabu umbali mrefu, Sasa anaweza kuvinunua akiwa chumbani kwake tu.

    Amazon wanafanya Biashara ya kuuza vitabu, Ila Biashara ya kuuza vitabu siyo ngeni kwenye macho ya watu. Ni Biashara ambayo imekuwepo kwa siku nyingi sana ila Amazon wameipa uhai zaidi kwa kuiongezea teknolojia na intaneti.

    Wewe pia kwa Biashara yako unayofanya unaweza kufanya kitu Kama hiki. Unaweza KUONGEZA teknolojia au intaneti. Huo Ni ubunifu rafiki yangu

    Usiache kuchukua kitabu changu cha JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO kwa 7,000 tu/- softcopy. Hki pia kimebuniwa kwa namna ya kipekee. Na kinauzwa kwa njia ya kibunifu ya mtandao, hahaha

    Ukifanya kitu unachopenda ubunifu unakuw amwingi

    Kuna siku nilikuwa nikiongea na mteja wetu mmoja ambaye yuko mkoani Mara (Msoma mjini). Siku hiyo alikuwa amepokea kitabu cha jinsi ya kufikia NDOTO ZAKO na kuanza kukisoma.

    Kitu cha pekee nilichopenda kutoka kwake ni usemi wake anaosema kuwa ukifanya kitu unachopenda, Ubunifu unakuwa mwingi.

    Na hiki kitu nimeona nikushirikishe na wewe pia.

    Kuna utafiti unaonesha kuwa watu wengi wanakufa siku ya jumatatu baada ya kula Bata wikendi halafu jumatatu wanaamka na kwenda kufanya kazi wasiyopenda. Hicho kitu tu, kinawakatisha tamaa.

    Ndiyo maana nimeupenda huu usemi, kiasi cha kuwa tayari kukushirikisha huu usemi na wewe.

    Ujumbe mkubwa ninaotaka kusisitiza hapa ni kuwa ukifanya kitu unachopenda, ubunifu unakuwa mwingi.

    Ukifanya kitu unachopenda hutachoka Ukifanya kitu unachopenda ubunifu unakuwa mwingi.

    Thomas Edison alikuwa analala saa tatu kwenye maisha yake na kuamka mapema kwenda kazini. Siku moja aliulizwa kwa nini unafanya sana kazi.

    Aliwajibu watu kwa kuwaambia kuwa sijawahi kufanya kazi.

    Umeona ee! Alikuwa anafanya kitu anachopenda. Hivyo, kwake hakuona kama hiyo ilikuwa kazi.

    Hivi wewe unafanya unachopenda kweli? Unafanya unachopenda?

    Ngoja nikukumbushe, “ukifanya kitu unachopenda, ubunifu unakuwa mwingi”.

    Ubunifu Unaboresha Biashara Yako

    Kama wewe umekuwa mtumiaji wa muda mrefu kidogo wa mtandao wa WhatsApp utagundua kuwa mtandao huu umekuwa unafanyiwa marekebisho ya hapa na pale kila mara. Kuna kipindi haya mambo ya status au WhatsApp business hayakuwepo.

    Nakumbuka suala zima la kubold, italicize, underline na strikethrough na yenyewe hayakuwepo.

    Ila kadiri siku zilivyoendelea yamewekwa. Hayo ni machache tu kati ya marekebisho mengi ambayo wamefanya.

    Ninachotaka kukwambia ni kwamba kwenye biashara yako, ni vizuri kuwa mtu wa kufiria nje ya boksi na kufikiria zaidi ya hapo ilipo kwa sasa.

    Ubunifu utaitofautisha sana biashara yako na biashara za watu wengine. Maana hata ukisema ufanye biashara ambayo haijawahi kufanywa hapa duniani. Ndani ya miezi sita tu, kuna watu watakuona ukiifanya na wenyewe wataanza kuifanya. Kumbe basi, kitu pekee ambacho kinaenda kukutofautisha wewe na wengine ni ubunifu.

    Ubunifu Siyo Mpaka Uwe Na Wazo Ambalo Halijawahi Kuwepo

    Wengi wanapofikiria ubunifu basi wanadhani, mbunifu yeyote anapaswa kuja na wazo la kipekee sana na wazo ambalo halijawahi kuonekana. Unaweza kuja na wazo la kawaida, ila kwenye biashara yako likawa linaleta mapinduzi.

    Inashauriwa walau kila siku uwe unafikiria mawazo ya kawaida kumi tu na kati ya hayo utoe moja au mawili ambayo utayafanyia kazi. Ukiwa mtu wa kufikiria hivi ni uhakika kuwa mwaka mmoja baadaye, kama ni biashara, lazima tu utakuwa umeisukuma mbali.

    Ubunifu Siyo Mpaka Uwe Profesa

    Ubunifu ni kitu tunazaliwa nacho. Ndiyo maana utagundua kwamba kila mtoto huwa anapenda kuumba vitu mbalimbali kwa kutumia udongo, mchanga au malighafi zozote anazoona zinamfaa.

    Kwa hiyo hiki kiwe kiashiria kwako kuwa UBUNIFU ni kitu tunacho, tumezaliwa nacho na tunaenda nacho popote. Kadiri ambavyo utautumia ubunifu kwenye kazi, biashara au eneo lolote, ndivyo utakavyoimarika zaidi na zaidi.

    Moja kati ya vitu muhimu sana katika biashara, mahusiano na kazi ni ubunifu. Ni kupitia ubunifu mtu unaweza kuja na mbinu mpya za kuongeza wateja, ni kupitia ubunifu unaweza kujua ni bidhaa gani ukiiboresha zaidi itakuongezea wateja zaidi. Ni kupitia ubunifu utajua ni bidhaa gani ukiipunguza  au ukiiondoa kwenye mfumo wako wa biashara utakuwa hujapungukiwa na kitu. Kwa hakika binafsi nauita ubunifu moyo wa biashara.

    Sasa ubunifu ni nini?

    Mpaka hapa utakuwa unajiuliza huu ubunifu unaoongelewa ndio unafananaje? Ndio nini haswa?

    Vyanzo mbali mbali vimeudadafua ubunifu kama matumizi ya njia bora zaidi zinazokidhi kutatua changamoto mpya, changamoto ambazo tayari zipo lakini hazijapatiwa ufumbuzi bado, au changamoto zilizopo kwenye soko au jamii kwa kipindi husika.

    Hata hivyo kwa mantiki ya andiko hili, tutatumia maana ifuatavyo UBUNIFU NI HALI YA KUJA NA WAZO JIPYA LA KUBORESHA, KUIMARISHA AU KUBADILISHA KITU KATIKA NAMNA YA UPEKEE.

    Ubunifu katika biashara ni wa aina mbili. Kwanza kuna ubunifu mlalo na ubunifu sambamba.

    Ubunifu mlalo ni aina ya ubunifu ambapo mtu unakuwa na kitu kimoja ila unakikuza kitu hicho hicho zaidi na zaidi. Mfano mtu unagundua kwamba kalamu za aina fulani zinapendwa sana na watu katika eneo langu. Basi unaongeza uzalishaji wa kalamu za aina hiyo hiyo ili ziwe nyingi zaidi. Huu ndio unaitwa ubunifu mlalo.

    Ubunifu sambamba. Huu ni ubunifu ambao unatokea pale unapokuwa unazalisha kitu kimoja ila ukagundua kwamba ili kitu hiki kifanye kazi vizuri basi hapa tunahitaji kitu kingine cha ziada. Kwa kutumia mfano wetu hapo juu. Unazalisha kalamu ila unagundua kwamba ili kalamu yako ifanye kazi vyema basi inahitaji daftari. Hivyo unaanza kuzalisha na daftari. Huu ndio  ubunifu sambamba. Ubunifu sambamba tunaweza kuuona katika maeneo mengi sana kwenye maisha yetu. Ukiangalia uwepo wa simu umesababisha uwepo wa laini za simu. Huu ni ubunifu sambamba. Uwepo wa viatu umezalisha uhitaji wa soksi huu nao ni ubunifu sambamba.

    Mtu anayeuza runinga lazima tu atatakiwa kuwa na remote na hata ving’amuzi, huu pia ni ubunifu sambamba.

    Jinsi ya kutumia aina hizi mbili za ubunifu.

    Bila shaka mpaka hapo utakuwa unajiuliza, hivi hizi aina mbili za ubunifu zitanisaidiaje kwenye biashara zangu?

    Jibu ni rahisi sana. Kama kuna biashara yako unafanya sasa hivi. Angalia ni bidhaa gani inapendwa zaidi na watu. Ukishaipata bidhaa ya namna hii basi izalishe zaidi na hakikisha unaongeza mauzo. Kumbuka mapato makubwa sana kwenye biashara yako hayatoki kwenye kuuza kila kitu. Ila yanatokea kwenye kuuza bidhaa chache kwa wingi sana. Sasa hapa unahitaji kukaa chini na kujiuliza ni bidhaa gani hizi chache ambazo nikizizalisha kwa wingi zitaongeza mapato makubwa sana.

    Au ni bidhaa gani nikiziongeza kwa wingi kwenye mzunguko bado nitazidi kuuza sana. Hapa utakuwa umetumia ubunifu mlalo.

    Unaweza pia kutumia ubunifu wima kwa kuangalia aina ya bidhaa ambayo ukiizalisha itakuwa inaendana na ile ambayo ulikuwa hapo awali. Jiulize ni bidhaa gani inaweza kwenda sambamba na bidhaa ninayouza sasa hivi na ikauza vizuri bila shida? Mfano rahisi sana ni pale unapokuwa unauza majiko ya gesi. Unaweza kuongeza kitu cha ziada kwa kuuza vyombo vingine vinavyotumika jikoni. Ukiweza kuvijua vitu hivi vinavyoenda sambamba na ile bidhaa ya awali baasi hapo utakuwa umetumia ubunifu sambamba.

    Kwani kuna ulazima wa kutumia ubunifu kwenye biashara?

    Zama zimebadilika, maisha nayo yamebadilika, lakini pia mfumo wa uendeshaji wa biashara umebadikika.

    Katika zama za sasa biashara zinazoendeshwa kibunifu ndizo biashara zinazopendwa na watu. Kwa hiyo ubunifu sio tena suala la hiari, ni lazima. Tungekuwa kwenye miaka ya 50 na 60 kabla uhuru ambapo maduka na wafanyabiashara walikuwa wachache sana, hapo suala la ubunifu tungeliweka pembeni na kushughulika na mambo mengine. Ila kwenye zama hizi hapa hakuna jinsi ubunifu ni lazima.

    Lazima kuwepo na sababu za kwa nini watu waje kununua kwako na sio kwa rafiki yako mwenye duka na anauza bidhaa kama unazouza. Sasa hapo ubunifu ndipo unaingilia katikati. Kwa hiyo ubunifu ni lazima wala sio ombi!

    Ubunifu ni muhimu kwenye biashara, michezo, sanaa, uigizaji, ufundishaji, mziki, upambaji n.k. yaani maisha na ubunifu ni vitu ambavyo hatuwezi kabisa kuvitenganisha 

    Sasa kama ubunifu ni muhimu kwa nini watu sio wabunifu?

