MTAJI:Kila Kitu Unachohitaji Kujua


Ndugu Godius Rweyongeza akifundisha semina kwa wafanyabiashara. Wasiliana naye wasap kwa KUBONYEZA hapa

Kwenye kitabu chake Cha MAISHA NI MTIHANI, Fr. Faustine Kamugisha anatupa tafakuri moja nzuri sana. Anasema maisha ni MTIHANI. Ukiwa na chakula ni MTIHANI, usipokuwa nacho ni MTIHANI pia. Ukioa ni MTIHANI na usipooa ni MTIHANI pia. Ukiwa na ndugu ni MTIHANI ila usipokuwa nao ni MTIHANI pia.

Fr. Kamugisha kaainisha vitu ambavyo ni MTIHANI, na ukiangalia unaona kweli maisha ni MTIHANI, yaani KITU chochote ukiwa nacho tayari ni MTIHANI ila usipokuwa nacho ni MTIHANI pia.

Tukichukukie mfano wa ndugu au marafiki, ukiwa nao ni mtihani. Ila pia usipokuwa nao ni mtihani mkubwa pia.

Kwenye andiko langu la Leo ninazungumzia zaidi kuhusu MTAJI. Naam, MTAJI wa kuanzisha biashara, ukiwa nao ni mtihani, ila usipokuwa nao ni mtihani pia😁.

SOMA ZAIDI: MITAJI 21 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA

Jinsi Ya Kupata Mtaji Wa Biashara

Iko hivi kuna Watu wana changamoto kwamba wanashindwa kuanzisha biashara kwa sababu hawana MTAJI. Na kuna Watu wanashindwa kuanzisha biashara kwa sababu wana MTAJI. Hivi vitu ukivitafakari unaweza kuona kama masihala, ila ndivyo ukweli ilivyo. Nimewahi kueleza siku za nyuma kuwa Biashara Ni Zaidi Ya Mtaji PESA. Ila kwa mantiki ya makala ya leo, tujikite kwenye MTAJI PESA, na hata tukiongelea MITAJI mingine ambayo siyo pesa, mwisho wa siku tuone ni kwa namna gani inaweza kugeuzwa kuwa pesa? Hivyo, popote pale nitakapotumia neno mtaji kwenye makala hii, ifahamike kama Pesa ya kuanzisha biashara.

Sasa swali ni kwamba nifanyeje ikiwa Sina MTAJI Ili niweze kupata MTAJI?

Ukweli ni kuwa kama hauna MTAJI haupaswi kuogopa. Inawezekana kwa wewe kupata MTAJI vizuri tu endapo utaanza kutumia vitu ulivyonavyo Sasa hivi. Kwenye makala hii, vitu hivi sitavieleza kwa undani sana, ila kwa haraka nitakushauri ukasome kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA, ambacho sehemu ya tatu ya kitabu hiki, inaeleza kwa undani mitaji 21 iliyokuzunguka na jinsi unavyoweza kuitumia. Hivyo hapa ninaenda kutaja baadhi ya mitaji unayoweza kuanza kutumia mara moja.

Moja Anza kutumia NGUVU ZAKO mwenyewe. Tafuta kazi yoyote halali unavyoweza kufanya kwa kutumia NGUVU Yako ukalipwa. Naomba ieleweke kwamba huwezi kukosa kila kitu, ukose mtaji PESA na ukose nguvu. Tumia ulichonacho kwanza (NGUVU) kupata ambacho hauna (MTAJI FEDHA). Na hata wahenga wetu waliwahi kusema kwamba mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe. chukua hiyo.

Pili, tumia kipaji chako kulipwa. KIPAJI CHAKO NI DHAHABU. unachotakiwa kufanya ni kukitumia kipaji chako. Tena kwenye ulimwengu wa leo imekuwa rahisi sana kuonesha kipaji chako kuliko muda mwingine wowote, vitu ambavyo hapo zamani za kale vilikuwa vinaonekana kama haviwezekani, kwenye ulimwengu wa leo wa intaneti vimewezekana vizuri sana. Tumia mitandao ya kijamii kuonesha kipaji chako. Kama utakitumia vizuri, kitakulipa.

Tatu tumia muda wako vizuri. Wahenga wetu walishatuambia kwamba muda ni mali. na kama muda huu ukitumiwa vyema maana yake unaweza kukuinua na kukusogeza sehemu nzuri. Moja ya kufahamu ni kwamba hakuna mtu mwenye muda wa kufanya kila kitu. Hivyo, ukiongea vizuri na watu unaweza kutumia muda wako kufanya baadhi ya vitu vyao na wao wakakulipa. Inawezekana mtu ana kipato kizuri, lakiini hana muda wa kuosha gari lake, wewe ukamsaidia kwa hilo, inawezekana mwingine ana kipato kizuri lakini hana muda wa kuandaa chakula kizuri kwa ajili ya afya yake na familia yake, wewe ukamsaidia kwenye hilo. Muda wako ni mali utumie vizuri. Na hata kama sasa hivi huna jambo kubwa linalokuingizia kipato kupitia muda wako, angalia vitu vidogo unavyoweza kuanza kuvifanyia kazi mara moja vikakulipa sasa au hata baadaye.

SOMA ZAIDI: Jinsi ya Kuanzisha Biashara Kubwa Kwa Mtaji Kidogo

Nne ni Ujuzi au uzoefu wako. Una ujuzi fulani, umekuwa unajua namna ya kuandaa matangazo ya kuweka mtandaoni, unajua kuendesha mitandao ya kijamii kwa manufaa, unajua kuhariri video au makala, unajua  kupamba, unajua kufundisha au chochote kile unachojua. Hicho ni pesa. Kiufupi ni kwamba mwenye ujuzi halali njaa. Kama una ujuzi na unalala njaa, kosa lako haujajua namna ya kuufanya ujuzi wako ukulipe, jifunze hilo. Na hapa nashauri ukasome kitabu cha KIPAJI NI DHAHABU ile sura ya tano, ya sita na ya nane pamoja na kitabu cha TENGENEZA PESA KWA KUUZA UNACHOJUA. Utanishukuru baadaye. Wasiliana na huyu akupe nakala yako. 0755848391 AU 0745848395 sasa hivi.

Tano ni konekisheni ulizonazo. Hizi zitumie pia kupata mtaji, konekisheni ulizonazo unaweza kuzitumia kupata mtaji, au watu hao wakakuunganisha na wengine ambao wanaweza kuwa watu wenye manufaa kwako. Konekisheni zako ukizutumia vizuri zitakuinua kwa sababu hata baada ya kuanzisha biashara, utahitaji kutumia konekisheni zako kupata wateja. Kwenye makala ya kesho, nitaeleza zaidi juu ya suala zima la konekisheni. Usiikose, jiunge hapa ili kupata kiti cha mbele, ikitoka tu wewe unayo. JIUNGE HAPA

Sasa kwenye hiki kipengele ninaishia hapa, kupata makala na mafunzo zaidi kuhusu MITAJI ILIYOKUZUNGUKA NA NAMNA UNAVYOWEZA KUITUMIA KWA MANUFAA, HAKIKISHA UNASOMA KITABU CHA NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA. 

Ndugu Godius Rweyongeza akifundisha misingi ya kusimamisha biashara Imara
Ndugu Godius Rweyongeza akifundisha misingi ya kusimamisha biashara Imara

Swali nifanye biashara Gani endapo Nina MTAJI kidogo?

Yes, ikitokea kwenye vitu ambavyo nimeainisha hapo mwanzo umevifanyia kazi na umeanza kupata MTAJI, Sasa unafanya biashara Gani na huu MTAJI kidogo.

Ukweli ni kuwa ni biashara za kufanya kwa MTAJI huuhuu kidogo ni nyingi. Naweza nisiweze kuzitaja zote hasa kwenye makala hii ila nashauri uangalie vitu vifuatavyo kwenye hiyo biashara unayotaka kuanzisha.

Moja, iwe biashara ambayo unaweza kuanzia kwa MTAJI kidogo

Pili, iwe biashara ambayo itaingiza pesa KILA siku. Kwa vile MTAJI wako BADO ni kidogo, siahauri tuanze kufanya biashara ambayo itashikilia MTAJI wako kwa muda mrefu, badala yake iwe biashara ambayo unaweza kuuza kwa haraka na kupata Hela Kisha ukairudisha kwenye biashara.

TATU, iwe biashara Kutoka kwenye sekta ambayo inapendwa na wengi. Kwa MTAJI kidogo ulio nao huna jeuri la kuanzisha biashara kwenye eneo ambalo utahitaji kutumia NGUVU kubwa kuwashawishi Watu, inatakiwa kiwe KITU ambacho Watu wamezoea na wewe utantumia NGUVU kidogo kuwaeleza Watu.

NNe iwe biashara ambayo gharama za uendeshaji ni ndogo. Kwa kuanzia, usianzishe biashara ambayo utatakiwa kutumia gharama kubwa za uendeshaji kama ulipaji wa kodi, vifaa, watu, n.k Anza na biashara ambayo gharama zake za uendeshaji ni ndogo tu.

Tano, anzisha biasahara ambayo unaweza kufanya hata katika mazingira ya nyumbani au siyo mbali na nyumbani. Yaani, isiwe biashara ambayo utaanza tena kusafiri umbali mrefu. Kumbuka unaanza na kile ulichonacho sasa, kisha unafanya yanayowezekana sasa kabla y akuja kufanya yasiyowezekana.

