Author: Godius Rweyongeza

  • Unachohitaji wewe siyo hamasa zaidi bali ni matendo zaidi

    Mara kwa mara watu wamekuwa wanatafuta hamasa ya kufanya kitu. Ukweli ni kuwa huhitaji hamasa pekee ili kufanikisha lengo na ndoto yako kubwa. Bali unahitaji matendo ili uweze kufanyia kazi malengo na ndoto zako ziweze kufanikiwa. Nakwambia hivi kwa sababu hamasa huwa haidumu, hamasa ni kitu cha muda mfupi ambacho kinapotea. Hivyo ili ufanikishe malengo…

  • Jinsi ya kupunguza najuto yako utakapokuwa umezeeka

    Moja ya changamoto kubwa ammbayo huwa inawakuta watu ambao wanakuwa hawafanyii kazi malengo na ndoto zao ni kwamba wanapofikia mwisho wa maisha yao basi wanakuwa na majuto mengi ambayo yanawaandama kutokana nay ale ambayo hawakuweza kufanyia kazi. Sasa wali kubwa ambalo unaweza kuwa unajiuliza ni kuwa je, kuna namna ambavyo naweza kupunguza haya majuto kwenye…

  • Kishiria kuwa umechelewa kufanya maamuzi

    Rafiki yangu, kila siku kuna maamuzi ambayo tunatakiwa tufanye, yanaweza kuwa ni maamuzi ya nani uwe naye kwenye mahusiano, maamuzi ya biashara gani ufanye, maamuzi ya sehemu gani uende kutembelea. Maamuzi ya aina gani ya matangazo ufanye. Maamuzi ya nani umwajiri, nani umwondoe kazini au nani umpandishe cheo. Maamuzi ya shule gani mwanao asome au…

  • Kuanguka ni kiashiria kuwa kuna kitu unafanya

    Kuanguka siyo tatizo, kuanguka ni kishiria kwamba kuna kitu unafanya na ndiyo maana unakutana na vikwazo. Kumbe kuanguka kwako usikuone kama kigezo cha wewe kutoendelea mbele. Bali kuone kama sehemu ya wewe kuendelea kusonga mbele ili kuja kufanya makubwa zaidi. Kadiri unavyokua, maanguko yako yanakuwa makubwa zaidi. Na yanajulikana kwa watu wengi zaidi kuliko pale…

  • TAARIFA KWA UMMA

    Siku za karibuni whatsap zimepatwa na changamoto na changamoto ya kufungiwa, kitu ambacho kimenifanya nikawa siwezi kupata jumbe zenu moja kwa moja. Nimejaribu kufungua akaunti nyingine za whatsap ambazo nazo pia zimefungiwa pia. Hivyo, kwa sasa nimeamua kuwa nitatulia kutumia whatsap kwanza. ila nitakuwa natumia telegram. Unaweza kunifikia kwa haraka telegram kwa namba hii ya…

  • Wewe unafahamika Kwa kitu Gani ?

    Moja ya uamuzi unaohitaji kufanya ni Uamuzi wa namna unavyotaka ufahamike kwenye maisha Yako. Nimekuwa nikisisitiza hiki kitu mara Kwa mara, lakini cha kushangaza ni kuwa Watu wengi wamekuwa Bado wanarudia kufanya makosa yaleyale Kila mara. Ngoja nikwambie KITU, watu wengi unaowafahamu, huwafahamu Kwa sababu wanafanya Kila kitu au walikuwa wanafanya Kila kitu, bali unawafahamu…

  • Kufa Leo, uishi milele

    Ikiwa inamaanisha pambana Leo Ili juhudi zako ziendelee kukusaidia Mpaka kesho. WEKEZA Leo ule vinono kesho. Kubali kupoteza Leo, Ili kesho kesho kutwa upate Kila kitu. Ukweli ni kuwa maisha Yana trade off. Huwezi kupata Kila kitu unapokihitaji. Kuna baadhi ya vitu unahitaji uvipoteze Leo, Ili ufanye vingine lakini ukiwa Unajua kesho Utapata zaidi. Na…

  • Wiki Hii Nipo Nasoma Kitabu Cha Elon Musk. Kitu Kimoja Unachopaswa Kufahamu Kwanza

    Wiki hii nipo nasoma kitabu kizuri sana Cha ELON MUSK: Kilichoandikwa na Walter Isaacson mtalaam wa kuandika vitabu vya wasifu (biographies). Kwa Kuwa Bado naendelea kukisoma Kwa Sasa sitasema mengi zaidi ya kusema kuwa bila kujali unezaliwa wapi, Bado unaweza kuweka alama kwenye hii Dunia Huhitaji ruhusa ya watu wengine zaidi ya ruhusa Yako tu…

  • Je, ni kwa namna gani wewe unaitumia simu yako kwa manufaa?

    Wakati mwingine ukiambiwa kwamba simu yako ina uwezo mkubwa, unaweza kudhani ni masihala vile. Leo nimechapa mawasiliano (namba za simu) yaliyo kwenye moja ya email yangu. Nimepata karatasi zenye  kurasa 131 Na kila ukurasa umejaa juu mpaka chini. Nilipobeba karatasi zenye haya mawasiliano mkononi ndiyo nikagundua ni kwa namna gani simu yangu imebebeba vitu vingi…

  • Kama Hujisikii Kufanya Kazi

    Huwa inatokea kwamba ninaanza kuandika huku nikiwa sijui ni kitu gani cha kuandika. Sijapangilia mada ya kuandika lakini muda huohuo napaswa kuandika na kuonesha kitu kwa watu wangu wa nguvu kama wewe hapo. Na siku ya leo ni mojawapo. Hata hivyo huwa ikitokea siku kama hii, kitu cha pekee ambacho huwa natakiwa kufanya siyo kuacha…

  • Wiki ya Huduma Kwa Wateja

    Habari ya asubuhi upande wa huko Hii ni wiki ya huduma kwa wateja. Na nimeona nikupe taarifa muhimu sana rafiki yangu. Na taarifa hii ni kwamba wiki hii una kila sababu ya kuwasiliana na wateja wako. Mpigie hsimu hata mteja mwambia kwamba hii ni wiki ya huduma kwa wateja na nimepiga simu kwa ajili ya…

  • Hiki Ndicho Kitu Unachopaswa Kuwa Na Wasiwasi Nacho Kwenye Maisha Yako

    Rafiki yangu mpendwa, salaam Bila shaka unaendelea vizuri kabbisa. Hongera kabisa kwa siku hii nyingine ya kipekee. Leo ni Jumamosi ya tarehe 16, mwezi wa tisa mwaka 2023. Ni siku bora kabisa ambayo naamini umeweza kuitimia kwa viwango vikubwa. Siku ya leo kuna kitu kimoja tu ambacho ningependa kukwambia na kitu hiki siyo kingine bali…

  • Cha kufanya kama unaanzia chini kweye maisha

    Rafiki mpendwa salaam, bila shaka unaendele vizuri kabisa. Hongera kwa kazi. Mimi naendelea vizuri nikiwa hapa Morogoro mji kasoro bahari. Siku ya leo nataka nikwambie kitu kimoja ambacho unapaswa kufanya kama unaanzia chini kwenye maisha. Unajua ni kitu gani hiki. Kwanza ni kuchagua kitu ambacho utafanya. Hiki ni muhimu sana, watu wengi huwa hawapati nafasi…

  • Vyanzo Vingi vya KIPATO ni kama miguu ya Meza.

    Vyanzo Vingi vya KIPATO ni kama miguu ya Meza. Meza iliwa na mguu mmoja na mguu huo ukavunjika. Maana yake Meza hiyo kwishney!! Ila Meza iliwa na miguu minne, Mmoja ukivunjika. Itatetereka kidogo, ila Bado itakuwa imesimama. Kama ambavyo nimekuwa nakwambia, kama hauna vyanzo vingi vya vipato. Basi utakuwa na Vyanzo Vingi vya mahangaiko. Kuwa…

  • Tabia za kimasikini unazopaswa kuachana nazo sasa hivi.

    Rafiki yangu mpendwa salaam, leo ningependa kukwambia tabia za kimasikini ambazo unapaswa kuachana nazo. Achana na tabia hizi kwa manufaa yako. Kwanza ni vitu ambavyo vinapoteza nguvu zako. Hivi ni vitu vyote ambavyo vinapoteza nguvu zako vitu kama pombe, sigara, ulevi wa aina yoyote, kula vyakula vya hovyo na mambo mengine kama hayo. Pili, ni…

  • Ukiuza vitabu vyako vyote ambavyo umewahi kununua utapata shilingi ngapi?

    Ukiuza vitabu vyako vyote ambavyo umewahi kununua utapata shilingi ngapi? Leo kuna mtu nilikuwa naongea naye, akaniambia vitabu ambavyo nimewahi kununua, nikiviuza vyote naweza kujenga nyumba kubwa ya kifahari. Hiki kitu kikawa kinanitafakarisha kuhusu wewe … Hivi wewe ukiuza VITABU vyote ambavyo umewahi kununua unaweza kufanya nini? Vitabu vinakufanya uone mbali hata wewe ni mfupi?…

  • Siri ya mafanikio ya kweli ni hii hapa

    Usiache kufanya jambo lako kwa sababu huoni matokeo ya muda mfupi. Badala yake kaza. Endelea kupambana kwa muda mrefu Kuna watu wengi hawafanikiwi kwenye maisha kwa sababu ya kujaribu vitu vingi kwa muda mfupi na kuacha. Sikiliza chagua kitu kimojaKifanye kwa uhakikaKifanye kwa muda mrefu bila kuacha.Bobea kwenye hicho kiasi kwamba hakuna mtu ambaye anaweza…

  • Kauli Yenye Nguvu: Ni bora Ufe Ukiwa unafanya unachopenda…

    Rafiki yangu mpedwa salaam, hongera sana kwa siku hiii ya leo. Siku ya leo ningependa tu kukushirikisha kauli moja ambayo unapaswa kuwa unajiambia kila siku kwenye biashara na kwenye kitu chochote kile unachofanya. Mara nyingi ukianza kufanya kazi au kitu chochote huwa wanatokea watu ambao wanakuwa na maoni ya kukushauri juu ya nini cha kufanya…

  • Kheri ya MWEZI WA SEPTEMBA

    Siku zinaenda balaa, ni kama jana tu nakumbuka watu walivyokesha wakiusubiri mwaka mpya. Watu walivyokuwa na mbwembwe za mwaka mpya na mambo mapya, hivi kwenu haya mambo yapo, au ni ushamba wa huku nilipo tu! Tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu wengi ambao huwa wanaweka malengo. Huwa wanayasahau malengo yao kufikia januari 19, je, wewe malengo…

  • Kazi inayolipa kuliko zote duniani. Jifunze kazi hii utaishi kama mfalme

    Rafiki yangu wa ukweli, bila shaka unaendele vizuri, siku ya leo ningependa kuleta kwako kazi ambayo inalipa kuliko zote hapa duniani. Na kazi hii siyo nyingine bali ni kazi ya kuuza. Ni kazi ambayo mtu yeyote ambaye yuko tayari kujifunza anaweza kujifunza. Haina ukomo wa kipato. Unaweza kupata zaidi kadiri unavyouza. Ukiuza zaidi unalipwa zaidi.…

X