    Mbali na kwamba tumeona ubunifu ni muhimu sana kwenye biashara na maisha ya kawaida bado ubunifu haujapewa kipaumbele hata kidogo kwenye bara la Afrika. Kuna watu wengi sana wamezaliwa na vipaji vikubwa sana vya kubuni na kuja na mbinu mpya ila bado hawajavitumia. Hizi hapa ni sababu zinazofanya watu wafanye vitu kwa namna ile ile kila siku bila kuongeza thamani za kibunifu.

    1.  KILA MTU ANAFANYA HIVYO

    Mara nyingi sana watu wapo katika mazingira ambayo kila kinachofanyika basi kinafanyika kwa namna ile ile tu.

    Yaani kwamba ameamka asubuhi, ameoga na kuzunguka  huku na kule, na kila mtu anafanya hivyo basi na yeye anaishi hivi. Maisha haya hayawezi kuzalisha wabunifu wakubwa. 

    2. BABU ZETU WALIKUWA WANAFANYA HIVI

    Hivi ushawahi kuthubutu kufanya kitu ukasikia mtu anakwambia “usifanye hivyo, babu zetu hawakuwahi kufanya kitu kama hicho“. Yaani watu wanatengeneza sheria zao wenyewe, wanazipitisha wao wenyewe na kutaka ziwe sheria za watu wote.

    Sasa kwamba baba au babu alikuwa anafanya vile ina athari gani na mimi nikifanya kwa namna nyingine. Maneno haya yanatumiwa sana na watu ila kiukweli ni kwamba hata hayajengi na hayana mantiki. Hivyo ni vyema kabisa kwa wewe kama wewe kujua kwamba tunapaswa kubuni na kuja na mbinu mpya za kibunifu kila wakati.  Kuendelea kufanya vitu kwa namna ile ile kila siku hakuwezi kukuinua na kutusogeza mbele Tanzania na Afrika nzima kiujumla. Nipo nafikiri kama Albert Einstein angeendelea na fikra zile zile za mababu wetu walikuwa wanafanya hivi angeweza kugundua sheria MC²?

    Hivi kama Mark Zuckerberg angeendelea kushikilia imani ya kwamba babu zetu walikuwa wanawasiliana hivi, angeweza kuja na mtandao wa kijamii wa facebook. Ebu watanzania badilikeni kabisa. Achana na mambo ya babu zetu walikuwa wanafanya hivi au vile. Sasa zama zimebadilika, maisha nayo yamebadilika hivyo na wewe unahitaji kubadilika, kubuni na kuja mbinu mpya zitakazoisaidia jamii. Acha ya kale yaitwe ya kale ila sasa panga mambo mapya ya kibunifu.  

    3. KELELE ZA DUNIA

    Tunaishi kwenye dunia yenye kelele nyingi sana. Kuanzia asubuhi utasikia miziki inapigwa kila kona, magari yanapita kwenye maeneo yetu ya kazi, watu wanaongea na kupiga kelele. Yaani ni vurugu mechi.

    Bila ya mtu kuamua kuthubutu kujitenga na dunia kwa muda ili kutulia na kujitafakari basi maisha yataendelea hivi hivi tu. Kutokana na hali  hii basi hapa mtu unahitaji muda wa kupumzika, kujitenga na watu na kufikiri kwa kina juu ya maisha yako, biashara, mahusiano n.k hapa ndipo unaweza kuja na mawazo mapya ya kuendeleza na kuibua ubunifu wako

    4. UOGA

    Hivi watu watanichukuliaje? Hili ni swali lililo kwenye akili za watu walio wengi sana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mtu alikuwa amezoeleka kwa namna ya kawaida kwa watu na yeye tayari amehajijengea picha ya namna hiyo kama vile ni kweli. Ingawa sio. Huu uoga huu sio wa kuendekeza hata kidogo. Vijana wa Tanzania na Afrika, umefika wakati wa kuchukua hatua kubwa sana na kuhakikisha kwamba tunaibua ubunifu ulio ndani yetu.

    5. UKOSEFU WA VIPAUMBELE

    Watu wengi huwa hawana utaratibu wa kupangilia kazi wanapoamka asubuhi.  Hivyo kujikuta wanafanya kazi kwa mazoea. Kufanya kazi kwa mazoea hakuwezi kuleta ubunifu kazini. Hivyo wewe kama mbunifu unahitaji kutenga muda kidogo wa kuhakikisha unafanya kitu kwa kukiboresha zaidi na zaidi.

    Usijifanye umebanwa kiasi kwamba huwezi kuangalia ni kitu gani bora zaidi unaweza kufanya ili kuboresha biashara au kitu chochoe unachofanya.

    Na hili litawezekana kama utapangilia ratiba yako kila siku unapoamka.

    Haya ndio mambo matano yanayoua ubunifu katika bara letu la Afrika na haswa Tanzania yetu. Ukiyaepuka haya rafiki yangu nina hakika utakuwa mbunifu mzuri kwenye eneo lako la kazi, biashara, michezo kutaja ila vichache.

    Hatua tatu za ubunifu

    Ubunifu hupitia katika hatua mbalimbali mpaka kitu kinapokuja kuonekana. Sio tu suala la kulala na kuamka ukisema mimi ni mbunifu.

    Ukizipitia hatua hizi utakuwa mbunifu mzuri sana katika dujinia hii.

    1. Hatua ya kwanza ni kutambua. Hii inaweza kuwa ni

    • Kujitambua wewe mwenyewe. Wewe ni nani? Kitu gani ambacho unaweza kukibuni? Ujuzi gani ulio nao unaweza kukuogezea ubunifu ukawa bora zaidi!
    • Kutambua kile unachohitaji, (je unahitaji kubuni nini? Mwonekano wake ukoje? Je,mwonekano unaweza kubadilika baadae? Kitu gani kinakusukuma wewe kusema hivyo?

    2. KUKIFANYIA KAZI. (ACTION)
    Ukishatambua wewe ni nani?
    Kitu gani unahitaji ili kuwa bora zaidi. Sasa hatua inayofuata ni kufanyia kazi kile kilicho ndani yako. Kuhakikisha kwamba unakiboresha. Hapa utahitaji kutumia nguvu na muda wako kubadili kile kilicho akilini mwako. Kama akilini mwako kuna mawazo hakikisha kwamba unayafanyia kazi.Yaweke katika matendo.

    Soma Zaidi; Vitu Utakavyojifunza Kwenye Kurasa Za Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni

    3.Matokeo

    Angalia kile kinachofanya kazi na kile ambacho hakifanyi kazi.

    kinachofanya kazi endelea nacho. Kisichofanya kazi achana nacho.

    Tukutane siku nyingine kwenye makala ya kuelimisha na kuhanasisha kama hii.

  • Vitu vitano ambavyo hupaswi kuvipoteza kwenye safari yako ya mafanikio

    Siku ya leo nataka nikwamie vitu viwili vikubwa sana ambavyo hupaswi kupoteza kwenye safari yako ya kufikia ndoto zako.

    Kwanza usipoteze ndoto yako kubwa

    Hiki ni kitu muhimu sana. ukipoteza ndoto zako maana yake unapoteza ile motisha na ile nguvu ya kukusukuma wewe kuweza kufanya kitu cha tofauti. Mara zote na sehemu zote hakikisha kwamba haupotezi ndoto yako kubwa uliyonayo.

    Ndoto kubwa ndiyo inakupa motisha na nguvu ya kusongambele mara zote.

    Pili haupaswi kupoteza kitu ambacho umetafuta kwa hela yako

    Kama kuna kitu umekinunua kwa hela yako, hela ambayo umeitafuta kwa nguvu zako zote, usikubali kitu hiki ukipoteze kirahisi. Kitunze vizuri kwelikweli.

    Tatu, usikubali kupoteza uaminifu ambao watu wanao juu yako

    Kama kuna watu wanakuamini, usikubali kupoteza uaminifu huo kwa vizutu vya kijinga.

    Nne, usikubali kupoteza mahusiano yako

    Mahusiano yako ni muhimu kwa ajili ya mafanikio yako. Hakikisha unayapa kipaumbele mahusiano yako

    Tano, usikubali kupoteza afya yako.

    Afya yako ni muhimu sana kwako. hakuna hata mtu mmoja ambaye huwa anaweza kufanikiwa kwa viwango vikubwa bila ya afya. Ukifanikiwa huku ukiwa unaumwa, hutaweza kufurahia mafanikio hayo makubwa uliyokutana nayo.

    /

  • NGUVU YA KUFANYA MAZOEZI

    Ukitoa jasho jingi wakati wa mazoezi, utavuja damu kidogo wakati wa vita

    Siku moja rafiki yake Kobe Bryant alimtembela Kobe,  sasa wakati wanaongea wakawa wamekubaliana kuwa kesho yake alfajiri yule rafiki yake Kobe ambaye pia alikuwa kocha angekuja kushirikiana na Kobe kwenye kumsaidia kufanya mazoezi. Wakawa wamekubaliana muda wa kukutana ambao ulikuwa ni saa kumi alfajiri sana. Kisha wakaagana, wakati wanaagana yule rafiki yake Kobe Bryant alimwacha Kobe anafanya mazoezi.

    Rafiki yake Kobe Bryant alikuwa na uhakika kuwa Kobe hawezi kuamka na kuwahi kesho muda huo waliokubalilana, hivyo hata kesho yake alivyokuwa akielekea uwanjani alikuwa na uhakika kabisa kuwa Kobe hawezi kuwa amefika uwanjani, ila cha kushangaza ni kuwa alikuta kobe tayari ameshafika uwanjani akiwa anafanya mazoezi. Lakini kilichomshangaza zaidi ni kuwa Kobe Bryant alionekana kama mtu ambaye alikuwa akifanya mazoezi kwa muda mrefu kabla yake. Kadiri rafiki yake huyo alivyofuatilia alikuja kugundua kitu kimoja kikubwa sana, aligundua kuwa kobe Bryant alikuwa ni mmoja wa watu ambao walikuwa wanathamini sana mazoezi na hivyo alikuwa anaweka nguvu kubwa sana kwenye kufanya mazoezi.

    Moja ya kitu ambacho watu wengi huwa wanachukulia poa sana ila nimekuja kugundua kuwa watu ambao wanafanya vizuri karibia kwenye kila sekta wanakitumia ni kufanya mazoezi ya kutosha nyuma ya pazia. Hiki ni kitu cha kushangaza sana, ila ni kitu ambacho kinafanya kazi na ni kitu ambacho wewe mwenyewe unahitaji kuhakikisha kwamba unakifanyia kazi kwenye maisha yako.

    Lakers at Wizards 12/3/14

    Kobe Byrant

    Mazoezi yanakujenga

    Sina shaka umewahi kusikia usemi kwamba practice makes perfect. Yaani, kwamba mazoezi ndiyo yanakuimarisha na kukufanya kuwa bora zaidi. kuna siku nilikuwa nasoma kitabu cha Steve Jobs, kinaitwa Presentation Secrets of Steve Jobs.

    Ujue Steve Jobs ni miongoni mwa watu ambao walikuwa akitoa hotuba za kipekee sana kwenye maisha yake. Hotuba zake zilikuwa zikivutia watu kiasi kwamba watu walikufunga safari kutoka mbali na tena wengine walikuwa wakilipia miezi mingi kabla ya siku yake ya kutoa hotuba ili tu wapate viti vya mbele siku anapotoa hotuba.

    Hata leo hii ukifuatilia hotuba zake mtandaoni, utagundua kuwa ni miongoni mwa hotuba chache ambazo zimeangaliwa mara nyingi zaidi kuliko waneni wengine. Sasa nini siri iliyo nyuma ya hotuba hizi? Siri kubwa sana iliyo nyuma ya hotuba hizi ni kuwa, Steve Jobs alikuwa akifanya mazoezi na kujiandaa kwa siku nyingi kabla ya siku yenyewe ya tukio. Unaambiwa alikuwa akijiandaa kwa siku `100 kabla ya siku yenyewe ya hotuba.

    Mtu akikukwambia siku 100 za maandalizi kabla ya siku ya hotuba unaweza kuchukulia poa, ila ukweli ndio huo. Mazoezi ni moja ya kitu muhimu zaidi kwenye kitu chochote kile unacahofanya.niambie kitu chochote kile unachotaka kufanya, nami nitakwambia kwamba fanya mazoezi.

    • Unataka kufaulu mitihani, basi fanya mazoezi mengi kabla ya siku za mitihani.
    • Unataka kujifunza lugha ya kigeni kama kiingereza, kifaransa, kichina au kiarabu, basi fanya mazoezi ya kutosha.
    • Unataka kunoa kipaji chako na kukifanya kiwe bora zaidi, fanya mazoezi.
    • Unataka kuandika maandiko mazuri kama mimi, basi fanya mazoezi.

    Kwa kitu chochote kile unachotaka kufanya na kukifanikisha kwa viwango vikubwa basi fanya mazoezi.

    Kijana mmoja siku moja alisikia stori ya Michael Jackson, ujue michae Jackson ni mmoja wa wasanii ambao wameacha alama kubwa mpaka leo na mpaka leo hii bado anakumbukwa sana kwa miziki yake na jinsi ambavyo alikuwa akitikisha dunia kwa miondoko yake kwenye muziki.

    Sasa kijana huyu aliambiwa kuwa Michael Jacksoni alikuwa akifanya mazoezi kwa saa zaidi ya 8 kila siku, alishangaa sana. Tena alianza kubisha kwa kusema kwamba Michael Jackson alikuwa mchezaji (dancer) kwa asili hivyo hakuhitaji kufanya mazoezi. Ila ukweli unabaki kuwa mazoezi ndiyo mama wa kila kitu.

    Watu wengi unaowaona kwamba wana vipaji vya asili kabisa, au vipaji vya kuzaliwa navyo, siyo kwamba walizaliwa wakiwa hivyo, bali ni mazoezi ya kutosha ndiyo yanawafanya waweze kuwa walivyo.

    Unachopaswa kufahamu ni kuwa kuna watu wengi sana ambao wana vipaji ila hawajaweza kufanya vizuri kwa sababu tu hivyo vipaji vyao hawakuvifanyia mazoezi. Mazoezi kwenye maisha ndiyo kila kitu.

    Ebu chukulia mfano tu wa kawaida wa mchezaji wa mpira aliye kwenye timu ya taifa ni wazi kuwa kabla ya kucheza kwenye timu ya taifa anakuwa tayari ameshachezea timu nyingi sana huku nyuma ya pazia. Na kama ni mazoezi anakuwa ameshafanya mengi na ya kutosha, lakini kadiri anavyokua anakuwa ndivyo anaongeza mazoezi zaidi kwenye kile anachofanya.

    Ndiyo maana utasikia kuwa timu ya taifa imeweka kambi eneo fulani, lengo lake likiwa kwamba wachezaji wake waweze kufanya mazoezi.

    Wachezaji kama akina Ronaldo au Messi, mbali na umaarufu wao wote, ila bado leo hii wanaendelea kufanya mazoezi mengi na ya kutosha bila ya kurudi nyuma. Hiki kitu kinatuonesha kuwa kama kuna siri ya pekee ambayo tunahitaji kuikumbatia basi ni kufanya mazoezi.

    Mazoezi yanakujengea kujiamini

    Kadiri unavyofanya mazoezi zaidi, ndivyo unavyoongeza kujiamini kwenye kile ambacho unafanya. hivyo basi kama unataka kujiamini zaidi, ongeza mazoezi ambayo unafanya. Na hili lipo wazi kabisa, kama kuna watu wawili ambao wanapaswa kusimama mbele ya watu na kuongea, mmoja akajiandaa kwa siku nyingi nyuma ya pazia.

    Akafanya mazoezi kwa kujiuliza maswali ambayo watu wanaweza kumuuliza wakati anawasilisha mada yake na hata kuyaandalia majibu, akajipanga atakavyowasilisha pointi moja baada ya nyingine, lakini pia akajipanga mpaka namna atakavyovaa siku ya tukio. Na mwingine akapuuzia kufanya maandalizi na mazoezi, mpaka dakika za mwisho kabla ya kusimama mbele ya watu ndio akaanza kujiandaa. Ni wazi kuwa aliyejiandaa kwa siku nyingi atakuwa anajiamini zaidi kuliko yule ambaye hakujiandaa.

    Mazoezi yanakujegea kujiamini

    Kanuni muhimu kwenye mazoezi

    Kama kuna kitu muhimu sana ambacho unahitaji kukifahamu linapokuja suala zima la mazoezi ni kuwa, usifanye mazoezi unapojisikia kufanya mazoezi. Usifanye mazoezi mara moja kisha kusahau na kuja kufanya mazoezi siku nyingine nyingi za baadaye.

    Mazoezi yanapaswa kuwa sehemu ya maisha yako ya kila siku. Kadiri kitu unavyokuwa ukiyafanyia kazi ndivyo ambavyo unakuwa unazidi kuimarika zaidi na zaidi kwenye hicho kitu. Hivyo, kitu kikubwa na cha msingi ni kuwa usisubri mpaka siku ambapo utaweza kufanya mazoezi kwa mara moja, tu endelea kufanya mazoei kila siku bila ya kurudi nyuma. Yafanye mazoezi kuwa sehemu ya pili ya maisha yako.

    Fanya mazoezi kwa bidii zako zote, ila unapoenda kuonesha kitu ulichofanyia mazoezi kifanye kama vile umezaliwa nacho.

    Tayari tumeona kuwa hakuna mtu ambaye anazaliwa akiwa anajua kila kitu kiasi kwamba hatahitaji kufanya mazoezi. Tayari tumeona kuwa watu wote wanaofanya makubwa kwenye kila sekta wanafanya mazoezi makubwa nyuma ya pazia. Yaani, wanafanya mazoezi mpaka ile dakika ya mwisho.

    Sasa siku siyo nyingi kuna kitabu nilikuwa nasoma, japo sikumbuki vizuri ni kitabu gani na wala sikumbuki jina la mhusika aliyedokezwa kwenye kile kitabu, ila ninachokumbuka kwenye kile kitabu walikuwa wakimwonglea mwigizaji mmoja ambaye alikuwa akifanya vizuri sana.

    Yaani, kuna igizo moja ambalo alikuwa akiliigiza kwenye kila jukwaa, na watu wengi walikuwa wakilipenda. Sasa baada ya igizo hilo kuwa maarufu, mwandishi wa habari alienda kumhoji ili aweze kupata mawili matatu, kutoka kwa mwigizaji yule.

    Hivyo, mwandishi alienda nyuma ya pazia (eneo ambapo waigizaji wanakaa kabla ya kuingia jukwaani kuigiza). Kilichomshangaza mwandishi wa habari ni kuwa alikuta mwigizaji yule akiwa bado anafanya mazoezi kwenye zile dakika za mwisho kabla ya kuonekana kwenye jukwaa. Hivyo, mwandshi wa habari alipaswa kusubiri kwa muda mrefu kabla ya kuonana na mwigizaji, pale mwigizaji alipomaliza kufanya mazoezi, akiwa anaelekea jukwaani, ndipo mwandishi wa habari alipata kumuuliza swali. Inakuwaje unafanya mazoezi wakati umekuwa ukiigiza igizo hilohilo kila mara?

    Yule mwigizaji alisema, kwa sababu mazoezi ndiyo yananifanya kuwa imara zaidi na yananifanya nijiamini ninapoenda kuigiza.

    Rafiki yangu,  unaona ee, mazoezi yana nguvu kubwa sana.

    Kama kuna vitu vitatu ambavyo ninaweza kukwambia uvipe kipaumbele kwenye maisha yako, kipaji chako, biashara yako n.k. basi vitu hivyo vitakuwa kama ifuatavyo,

    • Kwanza yatakuwa ni mazoezi
    • Pili ni mazoezi na
    • Tatu ni mazoezi

    Naam, nne ni mazoezi tena. Usipuuze mazoezi maana mazoezi yana nguvu kubwa sana, hivyo usiyachukulia poa hata kidogo.

    Kitu kimoja nilichokuja kujifunza kuhusiana na mazoezi ni kuwa unapaswa kufanya mazoezi ya kutosha nyuma ya pazia, ila unapoenda mbele ya watu wasilisha kama vile ulizaliwa hivyo. Wasilisha kama vile huwa hufanyi mazoezi.

    Kufanya mazoezi ni mama wa kujifunza

    Wakati nasoma O-level kuna mwalimu  mmoja ambaye alikuwa akipenda sana kutwambia usemi wa kilatini. Usemi huu unasema hivi, repetitio est mater studiorum. Ukimaanisha kuwa mazoezi ndiyo mama wa kujifunza au kusoma. Kadiri unavyofanya mazoezi zaidi, ndivyo unaimarika na kuwa bora zaidi, na kadiri unavyopuuzia mazoezi ndiyo unazidi kudorora.

    Kiwango kimeshuka

    Sina shaka umewahi kusikia watu wakisema kwamba mtu fulani kiwango chake kimeshuka siku hizi. Na hasa kwa wachezaji. Wengi huwa unakuta kwamba kiwango chao kinashuka kwa sababu tu kupunguza kufanya mazoezi au kutofanya mazoezi kabisa.

    Mwingine huwa unakuta kwamba anapokuwa chini anakuwa anajituma sana anafanya mazoezi, ila kadiri anavyokuwa anazidi kukua na kufikia viwango vya juu, basi analewa ule umaarufu na fedha kitu ambacho kinamfanya aache kufanya mazoezi na mwisho wa siku anajikuta ameshuka kiwango.rafiki yangu, usikubali kiwango chako kishuke kwa sababu ya kutofanya mazoezi. Kumbuka mazoezi ndiyo mama wa ujuzi wowote unaotaka kujenga.

    Upo tayari kujiandaa kwa miaka minne?

    Mashindano ya olympiki ni miongoni mwa mashindano yenye nguvu sana. Yanapendwa na watu lakini pia washiriki wake huwa wanajiandaa kwa kipindi kirefu kabla ya mashindano yenyewe. Washiriki wa mashindano hayo wanajiandaa kila siku kwa kipindi cha miaka minne kwa ajili ya shindano ambalo linadumu kwa dakika kadhaa kisha kupotea. Na ndani ya dakika hizo ndipo mshindi huwa anapatikana na kupewa zawadi nono.

    Sasa swali langu kwako siku ya leo ni kwamba je, na wewe upo tayari kuweka kazi na juhudi kwa kipindi cha miaka minne, mitano sita mpaka kumi mfululizo kabla ya kupata matokeo na kula vinono ambavyo ungependa kupata? Unapaswa kuwa tayari kufanya hivi kwa sababu mafanikio makubwa huwezi kuyapata kwa usiku mmoja tu. Mafanikio makubwa ni matokeo ya vitu vidogo vidogo ambavyo unafanya kila siku vikiunganishwa kwa pamoja. Usiidharau siku moja na kukaa ukisubiri ufike mwisho wa mwaka ambapo utapata mafanikio makubwa, badala yake fanya kitu leo. Ukiunganisha hivi vitu vidogo vidogo, mwishoni mwa mwaka utakuwa umeweza kufanya makubwa.

    Siku moja Piccasso alikuwa akitembea mjini, alikutana na mama mmoja ambaye alimwomba amchoree picha. Kwa harakaharaka yule mama alichukua penseli na karatasi , kisha akampa Picasso. Picasso alichora hiyo picha ndani ya sekunde 30, ikawa imekamilika. Ilikuwa inapendeza sana. Sasa baada ya kuwa amemaliza kuchora hiyo picha, Picasso alimwambia yule mama kuwa hii picha ina thamani ya dola milioni moja.

    Yule mama alishindwa kujizuia na kumwuliza, unafanyaje kuchora picha ndani ya sekunde 30 yenye thamani ya milioni. Na mimi ningependa kujifunza huu ujuzi ili niwe nalipwa milioni ndani ya sekunde thelathini.

    Huku akiwa na tabasamu usoni, Picasso alijibu kwa kusema kuwa, imemchukua miaka thelathini ya mazoezi kuweza kuchora picha ndani ya sekunde 30 yenye thamani zaidi ya dola milioni moja.

    Lada hapa swali langu kwako ni kuwa je, upo tayari kuweka muda wa kutosha kufanya mazoezi ili uweze kubobea kwenye ujuzi na kile ambacho umeamua kufanyia kazi?

    Pablo Picasso katika ubora wake

    Hivi Ndivyo Mazoezi Yanaweza Kukufanya Ule Meza Moja Na Mfalme

    Katika mazingira yetu ya sasa hivi wafalme sio watu waliozoeleka sana kulinganisha na kipindi cha nyuma. Zamani kidogo ulikuwa unakuta kabila au nchi fulani ina mfalme wake ambaye watu wote wanamsikikiza na sauti yake iko juu kwenye masuala ya utawala.

    Lakini pia mfalme kama kiongozi alikuwa anapata vitu vyote vizuri. Yaani kwake nguo zilikuwa ni nguo bora sana kuliko mtu mwingine, chakula chake kilikuwa ni chakula bora sana, malazi yake yalikuwa ni ya kipekee sana. Sio hivyo tu hadi usafiri wake ulikuwa ni wa kipekee, ardhi ya mfalme ilikuwa ni ardhi yenye rutuba kweli kweli. Kwa mazingira ya sasa hivi mfalme ndio raisi wa nchi.

    Lakini kwa mantiki ya andiko hili mfalme sio rais tu. Naomba nitoe maana ya mfalme kulingana na ujumbe wa leo. Mfalme ni mtu ambaye amefikia mafanikio makubwa iwe ni kiuchumi, kiuongozi, kiroho, kimahusiano, n.k

    Mtu ambaye wewe ungependa kukutana naye au pengine umekuwa na shauku ya kukutana naye kwa siku nyingi sana ila hutapata nafasi hiyo kutokana na utofauti uliopo kati yako na yeye kimafanikio.

    Hawa ni watu ambao stori za kitaani huwa tunaishia kusema walikuwa na bahati. Pengine huwa tunasema walibahatika kurithi mali za mjomba, baba, shangazi au ndugu fulani. Au ni wale watu ambao wengine wanasema alikutana na jini likampenda basi likampa utajiri. Hahaha.
    Na pengine wapuuzi wengine wanasema amejiunga freemason.

    Je, kuna watu ambao umewahi kusema maneno kama haya juu yao. Je, kuna watu wa namna hii ambao ungependa kukutana nao ila hujui utawezaje? Leo hii ninakuja kwako na namna rahisi sana ya kukuwezesha kukutana na watu hawa na pia mbinu hizi zitakuwezesha kuwa mmoja wao.

    Moja anza kwa kujiuliza una nini? Ni kitu gani ambacho unaweza kuanza nacho kikakusogeza mbele. Je, una kisomo fulani? Au una kipaji fulani? Au utaalamu fulani?

    Ukishajua kile ulichonacho kinachofuata ni wewe kuamua kuwa gwiji kwenye hicho kitu. Usihangaike na mengine. Ebu tuchukulie mfano umejikuta wewe una ujuzi na kisomo cha sheria. Basi unaamua kukomaa hadi kuwa gwiji wa sheria. Mpaka kieleweke. Hakikisha kama katika nchi hii wanatafuta wanasheria watatu mabingwa basi na wewe unakuwepo. Suala hili halitakuchukua mwaka mmoja au miwili. Ni suala la muda mrefu. Kuanzia miaka saba mpaka kumi na tano!!!!!!!!!

    Lakini ukiweza kutoboa hapa. Jua utakula meza moja na wafalme. Kwanza utakuwa mtu ambaye anafutwa sana jambo ambalo litapelekea wewe kulipwa sana. Jambo ambalo litapelekea wewe kupata vizuri sana ambavyo ulikuwa unatamani (gari, nyumba, n.k)

    Jambo hili halitawasili kwako kirahisi rahisi kama unavyofikiri, litahitaji kuwekeza katika kusoma. Litahitaji pia uwekeze katika kufanya mazoezi ya kitu hicho.

    Ebu tuchukulie mfano wetu hapo juu. Umejikuta una kisomo cha sheria, basi utapaswa kufanya mazoezi ya masuala ya sheria kila iitwayo leo. Utahitaji kusoma sana vitabu vya sheria kuliko mtu mwingine aliyekuzunguka. Kumbuka, ukitoa jasho jingi sana wakati wa mazoezi, utatoa damu kidogo wakati wa vita.

    Huwezi kuwa komando kwa mazoezi ya mgambo

    Wakati naelekea kumalizia andiko langu, ningependa kusistiza kitu kimoja. Kwa vile nimesema unapaswa kufanya mazoezi, usiishie tu kujionesha kuwa na wewe unaweza kufanya mazoezi, kama utaamua kweli kufanya mazoezi basi unapaswa kuwa tayari kufanya mazoezi kwelikweli kulingana na kitu chako. Ufanye mazoezi kulingana na kule unapotaka kufika. Ni wazi kuwa huwezi kuwa komando kwa kufanya mazoezi ya mgambo. Huwezi kuwa mwana

    Sasa kabla sijamalizia kuna vitu muhimu hapa ambavyo ningependa kusisitiza kuhusu kufanya mazoezi.

    • Mazoezi yanaweza kukusaidia kufanya yasiyowezekana yakawa yanayowezekana.
    • Ukifanya mazoezi ya kutosha wakati wa amani, utatoka damu kidogo wakati wa vita.
    • Mazoezi yanakufanya kuwa imara zaidi.
    • Mazoezi yanaweza kukufanya ufikie kitu chochote kile unachotaka.
    • Mazoezi yanaweza kumfanya kilaza kuwa gwiji, yanaweza kumfanya mchezaji wa kawaida kuwa mchezaji wa kimataifa, mwimbaji wa kawaida kuwa  mwimbaji mwenye jina kubwa,  na yanaweza kufanya maajabu kwako pia. Na hapa huhitaji konekisheni, wala kipaji bali unahitaji mazoezi.
    • Kujifunza peke yake bila mazoezi hakuna maana Ebu fikiria ukae ujifunze kuhusu mbinu zoote za kushona suti, bila kuzifanyia kazi. Au ujifunze kuhusu kucheza kucheza kinanda bila ya kufanyia mazoezi haya maarifa uliyojifunza. Ni wazi kuwa kwa vyovyote vile huwezi kubobea, hivyo raha ya maarifa na kila kitu unachojifunza ni kukifanyia mazoezi.
    • Unapofanya mazoezi ni sawa na mtu ambaye anakuwa anafanya uwekezaji. Muunganiko wa mazoezi yale unayokuwa unafanya mara kwa mara baada ya muda unaleta matokeo makubwa.

    Katika andiko linalofuata tutaona dhana ya saa elfu kumi kwa undani zaidi na jinsi ambavyo unaweza kuitumia hii dhana kwa manufaa makubwa kwako.

  • Njia nzuri ya kuwaambia watu wakulipe katika kipindi hiki ambacho gharama za miamala zimeongezeka

    Nakumbuka mwaka juzi baada ya kuwewa kwa tozo za miamala kwa njia ya simu niliandika makala moja ndefu sana kuhusiana na namna ambavyo tungeweza kukabialiana na hiyo hali kwa ustadi zaidi.  Utakumbuka kwenye hiyo makala nilieleza wazi kuwa moja ya eneo ambalo tunapaswa kulitumia vizuri kwenye kuweka akiba katika kipindi hicho ambacho miamala ya simu ilikuwa imeongezewa tozo ilikuwa ni benki. Sasa hivi ninapoandika hapa, benki nako kuna makato, sasa swali ni je, wapi tena tuweke  fedha yetu. Malipo yetu yafanyikeje katika kipindi hiki.

    Kabla sijaandika sana kabisa, ningependa kusisitiza jambo moja tu. Ni ukweli kutuma au kupokea fedha kwa njia ya benki au simu hakutakwepeka kwa asilimia 100. Na njia ambayo ninakuelekeza leo, inafanya kazi sanasana  kama mtu anakutumia hela na wewe huna shida nayo ya haraka. Ila kama fedha hiyo unaihitji kuitumia leo au kesho, basi njia hii haitakufaa kiviile, katika mazingira kama hayo, benki au miamala ya simu ndiyo utalazimika kutumia. Ila siyo vibaya ukiifahamu hii njia, ninaamini muamala mmoja mmoja unaweza kuamua kuwa utumwe huku.

    Na njia hii ninayoiongelea ni mtu kukuwekea fedha zako kwenye akautni za uwekezaji za UTT

    Kwa yule ambaye hajui UTT AMIS ni taasisi ya kiserikali iliyo chini ya wizara ya fedha.Kazi kubwa ya taasisi hii ni kukusanya fedha za watu wenye mitaji midogo na mikubwa, kisha kuwekeza fedha hizi kwa niaba ya hao watu.

    Faida yote inayopatikana kwenye uwekezaji huu, inakuwa ni faida ya wawekezaji husika.

    Katika hali ya tozo ambayo tunapitia kwa sasa, tumefikia hatua ambapo mtu utahitaji kuwekeka fedha zako huku. Kwa nini

    Kwanza kama mtu anakuwekea fedha huku makato ni madogo wakati anakuwekea, makato ni ya mtandao wa simu husika na wala hata hakuna tozo za serikali.

    Pili ni kuwa fedha yako ikikaa huku inapata ongezeko la thamani. Ikumbukwe kuwa fedha yako unayopaswa kuiweka huku ni ile fedha ambayo huihitaji kwa haraka. Kwa hiyo, kama ambavyo huwa tunawaambia watu watuwekee fedha benki, tunaweza kuwaambia pia watu watuwekee fedha kwenye akaunti zetu za  UTT na fedha zetu zikakaa huko.

