-
Mchakato ni bora zaidi kulliko malengo
Kwenye mojawapo ya kitabu cha Robert Kiyosaki, ameandika kwamba watu wengi huwa wanapambana kuweka malengo ila huwa wanasahau kitu kimoja muhimu sana. na kitu hiki siyo kingine bali ni mchakato wa kufanyia kazi malengo na ndoto ambazo mtu unakuwa nazo.
Kumbe moja ya changamoto ambayo inawakumba watu wengi wanaoweka malengo siyo tu kuweka malengo, bali ni kuweka malengo na kutoyafanyia kazi. suluhishio la hili ni kuwa n mchakato kamili wa kufanyia kazi malengo yako mpaka yatimie. Na hapa ndipo unakuja huo usemi unaosema kwamba mchakato ni bora zaidi kuliko malengo.
Unajua kwa nini watu wengi huwa wanaweka malengo kwa mfano malengo ya kuweka akiba ila bado huwa wanashindawa kuyafanikisha ilihali malengo hayo huwa ni mazuri na ya kupendeza. Ukweli ni kwamba mchakato wa kufanyia kazi malengo hayo ndiyo huwa unakosa.
Kumbe, mchakato wa kufanyia kazi malengo na ndoto zako ni bora zaidi kuliko malengo yenyewe.
Unapokuwa na mchakato maana yake, malengo yako unayapa nguvu. malengo yako unawekea mfumo wa kufanyika hata kama haupo. malengo yako unayapa uhai.
Mfano kama lengo lako ni kuweka akiba. unaweka mfumo wa kukata hela kwenye akaunti yako kila inapoingia. au kila baada ya muda fulani. hapo unakuwa umeweka mchakato. na mchakato huu utakuwezesha wewe kufanikisha lengo lako bila wasiwasi wowote. Ndiyo maana nakwambia kwamba mchakato ni bora zaidi kuliko hata lengo lenyewe unalokuwa nalo.
SASA SWALI la kujiuliza siku ya leo ni kwamba je, una malengo yoyote ambayo umeyaweka kwenye maisha yako. kama una malengo, basi ni jukumu lako kuhakikisha kwamba unayawekea mchakao wa kuyafanyia kazi haya malengo bila kuacha.
kama utakwama kwenye kuweka mchakato wa kufanyia kazi malengpo yako, basi tunaweza kuwasiliana sasa. Tuwasiliane kupitia barua pepe godiusrweyongeza@gmail.com ili niweze kukusaidia kwenye hilo.
Kumbuka kwamba lengo lolote lile unaloweka, linaweza kuwekekewa mchakato wa kulifanyia kazi. changamoto inakuwa tu pale unapokuwa hujui namna ya kuweka mchakato kwenye lengo lako ili liweze kufanikiwa. lakini fahamu wazi kuwa mchakato wa kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa, ni bora zaidi kuliko malengo yenyewe.
KUMBUKA Pia kwamba, kama hujui namna ya kuweka mchakato halisi wa kuweka malengo, basi unaweza kuwasiliana nami ili niweze kukusaidia kwenye hili.
Ni mimi rafiki yako
Godius Rweyongeza
07555 848 391
Morogoro-Tz
-
Fanya kitu hiki kila siku ili uweze kuishi ndani ya siku yako kwa ushindi mkubwa sana
Kabla ya kuianza siku yako, hakikisha umeipangilia vizuri. Hakikisha unajua kila kitu unachoend akufanya ndani ya siku husika kwa usahihi. HILI LITAKUSAIDIA SANA KUONDOA MWANYA WA WEWE KUFANYA MAMBO AMBAYO SIYO SAHIHI
Kumbuka kwamba unapoipoteza siku moja, unakuwa siyo tu unaipoteza hiyo. unakuwa unapoteza maisha yako. Sasa utapoteza maisha yako mara ngapi? kumbuka muda unaopita leo haurudi tena. Ukienda ndiyo umeenda huo. Ni muhimu sana kwako kuhakikisha kwamba muda wote na mara zote unakuwa na ratiba maalum ili kujiepusha na kupoteza muda kwa kufanya vitu ambavyo siyo vya msingi.
Unapokuwa bize kwenye ratiba yako muda wote maana yake unakuwa unaifanya akili yako pia iwe bize. Usipokuwa bize ni sawa na kutimiza ule usemi unaosema kwamba an empty miund is devils workshop.
Hii ndiyo kusema kwamba ukisoma kitabu unajiepusha na majanga mengi.
-
Barua za warren Buffet

Moja kati ya wawekezaji wakubwa sana tulionao kwenye nyakati zetu ni Warren Buffet. Huwa anaandika babrua kila mwaka kwa wawekezaji waliowekeza kwenye kampuni yake ya Berishire Hathaway.Ninaenda kuwa nasoma barua zake zote mmoja baada ya nyingine, kila siku. Nitakuwa nakushurikisha hapa ninachojifunza ili na wewe uweze kujifunza na kufanyia kazi kile unachojifunza.
Endelea kufuatilia mafunzo zaidi hapa bila ya kukosa
Kariobu sana
-
Jinsi Bei ya Kuchapisha Kitabu Inavyopangwa: Mambo Muhimu ya Kuzingatia
Moja ya swali ambao watu wengi huwa wanauliza ni kuwa je, kitabu changu kitagharimu kiasi gani kutoa nakala moja? Jibu la hili swali haliwezi kuwa sawa kwa watu wote. Hii ni kutokana na sababu kadhaa ambazo ndizo huwa zinatoa mwongozo kwenye uchapishaji wa vitabu. Sababu hizi ni pamoja na:
1. Ukubwa wa kitabu. Kitrabu chenye ukubwa wa kurasa 50 hakiwezi kutolewa kwa bei sawa na kitabu chenye kurasa 150 kama vitu vingine vyote viko sawa.
2. Idadi ya nakala unazotoa. Mara nyingi kama unatoa nakala nyingi kuanzia mia tano, bei yake huwa inakuwa chini ukilinganisha na pale unapotoa nakala chache.
3. Rangi na vielelezo. Kama kitabu chako kina vielelezo vya rangi, na kinatakiwa kitolewe kwa rangi bei yake itakuwa juu kidogo ukilinganisha na kitabu ambacho kitatolewa kwa black and white.
4. Mpangilio wa kitabu. Vitabu huwa vinapangiliwa kwenye mifumo tofauti, mfano A4, A5, A6, B5 na mifumo mingine. Hiki ni kitu kingine kitakachoamua bei ya kitabu chako kimoja kinachotolewa iweje. Kitabu cha kurasa 100 cha A5 hakiwezi kuwa na bei sawasawa na kitabu cha kurasa 100 cha A6 hata kama vitu vingine ni sawa kama rangi n.k Kitabu cha A5 bei yake itakuwa ni kubwa kidogo. Wakati huohuo wakati kitabu cha A4 bei yake itakuwa ni kubwa zaidi.
Hivyo ndivyo vitu ambavyo huamua bei ya nakala moja ya kitabu unayotoa iwe na bei kiasi gani.
Kama umeandika kitabu na ungependa kutoa nakala zako. Tuwasiliane nikueleze zaidi ni nini unachotakiwa kufanya ili utoe nakala zako mara moja. Nicheki hapa kwa maelezo zaidi

Kuna raha yake kwenye kutoa nakala ngumu
-
Mfungo
Sizungumzii mwezi wa Ramadhan, wala Kwarezima. Nazungumzia mfungo.
Kwamba kuna kitu ulikuwa unafanya, ila kinakutoka kwenye mstari wa kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa. Sasa unaamua kwamba nafuga na ninaacha kukifanya kwa wiki moja.
Kwa mfano ulikuw aunatumia muda mwingi facebook, au youtube au tiktok, unaamua sasa kwa wiki moja ijayo naondoa hii tiktok kwenye simu yangu, na muda ambao nilikuwa nautumia huku ngoja niuweke kwenye kazi.
Yaani, kwamba ile tabia ambayo huipendi, ambayo inakukwamisha unaachana nayo, unajenga tabia mpya, nzuri ya kukufanya usongembele.
Hii unaweza kuifanya hata leo….Usisubiri mwezi wa ramdhan au Kwarezima.
Hivi ndivyo utazidi kuwa bora kwenye maisha yako, hivyo ndivyo utazidi kufanya mazuri na kuwa imara zaidi.
Ni kitu gani ambacho unaenda kufunga kuanzia siku ya leo?
Tujadiliane hapa chini
-
Twende kidijitali mwaka 2025
Rafiki yangu, najua umekuwa unatumia mtandao wa intanenti kwa muda. Lakini kitu ambacho sina uhakika nacho ni kama umekuwa ukiutumia mtandao huu kwa manufaa. Sasa, 2025 twende kidijitali rafiki yangu.
Unajua kwa nini nakwambia hivi, kadiri siku zinavyokwenda, mambo yanazidi kufanyika kidijitali zaidi. Mfano, siku hizi unaweza kuwa nyumbani asubuhi mpaka jioni na mambo yote yakaendelea bila kukwama.
Unaweza kuwa nyumbani na ukafuatilia kila kitu kinachoendelea ofisini kwako kupitia camera ambazo zinapatikana kwa bei nzuri madukani.
Unaweza kuwa nyumbani ukaagiza chakula kikaja mpaka hapohapo.
Unaweza kuwa nyumbani ukatoa au ukaweka hela benki.
Ukawatumia watu hela na mengine mengi.
Unaweza kuwa nyumbani kwako, ukaagiza bidhaa China.
haya yote yanawezekana kwa sababu biashara nyingi zinaenda kidijitali.
sasa cha kujiuliza wakati watu wanaweka biashara zao mtandaoni, wewe biashara yako au kipaji chako kipo huku?
Ndiyo maana, nataka uende kijitali mwaka 2025.
na kwenye hili sina mengi.
nina mabo yafuatayo ambayo kama utayafanyia kazi, yatakuweka mtandaoni moja kwa moja.
moja, fungua tovuti na blog ya biashara yako. Huku weka taarifa za biashara yako, ili iwe rahisi watu wakiingia mtandaoni na kutafuta taarifa za biashara yako wazipate.
Huku weka na bidhaa ulizonazo, na namna watu wanavyoweza kuzipata.
Pili, fungua akaunti kwenye mojawapo ya mtandao wa kijamii. kwakuanzia usianze na kila mtandao wa kijamii, hutaweza. Itakuwa ngumu kwako kuwa instagram, facebook, linkeldn, twitter, tiktok na mitandao mingine ya kijamii. Chagua mtandao mmoja tu. anza na huo. Fungua akaunti huko, na weka maudhui yanaoendana na biashara yako.
hapo sasa umeanza kwenda kidijitali.
Ukishakuwa na wafuasi wa kutosha kwenye mtandao huu, utatanua na kwenda kwenye mitandao mingine.
Kama utahitaji msaada zaidi kuhusu kwenda kijiditali, tunaweza kupanga kufanya mazungumzo ya dakika 15 kati yangu mimi na wewe, ili nikupe ushauri unaoendana na kile ambacho unafanya.
Jibu ujumbe huu kwa kutuma neno KIDIJITALI 2025 ili tupange ratiba ya kuongea.
-
Kufufuka
Kheri ya pasaka rafiki yangu.
Kwa wakristo pasaka, ni kufufuka.
Hata kama wewe siyo mkristo, bado hapa kuna kitu cha kujifunza. Na kitu hiki siyo kingine bali ni kufufuka.
Nataka na wewe ufufuke.
Kwenye maisha ya kila siku tunaanguka. Tunakumbana na vikwazo vingi ambavyo vinatuzuia kusongambele na kufanya makubwa. Tunaanzisha biashara zinakufa.
Muda mwingine mahusiano yetu yanaptia kwenye changamoto. Hivi vitu VYOTE tunaweza kuvifananisha na kufa.
Sambamba na hayo yote ni kwamba, bado tunapaswa kufufuka bila kujali tunapitia changamoto ngapi. TUFUFUKE.
Kumbuka kwamba, kama tuko hai kwenye maisha yetu, lazima tutakutana na nyakati nyingi za KUFA, ILA BADO TUNAPASWA KUFUFUKA.
TUFUFUKE.
Imeandikwa nami rafiki yako
Godius Rweyongeza
-
Pale unapokuwa huoni matokeo
Ni rahisi kuacha kufanya pale unapokuwa huoni matokeo ya haraka. Ila ukweli ni kuwa kamwe usiache kufanya kwa sababu tu huoni matokeo ya haraka, badala yake endelea kukaza.
Kukomaa kwa muda mrefu kutakuweka kwenye hali ya kupata matokeo mazuri kuliko vile unavyofanya kwa muda mfupi na kuacha. Mfano, ukiwekeza mara moja na kuacha, au ukiweka akiba mara moja na kuacha, utashindwa kuona matokeo yanayotokana na mwendelezo na uvumilivu.
Mfano mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi. Unaweza kujichagua mwenyewe kwa kuhakikisha unakuwa na sera nzuri ambazo zitakuinua kiuchumi miaka mitano ijayo, kisha ukaamua kuwekeza kwa nguvu zote kwa miaka mitano ijayo bila ya kuacha, nakuhakikishia kuwa kama ukifuata sera zako bila kuacha kwa miaka mitano ijayo bila kuacha, utaweza kufanya makubwa sana.
2025 JICHAGUE MWENYEWE. Kuna ebook ya bure inayokuonesha namna na wapi ujichague mwenyewe mwaka 2025. Nitakuwekea hapa moja kesho, hakikisha unafungua makala hiihii kesho kwa ajili ya kujifunza zaidi
-
Nguvu ya Kuweka Malengo-1
Unapokuwa na malengo unapambana kwa vyovyote vile kuhakikisha unayafanikisha malengo Yako ndani ya muda husika.
Ila ukiwa huna malengochochote kinachotokea mbele yako ni lengo.

Hivyo basi jitahidi kuhakikisha kuwa na malengo, weka malengo yafanyie kazi.
kumbuka usipokuwa na malengo, chochote kitakachotokea mbele yako kitakuwa ni lengo.
-
NGUVU YAKO KUBWA IWEKE HAPA
Rafiki yangu, nguvu yako kubwa iweke kwenye kile unachofanya. Badala ya kuiweka nguvu kubwa kwenye vitu ambavyo hupendi.
Inawezekana kuna vitu hupendi kwenye siasa, kwenye michezo na mabo mengine. Ila ukwlei ni kuwa nguvu yako kubwa inapaswa kuwekwa kwenye vitu ambavyo unapenda.
Kama ni biashara, hapo ndipo unapaswa kuwekeza nguvu zako.
Kama ni kazi, iwekeze hapo.
Wewe ni zaidi ya hivyo vitu vinavyokusumbua na vinavyokupotezea muda wako.
Imeandikw name rafiki yako
Godius Rweyongeza