-
Jinsi Ya Kushughulika Na Fedha Unazopata Kutokana Na Kipaji Chako

Limekuwa ni kama jambo la kawaida kusikia watu waliokuwa na vipaji na watu ambao wakati fulani walikuwa wakiingiza fedha nzuri kupitia vipaji vyao wakiwa hawana fedha. Vyombo vya habari, vimekuwa vikiripoti kuwa hawa watu hawana fedha na muda mwingine kupitisha mchango ili hawa watu waweze kupata mahitaji yao ya muhimu au hata kupata sehemu ya kukaa. Wengine huwa wanafukuzwa nyumba walipopanga na hivyo kuwaletea fedheha na kujenga picha mbaya kwa watu wenye vipaji. Kitu hiki kinafanya vyombo vya habari ndio visaidie kupitisha mchango ili watu hao waweze kuchangiwa.
Japo vyombo vya habari vimekuwa vikifanya hivi kwa mazoea, na vimekuwa vikifanya vizuri, ila hili siyo jambo ambalo tunapaswa kulifumbia macho na kuacha kulifundisha ili yeyote atayesikia la mkuu, asije akavunjika guu, halafu eti mkuu mwenyewe ni mimi, hahaha. Kama mtu ana kipaji chake na kipaji chake kinamwingizia fedha nzuri sasa hivi, basi hata miaka mingine mbeleni baada ya kustaafu, hapaswi kuendelea kulalamika wala kupungukiwa na kitu, ndio maana hii sura nimeiandaa maalumu kwa ajili ya hili jambo.
Kuna tatizo kubwa
Kuna sehemu kuna tatizo kubwa na hili tatizo tunapaswa kuhakikisha tunalifanyia kazi ili kuliondoa. Maana, ukiachana na watu wenye vipaji na ujuzi wao, hata wafanyakazi na watu ambao wamekuwa wanaingiza kipato kizuri kwa miaka yao yote ambayo wamekuwa wakifanya kazi, mara tu baada ya kustaafu unakuta kwamba wanakuwa na ukata mkubwa sana wa fedha. Sasa kumbe hili jambo tunapaswa kulipigia kelele, ili watu waweze kujua namna sahihi ya kuishi na hela zao, kuzitumia kwa manufaa, kuziwekeza ili hata baadaye watakapostaafu, waweze kustaafu kwa raha mustarehe, wakiwa na uhakika wa mzigo mkubwa wa hela nyuma yao.
Watoto wanaorithi mali
Wengi wamekuwa wakifananisha watu wenye vipaji (wakimbiaji wa mbio za marathoni, wanamziki, wanamichezo na wengineo) na watoto ambao wanarithi mali…
Yaani, kwamba wote hawa wana vitu viwili ambavyo vinafanana, kwanza ni kupata mali nyingi kwa wakati mmoja na pili ni kuzitapanya au kuzitumia hizo mali zote na baadaye kubaki bila ya fedha
Tafiti nyingi zimerudiwa mara kwa mara na kuonesha kuwa watoto ambao huwa wanarithi mali, asilimia kubwa sana ya watoto hawa wanaishia kupoteza hizo mali ndani ya muda kidogo na baadaye kuishia kwenye umasikini mkubwa sana. Kitu hiki pia kimekuwa kikitokea kwa watu wenye vipaji vyao. Mtu anakuwa ana kipaji anafanya vizuri, anapata fedha, na halafu hizo fedha anazitapanya na mwisho wa siku anabaki bila ya fedha yoyote ile. Hiki kitu baadaye kinamfanya aishiwe na hata kufikia hatua ya kuombaomba kwa watu na kwenye vyombo vya habari. Swali linabaki je, mzunguko kwa watu wote vipaji unapaswa kuwa hivi?
Yaani, ina maana kwamba kila mtu mwenye kipaji anapaswa kufikia hatua ambapo ataishiwa fedha na kuanza kuomba msaada li kujikimu na maisha yake?
Usiilalamikie serikali
Kuna wamekuwa wakiilalamikia serikali kuwa haiwajali baada ya kuwa wamestaafu kufanya kazi. sasa kabla hatujafika huko kote, ebu ngoja tuweke msingi wakati ukiwa unapokea fedha. Ili uweze kuitumia vizuri hii miaka yako ambayo uko kazini kwa ajili ya kuhakikisha kuwa hii miaka inakuwa yenye manufaa makubwa kwako, kiasi kwamba utakapostaafu au likitokea jambo lolote la kukufanya usiendelee na kazi basi uwe na chanzo cha uhakika cha kukuingizia fedha.
Na kitu kingine na muhimu cha kufahamu ni kuwa maisha ni wajibu wako, hivyo kama maisha ni wajibu wako, unapaswakuubeba huu wajibu wa maisha yako kwa asilimia 100.
Usisishindane kufanya starehe unapopata fedha
Wengi wanapokuwa na nguvu na wanapopata fedha basi kitu cha kwanza wanachofanya ni kuonesha kwamba wanazo hizo fedha. Utasikia watu wanasema kwamba tumia fedha zikuzoee. Au ponda mali kufa kwaja. Utasikia mwingine anasema kwamba hapa duniani tunaishi mara moja. ni kweli tunaishi mara moja hapa duniani, na unapaswa kufurahia maisha yako na uwepo wako hapa duniani, ila sasa usitumie fedha kiasi cha kupitiliza wakati hujajenga misingi ya kukuingizia fedha hata kama umelala.
Kama umewahi kufuatilia watu wenye fedha siyo watu ambao huwa wanatumia fedha zao hovyohovyo, badala yake ni watu ambao huwa wanaitumia fedha zao kwa manufaa kabisa.
Wanawekeza na wanajenga vyanzo vya kipato katika kuhakikisha kwamba wanakuwa na fedha zaidi. Na wewe fuata nyayo zao. Na hapa chini ninaenda kukuonesha ni kwa namna gani unaweza kufuata nyayo za hawa watu ili uweze kufanya makubwa.
Anza kufuata misingi ya fedha
Kila kitu kwenye maisha kina sheria na misingi yake. Daktari anayefanya matibabu kuna misingi na sheria ambazo anapaswa kuzifuata kwenye matibabu, hivyo hivyo kwa mwanasheria, kuna misingi na kanuni ambayo anaifuata kwenye kazi yake.
Kitu hiki mara nyingine huwa kinaitwa miiko ya kazi. hizi ndizo kwa kiingereza zinaitwa dos and donts. Yaani, vitu vya kufanya na vitu ambavyo siyo vya kufanya.
Sasa kuna misingi ya kukuza kipaji chako ambayo, kiuhalisia nimeielezea kwenye kitabu cha KIPAJI NI DHAHBU, nashauri sana uweze kupata kitabu hiki cha kipekee ila kwa leo tutaongelea upande wa fedha, upande ambao umekuwa ukiwasumbua watu wengi. ili pale utakapokuwa umeanza kupata fedha kutokana na kipaji chako basi, usije ukayumba wala kutetereka sehemu.

