-
Kiashiria Kuwa Unatakiwa Kuchapa Kazi Kubwa Zaidi Ya Unavyofanya Sasa
Ukiona bado unatumia nguvu kubwa kujieleza kwa watu ili waweze kukufahamu wewe ni nani, basi fahamu kuwa bado unahitaji kuweka juhudi kubwa na kazi kubwa zaidi, ili kupata unachotaka.
Chapa kazi kiasi kwamba ifikie hatua, ukisema kwamba mimi ndiye John Makene, basi kila mtu ajue wazi kuwa ni wewe, siyo unaanza kujieleza sana ili ufahamike.
SIku njema.
rafiki yangu, twende zetu youtube leo ukatazame nilichokuandalia
-
Kitu Kimoja Muhimu Unachohitaji kufahamu Kuhusu Uwekezaji
Rafiki yangu leo nataka nikwambie kitu kimoja na muhimu sana unachohitaji kufahamu kuhusu uwekezaji. Na kitu hiki siyo kingine bali ni kuwa usiwekeza kwenye kitu ambacho wewe mwenyewwe huelewi.
Kamwe usikubali kuitoa fedha yako ambayo umeihangaikia kwa jasho kubwa kuiwekeza kwenye kitu ambacho wewe mwenywewe huelewi.
Hakikisha kabla ya kuwekeza unajirisha kwa undani kuwa kitu unachoenda kuwekeza unakielewa vizuri na kwa undani.
Kama kitu hukielewi, basi uweke fedha yako hapo.
-
Kitu Muhimu Kuhusu Fursa
Habari ya upande wa huko rafiki yangu, bila shaka unaendelea vizuri kabisa.
Mimi nakusalimia hapa kutoka mjini Morogoro.Leo nimeukumbuka ujumbe mmoja ambao niliwahi kuusoma siku za nyuma.
Ujumbe huu sijauandika mimi, ila una funzo kubwa sana kuhusiana na fursa. Na ningependa na wewe uusome.Sina shaka utaniambia kitu kikubwa ulichojifunza baada ya kuwa umeusoma. Ujumbe mwenyewe huu hapa chini.
Ukipata nafasi ya kufika kule Mbozi, Mbeya ukakutana na habari za watu wanaotajirika kutokana na kilimo cha kahawa, kwa kweli unaweza kuwehuka, na kujiona kama mtu uliyechelewa kweli kweli.
Wakati unarudi, kama ukishuka Mafinga, Njombe na kufuatilia stori na kutazama mamilionea walioupata umilionea kutokana na biashara ya miti na mbao, unaweza kudhani kwamba hapa duniani fursa inayowatoa watu kiuharaka ni mbao pekee!
Pitia maeneo ya Ruaha Mbuyuni, Iringa kutana na wakulima wa nyanya na vitunguu wakikuonesha coaster walizonunua kwa kilimo cha msimu mmoja pekee. Aisee kama una akiba utanunua shamba muda huo huo na kuachana na ajira kama ulikuwa mwajiriwa.
Ukitoka pale ukaenda mpaka Mang’ula na Ifakara Morogoro, ukakutana na habari za watu wanavyopiga hela kwenye mpunga, kichwa chako kinaweza kuwaka moto. Unaweza kujizaba vibao na kujimaindi, afu utajiuliza, “Nilikua wapi siku, zote hizi?”
Ukitoka kule jisogeze mdogo mdogo hadi Kariakoo, Dsm kisha kutana na wafanyabiashara wa maduka pale ambao wana gepu la kufuata bidhaa kule China, Uingereza na Dubai. Utapigwa na butwaa utakapoona watu wakiongelea milioni mia tatu, milioni mia saba, bilioni mbili kama vile wanaongelea elfu kumi kumi.
Usipokua na utulivu unaweza kuamini kwamba biashara zinazolipa ni maduka na unaweza kuanza kufight kupata fremu pale!Usiende kwanza Zanzibar, bali chukua hata bus au Fastjet uende chapchap kule Arusha. Hapo kutana na stori za mabilionea wa madini wanaotikisa jiji.
Ukisimuliwa ABC za madini na namna ya kucheza nayo, unaweza kuacha kila kitu na kuanza kuhangaika na biashara ya madini. Hapo sijakutajia jeuri utakayoiona kwa watu wanaofanya biashara ya utalii. Nakwambia hela ulizozisikia Kariakoo utaziona ni cha mtoto sana!
