-
Hii ndiyo sifa kubwa ya kitabu unachopaswa kuandika
Rafiki yangu, sifa moja kubwa ya kitabu unachopaswa kuandika ni kwamba kitabu chako kinapaswa kujikita kwenye kujadili mada moja kwa undani zaidi. Mtu anapochukua kitabu, tunategemea kwamba anapaswa kupata maarifa ya kina kuhusiana na kile ambacho umeandika.
Si jambo zuri kuandika kitabu cha kila kitu.
Ndiyo maana huwa tunaandika kitabu cha pili au cha tatu na kuendelea.

-
Nukuu 14 Za Kufikirisha
1.

2.

3.

4.

5.

6.

7.

8.

9.

10.

11.

12.

13.

14.

-
Namna Rahisi Ya Kujifunza Ujuzi Utakaokulipa
Ni ujuzi gani ambao unalipa zaidi na ninawezaje kujifunza ujuzi huu. hapo zamani za kale kama ulitaka kujifunza ujuzi kama huu, ulitakuwa kuhakikisha kwamba unakutana na wabobezi na kujifunza kutoka kwao kwa kufanya. Kitu hiki kiliitwa uanagenzi. Leo hii mfumo wa uanagenzi ni kama umepotea na kuja katika mfumo wa tofauti kabisa.
Ambapo leo hii mtu yeyote mwenye nia ya kujifunza anaweza kujifunza na kunufaika na mafunzo ambayo yanatolewa na walimu mwengi mfano kupitia youtube. Linawezekanaje hili, hayo na mengine mengi nimyaeleza kwenye video hi hapa.
-
Naomba kuanzia leo hii uanze kumfuatilia mtu huyu, hutajutia…

Naomba kuanzia leo hii uanze kumfuatila mtu huyu, hutajutia…
Moja ya kitu ambacho watu wengi wanakosea ni kufuatilia maisha ya watu wengine kuliko wanavyojifuatilia maisha yao binafsi. Ninachotaka ufanyie kazi rafiki yangu kuanzia leo ni kuanza kujifuatilia maisha yako mwenyewe.
Inawezekana moja ya kitu kinachokufanya wewe ufuatilie maisha ya watu wengine ni kwa sababu haujijui.
Hauju ni kitu gani unapaswa kufanya.
Haujui ni kipaji gani ulichonacho.
Hiki kitu kinakupelekea wewe kufuartilia maisha ya watu wengine., unafuatilia wengine wanaishije, unafuatilia wengine wanakula nini na mengine mengi.
Huyo hapaswi kuwa wewe.
Leo jipe kazi moja tu. Kazi ya kujifuatilia wewe mwenyewe. Kwamba wewe ni nani, kwa nini uko hapa duniani na nini haswa ambacho unapaswa kuwa unafanyia kazi? Jipe hili jukumu rafiki yangu, nina uhakika kwa kujifahamu mwenyewe utaweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Hakuna ukuaji wowote utakaoupata kwa kufuatilia maisha ya watu wengine. Lakini utaweza kupata ukuaji mkubwa kwa kitendo cha kujifuatilia mwenyewe tu. Hivyo, jifuatilie mwenyewe kwanza.
SOMA ZAIDI: Mfuatilie huyu jamaa kwa mwezi mmoja tu, wewe mwenyewe utaniambia utakachoona
Umekuwa name rafiki yakow a ukweli
Godius Rweyongeza
Nifuatilie youtube kupitia hapa
-
Nukuu 15 Za Kufikirisha

2.

3.

4.

5.

6.

7.

8.

9.

10.

11.

12.

13.

14.

15.

-
Muda mzuri wa kupanda mti ilikuwa ni miaka 10 iliyopita…muda mwingine mzuri zaidi ni sasa
Wahenga wanasema kwamba muda mzuri wa kupanda mti ulikuw ani maiaka 10 iliyopita, na muda mwingine mzuri zaidi ni sasa.
Chukua hatua sasa.
-
Njia ya kukusaidia kufanya makubwa
rafiki yangu mpendwa, wengi wamekuw awnatamani kufanya makubwa kwenye msiah ayo. hata hivyo, siyo waote wamekwuwa wanaishia kufanya makbwa. Mjaya sababu kwa nini watu wengi hawawezi kufanya makubwa ni kwa sababu hawajui kitu kimoja u, ambacho nimekieleza zaidi kwebye kitabu hiki.
-
Mtag ambaye ungependa ujumbe huu umfikie

Kwenye vipindi mbalimbali vya redio huwa kuna kipindi cha kutuma salamu na ujumbe.
Kama kuna mtu ambaye leo hii ungependa ujumbe huu umfikie mtag hapa ili aje auone.
UWE NA SIKU NJEMA
-
Hiki Ndiyo Kiwango cha mafanikio ambayo unapaswa kuyapigania

/
Rafiki yangu aliwahi kuniambia kwamba kuna wakati aliangalia tamthiliya. Kwenye tamthilya hii kuna jamaa aliachwa na mke wake. Mke alimwacha kwa sababu jamaa hakuwa na hela.
Badala ya kukimbilia kuingia kwenye mahusiano mengine ili amuoneshe ex wake kwamba hajamkomoa kwa kuachwa. Jamaa aliamua kuanza kupambana ili kujenga biashara na kuzisaka hela.
Akapambana kwelikweli kiasi kwamba ikafikia hatu aambapo ex wake alikuwa ni shabiki wake kwenye vitu alivyokuwaanafanya.
Na siyo tu ex wake bali ex wake na mme wake wote kwa pamoja walianza kumshabikia jamaa.
Hiki ni kiwango cha mafanikio ambayo unapaswa kukipigani hasa unapoachwa kwa sababu huna hela. Badala ya kukimbili kufanya yale ambayo siyo ya muhimu. amua kwamba unaenda kuwekeza nguvu zako zote kwenye kutafuta pesa.
Badalaya kutafuta mchumba mwingine ili utambe kwa ex wako kuwa amekuacha kwa bahati mbaya, amua kwamba unaenda kuwekeza muda wako na nguvu zako kwenye kipaji, kujenga ujuzi au kitu ambacho kitakufanya kuwa mtu wa pekee.
Amua kuachana na kitu kingine chochote ambacho kitakuwa kinyume na hapo.
Ni kwa namna hiyo utaweza kujiondoa kwenye hali ya kuwa unaachwa kila wakati kwa ajili ya pesa rafiki yangu. Pambania malengo na ndoto zako kubwa kuanzia sasa.
Nakutakia kila la kheri.
-
Kitu Hiki Unapaswa Kukibadili Mara Moja

Moja ya siku ambayo watu huwa wanaadhimisha ni siku ya kuzaliwa. Ukiachana na sikukuu ya kuzaliwa kuna sikukuu maarufu sana ambazo huwa tunaadhimisha, ikiwa ni pamoja na Eid, Pasaka, Krismasi, Mwaka mpya na nyingine..
Ukiziangalia hizi sikukuu zote zina kitu kimoja ambacho kinaziunganisha. Hizi sikukuu zote huwa zinatokea kwa sababu ya kalenda. Ni sikukuu za kikalenda.
Hii nbdiyo kusema kwamba furaha yote ambayo huwa unakuwa nayo siku ya sikukuu hizi inatokana na kalenda. wewe hakuna juhudi zozote ambazo unaweka kuhakikisha sikukuu hizi zinatokea.
Utake usitake lazima tu sikukuu hizi zitakuwepo.
Hivyo, kufurahia kwenye sikukuu hizi ni jambo zuri lakini usisahau kuwa kitu unachoshangilia kwamba kimetokea hujakisababisha wewe.
Ninachotaka uanze kufanyia kazi baada ya hapa ni wewe kuhakikisha unaanza kupambania malengo yako makubwa. Mwaka huu usiishie tu kushereheakea sikukuu ya kuzaliwa na sikukuu nyingine ambazo ziko nje ya uwezo wako. Yaani, sikukuu ambazo hujazisababisha wewe kutokea., Bali sambamba na mafanikio mengine ambayo utasherehekee mwaka huu basi uweze kusherehekea na mafaniko ambayo umeweza kusababisha mwenyewe.
Kuna kitu kimoja ambacho kama utakipambania unaweza kukileta kwenye uhalisia. Ni kitu gani hicho kimoja? hiki ndicho kitu pekee ambacho unapaswa kukipambania usiku na mchana na bila kukwama wala kuyumbishwa na mtu yeyote.
Kama utaanza kupambania malengo na ndoto zako leo, nakuhakikishia kuwa wanaoonak kama huwezi kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa, kuna siku hawahawa watakuwa wanakushangilia kuwa umeweza kuzifanyia kazi ndoto zako mpaka zikaja kwenye uhalisia.