Ili kupata kitabu hiki, wasialiana nami kwa 0755848391 sasa Kwanza kifanye kipaji chako kama biashara
Unajua kwa nini nasisitiza hili la kukifanya kipaji chako kuwa kama biashara
Kwanza ni kwa sababu watu wengi wamekuwa wakifanyia kazi vipaji vyao kama hobby. Hobby ni kitu unafanya tu ilimradi umefanya kwa ajili ya kujifurahisha.
Siku moja nilikuwa naongea na rafiki yangu mmoja kuhusiana na huduma nyingi ambazo tulikuwa tunapata kwa rafiki zetu wakati tuko chuoni, mtaani huduma hizohizo zinalipiwa gharama kubwa ila pale chuoni tulikuwa tunazipata bure kabisa. Kumbe hata hawa ndugu zetu wangeweza kuweka vipaji vyao katika mfumo wa kibiashara na hivyo kuweza kupokea fedha na hata kujenga biashara zaidi ambayo ingewafikia wengi.
Kwa kusema hili sIyo kwamba nakataza watu kutoa msaada au kusaidia. Ila msaada usipitilize kiasi cha mtu kujisahau.
Mfano wa huduma mojawapo ambayo tulikuwa tunapatabure pale chuoni ni huduma ya kutengenezewa simu na marafiki wa karibu pale inapoharibika. Unakuta mtu ana ujuzi wa kutosha kwenye hili kiasi kwamba simu yako ikiharibika anaitengeneza na kuirudisha kwenye uimara wake, anaitengeneza vizuri bure. Kitu ambacho ni kizuri. lakini walau angeweza kuchaji kiasi kidogo kwa ajili ya kuifanya hiyo huduma yake iweze kusongambele zaidi. Huduma hizihizi huku mtaani, tunazilipia, kwa mwanachuo pia unaweza kuweka kiasi kidogo tu cha watu kukulipa na hivyo kupata fedha za hapa na pale za kuendesha maisha chuoni na kujenga ukiwa chuoni au baada ya chuo.
Kitu kingine cha kuongezea hapa ni kuwa, mtu akikosa huduma ya kwako ya bure ataenda mtaani kwa mtu ambaye anatoza hela na ataitoa hela. Mfano simu yake ikiharibika na wewe kipindi hicho ukawa umesafiri, au unaumwa na huwezi kuitengeneza, kwa sababu anaihitaji kwa haraka ataenda kwa mwingine na atamlipa hela ili simu yake itengenezwe kwa haraka, sasa kwa nini na wewe usiwachaji watu kiasi kidogo ili wakulipe kwa hiyo huduma unayotoa. Fikiri kibiashara.
Lakini pia nasisitiza kwamba ufikiri kibiashara zaidi kwa sababu, ukishaweka mfumo kwenye biashara yako, ni wazi kuwa kipaji chako kitendelezwa baada hata ya wewe kuwa umezeeka au hata baada ya kufa. Kuna watu wengi wana vipaji vizuri vya kupika, ila wachache wameweza kufanya vipaji vyao kuwa biashara. Ebu chukulia mfano rahisi tu wa kupika maandazi. Kuna watu wengi wanapika mandazi, ila ni wangapi wameweza kusambaza mandazi yao kama Bakhresa? Sidhani hata kama Bakhresa ana kipaji cha kupika mandazi, hahaha. Ila tofauti kubwa kati ya Bakhresa na watu wengine wanaopika maandazi ni kuwa Bahkhersa yeye anafikiri kibiashara zaidi.
Hivyo, yeye ameweka mfumo wa kibiashara kwenye mandazi yake. Mfumo huu upo kuanzia kwenye kupika mandazi, kuyapaki, kuyasambaza mpaka kuyauza sokoni. Hiki kitu kinafanya maandazi yake yaweze kuuzika siyo kwenye eneo alipo yeye, bali yanauzika karibia nchi nzima. Wakati hapo mtaani kwenu kuna mama ambaye anapika maandazi na hayo maandazi hata hayajasambaa mtaa mzima mnapoishi.
Sijui unanielewa hapo. kumbe na wewe anza kufikiri kibiashara, anza kufikiri Bakhresa, Bakhresa ili na wewe kipaji chako uweze kukiwekea mifumo ya kibishara na kukifanya kweze kwenda mbali zaidi hata kama hautakuwepo.
Mfumo wa biashara utafanya kipaji chako kiweze kusogea. Unaanzaje sasa kuweka mfumo wa biashara kwenye kipaji chako,
Hivi hapa ndivyo unaweza kuanza
Kwanza anza wewe kufanyia kazi kipaji chako. Hiki sihitaji kukieleza zaidi, maana tayari nimeshakieleza kwa kin kwenye kitabu cha KIPAJI NI DHAHABU. Nakala ya kitabu hiki ni elfu tano tu. kupata nakala hii, tuma fedha kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Pili, angalia majukumu yote ambayo unafanya kwenye biasahra yako. Kisha yagawe hayo majukumu, angalia yale majukumu ambayo ni ya muhimu sana na yanahitaji uwepo wako, wewe yafanye hayo. Majukumu mengine wape watu wakusaidie kuyafanya.
Tafuta watu kukusaidia kwenye hayo majukum ili nao waweze kufanya hayo majukumu huku wewe ukiweka nguvu kubwa zaidi kwenye yale majukuu ya muhimu sana kwako.
Nne, weka mfumo wa namna vitu vinavyofanyika. Kwa mfano kwamba wakati wa kutengenza mandazi, haya ndiyo mambo ambayo kila mtu anapaswa kuzigantia. Hii itakusaidia kiasi kwamba hata kama hautakuwepo, majukumu yako yataweza kuendelea mbele zaidi bila ya kurudi nyuma. Lakini pia hii itasaidia kwamba hata kama yule uliyemwajiri akitoka, bado utakuwa na uhakika kuwa shughuli zako zinaendelea bila ya kurudi nyuma tena kwa ubora ule ule.
Umeshawahi kuona watu wanakataa kununua chakula kwa sababu mhudumu fulani hayupo siku hiyo. Changamoto inakuwa pale ambapo mhusika mmojawapo kwenye biashara anaondoka, ubora unapungua, au kama ni huduma kwa wateja ndio siku hiyo inakuwa sifuri.
Sasa mfumo ni mwongozo. Unapaswa kufuatwa bila kujali wewe upo au haupo. Unapaswa kufuatwa bila kujali mtu fulani uliyemwajiri yupo au hayupo. Rafiki yangu lifanyie kazi hili kwenye kipaji chako pia.
Nne, simamia mfumo. Hapa hakikisha kwamba kila kitu kwenye mfumo kinaenda sawa kama inavyostahili.
Tano weka mtu wa kusimamia mfumo, hapa unaweka mtu wa kusimamia mfumo, huyu anasimamia kiasi kwamba hata kama haupo kila kitu kinaendelea. Ukiwa na mfumo mzuri hata ukifa, kila kitu kinaendelea. Ndio maana leo hii unaona kampuni kama cocacola zinazidi kusongambele. Unajua Cocacola ilianzishwa mwaka gani? Utakuwa sahihi, ni mwaka 1892. Ni zaidi y a miaka 100. Mwanzilishi wake alishakufa miaka mingi sana iliyopita, ila kitu kimoja kilicho nyuma yah ii kampuni na kinachoifanya iendelee kusonga mbele ni mfumo unaosimamia uzalishaji wa bidhaa zake. Hakuna hata siku moja utakunywa cocacola ukuta kuwa ile ladha imebadilishwa, ladha ni ileile kila siku. Ladha ni ileile ukiwa Tanzania, Uganda, Afrika kusini au kazikazini! Kwa nini? kwa sababu ya mfumo ulio nyuma ya utengenezaji wa soda hii. kuna vitu ambavyo unapaswa kuzingatia. Na ukizingatia hivyo tu, basi umemaliza. Na wewe unapaswa kufanya hivyo, tengeneza mfumo kwa ila kitu.
Tengeneza mfumo kwenye uzalishaji, watu wajue mchakato wote wanaofuata kwenye kutengeneza bidhaa au kutoa kitu. Mama anayepika maandazi mtaani kwako, anapika mandazi matamu sana, ila siku asipokuwepo kutengeneza mandazi yale, akaja mwanae ujue siku hiyo yanatengenezwa maandazi ya hovyo. Kwa nini? kwa sababu mama anajua mchakato wote wa kutengeneza mandazi, ia sasa ule mfumo haufahamiki kwa mtoto. Hakuna sehemu umeandikwa. Kwa hiyo uandike huo mfumo wako, ili kila anayefanya kazi kwenye kitengo husika akae akiujua huo mchakato wa kufuata.
Sita wakabe hao watu uliowaweka kusimamia mfumo
Saba ongeza juhudi zaidi kwenye kusimamia mfumo na kwend ambali zaidi.
Sambamba na kuweka mfumo sahihi wa kibishara kwenye kipaji chako unachofanya unahitaji pia kuweka mfumo sahihi wa kifedha kwenye kipaji chako. Na kwa kuanzia, anza na vitu rahisi tu. anza na kuhakikisha unajua mapato na matumizi. Yaani, fedha yote inayoingia ijulikane na fedha yote inayotoka ijulikane. Hiki kitu ni kidogo sana ile chenye nguvu kubwa sana.
Halafu hao watu hao ambao unawaita ili kukusaidia kazi za hapa na pale hakikisha kwamba unawaliipa. Niwazi kuwa na wao wana ndoto na malengo ambayo wanegependa kutimiza, hivyo kwa kile kiasi utakachowalipa, watakuwa na uwezo wa kuanza kufanyia kazi malengo na ndoto zao huku wakiendelea kukusaidia wewe. hivyo, walipe. Kazi yako kubwa itakuwa ni kuhakikisha kuwa unaajiri pale ambapo mtu atakuwa anahitajika kwenye biashara ili aweze kusaidia majukumu fulani, kitu ambacho kitakusaidia wewe na timu yako kuweka nguvu kwenye kukuza mauzo zaidi na hivyo kuweza kuwalipa.
Kwa hiyo utatoa kiasi utawalipa. Na wewe mwenyewe utajilipa mshahara wa kawaida.
Kisha faida itakayobaki iwekeze.
Na kwa kuwa nataka nikupe mwongozo kamili, sikiliza nenda kawekeze fedha yako kwenye mifuko ya uwekezaji ya pamoja, iliyo chini ya UTT.
Najua watu wengi watakushawishi kuhusu kuwekeza kwenye maeneo mengi mengi kama kilimo, bitcoin, na mengine mengi. Lakini kwa kuwa wewe nguvu yako kubwa unaiweka kwenye kipaji chako, huhitaji kuwekeza nguvu kubwa kwenye maeneo mengine, nguvu yako yote iwekeze kwenye kipaji chako na hata unapoongea na timu yako, wasukume wafanye vizuri zaidi ili kipaji chako kama bishara kiweze kufika mbali, ila kwa vyovyote vile hakikisha kuwa hautawanyi nguvu zako kwa kuziweka kwenyea maneo mengine ambayo huyafahamu, badala yake wekeza nguvu zako zote kwenye kipaji mpaka kifikie ngazi kubwa za kimataifa.
Kwa hiyo, uwekezaji wako wote ufanyie kupitia mifuko ya uwekezaji wa pamoja ya UTTt
Najua utakuwa unajiuliza UTT ni kitu gani na hii mifuko ya pamoja inafanyaje kazi, hiki kitu sitaweza kukieleza kwa kina kwenye makala hii. Ila nimeandika kitabu kinaitwa maajabu ya kuwekeza kwenye hisa, hatifungani na vipande. Nashauri sana uweze kupata kitabu hiki cha kipekee, kwa kuwasiliana nami kwa 0755848391
Ngoja nikwambie kitu, unapowekeza kwenye hii mifuko unakuwa unaifanya fedha ikufanyie kazi hata kama wewe haupo, kitu ambacho kinakutengenezea maisha mazuri ya hapo baadaye. Lakini pia ni sehemu ya wewe kuweka akiba na kuteng eneza kesho yako bora.

Umeshapata kitabu hiki Cha Maajabu ya Kusoma Vitabu? Gharama yake Ni 5,000 Asante sana,
Nakutakia kila la kheri
Godius Rweyongeza (SONGAMBELE)
0755848391
Morogoro-Tz
SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA CHINI
-
Jinsi Kizazi Kinachostaafu Kinavyoweza Kuandaa Kizazi Kijacho

Mara kwa mara nimekuwa nakutana na watu wazima wenye umri wa miaka 50 na zaidi au niseme watu walio kwenye umri wa miaka ya kustaafu, kila ambapo nimekuwa nikiongea na watu hawa kuhusiana na vipaji basi wenyewe moja kwa moja wamekuwa wakiniambia kuwa umri wao umeshaenda, hivyo kwao huu sio muda tena wa wao kunoa au kuendeleza vipaji.
Kitu kimoja ambacho nimekuwa nikiongea nao ni kuwa wao wanaweza kuwa sehemu ya kuwasaidia kizazi kijacho (, watoto wao, wajukuu wao na vijana wengine) kugundua vipaji vyao, kuvinoa na kuviendeleza. Hiki ni kitu ambacho naamini kinawezekana kabisa kufanyika na mzee yeyote yule anaweza kusaidia kutengeneza taifa bora kwa siku za mbeleni.
Jack Ma aliwahi kusema kwamba unapofikisha umri wa miaka 60 na zaidi ni muda wa wewe kuhakikisha unaandaa kizazi kjacho. Nadhani, wazee wote ambao wanasema kwamba kwa sasa hawawezi kugundua wala kuendeleza vipaji vyao, basi walau hata hawawezi kushindwa kushiriki kwenye kuandaa kiazazi kijacho.
Tukiwa na kizazi kizuri kinachojitambua, kizazi ambacho kila kijana anajua uwezo wake na kwa nini yuko hapa duniani. Kizazi ambacho kila kijana anatumia uwezo alio nao ndani yake, ni wazi kuwa tutatengeneza taifa zuri na bora sana kuwahi kutengeneza hapa duniani.
Na hiki ni kitu ambacho tunapaswa kupigania.
Kama wewe una watoto au wajukuu ambao unakaa nao, kwa nini usitoe sehemu ya muda wako katika kufuatilia na kuangalia uwezo wao walio nao na huku ukiwasaidia kuutumia huo uwezo kwa manufaa ya sasa hivi na siku zijazo.
Wewe una uwezo mkubwa sana
Kuna kitabu nilikuwa nasoma, ila sikumbuki mwandishi ni nani. Kwenye hiki kitabu mwandishi akawa anaeleza kuwa alikuwa anakaa bibi yake, pale kwa bibi yake walikuwa wanakaa watoto kama kumi hivi na zaidi. Sasa siku moja bibi yake alimwita pembeni huyu mjukuu wake kwa ajili ya maongezi binafsi ambapo watoto wengine hawakuwepo. Kijana alimsikiliza bibi yake kwa umakini mkubwa sana, bibi yake alimwambia kwamba, nimeangalia kati ya vijana wote wanaokaa hapa, nimeona kwamba wewe una uwezo mkubwa sana na ninakuhakikishia kwamba siku moja wewe unaenda kufanikiwa sana.
Bibi yake akamsisitiza kuwa aende autumie huo uwezo wake vizuri kuhakikisha anafanya makubwa kwenye maisha, na mwisho kabisa akamwabia asimwambie mtu hayo aliyomwambia.
Mwandishi alisema hiki kitu 5 kilimpa nguvu kubwa sana kwenye maisha.
Baadaye alikuja kugundua kuwa bibi yake alikuwa na utaratibu wa kumwita kila kijana wake mmoja mmoja na kumwambia maneno hayohayo, kumbe siyo yeye tu alikuwa ameambiwa hayo maneno. bali watoto wengine walikuwa wameambiwa hayo maneno, lakini bado kujua hilo halikumkatisha tamaa. Alichukua kile alichoambiwa na bibi yake moyoni na kuamua kukifanyia kazi ili kuhakikisha anafanya makubwa kwenye maisha.
Wewe pia kama mzazi unaweza kuwatia moyo watoto na wajukuu kwa kuwaambia maneno mazuri ambayo yatawasukuma kufanya kitu cha tofauti kwenye maisha yao. Na muda mzuri ni sasa.
Muda mzuri wa kupanda miti
Kuna msemo mmoja wa kiafrika unaosema kwamba muda mzuri wa kupanda mti ulikuw ani miaka ishirini iliyopita, ila muda mzuri zaidi ni sasa. Unajiuliza hivi kupanda miti na kunoa vipaji sasa vinaendanaje? Ninachotaka nikwambie hapa ni kuwa kama wewe hukuweza kugundua kipaji chako ukiwa kijana, basi wewe unaweza kusaidia vijana na watoto kugundua vipaji vyao pia.
Na wakishagundua vipaji vyao, wafuatilie kwenye kuvifanyia kazi mazoezi na kuhakikisha vipaji hivyo vinakuwa vyenye manufaa kwao pia.
Nimewahi kusikia stori, kuwa baba yake Mbwana Samatta alikuwa anamfuatilia nyuma kuhakikisha anafanya vizuri kwenye mchezo, na hata alikuwa na mfumo wa kutoa zawadi au adhabu kama Samatta angefunga.
Yaani kwamba walikuwa wameweka mkataba kwamba kama Samatta atafunga goli, basi baba yake atamzawadia shilingi elfu mbili, na kama atafungwa basi yeye anapaswa kulipa faini ya elfu mbili.
Japo sina uhakika na hili kwa asilimia mia moja. lakini hiki kitu kinaweza kuwa kitu chenye manufaa kwa wazazi, kukitumia kwa watoto. Unaweza kutumia mfumo wa zawadi na adhabu kumsaidia mwanao, mjukuu au mtoto yeyote kwenye kunoa na kuendeleza kipaji chake.
Mfano unaweza kununua zawadi na kuja nazo pale nyumbani, hizo zawadi ukaziwekea sharti ya kuzipata.
Mfano unaweza kumwambia kuwa utapata zawadi hii endapo utafanya hiki na kile, utapata zawadi hii endapo utakamilisha hesabu zako za darasani.
Utapata zawadi hii endapo utafanya homework na kuimaliza. Hiki kitu kikampa motisha mtoto kufanyia kazi kipaji chake cha hesabu au kusoma, na hivyo kumsaidia kuboresha zaidi kile kilicho ndani yake,
Lakini pia ni motisha kwa mtoto maana anakuwa anajua kwamba endapo hatafanya mazoezi au hatakamilisha jambo fulani basi hatapata zawadi yake uliyomwandalia ambayo kwake ni adhabu.
Hiki kitu kina nguvu kubwa sana, maana mtoto anapokuwa anajua kuwa nyuma yake mara zote kuna wazazi ambao wanafuatilia kile anachofanya, basi ni hakika kuwa huyu mtoto atajitahidi kuhakikisha kwamba anafanya vizuri. Pale mzazi anapokuwa ni shabiki namba moja wa mwanae, ni wazi kuwa mtoto anakuwa hataki kumwangusha mtoto wake kwenye kile anachofanya

Tujenge utaratibu wa kufuatilia. Kazi za wanetu
Kama mzazi na mtu ambaye anaanda kizazi kijacho cha vijana, basi ni muhimu sana ukajenga utaratibu wa kufuatilia vitu ambavyo mwanao anakuwa anafanya. hata michezo ya kawaida, vinampa nguvu kubwa sana, lakini wakati huo vinamwepusha kufanya mambo ambayo siyo maana anakuwa anajua kuna mtu nyuma yangu ambaye anafuatilia kila ninachofanya.
Kwenye kitabu chake cha Think Big, mwandishi Ben Carson anaeleza namna ambavyo mama yake alikuwa akifuatilia kazi zake anazofanya na hat kumpa kazi ya kusoma vitabu viwili kila wiki. Hiki kitu tu, kilimfanya kijana huyu ajenge utaratibu wa kusoma vitabu, kitu ambacho baadaye maishani mwake kilikuja kuwa chenye manufaa makubwa sana kwake. Katika harakati za kuandaa kizazi kijacho, tunaweza kujifunza hapa pia.
Siku moja kwenye kundi mojawapo la whatsap kulikuwa na mjadala wa namna ya kuandaa kizazi kijacho, ila walikuwa wakizungumzia zaidi kwa upande wa fedha na uwekezaji. Kutoka kwenye huu mjadala nimeona nikushirikishe kipande kimoja muhimu sana ambacho na unaweza kunufaika nacho.
…..kufundisha watoto ni raha sana
…take it easy as a game play
Mfano:
Unawapa Task eg.MAKING MONEY
1) Mwambie somo lolote akipata above 90%… ana jishindia Tzs10,000.Hivyo more 90% means more money..getting rich
2) Na hizi pesa ….yeye ndio ana keep recprds kwenye note book yake.Humpi cash.Akitaka kuspend kwenye toys anapunguza kwenye balance yake.
3) Mshindanishe na nduguze.They will all improve the grades….enjoy the proces,stay motivated….while learning about Money, practically….with adrenalin pump
5)Pia mpe vitabu kuhusu Money ,Investments na Self Development…….. kila kitabu akimaliza aandae presentation…..anakuhadithia, [akifanya vizuri] mzawadie Tzs15,000 [kwa] kila presentation…..utashangaa walivyo smart na idadi ya vitabu atakavyosoma
6) Akifika 18yrs, akapata NIDA, immediately …mpe balance yake…anaanza trading and investment….on his own…..tena kwa pesa yake aliyoitengeneza mwenywewe.
*Money Runs The world…..kids enjoy earning it too*
…i have tested it…several times…. it works very well….. kids are lovely learning partners.Utajikuta na wewe unajifunza mengi ili kumlainishia…akuelewe..same time mna tengeneza bonge la parent-child relationship
…also gets you to learn human behaviour arround money & investments via little beings
…ukija baadae kumfundisha technical and fundamental approaches…..hashangai chochote….kuhusu patterns,candlestics,risk management,money psychology,sentiments etc….kwani ulianzia kwenye DNA of money….yaani X & Y chromosomes of money , to be specific
Maisha yanapokupa limau unatengeneza juisi
Mzee mmoja baada ya kuona kwamba umri wake umeenda na hawezi tena kuingia uwanjani na kuanza kujifunza mpira, aliona atatumia kipaji chake kufundisha watoto na vijana mpira wa miguu, hivyo alijifunza ukocha wa mpira wa miguu na kuanza kutoa mafunzo kwa kizazi kijacho. Baada ya hapo alienda mbali zaidi na kuwa na shule maalumu ya kuwafundisha vijana na kuandaa kizazi kijacho. Kwa jinsi hiyo hakuruhusu kipaji na uwezo wake ufe bila ya yeye kuutumia kama ambavyo alikuwa anatakiwa kuutumia.
Wewe pia pengine umri wako umeenda na unaona kwamba huwezi kurudi nyuma na kuanza kunoa kipaji chako upya, ila kitu kimoja cha uhakika ni kuwa kuna namna unavyoweza kusaidia kizazi kingine huku wewe ukinufaika pia.
Pengine unaweza hata kuandka kitabu na kutoa mafunzo kwa vijana na kuwaasa wasifanye makosa kama ya kwako uliyofanya kwenye kunoa na kuendeleza kipaji chako.
-
Ukipenda pesa, lazima upende na kazi

Rafiki yangu mpendwa, vitu vingi vilivyo hapa duniani huwa vinaenda viwili viwili.
Mfano ukiongelea juu, lazima kuwepo chini.
Ukisema mbele lazima kuna nyuma
Ukizungumzia kulia sharti kuwepo kushoto piaSasa hiki kitu kina funzo kubwa sana kwetu na hasa kwenye kutafuta fedha na mafanikio.
Na ujumbe ni kuwa ukipenda fedha lazima upende kazi.Ni wazi kuwa huwezi kupata fedha bila ya KUWEKA kazi kwanza. Lakini pia ili upate fedha zaidi Unapaswa kuijua misingi ya fedha kwenye uwekezaji, na kuifanya fedha ukifanyie kazi zaidi. Komaa humohumo.
Fanya kazi kwa bidii
Pata pesa.
Weka akiba
Wekeza
Rudia tena hayo.Kila la kheri
Godius Rweyongeza -
KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kukigundua, Kukinoa Na Kukitumia Kipaji Chako Kwa Manufaa

Kwenye kurasa za kitabu hiki nimeeleza kipaji kwa kina kiasi kwamba kama kitabu hiki anakisoma mtoto wa miaka sita aweze kunielewa.
Kwenye sura ya kwanza nimeanza kwa kueleza kwamba kipaji ni kitu gani? Ambapo nimeeleza dhana nzima ya kipaji na jinsi kinavyofanya kazi.
Kwenye sura ya pili nimeeleza namna ambavyo unaweza kugundua kipaji chako. Je, unajiuliza ni kwa namna gani ambavyo unaweza kugundua hicho kipaji chako? Basi nenda moja kwa moja kwenye sura ya pili.
Kwenye sura ya tatu nimeonesha mbinu unazoweza kutumia kwenye kunoa na kuendeleza kipaji chako. Hapa utakutana na mbinu za kukusaidia wewe kuweza kupeleka kipaji chako mbali. Na kwenye sura ya nne tutaona kwa nini watu hawathamini vipaji vyao.
Kwenye sura ya tano tutaona mbinu zitakusaidia wewe kutengeneza fedha kwa kutumia kipaji chako.
Tunaishi kwenye ulimwengu wa intaneti. Na hapa tutaingia kwenye sura ya sita ambapo tutaona namna ambavyo unaweza kupeleka kipaji chako kwenye mtandao na kunufaika na intaneti.
Kwenye sura ya saba tutaona kipaji na elimu. Kwa nini elimu inapewa kipaumbele zaidi kuliko kipaji na je, kuna ulazima wowote wa kuendeleza kipaji chako au ukomae tu na elimu?
Uko tayari kwa ajili ya safari hii ya kipekee? Basi wacha tuianze kama ifuatavyo.
-
KIPAJI NI DHAHABU:Jinsi Ya Kukigundua, Kukinoa Na Kukitumia Kipaji Chako Kwa Manufaa
∞∞∞∞∞UTANGULIZI∞∞∞∞∞

