Habari ya leo rafiki yangu mpendwa. Siku ya leo tarehe 11 wakati nafikiria cha kuandika, nimekumbuka nukuu ya John D. Rockefeller.
Kama ulikuwa hujui John D. Rockefeller alikuwa ni bilionea wa kwanza nchini marekani kufikia kiwango kikubwa. Kwa Afrika Mansa Munsa ndiye baba lao na utajiri wake haujafikiwa na yeyote mpaka leo duniani kote.
Basi bwana, leo acha niendelee na habari za Rockefeller, siku nyingine tukipata nafasi, tutamwongelea Mansa Musa.
Sasa Rockefeller siku moja alisema kwamba, wamebarikiwa wale ambao wanaanzia chini na kupambana mpaka kufika juu.
Rockefeller mwenyewe alikuwa ameanzia chini kabisa, hivyo alikuwa anajua nguvu ya kuanzia chini. Nguvu ya kuanza kidogo Kisha ukakuza hicho kidogo.
Najua na wewe unataka kufika mbali, Ila utapaswa kufikiria kuhusu kuanzia chini, Kisha kuendeleza kile kidogo mpaka kiwe kikubwa.
Hiki kitu kikanifanya nikumbuke stori ya kijana mmoja ambaye wakati akiwa chuoni aliona jinsi ambavyo kamera za Kijapani zilikuwa zinatawala soko la Marekani na hivyo kufanya kamera za Kijerumani kutoweka kwenye soko la Marekani. Alijiuliza hivi kama kamera za Kijapani zimeweza kuteka soko la Marekani, sasa haiwezekani kwa viatu vya Kijapani navyo kuchukua nafasi ya viatu vya Kijerumani.
Ilipofika wakati wa kuwasilisha wasilisho la utafiti wa kuhitimu chuo aliwasilisha mada inayohusiana na hicho kitu, wanafunzi wengi darasani walionesha kutopendezwa na hiyo mada. Profesakwa kumhurumia akaamua kumpitisha kama amefaulu.
Baada ya chuo jamaa akaona isiwe kesi, akaamua kuomba fedha kwa baba yake ili aweze kuitembea dunia. Akatembea nchi nyingi za Ulaya na hatimaye akafika Japani. Akiwa Japani akaona sasa huu ndio muda muafaka wa kuhakikisha kwamba ninafanya dili ambalo limekuwa kichwani mwangu kwa siku nyingi.
Dili la kuanza kuuza viatu vya kijapani Marekani. Hivyo, akaanza kutafuta kampuni ambazo zinatengeneza viatu, kampuni ambazo hapo baadaye zitapaswa kumtumia viatu ili awe anauza. Baada ya kwenda huku nakule akawa amekutana na kampuni moja ambayo walikubalina kuwa watamtumia pea kadhaa za viatu kwa dola 50 tu. Jamaa akaomba tena fedha kwa baba yake na kuweka oda ya viatu, kisha akaendelea na safari yake ya kuizunguka dunia. Akazunguka mpaka akafika hapo mjini Nairobi nchini Kenya kisha akarudi kwao.
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Kampuni ya Nike, na mtu anayeongelewa hapo siyo mwingine bali ni Phil Knights Mwanzilishi wa kampuni hiyo. Mtu huyu alikuwa na maono makubwa ya kufanya viatu vya Kijapani vitawale nchini nmarekani na kuviondoa viatu vya Kijerumani. Aliendelea mbele mpaka hapo baadaye akaja kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya kuzalisha viatu.
Na hili hapa linatupelekea kwenye sababu moja ya msingi ya kwa nini unapaswa kufikiri kikubwa na kuanza kidogo. sababu hii ni kwamba muda mwingine mtu unakuwa na ndoto kubwa ila hauna fedha za kutosha za kukufanya wewe uweze kufanikisha malengo na vitu vikubwa unavyofikiria. Hivyo, kwa kukosa mtaji wa kufanya hivyo, wewe hapo unapaswa kuanza kidogo.
Sababu ya pili ni ukosefu wa rasilimali muhimu za kukuwezesha wewe hapo kufaya makubwa kwa wakati mmoja ndio maana unapaswa kuanza kutumia rasilimali zilizopo. Ili uweze kufanya makubwa unahitaji rasilimali kama muda wa kutosha, watu, elimu n.k. lakini unakuta kwamba hauna hivi vitu vyote, hivyo unapaswa kuamua kwamba unaenda kuanza kidogo kisha baadaye kukuza rasilimali hizo ili ziweze kuwa kubwa zaidi kadiri unavyokuwa unaendelea na safari.
Sababu ya tatu ni kuwa wakati mwingine kuanzia juu siyo bora kwa afya yako. Kuna watu wameanzia juu na kujikuta kwamba wamefeli vibaya sana hapo baadaye, hivyo basi badala ya wewe kuja kufeli na kuanguka vibaya hapo baadaye unapaswa kujijengea utaratibu wa kuanza kidogo na kukua kadiri unavyokuwa unaenda.
Sababu ya nne ni kujiimarisha kadiri unavyokuwa unakua. Kufika kileleni ghafla kunaweza kukufanya upoteze kila kitu na hivyo kukufanya uanze upya. Hata hivyo unapokuwa unatoka chini an kuzidi kupanda juu, ni wazi kuwa utajikuta unaujua mchakato wote unaohitajika ili kukufanya wewe uweze kufika juu na hata ukianguka bado unaweza kusimama.
Sababu ya tano ni kuwa unapata nafasi ya kufanyia kazi vitu vidogo na kuona vipi vinafanya kazi kwa ubora huku ukiendelea kuboresha bidhaa zako. asilimia kubwa ya kampuni kubwa zote tunazozifahamu siyo kwamba zilianzia hapo zilipo leo. Unakuta kwamba zimeshawahi kujaribu bidhaa mbalimbli kabla ya kufikia zilipo leo hii, hata hivyo katika kujaribu huko ndiko zimekuta kwamba bidhaa fulani zinapendwa zaidi na watu na hivyo kujikita kwenye hizo bidhaa ambazo zinalipa zaidi.
Mfano, ukifuatilia kampuni kama Toyota, leo hii inafahamika kwa kutengeneza magari ila siyo kwamba kampuni hii ilianzia hapa, kuna sehemu ilianzia, ikajaribu vitu mbalimbali mpaka kuja kufikia hapa ilipo siku ya leo. Kuna kipindi kampuni hii hapa ilikuwa inauza cherehani.
Kompyuta za kwanza za kampuni ya Apple hazikuwa bora kama hizi tunazoziona leo hii. Ukiaziangalia kompyuta za miaka hiyo ya 80 au 70 ,mwishoni utagundua kwamba zilikuwa siyo nzuri kama hizi tunazozitumia leo hii. Kumbe hawa watu walitengeneza kompyuta za kawida, wakazipeleka sokoni, wakaona jinsi soko lilivyokuwa linafanya kazi na hatimaye sasa wakawa wameweza kuboresha kile walichokuwa wanafanya na kupata kitu ambacho kilikuwa ni bora zaidi.
Sita ni kukujengea msimamo binafsi. Hii inatokana na ukweli kwa345tyumba unajiwekea utaratibuw akufanya vitu vidogo kila siku kwa mwendelezo ambao hapo baadaye unakuja kukupa matokeo makubwa.kwa sababu vinakuwa vitu vidogo, basi matokeo yake hayaonekani kwa muda ila mkusanyiko wake baada ya muda unaleta matokeo makubwa. ebu tuchukulie mfano wa watu watatu wenye kipato sawa, wanafanya kazi ileile ofisini kwa muda uleule kwa siku zilezile za kazi. wanapata likizo kipindi kilekile cha mwaka na kipato chao ni kile ni kile. Ila kati ya hao mmoja wao tumwite Baraka, Mwingine tumwite Furaha na mwingine tumwite Busara.
Sasa watu hawa wakawa na tabia tofauti. Baraka kila anapopata mshahara anaamua kutoa asilimia kumi ya kipato chake na kukiweka kama akiba kisha kutumia kiasi kilichobaki. Kila mwezi anaawekeza kiasi kidogo cha kipato chake kwenye kununua vitabu ambavyo huwa anasoma kurasa kumi kila siku. Huwa anahakikisha kwamba anapata walau wazo moja kwenye kitabu na kisha analifanyia kazi. amejiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi kwa dakika chache kila siku. Anapangilia ratiba zake na anahakikisha kwamba ana muda wa familia yake kila siku. Ametenga pia dakika za kufanya tahajudi na hata kuandika mawazo ambayo huwa yanakuja kichwani mwake.
Kwa upande mwingine Furaha yeye anafanya vitu kama ambavyo mtu mwingine anafanya.
Wakati, Busara kila mwezi anafanya vitu vya ajabu, mara zamu hii unakuta kanunua runinga, mwezi ujao spika, mwezi mwingine anatumia kiasi kikubwa kwenye michezo ya kubahatisha ili ashinde fedha nyingi. Anatumia muda mwingi kwenye kuangalia runinga na sasa ameanzisha tabia mpya ya kula chipsi mayai na vyakula vingine vitamu kila anapokuwa anaangalia runiga. Watu hawa kwa mara moja huwezi kuona tofauti zao mwanzoni wanapoanza kufanya hivi vitu. Baada ya miezi mitano unaweza pia usione tofauti kubwa miongoni mwa watu hawa. Ila baada miaka miwili, ni wazi kuwa utofauti kati ya hawa watu itakuwa imeanza kuonekana. Baada ya miaka mitano, utofauti wao utakuwa mkubwa. Wengine wanaweza kuanza kukimbilia kurahisha kwa kusema kwamba Baraka ameenda kwa wanganga ila kumbe ukweli ni kwamba, hakuna mganga wala nini? Ni nguvu ya vitu vidogo sasa inaanza kujionesha yenyewe
Kama umeweza kufanya makubwa ukiwa na rasilimali za kawaida, utaweza kufanya makubwa zaid ukiwa na rasilimali kubwa
Saba, kukuondolea msongo. Ujue unapokuwa na jukumu kubwa na unaliangalia kwa ukubwa wake unaweza kujikuta kwamba unapata mpaka msongo. Ila ukijua kwamba katika kitu hicho kikubwa unachukua hatua ndogo ndogo hii inaweza kupelekea wewe kupunguza msongo.
Ebu chukulia umepewa kazi ofisini ila umeiweka na unakuja kuanza kukimbizana nayo siku moja kabla ya siku yenyewe ambapo kazi inahitajika. Ni wazi kuwa siku hiyo utakuwa na msongo wa hali ya juu kwa maana usipokamilisha hiyo kazi siku hiyo, kesho yake utapata taabu sana. Unakuwa na hofu ya kuwa pengine utapoteza kazi yako au kukatwa mshahara. Au unaogopa kuaibika mbele ya rafiki zako wakati unawasilisha hiyo kazi. Kitu hiki kinapelekea wewe kufanya kazi hii hovyo hovyo kabisa. kesho utaenda kazini ukiwa na msongo zaidi maana kazi utakuwa unajua umeifanya chini ya viwango. Utakuwa unahofia bosi wako atasemaje akiona kazi ya hovyo unayoenda kuwasilisha. Kitu hiki ni wazi kuwa kitakunyima amani na kuleta msongo mkuwa. Hali hii itakusababishia msongo.
Ila kama kazi hiyo hiyo utaipata na siku hiyo ukaipangia ratiba ya kuanza kuifanya kidogokidogo utajikuta kwamba umeweza kuifanikisha , kiasi kwamba siku ya mwisho hautapata shida ya kukamilisha kazi yako na wala hutakuwa na hofu ya kuwasilisha kazi yako kwa bosi maana utakuwa unajua kwamba kazi yako umeifanya kwa viwango, umeihakiki akuirudia kuhakikisha kuwa kazi ya kimataifa. Kiufupi hautakuwa na msongo wowote.
Kwa mwanafunzi ambaye yuko shule naye anaweza kuondoa msongo wa kuhakikisha kwamba anajipangia ratiba ya kusoma hata kama hana mtihani. Hii itamwondolea msogo pale mitihani itakapokaribia. Lakini akisubiri mpaka siku ya mwisho ndiyo aje kusoma, ni wazi kuwa atapata taabu sana.
Nane. Kukujengea nidhamu. Ukifanya vitu vidogo vidogo kwa muda mrefu bila kuacha hata kama ni vidogo, ule mkusanyiko wako utakufanya uonekane kama ni wa kipekee au mtu kutoka dunia nyingine wakati umejijengea nidhamu ya kutoacha tu.
Tisa, Kukufanya uweze kufikia mambo makubwa
Kila siku unapoamka asubuhi unakuwa na nafasi ya kuchagua ni kitu gani unaweza kufanya kati ya vitu vingi vinavyokuwepo mbele yako. Unaweza kuamua kuitumia vizuri asubuhi yako ya siku husika au kuitumia vibaya pia. Kwa mfano unaweza kuamka asubuhi na kuwasha runinga hapohapo na kuanza kuwaangalia watu wanaofanya mazoezi huku ukiwahukumu, na hata kuwacheka. Unaweza kusema mbona huyu hapa hafanyi mazoezi inavyostahili, mbona huyu hakimbii, mbona huyu hafanyi hivi, baada ya hapo unaaweza kuamua kuingia mitandaoni na kuanza kufuatilia habari nyepesinyepesi na matukio yanayoendelea, kabla hujajua, zitakuwa zimepita saa tatu mpaka nne, upo mtandaoni tu unatafuta vitu visivyoeleweka. Baada ya hapo unaweza kuanza kuongea kwenye simu na rafiki zako, mkijuliana hali na kuulizana yale yalilyotokea kwenye mechi za jana au wikendi.
Baada ya hapo utaenda kazini, huku ukiendelea kusikiliza taarifa ya habari na habari nyingine nyepesinyepesi kutoka kwenye vituo vya redio au kupitia mtandaoni. Ukifika kazini utasalimiana na rafiki zako na kuanza kumwongelea rafiki yenu ambaye amepokea fedha zote na kwenda kuhonga badala hata ya kunununua kiwanja. Mpaka hapa utakuwa umechoka, huku ukidonoa kazi kidogo, kidogo.
Baada ya kazi utarudi nyumbani na kuwahi kijiweni kwanza ili upige soga na awashikaji kisha utarudi nyumbani na kufikia kwenye kochi, ukifungulia runiga na kuendelea kuangalia tamthiliya. Kabla hujajua utajikuta kwamba hauna tena muda wa kupika chakula, na hivyo moja kwa moja utaagiza chipsi yai ambayo utakula wakati inakusinidiza kuangalia thamthiliya yako, na unakuja kustuka muda ukiwa saa saba za usiku, happo ndiyo unakumbuka kwamba unapaswa kulala. Kesho yake unaamka saa mbili kisha mzunguko unajirudia.
Hali ni tofauti kwa mtu ambaye anaamka asubuhi na kuanza kupangilia ratiba yake, huku akionesha ni vitu gani ambavyo atafanya na vitu gani ambavyo ataepuka navyo na kisha kuanza kufanyia kazi mpango wake wa siku husika. Jioni anarudi kutokana kazini na kufanya mazoezi, kisha anaanza kusoma vitabu vya kumwongezea maarifa. tofauti kati ya watu hawa wawili ni ndogo sana ila kwa muda mrefu tofauti hii itageuka kuwa tofauti kubwa sana
Hii ni tofauti ndogo kutoka kw watu