Notice: Function WP_Interactivity_API::_process_directives was called incorrectly. Interactivity directives failed to process in "" due to a missing "DIV" end tag. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.6.0.) in /home/songambele/public_html/wp-includes/functions.php on line 6085
Home - SONGA MBELE

Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Hivi unajua Nini kuhusu uwekezaji wa hisa, hatifungani na VIPANDE?

    Katika kuongea kwangu na rafiki zangu. Nimekuja kugundua kitu Kimoja kutoka kwa Watu kadha wa kadha ambao nimeongea nao.

    Hawana ufahamu kamili kuhusu uwekezaji wa hisa au hawajui kabisa.

    Hiki kitu Godius, Kimenikusuma niandae kitabu kinachohusu uwekezaji wa hisa, hatifungani na vipande kwa ajili yako.

    Ni kitabu ambacho hupaswi kukikosa rafiki yangu. Ndani yake unaenda kujifunza vitu vigumu kwa lugha rahisi.
    1. Utapata kujua hisa ni Nini?
    2. Kwa nini unahitaji KUWEKEZA KWENYE HISA
    3. Vigezo vya KUZINGATIA KABLA YA HUJAWEKEZA FEDHA YAKO
    4. SOKO LA HISA TANZANIA NA JINSI LINAVYOFANYA KAZI.
    5. NAMNA YA KUSOMA RIPOTI ZA DSE
    6. MFUKO WA PAMOJA WA UWEKEZAJI
    7. MIFUKO YOTE YA UTT IKIWA IMEELEZWA KWA KINA NA KWA LUGHA RAHISI
    8. NJIA RAHISI YA KUTUMIA KIKOKOTOZI CHA UTT AMIS
    9. HATIFUNGANI NI NINI?

    Na Mambo mengine mengi….

    Kitabu kitajibu maswali yako na dukuduku zako zote kuhusu uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.

    Sasa umefika wakati wa wewe kuchukua hatua ili kuhakikisha kwamba unapata kitabu hiki cha kipekee. Huu ni uamuzi bora ambao utafanya ndani ya huu mwaka na utakuwa na manufaa makubwa kwako. Sasa chukua hatua upate kitabu hiki kwa 20,000/- tu.

    Utatumiwa kitabu hiki popote pale utakapokuwa. Kama utakuwa mbali kidogo, utaongeza gharama za kusafirisha kitabu ambazo ni 5,000/-

    Kwa hiyo jumla utalipia 25,000/-

    Chukua uamuzi Sasa hivi. Lipia kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Kumbuka kuwa endapo hutalipia Leo hii. Mwaka mmoja au miaka mitano ijayo, bado utakuwa unaendelea kushangaa shangaa tu, ukiwa hujui chochote kuhusu hisa. Sasa kwa nini usichukue uamuzi ili upate hiki kitabu?

    Haya lipia Sasa Sasa kwa 0755848381 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Karibu sana.

  • Zifuatazo ni mada 15 utakazojifunza kwenye semina ya Kufungua mwaka 2023!

    Wahenga wanasema hayawi hayawi, Sasa yamekuwa. Rafiki yangu wa ukweli, kwa siku sasa nimekuwa nikikwambia juu ya habari Semina ya Kufungua mwaka 2023. Najua umekuwa unajiuliza hivi hii semina itafanyika kweli? Jibu langu Ni kwamba lazima semina ifanyike bila kukwama. Maana mwaka 2023 haturembi mwandiko

    Semina hii itaanza tarehe 15.1.2023 na itadumu mpaka mwezi wa Pili mwanzoni. Gharama ya hii semina Ni 15,000/-. Gharama ya Semina inalipwa kwa namba 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Lengo la hii semina Ni kwamba ujifunze njia za uhakika zitakazokuwezesha wewe ulipwe walau mara mbili zaidi mwaka 2023! Na zifuatazo ni mada utakazojifunza

    Tarehe 14 Utangulizi wa Semina Mambo Muhimu ya Kuzingatia.
    Mada: Nini maana ya THAMANI BINAFSI NA JINSI YA KUJUA THAMANI YAKO!

    Tarehe 15: JINSI YA KUWEKA MALENGO, KUYAFANYIA KAZI NA KUYATIMIZA 2023: JINSI MALENGO YANAVYOWEZA KUONGEZA THAMANI YAKO

    Tarehe 16: JINSI UNAVYOWEZA KUWA NA KITU AMBACHO HAKUNA MTU ANAWEZA KUKIFANYA. NA KWA NINI NI MUHIMU KWENYE ULIMWENGU WA LEO WA KOMPYUTA, INTANETI NA ROBOTI

    Tarehe 17: AINA TATU ZA UJUZI UNAOUHITAJI ILI KUONGEZA THAMANI YAKO 2023 ILI KULA MEMA YA NCHI!

    Tarehe 18: KWA NINI UNAHITAJI KUACHA MAZOEA NA KUFANYA KAZI ZAIDI YA UNAVYOLIPWA. NA MATOKEO GANI UNAPASWA KUTEGEMEA

    Tarehe 19: NGUVU YA KUFANYA MAZOEZI + NGUVU YA SAA ELFU KUMI

    Tarehe 20: JINSI UBUNIFU UNAVYOWEZA KUKUONGEZEA THAMANI YAKO BINAFSI NA KUKUINUA KWENYE BIASHARA.

    Tarehe 21: JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA WAKO MWENYEWE (Njia 10 zilizothubitishwa)

    Tarehe 22: MWAKA 2023 USISHINDANE KWA BEI LABDA KAMA WEWE NI ROCKEFELLER! MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI KUJITOFAUTISHA

    Tarehe 23: UNAHITAJI KUWAHUDUMIA WATU WENGI ZAIDI: JINSI YA KUFANYA HIVYO 2023……

    Tarehe 24: JINSI YA KUSIMAMIA UKICHOPANGA NA UNACHOSEMA 2023

    Tarehe 25: VITU VITAKAVYOKUFANYA UHESHIMIKE 2023

    Tarehe 26: HUHITAJI KUWA NA PLAN B 2023 (SABABU 15 ZILIZOTHUBITISHWA)

    Tarehe 27: KUWA ORIGINAL 2023

    Tarehe 28: MUDA, MALI YENYE THAMANI: JINSI KUTUNZA MUDA WAKO 2023

    Tarehe 29: UNAHITAJI KUWA NA VYANZO VINGI VYA KIPATO

    Tarehe 30: JINSI YA KUONGEZA KUJIAMINI KWAKO na MATOKEO YAKE KWENYE KUONGEZA THAMANI YAKO BINAFSI

    Huo ndio mkeka wetu wa mwaka 2023! Haturembi mwandiko! Njoo ujifunze JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO mwaka 2023! Nakuhakikishia utakayojifunza ukiyafanyia kazi, yataongeza kipato chako mwaka 2023 walau mara mbili. Na hiki Ni kiwango Cha chini. Watu watakaohudhuria hii semina Nina hakika wataupiga mwingi Sana.

    Lakini siishii hapo. Baada ya semina, nitakupa audio, yenye mafunzo yoote ili uweze kuisikiliza kwa mwaka mzima utakaofuata.

    Mwaka 2023! Haturembi mwandiko!
    Kama na wewe hutaki kuremba mwandiko, basi njoo ujiunge na hii semina. Lipia 15,000/- yako Sasa kwa namba ya simu 0755748391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Karibu sana

    Mwaka 2023! Haturembi mwandiko!

  • Sababu yako ni ipi

    Kila kitu huwa kinafanyika kwa sababu…

    Kuna mtu unayeweza kuwa unawona anafanya jambo fulani, ukafikri labda yeye ana kipaji na uwezo mkubwa kukliko wewe, ila baadaye ukija kufuatilia ukagundua kwamba suala kubwa siyo kwamba ana uwezo  mkubwa kulliko wewe. Siyo kwamba ana konekisheni nyingi kuliko wewe, siyo kwamba amebarikiwa kuliko wewe, labda tu ni kwamba ana SABABU KUBWA KULIKO WEWE. Yaani, ile kwa nini yake ni kuwa

    Sababu ndizo huwa zinatusukuma sisi kufanya jambo fulani au kutofahanya jambo fulani. Sababu ndizo huwa zinatusukuma sisi kujituma kwenye kufanyia kazi jambo fulani au kutofanya na kuacha jambo fulani.

    Ukiwa na sababu kubwa ndiyo inakusukuma wewe kuamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kwenda kufanyia kazi malengo na ndoto zako, huku wengine wakiwa wamelala. Sababu haihitaji visingizio. Sababu haihitaji urudi nyuma, sababu haihitaji urembe mwandiko.

    Sababu inahitaji kitu kimoja tu uzalishe matokeo.

    Wewe sababu kubwa inayokusuma wewe kufanyia kazi malengo yako ni ipi. Au visingizio ndivyo vimekutawala?

  • Jibu la kuwapa watu wanaokuja kukopa kwako

    Rafiki yangu nadhani moja ya shida Kubwa ambazo zinawakumba watu wengi ni kushindwa kuwa na nidhamu ya fedha. Hivyo, kwa sababu hawana nidhamu ya na fedha. Wanatumia fedha zao hovyo na bado wanakuja kwako wakitaka uwakope.

    Ninachotaka kukwambia leo ni kuwa  kama hawana nidhamu na fedha zao, usitegeemee  kwamba ukiwakopa watakuwa na nidhamu Na fedha yako. Na Wala siyo kwamba unakuwa unawasaidia kama unavyodhani, badala yake unakuwa unazalisha tatizo.

    Hawakuwa na nidhamu Na fedha yao, hawatakuwa na nidhamu yako. Wataitumia hovyohovyo. Itaisha na watashindwa kukulipa.

    Wewe utakuwa umejipa jukumu la kudai. na kama unavyojua, kukopa ni sherehe ila kulipa ni matanga.

    Sasa ili kuondokana na Hali hiyo, hakikisha kuwa haukopi kabisa. Ipende pesa yako, vizuri sana kuliko unavyopenda kitu kingine rafiki yangu.

    MTU akikwambia naomba unikopeshe kiasi fulani Cha fedha, mjibu hivi.

    Nashukuru sana kwa KUNIAMINI sana na kuniona mimi kuwa mtu ambaye naweza kukusaidia

    Nilitamani sana nikusaidie siku ya leo, Ila umechelewa kidogo kuniambia. Laiti ungekuja asubuhi ningeweza kukusaidia vizuri Sana.

    Maana muda si mrefu nimetoka kufanya muamala mkubwa. Hivyo sitaweza kukupa hela maana muamala niliyofanya umechukua hela nyingi na bado hapa natafuta nyingine za kuongezea.

    Kwa Leo nakushauri ujitahidi uangalie sehemu nyingine.

    Asante sana kwa KUNIAMINI.

    Kalili hii kauli, na itumie hii mara zote. Ukishamwambia mtu hivyo, anakuwa hana cha kusema zaidi ya hapo.

    Itakusaidia sana

  • Dakika moja ya vitendo, ni bora kuliko maelfu ya dakika za maneno

    Wakati tunasoma O-Level tulikuwa na jamaa mmoja hivi ambaye angeweza kukutisha kuwa atakupiga. Kwa vitisho vyake tu, ungeweza kudhani jamaa ana manguvu kama HAWAFU? Kwanza unamjua Hawafu kweli? HAHAH.

    Hii stori ya Hawafu mwenye nguvu tuiache kwa ajili ya siku nyingine. Ila kama umeikumbuka vizuri unaweza kunijuza kikashani kwa kujibu ujumbe huu.

    Ssasa tuendelee na jamaa yetu. Jamaa angeweza kukutishia kwa maneno tu mpaka ukanyoosha mikono juu kuwa umeshindwa. Sasa kutokana na vitisho vyake, siku moja alikuja kumtishia jamaa ambaye hatishiki. Siku hiyo moto uliwaka…..

    Unataka kujua nini kilitokea…

    Hahah, niache kwanza. Maana ilikuja kugundulika kuwa jamaa hana nguvu ila vitisho tu.

    Sasa ninataka kukwambia nini siku ya leo.

    Ninachotaka kusisitiza kwako siyo kwamba uanze kupigana na watu kuonesha kwamba una nguvu. Badala yake, nataka nikusisitize jambo moja la msingi sana. na jambo hili ni kwamba mwaka huu ukawe wa vitendo kwako kuliko maneno. Ndio maana mwaka huu tunaenda kwa kauli mbiu kwamba haturembi mwandiko.

    Ni vitendo tu rafiki yangu.

    Kwa hiyo mwaka huu, punguza maneno. weka kazi. punguza maneno. weka kazi. punguza maneno weka kazi

    Ni hivyo tu.

    Kwenye kitabu changu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI nimemwongolea jamaa mmoja ambaye alikuwa anapenda sana kazi. na yeye muda wa kufanya kazi alikuwa anajua maneno matatu tu pale ulipokuwa ukimwongolesha.

    Nashauri na wewe utumie haya maneno pia. Kujua haya maneno muhimu ya kutumia wakati wa kazi na kupata kitabu chenyewe basi fanya hivi.

    Pata nakala yako leo hii.

    Nakala laiani ni 10,000/- na nakala ngumu ni 15,000/.

    Kitu kingine muhimu sana kwako ni kwamba tuna semina.

    SEMINA YA KUFUNGUA MWAKA MPYA 2023. Na semina hii itaanza tarehe 15. Januari, hii. na itadumu kwa siku 15 mfululizo mpaka tarehe 30.

    Semina hii itafanyi ka kwa njia ya mtandao. Na kwa siku 15 zote za semina utalipia 15,000/-.

    Ili kujiunga na semina hii. wasilina nami kwa 0755848391.

    Karibu sana.

  • KITABU: MAAJABU YA KUSOMA VITABU

    Mwezi septemba mwaka 2019 niliandaa kitabu kifupi cha Maajabu Ya Vitabu. Kitabu hiki hapa nilikisambaza bure mtadaoni. Kimetokea kuwa moja ya kitabu cha Kiswahili ambacho kimesomwa na watu wengi sana.

    Mwanzoni sikutegemea kama kitabu hiki kingesomwa na watu wengi sana. Ila kilichotokea toleo la kwanza la kitabu hiki hapa kilisomwa na maelfu kwa maelfu ya watu. Asilimia kubwa ya wasomaji wa toleo la kwanza wakawa wananitafuta na kueleza jinsi kitabu hiki kilivyobadili fikra zao kuhusu usomaji wa vitabu. Kuna watu wamejenga tabia ya kusoma vitabu mara baada ya kuwa wamesoma kitabu kile na sasa hivi watu hao ni wasomaji wazuri wa vitabu.

    Kwa hiyo, kitabu hiki kikaniunganisha na wahariri, wasomi, wakulima na watu wa kila aina kutoka ndani na nje ya nchi. Wengi wao tumejenga urafiki baada ya kuwa wamesoma hiki kitabu mpaka leo hii. Wapo waliosoma kitabu hiki hapa wakasema kwamba mimi lazima nisome na vitabu vyako vingine. na kweli wakawa wamechukua hivyo vitabu na kuvisoma pia.

    Kila aliyesoma kitabu hicho alimtumia na mwenzake ili asome. Hivyo, kwa njia hiyo kikazunguka kila kona ya nchi hii na dunia nzima kiujumla kwa wasomaji wote wa lugha ya Kiswahili.

    Hata hivyo, kadiri muda ulivyokuwa unaenda nikaendelea kuboreshakitabu hiki hapa. na hivyo, leo hii napenda kukwambia kwamba lile toleo la kwanza la kitabu cha Maajabu Vitabu halipo tena. Sasa tuna toleo la pili ambalo limeboreshwa mara 30 zaidi ya lile toleo la kwanza. Kama ulisoma toleo la kwanza ukasema, “looo, hiki ni kitabu cha kipekee kweli!”

    Sasa ukisoma toleo la pili ni wazi kuwa , hizo looo, zitakuwa mara 30 zaidi. hahah.

    Utatumiwa kitabu chako bila kuchelewa.

  • Kwa nini huwa tunarudia kusoma vitabu

    umeshapata nakakla zako? Wasiliana na 0755848391 sasa kupata nakala zako. kila nakala bei yake ni 20,000/-
    umeshapata nakakla zako? Wasiliana na 0755848391 sasa kupata nakala zako. kila nakala bei yake ni 20,000/-

    Rafiki yangu umewahi kujiuliza kwa nini huwa tunarudia kusoma vitbu ambavyo tulishavisoma siku za nyuma. Nimeanza mwaka huu kwa kurudia kusoma kitabu cha THINK AND GROW RICH. Na mwaka huu kuna vitabu vingi ambavyo nitakuwa narudia kusoma zaidi ya hiki. Unajua kwa nini huwa tunarudia kusoma vitabu.

    Huwa tunarudia kusoma vitabu kwa sababu kwenye kusoma hicho kitabu kuna kitu cha ziada ambacho tutapata kutoka kwenye hicho kitabu ambacho pengine mara ya kwanza wakati tunasoma hicho kitabu hatukukipata.

    Huwa tunarudia kusoma vitabu kwa sababu mara ya kwanza wakati tunasoma kile kitabu tulikosoma kwa mlengo fulani.

    Mfano, kama inawezekana WAKATI nasoma kitabu hicho nilikuwa nataka kujifunza zaidi kuhusu kuweka akiba, kipindi hicho mambo ya kuwekeza yalikuwa hayajaingia kichwani maana hata hela yenyewe ya kuweka akiba ilikuwa ni shida, ila sasa hivi nasoma kitabu ili nijifunze zaidi kuhusu uwekezaji.

    Au pengine nilisoma kitabu kwa sababu nilikuwa nataka kujua namna bora ya kuingia kwenye mahusiano. Ila sasa hivi nimeshaingia kwenye mahusiano na sasa nataka kujifunza zaidi kujenga na kuboresha mahusiano.

    Au pengine nilisoma kitabu nikiwa najifunza namna ya kuanzisha biashara. Lakini sasa hvii nataka kujenga timu kwenye biasahara yangu.

    KWA HIYO RAFIKI YANGU, hivyo ndivyo vitu ambavyo vinatufanya tusome vitabu na turudie kusoma vitabu zaidi na zaidi.

    Unaporudia kusoma kitabu ambacho ulishasoma mara ya kwanzpata unajikuta kwamba kuna itu vya ziada ambavyo unakuwa unapata kutoka kwenye kile kitabu ambavyo hapo mwanzoni huku

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Mambo Muhimu Utakayojifunza Kwenye Kitabu Cha JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO

    Kitabu cha jinsi ya kuongeza thamani yako ni moja ya kitabu bora utakachosoma mwaka huu. Na leo nimetamani sana nikufungulie ndani ya hiki kitabu ili uweze kuona ni kitu gani hasa unaenda kupata kutoka kwenye hiki kitabu. Kipakue hapa chini

  • Ushauri Muhimu Kwa Mtu Yeyote Ambaye Ana Lengo La Kuweka Akiba 2023

    Hivi ulivyo mwanzo wa mwaka najua kuna watu wengi ambao wameweka lengo la kuweka akiba. Watu wanataka waweke akiba ili waweze kupata uhuru wa kifedha. Sasa siku ya leo ningependa kukwambia kitu kimoja muhimu sana, wewe ambaye umeweka lengo la kuweka akiba

    KABLA sijakwambia hiki kitu naomba kujua ni wapi utakuwa unaweka fedha zako za akiba. Je, fedha hizi utakuwa unaziweka benki, au fedha hizi utakuwa ukiziweka chini ya godoro?

    Kitu kimoja kikubwa ambacho ningependa kukwambia siku ya leo ni kwamba mwaka huu FUNGUA AKAUNTI YA UTT na fedha yako ya akiba uwe unaiweka huku.

    Pengine unajiuliza UTT amis ni nini?

    UTT ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja ulio chini ya wizara ya fedha. Ambao wenyewe kazi ni kukusanya mitaji kutoka kwa watu na kuiwekeza kwa niaba ya watu.

    Kwenye hii makala sitaeleza kwa undani zaidi kuhusiana na UTT. Kama utapenda kujifunza zaidi kuhusiana na UTT nashauri sana usome kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Hiki kitabu kina kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uwekezaji kwenye UTT.

    Humu kwenye blogu pia kuna makala nyingi kuhusiana na uwekezaji huu. ila kikubwa ninachotaka kusisitiza kwenye makala ya leo ni kuhusu mrejesho pale unapoweka hela yako.

    BENKI nyingi hazitoi riba kubwa kama ilivyo UTT. Na UTT imedhihirisha kuwapa mrejesho mzuri wawekezaji wake kwa muda mrefu zaidi.

    Hivyo kama kuna kitu ambacho nakushauri rafiki yangu ni kimoja tu. mwaka huu akiba yako iweke UTT badala ya kuiweka sehemu nyingine.

    Kila la kheri.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Baadhi ya vitabu vyangu vimesomwa kwa mfumo wa sauti yaani, audiobook. Na mojawapo ya kitabu cha aina hiyo ni kitabu hiki CHA NGUVU YA VITU VIDOGO KUELELEA MAFANIKIO MAKUBWA. Hakikisha unapata kitabu hiki mapema iwezekanavyo. Tuwasiliane kwa 0755848391

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Kama utashindwa kufanya vitu vyote ndani ya mwaka 2023, hakikisha kwamba haushindwi kufanyia kazi hiki kitu kimoja tu

    Rafiki yangu, sasa hivi ndio kwanza moto wa mwaka 2023 unakolezwa. Kama bado hujaanza kufanyia kazi malengo yako, kuna nafasi kubwa kuwa unaweza usije ukakamilisha haya malengo yako kama niliyoveleza kwenye makala ya jana.

    Siku ya leo ningependa kukwambia kuwa kama mwaka huu tutashindwa kufanyia kazi malengo yako na vitu vingine, basi hakikisha kwamba haushindwi walau kuanzisha biashara mwaka huu.

    Kweli. Uanzishaji wa biashara ni moja ya hitaji la muhimu sana, muhimu mno ambalo unapaswa kulifanyia kazi ndani ya mwaka huu mpya wa 2023. Pengine kwa siku umekuwa unajipa sababu na kujiambia kwamba mwaka huu nitaanzisha biashara, ila umekuwa huanzishai hizo biashara.

    Kitu kikubw aambacho ninataka kuhakikisha kwamba nimekwakwambia ndani ya huu mwaka mpya ni kuwa biashara ina faida nyingi sana ambazo pengine ulikuwa huzijui, au pengine umekuwa unazijua ila umekuwa unapuuzia. Au pengine siyo tu umekuwa unapuuzia, bali muda mwingine ni  uoga ambao umekuwa unakusumbua.

    Ukiwa na biashara, uwezekano wa wewe kulipwa mara mbili mpaka mara tatu au hata mara kumi zaidi ya unavyolipwa sasa hivi upo. Unaweza kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa hivi, endapo utakuwa na biashara kuliko pale ambapo unakuwa hauna biashara kabisa.

    Kama umeajiriwa utakubaliana na mimi kuwa mshahara wako huwa una ukomo. Yaani, hata ufanyeje kazi, mshahara wako hauwezi kuongezeka.

    Ila kwenye bisahra hali ni tofauti. Kadiri ambavyo unakuwa unaongeza juhudi ndivyo unakuwa unaongeza nafasi yako ya kufanya vizuri zaidi,

    Hivyo basi, rafiki yangu kama kuna kitu ambacho unapaswa kufanya ndani ya mwaka huu wa 2023 ni kuhakikisha kwamba umefungua biashara. Rafiki yangu, uwanja sasa upo wazi kwa ajili yako kufanya makubwa ndani ya huu mwaka wa kipekee wa 2023. Hakikisha kwamba mwaka huu haupiti bila ya wewe kuhakikisha umefungua biashara. Kila la kheri

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

X