Nakumbuka mwaka 2013 nilikutana na vijana wenzangu ambao walikuwa kwenye mjadala mkali kuhusiana na Messi, Ronaldo na Neymar. Kwenye mjadala huu walikuwa wakijadili kuhusiana na uwezo wa wachezaji hawa, huku wengine wakisema kwamba Messi na Neymar wana kipaji ila Ronaldo akiwa anatumia nguvu.
Nadhani kama wewe ni mpenzi wa soka, mijadala kama hii utakuwa unaifahamu ambavyo huwa inatokea sana. Na jinsi ambavyo huwa inateka umakini wa watu.
Kwenye mijadala kama hii watu huwa wanatoa hoja zao kwa nguvu kuonesha kwamba mchezaji fulani ni mzuri na ana kipaji kuliko mwingine.
Mijadala mingine ya aina hii huwa ni mijadala ya wasanii, ambapo huwa wanalinganishwa wasanii wawili. Umewahi kushiriki mjadala kama huo?
Hivi kwanza wewe mwenyewe unakijua kipaji chako?
Mjadala kama huu ndio ulinifanya nitafakari na kujiuliza hivi mimi mwenyewe nina kipaji gani? Je, hawa wanaozungumzia kipaji cha Messi, Neymar na Ronaldo wanajua vipaji vyao? Ukiwauliza wewe una kipaji gani wanaweza kukujibu? Na tokea hapo nikaianza safari ya kujitafuta ili niweze kujua kipaji changu. Maswali kama kipaji ni nini? Hivi ni kweli kila mtu amezaliwa na kipaji au kuna baadhi ya watu wachache tu ambao wamebarikiwa ndio walizaliwa na kipaji? Kipaji ni kitu cha kuzaliwa nacho au unaweza kukipata ukubwani?
Safari hiyo tu imenifunza mengi ambayo unaenda kukutana nayo kwenye ebook hii hapa ya kipekee.
Kila Mtu Kazaliwa Na Kipaji Ila Hapaswi Kulinganishwa Na Mwingine
Nakummbuka Albert Einstein aliwahi kunukuliwa akisema kwamba kila mtu ni gwiji, ila tatizo ni pale ambapo unamhukumu samaki kwa uwezo wake wa kupaa.
Hapo ndipo nilipogundua kumbe mimi na wewe tuna vipaji, ila sasa kipaji changu hakiwezi kufananishwa wala kulinganishwa na wewe.
Ni wazi kuwa kwa vyovyote vile samaki hawezi kuwa gwiji kwenye somo la kupanda mti, kupaa wala kukimbia. Yeye uwezo wake mkubwa upo kwenye kuogelea na huko lazima atafanya vizuri tu.
Sasa hivyo hivyo kwa kipaji chako. Hakiwezi kulinganishwa na mtu mwingine, unacho wewe na ni kwa ajili yako tu. Hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuwa na kipaji kama cha kwako.
Mgawanyo Wa Kitabu
Kwenye ebook hii hapa nimeeleza kipaji kwa kina hasa ili hata kama ebook hii anaisoma mtoto wa miaka sita aweze kunielewa kuhusiana na kipaji.
Kwenye sura ya kwanza nimeanza kwa kueleza kwamba kipaji ni kitu gani? Ambapo nimeeleza dhana nzima ya kipaji na jinsi kinavyofanya kazi.
Kwenye sura ya pili nimeeleza namna ambavyo unaweza kugundua kipaji chako. Je, unajiuliza ni kwa namna gani ambavyo unaweza kugundua hicho kipaji chako? Basi nenda moja kwa moja kwenye sura ya pili.
Kwenye sura ya tatu nimeonesha mbinu unazoweza kutumia kwenye kunoa na kuendeleza kipaji chako. Hapa utakutana na mbinu za kukusaidia wewe kuweza kupeleka kipaji chako mbali. Na kwenye sura ya nne tutaona kwa nini watu hawathamini vipaji vyao.
Kwenye sura ya tano tutaona mbinu zitakusaidia wewe kutengeneza fedha kwa kutumia kipaji chako.
Tunaishi kwenye ulimwengu wa intaneti. Na hapa tutaingia kwenye sura ya sita ambapo tutaona namna ambavyo unaweza kupeleka kipaji chako kwenye mtandao na kunufaika na inatenti.
Kwenye sura ya saba tutaona kipaji na elimu. Kwa nini elimu inapewa kipaumbele zaidi kuliko kipaji na je, kuna ulazima wowote wa kuendeleza kipaji chako au ukomae tu na elimu?
Uko tayari kwa ajili ya safari hii ya kipekee? Basi wacha tuianze kama ifuatavyo.
-
Ugunduzi mkubwa wa Zama Hizi…

Rafiki yangu moja ya ugunduzi mkubwa wa Zama Hizi ni kuwa wewe unaweza kubadili maisha yako na kuwa vyovyote vile unavyotaka.
Unaweza kuwa Tajiri
Unaweza kuufikia Uhuru wa Kifedha
Unaweza kuwa na mahusiano mazuri
Unaweza kuwa na familia bora n.k.Rafiki yangu yangu, hakuna ukomo wa vile unavyoweza kuwa au kufikia kwenye maisha. Labda tu ukijiwekea ukomo wewe mwenyewe.
Kitu chochote ambacho akili yako inaweza kushikilia na kukikubali, ujue kuwa hicho kitu kinaweza kufikiwa.
Sasa labda nikuulize wewe, ni kitu gani unataka kufikia maishani mwako? Kiandike chini kisha anza kukifanyia kazi. Kumbuka,
unaweza kubadili maisha yako na kuwa vyovyote vile unavyotaka.Umekuwa nami rafiki yako,
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz

l
-
Usifanye kitu mara moja…

Kama unataka kubobea kwenye kitu, usifanye hicho kitu mara moja. badala yake kifanya mara kwa mara na kwa mwendelezo. Kadiri unavyofanya kitu au kazi mara kwa mara inakupa nguvu na ufanisi na hata kujiamini.
Marudio yako kwenye kufanya kazi yanakufanya uzidi kubobea na hatimaye unakuwa bingwa.
Mchezaji bora wa mpira wa miguu siyo yule ambaye anafanya mazoezi mara moja, kisha akatulia. Bali ni yule anayefanya mazoezi ya mara kwa mara.
Mwimbaji mzuri siyo yule anayeimba mara moja, kisha akasahau.. bali yule anayefanya mazoezi ya kuimba mara kwa mara.
Hata kama unajua wazi kabisa kuwa una kipaji kikubwa cha kufanya vitu, usifanye hicho kitu mara moja, kisha ukatulia, kuwa na mwendelezo kwenye kazi au kile ambacho unakifanya. Kadiri unavyokifanya kwa mwendelezo ndivyo unavyokuwa mbobevu.
Unataka kuwa mwandishi mbobevu, basi usiandike mara moja tu na kutulia, badala yake andika mara kwa mara na maandiko mengi kadiri uwezavyo.
Unataka kufikia uhuru wa kifedha? Usiweke akiba mara moja na kutulia, au usiwekeze mara moja kisha ukasahau kila kitu, badala yake endelea kuweka akiba mara na kila unapopata fedha mfukoni.
Unataka kuwa mwimbaji wa kimataifa? Usiimbe mara moja tu na kusahau, kuwa na mwendelezo wa kile unachofanya.
Rafiki yangu, mkusanyiko wa hivi vitu vidogovidogo unavyofanya mwisho wa siku vinakuwa vitu vikubwa, kweli.
Hiki ni kitu kilichonisukuma kuandika kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA. Kitabu ambacho nina uhakika kitakusaidia na wewe kwenye hii safari ya kufanya makubwa
Pata nakala yako siku ya leo, utanishukuru siku zijazo.
Nakala moja ni elfu 20,000/- tu za kitanzania. Utatumiwa popote pale ulipo. Kupata nakala hii, utatuma fedha kwa namba 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA
Mara tu baada ya kutuma fedha yako utatutaarifu, ili tukutumie nakala ya kitabu hiki. Unakipokea popote pale ulipo duniani.
Ubora ni kuwa kuna audiobook pia. Je, ungependa kupata audiobook ya kitabu hiki cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA? Kama jibu lako ni ndio, basi umeshakipata mpaka hapo. Tuma elfu kumi tu kwa ajili ya audiobook, itume kwenda nambari ya simu 0684408755.
Kumbuka. Hardcopy inauzwa kwa elfu 20,000/- na audiobook inauzwa kwa elfu kumi (10,000/-) tu.
Kila la kheri.



-
Uchambuzi Wa Kitabu: 25 Hours a Day; Going One More to Get What You Want

Mwandishi: Nick Bare
Mchambuzi: Hillary Mrosso
Simu: 255 683862481UTANGULIZI
Karibu katika uchambuzi wa kitabu bora sana cha 25 Hours a Day. Kikiwa na maana ya kwenda hatua moja zaidi kupata kila unachokitaka. Mwandishi ametumia uzoefu wake wa kijeshi kutengeneza nidhamu kubwa kwenye maisha yake binafsi, maisha ya biashra na mafanikio. Kama unavyojua jeshini kikubwa ni nidhamu ya kufanya mambo. Jeshini hawataki maelezo kwanini umeshindwa kufanya jambo ulilotakiwa kufanya, jeshini ni matokeo ndio yanayotakiwa. Kama umekosa nidhamu, umakini, kujituma, na hamasa ya kufanyia kazi ndoto zako. Basi hiki ndio kitabu kinachokufaa zaidi kukisoma.Katika uchambuzi nimekuandalia mambo 75 niliyojifunza katika kitabu hiki. Karibu tujifunze.
- “Usipomlilisha ng’ombe wako atakufa”. Hii ni kauli inayotumika kila eneo la maisha, usipolisha ndoto zako zitakufa, usipolisha biashara zako zitakufa, usipolisha kampuni yako itakufa. Maana yake vitu havitatokea tu kwenye maisha yako bila kuvifanyia kazi ili vitokee.
- Vitu vikubwa unavyoviona vimetokea kwa watu wengine inamaana kuwa walivifanyia kazi, waliingia gharama kubwa kuvifanya vitokee. Jifunze kupitia wao, hasa uvumilivu na nidhamu iliyowafanya wafikie ndoto zao.
- Ili uweze kufanyia kazi ndoto zako lazima uwe na umiliki mkubwa wa muda, usikubali mambo na changamoto zikupeleke zinavyotaka, unatakiwa kushika usukani, uwe dereva na ufanye yale yalio ya muhimu kufikia ndoto zako.
- Kila unachotamani kukifanya kwenye maisha yako, itakuhitaji kujitoa vya kutosha kabisa. Mfano, mwandishi wa kitabu hiki Nick Bare anasema, chochote alichotamani kwenye maisha yake, aliingia gharama na kujitoa kukifanyia kazi kwa asilimia 100.
- Mwandishi wa kitabu hiki cha kipekee Nick Bare anasema, hakuna anayefanikiwa kwenye maisha yake kwa kutofanya chochote. Hakuna mafanikio yatakuja kwako ukiwa umekaa tu au umesimama tu, mafanikio yanataka ujitoe kwa viwango vya juu sana.
- Tunatakiwa kuwa na shauku na njaa kali sana ya kufanikiwa na kufanyia kazi malengo na ndoto zetu, chochote unachoona unapaswa kukifanya ili ufanikiwe unatakiwa kujitoa kwa asilimia zote ili ufanikiwe.
- Mwandishi anasema, vifuatilie vitu vigumu unavyotakiwa uvifanye ili ufanikiwe kwenye maisha yako. usiache magumu ndio yakufuate wewe, wewe ndio unatakiwa kuyafuata magumu na kuyatatua ili ukue na kufanikiwa.
- Kuwa tayari kukabiliana na mambo magumu na vikwazo kwenye safari ya maisha yako; mafanikio yamejificha kwenye mambo magumu yaliyopo kwenye maisha yako.
- Kuwa tayari kupokea upinzani kutoka kwa watu wako wa karibu, maana wanaweza kukukatisha tamaa, wanaweza kukuumiza, wanaweza kukutenga, wanaweza kukuonea wivu; mwandishi anasema kuwa tayari kukabiliana nayo.
- Kuna wakati miili yetu inachoka na inapeleka taarifa kwenye fahamu zetu ili tusitishe tunachokifanya. Mwandishi anasema, hali hiyo ikitokea hutakiwi kuacha unachokifanya badala yake unatakiwa kuendelea kufanya kazi.
- Mafanikio hayaji kwa watu wanaoacha kufanya jambo ambalo linawapeleka kwenye mafaniko yao pale wanapochoka. Mafanikio yanakuja pale unapoenda zaidi ya uchovu unaoupata kwenye mwili wako.
- Akili yako haitakiwi kukubaliana na kila kinacholetwa na mwili, kuna wakati akili zinataka tuendelee kufanya kazi na kujituma, lakini mwili hautaki unakwambia umechoka, unakuletea uchovu, maumivu, usingizi. Bare anasema, unatakiwa kuwa na nguvu juu ya mwili wako ili kufanyia kazi ndoto zako.
- Nick Bare, anasema wakati wakiwa katika ratiba za kijeshi, huwa hawaachi kwasababu wamechoka, au miili yao inaleta maumivu, wanaacha pale wanapokamilisha ratiba ya siku au jambo hilo au mtu anapoumia au kuvunjika.
- Ili kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa, nguvu za mwilini pekee hazitoshi, tunatakiwa kuwa na nguvu za akili ambazo hazitakubaliana na taarifa za mwili kwamba tumechoka, tunaumia, tunahitaji kupumzika, tuna njaa.
- Bare anatufundisha kuwa akili ndio inatakiwa kuendesha mwili na sio mwili uendeshe akili. Akili ikiwa na nguvu na ushawishi itakutoa kwenye kufanya mambo ya kinyonge, utajituma sana, utaondoka kwenye comfort zone.
- Furaha kubwa tunaipata pale tunapotatua mambo magumu kwenye maisha yetu. Zifuatilie ndoto unaziona ni ngumu kwenye maisha yako, ifuatilie biashara uanayoina ni ngumu kwenye maisha yako kuifanya, ifuatilie kazi unayoina ni ngumu kuipata au kuifanya na uifanye; endapo utafanikiwa kuvuka hapo utakuwa mwenye furaha sana.
- Nick Bare ansema, juhudi na kujitu kwenye maisha yake kunatokana na mfano mzuri kutoka kwa wazazi wake ambo walikuwa wanafanya kazi kwa bidii sana. Bare anasema kuna wakati anamuona baba yake akifanya jambo kwa kujituma kwa muda mwingi kuliko ilivyo kawaida.
- Ukiusikiliza mwili wako kwenye kila taarifa inayokupa hutaweza kukabiliana na mambo magumu yatakayotokea maishani mwako, hutafurahia mafanikio makubwa, utakuwa mtu wa kawaida na masikini.
- Usighairishe mambo muhimu kwenye maisha yako, usikatie tamaa ndoto zako au mafanikio yako. Kuwa msitari wa mbele kabisa kutetea ndoto zako, jitoe kwa isivyokawaida ili kufikia mafanikio yako.
- Unatakiwa kuwa na ufahamu wenye nguvu sana ili uamue kufanya mambo muhimu kwenye maisha yako. Usipofanya hivyo mwili utakunyanyasa sana, na hutaweza kufikia mafanikio yako unayoyatamani.
- Yafanye maumivu unayoyapata mwilini mwako ndio yawe mafuta, yawe kichocheo cha wewe kuzidi kusonga mbele na sio yawe ndio njia ya kuacha kufanya ulichokuwa unafanya. Yafanye maumivu yakusukume kuchukua hatua za ziada zaidi.
- Zivunje rekodi zako mwenyewe, vunja ukomo uliojiwekea, sehemu ambazo uliona huweza kuzifikia dhamiria kuzifikia hata kama ni kwa maumivu makali, utajiona mwenye furaha sana utakapofikia matumizi makubwa ya uwezo wako.
- Ondoa kabisa ukomo unaoletwa na mwili wako, hata kama mwili wako unakuomba upumzike au uache jambo muhimu unalolifanya kwasababu ya maumivu au uchovu, usikubali, ufanye mwili wako uwe sehemu kubwa ya kukulea mafanikio makubwa unayoyatamani.
- Usikubali mwili wako uwe kikwazo cha wewe kufikia ndoto zako, dhibiti hisia za mwili wako na ulazimishe mwili wako kufuata ratiba yako muhimu.
- Kabiliana vikali na hisia za uchovu na raha ambazo mwili unataka uzifuate ili uache kufanya mambo muhimu kwenye maisha yako. kabiliana vikali sana dhidi ya comfort zone.
- Mwandishi anaseama, alipoteza fedha nyingi, muda mwingi, na masaa mengi ya kulala alipokuwa anapambana kusimamisha biashara yake ya virutubisho, lakini hakukata tama hata siku moja.
- Mafanikio tunayoyataka kwenye maisha yetu yatatugharimu vingi sana, hvvyo ili kuyafikia hatutakiwi kuwa bianadamu wa kawaida, tunatakiwa kuwa wavulivu sana na kujifunza kwenye kila mabaya na mazuri yanayokuja.
- Bare anakiri kufanya makosa mengi sana kwenye safari yake ya mafanikio. Lakini anasema kwa kiasi kikubwa makosa hayo yalimfanya awe imara na kuongeza umakini kwenye kazi zake.
- Bare anasema, dhambi kubwa sio kufanya makosa, bali dhambi kubwa ni kufanya makosa na kutojifunza kutokana na makosa hayo.
- Makosa ni kiashiria kuwa kuna vitu unavifanya kwenye maisha yako, sehemu yenye usalama hakuna ukuaji, hakuna mapinduzi ya kweli hakuna mabadiliko.
- Watu wengi wanaona jambo zuri au kitu kizuri na kuishia kusema “natamani” ningefanya kama vile ili kuwa kama yeye, mwandishi anasema ondoa natamani au wish, fanya kazi inayohitajika kufika unayoyatamani kwenye maisha yako.
- Weka matendo kwenye matamanio yako, hakuna kitakachotokea kwa kuishia kutamani pekee. Wekeza nguvu, umakini na akili zako kwenye kufanyia kazi yale unayoyotamani kwenye maisha yako.
- Kama kweli una dhamira ya dhati kufikia mafanikio makubwa, basi unatakiwa kuachana na mambo yasio na tija kwenye maisha yako, weka kando kabisha mambo yote yasiyochangia ukuaji wako, au mafanikio yako.
- Watu wenye mafanikio wanaona mwanga na furaha kubwa iliyopo mbele ya changamoto wanazopitia. Hii ndio huwafanya wawe wavumilivu kukabiliana na changamoto wanazokuna nazo.
- Nick Bare anasema katika shule ya kijeshi alijifunza mambo magumu sana, alipitia nyikati nyingi ngumu na za giza ambazo zilimfanya imara sana. Mafunzo hayo aliyojifunza akiwa jeshini ndaio kwa kiashi kikubwa anayatumia katika kufanya jambo lolote hata kuanzisha kampuni yake ya Virutubisho.
