Miaka kadhaa iliyopita, mtandaoni kulikuwa na picha ya mtoto mdogo iliyokuwa inasambaa kama moto wa kifuu.
picha hii ilikuwa ikimwonesha mtoto mdogo tu, ambaye aliajiriwa na kampuni kubwa ya Google.
Sasa swali kubwa ambalo unaweza kuwa unajiuliza, ilikuwaje huyu mtoto mdogo akaajiriwa na kampuni kubwa kama GOOGLE.
Jibu ni moja tu, huyu mtoto alikuwa anajua ambacho watu wengi hawajui.
Kiufupi ni kwamba alikuwa ana ujuzi ambao watu wengine hawana. Na hiki ndiyo kitu ambacho kilimfanya huyu mtoto sasa kuwa na nafasi ya kuajiriwa kwenye kampuni kubwa kama google.
Sasa ninachotaka kukwambia siku ya leo siyo kitu kingine bali ni kuwa na wewe pesa zako zimejificha kwenye kitu kimoja kikubwa sana. Na kitu HIKI siyo kingine bali ni ujuzi.
Swali ambalo ningependa ujiulize siku ya leo ni ujuzi gani ambao unao ambao watu watakuwa tayari kuulipia na hawatataka kukupoteza. Yaani, watu watakuwa tayari kulipa kiasi chochote kwa sababu tu ya ujuzi huo ulionao?
Pesa zako zimejificha kwenye ujuzi.
Kama leo hii hauna ujuzi wowote, ni muda wako muafaka sasa wa kuanza kujifunza ujuzi mpya.
Na ubora ni kwamba kwenye ulimwengu wa leo ni rahisi sana kujifunza karibia ujuzi wowote. Hakuna kitu chochote kile kitakachoshindikana kwako wewe kujifunza kwenye ulimwengu wa leo.
Unaweza kujifunza na kuelewa kitu chochote kile unachotaka.
Kuna kozi nyingi mtandaoni ambazo unaweza kujifunza, jifunze kupitia hizi kozi.
Kuna video nyingi mfano kwenye mtandao wa youtube tu, kuna video za kutosha ambazo zinaweza kukuelimisha kila kitu unachohitaji kujua kuhusu kitu chochote kile unachotaka
Hivyo, kazi yako kubwa ambayo unapaswa kufanya rafiki yangu, ni kuhakikisha kwamba unakuwa na ujuzi, ujuzi ambao utajifunza na kuanza kuufanyia kazi mara mooja hasa kwenye ulimwengu wa leo ambapo ujuzi ni kitu muhimu sana.
SOMA ZAIDI:
- Namna ya kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa vijana. Njia Saba Zilizothibitishwa (Njia Namba 2, 4 na 7 ni muhimu sana)
- Njia Tano Za Kujitofautisha Mwenyewe Kwenye Kile Unachofanya
- JINSI YA KUIBADILI DUNIA: Vitu Saba Vya Kufanya Kama Unataka Kuibadili Dunia
Ile video ya yule mtoto wa miaka 13 aliyeajiriwa na google nakuwekea hapa chini,
Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.
Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.
SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea
Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com
SOMA ZAIDI: Njia Saba (07) Bora Za Kutangaza Ujuzi Wako Kwa Watu