Sita, iwe bishara ambayo unaweza kuongeza au kupunguza mtaji muda wowote. Mfano biashara ya matunda, leo unaweza kuwa na mtaji wa kununua matunda tenga moja, kesho ukanunua tenga mbili. Kesho kutwa mtaji ukipungua unauza tenga moja kama kawaida.

saba iwe ni biashara inayohitaji ujuzi ulio nayo tayari, na si biashara ambayo inakuhitaji uanze kusoma sana kwanza.  Kumbuka unapaswa kuanza Na Ulichonacho kwanza

Nane iwe ni biashara unayoweza kutangaza kwa gharama kidogo. Kama unavyojua kila biashara inahitaji ufanye masoko. Sasa wewe huhitaji kuanzisha biashara ambayo itakugharimus ana kwenye masoko. Iwe ni biashara ambayo unaweza kufanya masoko ya gharama nafuu kama wasap status, kutumia profile yako ya facebook, ambayo unaweza kutangaza kwa gharama za chini ambazo unazimudu na ziko ndani ya uwezo wako kwa sasa.

Siku siyo nyingi nimeanza kulima uyoga, sehemu ya matangazo niliyofanya ilikuwa ni kutengeneza bango kwenye karatasi za kawaida, na kubandika maeneo yaliyokuwa na watu niliokuwa nawalenga. Matangazo haya ambayo hayajagharimu zaidi ya elfu mbili kutengeneza, tayari yananiletea watu wa maana kabisa. Hii ndiyo kusema kwamba baadaye nikitengeneza mengine, nitapata wateja wengi zaidi.

SOMA ZAIDI: Unawezaje Kujiajiri kwa Mtaji Kidogo?

Tisa, Iwe ni biashara ambayo inaleta wateja mara kwa mara. Siyo mteja akinunua mara moja ndiyo imeisha. Iwe ni biasahra ambayo mteja akinunua leo anaweza kununua tena baada muda fulani. Nikienda kunyoa leo, siyo zaidi ya wiki mbili zijazo nitalazimika kwenye kunyoa. Nikinunua maziwa leo, nitayahitaji na kesho, nikinunua majiya kunywa asubuhi naweza kuyahitaji mchana au jioni. Biashara za namna hii nzuri kwa kuanzia.

Kumi, iwe ni biashara ambayo inaweza kukua. Kumbuka lengo la kuanzisha biashara ni kwamba siku moja unataka kuwa mkubwa kibiashara, iwe ni biashara inayoweza kukua zaidi ya unayoianzisha hapo. Kwamba unaanza na kuuza mayai trei moja, baadaye unauza tano, baadaye unauza trei 1000 na kuendelea. 

Hakikisha pia unapata kitabu cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA. Kipate kwa kuwasiliana nami kwa simu 0755848391 au tumia 0745848395

Sasa je, ikiwa una MTAJI mkubwa ni biashara ipi unaweza kufanya?

Ukweli ni kuwa KANUNI za kuanzisha biashara ni zilezile hazijabadilika. Misingi ya kusimamia biashara ni ileile haijabadilika pia. Muhimu unapoanzisha biashara ya namna hii hakikisha

Moja unaangalia eneo lenye tatizo na uhitaji wa watu. 

pili, angalia tatizo ambalo linawasumbua sana watu na wewe unaweza kulitatua

tatu, angalia biashara ambayo inafanyika ila inafanyika kiholela, wewe unaweza kuweka ubunifu wako na kuifanya kitalaam na kibobevu zaidi. Inawezekana inafanyika na ina wateja ila wanaoifanya hawana nguvu ya mtaji ya kuleta bidhaa zinazotakiwa kwa wateja kwa wakati kwako hii inaweza kugeuzwa kuwa fursa.

SOMA ZAIDI: 

Ifahamu kanuni ya copycat

Ni muhimu sana kufahamu kwamba kwa biashara yoyote unayoianzisha ndani ya miezi sita kuna watu wataona biashara hiyo inafaa na wao watakuwa tayari kuianzisha. 

SOMA ZAIDI: WAZO LA BIASHARA AINA HII LAHUWEZI KULIPATA

Kazi ya kufanya leo

Leo nataka nikupe kazi muhimu sana. Zunguka mtaani na notebook, kisha angalia biashara zinazofanyika. andika kila bango la kila biashara unayoona. 

Kisha jiulize ni biashara gani unaweza kufanya, ni biashara ipi inafanyika kwa kawaida mimi naweza kuiongezea ubunifu?

Hakikisha umepata kitabu cha RASILIMALI ZA WATU WENGINE, ni kitabu kizuri kwa ajili yako. wasiliana na 0755848391 au 0745848395 sasa

Makala ya kesho itawekwa kwenye blogu ya SONGAMBELE ambayo unaweza kuifikia kupitia www.songambele.co.tz na itawekwa kwenye channel ya telegram pia ambayo unaweza kuifikia kwa KUBONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X