Unapoendelea kutafakari, rudi mtandaoni. Kama ukibahatika kukutana na watu wanaoitwa Network Marketing utakoma kuchagua. Wakikuelezea stori zao, wakikusimulia walivyonunua mavouge yao, wakikuonesha picha zao walizokua wanakula bata Dubai, Paris, Madagascar na Uamerikani, nakwambia korosho utaziona takataka.Mbao utazihesabu kama biashara ya utumwa, maduka ya Kariakoo utayaona kama michosho na mipunga ya Ifakara utaiona kama madudu flani ya walugaluga waliochelewa! Sasa mara kumi hata ya Network Marketing wa bidhaa, usiombe ukutane na fursa ya digital currency, hakika nakwambia utatembea kifua mbele ukiamini kutajirika ni ishu ya kufumba na kufumbua.
Hapo sijaamua kusafiri na wewe kwenda kwa wale tunaokinadi kilimo kama dhahabu inayoelea. Ukisikiliza wafuasi wa kilimo, ukasikiliza hesabu wanazokupatia unaweza kusema wanaohangaika na madini wanapoteza muda!
Ngoja niuchune kukupeleka kwenye fursa ya samaki kuzitoa Mwanza kupeleka Congo, ngoja nisikurushe roho na habari ya korosho, ngoja nikaushie habari ya ufuta!
KUNA MAMBO MATANO YA KUFAHAMU:-*1. Usipokua na utulivu wa fikra, hizi habari za fursa za biashara na ujasiriamali zinaweza kugeuka kuwa kama miluzi mingi, na itakupoteza.
2. Mtu yeyote asikudanganye ya kwamba kuna biashara bora kuliko nyingine. Kila biashara, fursa unayoiona huku duniani inao uwezo wa kutengeneza matajiri.
Kuna matajiri kutokana na kumiliki shule, wengine kwa kumiliki mabasi, wengine kwa kuwa na vituo vya mafuta, wengine kwa kilimo, wengine kwa udalali n.k.
Usisahau kuwa biashara inayomtajirisha mmoja, mwingine akiingia ndio inaweza kumfilisi na kumpoteza kabisa! Kawaulize waliolizwa kwenye kilimo, watakusimulia.
3. Mtu yeyote asikuchanganye na miluzi yake hata ukaamini kwamba kuna fursa inayoweza kumfaa kila mtu. Sio kila fursa inayompa faida John inaweza kukupa faida wewe Ashura.
Ukifuatilia kwa umakini utabaini kwamba mafanikio hayakai katika uzuri wa fursa, bali yanatokana na mchukua fursa.
Mwingine anaweza kujifunza na kumudu kuifanya network marketing, lakini mwingine nature ya network marketing haimfai, isipokua akienda kule Mafinga akazamia kwenye mbao, mwaka mmoja mbali unaona ana Semitrela zake mbili na mambo yanaenda.
Kuna watu wanapotea kiuchumi kwa kung’ang’ana na fursa kwa kukariri. Kisa kuna mtu alinunua Range Rover katika network marketing na wewe unaendelea kukomaa, mwaka wa tano sasa hata bodaboda huna,
kumbe ungeenda zako Mbozi kwenye Kahawa sasa hivi usikute na nyumba ungekua umejenga.
Kisa wanaoenda China wanatoka na wewe unahangaika na biashara za maduka, mwaka wa ishirini bado hakujasomeka na kumbe ungeenda zako kwenye madini huko Mererani muda huu ungekua umeshanunua helkopta yako!
4. Ni kweli kwamba inatakiwa tujifunze fursa mbalimbali, lakini ifike sehemu mtu uchague kukomaa na fursa fulani pasipo kurukaruka.
Utajiri hauji kwa mtu kuwa bize na kila fursa inayoingia, bali unakuja kwa kujifunza fursa nyingi na ku-stick na eneo moja, ama maeneo machache ambayo, utajitambulisha nayo na watu watakutambua.
Na ukishakua katika kukomaa na maeneo yako (fursa ulizoamua kukomaa nazo), usianze tena kuyumbayumba na kutamani ya wengine.5. Lazima ifike mahali utambue kwamba kila mtu anahitaji fedha za kutosha lakini hatuhitaji kiwango sawa cha fedha kwa sababu makusudi na malengo yetu hayafanani.
