Home


  • Kitu kibaya zaidi ya kutokuwa na macho ya kuona (utashangaa kusoma kitu hiki cha kipekee).

    Hellen Keller (1880-1968)  alikuwa mwandishi, mwanasiasa na Mwalimu wa chuo. Kwa miaka hiyo alikuwa ni kipofu wa kwanza kupata shahada ya Chuo kikuu. Siku moja alitoa hotuba moja ambayo iligusa maisha ya watu. Baada ya hotuba hiyo waandishi walikusanyika ili kumuuliza maswali ya hapa na pale. Wakati maswali yanaendelea kuulizwa alijitoleza kijana mmoja ambaye alisafisha koo na kusogea mbele  kidogo. Kijana huyu alikuwa ameitafuta nafasi hii kwa muda mrefu  na isitoshe alikuwa mchanga kwenye ulimwengu wa habari. Aliuliza, “kitu gani ni kibaya zaidi katika maisha zaidi ya kuwa kipofu”.
    Mara ghafla sauti ya miguno zikaanza kusikika. Mtu mmoja kwenye kundi la watu akasikika akisema, swali gani hilo achana nalo usilijibu. Mwingine akasema swali hilo linadhalilisha achana nalo.

    Lakini hali haikuwa hivyo kwa Hellen Keller. Alionekana kulipenda swali na hivyo aliwaashiria watu watulie ili aweze kujibu hilo swali. Alisema, “kitu kibaya zaidi katika maisha ni kuwa na macho bila ya kuwa na maono/ndoto”.
    Akamaliza.

    Unajua nini? Kuna watu walifikiri  kitu kibaya zaidi ya kuona kitakuwa labda ulemavu wa mikono au miguu. Ila alisema maono au ndoto ndio kitu kibaya zaidi.

    Swali kama hilo lingeulizwa kwa vijana wa zama  hizi  basi ungeshangaa. Kuna ambao wangesema kitu kibaya zaidi ni kutokuwa na mtaji wa kuanzisha biashafa, wengine wangesema kitu kibaya zaidi ya kukosa msaada wa serikali, wengine wangesema kitu kibaya zaidi ni kukosa elimu.

    Tunachojifunza kwa Hellen Keller ni kwamba maono ni mwongozo wa maisha.  Mtu mmoja amewahi kusisitiza kwa kusema kuwa, maono au ndoto sio zile unazoota ukiwa umelala. Bali ni kile kitu ambacho unakiona na kukiendea hata kama umefumba macho. Tena wataalam wanasema ndoto zako zinapaswa kuwa kubwa zaidi kiasi cha kukuogopesa hata wewe. Ndoto kubwa ziyakufanya
    1. Upate nguvu ya kusonga mbele hata pale mambo yanapokuwa ni magumu maishani mwako au unapokutana na changamoto

    2. Zitakufanya upangilie muda wako kwa vipaumbele.

    3. Zitakufanya utengeneze konekisheni za maana na kwa wakati.

    4. Zitakufanya ubaki ukiwa na motisha ya kufanya makubwa kwa wakati wote.

    Je, wewe ndoto zako kubwa ni zipi?

    Umekuwa nami,
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

  • Imethibitishwa. Mbinu Za Kitabibu Zinafaa Kutumika Katika Maisha Ya Kawaida Ya Kila Siku

