-
Mambo Matano (05) Usiyoyajua Kuhusu Fursa
Mara kwa mara ukiskiliza vyombo vya habari utagundua kwamba waafrika walio wengi wanahama na kusafiri kwenda nje ya bara la afrika na haswa ulaya ili kutafuta fursa. Wakati huohuo watu ambao sisi tunawaita wawekezaji wanatoka ulaya kuja Afrika kutafuta fursa pia.
Sasa labda swali linabaki fursa zipo wapi? Zipo ulaya au Afrika?
Je, wote tuhame twende ulaya kutafuta fursa?Leo hii nimekuandalia mambo machache kuhusu fursa ambayo ningependa uyafamu. Kabla sijaanza kukueleza mambo haya naomba kama bado hujajiunga na mfumo wetu wa kutokea Makala kwa email BONYEZA HAPA ili usipitwe.
Moja, fursa zipo kila sehemu. Ni wajibu wako kuangalia kwa jicho la kipekee namna gani unaweza kukamata fursa na kusongambele.
Pili, fursa ni kama daladla ikikupita moja nyuma inakuwepo nyingine ambayo inafuata.
Tatu, sehemu yenye matatizo mengi ndio sehemu yenye fursa kubwa. Afrika kuna matatizo mengi, hivyo fursa za kibiashara ni kubwa afrika kuliko ulaya
Nne, usikimbizane na kila fursa. Uwe makini na fursa ambazo utaamua kufanya na zipi utaachana nazo, yaani ambazo hutafanya. Sio kila fursa inakufaa
Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Huyu Ni Mtu Ambaye Unapaswa Kumfahamu Nje Ndani
Mara nyingi sana huwa tunajihusisha na vitu vingi sana. Unakuta mtu anafuatilia vitu vingi, kuanzia taarifa ya habari, kuangalia tamthiliya kufuatilia maisha ya watu mtandaoni na mambo mengine kadha wa kadha. Ila kuna mtu ambaye huwa unamsahau kumfuatilia kila siku. Na mtu huyu siye mwingine Bali wewe hapo. Yaani kabla hujafuatilia habari zilizotokea Darfur, au Kabla hujajua Trump kaongea nini. Unapaswa kuwa umejifahamu wewe kwanza.
Fahamu ni hatua gani umeweza kupiga. Ulikuwa wapi na wapi unataka kuelekea na ni vitu gani vinakukwamisha. Hivyo tu basi.Kwa hiyo kuanzia leo, anza kujifanyia tathimini wewe mwenyewe ili ujue wapi upo na wapi unapaswa kwenda ili kuweza kufikia ndoto zako kubwa.
Asante sana rafiki tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.
Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Hakuna Mafanikio Bila Kujitoa Sadaka
Hakuwezi kuwepo naafanikio makubwa bila ya mtu kujitoa sadaka nankuachana na vile vitu ambavyo anavipenda kwa muda ili aweze kupata mafanikio makubwa baadae.
Unapaswa kujitoa sadaka kwa kuachana na mawazo hasi na kuweka nguvu zako na muda wako kayika kufanya mambo ya maana. kama utawekabngugu zako na muda wako katika kufanya mambo ya maana, hamna jinsi lazima tu utaweza kufanikiwa. Mafanikio lazima yatakuja kama utaamua kuachana na vitu vidogo ambavyo havina maana.
Eric Shigongo James ameandika katika Kitabu chake kwamba, kuna watu kwa sababu ya tabia zao umasikini utaendelea kuwaandama tu na kuna watu kwa sababu tabia hata waukimbie utajiri utawafuata tu.
Unajua moja ya kitu kinachowafanya watu wafanikiwe na kuwa Matajiri ni kipi?
Ni kujitoa sadaka1. Wanajitoa sadaka kwa kusoma Vitabu
2. Wanajitoa sadaka ya kuweka akiba
3. Wanajitoa sadaka ya kuachana na taarifa za habari na magazeti
4. Wanajitoa sadaka kwa kuachana na mahusiano ambayo sio mazuri
5. Wanajitoa sadaka kwa kula Chakula bora
6. Wanajitoa sadaka kwa kuamka mapema
7. Wanajitoa sadaka kwa kuamua kufuatilia mambo yao na kuachana na mambo ya watu wengine.Je, wewe upo tayari kujitoa sadaka kwa kufanya nini?
Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Moyo wako Uko wapi?
“Fanya unachopenda” ni usemi ambao umekuwa unatumiwa kuwashauri watu ili waweze kufanya kitu cha kitofauti na kipekee sana.
Jambo hili ni la kweli ndio maana siku ya leo ningependa kutilia mkazo na kusisitiza kitu hiki kwa herufi kubwa.Watu wengi waliofanya makubwa katika sekta zao ni wale ambao walikuwa wanapenda kile wanachofanya. Na walikifanya kwa moyo na kujitoa.
Ukifanya kitu kwa moyo na upendo wako wote utaweza kukifanya kwa viwango vikubwa. Steve Jobs alikuwa na mapenzi na kompyuta, alijituma na alihakikisha anafanya kitu cha tofauti katika kila kitu ambacho alifanya.
Unajua kwa nini alikuwa anafanya hivi? Kwa sababu alikuwa anapenda kile anachofanya. Inawezekana Jobs alikuwa hahisi kama vile anafanya kazi. Mtu mmoja amewahi kusema kwamba unapofanya kile unapenda hutahisi kama kufanya kazi.
Inashauriwa kama Sasa hivi upo eneo ambalo halikufurahisi basi utapaswa kufanya mambo mawili,
1. Kuachana na unachofanya na kuanza kufanya kitu kingine unachopenda au
2. Kupenda unachofanya na kukifanya kwa bidii na moyo wote.Kazi ya kufanya leo. Jiulize Je, kwa sasa ninafanya kile ninachopenda?
Pili jiulize ni kitu gani ninapenda kufanya?
Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPAHakikisha umesubscribe kwenye YouTube Channel Yangu Ya Youtube Kwa Kubonyeza Hapa -
Mambo 25 Niliyojifunza Ndani Ya Miaka 25 Ya Kuishi Kwangu Hapa Duniani
Mwaka 1994, tarehe 5/8 ilikuwa ni siku ambayo kwa mara ya kwanza nilizaliwa na kuvuta pumzi ya kwanza ya dunia hii. Na leo hii ndipo naadhimisha miaka 25 ya kuzaliwa kwangu. Niseme kwamba hii ni siku muhimu ambayo imenifanya niweze kuona mengi, kukutana na watu wengi na kuzunguka maeneneo mengi.
Miaka yangu ishirini na tano ya kwanza nimeitumia nikiwa shuleni. Kwa hiyo kitu kikubwa sana ambacho nimekifanya ndani ya miaka hii ni shule tu basi. Sasa. Ndani ya miaka hii katika kusoma vitabu, kukutana na watu, kuongea na watu, kutembelea maeneo na kufanya vitu vingi sana nimepata kujifunza mambo ishirini na tano. Mambo haya ni muhimu sana kwangu, lakini pia wewe yataweza kukusaidia kufikia hatua kubwa.
1. Kila mtu amezaliwa na mbegu ya ubunifu ambayo ipo ndani yake. Kama ilivyo kwa mbegu ya kawaida inahitaji maji, hewa na jotoridi ili iweze kuota. Vivyo hivyo kwa mbegu ya ubunifu ambayo mimi na wewe tunayo, mbegu hii inahitaji kukuzwa kwa kuwekewa mazingira safi ambayo yataifanya iweze kuota kwa ubora zaidi, na mazingira haya ni kama kuipa muda wa kukua, kufanya mazoezi, na kujituma.
2. Muda mzuri sana wa wewe kuanza kufanya kitu ni pale ambapo unapata wazo. Ukipata wazo liweke katika matendo na anza kulifanyia kazi mara moja. Huhitaji kusubiri kila kitu kiwe sawa.
3. Eneo lenye matatizo makubwa ni eneo ambalo lina fursa nyingi. Kitu kikubwa ambacho unahitaji ni kuhakikisha kwamba unatatua changamoto ambazo zinaikumba jamii yako.
4. Unapokuwa kijana, huku ukiwa na nguvu nyingi, unakuwa ndio muda mzuri kwako kujaribu kufanya mambo mengi sana bila kuogopa. Jaribu vitu vingi kadri uwezavyo na vile vinavyofanya kazi endana navyo wakati vile ambavyo havifanyi kazi unaachana navyo.
5. Uoga ni kitu ambacho unakijenga wewe mwenyewe kwenye akili yako ila kiukweli ni kwamba hakina uhalisia. Hivyo usioogope kitu au mtu yeyote. Watu ambao unawaogopa wewe, wanakuogopa na wewe pia.
6. Ukweli ni kwamba hata yule au watu wale ambao wewe unawaogoopa na wao wanakuogopa wewe.
7. Kila mtu ni kiongozi katika maisha bila kujali cheo chake. Uongozi hauhitaji kuwa na cheo. Ila unahitaji wewe kupumua tu. Kuna vitu ambavyo unapaswa kuvifanyya hata kama hauna cheo na unapaswa kuvifanya kwa weredi mkubwa sana. Yawezekana wewe ni karani eneo fulani na hauna cheo ila ukiifanyakazi yako kwa ubora utakuwa umetimiza majukumu yako kama kiongozi. Wewe kama kiongozi unahitaji kuhakikisha kwamba kila kitu ambacho unakigusa unakifanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Huhitaji cheo ili kutumia kipaji chako. Huhitaji cheo ili kutatua matatizo yanayoikumba jamii yako.
8. Haijalishi umeanzia wapi kwenye maisha, una uwezo wa kutengeneza kesho bora kuanzia hapo ulipo na hatimaye kufikia hatua kubwa maishani. Kikubwa ambacho unapaswa kufahamu ni kwamba unapaswa kuanza na kile ulichonacho, kufanya kile ambacho kinawezekana ili hatimaye uweze kufanya kile ambacho wengine wanaona kwamba hakiwezekani kufanyika maishani.
Kuna watu walikuwa ni walinzi wa kampuni zao ila kwa kutumia hiyo fursa tu wamefikia hadi hatua ya kununua kampuni ambazo walikuwa wanafanya ulinzi hapo,
10. Fursa zipo kila mahali unapoenda. Na fursa zinakija kila wakati. Usifanye vitu kwa kukimbiakimbia bila mpango. Na fursa fulani ikikupita usihuzunike. Kumbuka kwamba fursa ni kama daladala, likikupita moja litakuja jingine ambalo utapanda.
11. Usiipe nafasi chuki kwenye maisha yako. Kama mtu atakukosea msamehe,usikae na chuki unajiukiza mwenyewe.
12. Ukimkumbuka mtu mjulie hali, ukimpenda mtu mwambie, mtu akikukosea msamehe maisha ni mafupi sana kwako kupoteza kwa mambo yasiyo na maana
13. Ni bora kuomba msamaha kuliko kuomba ruhusa. Mara nyingi unapokuwa unaanza kufanya kitu ambacho unacho kwenye ndoto zako kubwa, kuna watu watakuona kama umekengeka. Wapo watakaokukataza usifany kile ambacho unakifanya na wapo pia ambao watakucheka. Usiwasikiilize watu wa namna hii. Wewe fanya kitu ambacho unajua kabisa kwamba ni sahihi na hakivunji sheria za nchi. Kikifanikiwa kila mtu atafurahi sana ila kikikataa utaomba msamaha na kuendelea na kitu kingine. Kwa hiyo fahamu kwamba ni bora kuomba mshamaha kuliko kuomba ruhusa
14. Hakuna mtu anayeona unapoona wewe. Iwe ni mzazi, ndugu au jamaa. Kama wewe una ndoto kubwa sana usiwasilikilize watu. Kazana kutimiza ndoto zako.
15. Kuna vitu viwili muhimu sana ambavyo unapaswa kuvifanya maishani wako. Moja ni kupanda miti pili ni kuandika Kitabu. Kama utakosa kufanya vitu vingine vyote, basi fanya hivi.
16. Unapokuwa unafanya kazi au unatimiza majukumu fulani na ukaanza kujisikia kuchoka, ukweli ni kwamba unakuwa hujachokka bali hapo ndipo unapaswa kuanza kuhesabu moja na kuanza upya. Imethibitishwa kwamba unapojisikia kuchoka unakuwa umetumia asilimia 40 tu ya uwezo wako na unapaswa kujisukuma zaidi ili uweze kutumia asilimia 10 au 20 zaidi ili uweze kufanya mambo makubwa
17. Vitabu vina suluhisho la kila kitu ambacho wewe unakifahamu. Na watu wakubwa wote ambao unawafahamu walikuwa ni watu wa kusoma vitabu siku zote. Ukiona mtu amefanikiwa jiulize anaasoma vitabu gani ambavyo mimi hapa sisomi. Ukisoma vitabu vya watu waliofanikiwa na wewe lazima utafanikiwa tu.
18. Sikiliza zaidi unavyoongea. Umeumbwa na masikio mawili na mdomo mmoja. Unapaswa kuwa mtu wa kusikiliza zaidi kuliko unavyoongea. Na katika suala hili utahitaji kutumia kanuni ya 60-40. Ambapo kanuni hii inasema kwamba unapaswa kuwa msikilizaji zaidi ya unavyokuwa muongeaji. Yaani unapaswa kutumia asilimia 60 ya muda wako kusikiliza na asilimia 40 tu katika kuongea
19. Inawezekana kuishi bila kuangalia runinga wala kusikiliza redio. Na jambo hili nimeweza kulifanyia kazi na kuliishi kwa miaka mitatu iliyopita. Sijawahi kusikiliza runinga wala sina muda wa kusikiliza redio. Cha kushangaza ni kwamba sijawahi kukosa kitu chochote cha maana.
20. Usisubiri connection ili uanze. Tengeneza connection wewe mwenyewe.
21. Usilalamike. Usimlalamikie mzazi serikali au taasisi yotote. Kama kuna kitu hakifanyiki vizuri, tatizo ni wewe. Kama kuna kitu kinafanyika kwa ubora zaidi ni wewe umesababisha pia. Kumbuka, ukishinda ni juu yako. Ukishindwa pia ni juu yako.
22. Mtandao wa watu waliokuzunguka unaweza kukusukuma kufikia mafanikio au kushindwa kabisa. Kwa hiyo unapaswa kuwa makini sana unapochagua aina ya marafiki unaopaswa kuwa nao na kukuzunguka. Wanasema hivi, niambie rafiki yako nikwamhie tabia zako. Kuwa makini na marafiki unaochagua kuwa nao maishani.
23. Siku zote utavuna ulichopanda. Ukiona unapata matokeo ambayo huyataki kabisa basi jua kwamba umepanda kitu ambacho sio sahihi. Ili update matokeo ya tofauti unapaswa kupanda mbegu bora.
24. Maisha yana pande mbili ambazo zipo wakati wote. Huwezo kuzungumzia juu ukasahau chini. Huwezi kuzungumzia kulia bila kushoto, huwezi pia ukazungumzia uzuri bila ubaya. Utakapozungumzia mafanikio lazima pia utaongelea kujifunza. Kwa hiyo mzizi wa mafanikio ni kujifunza.
25. Unapaswa kuwa ndoto kubwa na kitu cha kukusukuma wewe kila siku. Kuwa na kitu ambacho kitakuamusha asubuhi na mapema na kufanyia kazi. Unapaswq kuwa na kusudi lako LA maisha.
Ndoto kubwa na malengo makubwa sanaUmekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Namna Watu Wa Kawaida Wanavyofanya Mambo Yasiyo Ya Kawaida
Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii njema sana ya leo. Kila siku inayokuja kwako imebeba baraka, hivyo hakikisha kwamba unaitumia vyema kufanya makubwa. Siku hii ya leo napenda tuongee laa undani na kuona ni kwa namna gani watu wa kawaida wanaweza kufanya mambo ambayo sio ya kawaida.
Watu wote ambao tunawaona wameweza kufanya mambo ambayo sio ya kawaida walikuwa wa kawaida katika jamii kama hizi tunazoishi sisi. Ni watu ambao wamevuta pumzi kama ambayo tumevuta sisi na ni watu ambao wamekutana na changamoto, pengine changamoto zao ni kubwa sana kuliko changamoto ambazo sisi tunakutana nazo. Ila watu hawa hawakukata tamaa, ndio maana leo hii wewe unawashangilia na kuyaona mafanikio yao kama vile sio kitu cha kawaida.
Kuna namna ambayo watu wa kawaida wanaitumia kufanya mambo ambayo sio ya kawaida. Na namna hii ndio ningependa kukushirikisha siku hii ya leo. Kama na wewe unapenda kushiriki kufanya mambo ambayo sio ya kawaida basi tafadhali sana Fanya yafuatayo.
1. Tafuta kitu kimoja au ndoto moja ambayo utasema hata iweje, mimi nitakufa na ndoto hii. Nitafanya na kuitimiza asubuhi, mchana na jioni bila kuchoka siku zote saba za wiki januari mpaka disemba mpaka kieleweke.
2. Kubali kuonekana kilaza na mwehu. Watu wengi waliofanya mambo ambayo sio ya kawaida ni watu ambao walikubali kufanya mambo ambayo yaliwapunguzia sifa zao. Kuna wakati walikuwa wanaonekana kama vilaza, watu wasiojielewa na watu ambao jamii iliona wamekuwa vichaa. Ila wao kwa sababu walikuwa wanasukumwa na ndoto kubwa. Kubwa kuliko maneno ya watu, waliweza kusonga mbele bila kukata tamaa.
3. Kubali kuchekwa. Kutokana na kwamba watu hawa walikuwa na ndoto kubwa sana, hivyo watu hawa walikuwa wanafanya vitu ambavyo havikuwahi kuonekana ni vya kawaida. Na walikuwa wanaongea mambo makubwa kiasi kwamba wanaonekana kama wamekeungeuka. Watu waliwacheka sana. Ila hawakukata tamaa, walisonga mbele na kuhakikisha kwamba hakuna kitu ambacho kinawakwamisha kufikia mambo makubwa.
4. Kumbatia matatizo.
Watu hawa ni watu ambao wamepitia katika matatizo makubwa, ila kwao matatizo hayakuwa tatizo. Bali matatizo yamekuwa dataja la wao kusonga mbele. Walijua wazi kabisa kwamba hakuna watu ambao hawana matatizo kabisa. Hivyo kwako ilikuwa ni au wabadilishe matatizo kuwa daraja la kusongambele au wayafanye matatizo kuwa fursa.
5. Soma Vitabu. Niambie mtu yeyote ambaye amefanikiwa ili nikwambie vitabu anavyosoma.
Kiukweli mpaka leo hii sijakutana na mtu mwenye mafanikio makubwa ambaye hasomi vitabu. Utakuta watu hawa wanajichimbia na kusoma vitabu na vitabu . Kwenye nyumba zao wana maktaba kubwa sana za vitabu ambazo wanazitumia mara kwa mara.
Wanasoma Vitabu ili waweze kupata mwanga wa kusonga mbele. Wanasoma Vitabu kupata mawazo mapya ya biashara.
Wanasoma Vitabu ili kuboresha kile ambacho walikuwa wanafanya.6. kuipa muda ndoto yao. hiki ni kitu kingine cha kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa. hawana papara ya kukimbilia mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi. wanaamua kuiipa muda ndoto yao huku wakiifanyia kazi hata kwa kutokea chini.
Hii ndio siri ambayo watu wanaofanya mambo yasiyo ya kawaida wanaitumia. Kumbuka kwamba watu hawa ni watu wa kawaida kama wewe ila wanaweza kufanya mambo ambayo sio ya kawaida kwa kutumia kanuni na mbinu ambazo tumeziona hapo.Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391
Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391
kila la kheri
Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391
-
Hivi Ndivyo Unaweza Kuwa Gwiji Kwenye Mchezo Maisha
Maisha ni mchezo ambao unapaswa kujua namna ya kuucheza. Hata hivyo mchezo huu una Sheria zake ambazo ni za kipekee sana. Hivyo unahitaji kuzifahamu Sheria hizi.
Kama ilivyo kwenye mchezo wa mpira wa miguu, sio kila mtu ni gwiji kwenye mchezo huyo. Vivyohivyo kwenye mchezo wa maisha. Sio kila mtu ni gwiji. Ila wewe unaweza kuugifikia ugwiji kwa kufanya yafuatayo.