Nikisema hivi, sikushauri uhangaike na fursa kwa motive ya hela pekee, bali ufanye vitu kama sehemu ya kuufurahia mchakato wa kazi, na fedha ziwe ni matokeo na sio lengo namba moja
Fursa zipo nyingi kuwa makini katika maamuzi.Wewe umejifunza nini kutokana na ujumbe huu.
Ebu weka maoni yako hapa chini
-
Tegemea hiki endapo utasoma kitabu Cha Godius Rweyongeza

Ni kitabu kipi Cha Godius Rweyongeza umewahi kusoma? Kama hujawahi kusoma kitabu chake chochote Basi huu unaweza kuwa Ni wakati wako muafaka wa kuhakikisha kuwa unasoma kitabu chake hata kimoja.
Kitu kikubwa unachopaswa kutegemea kutoka kwenye vitabu vyake ni kuwa kitabu chake chochote utakachosoma utapata thamani zaidi ya vile ulivyolipia.
Ukinunua kitabu Cha elfu tano, Basi ujue ulipaswa kulipia elfu kumi au zaidi. Kitabu unachostahili kulipia elfu hamsini unakipata kwa elfu ishirini au chini ya hapo.
Unaweza kudhani nakudanganya. Ebu msikilize huyu hapa

Au huyu

Bado huamini tu, ebu muone na huyu

Zaidi zaidi, pata nakala ya kitabu na wewe uvune makubwa yaliyo vitabuni mwake.

Ni kitabu kipi ungependa kusoma Kati ya Hivi
1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI
2. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO
3. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
4. MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE
5. JINSI YA KUWEKA AKIBA
6. JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU
7. MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE
8. KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kugundua, Kunoa Na Kuendeleza Kipaji Chako9. JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO

-
Ni marufuku kwako kutumia hii kauli kuanzia leo hii
Moja ya kauli ambayo watu wamekuwa wanapenda kutumia ni kauli ya ninapoteza muda. Mtu anapotumia kauli hii maana yake hana kitu chochote cha maana cha kufanya kwa sasa, hivyo, kitu pekee anachoweza kufanya ni kupoteza muda.
Hivi kweli rafiki yangu, unaweza kukosa kitu cha maana cha kutumia kwenye muda wako. Kuanzia leo hii nataka kabisa uachane na dhana ya kuwa unapoteza muda. Ukijikuta upo kwenye hali ya kupoteza tu muda ili saa zisogee, basi jiulize ni kitu gani cha maana ambacho unaweza kufanya
Au jiulize ni uzalishaji gani ambao unaweza kuutumia ndani ya huo muda wako. Rafiki yangu, kwa vyovyote vile usikubali kuwa mmoja wa watu ambao wanapoteza muda.
Muda ni mali, sasa kwa nini ukubali kupoteza mali. Utumie muda wako kwa manufaa kuanzia leo hii. kama huoni kitu gani ambacho unaweza kufanya na muda wako, basi chukua kitabu usome. Tena unaweza kuanza kwa kusoma hata kitabu cha bure ambacho huwa natoa hapa jukwaani. Kukipata nitumie ujumbe wenye baruapepe yako kwa whatsap namba 0755848391. Name nitaktuma kwako bila kuchelewa.
Kwa vyovyote vile rafiki yangu, usikubali kabisa kuwa unapoteza muda kwenye maisha yako. Muda ni mali, ujali na utumie vizuri sana. Kila la kheri
-
Kitu cha kufanya kama unataka kupata matokeo ya tofauti

Moja ya kitu ambacho watu huwa wanapenda kwenye maisha ni kupata maisha ya tofauti na maisha mazurri. Sasa leo nataka nikuoneshe ni kitu gani haswa unapaswa kufanya kama unataka kupata matokeo ya tofauti kulinganisha na vile ambavyo umekuwa unapata siku zote.
Kwanza kabisa kama unataka kupata matokeo ya tofauti unapaswa kuwa mtu wa tofauti. Hapa maana yake matendo yako na hata maneno yako ambayo umekuwa unatumia siku zote vipaswa kubadilika ili uweze kuendana na haya matokeo mapya ambayo unayataka. Huwezi kupata matokeo ya tofauti kwa kuendelea kufanya vitu vilevile kila siku, ambavyo umekuwa unafanya siku zote.