- Kikubwa alijifunza nidhamu, bila nidhamu huwezi kukamilisha jambo lolote. Wengi wanashindwa kufanya makubwa kwenye maisha yao kwa sababu hawana nidhamu ya kuvumilia na kukaa kwenye jambo wanalolifanya ili likamilike.
- Nidhamu itakufanya kukabiliana na kuishi kwenye nyakati ngumu na kufanyia kazi malengo yako, nidhamu itakufikisha kwenye kilele cha ndoto zako.
- Mwandishi wa kitabu hiki anashuri tujifunze kama mashine. Anasema jigeuze uwe kama mashine linapokuja suala la kujifunza na kujiongeze maarifa.
- Hakuna kitu muhimu kwenye maisha yetu kama muda. Muda ndio huamua mafanikio yetu, muda ukishaenda hauudi tena. Muda ni maisha. Utumie vizuri kufanya yale muhimu kwenye maisha yako.
- Ili uwe na matumizi mazuri ya muda wako jifunze kuweka vipaumbele. Vipaumbele ndio vitakufanya utumie muda wako vizuri na kwa ufanisi mkubwa.
- Mwandishi anasema kwenye jambo lolote unalotaka kufanya kwenye maisha yako, kuna taarifa nyingi kuhusu jambo hilo kwenye mitandao kama google, youtube, nk. hivyo usiogope kuanza kwasababu ya kukosa taarifa.
- Bare anasema hana tabia ya kuhaika kuwatafuta watu hovyo ili kuuliza mawali au kuomba ushauri. Anasema kabla ya kufanya hivyo huwa anaingia kwenye mitandao na kuanza kutafuta taarifa za jambo hilo kwanza.
- Mwandishi Bare anasema, tunatakiwa kufaidika na fursa zilizopo mtandaoni za kujifunza, anasema kuna mitandao mingi sana ya kijamii kwa ajili ya jambo lolote lile, itumie kusaidie, mfano wa mitandao hiyo ni websites, podcasts, books, blogs, vlogs, YouTube.
- Kwa kujifunza utaokoa gharama kubwa sana unazaoweza kuingia, tafuta taarifa za awali wewe mwenyewe kwanza. Jipe Jukumu la kujielimisha ili uondoe mambo ambayo huyajui kuhusu kazi yako, biashara yako, afya yako, au fedha.
- Kujifunza ni uwekezaji muhimu sana kwako binafsi, wekeza kwenye kujifunza na kupata maarifa ya kutosha kuhusu jambo unalotaka kulifanya.
- Bare anasema kipndi akiwa katika mafunzo ya kijeshi huko Korea, alitumia muda wake wa ziada kujifunza sana namna ya kutengeneza kampuni, namna ya kutengeneza videos nzuri, namna ya kuchukua video, kuongea na kufundisha.
- Tumia muda wako wa ziada kujifunza sana, jua sana kila unachokifanya, kuwa na taarifa za kutosha kuhusu jambo hilo. Wekeza kwenye maarifa, jifunze kila siku kama mashine.
- Kuna maarifa bora sana katika kipindi hiki kuliko nyakati zote zilizowahi kupita hapa duniani. Bare anasema kipindi cha zamani watu walikuwa wanatunza na kuhifadhi taarifa kama dhahabu, lakini zama hizi mambo ni tofauti kabisa kila mtu anaweza kuwa na taarifa anazozitaka.
- Jilazimisha sana kupata maarifa, tengeneza kiu kali ya kujifunza, na kwa kufanya hivyo utakuwa mtu bora sana.
- Jua kwa hakika ni taarifa gani unazihitaji, na ukianza kuzitafuta zingatia hilo, usiwe mzururaji, na hujui unatafuta taarifa gani, usije kupoteza muda wako wa thamani.
- Maisha sio kitufe fulani unajibonyezea tu na mambo yanaenda, maisha sio hisia hisia fulani tu. Maisha yanataka kujitoa sana, maisha yanataka kazi kweli kweli, maisha hayataki njia za mkato. Maisha yanataka ufanye vitu, ufanye kazi ili mambo yatokee.
- Kuna watu wanahisia kwamba kwajinsi walivyo au kwa namna walivyo basi wanastahili kutunukiwa mambo mazuri kwenye maisha yao.
- Hakuna anayejali kuhusu wewe, hakuna anayekosa usingizi kutokana na shida zako. Hivyo amka pambana na ndoto zako umiliki maisha mazuri unayoyataka.
- Acha kuwa na mategemeo kuwa kwasababu upo mahali fulani, au uko na mtu fulani basi utakuwa na maisha mazuri au unastahili maisha mazuri. Fanyia kazi ndoto zako zinazokunyima usingizi, furaha na amani.
- Hakuna atakayekuja na furushi la fedha au dhahbu akupe akwambie,unajua wewe ni mtu mzuri sana au wewe ni mpole au mwema sana basi chukua hizi fedha kama zawadi, jambo hili haliwezi kutokea kwako; mambo mazuri hayaji usipojisukuma fanya kazi kubwa kufikia mafanikio unayoyataka.
- Kuna wengine wameridhika na vyeo walivyo navyo na kujiona wameshapata kila kitu. Hivyo wanakuwa na kiburi hawataki kujituma tena, wanaona wamefika. Mwandishi anasema hakuna kitu kibaya kama kupata cheo na kujisahau na kuacha kutumia uwezo wako kufanya mambo makubwa.
- Mwandishi anasema kuna wakati anaona hajapata kile anachokitaka, anachofanya ni kuwafikiria wale walio na kitu hicho na gharama kubwa walioingia kupata kitu hicho. Kwa kufikiria hivyo anajisukuma zaidi kufanyia kazi malengo yake.
- Kama umeshindwa kuzalisha fedha mwaka huu unatakiwa kujiuliza tatizo ni nini? Nini hukufanya, nini ambacho unatakiwa kufanya ili uzalishe fedha unazotakiwa kuwa nazo.
- Jua huna wa kumlaumu kwa umasikini wako, kukosa fedha, kazi au maisha mazuri unayoyataka. Jipe Jukumu la kutengeneza maisha yako yawe bora, acha lawama na uvivu.
- Jiondoe kwenye comfort zone, ondoka kabisa kwenye maisha ya usalama. Ingia kwenye mapambano, kuondoa umasikini na ujinga kwenye maisha yako.
- Kuondoka kwenye comfort zone ni kufanya zaidi ya hisia za mwili wako, hata kama unahisi umechoka au maumivu, hata kama itakugharimu upoteze masaa mengi ya usingizi, itakugharimu kuacha baadhi ya ratiba za kula, itakugharimu kuacha na marafiki wasio na mchango maishani mwako.
- Kuondoka kwenye comfort zone, ni kuweka nidhamu kali sana ili ukamilisha jambo unalolifanya hata kama huna hamu au hamasa ya kufanya jambo hilo.
- Kuondoka kwenye comfort zone ni kuacha kutoa sababu kwanini hujafanya jambo ambalo ulitakiwa kulifanya.
- Kuondoka kwenye comfort zone, ni kujisukuma isivyo kawaida katika kutumia uwezo wako wote kufikia ndoto zako na mafanikio unayoyatamani.
- Kuondoka kwenye comfort zone, ni kuacha kujihurumia, kuwa mtu wa matokeo, kuwa mtu wa matendo kuliko maneno pekee.
- Kuondoka kwenye comfort zone, maana yake ni kuachana na raha za muda mfupi kwa ajili ya kuwekeza nguvu zako zote kujenga maisha yako ya sasa na ya baadaye yawe bora.
- Kuondoka kwenye comfort zone, ni kuanzisha biashara, kuipambania na kuwa tayari kupokea changamoto zote bila kukata tamaa.
- Bila nidhamu hutawaweza kujitoa kikamilifu kufanyia kazi ndoto zako. Hutakuwa na umakini hutakuwa na muda wa kufanya mambo muhimu.
- Unapofanya jambo lolote lililopo kwenye ratiba yako, lifanye kwa nguvu zako zote, akili yako yote, hisia zako zote. Nenda mzima mzima kulifanya jambo hilo.
- Usifanye jambo huku nusu ya akili yako ipo kwenye mambo mengine, unapojitoa jitoe kweli na sio nusu nusu. Zamia kabisa hadi jambo unalolifanya liishe.
- Toa asilimia 100 za umakini wako, akili yako, nguvu zako, kwa kufanya hivyo utazalisha kazi bora, na ufanisi wako utakuwa wa Kiwango cha juu sana.
- Unapjitoa asilimia 100 kwenye kufanya jambo lolote, maana yake utakuwa na wakati mzuri wa kutumia uwezo wako wa zaida uliolala, ubunifu wako na nguvu zako zilizolala ambazo hukujua kama unazo.
- Usikubaliane na ukomo uliojiwekea kwamba ndio mwisho wako hapo. Usikubaliane na maoni ya watu walioweka ukomo kwenye uwezo wako. Hapa una jambo kubwa la kuwahahikishia kuwa hawakuwa sahihi kukuwekea ukomo kwenye maisha yako.
- Weka jitihadi za ziada kuwenda mbali kabisa na ukomo uliojiwekea na waliokuwekea watu wengine. Wewe una uwezo wote wa kufanya makubwa na kufanikiwa kwa viwango vya juu sana.
- Kila siku inayokuja kwenye maisha yako, hakikisha unaishinda siku hiyo, hakikisha unapata ushindi, usiache siku hiyo ikushinde. Maana yake fanya yote muhimu uliyoyapanga kuyafanya ndani ya siku hiyo.
Asante kwa kusoma uchambuzi wa kitabu hiki, mshirikishe na mwingine maarifa haya.
@Hillary Mrosso_09.09.2022
-
Aina Tatu Za Ujuzi Unaohitaji Ili Kuongeza Thamani Yako Na Kula Mema Ya Nchi
Kwenye hii makala ningependa tuongelee aina tatu za ujuzi ambao ukiwa nao kwenye hizi zama ni wazi kuwa unaenda kufanya vizuri na hata kuweza kufikia viwango vikubwa na vya hali ya juu sana kuliko unavyotegemea. Najua umewahi kushauriwa kujifunza aina nyingi za ujuzi, ila kwenye aina hizo zote za ujuzi ambao umewahi kushauriwa kuwa nao, hapa kuna aina tatu tu za ujuzi ambapo ukiwa na ujuzi mmojawapo ni wazi kuwa utaweza kufika mbali na hata kufanya makubwa zaidi.
Kama umewahi kusikia kuwa kuna watu wanakula mema ya nchi, basi kwa aina hizi za ujuzi ambao utajifunza hapa, ukiweza kuzifanyia kazi vizuri, ni wazi kuwa na wewe lazima tu utaenda kula mema ya nchi. Nadhani mpaka hapo umenielewa vizuri. Sasa aina zenyewe za ujuzi hizi hapa:

Ujuzi wa kwanza ni ujuzi wa uandishi.
Na hapa siyo tu kuandika, bali kuandika ilimradi umeandika, bali kuandika andiko ambalo linavutia na linashawishi watu kusoma na hata andiko ambalo linasukuma watu kutoa fedha mfukoni na kukulipa wewe.
Lakini ngoja kwanza tujiulize hili swali la muhimu
Uandishi Ni Kitu Gani?
Uandishi ni ujuzi wa kuwasilisha mawazo kwa watu kwa lengo la kuhamasisha, kuelemisha, kuburudisha, kuchekesha au lengo lolote lile analokusudia mwandishi.

Uandishi umebaki kuwa ni ujuzi muhimu sana kwenye uliwengu wa leo. Mbali na kuwa sasa hivi kuna watu wanapenda kuangalia video kwenye mitandao inayoonesha video kama youtube na tiktok, au picha kwenye mitandao ya picha kama instagram, ila ukweli ni kwamba, uandishi unabaki kuwa moja ya ujuzi muhimu sana kwenye zama za leo. Uandishi haujachuja na pengine ni ujuzi ambao unaweza kukutoa wewe hapo.
Zama Zimebadilika
Kwanza nipende kutangulia kwa kusema kwamba tunaishi kwenye ulimwengu ambao umebadilika sana. Yes sure, ulimwengu wa sasa umebadiika sana kuliko ilivyokuwa zamani. Kuna kipindi ambacho watu walikuwa wanawinda kwa ajili ya kupata chakula.
Baadaye kikaja kipindi ambapo watu walikuwa wanalima kupata chakula, na tena baadaye kikaja kipindi ambapo watu walikuwa wanafanya kazi viwandani kwa ajili ya mshahara ambao ungetumika kununu chakula. Ulimwengu wa sasa hivi umehamia mtandaoni. Na hata unasoma makala hii mtandaoni.
Uandishi umebaki kuwa mfalme kwenye ulimwengu huu wa mtandao. Kwa hiyo hizi picha zinazosambaa mtandaoni na kuvuma, hazisambai tu kwa ajili ya kusambaa, nyingi zinazosamba, utakuta kwamba zina maneno fulani, hata kama maneno kidogo. na hayo maneno yanaandikwa au kuandaliwa na mtu mwenye uelewa mzuri wa uandishi. Kwa hiyo vitu kama nukuu au maandishi mengine yanayosambaa kwa kasi, niseme pia ni sehemu ya uandishi. Ukiujua uandishi vizuri vitu vingine vidogo havitakuhangaisha.
Uandishi ni ujuzi wa karne ya 21
Ukiwa vizuri kwenye uandishi, hutakaa uhofie uwepo wa vitu vingine kama mitandao ya picha au video kwa sababu, huku kama mwandishi bado unafit vizuri tu.
Kwa mfano, unaweza kuandika andiko lako, na kulisoma kwa sauti au hata kuligeuza kwenye video kwa kuongeza picha na vitu mbalimbali. kwa hiyo ukajikuta kwamba unafanya vizuri kwenye ulimwengu wa uandishi lakini pia unafanya vizuri kwenye ulimwengu wa sauti na video pia.
Kwenye ulimwengu wa leo baadhi ya taaluma zinachukuliwa na mashine. Kwa mfano, taaluma ya ukarani inachukuliwa na mashine, sasa hivi kuna roboti ambazo zinaweza kufanya upasuaji, kwa hiyo kama wewe ni daktari, upo hatarini kuondolewa na mashine.
Siku hizi kuna hoteli na migahawa haina wahudumu au zina mhudumu mmoja tu. tangu unafika kwenye hoteli mpaka unatoka, unahudumiwa na mashine tu, kwa hiyo kama wewe ulikuwa ni mhudumu wa hoteli au mgahawa, kazi yako ipo hatarini…..
VIDEO FUPI YA ROBOTI ZINAVYOHUDUMIA WATEJA HII HAPA
Sasa vipi kuhusu uandishi..
Ndio, kuna roboti ambazo zinaandika pia…Hahah
Lakini ni kitu gani kinaufanya uandishi kuwa kitu cha kipekee?
Ni kweli kuna roboti ambazo zinaweza kuandika, lakini hizi roboti haziwezi kuja na kitu original (O.G). Zinaandika kwa kutumia taarifa ambazo zipo mtandaoni kwa sasa. lakini haziwezi kutengeneza kitu cha tofauti ambacho hakijawahi kuwepo…na wala hicho kitu hakitatokea kwa siku za karibuni kwa sababu uandishi ni kitu ambacho kinahusisha hisia pia.
Mwandishi anapokuwa anaandika, kuna hisia fulani hivi anakuwa nazo, kwa hiyo uandishi ni kama sehemu ya kuhamisha zile hisia na kuziweka kwenya maandishi
Mashine hazina uwezo wa kuwa na hisia
Kwa mfano mtu anayeandika juu ya sherehe ya jana iliyofana. Hisia anazokuwa nazo wakati anaandika andiko lake, ni hisia ambazo roboti haiwezi kupata.. hata kama roboti ilikuwepo kwenye sherehe, haiwezi kuwa na hisia hizo…Ebu sema oyooo…
Kwa hiyo hicho kitu kinafanya sasa uandishi uwe wa kipekee na ujuzi ambao unapaswa kuwa nao kwenye karne hii ya 21
Lakini pia kama ambavyo nimekwambia, ukijua uandishi tu, unaweza kwenda mbele na kuhakikisha kwamba, unautumia kwenye maeneno mengine kama mafunzo ya picha, mafunzo ya sauti, video n.k.
Ukiujua uandishi vizuri unaweza kuutumia kwenye mauzo na ukafaa.. unaweza kuhamia kwenye kilimo na ukaandika kitu kinachoeleweka na watu wakakisoma
Unaweza kuandika kuhusu michezo
Unaweza kuhamishia uandishi wako kwenye tasnia ya uigizaji. Yaani, popote pale utakapoenda na ujuzi wako wa uandishi, unakubalika. Hapa ningekuwa naandika kwa kimombo, ningesema the sky is the limit, ila kwa kuwa siandiki kwa lugha hiyo, naacha sisemi. hahaha
Halafu kabla sijasahau, ujue uandishi ni ujuzi ambao ukishaujua,, umeujua!
Kuna ule usemi wa kwamba kama ipo ipo tu… Ni kweli kwamba utapaswa kuendelea kunoa ujuzi wako wa uandishi mara kwa mara. Ila walau kuna kitu kimoja ambacho mimi nina uhakika nacho, uandishi ni kitu ambacho hakiwezi kuondolewa kwako… ukishaujua umeujua na unaweza kukuumia kwenye sekta yoyote ile…
Ufanye uandishi ukutambulishe kwa namna kipekee
Nimesema kwamba zama za sasa zimebadilika, nimesema kwamba uandishi ni kitu pekee ambacho kwa sasa hakitachukuliwa na roboti, lakini pia nataka niseme kwamba, utumie uandishi kukutambulisha na kujenga ujuzi mpya katika namna mbayo hakuna roboti inaweza kufanya kufanya kazi yako.
Ebu fikiria kama wewe ni daktari na tayari roboti zimeshaanza kutibu watu, sasa unaonaje ukiunganisha utalaamu wako na uandishi (idea sexing), hapa uhakika ni kwamba, uandishi unaenda kukutambulisha vizuri sana.
Kumbe kwa kuunganisha uandishi na kitu chochote kile ambacho unajua sasa hivi, utakuwa mtu wa pekee na wa tofauti sana.
Kama wewe ni mhasibu, ukiongeza na uandishi kwenye uhasibu wako, utakuwa umetengeneza kitu kingine cha tofauti.
Kama wewe ni mwalimu, ukiongeza na uandishi, utakuwa umetengeneza kitu kingine cha tofauti kabisa.
Sasa nataka kuanzia leo uanze kuufanyia kazi uandishi. Swali langu kwako unaenda kuwa unaandika kuhusu kitu gani? Ni kitu gani?
Kama mpaka hapo huelewi ni namna gani unaweza kuandika, naomba upate kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. Hiki kitabu kitakufumbua macho kwa namna ambayo hukutegemea kwenye suala zima la uandishi.
Kwenye makala hii nilitaka tu kukuonesha nguvu ya uandishi, na jinsi ambavyo uandishi ni ujuzi muhimu unaopaswa kuwa nao kwenye hizi zama tunazoishi kwa sasa.
Ujuzi wa pili ni UJUZI WA KUUZA
Huu ni ujuzi mwingine muhimu sana. Ujue kwa namna moja au nyingine katika maisha utalazimika kuuza. Ukisimama mbele ya watu kuongea ujue unauza. Ukimshawishi mtu au ukitaka mtu akubali falsafa au hoja yako basi ujue kwamba unakuwa unafanya mauzo, ukitaka kumpata mwenza lazima utatakiwa kufanya mauzo, na hata kama unahubiri bado ni uuzaji, ukitaka mwajiri wako akuongezee mshahara hayo ni mauzo pia.
Kwa hiyo jifunze namna bora ya kuuza ambayo itawafanya watu wanunue unachouza. Jua saikolijia ya watu ili ikusaidie katika aina ya mauzo unayofanya.
Ukiweza kuwa muuzaji mzuri basi ni wazi utaongeza thamani yako kwa viwango vikubwa sana. Ila kama haujui kuuza utalala njaa rafiki rafiki yangu.
Unaweza kushangaa na kujiiuliza hivi kuwa si bora niwe na bidhaa nzuri? Ndio unapaswa kuwa na bidhaa nzuri, ila kama huwezi kuiuza haitasaidia. Bidhaa nzuri bila kujua kuuza vizuri utakaa nayo wewe tu.
Kwenye kitabu cha Rich Dad Poor Dad, mwandishi amesema kwamba kuna siku alikutana na mwandishi mchanga ambaye alikuwa anataka kujua ni kwa jinsi gani anaweza kutengeneza fedha kupitia uandishi.
Kiyosaki akawa amemwambia kwamba anapaswa kujifunza kuuza. Kiyosaki aliendelea kumwambia yule mwandishi mchanga kuwa, mimi sio mwandishi bora ila muuzaji bora. Hata ukichukua kitabu changu, hakuna sehemu utakuta imendikwa kuwa mimi ni mwandishi bora. ila imeandikwa kuwa mimi ni muuzaji bora (bestselling author).
Kwa hiyo kitu kimoja cha kuondoka nacho siku ya leo ni kuwa unapaswa kuhakikisha unajifunza uuzaji.
Uuzaji ndio unaleta fedha kweye biashara na kwenye maisha ya kila siku. Bila kufanya mauzo biashara zinakufa, bidhaa zinakufa, vipaji vinapotea na mengine mengi.
Lakini kinyume chake ni tofauti, ukiweza kufanya mauzo vizuri, maana yake utapata fedha na ukiwa na fedha hakuna kitu ambacho kinaweza kukushinda kufanya. Na mauzo ndiyo yanaleta fedha.
Ukifuatilia vizuri, watu wanaolipwa zaidi hapa duniani siyo watu wengine bali ni watu wa mauzo (salesmen and women). Watu ambao wameujua vizuri ujuzi huu hawalipwi mshahara, bali wanalipwa kwa kamisheni.
Watanzania wengi hawajui malipo ya kamisheni hivyo huwa wanapenda mshahara, ila malipo ya kamisheni ukiyaelewa vizuri, unaweza kumwabia bosi wako leo aache kukulipa kwa mshahara, badala yake akulipe kwa kamisheni.
Unajua kamisheni ipoje, malipo ya kamisheni ni pale ambapo mnakubaliana na mtu uakulipe kulingana na mauzo unayokuwa unafanya. Kadiri unavyoongeza juhudi kubwa zaidi kwenye kuuza na kufanya mauzo zaidi, ndivyo ambavyo unaweza kulipwa zaidi.
Kwa mfano mkkikubaliana kuwa ulipwe kwa kamisheni ya asilimia 5, 10 au 20 malipo yako yatakuwa hivi kwa kila mauzo utakayofanya.
KAMISHENI YA ASILIMIA Mauzo 5% 10% 20% 10,000 500 1,000 2,000 100,000 5,000 10,000 20,000 1,000,000 50,000 100,000 200,000 10,000,000 500,000 1,000,000 2,000,000 100,000,000 5,000,000 10,000,000 20,000,000 Kwa aina hii ya malipo, ukomo kwenye kulipwa ni wewe mwenyewe. Yaani, wewe ndiye unaweza kuamua ulipwe sana au ulipwe kidogo kwa sababu kadiri unavyokuwa unaweka juhudi kwenye kazi ndivyo ambavyo unalipwa zaidi. hivyo, juhudi zaidi maana yake zinaleta matokeo makubwa zaidi.
Sasa unajifunzaje ujuzi huu. Anza kwa kusoma kitabu cha How I raised myself from failure to success in selling. Hiki kitabu kitakupa mwongozo na mbinu za mauzo ambazo huwezi kuzipata sehemu nyingine.
Ukizutimua mbinu zilizo kwenye hiki kitabu, ni uhakika kuwa utaweza kufika mbali, tuwasiliane kwa songambele.smb@gmail.com ili niweze kukutumia kitabu hiki usome.