    Hongera sana rafiki kwa kuiona siku hii ya leo. Ikiwa ni tarehe 29 August
    Ukienda hospitali unaumwa utataja tatizo lako kwa mtaalamu wa Afya. Mtaalamu huyu wa Afya kwa kutumia ubobezi wake atakupima au atakusikiliza tu na kisha kutoa dawa. 
    Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa wataalamu wa afya wa hospitalini ila kwa leo napenda tuyajue haya mawili ambayo yamethibitika kufanya kazi kwenye maisha ya kawaida.
    Kinapatikana kwa sh. 10,000/-
    KWANZA, mtaalam wa Afya atakupa dawa kulingana na ugonjwa wako. Haijalishi unaipenda au huipendi. Haijalishi unampenda yeye au humpendi yeye. Ile dawa unapaswa kuitumia. 
    Sasa kwenye maisha ya kila siku. Imethibitika kwamba ukweli wa jambo fulani ukitolewa. Haijalishi unaupenda au huupendi. Haijalishi unampenda aliyeutoa au hupendi aliyeutoa ukweli unabaki kuwa ukweli tu. Na huna budi kuufuata. Hivyo jitahidi kuanzia leo kuuchukua ukweli na kuufanyia kazi bila kujali umetolewa na mtu aliye juu ya wewe au aliyechini. Ukweli unabaki kuwa ukweli siku zote.
    Mfano wa ukweli ambao utapaswa kuukubali ni huu hapa.
    Huwezi kutatua matatizo kwa namna ile ile ya kufikiri iliyosababisha matatizo.
    Huwezi kuondoka kwenye madeni kama utaendelea na fikra zilezile ulizokuwa nazo wakati wa kukopa. Huu ni ukweli. Na hivyo utapaswa kuchukua hatua za tofauti ili uweze kuondokana na madeni.
    Kama fikra zako zilikuwa kwamba madeni katika maisha hayaepukiki, basi sasa unapaswa kufahamu kwamba madeni ni utumwa. Ukianza kuyaona madeni kama utumwa ujue kwamba umetokea kuona vitu kwa namna ya tofauti ambayo ulikuwa hujaitumia hapo awali.
    PILI; Mtaalamu wa afya akishagundua kwamba una ugonjwa fulani atakupa dawa ambazo utazitumia kwa maelekezo yake. Anaweza kukupa maelekezo kwamba utumie hizo dawa mara tatu kwa siku. Au utumie dawa hizo mara mbili kwa siku. Kama kweli upo makini na afya yako basi utafuata maelekezo ya daktari bila kipingamizi ili uweze kupona.
    Sasa imethibitishwa kwamba kuna dozi unahitaji ili uweze kufanya mambo ya tofauti.
    1. Dozi ya kusoma vitabu mara tatu kwa siku. Kama kwa siku unaweza kupata muda wa kula mara tatu mfululizo bila kuacha sasa unashindwa nini kusoma vitabu mara tatu mfululizo. Soma vitabu asubuhi, mchana na jioni kama vile umepewa dozi kutoka kwa mtaalamu wa afya.
    2. Fuata maelekezo mpaka upone. Hakuna daktari anayekwambia tumiatumia hii dozi ukijisikia kupona achana nayo. Sharti ni kwamba dozi lazima iishe. Vivyo hivyo kwako. Ukitaka kupata matokeo ya tofauti sharti lazima ukubali kulipa gharama na kuvumilia mpaka mwisho.
    Hizo ndizo mbinu za kitabibu zilizothibitishwa kufanya kazi kwenye maisha ya kawaida.  
    KUMBUKA: utapaswa kuupokea ukweli kama ulivyo na kuufanyia kazi, lakini pia utapaswa kufanyia ukweli huo mwanzo mpaka mwisho. 
    Jiunge nami kwenye kundi la THINK BIG FOR AFRICA ili tuambizane ukweli na kuchukua hatua kila siku.
    Umekuwa nami,
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

  • Hili Ni Jina Ambalo Unapaswa Kuacha Kulazimisha Kujiita

    Siku hizi kumekuwepo na watu wengi ambao wanajiita wajasiliamali. Uwepo wa mitandao ya kijamii pia umerahisisha hili kwa kufanya watu wengi waandike kwenye akaunti zao kwamba wao ni wajasiliamali. Pengine utakuta mtu anajitambulisha kwa watu kwamba yeye ni mjasiliamali. Yaani ujasiliamali umekuwa kama cheo vile. Kama vile watu wanavyoitwa daktari, mwalimu, waziri n.k Sasa pia inaelekea kuna cheo kipya cha mjasiliamali.

     Sasa labda tujiulize ni sahihi kujitambulisha kwa watu kwamba wewe ni mjasiliamali?
    Kabla ya kujibu hili swali tujiulize, labda ujasiliamali ni nini? Ujasiliamali ni ile hali ya kutatua matatizo ya watu (hii ndio maana ya mjasiliamali kama ilivyo kwenye Kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI). Na ukiangalia wajasiliamali ambao wamewahi kugusa maisha ya watu hapa duniani hawakuwahi kujiita wajasiliamali. Fuatilia watu kama Thomas Edison, Henry Ford, Andrew Carnegie, Steve Jobs, John Rockefeller na wengineo wengi. Kamwe watu hawa hawakuwahi kujiita wajasiliamali Bali walichofanya ni kuuishi ujasiliamali, hivyo tu. Walitatua matatizo ya watu  na kusongambele.

    Soma Zaidi: Vitu Vinne Vinavyowafanya Waajiriwa Kuendelea Kuajiriwa

    Sasa ngoja turudi kwenye swali na tujiulize. Je, ni sahihi kujiita mjasiliamali. Jibu ni kwamba Sio sahihi. Weka nguvu kubwa sana katika kutenda zaidi kuliko kushawishi watu wakuone wewe kama mjasiliamali. Badala ya kutumia muda mwingi kushawishi watu kwamba wewe ni mjasiliamali, waoneshe watu kwamba wewe ni mjasiliamali.

    Asante sana. Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

    Umekuwa nami,
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

  • Kitu Muhimu Unachopaswa Kurekebisha Kwenye Biashara Yako

    Ni siku nyingine bora sana rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii ya leo.

    Katika biashara kuna mambo mengi sana ambayo unaweza kufanya. Kutunza kumbukumbu, kutafuta wateja wapya, kuuza, kutafuta watu wa kuajiri na mengine mengi. Leo hii napenda nikwambie kitu kimoja muhimu sana ambacho unapaswa kukijua kuhusu biashara yako. Na kitu hiki sio kingine bali ni ukweli kwamba biashara yako inahitaji ukaribu wako.
    Kama biashara yako inaanza itahitaji uilee na kuikuza kama mtoto.
    Kama tayari imekua biashara yako itahitaji kupanuka zaidi, kuongeza mauzo na kusimamiwa kwa umakini zaidi.

    Kama unavyoona katika kila hatua ya ukuaji wa biashara yako, uangalizi ni jambo la muhimu sana. Jitahidi sana kuhakikisha unakuwa karibu na biashara yako muda wote. Ijue nje ndani bila kuacha kitu.
    Hili ndilo jambo muhimu unalopaswa kulifahamu kuhusu biashara yako.

    Asante sana rafiki yangu. Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio

    Umekuwa nami,
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

  • Haya Ni Mambo Mawili Ambayo Nategema Kutoka Kwako

    Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana kwa zawadi ya siku hii njema ya leo. Kwa siku Sasa nimekuwa nakushirkisha maarifa ya kukuinua ili ufikie kwenye viwango vya juu kupitia kwenye blogu hii hapa. Leo hii ningependa uyajue mambo mawili ambayo nayategemea kutoka kwako.

    1. Kufanyia kazi kile ambacho unajifunza  kwenye blogu hii.
    2. Kumshirikisha walau mtu mmoja kile unachojifunza. Jambo hili litakusaidia wewe utakapokuwa umefima kileleni, huku Nyuma hakutakuwepo na watu wa kukuvuta na kurudisha nyuma. Maana watu wako wote wa karibu utakuwa umewapa maarifa na wao wameinuka.

    Umekuwa nami,
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

  • Hii Ni Kauli Ya Kishujaa Ambayo Unaweza Kuisema Unapokuwa Umekwama Na Watu Wanaonekana Kwenda Kinyume Chako

    Watu wenye ndoto kubwa sana huwa wanafika sehemu ambapo wanakwama kabisa na hali huwa inaonekana kwenda kunyume na matarajio yao. Hapo ndipo watu waliokuwa wakiwaamini tangu mwanzo huanza kuonesha mashaka na pengine kutaka kuwakimbia.  Kiukweli ni kipindi kigumu ambacho watu hawa hupitia ila kwa sababu wana ndoto kubwa wanavumilia na hatimaye kwenda wanapotaka.

    Hiki ndicho kilimtokea Steve Jobs, mwanzoni mwa miaka ya tisini. Kampuni yake ya NEXT ilikuwa inaanguka vibaya sana na kila mtu alipoteza ile imani aliyokuwa nayo kwa Steve Jobs. Hata wale waanzilishi wa kampuni walimkimbia. Wafanyakazi wengine walikimbia na kuanza kuona kama mtu ambaye amepoteza mwelekeo na mtu ambaye hataweza kufanya makubwa tena maishani.
    Hapo ndipo Steve Jobs alisimama wima na kuwaambia wafanyakazi wa wawekezaji na waanzilishi wengine wa kampuni. Alisema, “kila mtu anaweza kuondoka hapa isipokuwa mimi tu”.
    Hii ni kauli ya kishujaa unapokuwa unaendea ndoto zako. Hii ni kauli ambayo itaonesha bado unaamini katika ndoto zako na unaweza kwenda mbali zaidi. Kauli hii itaongeza nguvu na kuwafanya hata wale waliokuwa wanataka kukukimbia basi wajihoji na kurudi nyuma kidogo.

    Hali kama hiyo iliyomtokea Steve Jobs imewahi pia kutokea Jack Ma mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kampumi yake ilikuwa inaonekana kama inakufa na haikuwa na mwelekeo mzuri. Jack Ma alisimama wima na kusema,
    Ambaye anaona kampuni inakuga aondoke.
    Ambaye amesubiri kampuni ipelekwe IPO ili apate pesa aondoke.
    Ambaye anakuja hapa kufanya kazi bila kuwa na imani na kampuni aondoke.
    Ambaye hapendi kazi anayoifanya aondoke.

    Kwani unadhani kuna aliyeondoka? Watu wote ilibidi wakae maana shujaa wao alishaonesha anaamini kile anachofanya na atakipigania mpaka mwisho.
    Kauli hizi zimetolewa na watu tofauti ila maana yake bado ni ile ile.

    Kwa hiyo na wewe unaweza kuchagua mojawapo na kuitumia au ukatumia zote kwa wakati mmoja. Ni hivyo tu rafiki yangu.

    Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

    Asante.

     Kama bado hujajiunga na mfumo wetu wa kutokea Makala maalum kwa watu maalum BONYEZA HAPA
    Umekuwa nami,
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

  • Ungekuwa Wewe Ungefanyaje?

    Hivi kama wewe ndio mteja na hiyo biashara unayofanya Sasa hivi inamilikiwa na mtu mwingine ungeenda kweli kununua hapo? Je, kitu gani kingekufanya ukanunue. Je, kama wewe ungekuwa mwajiri na na kazi unaoifanya inafanywa na mtu mwingine. Je, ungeendelea kumbakiza kwa utendaji huo? Kwa nini?

    Hivi kama wewe ungekuwa tayari umefikia ndoto zako zoote za maisha ungefanyaje? Je, ungekuwa unafanya unachofanya sasa hivi?
    Je, kama wewe ungekuwa ndiwe mtu bora zaidi katika kazi unayofanya Sasa hivi duniani, ungekuwa unafanya nini?

    Hili ni swali muhimu sana kujiuliza rafiki yangu. Linakupa majibu ambayo kama utayafanyia kazi basi hutabaki kama ulivyokuwa hapo awali. Badala yake unapiga hatua. Kwa hiyo mara kwa mara jiulize. Ningekuwa Mimi ningefanyaje?
    Kama  utapata jibu ambalo linakuhitaji urekebishe. Rekebisha mara moja ili uweze kusonga mbele.

    Asante sana.

    Umekuwa nami,
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

  • Kiu Muhimu Unachopaswa Kujifunza Na Kuvifahamu Kiundani

    Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii njema sana. Leo imekuwa siku bora sana kwetu, ni siku ya kipekee sana ambayo unapaswa kuitumia kufanya kitu ambacho kitabadili maisha yako na kukufanya usonge mbele.

    Kuna kitu kimoja tu ambacho unapaswa kukifahamu haswa na unapaswa kukifahamu kiundani. Na kitu hiki ni MAUZO.
    Kila mtu katika maisha huuza. Iwe ni mtoto au mtu mzima. Iwe ni amesmomea kuuza au hajasomea. Ila kila mtu anauza.

    Iko hivi unapoongea na mtu ukijaribu kumshawishi akubari kile unachomwambia ujue unauza mawazo yako.
    Kama wewe ni mwanasiasa unashawishi watu wakupigie kura ujue kwamba upo unauza Sera.
    Kama wewe ni mrumishi unahubiri neno la Mungu, ujue upo unauza.
    Hata kama unamshauri mtu afanye mabaya bado wewe unauza
    Kama wewe ni Mwalimu unafundisha   wanafunzi waelewe na wafaulu mitihani, jua kwamba unauza.
    Kama wewe huna kazi unatembea na vyeti kutafuta kazi jua kwamba upo unauza kisomo chako ili ukubariwe na kupewa kazi.
    Kama wewe ni unatafuta mchumba na ungependa akukubalie basi jua kuna kitu unauza.

    Naamini, mpaka hapo ushaelewa ni kuuza ni nini!
    Kwa hiyo kuanzia leo jifunze, jifunze jifunze kuuza.

    Kwa siku Chache zijazo, tutaendelea kujifunza juu ya suala zima la kuuza na kwa jinsi gani litakusaidia kufikia makubwa.