Albert Einstein aliwahi kunukuliwa akisema kwamba ujinga ni kufanya vitu vilevile huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti. Kumbe kama unataka kupata matokeo ya tofauti rafiki yangu sharti uwe tayari kufanya vitu vya tofauti kuliko ambavyo umekuwa ukifanya siku zote. Labda utakuwa unajiuliza hivi hivi vitu vya tofaut ambavyo ninapaswa kufanya ni vitu gani. Ninachotaka kukwambia ni kuwa kama hujui ni kitu gani cha tofauti ambacho unaweza kufanya, basi fanya kazi kwa bidii kwenye kazi yako kuliko ambavyo umekuwa unafanya na kuliko mtu mwingine yeyote.
Kama hujui kitu cha tofauti cha kufanya, basi soma vitabu mbalimbali kuhusiana na fedha, malengo na maendeleao binafsi, kisha fanyi kazi kile unachojifunza kutoka kwenye vile vitu unavyojifunza.
Kwa jinsi hiyo utakuwa umeanza kufanya kitu cha tofauti.
Tumia muda wako vizuri, badala ya kutumia muda wako kufanya vitu ambavyo siyo sahihi, tumia muda wako vizur kufanya kitu ambnacho ni sahihi kwako mara zote.
-
Umefanya uamuzi uliobora sana
Habari ya leo
Mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE
Ninajua kwamba umeomba kupata KITABU CHA BURE . lakini pia nimeona siyo vibaya ukijua mimi ni nani na kitu gani utegemee kupata kwangu na SONGAMBELE kiujumla.Bila kuongeza la ziada napenda kukutaarifu kuwa kitabu chako kimeshatumwa kwenye baruapepe yako, ila kama hukioni unaweza kukipakua kwa KUBONYEZA HAPA
Kwa miaka zaidi ya mitano sasa nimekuwa nikiandika kwenye blogu hii ya SONGA MBELE. Kwenye blog hii nimekuwa nikiandika makala mbalimbali kuhusu biashara, ndoto zako na malengo yako na jinsi ambavyo unaweza kuyafikia.
Lakini zadi ya hapo, nimewasaidia watu kama wewe kuweka malengo, kuyafanyia kazi mpaka kuyatimiza. Wengine bado ninaendelea nao mpaka leo hii.
Hiki kitu ndicho ningependa nifanye kwako pia
Kila mara nitakuwa nakutumia jumbe fupi na makala zenye kukuelimisha na zitakazokusaidia wewe kuweza kupiga hatua na kufika mbali zaidi kwenye baruapepe yako. Nitafanya hivyo aidha kupitia kwenye makala, video na mafunzo ya sauti.
Lengo ni kukusaidia wewe kufikia malengo yako haraka iwezekavyo.
Na hilo litawezekana kama wewe utaendelea kuwa na mimi
Kiufupi, ukikaa pamoja nami- utajifunza namna ambavyo unaweza kuweka malengo.
- kuyafanyia kazi mpaka kuyatimiza kwa kutumia mbinu ambazo mimi na wengine wengi tumetumia kwa manufaa
- Pia utajifunza namna ya kuanzisha na kukuza biashara yako
- Bila kusahau kipaji chako
Baada ya kusema hayo, naomba ubonyeze hapa kupakua kitabu chako cha BURE
Kitabu hiki kitakusaidia wewe; kuanza kusoma vitabu. kitu ambacho ni muhimu sana hasa kama unataka kufikia malengo yako.
Vitabu vina mchango mkubwa kwa mtu ambaye anataka kufanya makubwa na kuufikia ukuu.
Na ndio maana kwenye safari yetu tunaanza kwa kukuonesha MAAJABU KUSOMA VITABU.
Na bado nina vitu vingi vya bure vya kukusaidia wewe kufanyia kazi malengo mpaka ukayafikia.Kitu unachopaswa kufanya wewe ni kuhakikisha kila mara unatembelea barua pepe yako ili kupata mafunzo zaidi lakini pia kutembelea blogu ya SONGAMBELE. kila mara maana hapa naandika makala mbili mpya kila siku
Tutaongea
Ni mimi Godius Rweyongeza (Songambele).
SONGAMBELENB: Kama umepokea kitabu hiki cha zawadi. Naomba unitumie ujumbe kwa barua pepe yangu ya godiusrweyongeza1@gmail.com kuniambia umekipokea.Nitafurahi sana kuona ujumbe wako. na nitaweza kuujibu ujumbe wako punde tu baada ya kuupokea. Huwa najibu jumbe zote ambazo zinatumwa kwangu. -
Jiwe la uzito wa tani moja kwa wale ambao hawataki kuweka akiba
Moja ya sababu ambazo watu huwa wanatoa linapokuja suala zima la kuweka akiba ni kuwa hawawezi kuweka akiba kwa sababu wana vitu vingi vya kufanya na fedha. Utakuta mtu anakwambia kwamba nina kodi, ya nyumba na bili nyinginezo ambazo ninapaswa kulipa na hata fedha hainitoshi.
Kitu kimoja cha muhimu sana na cha kushangaza ni kuwa watu hawa watu huwa wanapambana kuhakikisha kwamba wanalipa hizi bili ila huwa wanajisahau kwenye suala zima la kuweka akiba na kuwekeza.
Bili zao hata zikiongezeka huwa wanahakikisha kuwa wanatafuta namna ya kuzilipa ila huwa hawatafuti namna ya kuhakikisha kuwa wanaweka akiba.
Sasa leo ninachotaka kukwambia ni kuwa fanya uwekaji wa akiba na uwekezaji kama ulipaji wa bili. Yaani, kama ambavyo unalipa bili zote bila kujali bili hizo zimeongezeka au zimebaki palepale. Hivyo hivyo, unapaswa kuweka kipaumbele kwenye kuweka akiba na kuwekeza. Kamwe usikubali kuishi maisha bila ya kuweka akiba wala kuwekeza. Ni muhimu sana kwako kuweka akiba. Ni muhimu mno kiasi kwamba haupaswi kupuuzia kitu kama hiki hapa rafiki yangu.
Kuweka akiba kwako kuwe kipaumbele kama vile unalipa kodi ya nyumba. Kuweka akiba kwako kuwe kipaumbele kama vile unanunua luku ya umeme.
Kuna baadhi ya familia umeme ukikitatika, utakuta kwamba kwenye familia wanahaha, kama baba au mama ambaye anapaswa kununua umeme hayupo wakati umeme unakatika, basi wanafamilia wote watatafuta namna ya kuhakikisha kwamba wanawasiliana naye hata kwa kumpigia simu, hata kama wanaomba simu kwa jirani.
Sasa nataka na wewe ufanye uwekaji wa akiba kuwa kipaumbele. Mwambie mpaka mwenza wako awe anakukumbusha kuweka akiba kama kitu cha kwanza. Asikukumbushe tu kulipa kodi ya nyumba kwa sababu mkifukuzwa kwenye nyumb mtaaibika, asikukumbushe tu kulipia umeme kwa sababu mkikaa bila umeme hawezi kuangalia tamthiliya, akukumbushe pia kuweka akiba na kuwekeza kwa sababu usipofanya hiki kitu, itakuwa aibu kwako miaka mingi ijayo mbeleni. Fanya uwekaji wa akiba kuwa kipaumbele kwenye maisha yako tena kiwe kipaumbele kikubwa sana. Usipuuzie uwekaji wa akiba na uwekezaji rafiki yangu.
Kila la kheri, hilo ndilo jiwe langu kwa watu ambao hawataki kuweka kuweka akiba siku ya leo.
Kujifunza zaidi nashauri usome kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA.
Hiki kitabu kitakufungua vitu vingi sana kuhusu uwekaji wa akiba na namna ambavyo unaweza kuwa wenye manufaa kwenye maisha yako. Halafu kitabu chenyewe ni elfu tano tu. Ndio, elfu tano ya kitanzania. Namba ya malipo ni 0755848391 na jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Karibu sana
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza (Songambele)
0755848391
Morogoro-Tz
-
Kitu ambacho kitakufanya uweze kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa
Watu huwa wanatafuta siri za mafanikio na kuwafikisha mbali. Kama Kuna Siri ya mafanikio ambayo Unapaswa kuifahamu ambayo itakuwezesha kuongeza kipato Chako zaidi ni kufanya kazi zaidi ya vile unavyolipwa.
Yaani, kujituma zaidi na kuchapa kazi zaidi ya ambavyo unalipwa. Hiki kitu kitakufanya uweze kulipwa zaidi.
Kwa sababu kama MTU akikupa kazi yake na ukaifanya kwa viwango vikubwa Kuliko alivyokuwa anatarajia tangu Mwanzo. Ni wazi kuwa Huyu MTU hawezi kukusahau.
Lakini pia huyu MTU atakuletea watu wengine zaidi.
Ebu tuchukulie mfano wa kawaida labda wewe Ni fundi cherehani. Mtu amekuja kwako na kitambaa anataka suti. Ukamtengenezea suti nzuri sana kwa viwango vya juu Kuliko hata alivyotazaamia.
Unadhani zamu ijayo akitaka kutengeneza suti atamtafuta nani? Au unadhani rafiki yake akitaka kutengeneza suti atamwelekeza kwa nani?Jibu lipo wazi kabisa… yeye atakuja kwako na rafiki yako atamwelekeza kwako.
Hiki kitu ukiendelea kukifanya kwa muda mrefu. Utaweza kupongeza kipato Chako Mara dufu mpaka Mara Kumi zaidi.
Wakati wengine watakuwa wanalia kuwa hawana kazi za kufanya wewe utakuwa nazo za kutosha.
Anza kufanya kazi zaidi ya unavyolipwa. Kila la kheri.
-
Jinsi Ya Kupata Wazo La Kuandika Kitabu
Kuna watu huwa wanafikiri labda ili kuandika kitabu basi unapaswa kuwa na wazo la kipekee sana ambalo halijawaji kutokea Hapa duniaani.
Siyo kweli. Unaweza kuwa na wazo la kawaida tu, Ila wazo Hilo ukalikuza na kulifanya kuwa kitabu kizuri sana. Bado huamini!
Mfano kwenye picha ya kawaida tu ambayo watu wanachukulia poa wewe unaweza kupata kitabu kizuri sana.
Nakumbuka juzi nikikushirikisha kuhusu mama aliyenunua kitabu changu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU wakati wa maonesho ya nanenane.
Wakati namtumia kitabu hiki kwa WhatsApp niligundua kitu kimoja. Na kitu hiki ilikuwa Ni picha aliyokuwa ameweka kwenye profile yake. Niliipenda ile picha, kiasi nikamwambia hii picha ina kitabu ndani yake.
Unaweza kuiona picha yenyewe hapa

Akiwa bado haamini amini Kama hiyo picha inaweza kutoa kitabu, nilichukua karatasi na kalamu na kuanza kuandika kichwa Cha kitabu. Nikamwambia kutoka kwenye hii picha kichwa Cha kitabu kinaweza kuwa hiki.
Baada ya hapo nikashuka chini na kuandika UTANGULIZI. Nikakwambia kwenye utangulizi andika hiki na hiki.
Kisha nikaendelea mbele kwenye sura ya kwanza mpaka ya nne.
Kisha nikakwambia sura nyinginezo utatafuta mwenyewe.
Hivyo, ndivyo waandishi huwa tunapata vitu vya kuandikia.
Kwa kitu chochote unachokiona kuna kitu chaa kuandika ndani yake, itategemea tu na mamna unavyokiangalia kitu.
Tukichukulia mfano wa mti.
Daktari akiona mti, anaona dawa ndani yake.
Mwimbaji akiona mti, anaona wimbo ndani yake.
Mpishi akiona mti anaona kuni
Wakati msafiri akiona mti, anaona kivuli na sehemu ya kupumzila
Fundi seremala kwenye mti huohuo ataona kitanda Safi kabisa.
Kumbuka mti ni uleule Ila kile watu wanachoona kwenye ule mti ndio kinatofautiana.
Na kwenye uandishi hivyohivyo, unaweza kuona kitu ukakichukulia kawaida. Mwingine akaona kuna Kuna kitabu ndani yake.
Ukiwa Kama mwandishi jitahidi kupata walau wazo moja la kuandika kwenye kila kitu unachokiona au watu unaokutana nap.
Bado unaona haiwezekani tu. Sikiliza, nenda kasome kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. Hiki kina kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi wa vitabu na Makala.
Halafu kinauzwa elfu tano tu. Na unatumiwa kwa simu au baruapepe yako.
Yule mama wakati anaendelea kukisoma akisema haya

Mambo ndiyo hayo. Lipia elfu tano sasa kwa 0684408755jina Ni GODIUS RWEYONGEZA
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz