Home


  • Vitu 9 ambavyo hupaswi kuchoka kufanya

    Katika maisha Kuna vitu hata iweje huwezi kusema umechoka kuvifanya. Huwezi kusema nimechoka kupumua, maana ykiacha kupumua tu huo ndio mwisho wako. Huwezi kusema nimechoka kula, wala huwezi kusema nimechoka kulala, kuanzia leo sitalala tena. Ni vitu vya asili ambavyo mwili wako unahitaji ili uendelee kuwa imara zaidi.

    Wewe pia Kuna vitu unapaswa kujiwekea utaratibu wa kuvifanya bila kuchoka. Ifuatayo ni orodha ya vitu ambavyo hupaswi kuchoka kufanya.

    1. Usichokwe kuweka akiba wala kuwekeza.

    2. Usichoke kusoma vitabu maana vutakusaidia kuongeza maarifa, ufahamu na kipato.

    3. Usichoke kusamehe maana kutosamehe kunakuumiza wewe mwenyewe.

    4. Usichoke kuongeza kipato chako.

    5. Usichoke kutengeneza bidhaa bora zaidi

    6. Usichoke kutoa huduma nzuri

    7. Usichoke kushukuru

    8. Usichoke kusema ukweli

    9. Usichoke kuisimamia ndoto yako.

    Rafiki yangu, hivyo ni baadhi ya vitu ambavyo hupaswi kuchoka kuvifanya. Unaweza kuongeza vingine zaidi.

    Je, umeshapata vitabu vipi vya kwangu vya kiswahili.

    Chagua vitano Leo kwa elfu kumi tu.

    Ingia hapa uchague 

    https://www.getvalue.co/home/seller_collection/393

    kisha ulipie elfu kumi kupata vitabu hivyo vitano.

    Lipia kwa Airtel money 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

  • FANYA UNACHOPENDA

     

    Mara nyingi watu hupenda kufanya kazi fulani kwa sababu aidha ya kifedha au kutafuta umaarufu au pengine kwa kulazimishwa na wazazi.

    Lakini kazi hizi huwa hawazifanyi kutoka moyoni au Wala huwa haziwapi motisha. Ni muhimu sana ufanye kitu unachopenda kuliko kulazimisha au kulazimishwa kufanya kitu usichopenda.

    Kama ni fedha au umaarufu utaupata kwa kufanya usichopenda, ila ndani mwako utakuwa unahisi kama kuna kitu hakiko sawa mara zote. Na kitu hiki kikiendelea kwa muda mrefu utajikuta ukiishi kama vile huishi. Yaani, utakuwa mtupu.

    Ndiyo maana Benjamin Franklin aliwahi kusema kwamba kuna watu wanakufa wakiwa na miaka 25 na kuzikwa wakiwa na miaka 75. Mojawapo ya kitu kinachowafanya watu wafe wakiwa na miaka 25 ni kwa sababu wanafanya kitu wasichopenda. Hivyo, wanapita tu kwenye maisha wakiwa wanafanya kazi au kitu ambacho hakiwapi ukamilifu wa ndani.

    Kazi ya kufanya leo. Tafuta kitu au kazi unayopenda na Anza kufanya hiyo. Inaweza ikawa haikulipi vizuri leo ila baada ya muda itaweza kukulipa vizuri kwa sababu utakuwa unaifanya kutoka moyoni tena kwa nguvu na akili zote.

    Kazi usiyoipenda utaifanya sawa, lakini inaweza kwa kuwa haitoki moyoni, ufanisi kwenye hiyo kazi utakuwa ukipunguka kidogo kidogo bila ya wewe kujua. Mwisho wa siku utajikuta  umeingia pabaya.

    GODIUS RWEYONGEZA

    0755848391

    Morogoro-Tz

  • Kitu hiki lazima tu kitokee maishani mwako

     

    Kuna vitu katika maisha lazima tu vitokee. Vinatokea uwe unavipenda au huvipendi. Vyenyewe vinatokea tu.


    Jua linachomoza na kuzama, bila kujali unapenda au hupendi.
    Dunia inajizungusha kwenye mhimili wake, bila kujali una chuki nayo au unaipenda.
    Ukiruka juu, sharti utarudi chini bila kujali unapenda au hupendi.

    Mojawapo ya kitu kingine ambacho lazima kitokee kwenye maisha ni mabadiliko. Uwe unapenda au hupendi mabadiliko lazima tu yatatokea.

    Ndio maana unaona kila zama huwa zina matajiri ambao huwa wanatengeneza mabilioni ya fedha ya kutumia fursa ya mabadiliko fulani vizuri.

    Mansa Musa alikuwa tajiri mkubwa kuwahi kutokea duniani kwa sababu alitumia fursa ya kuuza chumvi na dhahabu enzi zake vizuri. Unaweza kushangaa chumvi?!! Ilimtajirishaje mtu?? Ukweli ni kwamba kipindi chake chumvi ilikuwa dili kubwa Kama ambavyo miaka ya 1800 viwanda vilikuwa dili kubwa pia.

    Kitu Kikubwa ninachotaka ni wewe kuhakikisha unasoma mabadiliko na kuyatumia kwa manufaa.

    Ni hayo tu
    NAKUKUMBUSHA TU. Kama hukupata nakala ya kitabu cha MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE kwa elfu sita tu (6,000/-) changamka utumie fursa hii leo hii. Kuanzia mwezi ujao kitabu kitarudi kwenye bei yake ya elfu kumi.

    Hivyo kipate Leo kwa elfu sita tu. Cha kufanya Sasa. Tuma elfu sita (6,000/-) kwa MPESA 0755848391 au Airtel money 0684 408 755
    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    CHANGAMKA SASA.

  • Madhara Ya Kuwa Na Mahusiano Na Mtu Zaidi Ya Mmoja

     

    Kama una ndoto kubwa na umekuwa na mpango wa kuja kuwa na mahusiano na watu wawili, au tayari una mahusiano na watu wawili ni bora ukauhairisha au kuondoa kabisa huo mpango. Yafuatayo ni mdhara ya kuwa na mahusiano na zaidi ya mtu mmoja.

    Kwanza utapoteza nguvu zako nyingi kwa watu hao ambao umeingia nao kwenye mahusiano. Hizi ni nguvu ambazo ungeweza kuzitumia kufanya kazi zako za maendeleo.

    Pili, utapoteza muda wako ambao ungeweza kuutumia kufanikisha NDOTO zako.

    Tatu, utapoteza fedha ambazo zingekusaidia kufanikisha NDOTO zako kubwa. Na kama unavyojua muda ni mali.

    Hayo ni madhara ya kuwa na mahusiano na zaidi ya mtu mmoja. Epuka kitendo hiki kwa nguvu zako zote.

  • Kitabu cha KUTOKA UMASIKINI MPAKA MAFANIKIO CHA ERICK SHIGONGO.

    Kwenye kitabu hiki Erick Shigongo ameeleza historia ya maisha yake na kutoa mafunzo kadha kadha kuhusu maisha

    Kitabu hiki ni kizuri sana, nashauri kila mwenye kiu ya mafanikio makubwa akisome. Utajifunza mengi kuhusu kutoka umasikini mpaka mafanikio makubwa kupitia stori ya Erick Shigongo ambaye maisha yake yalikuwa duni sana, kuliko hata wewe ila akaweza kupasua anga na kufikia viwango vikubwa.

    Utajifunza na kuona ni kwa jinsi gani na wewe unaweza kufanikiwa pia kupitia mbinu mbalimbali alizoshirikisha mwandishi huyu.

    Moja ya kitu ambacho nakikumbuka sana kutoka kwenye kitabu hiki ni kauli inayosema kwamba; Kuna watu kwa tabia zao wataendelea kuwa masikini na Kuna watu kwa tabia zao hata waukimbie utajiri, utazidi kuwafuata tu.

    Leo nimeona nikushirikishe hili ili na wewe ujitathimini tabia zako. Hivi ni kweli wewe ukiamua kuukimbilia utajiri utakufuata kweli au utaendelea kuwa masikini tu kutokana na tabia zako?

    Jiulize una tabia gani. Na je, hizo tabia zinakupeleka wapi?

    Soma zaidi:

    Watanzania Tujenge Utaratibu Wa Kukubali Vitu Vyetu.


    UCHAMBUZI WA KITABU CHA SUGU; MAISHA NA MUZIKI. Mambo 14 niliyojifunza kwenye kitabu hiki kinachoeleza Maisha ya Sugu Kutoka Mtaani Mpaka Bungeni

     

    Kila la kheri.

    GODIUS RWEYONGEZA
    Morogoro-Tz

  • Fursa iliyotengeneza mabilionea kwenye karne ya 21

     

    Madalali ni watu ambao wamekuwepo kwa siku nyingi sasa. Kazi yao kubwa imekuwa ni kuunganisha eneo moja lenye bidhaa na jingine lenye uhitaji.

    Kama una uhitaji wa chumba cha kupanga unamwona dalali anayekuunganisha kilipo.

    Kiufupi wenyewe wamekuwa wanaingia katikati ya mlaji na mzalishaji.

    Kwenye karne ya 21 udalali ndio umetengeneza mabilionea kwa wingi. Mtandao wa amazon na alibaba ni ya kidalali inayounganisha  kati ya wazalishaji na walaji wa mwisho wa bidhaa.

    Mtandao wa Uber ni wa kidalali pia. Unaunganisha kati ya wenye teksi na wasafiri.

    Google pia ni mtandao wa kidalali, unaunganisha mwenye taarifa na mwenye uhitaji nazo.

    Ukiangalia mitandao yote hiyo imetengeneza mabilionea wakubwa. Hivyo, kwenye karne hii ya 21 ukitaka kuwa bilionea, basi kuwa dalali wa kidigitali. Unganisha watu na huduma wanayoihitaji.

    Kila la kheri.

    Umeshapata kitabu cha MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE

    Kama bado fanya hivi, tuma elfu sita (6,000/-) kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA Sasa ili upate kitabu hiki cha kipekee sana.

  • Asilimia 99 ya Maisha ya Watu Hujihusisha Na Vitu Hivi

    Leo nimekuandalia vitu ambavyo huwa vinachukua muda wa watu japo huwa havina manufaa yoyote kwao. Ni jukumu lako kuvifahamu na Kisha kuamua kuachana navyo.

    1. Watu wengi hupoteza muda mwingi wakihofu jinsi watu wengine wanavyowafikiria, wakati na wao wanahofu wanasemwaje.

    2. Watu wengi huishi maisha kwa kutaka kuwaridhisha wengine; wakati mtu pekee wanayepaswa kumridhisha ni wao wenyewe.

    3. Watu hutumia muda mwingi kwenye mahusiano yanayowaumiza wakitarajia  yatakuwa mazuri muda wowote.

    4. Watu wengi hutumia mida mwingi kuongea umbea na kuwasema watu. Ukweli ni kwamba mtu anayemsema mwingine mbele yako. Atakusema na wewe mbele ya wengine.

    5. Watu wengi hutumia muda mwingi wakijaribu kuishi aina fulani ya Maisha ili waendane na jamii husika. Kitu ambacho huwa kinawafanya wasiishi uwezo wao halisia.

    6. Watu wanatumia muda mwingi kufanya kazi ambayo hawaipendi. Wakishindwa kutoa hata dakika kidogo tu za kufanya kitu wanachopenda.

    7. Watu wengi wanatumia muda mwingi kutafuta fursa nzuri ya kufanyia kazi. Kitu ambacho huwa kinawafanya wakimbizane kutoka fursa moja kwenda nyingine.

    Pata nakala ya kitabu cha MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE Leo kwa elfu sita (6,000/-)

    Tuma sasa elfu 6 kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    KARIBU
    NI MIMI
    GODIUS RWEYONGEZA
    +255755848391
    MOROGORO-TZ

  • Hiki Ndicho Kitakachotokea Miaka Mitano Ijayo…

     Miaka mitano ijayo utakuwa jinsi ulivyo ,isipokuwa kwa vitu viwili. Vitabu unavyosoma na watu unaokutana nao. Watu unaokutana nao wana uwezo wa kukubadili na kukufanya mpya. Watakupa mtazamo wao, fikra zao, ujuzi n.k.

    Ukitaka kwenda MBALI ambatana na watu sahihi.

    Vitabu pia ni muhimu sana. Vitabu muda mwingine vinaweza kukukutanisha na watu sahihi. 

    Muda mwingine kama hupati watu sahihi, basi unapaswa kuvifanya vitabu kuwa rafiki yako wa kweli.

    Kwa kulifahamu hili, nimekuandalia kitabu cha MAISHA NI FURSA: ZIBEBE ZIKUBEBE. Ili kiweze kuwa mwongozo kwako kwenye suala zima la fursa.

    Hakikisha unapata kitabu hiki cha kipekee, ambacho kinapatikana kwa bei nafuu tu  ya elfu sita (6,000)/-)

    Kupata nakala ya kitabu hiki lipia elfu sita kwa

    MPESA 0755848391

    Airtel money: 0684 408 755

     Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    NB. Kitabu hiki ni soft copy.

    Ni mimi

    GODIUS RWEYONGEZA

    +255755848391

    MOROGORO-TZ

  • USIPOZIBEBA FURSA, HAZITAKUBEBA

     

    Moja ya shida ya watu ambao huwa wanashindwa kutumia fursa ni kujuta mbeleni.

    Ndio baadaye unakuja kusikia mtu anasema kuwa;
    ๐Ÿ‘‰ Mtu fulani tulisoma wote.
    ๐Ÿ‘‰Mtu fulani tulianza kazi kwa pamoja.
    ๐Ÿ‘‰Maeneo fulani viwanja vilikuwa   vinauzwa kwa bei ndogo ila sasa havishikiki.
    Ne  mengine mengi

    Hiki ni kiashiria kimojawapo kuwa mhusika hakutumia fursa zilizojitokeza maishani mwake vizuri. Usipozitumia fursa vizuri, ni ukweli kuwa haziwezi kukubeba.

    Pata kitabu cha MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE leo kwa elfu sita (6,000/-) tu leo.
    Nakala hii imesheheni mambo mengi mazuri kuhusu fursa.
    ๐Ÿ‘‰kimeeleza maana ya fursa: kwenye kitabu utakutana na zaidi ya maana kumi za fursa.
    ๐Ÿ‘‰ utajua jinsi ya kuziona fursa.
    ๐Ÿ‘‰ Utajua kwa nini watu hawazioni fursa hata japo mimi ninasema fursa zipo za kutosha
    ๐Ÿ‘‰ Tutajibu swali la kwa nini maisha ni magumu japo fursa zipo nyingi.
    ๐Ÿ‘‰ Tutaona maeneo zilipojificha fursa
    ๐Ÿ‘‰Tutaona fursa zilizohama kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Hizi ni fursa ambazo zilikuwepo miaka mingi sana iliyopita na bado zipo sasa hivi; yaani alizitumia babu yako mpaka wewe kitukuu
    ๐Ÿ‘‰  Tutaona jinsi ya kuhamisha fursa kutoka eneo moja kwenda jingine
    ๐Ÿ‘‰ Jinsi ya kugundua fursa mpya
    ๐Ÿ‘‰ Vigezo vya kuitambua fursa ya kweli na mengineyo mengi.

    Hakikisha unapata nakala yako leo kwa elfu sita (6,000/-) tu.  

    Lipia kwa:

    MPESA 0755848391

    Airtel money: 0684 408 755

     Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    NB. Kitabu hiki ni soft copy.

    Ni mimi

    GODIUS RWEYONGEZA

    +255755848391

    MOROGORO-TZ

  • Kwa Nini Asilimia 1 Tu Ya Watu Duniani Ndio Hufanikiwa Sana

    Tafiti nyingi zimeonesha kuwa asilimia 1 ya watu duniani ndiyo wenye mafanikio makubwa kukiko wengine. Na hiki kitu kinaelekea kuwa kinafanya kazi kila sehemu.

    Asilimia 1 ya watu ndio wanaoohodhi mitandao tunayoitumia mara kwa mara. Ndiyo maana juzi anguko la mitandao ya facebook limeleta taharuki kubwa sana.

    Asilimia 1 ya watu ndio wanaomiliki mashamba makubwa na ndio wanaozalisha kwa wingi kuliko asilimia 99 iliyobaki.

    Na mwendelezo huu unaweza kuuona karibia kwenye kila sekta.

    Sasa kwa nini watu wachache tu ndio wanabarikiwa hivi?
    Kwa sababu maisha ni fursa. Wale wachache ambao wanakuwa tayari kubeba fursa hizi na kuzitumia ndio ambao wanabarikiwa zaidi, huku wale ambao hata hawana jicho la fursa wakiendelea kubaki vilevile. Na fursa ukizitumia lazima tu zitakubeba. Kitu hiki kinawafanya watu wachache sana kufanikiwa ukilinganisha na wengine.

    Hivyo, basi unapaswa kubadili mtazamo wako na kuanza kuangalia maisha kwa mtazamo wa kuziona fursa. Maisha Ni Fursa Zibebe.

    Kwa kuona hili, nimekuandalia kitabu kinachoitwa MAISHA NI FURSA. ZITUMIE ZIKUBEBE , kwenye kitabu hiki nimekueleza kwa kina kila kitu Unachohitaji kujua kuhusu fursa. Ni kitabu ambacho nisingependa kuona unakikosa.
    Hakikisha unapata nakala yako leo.
    Kupata nakala yako, tuma elfu sita tu (6,000/-) kwa
    Airtel money: 0684 408 755 au

    Mpesa 0755848391

    kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Baada ya malipo utaniambia nikutumie kitabu.

    NB. Kitabu hiki ni soft copy.

    Changamka sasa upate nakala yako.

X