    Lakini pia ni sehemu salama. Kama nilivyokudokeza hapo mwanzo UTTAMIS ni ni taasisi ya kiserikali iliyochini ya wizara ya fedha. Hivyo, usalama wa fedha yako ni mkubwa sana

    Ni sehemu ambayo inakuwezesha kuweka kiwago cha chini kuanzia elfu tano. Hii inategemea na aina ya mfuko ambao unakuwa umechagua, ila kwa aina nyingi ya mifuko ya UTT unaweza kuweka akiba kwa kiwango cha chini cha elfu tano tu

    Ni akaunti pekee ambayo ukitaka kuangalia salio haukatwi. Utt wana mfumo wao wa kukusaidia wewe kuangalia salio ambapo ukitaka kuangalia salio unatuma ujumbe kwenda uwekezaji@utt.co.tz bila gharama yoyote ile na unaambiwa taarifa zako za uwekezaji bila kukatwa gharama yoyote ile

    Kwa hiyo rafiki yangu, kama kuna malipo ambayo unapaswa kulipwa ila fedha yake huihitaji kwa haraka, basi waambie watu wakulipe kupitia UTT.

    @songambele

  • Sehemu sahihi ya kuweka akiba yako

    Jana kwa nyakati tofauti watu watatu walinipigia na kuniuliza swali ambalo kwangu lilikuwa ni kama swali moja tu. japo kila mtu alikuwa na namna yake ya kulitoa hilo swali, ila kilichonishangaza ni kuwa hilo swali lilikuwa  na vipande vitatu muhimu ambavyo vinafanana.

    • Kwanza kila mtu alitaka kuweka akiba sehemu nzuri
    • Sehemu ambayo haina makato
    • Sehemu ambapo ataweka kwa muda mrefu
    • Sehemu ambapo atapata fedha yake ikiwa imeongezeka zaidi ya alivyoiweka mwanzoni

    Sasa watu hawa watatu wamenifumbua macho na kunionesha kuwa pengine na wewe ungependa kuijua sehemu ya aina hii. Ndio maana siku ya leo nimeona, siyo vibaya, wacha nikuandalie makala ya kina inayoeleza hili suala ili na wewe uweze kuliewa.

    Kwanza unaweza kuwa unajiuliza, hivi kweli sehemu ya aina hiyo ipo kweli?

    Yaani, kwamba ipo sehemu ambapo unaweza unaweza ukaweka akiba yako kwa usalama, haina makato kwa kipindi chote ambacho umeweka akiba, na baadaye ukataka kuitoa, ukaitoa ikiwa imeongezeka zaidi ya vile ulivyokuwa umeiweka? Sehemu ya aina hii ipo kweli?

    Jibu ni ndio sehemu ya aina hii ipo ila haiwezi kuwa benki. Kwa sababu benki mara zote kwenye akaunti yako huwa kuna makato pale unapoweka fedha yako, benki huwa wanakukata kukutunzia fedha yako. Kwa hiyo sehemu ya aina hii haiwezi kuwa benki.

    Lakini kabla hujazilaani benki, naomba unielewe kwa kitu kimoja kwanza na cha msingi sana. Mimi nina akaunti ya NMB, kama sijakosea akaunti hii inaitwa akaunti ya mwanachuo au akaunti ya mwanafunzi. Kwenye akaunti hii huwa hawakati fedha pale unapoweka fedha  yako huku. Fedha yako huwa inaendelea kubaki kama ilivyo hata kama ikikaa kwa muda mrefu, labda makato ni pale tu ambapo huwa natoa fedha. Labda kama sera za uendeshaji wa akaunti hii zimebadilika. Ila kama hazijabadilika, basi hii inaweza kuwa akaunti nzuri kwako. ubora ni kwamba NMB wanaruhusu ufungue akaunti hii hata kama wewe siyo mwanafunzi.

    Lengo lao ni kusaidia watu kujijengea utaratibu wa kujiwekea akiba. Na mimi nawaunga mkono. Kwa nini? kwa sababu tafiti nyingi zimeonesha kuwa watu wenye akaunti ya benki, walau huwa wanajiwekea akiba ukilinganisha na watu ambao hawana akaunti ya benki. Sasa kama wewe hauna akaunti ya benki, nadhani unaweza usiwe na akiba yoyote ile mfukoni, au uongo?

    Enewei, tuachane na hilo, maana tangu mwanzo niliahidi kukwambia eneo unapwoeza kuweka akiba na baadaye ukaitoa ikiwa imeongezeka ila siyo benki. Halafu eti bado naendelea kuongelea masuala ya benki…

    Sasa baada ya kusema hayo, naomba tuone eneo ambapo

    • unaweza kuweka fedha yako,
    • Sehemu ambapo hakuna makato
    • Sehemu ambapo utaweka kwa muda mrefu
    • Sehemu ambapo utapata fedha yake ikiwa imeongezeka zaidi ya ulivyoiweka mwanzoni

    Hiki ni kitabu kizuri sana ambacho unapaswa kusoma. Gharama yake ni elfu tano tu.

    Walau sehemu hii siyo benki.

    Sehemu yenyewe ni kwenye akaunti za uwekezaji wa pamoja za UTT

    UTT ni taasisi ya kiserikali iliyochini ya wizara ya fedha ambayo inawakutanisha wawekezaji wote wenye mitaji midogo na mikubwa na kuwasaidia kuikusanya hiyo mitaji, kisha kuiwekeza sehemu salama.

    UTT imekuwa inafanya kazi hapa nchini karibia mwaka 20 sasa, ila cha kushangaza watanzania wengi hawana uelewa juu ya UTT na hata wengine hawajawahi kusikia habari za UTT.

    Ukiweka fedha yako UTT inakuwa sehemu salama, maana fedha yako zinakuwa chini ya taasisi ya kiserikali, lakini sambamba na hilo fedha yako inakuwa chini ya watalaamu ambao wataiwekeza sehemu salama ambazo wao wanajua. Kitu hiki kinafanya uwekezaji wako unakuwa salama na hata baadaye uwekezaji unakuja ukiwa na mrejesho mzuri.

    UTT AMIS kama inavyofahamika, ina mifuko sita ya uwekezaji ndani yake. Mifuko hii imeanzishwa kwa dhana na malengo tofauti kulingana na aina ya mfuko.

    Mfano mfuko wa umoja ambao pia ni mfuko mkongwe kwenye mifuko yote ya UTT, Ebu angalia picha hiyo  hapo chini

    Mfuko mwingine ni mfuko wa ukwasi ambao maelezo yake ya mafupi haya hapa

    Kwa kuwa hii makala lengo lake siyo kueleza mifuko yote ya utt kwa undani, nimedokeza hiyo mifuko mwili tu kwa kuwa ndiyo nataka kuiongelea zaidi kwenye makala ya leo.

    Kwa hiyo, kama una fedha zako na ungependa kuiwekekeza basi nashauri uweze kuiweka kwenye mfuko mmojawapo hapoo juu. Aidha mfuko wa umoja au mfuko wa ukwasi.

    Ukiweka fedha yako kwenye mfuko mmojawapo hapo juu, ni uhakika kuwa baada ya muda fedha yako itakuwa imeongezeka, maana mifuko hii imekuwa na mrejesho mzuri kila mwaka. Ambapo kwa wastani tangu kila mfuko umeanzishwa umekuwa na mrejesho wa asilimia 13.5. Hii maana yake kwamba ukiweka fedha yako huku, kwa kila kiasi ambacho utaweka huku, unapata ongezeko la silimia 13.5.

    Ikumbukwe kwamba huo ni wastani. Hii ndio kusema kwamba kuna miaka ambapo uwekezaji huo unaweza kuwa juu kama ulivyoona hapo juu. Na kuna miaka ambapo mrejesho huu unaweza kuwa chini.

    Kwa hiyo rafiki yangu, kwa kuwa leo nilitaka kukwambia sehemu nzuri ya kuwekeza fedha yako, basi naona lengo lengu kama nimeweza kulifikia.

    Kazi yako ya fuanya siku ya leo.

    Nenda kafungue akaunti ya Utt, ubora ni kuwa unaweza kufungua akaunti hata kwa simu yako.

    Bonyeza *150*82# uanze kufanya hivyo.

    Au unaweza kufungua akaunti kupitia aplikesheni yao iliyo kwenye playstore. Inaitwa UTT AMIS

    Kwa maelezo zaidi ya ndani kabisa, nashauri uweze kupata ebook yangu inayoitwa MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE pamoja na ebook nyingine inayoitwa MAAJABU YA KUWEKA AKIBA. Hizi ebooks hizi zitakufaa sana rafiki yangu.

    Kila ebook gharama yake ni 5,000/- tu. Ona huyu mwenzako aliyekisoma hapa anavyosema

  • Uchambuzi wako pendwa umesomwa kwa sauti (Kitabu cha how to stop worring and start living)

    Wiki hii kweney blogu ya songambele tumefanya uchambuzi wa kitabu c ha How to stop worrying and start living. ni uchambuzi ambao umesomwa na watu wengi na wengi wameupenda. kutokana na hilo tumeona ni vyema ukasomwa kwa sauti, na hiki kitu ndicho kimenisukuma niulete hapa siku ya leo.

    huu hapa chini ndio uchambuzi wa kitabu cha How to stop Worrying and start living

  • Mtazamo mzuri kuhusu intaneti

  • Vitu Vitano Vitakavyokuzuia wewe kufanikisha malengo yako

    Siku siyo nyingi nilipokea ujumbe kutoka kwa mmoja wa watu wanaofuatilia kazi zangu mtandaoni. Kitu kikubwa sana ambacho aliweza kuniambia ni kuwa anapata changamoto hasa anapoweka malengo, anashangaa siku zinaenda ila hayo malengo yake hayatimiii.

    Sasa siku ya leo kwa namna ya kipekee ningependa kumjibu huyu rafiki pamoja na watu wengine wengi ambao wanawakuwa na shida kama hii hapa ili sote kwa pamoja tukitoka hapa twenda kufanyia kazi malengo yetu kwa manufaa na kwa namna ambayo ni bora zaidi.

    Kabla sijaingia ndani zaidi, ningependa sana kukwambia kuwa karibia kila mwanzoni mwa mwaka watu wengi huwa wanaweka malengo makubwa ambayo watayafanyia kazi ndani ya mwaka huo, ila cha kushangaza ni kuwa mpaka kufikia tarehe 19 januari watu wengi huwa wamesahau malengo yao, na wachahe ambao huwa wanaendekea kukumbuka malengo ndio huweza kuendelea nayo mbele kidogo huku wachache zaidi wakiwa ndio wanafikia malengo yao. Sasa swali kubwa sana ambalo mtu unaweza kujiuliza ni kwa nini?

    Jibu ni kwamba ule mkumbo na motisha ya tarehe moja vinakuwa vimeisha. Mwanzoni unapokweka malengo unakuwa na motisha kubwa, ila kadiri siku zinavyokuwa zinazidi kwenda, ile motisha inapotea, sasa watu huwa wanaishia hapo. ila sasa wewe haupaswi kuishia hapo, baadala yake unapaswa kuendelea kujisukuma zaidi ili uweze kufika kule unapotaka kufika. Na utaweza hili kama utajiwekea utaratibu wa kuwa unajikumbusha malengo yako karibia kila siku. Kila siku hakikisha kwamba unaandika chini malengo yako ambayo unayafanyia kazi, ili usiyasahau.

    Pili, usisubiri mpaka uwe kila kitu ili ufanyie kazi malengo yako. Kuna watu wanaweka malengo mazuri tu, ila kinachowafanya washindwe kuweza kufanyia kazi malengo yao na kuyatimiza ni kwa sababu wanasubiri mpaka wawe na kila kitu ili waje kufanyia kazi malengo yao. Naomba unisikilize kwa kitu, huhitaji kuwa na kila kitu ili uwezer kufanyia kazi malengo yako. Anza na kile ulichonacho, fanya kile kinachowezekana, mwisho wa siku utajikuta kuwa umeweza kufanya yasiyowezekana.