    Umekuwa nami,
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

  • Watanzania Tujenge Utaratibu Wa Kukubali Vitu Vyetu.

    Juzi nilikuwa kwenye daladala nasoma Kitabu cha  JINSI YA KUTOKA UMASIKINI MPAKA MAFANIKIO cha Erick Shigongo. Mara alijitokeza jamaa ambaye alikuja kukaa pembeni mwangu. Baada ya kuwa amekaa na kutulia, jamaa akawa ameona Kitabu nilichokuwa nasoma. Akaniomba akione. Sikuwa mchoyo, nikampa. Baada ya muda akanirudishia Kitabu changu.  Nikakawa nasikiliza kwa umakini ili nisikie atakachosema. Ila jamaa alikaa kimya.

    Baadae nilimuuliza ili nijue kitu gani kilimvutia kuniomba Kitabu na pia nilitaka kujua kama huwa anasoma Vitabu. Nilichokisikia ni mshangao mtupu!

    Jamaa: “mimi huwa nasoma ila sisomi vitabu vya kitanzania”!
    Mimi: “Eh kwa nini”? Niliuliza kwa mshangao!

    Jamaa: “Kwa sababu watanzania wengi wanakopi na hawajui kuandika”

    Nilicheka kimoyomoyo. Nikamuuliza ebu niambie Vivtabu gani vya kiingereza ambavyo umewahi kusoma! Jamaa akaanza kujing’atang’ata. Alikuwa hata haelewi Kitabu gani. Baada ya muda akawa kama amekumbuka kitu. Akasema “kitabu cha Ben Carson ila sikumbuki kichwa chake”. Alisema.

    Kwa upande wangu sikushangaa kumsikia mtu huyu anasema kwamba watanzania hawajui kuandika. Sikushangaa kabisaaa! Maana ni kawaida ya watanzania wengi kuvikataa vitu vyetu ambavyo tunavyo.

    Sikushangaa maana hata kuna asilimia kubwa sana ya watanzania wanaikataa ligi kuu ya Tanzania kwa kisingizio kwamba wanapenda ligi ya ulaya.
    Sikushangaa pia kwa sababu kuna watanzania wanasema wapo bongo kwa bahati mbaya.
    Sikushangaa kwa sababu kuna watanzania wanasema bora wangezaliwa kama mbwa ulaya.
    Sikushangaa maana kuna watanzania wanakataa kununua bidhaa zilizozalishwa Tanzania na kukimbilia za nchi nyijgine

    Kwa hiyo nilijua kwa hakika huyu naye ni mmoja kati ya hao watu.

    Nipende tu kusema kwamba watanzania tujenge utaratibu wa kupenda vitu vyetu. Binafsi kwa upande wa vitabu ninapenda zaidi vitabu vya kitanzania kuliko vitabu vilivyoandikwa na mtu wa nchi nyingine.

    Nipende tu kusema kwamba watanzania tujenge utaratibu wa kupenda vitu vyetu.

    Tupende tulipozaliwa maana kuna kusudi maalumu la sisi kuzaliwa tulupozaliwa leo.

    Wahenga wanasema mtu kwao.  Tafadhali sana, jijengee utaratibu huu.

    Nakushukuru sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

     Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

    Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

    kila la kheri

    Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391



  • Kitu Hiki kitatokea Pale Utakaposema Haiwezekani

    Hivi umewahi kufanya jambo na kuona haiwezekani. Au umewahi kufanya jambo na kuishia njiani? Shida ilikuwa nini?

    Inawezekana ulisema haiwezekani na ukaamua kuishia njiani. Ukweli ni kwamba hakuna kitu ambacho hakiwezekani ukiamua. Kila kitu kinawezekana.

    Ila pale unaposema kwamba haiwezekani unakuwa unajiwekea kizuizi cha kusongambele na kufikia viwango vikubwa.

    Sasa kinachotokea ni kwamba utakwama na kutulia. Wakati unaendelea na mkwamo wako utashangaa watu wasiojiwekea vikwazo akilini wanatimiza kile ulichosema  hakiwezekani. Kwa hiyo nipende tu kusema kwamba hakuna kisichowezekana. Kila kitu kinawezekana kama utaamua. Kama bado hujajiunga na mfumo wetu wa kutokea Makala maalum kwa watu maalum BONYEZA HAPA

    Umekuwa nami,
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

X