Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Hii ndiyo aina pekee ya malengo ambayo hayatafanikiwa ndani ya mwaka 2023

    Rafiki yangu, najua mwanzoni mwaka huu watu wengi wameweka malengo mengi ambayo watakuwa wakiyafanyia kazi.

    Ila leo hii nipo hapa kukwambia aina moja tu ya malengo ambayo watu wameweka na nina uhakika haya  malengo hayatimia. Malengo haya ni yale malengo ambayo watu wameweka na hawajaanza kuchukua hatua kuyafanyia kazi

    Sifa moja kubwa ya malengo ni kwamba ukishayaweka ni lazima uweze kuyafanyia kazi ili yaweze kuja kwenye uhalisia. Kama mwaka huu, umeweka malengo na bado hujachukua hatua kuhakikisha kwamba malengo yako hayo yanakuja kwenye uhalisia. Basi ujue kwamba malengo hayo hayatakaa yatimie, na hayo ndiyo malengo ambayo hayatafanikiwa kwa mwaka huu wa 2023.

    Rafiki yangu, hakikisha kwamba unaanza kuyafanyia kazi malengo yako ambayo umejiwekea kwa ajili ya mwaka huu wa 2023.

    Melngo makubwa+hatua kubwa=mafanikio

    Kila la kheri.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Viashiria vitano kuwa umeuanza mwaka mpya kwa kishindo

    Rafiki yangu, naomba nichukue nafasi hii kuhakikisha kwamba nakutakia kheri ya mwaka mpya 2023. Kheri ya mwaka mpya rafiki yangu.

    Mwaka huu naamini, utakuwa ni mwaka wako wa kipeke na mwaka wako wa kufanya makubwa. mwaka huu nina hakika ni mwaka ambao hautaremb  mwandiko. Na njia bora ya wewe kutoremba mwandiko ni kuhakikisha kwamba unaanza sasa hivi kufanyia kazi malengo yako bila ya kuchelewa. kwenye makala ya leo, ningepend akuingia kwa undani zaidi na kukueleza viashiria vitano vinavyoonesha kwamba kweli mwaka huu 2023 umeuanza kwa kishindo kikubwa kabisa.

    Kiashiria cha kwanza ni kuweka malengo.

    Kama tayari umeshaweka malengo. Basi hicho ni kiashiria cha kwanza kabisa kwamba mwaka huu umeuanza kwa kishindo kikubwa.

    Watu ambao huwa wanaweka malengo ni wachache sana. tafiti zinaonesha kwamba asilimia tatu tu ya watu ndio huwa wanakuwa na malengo. Yaani, malengo ambayo ni SMART. Unajua malengo SMART ni malengo gani.

    Neno SMART ni neno la kiingereza ambalo linasimama kwa ajili ya vitu vifuatavyo

    • S=Specific. Yaani, kwamba lengo lako ni lengo ambalo linaeleweka. Yaani, unapoweka lengo, wewe mwenyewe unapaswa kuelewa ni kitu gani unataka. Kinachowakwamisha watu wengi kikiwa kitu cha kwanza ni kuwa wenyewe huwa hawajui ni kitu gani ambacho wao wanataka.

    Lengo lako linapaswa kueleza kwa uhakika hasa ni kitu gani ambacho unataka, mpaka rangi ya hicho kitu.

    Lengo lako linapaswa kuwa linaeleweka kiasi kwamba akilisoma mtoto wa miaka sita, anapaswa kulielewa na kuweza kumweleza mtoto mwenzake wa miaka sita akaelewa.

    • M= Measurable. Lengo lako linapaswa kuwa linapimika. Ninaposema kwamba lengo linapimika nnamaanisha kwamba unaweza kupima na kuona kama unaelekea kwenye lengo lako au la!

    Mwishoni mwa mwaka jana, nilikuwa nikiwasiliana na rafiki zangu wengi, huku nikiwauliza ni nini malengo yao makubwa ndani ya mwaka 2023? Mmoja aliniambia kwamba lengo langu ni kufanya zaidi. Kufanya zaidi maana yake nini?

    Kufanya zaidi siyo lengo ambalo linapimika. Kama mwaka jana ulikuwa unakimbia mita 100. Mwaka huu ukikimbia mita 101 si utakuwa umefanya zaidi?

    Kama mwaka jana ulikuwa huweki akiba, mwaka huu ukianza kuweka shilingi mia moja si utakuwa umefanya zaidi. lengo lako linapaswa kuwa linapimika.

    Kwa mwaka huu wote ninaenda kuweka akiba ya shilingi laki mbili kila siku. Hilo ni lengo linapimika.

    Kwa mwaka huu wote ninanenda kuwa naandika makala yenye maneno 1500 kila siku. Hili ni lengo jingine ambalo linapimika.

    Kwa mwaka huu wote ninaenda kuwa naongea na wateja hamsini kila siku kwa simu. Hili ni lengo jingine ambalo linapimika.

    Siku ambayo unafikia lengo lako unajua. Na siku ambayo unakuwa hujafikia lengo unajua.

    Ila ukisema niteboresha biashara yangu. Sasa unaenda kuwa unaboresha nini kwenye biashara yako? Ukiongeza hata mfuko wa pipi mmoja si utasema umeboresha?

    Ila ukisema kwamba biashra yangu ina mtaji wa milioni 70. Mwaka huu, ninakuza mtaji wangu mpaka milioni 200 hapo sasa ndio unakuwa umeweka lengo linalopimika? Sijui unanielewa?

    • A= attainable. Moja ya kitu ambacho pengine hukijui ni kwamba watu wengi huwa wanaweka malengo makubwa sanasana kwa mwaka mmoja huku wakiweka malengo madogo ya miaka mingi ijayo. Mtu anataka akamilishe na kufanikisha kila kitu masiahani mwake ndani ya mwaka mmoja. Rafiki yangu, ninachotaka kukwambia ni kwamba, malengo yako ya mwaka mmoja yawe makubwa na ambayo yatakusukuma kufanya vitu zaidi ya vile ulivyokuwa umezoea.
    • R=Relevant., hapa maana yake malengo yako makubwa yanapaswa kuendana na ndoto zako kubwa za mbeleni au kazi au  biashara. Usiweke tu malengo ilimradi umeweka malengo
    • T= Lengo lako pia linapaswa kuwekewa ukomo wa muda. Yaani, lini unataka lengo liwe limekamika. Yaani, hakikisha umeweka lengo lako katika namna ambayo ineonesha lini ungependa kuwa umefikia lengo lako.

    Andika kufikia tarehe………..ninamiliki…….

    Kama umeuanza mwaka wako kwa kuhakikisha kwamba una malengo ambayo ni SMART, hicho ni kiashiria kuwa umeauanza mwaka wako kwa ushindi

    Kishiria cha pili kuw umeuanza mwka wako kwa ushindi ni kuwa umeshaanza kufanyia kazi malengo yako. Rafki yangu, ikumbukwe kwamba kuweka malengo ni kitu kimoja ila kufanyia kazi malengo ni kitu kingine kabisa. hivyo, basi kama unataka kujua kama kweli umeuanza mwaka wako kwa ushindi ni mpaka pale utapokuwa umeweza kuanza kufanyia kazi malengo yako.

    Kuweka malengo ni kitu kimoja, ila kufanyia kazi malengo ni kitu kingine.

    Na watu wengi huwa wanaweka malengo, ila wachache sana ndio huwa wanachukua hatua ya kuhakikisha kwamnba wamefanyia kazi malengo yao na kuyaleta kwenye uhalisia. Rafiki yangu, usiwe mtu ambaye anaweka malengo tu bila ya kuyafanyia kazi. weka malengo kisha anza kuyafanyia kazi.

    Kama ulikuwa hujaanza kufanyia kazi malengo yako anza leo hii. na siyo lazima ufanye kitu kikubwa sana ndani ya siku moja.

    Unaweza kuanza kidogokidogo kwa kuchukua hatua ndogondogo ambazo utaanza kufanyia kazi. ndio maana nakushauri sana uweze kusoma kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

    Hiki kitabu kitakufaa sana rafiki yangu

    Hiki ni kitabu ambacho kimesaidia wengi ndani ya mwaka 2022. Kitakusaidia na wewe kufanya makubwa ndani ya mwaka 2023.

    Pata nakala ya kitabu hiki leo hii.

    Gharama ya kitabu ni 20,000/-

    Kama upo nje ya mkoa wa Morogoro, utaongeza gharama ya usafiri ili kutumiwa kitabu.

    Kiashiria cha tatu kuwa umeuanza mwaka wako kwa ushindi ni  kama unafuatilia maisha yako zaidi ya unavyofuatilia maisha ya watu wengine.

    Kuna watu huwa wanapenda kufuatilia maisha ya watu wengine kuliko wanavyokuwa wanafuatilia maisha ya watu wengine. Unawakuta mtandao ni wakiwa wanafuatilia labda maisha ya msanii fulani au mtu fulani. Lakini wanachosahau ni kuwa wao wenyewe wana mambo mengi ya kufuatilia juu yao wenyewe. Hivyo, basi ili mwaka wako uweze kuwa wenye baraka n yingi na mafanikio makubwa unapaswa kuhakikisha kwamba unajifuatilia wewe mwenyewe kuliko ambaavyo unamfuatilia mtu mwingine.

    Jenga utaratibu wa kujifuajtilia wewe mwenyewe ndani ya huu mwaka kuliko ambavyo unamfuatilia mtu mwingine.

    Kila siku asubuhi weka orodha ya vitu ambavyo unaenda kufanya ndani ya siku husika.

    Kisha baadaye jioni, hakikisha kwamba unajifanyia tathmini kuona ni kwa namna gani umeweza kufanyia kazi orodha ya vitu ambavyo ulipanga asubuhi. Kwa kufanya hivyo, utaona wapi umeweza kufanya vizuri na wapi hukuweza kuafanya vizuri, lakini hilo litakupa picha na kukuonesha ni wapi ambapo unapaswa kubadili kwenye maisha yako ili kufanya maisha yako kuwa bora sana.

    Kiashiria cha nne kuwa umeuanza mwaka wako kwa kishindo ni kujikukumbusha malengo yako kwa kuyasoma walau mara mbili kila siku.

    Unapoweka malengo, unapaswa kujenga utaratibu wa kuyarudia kuyasoma pia kila mara.

    Unafanya hivyo kwa lengo la kuifanya akili yako, ijenge ione kwamba inaweza kufikia lengo lako na linawezekana vizuri sana bila ya shida yoyote ile.

    Kiashiria cha tano ni kuwa tayari umeshaanza kujifunza kitu kuhusiana na lengo lako. Rafiki yangu, kama kuna kitu muhimu sana ambacho haupaswi kusahau ni kwamba usisahau kujifunza na kujiendeleza zaidi kuhusuaiana na lengo lako.

    Kwa mfano, una lengo la kuwekeza kwenye hisa mwaka huu. unapaswa kuanza mara moja kujieleimisha kuhusiana na elimu ya hisa. Na kwa kuanzia unaweza kupata kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE ambacho kitakusaidia sana kwenye hili.

    Au pengine una lengo la kuanzisha kilimo cha samaki. Hapa unahitaji pia kuhakikisha kwamba unaaanzakujiendeleza kielimu kuhusiana na elimu ya kilimo na ufugani wa samaki.

    Haya ni mambo machache sana ambayo unapaswa kuhakikisha kwamba unayafanyia kazi na kuyuaeta kwenye uhalisia.

    Kujifunza ni jambo ambalo haliepukiki hasa kama umeweka malengo makubwa na unataka kufakika mbali ndani ya mwaka 2023. Rafiki yangu, malengo makubwa yanahitaji ujifunze na ufanyie kazi kile unachojifunza.

    Kiashiria cha ziada, umebadilli tabia zako. Yaani, kuna tabia ambazo najua unazo. Na tabia hizo haziwezi kukusaidia wewe kufanikisha malengo yako. Rafiki yangu, kama unataka kuhakikisha kwamba umeweza kufanikisha malengo yako ndani ya mwaka 2023, basi hakikisha kwamba unabadili tabia zako. niambie tabia zako, nami nitakwambia kama utawza kufanikisha malengo yako au la!

    Una lengo la kupunguza uzito, ila bado hujaacha tabia yako ya kula hovvyohovyo? Una lengo la kuweka akiba ila bado unahonga? Una lengo la kuongeza kisomo ila bado unazembea kusoma.

    Una lengo la kuanzisha biashara ila hata hujifunzi kuhusiana na biashara?

    Rafiki yangu,  hizi tabia unapaswa kuhakikisha kwamba unaziiishi ndani ya mwaka 2023 ili kupiga hatua. Na kama unavyoona. Wengi walitamanani kusikia nikiwambia kwamba kama ulikseha usiku kuusubiri mwaka mpya, basi umeuanza mwaka wako kwa ushindi.

    Au wengine walitaka niwaambie kwamba kama umeuanza mwaka wako kwa kuchati sana hapo umeuanza kwa ushindi. Kiufupi utakuwa umeuanza mwaka wako kwa ushindi kama umefanyia hivyo vitu vitano ambavyo nimekwambia kwenye makala ya leo.

    Bila kuongeza la ziada, mimi naishia hapo

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Nimepata kusoma kitabu cha THE YOUNG INVESTOR (Projects and activities for making your money grow)

    Hiki ni kutabu cha uwekezaji ambacho kimeandaliwa maalumu kwa ajili ya watoto, kinalenga kuwafundisha watoto juu ya uwekezaji na namna gani wanaweza kuanza kufanya uwekezaji.

    Hata hivyo mtu mzima kama wewe unaweza (na unapaswa) kukisoma kitabu hiki pia. Na kwa kuwa lugha iliyotumika kwenye hiki kitabu ni lugha rahisi kwa ajili ya kuwafanya watoto waelewe, wewe mtu mzima ukisoma kitabu hiki, utakielewa zaidi.

    Kitabu ni kidogo tu, kina kurasa kama 124 hivi, hivyo unaweza kukisoma ndani ya wiki moja kikaisha. Binafsi nimekisoma na kukielewa.

    Kuhusu mwandishi wa kitabu hiki
    Mwandishi wa kitabu hiki ni Katherine R. Bateman. Mwandishi ameandika kitabu hiki kwa ajili ya wajukuu wake. Anasema kwamba alikuwa na shauku kubwa ya kuwafundisha wajukuu wake kuhusu uwekezaji.

    Hivyo alianza kukusanya taarifa kwa ajili ya wajukuu wake, kila alipokuwa   anaongea na watu juu ya hilo, jibu alilopata kutoka kwa watu lililuwa kwamba akishaandika kitabu awataarifu wanunue nakala pia.

    Hili jambo lilimfanya mwandishi ahakikishe anaandika kitabu kinakamilika.

    Sasa hapa ningependa kukwambia yafuatayo ambayo nimejifunza kutoka kwenye kitabu.

    1. Kitu cha kwanza ambacho ningependa na wewe uondoke nacho ni kuwa na wewe utapaswa kuandika kitabu. Siyo lazima kiwe cha fedha kama hiki, lakini unaweza kuandika kitabu kinachoendana na ujuzi wako. Nakuhakikishia wanao na wajukuu wako watakipenda kitabu hicho. Kama wewe umekuwa mwanakwaya kwa miaka sasa, ebu hata tuandikie kuhusu safari yako ya kuimba, najua una mengi ya kuandika. Kama bado unakwama uandike nini, hakikisha unapata kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU (kwa saaa softcopy ni 5,000/).

    2. Hisa siyo makaratasi tu, na wala siyo cheti unachopata baada ya kununua hisa. Bali ni umililiki wa kampuni.

    3. Unapaswa kutawanya uwekezaji wako kwenye maeneo tofautitofauti. Kwenye hisa, hatifungani pamoja na vipande.

    4. Kama kuna kampuni unapenda kutumia bidhaa zake, hakikisha unanunua hisa zake pia.

    Kitabu kina mambo mengi, binafsi nimeandika machache tu kwa sababu nilitaka niweke kumbukumbu kuwa niliwahi kusoma kitabu hiki. Na njia ya mimi kuweka kumbukumbu ni kuandika makala kama hii hata kama ni fupi

    Ili unufaike na kitabu hilo, hakikisha unakisoma mwenyewe.
    Kipakue mwenyewe kwa kufuata mwongozo huu hapa

    Karibu sana

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

    Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA

  • Njia Mpya Ya Kupakua Vitabu Mtandaoni

    Kwa wale wanaopata shida kupakua vitabu Mtandaoni. leo nimekuja na suluhisho. hakikisha unaagalia video hii Mpaka mwisho. BONYEZA HAPA KUIANGALIA

    Hii video Ni muhimu Sana, hakikisha unaiangalia

    kila la kheri.

  • Nani anapaswa kusoma vitabu na kwa nini

    Kuna MTU kaniuliza swali hili, Nani anapaswa kusoma vitabu na kwa nini

    Jana kwa upande wangu imekuwa Ni moja ya siku moja bize Sana. niliamka saa nane usiku, nililala saa sita usiku. Na hapa nipo ikiwa Ni saa kumi alfajiri nimeahaamka.

    Ninaamka mapema hivi kila siku, ikiwa Ni lengo la mimi kupata muda wa ziada wa kujifunza na kusoma vitabu.
    Ikumbukwe sisomi kwa ajili ya mitihani, wala sisomi ili kupata cheti chochote.

    Labda kujibu swali lako vizuri zaidi nipende tu kusema kwamba MTU yeyote ambaye anajua kusoma na kuandika anapaswa Kuwa msomaji wa vitabu.
    Bila kujali wewe unafanya kazi ya kupiga debe
    Ni machinga
    Ni mfanya usafi  kwenye kampuni au mkurugenzi

    Unapaswa kujijengea utaratibu wa kusoma vitabu. Vitabu vitakujenga na vitabu vitakuwa na uwezo wa kukutoa hapo ulipo Mpaka uweze kufika unapotaka.

    Pata ebook Hii bure ili ujifunze umuhimu wa kusoma vitabu. Jaza taarifa zako hapa chini

    Kuna sababu nyingi kwa nini unapaswa kusoma vitabu, lakini sababu kuu ni kwamba unapaswa kusoma vitabu kwa sababu vitakufumbua macho na kukuonesha yale ambayo huwezi kuyaona kama ingekuwa husomi vitabu.

  • Ushauri Huu Haufanyi Kazi Kwenye Uwekezaji

    Mara kwa mara utasikia watu wanakwambia Kuwa unapaswa kuanza kwanza, mambo mengine utayajua wakati unaendelea na safari.

    Hicho kitu kinafanya kazi vizuri sana na nimekuwa nikikitumia kwa siku nyingi . Ila Sasa siku ya leo ningependa nikuongezee ushauri muhimu hasa kwa upande wa uwekezaji.

    Kwenye uwekezaji Ni muhimu kwako kufanya utafiti wa kina Kabla hujaamua Kuwa utawekeza kwanza na mengine utajua mbele ya safari.

    Utafiti Ni muhimu Sana kwenye suala zima la uwekezaji. Ni muhimu ufanye utafiti na kuhakikisha Kuwa umejiridhisha na uwekezaji unaoufanya.

    Kila la kheri.

  • App Itakayokusaidia Kutuma SMS baadaye, kupiga simu kwa wakati na kudai hela zako😂😂

    Katika makala ya leo tunaenda kuona namna ya kuandaa ujumbe leo na ukautuma siku ya krismasi au mwaka mpya. HutahItajika kuuandika tena au kuutuma tena
    Tutaona namna ya kupanga kumpigia siku za mbeleni na ukampigia kwa uhakika bila kukosa hata dakika 1
    Tutaona namna ya kupangilia watu wa kuwasiliana nao.
    Tutaona njia nzuri ya kukukumbusha kufanyia kazi majukumu yako na kuyafanikisha na mengine mengi.

    Kwa wale waliojiunga na emali list yangu watakumbuka kuwa huwa nawatumia ujumbe wa kuwapokea ambao huwa
    Unawaahidi kuendelelea kuwashirikisha vitu mbalimbali vya kuwasaidia kupitia makala na mafunzo ambayo ninatoa kwa njia ya baruapepe. Na hiki ni kitu ambacho nimekuwa nikikifanyia kazi. Kama wewe hujajiunga na email list yangu, hakikisha unafanya hivyo kwa KUBONYEZA HAPA 👇🏿 na kujaza taarifa zako kamili.



    Hiki kitu huwa nakifanyia kazi mara kwa mara na leo napenda kukuletea app ambayo inaweza kukusaidia SMS siku za mbeleni.

    Mfano tuseme,  nataka nikuandalie ujumbe mzuri wa kheri ya krismasi.

    Ila Sasa nataka niuandae ujumbe huu uje kwako siku ya krismasi Ila nataka niuandae Leo hii tarehe 18.12.2022. na ninataka ujumbe huu uje kwako tarehe 25.12.2022 saa moja asubuhi.
    Kwa kutumia app hii inawezekana.

    Au tuseme kwamba tumeongea leo tarehe 17 na umeniambia nikupigie tarehe 31 Disemba saa kumi na mbili na nusu jioni kabla hujaenda kwenye mkesha wa mwaka mpya.
    Halafu nikaongea na mwingine akaniambia nimpigie tarehe 23 asubuhi saa mbili. Nikawa na orodha ya watu ishirini na kila mtu Anataka mimpgie kwa muda wake, saa yake na tarehe yake. Utakumbukaje?

    Utaandika kwenye diary si ndio?  Kuandika Kwenye diary ndio suluhisho la Watu wengi Ila tatizo muda mwingine unaweza kusahau, na linapokuja suala la muda Kuna watu wengi ambao utajikuta huwapigii kwa wakati.

    Siku ya leo nina app ambayo nimekuwa naitumia na imekuwa inanisaidia kutuma SMS muda, saa na dakika ninapotaka.
    Imekuwa pia inanikumbusha kuwapigia watu muda, saa na dakika tulipokubaliana.

    Tuseme nataka nikutumie wewe ujumbe Leo saa kumi jioni. Lakini muda huu ninapoandika makala hii ni saa kumi na moja asubuhi. Hapa ninachofanya naandika ujumbe wako kama ifutavyo hapa chini

    Habari yako  [JINA LAKO], nakukumbusha kuwa leo jioni saa mbili tutakuwa na kikao cha Cha pamoja kwa njia ya mtandao wa zoom. Nakutakia maandaalizi mema kwa ajili ya kikao, tafadhali hakilisha unawahi.

    Halafu usisahau kutuma Ile laki tatu ya kozi tetu inayoendelea. Malipo yote yafanyike kwa namba ya simu 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Enewei, huu ujumbe ninaweza kuuandaa Sasa na ukaja kwako baadaye leo jioni.  Au siku yoyote ya tukio.

    Ninaweza kuandaa ujumbe huu na kuupanga uje kwako kwa kutumia APP inayoitwa DO IT LATER. Lakini Kuna mengine zaidi ya haya ambayo ningependa ujue kutoka kwenye hii APP.

    Vifuatavyo Ni vitu Tisa ambavyo app inaweza kukusaidia kufanya

    1. KUKUKUMBUSHA KUPIGA SIMU
      Mfano, tumeongea Sasa hivi na umeaniambia nikupigie tarehe 2.2

    Tukimaliza kuongea tu kwenye simu yakokitajitokeza kitu Kama hiki.

    App inavyoonekana baada ya kuwa umempigia mteja. Unaweza kuamua kumtumia ujumbe au kuweka reminder kwamba ikukunbushe lini utampigia tena

    Hapo nitachagua sehemu ya Call na Kisha nitapanga lini ningependa kuongea na wewe. Ambapo kwa upande wako Ni tarehe 2.2.2023

    Hiyo tarehe ikifika , muda na saa tukivyokubaliana. App itanikumbusha nikupigie.

    Wakati naendelea kuandika makala hii, app ilinikunbusha nimpigie Godius Rweyongeza. Hahah
    kama aPp imekukumbusha umpigie mu, lakini unaona umebanwa huwezi kumpigia kwa wakati huo. Unaweza kubonyeza SNOOZE kisha ukachagua lini utampigia

    2. KUTUMA SMS BAADAYE
    Nadhani tangu mwanzo nimeliongelea hili. App hii inaweza kunisaidia kuandaa ujumbe wa kuja kwako tarehe, muda, saa na dakika ninayotaka au tulivyokubaliana.

    3. KUTUMA SMS kwa mtu kwa kwa kurudia.
    Tuseme kwa mfano, birthday yako ni tarehe 1.1. kila mwaka.
    Halafu Mimi nataka kila tarehe 1 Januari niwe nakutumia ujumbe wa kukutakia kheri ya siku ya kuzaliwa. Lakini nahisi naweza kusahau, au sitaki niwe naurudia kuandika ujumbe huohuo kila mwaka. Naweza kuandaa ujumbe leo ambao utakuja kwako tarehe 1 Januari na utakuwa unakuja kwako kila mwaka tarehe moja Januari.

    Ujumbe unaojirudia kila wiki. Sihitajiki kurudia kuandika ujumbe huu kila wiki. Ikifika jumapili, wenyewe unaenda hewani.

    Kama umekuwa unapata changamoto ya ndugu kukwambia kwamba

    Ooh unajua huwa hautupigiagi.
    Ooh hata hutusalimii, siku hizi unalinga. Ngoja nikwambie kitu, kuanzia leo hawapaswi kukwambia huwasalimii.

    Wachukue hao ndugu zako wote. Waweke kwenye grup maalumu, Kisha waandalie ujumbe wa kuwatakia wikendi njema na panga ujumbe huo uwe unaenda kwao kila jumamosi saa nne asubuhi. Umemaliza. Ujumbe huo utakuwa unaenda kwao kila jumamosi asubuhi maisha yako yote, mpaka siku utakapoamua kubadilisha hilo.

    App inanikumbusha nimpigie kila alhamisi ya mwisho wa mwezi

    Ni hivyo tu.

    5. KUANDAA SMS NYINGI ZA KWENDA KWA MTU ILA ZIKAENDA KWA NYAKATI TOFAUTI
    Unaweza kuandaa sms nyingi za kwenda mtu na ZIKAENDA kwa NYAKATI tofauti.

    Mfano  unaweza kuandaa sms ya kwanza ya kwenda kwa MTU yenye ujumbe huu.

    Habari, tunakushuru Sana kwa kununua simu mpya aina ya…. Siku ya leo.
    Tumefurahi Sana kukuhudumia siku ya leo na tunakutakia kila kheri. Je, kuna Jambo lolote ungependa kuongea kuhusiana na huduma yetu? Kama unalo tafadhali usisite kutuambia, ahadi yetu Ni kwamba maoni utakayotoa tutayafanyia kazi.

    Asante Sana na karibu kwa maoni.

    Siku ya pili ukaandaa ujumbe wa kwenda kwa mtu huyuhuyu unaosema hivi

    Habari ya tangu jana, Sina shaka umeshaanza kutumia simu yako uliyonunua kwetu sisi….. Unaoionaje?

    Unaweza kuandaa jumbe nyingi na za kutosha kwenda kwa mtu yuleyule au kikundi cha watu. Mtu/watu unaweza hata kuwaandalia jumbe za mwaka mzima au hata miezi mitatu au minne ijayo.

    Kwa kutumia app hii hutasahau birthday za wateja wako au watu wako wa karibu maisha yako yote.  Wewe unaweza kusahau Ila app haitasahau, itakuwa inawatumia jumbe na wataona unawajali kweli.

    5. UNAWEZA KUITUMIA APP KAMA ALARM
    Hapa app itakukumbusha majukumu yako ya muhimu ya kufanya

    6. APP INAWEZA KUTUMA SMS KWENYE WHATSAP
    Mimi nimeijaribu kwa upande wa WhatsApp. App haifanyi kazi vizuri hasa pale unapokuwa unataka kutuma jumbe kwa watu wengi, Ila kitu kimoja Cha uhakika Ni kwamba kama umeandaa ujumbe wa kwenda kwa mtu mmoja, utaenda. Ni uhakika utaenda.

    Ila pia unapaswa kuwa mtandaoni.

    7. APP INAWEZA KUKUONESHA WATU AMBAO IMEAHAWATUMIA UJUMBE NA AMBAO IMEAHINDWA KUWATUMIA
    Kama kuna watu IMESHINDWA KUWATUMIA ujumbe, labda kutokana na kuwa simu yako ilikuwa imezima. App itakuonesha watu wa Aina hiyo. Na utaweza kuwarudia.

    Ila pia app itakuonesha watu ambao wamekamilishwa kwa kutumiwa jumbe au kupigiwa.

    App ikionesha missed call baada ya mtubkunipigia na kunikosa.

    8. APP ITAKUSAIDIA KUWAKUMBUSHA WANAOKUDAI WAKUTUMIE HELA YAKO😂😂
    Natania tu japo ni ukweli.

    9. APP INA UWEZO WA KUTAJA JINA LA MTU NA KUFANYA MENGINE MENGI.

    Kama unatuma ujumbe kwa wengi na ungependa kila mtu atajwe jina lake. App ina huo uwezo.

    Na mengine mengi sana…

    Ukitumia hii code wakati unatumia app. Itataja jina la mhusika kwenye ujumbe mfupi hata kama hukuandika jina hilo

    Cha kufanya sasa. Ningependa nikushike mkono kwa kukupa maelezo ya kina juu ya namna ya kuitumia app hii. Sitaki upate shida hata kidogo. Nipo hapa kukusaidia.

    NB: utapaswa kulipia 50,000/- ambapo utaelekezwa na kufunzwa kila kitu kuhusiana na app hii. Wewe mwenyewe utaipenda. Gharama utakayolipa kufundishwa ni ndogo kulinganisha na mengi utakayopata.

    Karibu sana

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

    Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA

  • STRIVE MASIYIWA

    STRIVE MASIYIWA

    Strive Masiyiwa ni bilionea wa Zimbambwe ambaye alizaliwa mwaka 1961 huko nchini Zimbambwe. Alikulia nchini Zimvambwe na baadaye alienda kusoma masomo ya chuo kikuu nchini Uingereza akisomea uhandisi. Baada ya masomo Strive Masiyiwa kama walivyokuwa watu wengine wazalendo wa kipindi kile alirudi nchini mwake kwa ajili na kuanza kufanya kazi na shirika la mawasiliano, akiajiriwa Kama mhandisi

    Masiyiwa anasema kwamba, kila mara  alipokuwa akitoka kazini alikuwacna mazoea ya kukutana na marafiki zake baa ili wapate moja baridi, moja moto.

    Siku moja katika maongezi na rafiki zake alipendekeza kuwa watenge kiasi kidogo Cha fedha, yaani na wawe wanaweka kiasi hicho kama akiba kwenye akaunti Yao ya benki. Alipendekeza wazo hili kwa watu 10 Ila waliochukua hatua na kuweka akiba walikuwa wawili tu.

    Mpaka hapo tunajifunza kuwa unaweza kuwa na marafiki wengi, Ila kumbe hao marafiki siyo wale wa kushirikiana na wewe katika upambanaji Bali wanakuwa marafiki wa bata tu! Ukiwa na mmarafiki wa Aina hii, mafanikio kwako yanakuwa magumu kwa sababu hawafikirii nje ya boksi, na hata pale wanapokuwa na wazo hawachukui hatua.

    Sisi kama mabilionea mafunzoni tuna mengi ya kujifunza kutoka kwake. Kuanzia namna unavyoweza kuanzia chini kabisa, ambapo Masiyiwa anasema kwamba kwake hakuna kilichobadilika, unaanza na kile ulichonacho, unafanya kinachowezekana ili mwisho wa siku uweze kufanya yasiyowezekana.

    kuja kwenye kukuza mtaji, kuja kwenye kujenga timu.
    Kuja kwenye kwenye kupambania ndoto, kusaidia watu na kutoa na vitu vingine.

    Asilimia kubwa ya vitu ambavyo tunafanya Sasa hivi Masiyiwa alivipitia miaka mingi iliyopita.

    Kadiri ya Forbes Masiyiwa Ni bilionea namba 1012
    Utajiri wake ni Dola bilioni 3
    Utajiri wake mkubwa unatoka kwenye mitandao ya simu

    Ambapo anamiliki zaidi ya 50% ya kampuni ya Econet Wireless

  • Makosa ambayo watu hufanya wanapotaka KUONGEZA chanzo kingine Cha kipato

    Utakuwa umegundua kuwa wiki hii nimekuwa nikikushirikiaha nakala zinazoeleza ni kwa namna gani unaweza KUONGEZA chanzo kipato Cha ziada.

    Sasa Leo napenda kukwambia kuwa bado sijamaliza nilichokusudia kukwambia. Kwenye hii makala ya leo ningependa ujue makosa ambayo watu hufanya wanapotaka KUONGEZA chanzo kingine Cha kipato. Makosa yenyewe ni

    Kosa la kwanza wanaanzisha chanzo kwenye eneo ambalo wenyewe hawajui.
    Kisa mtu kasikia kitu fulani kinalipa au kisa kaona mtu akifanya biashara fulani na ana MAFANIKIO, Basi utakuta kwamba na yeye anakimbilia kutaka kuwekeza huko au kuanzisha biashara ya aina hiyohiyo huku akiwa haijui Kwa undani. Ninachotaka kukwambia siku ya Leo ni kuwa unapaswa kuanzisha chanzo cha kipato kwenye eneo ambalo wewe mwenyewe tayari unalijua. Ninaposema unalijua simaanishi kwamba uwe umeshahawahi kulifanyia kazi, Bali uwe umelifanyia utafiti wa kina.
    Siyo kisa umesikia eti kuna crypotocurency na wewe unakimbilia huko.
    Au kisa eti unasikia mavi ya tembo ni dili na wewe unakimbilia kutafuta mavi ya tembo.

    Kuwa makini!

    Kosa la pili ni kutojua chanzo husika kitakuwa kinaingiza kipato kwa muda gani.
    Kila chanzo cha kipato huwa kinaingiza kipato kwa nyakati tofauti. Ni muhimu kwako kujua chanzo cha kipato kitakuwa kinaingiza fedha baada ya muda gani.

    Hatifungani huwa zinaingiza kipato kila baada ya miezi sita
    Kuna kampuni hisa zake huwa zinatoa gawio kila baada ya miezi sita na nyingine kila mwaka. Hayo yote unapaswa kuyajua.
    Uwekezaji kwenye miti huwa unatoa kipato baada ya muda mrefu. Kumbe basi ni jukumu lako kujua vizuri aina ya chanzo cha kipato na kitakuwa kinagiza kipato baada ya muda gani.

    Unahitaji kuwa na mchanganyiko. Vyanzo vinayoingiza kipato kila siku au kila wiki na vyanzo vinavyoingiza kila mwezi, baada ya miezi kadhaa na vile vya muda mrefu.

    Kama ndio unaanza wekeza zaidi kwenye vyanzo vinavyotoa kipato kila siku au kila wiki au kila baada ya siku chache.

    Kosa la tatu ni kubeti. Kuna wengi wanaofikiri kuwa kubeti ni chanzo, cha kipato. Vijana wengi wamenasa kwenye huu mtego. Hawafanyi kazi wala kujituma wakitegemea kubahatisha.

    Rafiki yangu, maisha hayabahatishwi. Yana kanuni zake, zipo wazi kabisa.
    Ukizifuata utafika mbali kabisa.

    Ndiyo maana tunaziongelea kwenye hii blogu kila mara.

    Kosa la nne ni kuanzisha chanzo Cha kipato kinachohitaji usimamizi mkubwa wenyewe wakiwa hawapo.

    Kuna vyanzo ambavyo vinahitaji usimamizi mkubwa mwanzoni. Kosa ambalo watu hufanya ni kuanzisha vyanzo vinavyohitaji usimamizi mkubwa mwanzoni huku wao wakiwa wapo mbali.

    Mfano mtu anaanzisha chanzo chake cha ziada kwenye kilimo biashara huku yeye akiwa mbali. Kilimo kina mambo mengi ambayo nyuma ya pazia yanahitaji kufanyiwa kazi, kumbe basi kitu kama hiki unahitaji ukianzishe ukiwa karibu ili kufanya usimamizi wa karibu.

  • Siri Hii Wanayoijua Matajiri Unapaswa Kuijua Pia

    Tujifunze kwa bahari

    Kila mwaka huwa kuna mito na vijito ambavyo huwa huwa vina maji na baadaye hukauka. Wakati mito hivi na vijito, vikikauka, bahari huwa haikauki hata siku moja.

    Unajua kwa nini bahari huwa haikauki, moja ya kitu ambacho huwa kinafanya bahari isikauke ni kwa sababu huwa inapokea maji kutoka kwenye vyanzo vingi. Kadiri ambavyo vyanzo hivi huwa vinaleta maji kwenye bahari ndivyo bahari huwa inazidi kuwa na uhakika wa kutokauka hata siku moja.

    Hiki kitu kikufundishe na wewe kuwa, kadiri ambavyo utakuwa na vyanzo vingi vya kipato, ndivyo ambavyo utakuwa na uchumi imara na usioyumba kuliko pale unapokuwa unategemea chanzo kimoja cha kipato.

    Sifa kuu ya matajiri
    Sifa kuu ambayo matajiri wanayo Ni sifa ya kuwa na vyanzo zaidi ya kimoja. Richard Branson ambaye ni mmoja wa matajiri wakubwa hapa duniani, anasemekana kuwa na vyanzo 42 vinavyomwingizia kipato. Na hapa ninaposema vyanzo 42 vinavyomwingizia kipato, simaanishi kipato tu cha kawaida, Bali kipato haswa kilichoshiba.

    Kila mtu kuna sehemu anaanzia
    Rafiki yangu na wewe Kuna sehemu unaanzia kwenye maisha, lakini usikubali kibaki hapohapo ukiwa na chanzo hichohicho. Una unwezo wa kukuza kipato chako zaidi ya hapo. Ongeza Vyanzo vya kipato walau uwe navyo zaidi ya kimoja

    SOMA ZAIDI

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

    Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA

X