    Tatu, usisubiri mpaka tarehe 31 disemba ili ufanyie kazi malengo yako. Wengine wanaweka malengo makubwa ila wanasubiri mwisho wa mwaka ili malengo yao hayo yaweze kutimia. Unachopaswa kufahamu ni kuwa malengo makubwa huwa hayatimii mwishoni mwa mwaka. Hivyo, badala ya wewe kusubiri mpaka mwisho wa mwaka ili uweze kutimiza malengo yako, anza kuyafanyia kazi siku ya leo hata kama ni kwa udogo.

    Nne,  watu waliokuzunguka. Moja kati ya usemi wenye ukweli mkubwa sana ndani yake ni usemi kuwa miaka mitano ijayo utakuwa jisnsi ulivyo isipokuwa kwa vitu viwili tu, watu waliokuzunguka na vitabu unavyosoma. Rafiki yangu, kama kuna kitu unahitaji sana ili kuweza kufikia malengo yako basi ni watu, hakikisha kwamba unazungukwa na watu ambao ni chanya na wale ambao wanaendana na malengo yako.

    Watu ambao ni hasi watakufanya ukwame na ushindwe kuweza kufkia malengo yako.

    Tano, kuweka malengo madogo sana. malengo madogo yanakunyima hamasa na yanakufanya ushidnwe kusonga mbele ila malengo makubwa yanakupa msukumo wa kufanya makubwa na kujisukuma zaidi. hivyo basi rafiki yangu nakushauri sana uweke malengo makubwa na kila mara uhakikishe  kwamba unajisikuma kwenye kuyafanyia kazi na kuyatimiza. Kamwe usirudi nyuma kwenye kufanyia kazi malengo yako.

    Kil la kheri

    Umakuwa nami rafiki yako wa ukweli

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

  • Uchambuzi Wa Kitabu: How To Stop Worrying and Start Living

    NB: kusikiliza makala hii kwa njia ya sauti. Bonyeza hapa

    Kitabu: How To Stop Worrying and Start Living

    Mwandishi: Dale Carnegie

    Mchambuzi: Hillary Mrosso

    Simu: +255 683 862 481

    Utangulizi

    Jina la kitabu hiki lenye maana ya Namna ya kuachana na hofu na kuanza kuishi. Ni kitabu bora sana kinachoelezea namna ya kukabiliana na hofu kwenye maisha yetu ya kila siku. Hofu imewalaza wengi katika vitanda vya hosipitali, hofu imewanyang’anya wengi afya, furaha, amani, utajiri, na fedha nk. Mwandishi wa kitabu hiki ametumia muda mwigi sana kufanya utafiti wa kina kwenye maisha ya watu wengi waliopitia nyakati ngumu zilizotawaliwa na hofu na kupata maoni yao na ndio kwa kiasi kikubwa yametumika katika uandishi wa kitabu hiki. Hiki ni moja ya vitabu bora sana kwa binadamu yoyote, hupaswi kabisa kukosa kusoma kitabu hiki, ni kama dawa na kinga endapo utayatumia yaliyoandikwa humu kukutoa kwenye aina zote za hofu ulizo nazo. Karibu kwenye uchambuzi huu muhimu.

    1. Kitabu hiki kinawafaa zaidi wale ambao wapo tayari kutekeleza yaliyoandikwa katika kitabu hiki, hii ndio faida na lengo la uandishi wa kitabu hiki, sio kwa ajili ya kujifurahisha na kufurahia namna kilivyoandikwa, ni kitabu kinachodai zaidi utekelezaji.

    2. Mwandishi wa kitabu hiki anasema, soma kurasa 40 za mwanzo za kitabu hiki, na endapo hutapata chochote cha kukusaidia kukabiliana na hofu ulizo nazo, basi, unachotakiwa kufanya ni kukitupa au kukichoma kitabu hiki.

    3. Maisha yetu ya baadaye yatakuwa bora kwa kufanya yale yaliyopo kwenye siku yetu ya leo, usifanye mambo ya kesho leo wala usifanye mambo ya jana kesho, wekeza kwenye kufanya yaliyopo kwenye siku yako.

    4. Mwandishi Dale Carnegie anasema tukumbuke moja ya maombi ambayo Yesu Kristo aliwafundisha wanafunzi wake, aliwaambia waombe mkate wa siku, na sio mkate wa kesho au jana, au mwezi ujao.

    5. Mkate wa siku hiyo ndio wa muhimu zaidi, maana yake kila siku ina mambo yake, huenda kesho usihitaji mkate ukahitaji kitu kingine, Mungu anakupa kile unachokihitaji sasa, yaani leo na sio unachokihitaji kesho au jana.

    6. Katika moja ya mafunzo muhimu Yesu Kristo aliyowafundisha wanafunzi wake ni kuacha kujisumbua au kuhangaika kwa ajili ya mambo ya kesho, aliwaambia iacheni kesho ijisumbukie yenyewe.

    7. Usighairishe mambo ya leo kwa kuhofia utaishije kesho, kesho ina mambo mengi na kuna mengi hutaweza kuyathibiti hivyo wekeza nguvu zako kufanya yale yaliyomo mbele yako, mbele ya siku yako, hii ndio njia nzuri ya kuondoa hofu kwenye maisha yako.

    8. Kuwa na mawazo mazuri kuhusu siku yako, itakufanya uipangilie na kufanya yote kwa ufanisi, mawazo mabaya yanaleta hofu na msongo wa mawazo ambao hupelekea kuairisha mambo muhimu ka kuhofia mambo usiyoyajua na usiyo na ukakika nayo.

    9. Ili maisha yetu yawe bora, tunahitaji siku moja bora, ili tuweze kufanya yote yaliyo bora kwenye siku hiyo. Siku zote jifunze jambo hilo, unahitaji siku moja tu.

    10. Andika hii sentensi kwenye karatasi na uibandike ofisini kwako au nyumbani kuwa, unahitaji siku moja tu kufanya makubwa. Siku moja, ukiipata siku hii moja fanya makubwa na ya muhimu kwenye siku hiyo.

    11. Fanya jambo moja kwa wakati, hatua moja kwa wakati hii dhana itakusaidia sana kuwa mwenye ufanisi unapofanya mambo muhimu kwenye siku yako.

    12. Epuka kuwa na mrundikano wa mawazo, au majukumu mengi ndani ya siku yako, maana hayo yatakufanya ushindwe kuianza siku yako kwa ushindi na pia yanaweza kukukatisha tamaa na utaishia kuchanganyikiwa na kukosa cha kufanya hii itapelekea uanze kuwa na hofu.

    13. Ukweli ni kwamba nusu ya vitanda vya hosipitalini vimetengwa kwa ajili ya wagonjwa hofu, ambao neva za miili yao zimeharibika kwa hofu waliyoitengeneza kwenye maisha yao kwa kuhofia mambo ya jana na kuwa na mashaka na kesho wasiyoijua.

    14. Panga kuishi maisha yako kikamilifu ndani ya siku moja, achana na usiyoyajua kuhusu kesho, achana na kujibebesha mizigo ya mambo yaliyokwisha kupita.

    15. Jifanyie wepesi kwenye maisha yako, amua kuishi maisha marefu kwa kuondoa hofu kwenye maisha yako, hofu inafupisha sana siku zako za kuishi, inakufanya uonekane mnyonge muda wote hofu ni mbaya jamani.

    16. Hadi unapofikia wakati wa kulala usibebe mzingo wowote wa madeni, hofu, chuki, uchungu, hasira kwnda nao kitandani, achilia, samehe, na ingia kitandani ukiwa mwepesi na ukilala usingizi wako utakuwa kama wa mtoto mchanga.

    17. Jikumbushe kila siku unapoianza siku yako, jiambie maneno haya, “wacha niishi siku hii moja tu vizuri”, jiambie hivyo kila siku. Kwa kufanya hivyo utawekeza nguvu zako zote kwenye kuifanya siku yako kuwa bora sana, na hatimaye maisha yako ya sasa na ya baadaye yatakuwa bora.

    18. Moja ya asili ya binadamu ni kughairisha kuishi, na kuanza kufikiria vitu ambavyo hata havipo kabisa, wengi wanaghairisha furaha, amani, upendo au mambo muhimu yaliyopo mbele yao na kuanza kufikiria vitu ambavyo hata havipo.

    19. Maisha ni yako, shughulika na yako, acha kutoroka maisha yako, maisha yako ni jukumu lako, yafanye maisha yako kuwa yenye furaha, amani na upendo wakati wote, uwezo huo unao.

    20. Mambo ya leo ndio muhimu, usiache kuishi sasa na kuanza kutatua matatizo ya kesho ambayo hujui itakujaje.

    21. Ifurahie siku yako, na panga kufanya makubwa uwezavyo ndani ya siku hiyo, Carpe diem. “Enjoy the day.” 

    22. Fanya kama mtunga zaburi aliyosema, Hii ndio siku aliyoifanya Bwana, tutaifurahia na kuishangilia. Hakusema hizi ndizo siku, au hii ndio kesho au jana aliyoifanya Bwana, alisema hii ndio SIKU aliyoifanya Bwana.

    23. Unapoamua kukabiliana na hofu zilizoko kwenye maisha yako, jiambie bila kuogopa, na agalia hali zote unazoweza kukabiliana na hofu hizo bila kujali. Unaweza kujiambia endapo nitafanya jambo hili ninalolihofia nitaenda jela? Au nitakufa?

    24. Pambanua kwa undani bila mashaka yoyote endapo utafanya unachohofia, ni kitu gani kibaya sana kitatokea kwenye maisha yako, ni kifo, au utaenda jela au ni nini kitatokea, ukiona hakuna kibaya basi acha kuogopa na ufanye jambo hilo.

    25. Unapodhamiria kufanya jambo muhimu kwenye maisha yako usiache hofu zikakuzuia kufanya, jifanyie tathimini fupi ya faida na hasara kisha chukua hatua sahihi.

    26. Mara kwa mara jiulize swali, kuna faida gani kwenye haya ninayoyaogopa? Hii hofu inanisaidia nini? Fikiria na chukua hatua mara moja uachane na hofu zinazokusumbua.

    27. Hofu inadumaza na kutufanya tushindwe kuchukua hatua kwenye maisha yetu, hofu zinaturudisha sana nyuma, amua kuondoka kwenye hofu uishi maisha yenye furaha na afya tele.

    28. Hofu nyingi tulizonazo zitapungua endapo tutajua uhalisia wa jambo na kukubaliana na matokeo yake. Wengi wamelimbikiza hofu zinazowaua taratibu kwa kushindwa kukubaliana na uhalisia wa mambo.

    29. Usipokuwa tayari kukubaliana na uhalisia ulivyo, siku zote utaishi kwenye hofu, mashaka, hasira, chuki na magojwa yatakuandama.

    30. Wachina wana msemo wao wa ajabu sana, wanasema amani ya moyo unaipata pale unapokubaliana na yaliyokwisha kutokea. Kama mambo yameshatokea huna unachoweza kufanya tena zaidi ya kukubaliana na matokeo yake.

    31. Wengi wameingia kwenye hofu kwasababu wameshindwa kukubali matokeo, na wanatumia muda mwingi, nguvu, na hisia zao kufikiria mambo yaliyopita. Hii ikiendelea ilaleta hofu, uchungu na hasira.

    32. Kubaliana na mabaya yaliyokwishatokea au ambayo hayajatokea, hii inatakufanya uishi kwa amani, tegemea mabaya yanaweza kutokea kwako au kwa mtu mwingine, hivyo usiogope maana kwa kuogopa au kuwa na hofu hutabadili chochote.

    33. Namna nzuri ya kukabiliana na kupanda au kushuka kwa sukari mwilini mwako ni kuwa tayari kuyapokea yote yatakayokuja kwenye maisha yako, haijalishi ni mazuri au ni mabaya, yapokee kama yalivyo, kwa kufanya hivyo utalinda afya yako na mwili wako.

    34. Kama wewe ni mfanyabiashara na hujui kupambana na hofu, unaweza kufa mapema. Kwenye biashara kuna mengi yasiyotarajiwa, hata ujiandae vipi, lazima kuna mengine yatakuja tu kukushangaza, hivyo kama wewe ni mtu wa hofu unaweza usifanikiwe na ukafa mapema.

    35. Mwandishi Dale anasema, asilimia 70 ya wagonjwa wanaoenda kumuona daktari wanaweza kupona maradhi na magonjwa yao endapo watakaa mbali na hofu na mashaka.

    36. Hofu na mashaka zinafanya mfumo wa neva za miili yetu kushindwa kufanya kazi vizuri, hivyo kupelekea madhara kwenye mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kusababisha neva za tumbo kupeleka taarifa za uzalishaji mwingi wa acidi ambazo huleta madhara kama vidonda ya tumbo.

    37. Mwandishi anasema, taarifa za kitabibu zinaonyesha wengi wenye vidonda vya tumbo ni kwasababu ya hofu na mashaka waliyo nayo kwenye maisha yao. Hivyo wengi wanaweza kupona au kutoingia kwenye madhara ya kupata magonjwa hayo kwa kuziepuka hofu.

    38. Hofu pia zinazalisha msongo wa mawazo ambao pia una madhara kwenye mwili wa binadamu kama vile kusababisha vidonda vya tumbo.

    39. Daktari Joseph Montague anasema, hatupati vidonda vya tumbo kwa vyakula tunavyokula, tunapata vidonda vya tumbo kwa vile vinavyotula. Anamaanisha sio aina ya vyakula ndio huleta vidonda vya tumbo, bali vidonda vya tumbo vinatokana na vile vinavyotula.

    40. Utafiti wa gazeti la Life magazine nchini Marekani unaonyesha kuwa, hofu, mashaka, uchoyo uliopitiliza, chuki na kushindwa kukubaliana na uhalisia wa mambo vimekuwa ndio chanzo kikuu cha vidonda vya tumbo, na vidonda vya tumbo vinaripotiwa kuwa moja ya janga kubwa linaliua watu watu duniani.

    41. Madakari bingwa kutoka katika kitengo cha hosipitali ya Mayo nchini Marekani wanasema nusu ya vitanda vya hosipitali vimejaa wagonjwa ambao wana matatizo ya neva. Matatizo ya neva huathiri utendaji kazi wa sehemu kubwa ya mwili, na kwa kiasi kikubwa husababishwa na hofu.

    42. Matatizo hayo ya neva sio kwamba yanasababishwa na neva kuharibika kutokana na michubuko ya nje, bali ni kutokana na hisia za kuchanganyikiwa, hofu, huzuni, hasira, kushindwa na kukata tamaa.

    43. Mwanafalsafa maarufu sana duniani Plato aliwahi kusema, madaktari wanakosea sana pale wanapojaribu kutibu mwili bila kutibu nafsi, ambayo imebeba hisia zote za mtu kama vile hisia za chuki, furaha, hasira, hofu nk. Huweze kutengenisha kutibu mwili pekee bila kutibu na eneo lake muhimu la hisiaa.

    44. Ni ukweli sayani ya utabibu imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutibu na kuondoa kabisa magonjwa mabaya kwa binadamu kama vile, surua, pepopunda, kipindupindu, ugonjwa wa manjano, malaria nk. Ambayo yalipeleka watu wengi kaburini.

    45. Hata hivyo, sayansi ya udakatri bado inakabiliwa na changamoto sana katika kutatua changamoto za magojwa ya kiakili, hisia, hofu, chuki, na msongo wa mawazo ambayo kwa kiasi kikubwa yanawasumbua sana watu wengi.

    46. Taarifa za kitabibu kutoka nchini Marekeni zinaonyesha kuwa mtu mmoja kati ya watu 20 anatatizo la kiakili, ambalo limechangiwa na msongo wa mawazo na hofu.

    47. Tafiti nyingine kuhusu afya ya akili zinaonyesha mtu mmoja kati ya sita walioitwa kwa ajili ya kushiriki kwenye vita ya pili ya dunia alikataliwa kutokana na matatizo ya kiakili. Matatizo haya ya kiakili kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na hisia za hofu na mashaka

    48. Kama unakabiliwa na nyakati ngumu kwenye maisha yako, ushauri ni kwamba usichukue nyakati ngumu ukazipeleka kwenye mfumo wako wa upumuaji au hisia, ukifanya hivyo utafupisha maisha yako.

    49. Utafiti wa Dkt. Wiliamu McGonigle kutoka taasisi ya meno nchini Marekani unaonyesha kuwa hofu na mashaka yanasababisha meno kuoza, hii ni kutokana na hisia mbaya za hofu na mashaka zina haribu uwiano wa mfumo wa madini ya Calciam mwilini na hivyo kusababisha meno kuoza.

    50. Hofu inaharibu hata mwonekano wako wa nje, hofu inaweza kukujengea muonekano usiovutia kabisa, ukaonekana wa ajabu, ukaonekana mzee kumbe ni kijana.

    51. Hakuna kitu kinaharibu mwonekano wako wa nje haraka kama hofu, mwonekano wako wa nje una maana sana kwenye maisha yako, hivyo usikubali uharibiwe kwa hofu.

    52. Hofu inakufanya ujioni mkosaji, hufai, hustahili na inakufanya ujione unaonewa, hofu inakujengea picha na taswira ambazo hazina uhalisia wowote.

    53. Ukiruhusu tu hofu kwenye maisha yako, ujue umeruhusu pia majirani zake wa karibu ambao ni vidonda vya tumbo na matatizo ya moyo kama shinikizo la damu nk.

    54. Hofu inaharibu nywele zako, zinaweza kupoteza rangi yake ya asili, hofu inaweza kufanya hata nywele zako za kichwani kupotea au kushindwa kuota.

    55. Hofu inaweza kukuletea magonjwa ya ngozi, inaweza kubadili hata rangi ya ngozi ya mwili wako, inafanya ngozi kusinyaa na kusababisha vipele majipu na muwasho.

    56. Unapokuwa na hofu huwezi kuzalisha chochote, zaidi sana utajiletea madhara makubwa yatakayokugharimu uhai, kama vile magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo.

    57. Hofu ni kama dripu za maji ya matone, ukiiruhusu inakutafuna hadi unaishia kujiua au kukufanya kuwa kichaa. Usiruhusu hofu kwenye maisha yako.

    58. Changamka na uwe mtu wa furaha, hii itaongeza kinga za mwili wako na kuimarisha afya ya mifupa yako, kumbuka mifupa yako inaweza kuharibika kwasababu ya hofu, hivyo ukaishia kupata kansa.

    59. Mwandishi Dale Carnegie anasema nusu ya majanga ya hofu yanayowapata watu ni kwasababu wanafanya maamuzi bila kuwa na taarifa za kutosha kuhusu jambo fulani.

    60. Tafuta taarifa za kweli kuhusu kinachokutia hofu, kwa kufanya hivyo utakuwa umetatua sehemu kubwa ya tatizo linalokusibu.

    61. Kuwa na utaratibu wako wa kuandika kila changamoto unayoipitia, pia ainisha njia utakazotumia kukabiliana na hiyo changamoto, fikiria unachoweza kufanya kuitatua changamoto hiyo na kisha chukua hatua mara moja.

    62. Jinsi unavyojikita kwenye kufanya majukumu yako kila siku ndivyo unavyoachana na hofu. Hofu inatabia ya kumtawala na kumtesa mtu ambaye hana cha kufanya kutwa nzima amekaa tu au amelala tu bila kufanya jambo lolote.

    63. Mfano, kama unasumbuliwa na hofu sana, nenda shambani, tengeneza bustani, nenda kwenye mazoezi, au nenda ukacheze mziki hii itakufanya uache kuwaza kuhusu hofu, (occupational therapy).

    64. Tafuta wastani wa jambo unaloliogopa kwamba litatokea kwenye maisha yako, mfano kama unaogopa kusafiri kwasababu kuna ajali, basi tafuta wastani wa magari yote yanayosafiri kisha angalia yanayopata ajali ni mangapi angalia wastani, ukiona ni mdogo, usiogope kuchukua hatua.

    65. Changaoto hazitufanyi kuwa na furaha au kutokuwa na furaha, ni jinsi tunavyozichukulia ndio huamua hisia zetu kwenye hizo changamoto.

    66. Bwana Yesu aliwahi kusema, Ufalme wa Mungu upo ndani yetu, hivyo ufalme wa shetani unaweza kuwa ndani yetu pia. Maana yake kama wema unakaa ndani yetu hata ubaya unaweza kukaa ndani yetu, hivyo wema na ubaya kukaa ndani yetu ni kutegemeana na maamuzi tunayoamua.

    67. Binadamu ni viumbe wa ajabu sana, wanaweza kubeba majanga, kushindwa na hata mambo machungu sana, hivyo pia anaweza kubeba ushindi furaha, amani na mafanikio. Tumeumbwa na uwezo mkubwa sana wa kuweza kupitia kila hali kwenye maisha haya, tuna uwezo kuliko tunavyodhani.

    68. Henry Ford aliwahi kusema kauli moja nzuri sana kuhusu mambo yanayotushinda maishani, alisema kama huwezi kukabiliana na jambo fulani ana achana nalo. Maana yake kama kuna jambo huwezi kulibeba kwenye maisha yako liache lijibebe lenyewe.

    69. Kuna mambo yapo kabisa nje ya uwezo wetu kama binadamu na hatuwezi kuyaathiri kwa namna yoyote ile, tutayaacha tu yatokee kama yaliyo. Ukitambua hilo hutakuwa na hofu na mashaka kwenye baadhi ya mambo, utakuwa na amani na utulivu.

    70. Mwanafalsafa mashughuri wa Roma, Epictatus aliwahi kusema, njia moja ya kuwa na furaha ni kuacha kuhofu na kuogopa vitu ambavyo vipo nje ya uwezo, au nguvu zetu kuvikabili.

    71. Kuna nguvu kubwa tunaipata pale tunakubali kuwa kwenye maisha kuna vitu vipo nje ya uwezo wetu kuvikabili, kuna vitu hatuna nguvu ya kuvifanyia chochote au kuviamulia, vipo nje ya uwezo wetu.

    72. Tunatakiwa kujua wakati wa kuwa chini na kuinama kuruhusu mengine yapite, hatuna nguvu za kukabiliana na kila kinachokuja mbele yetu, tukiwa wakaidi tunavujika, tujifunze kwa minazi na miti mingine.

    73. Mfano, miti na misitu minene iliyositawi inajua kanuni hii ya maisha, inajua lazima upepo uje na haiwezi kushindana na upepo maana vinaweza kuvunjika, hivyo hukunja matawi yake, huinama na kusujudu ili upepo upite zake.

    74. Tukubali kuomba Mungu atujalie neema ya kukubali vitu ambavyo hatuwezi kuvibadili, na kibali cha kubalidi yale tunayoweza kuyabadili. Na hekima ya kutambua tofauti.

    75. Tusiwe wakaidi, tunatakiwa kujifunza kushirikiana na yale yasiyoepukika kwenye maisha yetu, hii ndio siri ya furaha na kuishi maisha marefu.

    76. Usilazimishe mamba ambayo yalishatokea, usijaribu kuzoa maji yaliyokwisha mwagika. Imetokea imetokea basi, tafuta namna nyingine ya kuishi.

    77. Wacha yaliyopita yajizike yenyewe, huna cha kufanya zaidi, na endapo utayafuatilia basi ujue utapata ulichokitafuta ambacho ni hofu, sura mbaya na vidonda vya tumbo.

    78. Kumbuka, unapowachukia maadui zako maana yake unawapa nguvu juu ya amani yako, afya yako, usingizi wako, moyo wako nk.

    79. Waliokuudhi wanaweza waziwaze kabisa kuhusu wewe, wanaweza kuwa wapo sehemu wanafurahia maisha na kucheza muziki, wewe unaendelea kuumia na kutoa lawama kwao, kumbuka unajiumiza mwenyewe.

    80. Na aliyekuudhi atafurahia sana endapo atajua unaumia, unamuwaza au unamhofia kila mara. Jifunze kusamehe kwa ajili ya afya yako, nafsi yako, moyo wako, amani yako na furaha yako.

    81. Ndio maana unaona Yesu katika mafundisho yake alisema, “wapendeni adui zenu” akaendelea kusema semehe mara saba sabini, Yesu alijua njia nzuri ya kuwa na afya, furaha na amani muda wote ni kuishi kwa upendo na kusamehe.

    82. Kama utaishi na chuki, utashindwa kusamehe, basi jua hautakiwa mbali na shinikizo la damu, mashambulizi ya moyo, vidonda vya tumbo na magonjwa mengine. Jipende, samehe, achilia ishi kwa amani ukiwa na afya tele.

    83. Unajua hofu, uchungu, chuki vinatufanya tushindwe hata kufurahia chakula tunachokula, na hapo ndipo afya zetu zinapodorora.

    84. Hofu itakufanya uchoke hata kabla ya kuchoka, itakuondolea kila kitu kizuri kwenye maisha yako. Mwandishi wa kitabu hiki anasema hata kama tumeshindwa kuwapenda adui zetu, basi tujiepende wenyewe.

    85. Dale Carnegie anashauri, kabla hujalala usiku, samehe kila kitu na kila mtu, fanya hivyo maisha yako yote. Ili ulinde afya yako, amani na furaha yako.

    86. Maneno ya watu wanaokusema hayatakuvunja mifupa, jifunze kuyapuuza uendelee na maisha yako, kuna mambo mengi ya msingi unatakiwa kuyafanya kwenye maisha yako, usiwekeze kwenye maoni ya watu kuhusu wewe.

    87. Usijaribu kuwa sawa na adui yako, maana yake usiwe mtu wa visasi au ubaya, yashinde mabaya kwa mema. Usiache mabaya yakutawale ukaishia kuamua vibaya na kutengeneza hofu.

    88. Haitoshi kujisifia kuwa wewe ni mzalendo wa kweli, mzalendo wa kweli hana uchungu, visasi, chuki na wala hasira kwa mtu yeyote yule.

    89. Usiweke mategemeo kwamba kwasababu ulimsaidia mtu sana kwenye maisha yake basi atakuja kukushukuru au kukusaidia na wewe, ukiwa na mategemeo hayo unaweza kuwa mtu wa malalamiko na asiye na furaha.

    90. Ondoa mategemeo ya kusaidiwa, kusifiwa, au kupendwa ishi vizuri maisha yako bila kutegemea hayo mambo. Endapo utakuja kusaidiwa, kupendwa au kushukuriwa itakuwa ni jambo la ziada kwako, isiwe uhitaji maana ukitegemea ukikosa utaanza kutengeneza malalamiko na uchungu.

    91. Usitegemee watu watakuwa wema kwako, au watakutendea mema, wape watu nafasi kubwa ya kukosea na kukukosea hii itakufanya uwe na uwezo wa kukabiliana na kila hali kwenye maisha yako.

    92. Mwanafalsafa mahiri aliyewahi kuitawala Roma kwa mafanikio makubwa, Marcus Aurelius, aliwahi kusema, katika moja ya maandishi yake kuwa kila siku anapoamka asubuhi kwenda kazini anajiandaa kwenda kukutana na watu wachoyo, wabinafsi, wasio na shukrani, wakaidi, wenye kiburi na wakorofi. Alikuwa hashangazwi kabisa kukutana na watu hao maana bila wao hajui dunia ingekuwaje.

    93. Ndugu msomaji wa uchambuzi wa kitabu hiki, kumbuka siku zote watu wanaweza kukusahau hata kama uliokoa maisha yao kutoka kwenye kifo, wengine wanaweza wasikushukuru hata kama umewafanyia jambo zuri kiasi gani, ni asili ya binadamu, hivyo yakitokea hayo kwenye maisha yako yasikuumize kichwa kabisa.

    94. Mfano mzuri upo kwenye Biblia, Yesu aliponya vipofu 10, lakini ni mmoja tu ndio alirudi kushukuru. Jambo hili lilimfanya Yesu kuuliza nimeponya watu 10, amekuja mmoja kushukuru wengine 9 wameenda wapi? Ni asili ya binadamu kutoshukuru, ilitokea kwa Yesu, inaweza kutokea kwako pia, usishangae.

    95. Furaha na amani yako inatakiwa kutokana na wewe kuwafanyia wengine wema, na isiwe kinyume chake. Aristoto, moja ya wanafalsafa maarufu sana alinukuliwa akisema, mtu bora zaidi ni yule ambaye furaha yake ipo katika kutoa na kuwasaidia wengine na sio katika kupokea au kusaidiwa na wengine.

    96. Kama tunatafuta furaha kwenye maisha yetu tunatakiwa kujua, furha ya kweli ipo katika utoaji na sio upokeaje, hivyo tuache kabisa kutegemea shukrani au mema kutoka kwa wengine.

    97. Kuna wazazi wanapata shida sana, presha zao ziko juu, vichwa vinawauma kwa sababu walizaa watoto na kuwafanyia makubwa kwa mategemeo kuwa watoto hao watakuja kurudisha fadhila kwa wazazi wao au walezi wao. Kumbuka mfano wa Yesu Inaweza isiwe hivyo mara zote.

    98. Hapa simaanishi hatutakiwi kuwa watu wa shukrani, la hasha! Tunatakiwa kuwa wakarimu na kuwaonyesha wazazi wetu upendo, shukrani na fadhila. Lakini vitu hivyo visipotokea isiwe ndio wapandwe na hasira na kuishia kuwa na chuki.

    99. Kama tunataka kuwa na watoto wenye shukrani, wakarimu, tunatakiwa kuwa hivyo sisi wenyewe kama wazazi.

    100. Njia nyingine ya kuiua tabia ya hofu na mashaka ni kuhesabu baraka zako, angalia uliyonayo na sio yale ambayo huna, angalia faida na sio hasara, angalia suluhu na sio matatizo.

    101. Hofu inaweza kufa kabisa kwenye maisha yako endapo utajenga uhusiano mzuri na Mungu, hapa inabidi uwe mtu wa imani, fanya sala, maombi na shukrani kwa Mungu wako.

    102. Mahatma Ghandh, moja ya mtu mashughuri sana na baba wa taifa la India, alipigana vita vyote vya rohoni na mwilini na alishinda vita vyote bila kumwaga damu, moja ya kitu ambacho hakikukosekana kwenye maisha yake ni ibada na maombi.

    103. Ghandh anakiri katika maisha yake ya kuleta mapinduzi kwa taifa la India, asingeweza kustahimili vitisho, hofu, mashaka mashutumu mengi yaliyokuja kwake kama asingekuwa mtu wa sala na maombi. Maombi na imani yake kwa Mungu yalimfanya apate nguvu za kustahimili kila upinzani kwenye maisha yake.

    104. Hofu haiwezi kukaa kwa mtu mwenye imani, mtu mwenye uhusiano imara na Mungu, hofu na mashaka haziwezi kukaa pamoja na imani kwa Mungu. Imeandikwa kuwa, hatukupewa roho ya hofu na mashaka, bali roho ya nguvu.

    105. Mwandishi wa kitabu hiki anashauri tusome Zaburi ya 23. Hii itasaidia sana namna ya kukuza imani yetu kwa Mungu na itatuondolea hofu na mashaka.

    106. Usije ukakosa usingizi kwa sababu ya maneno ya watu juu yako. fanya mambo yako kwa uwezo wako wote, kwa ubora wa viwango vya juu sana, kisha waachie waendelee na kelele zao.

    107. Kama unajihisi uchovu na kuchoka, jipe muda wa kupumzika, relax na tafakari mazuri na namna ya kuboresha kazi zako.

    108. Usiogope kufanyia kazi malengo yako, hata kama itakugharimu kukosa usingizi, mwandishi anasema hakuna aliyewahi kufa kwa kukosa usingizi.

    109. Tafuta vitabu bora vya kusoma ili uboreshe imani yako, hata mahusiano yako na watu wako wa karibu, hii itaongeza kujiamini na kujiona mwenye mchango kwenye jamii.

    110. Hamasika kufanya mambo yako, tengeneza mazingira yote yawe mazuri na yatakayokufanya uhamasike kufanyia kazi ndoto zako, mfano kama ni ofisi hakikisha ipo katika mpangilio mzuri, taa, meza, kalamu nk.

    111. Fanya mambo yako kwa vipaumbele, zinagatia vipaumbele kwenye ufanyaji wa majukumu yako, la muhimu ndio lianze na lifuate jingine.

    112. Simamia masuala yako ya kifedha vizuri, pangilia bajeti yako na fanya manunuzi kulingana na bajeti yako, usitamani maisha ya mtu mwingine, boresha yako na yafanye unavyotamani yawe.

    113. Chukua tahadhari zote muhimu, kama vile kulinda afya yako, kazi zako, biashara yako na utajiri wako, unaweza kukata bima.

    114. Kuwa mwanamichezo, pasha misuli yako, furahi, cheka sana, usijichukulie serious saaana. Jicheke kwa uliyoyahofia ambayo hayakuwa halisi kama ulivyodhani.

    115. Kumbuka leo ni ile kesho uliyokuwa unaihofia jana, amua kuondoka kwenye hofu maana umeona hakuna uhalisia kwenye mambo mengi unayohofia.

    MWISHO:

    Kitabu hiki kina mbinu nyingi na mafunzo mengi yenye mifano halisi namna watu walivyotoka kwenye maisha ya hofu na kuanza kuishi maisha yao kwa furaha na kwa ujasiri. Napenda kila mtu akisome kitabu hiki kitatibu magonjwa mengi sana yanayoisumbua jamii yetu. haya ni machache kati ya mengi yaliyoandikwa kwenye kitabu hiki. Tafuta nakala yako ujisomee, utajishukuru siku zote.

    ©Hillary Mrosso 22.08.2022

X