Ujuzi wa tatu ni KUNENA
Siku moja kuna kijana alimwuliza Warren Buffet kuwa ni ushauri gani ambao unaweza kuutoa kwa kijana mwenye umri wa miaka 21 au 22 kuhusu mafanikio? Bila kusitasita Warren Buffet alimweleza kuwa ushauri wangu kwa kijana mwenye umri wa miaka 21 au 22 ni kuwa ajifunze na kuelewa kwa undani ujuzi wa kuwasilisha hoja kwa watu, na hii inaweza kuwa ni kwa njia ya maandishi au kuongea.
Kama umegundua kitu, ni kuwa makala hii inajihusisha zaidi na ujuzi huu mmoja wa kuwasilisha hoja zako kwa watu. ila ujuzi huu tumeugawa kwenye aina tatu ndogo za ujuzi ambapo hapa tayari tumeongelea ujuzi wa kuandika, ujuzi wa kuuza na sasa tunaongelea ujuzi wa kunena.
Huu ni ujuzi mwingine ambao unaweza kuongeza kipato mpaka asilimia 50 au hata zaidi.
- Wanasiasa
- Wafanyabiashara
- Wanamichezo na wengine wengi huwa wanatumia huu ujuzi
Huu ni ujuzi wa tatu muhimu sana. Kunena au kama kunavyofahamika kwa kiingereza ni public speaking. Huu ni ujuzi mwingine ambao ukiwa nao utaongeza thamani yako kwa viwango vikubwa sana.
Ni wazi kuwa huwa tunapenda sana watu ambao huwa wanaongea na kutoa hoja zinazovutia. Kuna mtu akisimama kuongea mwili unasisimuka kwa kuona jinsi anavyowasilisha mada yake. Hiki ni kitu ambacho na wewe unaweza kukijua na kukifanyia kazi kwa manufaa yako. Wanasiasa wanatumia sana hiki kitu wakati wa kampeni kwa ajili ya kuomba kura. Wasemaji wa timu za mpira wanatumia ujuzi huu pia kwa ajili ya kuvuta umakini kwenye vyombo vya habari.
Kila siku tunakutana na watu na tukiwa na watu hawa tunaongea, tunawasilisha na kujadili mada, tunacheka na kufurahi
Lakini unahitaji kujifunza kunena. Na kunena ni zaidi ya kuongea. Najua utauliza sasa kunena ni nini? Kwa haraka tu naweza kusema KUNENA ni KUONGEA NA WATU WAKASILIZA.
Sasa kuongea na watu wakusikilize wewe ni kazi. Na sio kazi ndogo. Nadhani imewahi kukutokea unaanza kumsikiliza mtu ila unagundua kuwa hana pointi za maana. Yaani amesimama mbele yako na wewe unaona wazi kwamba hakuna kitu cha maana anaongea.
Omba isikutokee wewe. Na namna nzuri ya kuomba ni kujifunza uneni kuanzia leo hii
Sasa zifuatazo ni mbinu saba unazoweza kutumia kwa haraka ili kuongeza ujuzi wako wa kunena.
Moja ni kutafuta fursa ya kuongea mbele ya watu, kwa kuanzia unaweza kuanza na hadhira ndogo tu watu wachache pengine hapo hapo nyumbani. Unaweza kuwakusanya ndugu zako wa karibu na kunza kufanya mazoezi mbele yao. Na hata muda mwingine siyo lazima uwaambie.
Kama huwa mnasali pamoja pale nyumbani unaweza kuwashawishi kuongeza na kipengele cha neno la Mungu, halafu kile kipande cha kufafanua neno la Mungu ukakibeba wewe, na ukautumia huo kama muda wako wa kuwasilisha yako na sehemu ya kujifunza uneni.
Lakini pia unaweza kuandaa kikundi cha watu na kuwaeleza kuwa utakuwa unafanya mazoezi ya kuongea mbele yao, hivyo unaomba wakupe mrejesho baada ya kuwa umewasilisha mada yako. Sana sana hawa wawe ni watu ambao wanaweza kukupa mrejeho bila ya kukuogopa.
Pili ni tenga muda wa kufanya mazoezi kwaa ajili ya kunoa ujuzi wako huu. Dakika kumi mpaka thelathini kila siku zitafanya kazi.
Tatu, hakikisha umeandika kwanza hotuba yako, kisha ifanyie mazoezi. Hiki ni kitu kidogo sana ila chenye nguvu kubwa sana. Kanuni muhimu kwenye kufanya mazoezi unayopaswa kuitumia ni kuwa, kama utatakiwa kuongea kwa dakika 12, basi utapaswa kujiandaa kwa dakika 120 kabla ya kutoa hotuba yako.
Nne, jifunze kwa kusoma vitabu. hiki kitu kitakufanya uongeze maarifa na kuielewa mada husika kwa undani, hivyo utaweza kuwasilisha mada yako huku ukiwa na uelewa mkubwa zaidi. Kadiri unavyosoma ndivyo unavyojua zaidi na watu wanapenda kusikiliza mtu mwenye kitu cha kusema na kadiri watu wengi wataavyokuwa tayari kukaa chini na kukusikiliza, ndivyo ambavyo kipato chako kitakuwa kinaongezeka zaidi.

Tano ukiwa kwenye kikundi cha watu, chagua mtu mmoja ambaye utakuwa unamwagalia wakati unaongea. Ujue ni muhimu sana kuangalia watu wakati uhnatoa hotuba yako, sasa ukianza kuongea mbele ya watu, kama unaogopa kuwaangalia watu, chagua mtu mmoja ambaye utamwangalia na kisha unaweza kuhama kutoka kwake na kuwangalia mwingne kadiri muda unavyoendelea.
USHAURI WANGU: Chagua aina moja ya ujuzi ambao unaweza kuanza kuufanyia kazi leo.
Usianze na kila ujuzi. Anza na ujuzi mmoja, ufikishe kwenye viwango vikubwa. Kisha kuza ujuzi mwingine. Mwisho wa siku utajikuta umeweza kujenga kila ujuzi.
Rafiki yangu hizo ndizo aina tatu za ujuzi ambao unapaswa kuwa nao.
-
Kitabu ChaNGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA: Utangulizi wa kitabu kama ulivyoandika kwenye kitabu chenyewe
Habari ya siku ya leo rafiki yangu, siku ya leo ningependa nikushirkishe Utangulizi wa kitabu cha NGUVU ya vitu vidogo kama ulivyoandikwa kwenye kitabu chenyewe. Nina hakika wewe mwenyewe utaufurahia, baada ya kuwa umesoma Utangulizi huu, usisite kujipatia nakala ya kitabu hiki kwa kuwasiliana nami mwandishi kwa simu 0755848391. Sasa utangulizi wenyewe huu hapa chini.

Gharama ya kitabu hiki ni 20,000/- za kitanzania Hivi umewahi kujiuliza kuwa vitu vidogo vinaweza kukusaidia kitu gani maishani mwako?
Hivi kwa mfano, kitu kidogo kama kuamka asubuhi na mapema kinaweza kukusaidia nini maishani mwako kikifanywa kila siku na kwa mwendelezo? Au je, kitu kidogo kama kuwekeza au kuweka akiba kikifanywa kila mara kwa muda mrefu kinaweza kukusaidia nini? Kwenye kitabu hiki hapa tunaenda kuona nguvu ya vitu vidogo na jinsi nguvu hii inavyoweza kukusaidia wewe kufikia mafanikio makubwa maishani mwako.
Mara nyingi sana watu huwa wana ndoto kubwa na malengo makubwa ya kufikia kifedha, kimahusiano, kibiashara au kikazi. Lakini cha kushangaza ni kwamba huwa hawafanyii kazi hizo ndoto kubwa walizonazo bali huwa wanasubiri itokee siku moja ya muujiza ambapo ndoto yao itatimia kwa asilimia zote.
Kitu hiki hakiwezekani. Ni wazi kuwa lako la mwaka haliwezi kutimia siku ya mwisho ya mwaka baada ya wewe kuwa umekaa mwaka mzima bila ya kufanya kitu chochote, badala yake kama kweli utaweka kazi na kufuata hatua zote unazopaswa kufuata ili kulifikia hilo lengo lako la mwaka basi utalifikia kwa kufanya vitu kidogo kidogo kila siku.
Kitu chochote kikubwa kinaweza kufanikishwa kwa kuchukua hatua ndogondogo na kwa mwendelezo na hatimaye kuzifanya ziwe hatua kubwa. Mafanikio makubwa siyo kufanya vitu elfu moja mara moja, ila kufanya vitu vidogo mara elfu moja, yaani, kwa mwendelezo na bila kuchoka. Hivi vitu vidogo hatimaye vinapelekea kitu kikubwa na mafanikio makubwa.
Confucius, mwanafalsafa wa Kichina aliwahi kunukuliwa akisema kwamba, “safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja”. Hii ndiyo kusema kwamba mambo makubwa siku zote huwa yanaanza kwa hatua ndogondogo kisha kuendelea kukuzwa. Hakuna kitu kikubwa ambacho unakiona leo hii ambacho kilianza kikiwa kikubwa hivyohivyo. Ndiyo maana wahenga walisema kwamba; “hata mbuyu ulianza kama mchicha.” Jogoo anayewika kuna siku alikuwa kifaranga.
Ukitaka kugundua kwamba vitu vikubwa huanza kwa udogo basi unaweza kuangalia ujenzi wa ghorofa. Huwa unaanza kwa hatua ndogo ndogo za kuchimba msingi, baadaye huwa wanaanza kuweka jiwe au tofali moja baada ya jingine hatimaye kitu kilichokuwa chini huwa kinaendelea kusimama na kufikia hatua ya kuwa kitu kikubwa sana.
Siku moja nilikuwa nasoma historia ya jengo ambalo limo kwenye maajabu saba ya dunia. Jengo hili siyo jingine bali ni jengo la Taj Mahal. Hili ni miongoni mwa majengo yaliyojengwa kwenye karne ya 15, na jengo lenye historia ndefu na kubwa sana. Unajua jengo hili lilijengwa kwa miaka mingapi? Unaweza kuwa sahihi. Lilijengwa kwa miaka ishirini na mbili (22). Kila siku watu walikuwa wanaweka tofali moja, siku nyingine tofali jingine, siku nyingine nondo, hatimaye lile jengo lilikamilika baada ya miaka 22!
Wajenzi hawakusubiri mwaka wa 22 ili wajenge hilo jengo. Ila walikuwa wakilifanyia kazi hilo jengo hatua kwa hatua kila siku bila kuchoka. Hili nalo litupe picha ya kuwa vitu vikubwa vinawezekana kufanyika na kuja katika uhalisia endapo vitafanyiwa kazi kwa kuanza kidogo kidogo, na kwa mwendelezo na kupewa muda ili viweze kuanzia chini na kukua.
Usidharau vitu vidogo. Kuna mfano, wa nyuki aliyeingia kwenye sikio la tembo na kuanza kupiga kelele. Tembo yule alianza kuruka huku na kule ili nyuki yule atoke kwenye sikio lake ila nyuki hakutoka. Tembo alianza kuangusha miti na kujibamiza kwenye miti pengine akidhani kwamba huyo nyuki atatoka ila huyo nyuki hakutoka. Baada ya muda mrefu wa kuhangaika, tembo alianguka na hivyo akawa amepoteza maisha. Kinaweza kuonekana kama kitu cha kushangaza, ila vitu vidogo muda mwingine huwa vina madhara makubwa sana.
Mbu ni wadogo, ila madhara yake ni makubwa. Sindano ni ndogo ila kikuchoma, wewe mwenyewe ni wazi kuwa utakipata cha mtema kuni. Kwa hiyo basi, nikuombe kuwa ujenge utaratibu wa kuheshimu vitu vidogo maana vinaweza kukupelekea kwenye mafanikio makubwa au la vikakupelekea kwenye anguko kuu maana kuna nguvu katika vitu hivi vidogo. Nguvu hii inaweza kukuinua ukiitumia vizuri ila ukiitumia vibaya itakuangusha. Na nguvu hii ndiyo tunaenda kuiona kwenye kitabu hiki
hapa.Endapo utakisoma kitabu hiki na kuanza kufanyia kazi yale utakayojifunza, sipati picha jinsi ambavyo utaanza kujenga six packs ambazo umekuwa unatamani kwa siku nyingi, akiba utakayoweka, vitabu utakavyoweza kuandika, utakavyoweza kukamilisha majukumu yako kwa wakati, jinsi utakavyoboresha mahusiano yako na mengine mengi.
Kila la kheri
Godius Rweyongeza
Februari 15,2020
Morogoro-Tz

kitabu hiki cha NGUVU YA VITU VIDOGO kinapatikana pia kwa mfumo wa audiobook kama inavyoonekana hapo juu na sample ya audiobook hii ha[o chini Rafki yangu, huo ndio utangulizi kutoka kwenye hiki kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA, nashauri sana uhakikishe kwamba umepata kitabu hiki cha kipekee. Gharama ya kitabu hiki ni 20,000/- tu. Ili kupata nakala ya kitabu hiki, tuma wasiliana na 0755848391 ili aweze kukutumia kitabu hiki popote pale utakapokuwa.



