Maneneo Sita (06) Ambapo Kila Kijana Mwenye Miaka 20-29 Anapaswa Kuwekeza


Habari ya siku hii ya kipekee rafiki yangu, karibu sana kwenye makala hii ya siku ya leo. Ambapo tunaenda kujifunza maeneo sita kwa kjjana yeyote mwenye miaka kati 20-29 anapaswa kuwekeza.

 

Labda unaweza kujiuliza kwa nini leo niongelee kuhusu miaka 20-29. Jibu lake ni kwamba, hiki ni kipindi ambapo vijana wengi wanakuwa na ndoto za kufanya makubwa, ndoto za kutengeneza utajiri, ndoto za kuwa wanamziki, ndoto za kugombea nafasi mbalimbali na kuchukkua nyadhifa serikalini. Hata hivyo, mbali na kuwa na ndoto hizi, asilimia kubwa ya vijana huwa haifanyi kitu chochote kuzileta kwenye uhalisia. Ndio maana siku ya leo, nikaona wazi kabisa nikuletee maeneo haya 6 ambapo kijana wa aina hii anaweza kuwekeza ili kutengeneza maisha bora.

 

Kitu kingine ni kwamba,  asilimia kubwa ya watu waliofanikiwa wakiwa na miaka 30, basi waliwekeza sana kipindi wakiwa na miaka 20 na kuendelea. Ukizungumziia akina Steve Jobs, Bill Gates, Mark Zuckerberg, Warren Buffet Hiki ni kipindi ambacho kijana anakuwa hana vitu vingi vya kupoteza hivyo kujitoa ni rahisi.  Bila kuongeza neno la ziada tunaanza kuona maneno yetu 10

ENEO LA KWANZA; NI KUWEKEZA KWENYE KUSOMA VITABU

Hili ni eneo muhimu sana kwenye maisha. Kusoma ni lenzi ambayo inakuonesha wpi unapaswa kwenda. Nimegundua kwamba, ukitaka kumuua binadamu mnyime maarifa. Kifo cha kukosa maarifa ni kikubwa kuliko vifo vingine. na kifo hiki kinaweza kupelekea kutokea kwa aina nyingine ya vifo haraka. Mtu akikosa maarifa ni rahisi kufa pia kiroho, kiakili na hata kupelekea kufa kimwili. Inawezakana aliyesema kwamba, baadhi ya watu hufa wakiwa na miaka 20 na kuzikwa wakiwa na miaka 80 alikuwa pia akimaanisha, kukosa maarifa kunaweza kupelekea huko.

 

Kwa hiyo kijana yeyote yule, asikubali kufa akiwa na miaka 20 huku akisubiri kuzikwa na miaka 80. Badala yake, aamue kwa dhati kwamba anaenda kuwekeza kwenye kujifunza na kupata maarifa sahihi. Vitabu vina kila aina ya maarifa. Hakuna kitu ambacho huwezi kujifunza kwenye vitabu. Labda uezembe tu ndio sijaona unafundishwa kwenye vitabu.

 

ENEO LA PILI; WEKEZA KWENYE MAHUSIANO BORA

Bila shaka, umewahi kusikia usemi kwamba, its not what you know but who you know. Ukimaanisha kuwa, sio kile unachojua kinachokupa mafanikio, bali yule unayemfahamu. Huhitaji kuwa umetoka kwenye famila ya kipekee ili uweze kufanikiwa kimaisha. Unaweza kuanzia popote pale na ukajenga mahusiano bora na watu na wengi.

Kitu muhimu ni kuanza kuwatumia watu ambao kwa sasa hivi wamekuzunguka. Ukikutana na mtu mmoja ambaye amepiga hatua na kukuzidi wewe, ebu muulize ni mtu gani  mwingine ambaye anaweza kukuunganisha naye na ukajifunza kutoka kwa huyo pia. Kwa kufanya hivi utashangaa sana kuona kwamba mtu mmoja atakuelekeza kwa mwingine na mwingine atakuelekeza kwa mwingine pia. Kwa hiyo mwisho wa siku utajikuta una mzunguko wa watu sahihi.

 

Wekeza pia kwenye mahusiano ya familia yako na ndugu zako. Kuwa na wakati wa kuwa nao na kama wako mbali, basi muda maalumu wa kuongea nao. Siku hizi mambo yamerahishwa. Unaweza kuwapigia whatsapp call. Au mnaweza kuongea na kufanya kikao cha familia kupitia simu (conference call) au kupitia skype. Mambo ni rahisi sana, tumia teknolojia kwa manufaa yako. Sio kila wakati teknolojia inakutuia wewe.

 

ENEO LA TATU; WEKEZA KWENYE KUJIFUNZA TABIA ZA KIMAFANIKIO

Kuna tabia za kimafanikio ambazo unapaswa kuwa nazo ila sasa hivi huna, hakikisha kwamba unawekeza kwenye hizi tabia ambazo hauna. Kitu kizuri ni kwamba unaweza kujifunza kitu chochote ambacho utaamua.

 

ENEO LA NNE; WEKEZA KWENYE NDOTO ZAKO

Hiki ni kitu kingine muhimu sana. kama ndoto yako ni kutengeneza utajiri basi ifanyie kazi. kama ndoto yako ni kuwa mwanamziki, muigizaji, mchoraji, mchekeshaji. Tumia kipindi hiki kuwekeza kwa nguvu zako zote huku.

 

Unaweza usianze kuona matokeo haraka kama ambavyo unatarajia, lakini hilo lisikukatishe tamaa. Endelea kusongambele. Kama kila siku unaweza kumfikia mtu mpya mmoja ambaye anaweza kuiona kazi yako, endelea mbele. Huyo mtu mmoja atakuletea mwingine mmoja. Na huyo mwingine atakuja na mwingine.

Kosa kubwa unaloweza kufanya kwenye kipindi hiki hap ni kuanzisha kitu kisha ukaishia njiani. Usithubutu kufanya hivyo.

 

ENEO LA TANO; WEKEZA KWENYE KUFANYIA KAZI UNAYOJIFUNZA.

Tayari nimekwambia uwe unasoma vitabu. Ila sasa haitoshi. Unapaswa kufanyia kazi yale ambayo unajifunza kila siku. Hivyo wekeza sana kwenye kuyatendea haki yale unayojifunza. Wahenga wanasema kwamba utamu wa ngoma sharti  uingie ucheze. Hvivyo hivyo kwa yale unayojifunza.

 

Kwa mfano, ukisoma kitabu cha The Richest Man In Bablon. Mwandishi anasema kwamba, unapaswa kujilipa wewe mwenyewe asilimia 10 ya kila kipato ambacho unaingiza.

Kwa hiyo wewe usiendelee na tabia zako hizo hizo za zamani.  Fuata mwandishi anachosema ili upate matokeo anayokwambia utapata endapo utafuata. Fuata kilichosemwa bila kujali upo kwenye hali gani. Ni bora ulale ulale njaa ukiwa na miaka 20 ila uweke akiba kuliko kuja kulala njaa ukiwa na miaka 30, 40 au 50.

 

ENEO LA SITA; WEKEZA KWENYE UJUZI MUHIMU

Kuna aina ya ujuzi ambao ukiwa nao utakulipa sana. kwa hiyo wekeza kwenye ujuzi huu. Na hapa ninaenda kutaja tu baadhi ya aina za ujuzi ambazo ukiwa nazo zitakupa

1. ujuzi wa kuwasiliana (sio kuongea)

2. ujuzi wa kunena (public speaking skill)

3. Ujuzi wa mauzo na masoko (marketing and selling skill)

4. ujuzi wa kuleta watu pamoja (people skill)

5. uongozi (leadership sikill)

6. ujuzi wa kuandika (copywriting skill)

Kwa kila ujuzi unaouona hapo, unaweza kujifunza na kuulewa vizuri tu, kama utaamua. Kama utahitaji msaaada wangu kwenye ujuzi wowote kati ya huo hapo tuwasiliane kwa whatsapp tu 0755848391.

 

Kama unavyoona rafiki yangu, hayo ndio maeneo muhimu ambapo unaweza kuwekeza ukiwa na miaka 20-29. Ila ni uhakika kwamba maeneo haya mwisho wa siku yatakuwa yenye manufaa makuwa kwako. ni juu yako sasa kuchagua eneo moja ambalo utaanza kufanyia kazi mara moja. kama mpaka sasa hivi hujui ni eneo gani unapaswa kuwekeza kwa kuanzia, basi anza na KUWEKEZA KWENYE KUJIFUNZA NA KUSOMA VITABU.

Mimi rafiki yako sina la ziada. Kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X