Home


  • Kitu Kinachoashiria Kuwa Hutafika Mbali Kimafanikio

     Kuna vitu vingi ambavyo vinaashiria kuwa hutaweza kufika mbali kiuchumi, hata hivyo kimoja kikubwa sana kati ya vyote ni KUTOJIFUNZA.

    Kama  hupati muda wa kujifunza na hasa kwa kusoma vitabu , jua hicho ni kiashiria cha wewe kuja kuanguka siku moja.

    Hili litatokea bila kujali unafanya kazi kwa bidii sana au una mtaji mkubwa, kwa sababu asili inaonesha kwamba kitu chochote ambacho hakikui basi kinakufa.

  • Kitu muhimu cha kufahamu kwenye zama hizi za teknolojia

    Tupo kwenye zama za teknolojia ambapo unaweza kufanya karibia kila kitu kwa mtandao. Unaweza kuongea na watu wa mbali kwa mtandao. 

    Unaweza kuonana na watu wa mbali kabisa kwa njia hiihii ya mtandao  unaweza kutuma na kupokea fedha na mambo mengine mengi. Kitu kimoja tu ambacho bado kimebaki na nguvu kubwa kwenye kipindi hiki ni nguvu ya kuonana.

    Hapa sizungumzii kuonana kwa Skype Wala zoom, bali kuonana ana kwa ana.

    Ndiyo. Bado kuonana ana kwa ana kuna nguvu kwelikweli.  Katika zama hizi, kama una jambo lako la nguvu unataka kuongea na mtu, ni muhimu uonane naye ana kwa ana.

    Ni rahisi kufikia uamuzi bora unapokuwa na mtu ana kwa ana kuliko anavyokuwa mbali.

    Kanuni muhimu ambayo binafsi huwa inaniongoza ni hii hapa.
    Kama unaweza kuonana na mtu ana kwa ana, usipige simu.
    Kama unaweza kupiga simu, usitume ujumbe.

    Kumbe ujumbe mfupi wa sms au whatsap uwe ni njia ya mwisho unayoweza kutumia baada ya kuona njia nyingine zimeshindikana.

    Karibu.

  • Daah! 50 Cent Kwa Hili Kaua!!

     

    Leo nimekikukumbuka kitabu cha the 50th Law kilichoandikwa na mwandishi nguli wa masuala ya vita, utawala na tabia za binadamu Robert Greene.

    Kitabu hiki amekiandika pamoja na 50 Cent na kiuhalisia kitabu hiki, kinazungumzia maisha ya 50 Cent na jinsi alivyoweza kufikia viwango vikubwa kimuziki na kimaisha.

    Kitu kimoja ambacho Waandishi Wa kitabu hiki wanasisitiza ni kutoogopa.

    50 Cent anasema kitu kikubwa ambacho unaweza kukiambatanisha na maisha yake ni kutoogopa. Yeye haogopi chochote kile maishani mwake. Na hicho kitu ndicho kimemfanya ashinde vikwazo ambavyo huwa hata vinawazuia watu kuchukua hatua ya kwanza.

    Waandishi wanasisitiz kwamba, usiogope. Kamwe usiogope kabisaaa kwenye maisha yako.

    Na mimi Leo napenda kukusisitiza kwamba usiogope 

    Kama wewe huwa unasoma Biblia, watalaamu wanakwambia kwamba kwenye Biblia Kuna USIOGOPE 365. Hivyo, hata Leo ulipoamka asubuhi, umeambiwa usiogope.

    USIOGOPE

  • KWA WAANDISHI WA VITABU:NI LUGHA GANI NZURI UNAPASWA KUTUMIA WAKATI WA KUANDIKA KITABU CHAKO?

    Kuna watu huwa wanauliza ni lugha gani inafaa kutumia kwenye kuandika? Kiswahili au kiingereza?

    Jibu la swali hili ni vigumu kulipata kwa mtu mwingine, badala yake wewe mwenyewe unapaswa kuangalia
    Watu uliowalenga.

    Kama wasomaji wako wanajua vizuri Kiswahili Basi waandikie kwa Kiswahili, au la kama wanauelewa na kiingereza waandikie kwa kiingereza.

    Kwa hiyo badala ya kujiuliza niandike kwa Kiswahili au kiingereza; jiulize wasomaji wangu ni watu wa aina gani? Je, wanaiweza lugha gani?

    Tumia taarifa hizo kwenye kuandika kitabu chako.

    Kupata kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 tuma elfu 5 kupata softcopy na elfu 15 kwa hardcopy.

  • Waandishi Wa Vitabu: Igeni Kitu Hiki Kimoja Tu Kutoka Kwa Wasanii Muziki

     

    Huwa napenda kusikiliza muziki wa bongo flava mara mojamoja ninapokuwa nimepumzika. Kama na wewe huwa unausikiliza walau hata mara moja moja nyoosha mkono juu tujuane.

    Ukifuatilia muziki huu hata kwa dakika tano tu, Kuna kitu kimoja ambacho utakigundua kwa wasanii na hiki ndicho ninataka tujadiliane leo. Kitu hiki siyo kingine bali ni kushirikisha kwa baadhi ya wasanii kwenye tungo zao mbalimbali.

    Utakuta msanii fulani ameshirikiana na msanii mwingine kutoa tungo fulani. Ni kitu ambacho ukikiangalia kwa juu juu unaweza kuona ni cha kawaida au hakina maana, ila ukikiangalia kwa jicho la kipekee utagundua kuna kitu Kikubwa cha kujifunza hasa kwa WAANDISHI.

    Labda tujiulize kwa Nini wasanii wa muziki huwa wanashirikiana? Sababu kubwa ni kupeana konekisheni na mashabiki.

    Unakuta msanii A ama wafuasi na mashabiki wake huku msanii B akiwa na wafuasi na mashabiki wake pia. Sasa wanapoungana kutengeneza wimbo mmoja kuna wafuasi na mashabiki wa msanii A wataanza pia kumfuata na kumsabikia msanii B na hivyohivyo kwa upande wa pili.

    Hakuna msanii anaogopa kushirikisha na mwenzake kwa kuogopa kuwa mwenzake ataondoka na wafuasi wake wote, badala yake wanashirikiana kadiri wawezavyo.

    SASA WAANDISHI TUNAWEZA KUITUMIAJE HII?

    Looo! Nimekumbuka kwamba naongea na waandishi na siyo wasanii wa muziki, ngoja sasa niache kuongelea masuala ya wasanii bwana niongelee mambo ya kiuandishi?

    Kwa Waandishi mnaweza kutumia hii njia kwa kushirikisha katika kuandika makala.
    Kuandika kitabu
    Kuatangaziana bidhaa au vitu vyenu.
    Kupost vitu vya mwenzako na mwenzako kupost vya kwako (hapa tafuta mwandishi ambaye mpo kwenye level moja au mnazidiana kidogo)
    Kukomenti kwenye maandiko ya mwandishi mwenzako kwa kuongezea pointi za maana zaidi. Hii pia inaweza kukuongezea idadi ya watu wanaofuatilia kazi zako.
    Kushiriki kikamilifu kwenye kundi la mwenzako na kutoa mafunzo.
    Kuweka Dibaji kwenye kitabu chako; Dibaji iwe imeandika na mtu ambaye ana jina kubwa kuliko wewe.
    Kuwaomba  Waandishi wengine wakuandikie neno fupi kuhusu kitabu chako (review).

    Na mengine mengi.

    Kwa hayo naamimi walau umelata kitu ambacho kinaweza kukusaidia Kama mwandishi.

    Kama wewe MWANDISHI ambaye uko siriazi na kuandika na unataka kwenda viwango vingine, Basi hakikisha umesoma kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30.
    Nakala laini (soft copy) inapatikana kwa 6500/- tu. Nakala ngumu kwa Sasa haipo. Tuwasiliane sasa kwa 0755848391 ili upate nakala yako

  • Majadala Mzito Kuhusu Kitabu Cha Kutoka SIFURI MPAKA KILELENI//GODIUS RWEYONGEZA

    Siku moja nilishiriki kwenye mjadala kwenye kundi la KITABU CHAT. ambapo mada kubwa ilikuwa ni KILICHOMO NDANI KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. Nilianza kwa kutoa utangulizi mfupi kuhusu kitabu hiki hapa cha kipekee sana.

    baada ya utangulizi na mae

    lezo machache, yalianza kuulizwa maswali. swali la kwanza kuulizwa lilikuwa ni hili hapa chini.

     “…mtu akifanya kazi huyaelekea malengo yake, ndivyo ambavyo 

    malengo nayo yanavyomfuata, hatimaye mtu pamoja na 

    malengo yake huweza kukutana sehemu…” haraka nimekutana na nukuu hii Godius Rweyongeza🔥🔥

    Aliyeuliza swali hilo hapo alitaka kujua haswa ni ujumbe gani uliojificha nyuma ya hiyo kauli. yafuatayo ni majibu niliyotoa

    hii maana yake kuwa huwezi kukaa ukiwa umebweteka na kusubiri malengo yako yaweze kutimia. Lazima uchukue hatua na kuanza kuyafanyia kazi malengo yako.

    Na kadiri unavyokuwa unayafanyia kazi malengo yako, ndivyo fursa zaidi za kutimiza malengo yako zinajitokeza. Kwa jinsi hiyo unakuta kuwa hata lile lengo ambalo lilikuwa linaonekana ni kubwa basi linaanza kutimia.

    Kiufupi ni kuwa kama unataka kuhamisha mlima, lazima uchukue hatua ya kuanza kutoa jiwe moja. usitegemee kupata bahati ukiwa umejifungia chumbani kwako. 

    kuwa tayari kutoka nje na kuanza kazi. humuhumu katikati mambo mazuri yatatokea na hivyo kurahisisha safari ya wewe kutimiza malengo yako. Hali kama hii haiwezi kutokea endapo utakuwa umelala tu chumbani ukiwa unasubiri labda siku moja mambo yaweze kukaa vizuri.

    Rafiki yangu, hivyo ndivyo nilivyojibu swali hilo hapo. 

    Jipatie nakala ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI leo pamoja na zawadi nyingine kedekede.

    Iko hivi, ukilipia kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI, nitakutumia vitabu vingine vinne, ambavyo Ni 

    1. MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.

    2. MAISHA NI FURSA ZITUMIE ZIKUBEBE

    3. SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA 

    4. Cha NNE utachagua mwenyewe  kutoka kwenye orodha ya vitabu vyangu hapa au 

    HAPA

    Utalipia kwa Airtel money namba 0684 408 755

    Changamka sasa. Hii ni ofa ya Leo tu

  • KUZA KIPAJI CHAKO

    Kipaji ni mauwezo fulani hivi ya asili ambayo mtu unazaliwa nayo na yanakuwezesha kufanya vitu kwa namna ya upekee sana.

    Mauwezo haya yanakutambulisha kwa watu kwa sababu hakuna mwingine ambaye anakuwa nayo. Na wala ya kwako hayawezi kulinganishwa na ya mtu mwingine. 

    Sasa nikuulize wewe, kipaji chako unakifahamu?

    Ni kipi? Na je unakifanyia kazi?

    Hakikisha unakitumia vizuri kipaji chako maana, siku ya mwisho utaulizwa namna ulivyokitumia kipaji chako😀😀.

    Kujua namna nzuri ya kugundua na kutumia kipaji chako hakikisha umesoma kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. Sura ya KUMI imeeleza kwa kina jinsi ya Kugundua kipaji chako, kukinoa na kukitumia kwa manufaa. Fungua ukurasa wa 52 kwenye kitabu ujionee mwenyewe.

    Kama huna kitabu hiki, rusha elfu 10 leo ili uweze kukipata. Nitakutumia na vitabu vingine vitatu ambavyo ni

    1. MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE

    2. MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE

    3. SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA

    Rusha sasa hivi kwa 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

  • Usiende Chuo Kusomea Uandishi Wa Vitabu; Badala Yake Fanya Hivi

    Siku kadhaa zilizopita nilipokea simu ya mtu aliyekuwa anataka nimwambie chuo kizuri kinachonoa Waandishi Wa Vitabu.

    Nilimjibu vizuri tu, ila hakuridhika na majibu yangu kwa maana yalipingana na kile alichokuwa anaamini kwa asilimia 100. Yeye alitaka kwenda chuo, asomee uandishi na apate cheti. Cheti cha nini sasa? Najua, jamii yetu imezoea kwamba ukiwa na cheti basi hapo unakuwa umefaulu na unaenda ku-win maisha.

     Baada ya siku kama tatu hivi nilipokea ujumbe huu hapa chini kutoka kwa mtu mwingine.

    Nadhani huyu alinifafuta na tuliongea kwa kina kuhusu hili.

    . Simshauri kwa Sasa apoteze fedha zake kwenda chuo kwenda kusomea UANDISHI. 

    Kuna kozi nyingi ambazo anaweza kusoma mtandaoni tena akiwa nyumbani, na akiwa anaendelea na shughuli zake za sasa. 

    Ni sawa kuingia darasani, ila kwa sasa asifanye hivyo.

    Afanye yafuatayo.

    1. Aanze kuandika

    2. Amtafute ‘mentor’ wa kumsaidia.

    3. Aoneshe kazi zake anazoandika aidha mtandaoni au kwa watu wake wa karibu.

    4. Apokee mrejesho wa kazi zake na aufanyie kazi.

    5. Atumie mrejesho anaoupata na mafunzo anayopata kuboresha uandishi wake zaidi.

    Kuna mengi ila kwa sasa hayo yanatosha.

    Najua ushauri huu ataupuuza. Ila walau ninachofahamu kwa sasa atapoteza muda wake kwenda kujifunza uandishi kwa ajili tu ta kupata CHETI ambacho mwisho wa siku hakitamsaidia chochote.

    Ngoja nieleze kitu zaidi hapa. Waandishi hawafahamiki Kama waandishi kwa sababu wanaVYETI. Waandishi ni waandishi kwa sababu wanaandika.

    Mimi siyo mwandishi kwa sababu Nina cheti; HAPANA. Sijawahi hata siku moja kuona mtu ananiuliza cheti changu cha kuwa mwandishi kipo wapi😊😊. 

    Kitu kingine ni kwa kuwa nguvu yake kubw ipo kwenye cheti kuliko kufahamu zaidi mchakato wa kuandika na kubobea kwenye uandishi, ataweka NGUVU kwenye kupata CHETI na atapata, ila hatakuwa mwandishi mzuri. Na hicho ndiyo kuantokea pia kwenye mfumo wa elimu. Wahitimu wengi wanahitimu na vyeti vizuri ila ujuzi SIFURI kutokana na ukweli kuwa waliweka nguvu kubwa kwenye VYETI kuliko kupata ujuzi.

    🖊️🖊️🖊️🖊️🖊️🖊️

    Nashauri asome kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 ambacho kimeeleza kila kitu anachohitaji kujua kuhusu uandishi👇👇

    Au awasiliane nami kwa 0755848391

  • FANYA UAMUZI SASA

    Bila kujali upo katika hali gani, Kuna wakati unapaswa kufanya UAMUZI kwamba sasa mimi nitaanzia hapa na nitaendelea mbele 

    Kataa kabisa kuendelea kusema kwamba sina mtaji

    Kataa kuendelea kulalamikia ugumu wa maisha.

    Chagua kuanzia hapo ulipo, miaka 10 ijayo utajishukuru kwa uamuzi huu.

    Amua Sasa kupata vitabu vitano kwa elfu kumi tu. Hii ofa mwisho wake ni  Leo hii

    Vitabu vyenyewe ni

    1. MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.

    2. MAISHA NI FURSA ZITUMIE ZIKUBEBE

    3. SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA 

    4. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI

    5. Cha tano utachagua mwenyewe kutoka kwenye orodha ya vitabu vyangu hapa

    https://www.getvalue.co/home/seller_collection/393

    Utalipia kwa Airtel money namba 0684 408 755

    Changamka sasa. Hii ni ofa ya Leo tu

  • Kinachotokea Unapokuwa Na Ndoto Kubwa

     Jana niliandika makala yenye vitu 9 ambavyo hupaswi kuchoka kufanya. Mmoja wa wasomaji wa amkala hiyo alinibu kwa kusema hivi

    Nami nikawa nimemjibu pia kwa ujumbe huu hapa chini

    Ni kweli unapokuwa unapambania ndoto kubwa watu watakuona mtu wa ajabu sana. 

    Watakuona kichaa, utaambiwa umechnganyikiwa na mambo mengine mengi.

    Na hili linawatokea watu wote wenye ndoto kubwa. 

    Kuwa na ndoto kubwa ni sawa na kucheza muziki ukiwa na earphone masikioni. Wengine hawausikii huo muziki ila kwako unakuwa umenoga. Wanaokuona unacheza watakuona kichaa tu, kwa sababu muziki unaocheza kwao hauna maana.

    Ndio  maana Steve Jobs anasema kwamba, watu wenye kichaa cha kutosha kiasi cha kufikiri wanaweza kuibadili ndio ambao huibadili. Kuna wakati unapokuwa na ndoto kubwa, unapaswa kukubali tu kuonekana kichaa.

    Nashauri sana usome kitabu changu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Kina mengi ya kueleza kuhusu ndoto.

X