Home


  • Namna ya kupangilia ratiba ya wiki hii kiporofessional

    Namna ya kupangilia ratiba ya wiki hii kiporofessional

    Rafiki yangu mpendwa, salaam

    Miongoni mwa ujuzi muhimu sana ambao unahitaji ili kufanikisha malengo Yako ya mwaka 2025 ni ujuzi wa kuipangilia wiki yako. Wiki ni ndogo sana ila usipoipangilia vizuri inapotea na ukipoteza wiki nyingi mfululizo, mwisho wa siku unakuwa umeupoteza mwaka wako. Maana mwaka una wiki 52 tu. Na kumbuka wiki yoyote unayoipoteza, hairudi hata kidogo.

    Sasa ya nini uupoteze mwaka mzima wakati Kuna uwezekano mzuri tu wa kufanya makubwa kwa kuanza kitu kidogo kama kuipangilia wiki yako.

    Anza wiki hii kuipangilia kila wiki yako.

    Ni majukumu gani uliyonayo?

    Ili kuipangilia wiki yako kiprofessional, anza kwa kujiuliza ni majukum gani yaliyombele yako kwa wiki inayofuata?

    Kisha yapangilie kulingana na umuhimu. Majukumu ambayo ni ya muhimu zaidi yape kipaumbele kwanza.

    Kwenye siku yako usipange vitu VINGI VYA kufanya. Ukiweza kuwa na vitu vitatu tu vinatosha, vikizidi visiwe zaidi ya sita. Hii itakusaidia kufokasi kwenye mambo machache ila utakayoyawekea NGUVU kubwa na kuyafanikisha pia.

    Unavyoianza wiki yako pia, hakikisha wiki hii unapanga muda wa kujisomea vitabu. Inashangaza kuona kwamba watu wanapangilia mpaka muda wa kula ila hawapangilii muda wa kujisomea. Changamoto kubwa ni kwamba, tumbo likiwa na njaa huwa linapiga kelele. Ndiyo utasikia mtu anasema; “nina njaa“. Ila akili yako ikiwa na njaa haisemi. Ila ilipata utapiamlo wa akili, utazidi kuwa nyuma mara zote. Hivyo, fanya kadiri uwezavyo kuhakikisha kwamba, kila siku unapata muda wa kujisomea.

    Pata kozi yoyote fupi. Online kuna kozi nyingi fupi. Kwenye ratiba yako weka muda wa kujifunza kozi yoyote fupi kuhusiana na eneo ambalo ungependa kulifahamu kwa undani. Inawezekana Hilo eneo tayari unalifahamy vizuri tu, lakini Kuna jambo moja au mawili unaweza kujifunza kuongezea au kutanua kile ambacho tayari unajua.

    Siwezi moja kwa moja kukwambia ujifunze kozi gani, ila fahamu ya kuwa kozi za namna hii zipo nyingi. Ni juu Yako kujua wapi unahitaji KUWEKEZA NGUVU ili uwe Bora zaidi. Maeneo ya kujifunza na kupata kozi kama hizi pia ni mengi, mfano skillshare, Udemy, Coursera, learn digital with Google, na nyingine nyingi kama zinavyoonekana kwenye picha hapo chini.

    Pia hakikisha unaondoa vitu vyote ambavyo siyo sahihi, vitu kama mitandao ya kijamii, kuangalia video YouTube, TikTok. Kiufupi ni hivi, usiwekeze muda wako sehemu ambazo siyo sahihi, mara zote wekeza muda wako eneo sahihi ili uweze kupata matokeo sahihi.

    Waangalie role models wako. Ni wazi kuwa Kuna watu ambao kwenye maisha Yako unatamani kuwa kama wao. Kwa Kila jambo unalotaka kufanya jiulize kama angekuwa [jina la role model wako] angefanya hivi? Kuna vitu VINGI unafanya ambavyo role model wako hafanyi. Viepuke.

    Anza kufanyia haya kwa wiki hii, tukutane hapahapa kesho kwa ajili ya somo la jingine zuri kama hili.

    Mpaka wakati mwingine.

    Mimi ni Godius Rweyongeza.

    Tuwasiliane 075584891

    Kitu kimoja Cha ziada😁

    Mwezi wa sita tunaenda kuwa na semina Babu kubwa.

    Itafanyika tarehe 28 na 29 Juni. Itakuwa siku ya Jumamosi na Jumapili.

    Hivyo, nichukue nafasi hii kukukaribisha sana kwenye semina hii ya kipekee rafiki yangu.

    Kwa maelezo zaidi kuhusiana na semina jiunge kwenye kundi la semina hapa👇🏿

  • Jinsi Ya Kuandaa Kizazi Cha Wafanyabiashara

    Juzi nilikuwa nasoma ujumbe wa mkurugenzi mkuu wa TELEGRAM.
    Alizungumzia namna kampuni za kichina zinavyofanya vizuri na namna ambavyo zitafanya vizuri kwa siku zijazo kutokana na mfumo mzuri wa elimu walionao.

    Kitu hiki kimenitafakatisha sana na Leo nikaona nikuandalie ujumbe muhimu wa namna Leo hii tunavyoweza kuanza kuandaa kizazi kijacho Cha wajasiriamali, kizazi ambacho kinaweza kwenda kupambana huko duniani, na kuleta mapinduzi makubwa.

    Kwa Nini nasema tuandae kizazi Cha wajasiriamali? Kwa sababu wajasiriamali ndiyo wanakuja na mawazo mengi ya kibunifu na ndiyo ambao wanaweza kukuletea mabadiliko MAKUBWA yajayo.

    Kinachofanya wachina wanaonekana tishio Leo hii ni kwa sababu ya wajasiriamali na wabunifu walio nao. Na kitakachofanya sisi tufanye MAKUBWA ni kwa sababu ya wajasiriamali tulionao pia.
    Hivyo basi rafiki yangu huu ni wakati wetu sisi kuanza kuandaa kizazi kijacho Cha wajasiriamali.

    Sasa tunawaandaaje. Kwanza, tuwaandalie mazingira ya kiushindani kama ambavyo anatuelekeza hapo mkurugenzi mkuu wa TELEGRAM. Pili, tuwaandalie mazingira ya kuanza kufanya biashara wakiwa wadogo. Aidha tunaweza kuwapa miradi midogo midogo nyumbani waisimamie.

    Tatu, tushirikishane nao kwenye biashara zetu. Sambamba na shule nzuri tunazowasomesha, tushiie tu hapo, wakitoa shule au siku za wikendi twende nao kwenye biashara au kazi tunazofanya. Na wao washiriki pia.

    Nne, Kuanzisha Mafunzo ya Ujasiriamali Mapema. Kwa kuwa hatutegemei kuwa na mfumo huu ukiwekwa kwenye elimu ka haraka. Basi tutakachofanya ni kuwapeleka watoto kwenye Mafunzo ya kibiashara sisi wenyewe au ili kuwafundisha misingi ya biashara, fedha, na ubunifu tangu wakiwa wadogo. Rafiki yangu Innocent huwa anatoa Mafunzo ya namna hii kila jumamosi.

    Tano, kuwahamasisha Kufikiri Kibiashara. Ni muhimu sana tuanze Kuwaelekeza watoto kuona fursa kwenye changamoto. Wajue wazo kuwa changamoto ni fursa. Kumbe, badala ya kutegemea ajira kama suluhisho pekee la maisha wafikiri nje ya hapo na tuwaelekeze hili mapema.

    Badala ya kuwaambia kwamba nenda shule USOME kwa bidii ili uje uajiriwe. Tuwaambie waende shule, wajifunze kwa bidii ili waje watumie ujuzi watakaojifunza kusaidia KUTATUA matatizo Yao.

    Sita, kuwajengea uwezo wa ubunifu na uvumbuzi. Kuwatia moyo kutumia mawazo yao kuunda bidhaa au huduma mpya zitakazosaidia kutatua matatizo ya jamii. Ni kwa namna Gani hili tunaweza kukifanya tukiwa nyumbani, ni kwa
    1. Kuwazoesha kuwapa maswali badala ya majibu
    2. Kutokuwa wepesi wa kujibu maswali Yao hata pale tunapokuwa tunajua majibu ya maswali Yao
    3. Kutowaepusha na magumu hata pale tunapoweza kufanya hivyo.

    Saba, kuwafundisha umuhimu wa akiba na uwekezaji . Kwa kila fedha unazowapa kwenda shule, waambie pia wajenge utaratibu wa kujilipa wenyewe kwanza kwa KUWEKA akiba. Akiba itawaba wakiwa wakubwa.

    Nane, kuwahamasisha kuchukua hatua bila hofu.
    Utasikia mzazi anamwambia mwanae, ukikokoaea kufanya kitu fulani nitakuua. Na kauli nyingine nyingi hasi. Badala ya kuwatishia hivyo, wahamasishe wachukue hatua hata kama muda mwingine wewe mzazi unakuwa na hofu au wasiwasi.

    Kuwaunganisha na wajasiriamali waliofanikiwa ukipata nafasi ya kushiriki semina au kukutana na watu waliofanikiwa nenda na wanao. Waone watu waliofanikiwa wanaongeaje, wanaishije, wanatendaje. Watajifunza mengi kwa kuona kuliko wewe kuwaambia kwa mdomo tu.

    Kuwajengea Uwezo wa Mawasiliano na Ushawishi
    Ni muhimu sana tuwafunze watoto wetu umuhimu wa kuwasiliana na kuwasiliana mawazo Yao. Maana itafikia hatua watakuwa na wazo, na watatakiwa kuliwasilisha kwa wateja au wawekezaji. Sasa bila ya kuwa na ujuzi mzuri wa mawasiliano hawataweza kufanya makubwa.

    Kuwafundisha maadili ya ujasiriamali. Maadili ya uaminifu, uvumilivu, bidii, na kujali n.k
    Haya pia ni maadili muhimu ambayo yatawabeba watoto wetu.

    Hayo ni mambo machache ya kuanza nayo.

    Wewe unaenda kuanza na jambo Gani

    By the way mwezi wa sita tutakuwa na semina, Na Moja ya mada itakayofundishwa ni mada ya NI NAMNA YA KUANDAA KIZAZI KIJACHO CHA WAJASIRIAMALI chini ya mkufunzi wetu Innocent Kavishe.

    Karibu sana kwenye semina hii ya kipekee.

    Karibu sana kwenye semina ya biashara na uwekezaji mwaka 2025

    Rafiki yangu mpendwa, kila mwaka huwa tunakuwa na semina tatu. Semina moja huwa inafanyika kuanzia tarehe 15-30 Januari KWA NJIA YA MTANDAO. Semina ya pili huwa inafanyika wikendi ya mwisho ya mwezi wa Juni (hii ni ya ana kwa ana), na semina nyingine huwa inafanyika septemba wiki ya mwisho (tarehe 24-30 septemba). Hii huwa inafanyika mtandaoni pia.

    Semina ya mwezi wa sita huwa ni semina ya ana kwa ana, na kwa mwaka huu 2025 itafanyika tarehe 29-30 Juni. Itakuwa ni siku ya jumamosi na jumapili. Itafanyika KINGSWAY HOTEL MOROGORO.

    Semina hii ya ana kwa ana imekuwa inafanyika na huu utakuwa ni mwaka wetu wa tatu mfululizo. Semina ya mwaka huu inaenda kuwa ya tofauti na ya pekee.

    Hivyo, nichukue nafasi hii, kukukaribisha sana kwenye semina ya biashara na uwekezaji mwaka 2025.

    Katika semina hii ya mwaka 2025 tumekuandalia mambo makubwa yafuatayo.

    SIKU YA KWANZA 29.6.2025:

    1. MISINGI YA KUKUZA BIASHARA KWENYE ULIMWENGU WA LEO
    2. JINSI YA KUAGIZA BIDHAA NJE YA NCHI (CHINA)
    3. MAMBO YA KUZINGATIA BAADA YA KUSAJILI KAMPUNI
    4. KUTUMIA RASILIMALI ZA WATU WENGINE kwa VITENDO
    5. JINSI YA KUJENGA BRAND YAKO
    6. ELIMU YA KODI KWA WAFANYABIASHARA

    SIKU YA PILI: 30.6.2025

    1. KUTOKA KUAJIRIWA MPAKA KUMILIKI BIASHARA (mwongozo kamili)
    2. ELIMU YA FEDHA NA UWEKEZAJI
    3. WANANDOA NA BIASHARA (misingi ya kusimamia biashara kama wenza na urithi kwa watoto)
    4. ITAWALE HOFU YA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA
    5. ELIMU YA FEDHA KWA WATOTO NA NAMNA YA KUANDAA KIZAZI KIJACHO CHA WAFANYABIASHARA
    6. KUFIKIRI NJE YA 18 2025 (MWONGOZO KUSIMAMIA BIASHARA ZINAZOJIENDESHA)

    Hizo ndizo mada ambazo tutazungumzia kwa undani mwaka huu. Kiukweli unaenda kuwa ni mwaka wa kipekee sana na mwaka wa kufanya makubwa.

    Imani yangu ni kwamba wewe…………………………..utakuwa mmoja wa washiriki wa semina yetu ya mwaka huu. Umekuw unakosa semina za miaka mingine yote,mwaka huu usikubali kamwe kuikosa semina hii.

    Pambana kadiri uwezavyo kuwepo kwenye semina yetu.

    Ada ya semina itakuwa 170,000/- kwa atakayeshiriki semina hii kwa siku mbili.

    Wakati kwa atakayeshiriki semina hii kwa siku moja ada ya semina itakuwa 100,000/- tu. Na atakayeshiriki semina kwa njia mtandao kwa siku zote mbili itakuwa 85,000/- tu

    Njoo tuungane mwaka huu kwenye semina hii ya kipekee ili uweze kufanya makubwa kwenye eneo la biashara yako na maendeleo binafsi.Bonyeza hapa sasa.

    Kuhusu malipo ya semina

    Kwanza chagua aina ya package ambayo utashiriki. Kama utashiriki kwa siku mbili au kwa siku moja au kwa njia ya mtandao.

    Unaweza kulipia ada yote ya SEMINA mara moja au unaweza kulipia kidogokidogo pia.

    Kwa mfano, unaweza kuanza utaratibu wa kulipia kila mwezi kwa kuigawa ada yote ya semina kwa miezi minne ambayo tunayo mbele yetu. Ukilipia 50,000 kila mwezi kuanzia sasa. Mpaka kufikia siku ya semina ada yote ya semina itakuwa imeshakamilika.

    Unaweza pia kuanza utaratibu wa kulipa kila wiki 15,000 tu.

    Au kila siku elfu mbili tu.

    Chukua hatua sasa uanze kulipia.

    Namba ya malipo ni CRDB: 0150984455500 JINA ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    Au TIGO PESA: 19016638 jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    Karibu sana rafiki yangu

    NB: kwenye ukurasa unaofuata nimekuambatanishia ratiba kamili ya semina na wakufunzi watakaondisha siku hiyo. KARIBU SANA.

    Ni mimi kijana wako

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

  • Njia Bora Ya Kufanya MAKUBWA Ni Hii by Godius Rweyongeza

    Pengine umekuwa unajiuliza ni kwa namna gani naweza kufanya makubwa kwenye maisha yangu?

    Ukweli ni kuwa haya makubwa unayotamani kuyafanya kwenye maisha yako, hayawezi kuja tu yenyewe bila ya wewe kufanya kazi.

    Njia bora ya wewe kufanya makubwa ni kwa wewe kuhakikisha kwamba unatoka hapo ulipo na kwenda kufanya kazi. Kwenye ulimwengu wa leo sambamba na teknolojia zote ambazo zimegunduliwa, hakuna teknolojia ambayo imechukua nafasi ya kazi.

    Hivyo basi fahamu wazi kuwa kazi ni kitu ambacho hutaweza kukikwepa kamwe. Kuwa tayari kufanya kazi na kuweka kazi pale panapostahili kazi ili uweze kupata matokeo ambayo unataka kupata.

    Tuendelee mbele ili uweeze kuangalia video hii yenye somo kubwa sana kwako. Bonyeza hapa kuiangalia.

    https://youtu.be/y-YR1fqBvTQ

  • ukijua kitu kifanyie kazi

    Utasikia mtu anakwambia kwamba hiki nakijua, nilijifunza chuo. Hiki nakijua…

    Kama unakijua kwa nini hukifanyii kazi? Rafiki yangu kitu kikubwa ninachotaka kukwambia siku ya leo ni kwamba kujua pekee hakutoshi. Unapaswa kujua vitu na kuvifanyia kazi pia.

    Hiyo ndiyo inaenda kuwa tiketi yako wewe kukfanya makubwa.

    Haitoshi tu kwa wewe kujua kuweka akiba, bila ya kuweka akiba.

    Haitoshi tu kwa wewe kujua kwamba ni muhimu kufanya mazoezi bila ya kuyafanya.

    kuna watu wengi wanajua vitu ila hawavifanyii kazi.

    sasa wewe utakuwa na tofauti gani na hao wengine.

    wewe unapaswa kujua vitu na unapaswa kuvifanyia kazi pia.

  • Nguvu ya kushambulia

    Kwenye timu ya mpira wa miguu huwa kuna wachezaji wa aina mbalimbali ila mojawapo ya wachezaji huwa ni washambuliaji. Hawa kazi yao huwa ni kuhakikisha muda wote wanasumbua kwenye lango la mpinzani ili mwisho wa siku waweze kuipatia timu yao ushindi.

    Endapo washambuliaji hawatafanya kazi yao ya kushambulia na badala yake wakaanza kujilinda dhidi ya timu nyingine maana yake ni kwamba, hiyo timu haiwezi kushinda. Haiwezi kushinda kwa sababu hailengi hata kufunga goli hata moja. Na ushindi unakuja kwa kufunga.

    Kadiri mnavyoshambulia kwa wingi ndivyo nafasi yenu ya kufanya vizuri inavyokuwa nzuri kuliko pale mnapokuwa hamshambulii

    Kwenye maisha ya kawaida hivyo hivyo. Wale wanaoshambulia, wana nafsi nzuri ya kufanya vizuri zaidi kuliko wale wanaokuwa hawashambulii.

    Wanaoshambulia ndiyo wanaofanya makubwa.

    Pengine unaogopa kushambulia kwa sababu unaogopa unaweza kushindwa goli na hivyo kuonekana kama hujui? Si ndiyo?

    Kwenye hili nikuletee nukuu muhimu sana ya Michael Jordan aliysema kwamba nimeshindwa mara nyingi sana, ndiyo maana nashinda. Kama unataka kushinda, shindwa kwanza.

    Kushindwa ni tiketi yaw ewe kufanya  makubwa sana.

    Nimewahi kabisa mpaka kuandika kitabu kinaitwa. Nyuma ya ushindi, kuna kushindwa, kushindwa, kushindwa. Kama hujawahi kupata nakala ya hiki kitabu, nakushauri ujipatie nakala yako mapema iwezekavyo. Kitakusaidia kukupa mwanga wa namna unavyoweza kufanya makubwa, hata katika mazingira ambayo unapitia changamoto.

    Kujipatia nakala ya kitabu hiki, naomba tuwasiliane kwa simu 0755 848 391

  • Shukrani

    Moja ya kitu muhimu sana ambacho unapaswa kukifanyia kazi ni kuwa mtu wa shukrani. Kila siku inayokuja kwako ni nafasi nyingine ya wewe kushukuru.

    Una mengi ya kushukuru kwenye maisha yako. Wengi huwa wanasubiri mpaka waone mambo makubwa ili waweze kushukuru. Ila ukweli ni kuwa kwa mambo yanayoendelea kwenye maisha yako, una mengi ambayo leo hii unaweza kukaa chini na kushukuru.

    Kila siku chukua notebook yako. kisha

    • Shukuru kwa ajili ya uhai wako
    • Shukuru kwa ajili ya kuwa na familia yako
    • Shukuru kwamba una mwenza
    • Shukuru kwamba una watoto
    • Shukuru kwamba umeweza hata kusoma hhii makala
    • Shukuru kwamba bado unaendelea kuipambania ndoto yako

    Hapa najaribu tu kukuonesha baadhi ya vitu ambavyo unaweza kuanza navyo kwenye kushukuru siku ya leo. Vipo vingi unavyoweza kushukuru na hivi ni baadhi tu.

    Kazi inabaki kwako.

    Siku ya leo ni jambo gani unaaenda kushukuru kwa kuwa nalo?

  • Watu

    Ili ufanikiwe unahitaji watu, tena watu sahihi.

    Hivyo basi rafiki yangu, pambana kuzungukwa na watu sahihi. Ukikaaa na watu ambao siyo sahihi watakuangusha.

    Unajua kwa nini watakuangusha, watakuangusha kwa sababu fikra zao ni za kuanguka wala siyo za kuinuka.

    Inabidi ukae na watu wenye fikra za kuinuka, ili uinuke.

    Swali langu kwkao siku ya leo ni je, ni kwa namna gani unakaa na watu sahihi kwenye maisha yako?

  • Usikose mara mbili

    Rafiki yangu, kwenye makala ya jana nilikusisitiza kitu kimoja muhimu sana. Kitu hiki ni kufanya kila unachofanya kwa msimamo, na kwa mwendelezo. Kama hukusoma hii makala, rudi hapa uisome kwa umakini mkubwa.

    Msimamo na mwendelezo.

    Kitu hiki ni kutokuacha kufanya kitu husika zaidi ya mara mbili. Ikitokea kuna siku umeshindwa kufanikisha kitu fulani ambacho umepanga kufanya,  basi walau kesho yake usishindwe kufanya hivyo.

    Usikose mara mbili. Kosa leo ila siyo na kesho pia.

    Pambana kadiri ya uwezo wako kuhakikisha haukosi kufanya jambo ulilopanga kufanya mara mbili mfululizo.

    Kama umepanga kuweka akiba, pambana uwezavyo usiache kuweka akiba mara mbili mfululizo. Kama umepanga kuwekeza, pambana kadiri iwezekavyo ushindwe kufanya hivyo mara mbili mfululizo.

    Ukiona umekosa siku ya kwanza, kufanya jambo fulani. Ukaona na siku ya pili pia hujaweza kufanya hivyo, basi ujue wazi kuwa hutaweza kuwa na mwendelezo kwenye jaambo lako na itakuwa vigumu kwako kuweza kufikia mafanikio makubwa

    Sasa swali la pekee ambalo n ingependa kukuacha nalo siku ya leo ni kwamba, ni kitu gani ambacho umekuwa unatamani kufanya kwa mwendelezo? Na ni kwa namna gani unaenda kukifanyia kazi kuanzia sasa hivi?

    Tukutane kwenye makala ya kesho

  • Msimamo na mwendelezo

    Rafiki yangu moja ya kitu cha muhimu sana kwa wewe unayetaka kufanya makubwa ni kuwa na mwendelezo kwenye kitu ambacho unafanya. Wengi huwa wanaweza kufanya kitu mara moja, ila siyo kwa mwendelezo. Wewe unahitaji kuwa na mwendelezo kwenye kazi na shughuli zako zote unazofanya.

    Ukianzisha kitu, usikifanye mara moja tu. Bali kifanye kwa mwendelezo kwa siku nyingi zinazofuata. Mafanikio ya kweli yapo kwenye kufanya vitu kwa mwendelezo ba siyo kufanya mara moja tu.

    Wengi huwa wanaweza kuanza kuweka akiba, ila siyo wote wanaweza kuwa na mwendelzo kwenye kuweka akiba.

    Wengi huwa wanaweza kuanza kufanya mazoezi, ila siyo wote ambao huwa wanakuwa na mwendelezo kwenye kufanya mazoezi. Wengi huwa wanaweza kuanza kunoa vipaji vyao, ila siyo wote ambao huwa wanakuw ana mwendelezo kwenye hilo.

    Na kwa sababu tu ya kukosa mwendelezo wengi huwa wanaishia kujishangaa kwa nini hawapati matokeo na mafanikio makubwa. Kumbe kinachowafanya wasipate mafanikio makubwa ni kwa sababu hawana mwendelezo kwenye kufanya kile ambacho wanaamua kufanya.

    Sasa rafiki yangu naomba nikwambie kitu kimoja muhimu sana. Kwa kitu chochote ambacho utachangua kufanya mwaka huu, hakikisha kwamba unakuwa na mwendelezo. Usifanye kitu na kuishia njiani. Bali kifanye kwa msimamo na kwa muda mrefu.

    Tukimwangalia mtu kama Warren Buffet ambaye amekuwa anawekeza tangu ana miaka 11 mpaka leo hii, tunachojifunza kwake ni kwamba amekuwa anawekeza kwa mwendelezo na kwa msimamo.

    Tukisoma historia ya mtu kama Kobe Brayant tunagundua kwamba alikuwa anaamka mapema na kuanza kufanya mazoezi, na anachelewa kulala. Na hii ndiyo ilikuwa ratiba ya kila siku. Unachogundua hapo ni mwendelezo.

    Au hata ukisikia Michael Jordan anasema kwamba, nimeshindwa mara nyingi sana ndiyo maana nashinda. Ni kwa sababu anakuwa na mwendelezo.

    Wewe pia kuwa na mwendelezo kwenye kitu ambacho unafanya.

    Usifanye kitu mara moja tu.

    Usifanye mara mbili. Hapana

    Fanya kwa mwendelezo na kwa msimamo. Kwa muda mrefu bila kuacha.

    Makala hii imeandikwa name rafiki yako wa ukweli.

    Godius Rweyongeza

    Tuwasiliane sasa kwa namba ya simu 0755848391

    Karibu sana

  • Mwezi januari unaisha, umeulaani au umeubariki? Umekuwa wenye Baraka kwako au wenye karaha?

    Rafiki yangu mpendwa, nichukue nafasi hii kukupongeza sana kwa kuumalizia mwezi wa Januari. Najua wazi kuwa haujawa mwezi rahisi, hivyo nikupongeze sana kwa hilo.

    Mwezi januari unapofikia tamati, ningependa kwa pamoja tufanye tafakari kuhusiaa na mwezi huu wa kipekee. Mwisho wa siku tujiulize kuwa mwezi huu umeubariki au umeualaani? Umekuwa wenye Baraka kwako au wa karaha?

    Kila mwaka huwa kuna mwezi Januari na kila mwaka kuna mwezi Disemba.

    Na sote tunafahamu kwamba kuna majukumu ambayo yako mbele yetu.

    Kwa wengi tunajua kwamba ukifika mwisho wa mwaka na hasa sikukuu, kuna sherehe. Kwa wengi matumizi ya pesa huwa yanakuwa juu. Huwa yanahusisha kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kitu ambacho huwa kinaongeza gharama za matumizi na kuzifanya kuwa kubwa zaidi

    Kwa kuwa huwa ni sikukuu huwa tunaenjoy, lakini wakati huohuo ni kama huwa tunasahau majukumu yetu ya muhimu.

    Majukum ya januari. Kwa upande mwingine ni kwamba Januari ni mwezi wa kipekee pia. kwa kuwa watoto huwa wanafunga shule disemba yote, januari baada ya sikukuu kuisha, huwa ni muda wa watoto kurudi shule sasa ili wasome.

    Na hapa ndipo swali langu la kwanza linapojikita leo. Januari inapoisha umeibariki au umeilaani?

    Najua unajua wazi kwamba una watoto wako. Labda mmoja au wawili, watatu n.k

    Hiki siiyo kitu ambacho mimi napaswa kukufundisha si ndio?

    Lakini pia unajua wazi kwamba watoto hawa wanapaswa kwenda shule Januari au la! Kwa mfano leo hii unaposoma hapa, unajua mwakani kwamba wanao watakuwa wanaenda shule au watakuwa hawaendi. Kama watakuwa wanaenda maana yake maandalizi ya mapema yanatakiwa kufanywa kuanzia leo hii. Changamoto ya watu wengi ukiwaambia wafanye maandalizi ya ada ya mtoto mwkani wanaona ni kitu cha ajabu sana. Wengi wataishia kukwambia siku bado. Lakini sasa unabaki unajiuliza. Bado nini? Sasa mtu huyuhuyu subiri ifike januari.

    Ndiyo anaanza kukwambia Januari ni ngumu na hizi ada za watoto. Sasa kwa maneno hayo unakuwa unaibariki Januari au unakuwa unailaani? Je, watoto wako unakuwa unajivunia kuwa nao au unalaumu?

    Yaani, ni kama vile hao watoto kuna mtu aliwaleta kwako ghafla na kukuamuru kwamba kuanzia leo hii hawa ni watoto wako, walee. Lakini kumbe watoto umewazaa mwenyewe, umewalea mwenyewe na sasa hivi kukosa kwako mipango ndiyo unaanza kuilaani Januari, na hata watoto wako unaanza kuwaona kama karaha? Haya ni ya kweli? Ebu jirekebishe bwana kuanzia mwaka 2025.

    Ujue kama unaweka malengo, huwa kuna malengo ambayo yanajirudia kila mwaka. Lengo la kulipa ada kila januari liweke kama lengo ambalo linajirudia kila mwaka.

    Pengine badala ya kusubiri kulipa ada Januari, unaweza kuwa unailipa mapema. Disemba au novemba.

    Nakumbuka mwishoni mwa mwaka jana nilikutana na mama mmoja aliyekuwa anajiandaa kwenda uchagaani kwa ajili ya likizo. Lakini kabla ya kufanya maandalizi ya kitu chochote, kitu cha kwanza alichofanya ilikuwa ni kuhakikisha amelipa ada zote za watoto.

    Siku hiyo nilikutana naye njiani anatabasamu, ikabidi nimuulize kulikoni, ndipo aliponiambia kuwa nimelipa ada zote za watoto, hapa hata nikienda nyumbani nikajisahau nikatumia hela zote, nitakuwa bado na uhakika wa ada za watoto kuwa zimelipwa.

    Nilichojifunza kwa mama huyu ni kwamba, badala ya kusubiri mpaka Januari uanze kulalamika kuhusiana na watoto wako, ANZA KUANDAA HIZI ADA MAPEMA. Kisha jipange kuhakikisha kwamba unailipa mapema kabla hujaila.

    Unapolalamika kuhusiana na kulipa ada Januari wakati ni wajibu wako. Ni kama unakuwa unaona karaha kuwa watoto wako. Ni kama unakuwa unawalaani kuwa bora wasingezaliwa.

    Makala hii imeandikwa na

    GODIUS RWEYONGEZA

    Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0755848391

X