1. Kusoma Vitabu na kujifunza kitu kipya kila siku.
Nimegundua watu wengi wanaofanya makubwa ni wasomaji wazuri wa vitabu. katika vitabu wanapata fikra mpya ambazo zinawafanya wasonge mbele. Ukikutana na Ben Carson, atakwambia soma Vitabu. Ukienda kwa Donald Trump atakwambia soma sana Vitabu. Ukikutana na Kamkwamba atasema, soma Vitabu kadri uwezavyo. Na Mimi ninasemaje? Soma Vitabu2. Kuweka katika matendo yale uliyosoma kwenye vitabu.
Usiishie tu kuwa msomaji wa Vitabu, kuwa mtekelezaji wa kile unachosoalma. Kiweke katika matendo nankifanyie kazi zaidi ya mtu mwingine.Haya ni mambo mawili ambayo kama utayafanyia kazi siku zote za maisha yako, basi utageuka kuwa gwiji
Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Mambo Matatu (03) Ambayo Vijana Wa Kitanzania Wanakosea ila Wanayafanya Kuwa Uhalisia
.
“Watanzania siku hizi mmeanza kuamka kidogo, kidogo. Ila bado itawachukua muda kidogo kuweza kufikia viwango vya watu kujituma bila kushurutishwa”
Alisema baba mmoja wa makamo ambaye ni mgeni hapa nchini.Hongera sana rafiki yangu na leo hii napenda nikwambie mambo ambayo watanzania wengi wamekuwa wanayafanya kimakosa na kuendelea kurudiarudia makosa haya haya kila siku. Ma bado wanageuza makosa hayo yawe ukweli. Yaani wanahararisha uongo kuwa ukweli.
1. Kutojali muda. Kuna usemi kwamba hakuna haraka barani Afrika. Hadi kuna mtu ameandika kitabu kuzungumzia suala hili. Na usemi huu umekuwa unakumbatiwa sana na watu kama vile ni katiba ya Tanzania na Afrika. Hapa unapaswa kubadilika. Anza kujali sana. Unapokuwa na miadi jitahidi kuwahi.
Unapokuwa na kazi, ondoa usumbufu na wala usiruhusu maongezi yasiyo na maana.
Usiahirishe kazi ya leo kwa ajili ya kesho. Hivi ndivyo utaweza kuutumia muda wako vizuri kufanya mambo mazuri.2. Kuzidisha ujamaa. Watanzania tuna ujamaa wa kiwango cha juu sana kiasi kwamba kizazi cha watoto wadogo wanakua wakijua kwamba maisha yao yote yataendeshwa kijamaa. Wanashindwa kujituma na kufanya kazi.
Unakuta kijana kahitimu chuo, baada ya hapo anaenda kwa mjomba kuwambia kwamba amehitimu Chuo. Na huko anamaliza mwezi mzima anakula na kunywa. Wala haambiwi kafanye kazi upate hela yako unitegemee. Utakuta yeye muda wote tu ni kuangalia tamthiliya na vitu vingine.Baada ya mwezi kijana anahama na kwenda kwa bibi au shangazi. Huko anawaambia kwamba amehitimu na anatafuta kazi. Anakaa huko mwezi mwingine mzima akila na kunywa.
Kwa hiyo unakuta mtu wa namna hii anakua akijua kwamba maisha sio wajibu wake.
Ndio hawa huwa tunawasikia mitaani wanasema kwamba nikienda kwa mjomba huwa sitamani kutoka, maana pale kila kitu kipo. Vijana kuweni makini sana, ukiona vyaelea vimeundwa.3. Kutojituma katika kazi. Vijana wengi wa kitanzania bila kusimamiwa kazi hazifanyiki. Na mwingine unakuta anakwambia kabisa kwamba mimi bila kusimamiwa basi kazi zangu zinakwama. Wewe hupaswi kuwa mtu wa namna hii. Unapaswa kuwa na moyo wa kujituma na ujitume kwelikweli.
Jisimamie wewe mwenyewe. Ukiweka malengo yako hakikisha kwamba unajisukuma ili uweze kuyafikia malengo yako ambayo umejiwekea.Vijana wa kitanzania amkeni. Tanzania ya kesho inajengwa na mimi pamoja na wewe. Asante sana, tukutane kileleni.
Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Viashiria Saba Vinavyoonesha Kwamba Umaskini Utakuandama Maisha Yako Yote
Kila mtu anapenda kufanikiwa. Hata mtoto ana uwezo wa kutambua na kujua kwamba kitu fulani ni bora zaidi ya kingine. Ndio maana utasikia mtoto mdogo anawaombea wazazi wake wapate gari, wanunue ghorofa na vitu vingine kama hivyo.
Hii ni ishara ya waziwazi kwamba utajiri unapendwa na kila mtu. Na ni ukweli usiopingika kwamba utajiri ni muhimu. Mbali na kwamba utajiri ni muhimu. Kuna watu ambao huwa wanafanya vitu vya kuwaondolea utajiri.
Ukikuta unafanya vitu vifuatavyo jua kwamba kwako, utajiri utausikia redionj maisha yako yoye.1. Ukipata hela unatumia yote
2. Unajikopesha kutumia hela ili uje ulipe kwa hela ambayo hauna mkononi.
3. Huongezi maarifa kuhusu pesa.
4. Unalala sana zaidi ya mtu mwingine chumbani kwako
5. Unalalamikia serikali, wazazi na watu wengine kwa makosa yako.
6. Unasubiri mabadiliko yasavaboshwe na watu wengine. Wewe sio msababisjaji waabasiliko.
7. Zembea kazi, wakati wa kazi jifiche.
8. Hairisha mambo ya leo kufanya kesho.Hivi ni viashiria sita vya waziwazi kwamba utajiri utabaki kuusikoa redioni. Ila kama una moyp na ungependa uupate utajiri fanua kinyume chake.
1. Weka akiba matumizi madogo zaidi ya mapato)
2. Usikope
3. Ongeza maarifa yako kuhusu pesa kwa kusoma Vitabu vinavyohusu pesa.
4. Amka mapema na fanya kitu ambacho wengine hawafanyi
5. Usilalamike. Fahamu kwamba maisha ni wajibu wako. Ukishinda ni juu yako, ukishindwa ni juu yako pia.
6. Kuwa sehmu ya mabadiliko. Fanya kama ambavyo Mahatma Gandhi anasema, “kuwa sehemu ya mabadiliko ambayo unapenda kuyaona”.7. Fanya kazi kwa bidii.
8. Fanya kazi ya leo, siku hii ya leo. Usisubiri mpaka kesho -
Huu Ndio Ukombozi Muhimu Ambao Wewe Hapo Unauhitaji
Neno ukombozi kwenye kamusi ya kiswahili sanifu linamaanisha, UOKOAJI WA WA WATU KUTOKA KWENYE HALI MBAYA AU DUNI.
Kumbe makala ya leo imejikita katika kuhakikisha unaelewa nini unapaswa kufanya ili kutoka kwenye hali mbaya.
Je, ni aina gani ya ukombozi unaihitaji?
Kitu kikubwa ambacho kinahitajika ni wewe kukombolewa kifikra. Ndio fikra zako ni kitu cha kwanza kabisa ambacho wewe hapo unahitaji. Na ukombozi wa fikra hauji tu hivihivi. Ukombozi wa fikra unakuja kwa wewe kupata maarifa sahihi. Maarifa sahihi ndio yatakupelekea wewe kuchukua hatua sahihi.
Maarifa sahihi ndio yatakupelekea wewe kufanya maamuzi sahihi.Huwa ninapenda kusema kwamba maarifa sahihi + hatua kubwa na sahihi huleta matokeo makubwa. Na huu ni ukweli.
Kwa hiyo kila siku tafuta kuhakikisha unapata maarifa sahihi. Ukishapata maarifa sahihi yafanyie kazi.
Labda utajiuliza ni wapi naweza kupata maarifa sahihi? Nipende kukwambia kwamba maarifa sahihi yanapatikana kwenye vitabu. Tafuta Vitabu sahihi usome. Soma soma na soma vitabu. Huku utapata maarifa sahihi ambayo yatakupa ukombozi wa fikra.
Asante sana. Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.
Karibu sanaUmekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA
