SIAFU: Viumbe Wadogo Akili Nyingi. Mambo 12 Ya Kujifunza


Wiki hii nimealikwa kufundisha kwenye kongamano la wanawake, jiandikishe na wewe uweze kuwepo

Moja ya viumbe ambao wanatafakarisha sana ni siafu. ni viumbe wadogo lakini wanafanya mambo makubwa. Leo hii nataka tuzame kwenye namna wanavyofanya kazi na masomo ambayo tunaweza kujifunza kwa viumbe hawa wadogo, viumbe wadogo wanaofanya makubwa.

1. Kufanya kazi, wanafanya kazi mpaka usiku. Viumbe hawa sijajua huwa wanalala saa ngapi, ila wanafanya kazi mchanana usiku.

Hiki ni kitu cha kwanza kabisa tunachojifunza kutoka kwa hawa viumbe, kufanya kazi. Unakuta mtu anafanya kazi kwa saa nane tu, anaangalia tamthiliya saa zingine nane na kulala. Lakini kama unataka kufanya makubwa lazima uwe tayari kufanya kazi zaidi ya hapo. Tumeona kwa mfano, mabilionea wengi wameripoti kufanya kazi kati ya saa 12 mpaka 16 na wachache mpaka saa 18 kwa siku. Yaani, huu ni muda ambao mtu anaweka kazi tu. Ukweli ni kuwa kama unataka kufanikiwa na kufanya makubwa ni wewe kufanya kazi kama wanavyofanya waliofanikiwa. Hii ni siri kubwa sana unayotakiwa kuifahamu. Vile vitu wanavyofanya watu waliofanikiwa, wewe fanya kama wao. Nakuhakikishia kitu kimoja cha ukweli kwamba, utaweza kwenda mbali. Na kama kuna kitu cha kwanza kabisa cha kuanza nacho, basi anza na kufanya kazi.

Mafunzo ya biashara na uchumi
Mafunzo ya biashara na uchumi na Ndugu Godius Rweyongeza

SOMA ZAIDI: KAMA UNATAKA KUFANIKIWA, KUBALI KULIPA GHARAMA

2. Wakiamua jambo lao hawashindwi. Sisi tuliokulia vijijini tunawajua, wanakuamsha hata kama ni saa 5 usiku au saa 9 kwa sababu umelala kwenye njia waliyoplan kupita. Hapo kumbuka umelala ndani, ila wanapenya na wanaingia na wanakuamsha.

Ninyi wengine mliokulia MJINI tupisheni, Unajua usingizi wa saa Tisa unavyonoga na hasa ukiwa mtoto, sasa muda ambao ndiyo umeanza kufurahia huo usingizi, siafu wanataka kupita na wewe unazingua umelala njiani kwao.  Unaonekana kikwazo, Na wao huwa hawana dogo, Kila jambo hata kama ni dogo wanalifanya kwa ustadi MKUBWA kama ambayo wangekuwa wanafanya kubwa. Kuna mtu eti unakuta anasema hii kazi siyo Ile ninayoipenda nifaifanya tu kwa sababu ya pesa, ikitokea kazi nzuri naacha naenda huko. Kajifunze kwa Hawa siafu.

Hawafanyi jambo lolote kwa udogo. Wakiamua ndiyo wameamua. Huwa hawana cha kurudi nyuma

3. Wakiamua jambo lao hawana Cha kuwazuia. Wanavuka mpaka mto wenye maji yanayotiririka kwa Kasi. Unaweza kwenda sehemu, maji yanaaptita kwa kasi ila waoa ndiyo wanavuka hapo bila stress. tayari wanajenga daraja lao na wanasonga mbele. Hiki kitu kinanikumbusha ule usemi wa Napolleon Hill unaosema kwamba lolote ambalo akili yako itaamua na kushikilia basi lazima italifikia. Kumbe na wewe ukiamua hakuna kinachoweza kukushinda. Inawezekana vizuri tu.

SOMA ZAIDI: Unataka kufanya vitu vya tofauti? Siri hii hapa

4. Wanapasiana taarifa kwa spidi kubwa. Ukiwaangalia siafu vizuri wakati wanaenda sehemu, kuna siafu ambao huwa wanaenda mbele na kuna ambao huwa wanarudi nyuma. Na hata ikitoea kwenye msafara wao ukawatibua kidodo, hawarudi nyuma wote, kuna wachache ambao huwa wanarudi nyuma kutoa taarifa kwa haraka kwamba huku kimenuka. Jiandae. Hili ni jambo muhimu sana la kuzingatia. Kwenye biasahra ili biashara yako iweze kwenda hatua ya ziada, lazima mawasiliano yawe ni ya hali ya juu, yawe ni ya haraka.

Kwenye mahusiano, ili yaweze kudumu, lazima mawasiliano yawe mazuri. Mawasiliano ni njia bora ya kufanya makubwa, kupeana taarifa za msingi. ni ufunguo muhimu wa jambo lolote la maana unalotaka kufanya.

SOMA ZAIDI: Jifunze Mawasiliano

5. Ushirikiano kwao ndiyo KITU kinachowafanya kuwa tishio. Mchwa mmoja kama mchwa mmoja Haogopeshi na hawezi kufanya MAAJABU, hawezi kuvuka mto, ila wakiwa wengi hata nyoka anasubiri. Hawana Ile ya kusema Mimi ni jeshi la mtu mmoja, ujue kwanza binafsi Huwa siwapendi watu wanaosema kwamba wao ni jeshi la mtu mmoja, kwa sababu ni vigumu kwa mtu yeyote kuwa jeshi la mmoja. Ni vigumu sana. Unajua kwa Nini. Ili uwe jeshi la mtu mmoja labda uwe unaishi kwenye kisiwa, iwe kwamba wewe unapika chakula Chako mwenyewe, unajisafirisha mwenyewe, unalima mwenyewe kwa mbegu ulizotengeneza mwenyewe.

Ukiona mtu anasema yeye ni jeshi la mtu mmoja ujue kabisa anajiamdalia njia ya kuangamia.

Kwanza hakunaga JESHI ambalo tena unaweza kusema ni la mtu mmoja. JESHI NI NI JUMLA YA WATU. Hivyo huwezi kusema wewe ni jeshi wakati uko peke Yako. Sharti muwe wengi.

SOMA ZAIDI: Dhana ya jeshi la mtu mmoja, je ni dhana halisi au tunahitaji kufikiri nje ya boksi?

6. Ukimchokoza mmoja umewachokoza WOTE. Kama walikuwa wanafanya kazi wataacha hiyo kazi wakushambulie kwanza, halafu watarudi kuendelea na kazi. Hawacheki na yeyote. Hapa tunajifunza kitu muhimu sana, USHIRIKIANO. Tunapofanya kazi, tufanye kazi kwa ushirikiano. Tuwe kitu kimoja, kauli ya mmoja wetu iwe ni kauli ya wote.

7. Hawana muda wa umbea. Haijalishi umewakasirisha kiasi Gani, wakishamaliza kukusambulia, hawakai kijiwemi na kunywa kahawa.  Wanaendelea na kazi yao ya mwanzo na kamwe hawajawahi kusahau kazi Yao.

8. Wanafanya kazi wanayopenda. Hili siwezi kulithibitisha sana, ila moyoni ninashawishika kusema hivyo, unajua kwa Nini…kwa sababu huwezi kufanya kazi usiyoipenda kwa muda mrefu hivyo tena kwa kujituma. Hili ni somo ambalo na sisi tunapaswa kuondoka nalo, kwamba, tupende tunachofanya. Mtu mmoja aliwahi kusema kwamba ukifanya kazi unayopenda hutahisi kama unafanya kazi kamwe. Naye Albert Einstein alisisitiza hili aliposema kwamba, ukikaa na msichana unayempenda kwa saa mbili, utadhani ni dakika mbili. Lakini ukikaa kwenye jiko la moto kwa dakika mbili, utadhani ni saa mbili.

Na mimi namalizia kwa kusema kwamba penda unachofanya.

SOMA ZAIDI: FANYA UNACHOPENDA

9. Kikwazo kwao ni njia. Huwezi kuwazuia siafu kwa kuwawekea kikwazo. Kwao kikwazo ni namna ya kusema kwamba endelea.  Kwenye maisha yetu ya kila siku pia tusiogope kikwazo. Ni ukweli usiopingika kwamba vikwazo vipo na vitaendelea kuwepo. Vikwazo kwetu isiwe changamoto, bali iwe ni njia. 

10. Hawasubiri kusimamiwa, hawana kiongozi ila kazi zao zinajulikana. Kama kuna kitu kikubwa sana cha kujifunza kutoka kwa hawa siafu ni utendaji kazi wao. Wana mfumo wao mzuri unaohahakikisha kwamba majukumu yao yanaendelea kufanyika na kukamilika. Hiki ni kitu muhimu sana kwenye maisha na hasa kwenye biasahra. Kwamba uwe na namna ya kufanikisha kila majukumu bila kujali kitu gani kinatokea. Bila kujali nani yupo au nani hayupo kwenye biashara. Unaweza kuwaua baadhi ya siafu, lakini hakuna jukumu lolote la msingi kwao ambalo linakwama.

Biashara yako inapaswa kuwa hivi. Iendelee kwenye hali zozote.

Lakini pia wewe uwe kiongozi mwenyewe na kila mmoja awe kiongozi. Ufanye kazi na watu wanaoweza kujisimamia wao, siyo wale ambao lazima wasimamiwe au uwe nyuma yao muda wote ili waweze kufanya kazi. 

SOMA ZAIDI: Usijilinganishe Na Wengine

11. Wanatunza akiba. Hawajisahau. kuna wakati siafu huwa hawaonekani. Wakati wa mvua sana, au wakati wa jua kali. Wanajichimbia wanapojua wao wakila na kunywa. Kitu kikubwa tunachokiona kutoka kwao ni KUWEKA AKIBA. Wanaweka akiba mara zote wakati wa mavuno, sisi pia tuendelee kuweka akiba mara zote.

SOMA ZAIDI: MAMBO MUHIMU KUHUSU KUWEKA AKIBA

12. Ukizubaa umekwisha. Siafu hawana dogo, hata kaka kazi Yao ni ndogo, ila lazima waifanye kwa UKUBWA. Kuna walevi walikaa kwenye njia zake kesho yake wakakutwa wamekufa, maana Hawa wadudu hawana dogo au kama nilivyosema mwanzoni hawacheki yeyote.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza

Jipatie vitabu vya Godius Rweyongeza kwa kuchagua HAPA.

Wasiliana nami wasap hapa

Hakikisha umepata kitabu cha RASILIMALI ZA WATU WENGINE, ni kitabu kizuri kwa ajili yako. wasiliana na 0755848391 au 0745848395 sasa

Makala ya kesho itawekwa kwenye blogu ya SONGAMBELE ambayo unaweza kuifikia kupitia www.songambele.co.tz na itawekwa kwenye channel ya telegram pia ambayo unaweza kuifikia kwa KUBONYEZA HAPA

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X