Umekuwa unakwama kufika mbali kwenye maisha na kushindwa kufikia ndoto zako kwa sababu tu hujawa na ndoto kubwa kiasi cha kutosha. Maneno ya busara yanasema hivi,
unapaswa kulenga kuifikia nyota kiasi kwamba hata ukishindwa uufikie mwezi.
Sasa ebu fikiria hili, wewe ndoto yako siyo kubwa kiasi cha kulenga kuifikia nyota badala yake umelenga kufika kileleni mwa mti, unadhani ukishindwa utaangukia wapi? Si utaangukia baharini?
Kuanzia Leo hii weka ndoto zako kubwa Kisha anza kuzipambania.
Ndoto ndogo hata hazihamasishi. Ndoto kubwa zinakupa nguvu kubwa muda wote wa kuendelea kuzipambania.
Halafu nataka nikwambie kitu. Watu hawaweki ndoto kubwa sababu tu zinawezekana kufikika. Hapana, watu tuna ndoto kubwa sababu kwanza ndoto kubwa zinatuhamasisha kufanya makubwa.
Lakini pia kwa sababu ndoto kubwa inakufanya uutumie uwezo wako mkubwa ulio ndani yako kwa nguvu zako zote.
Lakini pia labda niseme ndoto kubwa ndio njia pekee iliyobaki ya kuweza kuishi vizuri hapa duniani. Ndio hakuna njia nyingine .
Zamani Darwin alikuja na nadharia ya survival of the fittest. Kadiri ya nadharia hii ni kwamba viumbe vyenye nguvu ndivyo vyenye uwezo wa kuishi huku vile ambavyo havina nguvu vinakufa.
Kama kikiwekwa chakula mezani na chakula kikawa ni kidogo, viumbe wenye nguvu ndio watakula na wale ambao hawana nguvu wataishia kujilamba midomo tu. Hali hiyo ikiendelea kwa muda mrefu ndio sasa unakuta viumbe ambao hawana nguvu wanakufa, wanabaki wale wenye nguvu tu.
Dunia ya sasa naona imehamia huko ila Kuna watu hawajastuka na mimi hapo nakuonea huruma sana. Kwa sababu unaenda kutoweka.
Kwenye zama za sasa kuwa na ndoto kubwa limebaki kuwa ni hitaji la lazima (basic need).
Kwa nini? Kwa sababu ndoto kubwa ndiyo njia pekee ya wewe kuendelea kuishi kwenye ULIMWENGU wa leo.
Ebu wewe chukulia watu wote ambao unawafahamu wamefanya makubwa kwenye zama za sasa. Orodhesha hata watu 10 unaowafahamu. Hakuna hata mmoja mwenye ndoto ndogo au ndoto za kawaida. Wote wana ndoto kubwa.
Chukulia mtu kama,
Elon Musk na ndoto yake kubwa ya kwenda sayari za mbali.
Kwenye ulimwengu wa sasa kama unataka kufanya makubwa na basi kuwa na ndoto kubwa, Kisha zipambanie kila kukicha.
Kuwa na ndoto za kuufikia uhuru wa kifedha
Kuwa na ndoto za kukuza kipaji chako kimataifa
Kuwa na ndoto kubwa haswa; Kisha Anza kuzifanyia kazi.
Ukubwa wa ndoto usikuogopeshe. Wewe anza kuzifanyia kazi hiyohiyo ndoto yako kwa kuanzia hapohapo ulipo.
Rafiki yangu, kiufupi kuwa na ndoto kubwa.
Nakumbuka kuna mtu aliwahi kusema kuwa rafiki zangu ni watu wenye ndoto kubwa. Siwapendi wenye ndoto ndogo. Binafsi na mimi siwapendi wenye ndoto ndogo. Kama wewe una ndoto ndogo, bora tu usiwe rafiki yangu maana hata utanikwamisha mimi.
Utatoa nguvu hasi kwangu. Mimi nataka marafiki wenye ndoto kubwa na ambao wameamua kuwa watazifanyia kazi ndoto zao kubwa au la watakufa wakiwa wanazipambania.
Wewe unayo ndoto kubwa?
Kama hauna ndoto kubwa basi leo hii hakikisha unaanza kusoma kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO ili kikupe mwongozo wa kuwa na ndoto kubwa. Lakini pia kitabu hiki kitakusaidia wewe kuweza kuzifikia.
Kina kila kitu, unachohitaji kujua kuhusu ndoto zako. Leo hii lipia 19800 upate nakala ngumu au elfu 10 upate softcopy.
Changamka sasa.
Umeshajiunga na THINK BIG FOR AFRIKA wewe? Jua zaidi hapa
One response to “Kinachokwamisha wewe kufika mbali.”
Shukrani sana kiongozi