-
Hasara Tano zitakazojitokeza endapo wewe utaacha kutimiza ndoto zako
Tafiti zinaonesha kwamba ni asilimia moja tu ya watu duniani ndio wanaofurahia mazuri na kumiliki asilimia kubwa sana ya uchumi. Ni asilimia moja tu ya watu ambao huwa wanafikia ndoto zao maishani huku wengine wakiishia njiani.Watu huacha kufuatilia ndoto zao kwa sababu wakatikufuatilia ndoto zako ni sawa na kuamua kujitupa kwenye maji ili kuogelea. Waogeleaji wengi huishia kati kati kwa sababu huwa hawaoni alama ya kumalizia iko wapi. Yaani wewe hupaswi kuacha kwa sababu umekutana na changamoto na hivyo kuifanya alama ya kumaliza iwe mbali sana. Kama alama hii haionekani, haimaanishi kwamba sasa huo ndio wa mbio. Na wala haimaanishi kwamba hautafikaSasa hapa kuna hasara tano ambazo zitajitokeza endapo wewe hapo utaacha kufuatilia ndoto zako.1. utafanya mambo yaonekane ni magumu zaidi ya yalivyo. Ni ukweli kwamba mambo ni magumu. Ila sio kwa kiwango kikubwa kama ambavyo unataka kuuonesha ulimwengu.Kwa hiyo utapaswa kusonga mbele. Ushindi huwa haupatikani kwa kuacha kufanya kitu bali kwa kusonga mbele na safari mpaka mwisho wa safari.2. utapoteza muda wako, pesa na nguvu zakoPale unapoanza kufanya kitu lazima kuna utawekeza kitu kwenye kutimiza ndoto zako. Utwekeza muda, utwekeza nguvu, utawekeza pesa na vitu vingi. Sasa kama ukiishia njiani utakuwa umeamua kupoteza vitu vyote hivi kabla hujafikia mwisho kabisa.Hata kam utasema kwamba mbona nilikuwa sijaweka pesa sana hapa. Ila ukweli ni kwamba muda wako ni pesa pia. Kama usemi wa kiingereza unavyotuasa kwamba muda ni pesa au muda ni mali.Ngoja nikwambie kitu kukhusu vikwazo na matatizo na changamoto utakazokutana nazo njiani. Unapokuwa umeweza kutatua changamoto hizi, ukweli ni kwamba hata hukumbuki kwamba umeshapitia kwenye changamoto kama hizo hapo. Utakachokuwa unaona machoni kwako ni ushindi ambao tayari unao mbele yako.3. Utawanyima wengine hamasa ya kusoga mbele. Kuna watu wanakuangalia wewe hapo kama mfano wa kuiga maishani mwako. Inawezekana sio wengi sana ila wapo. Sasa ukiamua kuishia njiani. Maana yake utakuwa umeamua kuwakatisha tamaa hawa hapa ili waone kwamba maisha ni magumu na ni vigumu kufanya maajabu maishani mwao.Hivyo basi usikubali kabisaa kuipoteza ndoto yako na kishia njiani.Jipatie nakala ya kitabu cha Jinsi ya kufikia ndoto zako ili uweze kujifunza mengi kuhusu ndoto yako sasa. tuwasiliane kwa 0755848391 -
Huyu Ndiye ARNOLD SHWARZENEGER Na Mambo Matano Ya Kujifunza Kutoka Kwake
Moja kati ya watu ambao dunia inawafahamu kwa kufanya makubwa basi ni mwigizaji wa mjengaji wa viungo vya mwili (body builder) Arnold Schwarzenegger.Huyu akiwa mtoto, wazazi wake walimpeleka ili akajifunze mpira wa miguu. Alikuwa anaenda kila siku na kufanya mazoezi kama wengine wanavyofanya ila kwake hicho hakikuwahi kuwa kitu ambacho kinamsukuma zaidi. Kila mara alihisi kama kuna kitu ambacho hakijakaa sawa ila hakujua hicho kitakuwa ni kitu gani. Siku moja mwalimu wake wa mpira alimwambia Anord na wanafunzi wengine wa mpira wa miguu wawe wanaenda kufanya mazoezi ya kunyanyua vyuma kila siku kabla ya kuanza kucheza mpira. Siku Arnold alipoanza kunyanyua vyuma, ndio aliona kile kitu ambacho alikuwa anakitafuta kila siku sasa ndio amekipatia jibu. Kile kitu ambacho kilikuwa hakijakaa sawa, sasa ndio alijua ni kitu gani hicho. Aliona kwamba eneo ambalo alipaswa kuwa ni hapo kwenye kunanyua vyuma na wala sio sehemu nyingine.Kuanzia siku hiyo akaachana na kucheza mpira wa miguu na kuanza kufanya mazoezi ya kujenga mwili.Ikawa katika usoma magazeti Arnold alikutana na hadithi ya Reg Park. Huyu alikuwa njenga viungo wa uingereza ambaye alishinda tuzo ya mr. universe na baadae kuingia kwenye tasnia ya uigizaji. Alifanya vizuri huko na kupata hela ambazo alizitumia kujenga eneo zuri la kufanyia mazoezi.Tayari Arnold alikuwa na mtu wa kumwangalia. Tayari alikuwa na ndoto. Alitaka kuwa kama Reg Park.Lakini sasa kuna tatizo ambalo lilijitokeza. Watu hawakuelewa ndoto yake. Wazazi wenyewe hawakumwelewa. Hata baada ya yeye kushinda tuzo yake ya kwanza ya Mr. universe, wazazi wake hawakumwelewa.Alijituma na hatimaye kupata tuzo ya m r. universe na baadae kupata tuzo za mr. olypia mara tatu mfululizo.Hii ndio kusema kwamba kama Anord angeendelea na uchezaji wa mpira basi huyu tunayemjua leo asingekuwa ni yeye bali mtu mwingine.
Sasa kuna mambo manne ambayo tunaenda kujifunza kutoka kwa Arnold1. Kuwa na ndoto na maono ya kufanyia kazi maishani mwako.Arnold anasema kwamba ndoto na maono ndivyo vinakuelekeza wapi unapaswa kuwenda wapi. Vinakuonesha njia sahihi ya kufuata ili kuweza kufika huko. Anaendelea kusema hivi “unaweza kuwa na meli bora sana na ukawa na nahodha wazuri kuliko wote duniani ila kama haujui unaelekea wapi ujue utazunguka huku na huko na mwisho wa siku hautafika sehemu ya maana”2.Kamwe usifikiri kwa udogoArnold anasema kwamba siku zote lenga kupata nyota. Na kinachowafanya watu wasifikirie kuwa na ndoto kubwa ni kwa sababu tu ya kuogopa kushindwa. Unachopaswa kufahamu ni kwamba kama hauna ndoto kubwa tayari umeshashindwa.Yeye kwenye maisha amekuwa anaweka ndoto kubwa na ambazo mpaka sasa hivi amezifikia kwa viwango vikubwa sana. Alikuwa na ndoto ya kuwa body builder mkubwa na aliweza kuifikia na kupata tuzo nyingi kwenye hilo eneo.Alikkuwa na ndoto ya kuwa mwigizaji anayelipwa sana. Ameweza kufanikisha hilo pia kwa viwango vikubwa.Alikuwa na ndoto na kuwa kwenye nafasi kubwa kisiasa. Ndoto hiyo iliweza kufikiwa kwa yeye kuwa gavana na jimbo la California nchini Marekani.Anasisitiza mimi na wewe tuwe na ndoto kubwa kubwa.Hapa ndipo naukumbuka tena ule usemi wa Donald Trump unaosema kwamba, katika maisha yako utapaswa kufikiri na kama utapaswa kufikiri kwa nini usifikiri kwa ukubwa zaidi?3.Achana na wakatisha tamaa.Arnold anasema kwamba katika maisha utakutana na watu ambapo wanakatisha tamaa..Lakini kamwe, usikubali wakatisha tama wakurudishe nyuma kwenye maisha yako Mtu akisema haiwezekani wewe sikia inawezekana.Mtu akisema haijawahi kufanyika sikia inafanyikaMtu akisema hapana unapaswa kufahamu kwamba hiyo ndio NDIO. Kuna usemi kutoka kwa Nelson Mandela ambao unasema kwamba siku zote huwa haiwezekani mpaka pale mtu anaposababisha kile kitu na kiwezekane. Unaweza kuweka rekodi mpya.Arnold anasema kwamba laiti angewasikiliza watu basi ndoto zake zingeishia njiani. Alipotaka kuhamia marekani wakasema kwamba haiwezekani, aliposema kwamba anataka kuwa mjenga mwili mkubwa sana wakasema hayo yanafanyika Marekani wala sio kwao Austria.4. kubali kuwekeza muda wa kutosha kabla ya kufikia ndoto yako.Arnold anasema kwamba kufikia ndoto zako sio rahisi hata kidogo. Utapaswa kuweka juhudi na kutumia muda wako mwingi kufanya mazoezi na kufanya vile ambavyo watu wengine hawafanyi.Mfano Arnold anasema kwamba kuna kipindi alikuwa anafanya mazoezi kwa masaa matano kila siku. Baada ya hapo anaingia darasani kujifunza kuigiza. Baada ya ya hapo anajifunza kiingereza.Anasema kwamba aliyaweza haya yote kwa sababu alikuwa anapangilia ratiba yake vizuri na kuhakikisha kwamba haipiti sekunde.Arnold anashauri ulale masaa sita tu kila siku na masaa mengine 18 uyatumie kufanya kazi na kujinoa kwenye kitu ambacho unafanya. Kama unajihurumia kiukweli unaweza usiyaone mafanikio makubwa sana maishani mwako.Pia anashauri usiache ratiba yako huru sana kiasi cha kukufanya upoteze muda wako mwingi. Hakikisha kila dakika inakuwa na kitu ambacho unafanya.5. kubali kutoka jasho na damu kabla ya kufikia kilele cha mafanikio.Arnord ni miongoni mwa wale watu wanaoamini usemi wa waziri mkuu wa uingereza Winston Churchill wa damu, jasho na machozi.Na kwa hili hapa anatolea mfano wake kipindi akiwa anaigiza. Anasema kwamba kuna siku alitokwa na damu wakati anaendelea kuigiza kwenye magoti. Director akwambambia waishie hapo ili Arnord apate matibabu kwanza. Lakini yeye alisema kwamba anachotaka kuona ni kile kilichompeeleka hapo kimekamilika. Kwa hiyo waliendelea kurekodi tamthiliya wakati yeye anatokwa na damu mpaka ikaisha.Anasema kwamba kwenye maisha, nyakati kama hizi utakutana nazo sana. Lakini hupaswi kukata tama bali unapaswa kunyanyuka na kusonga mbele bila kukata tamaa.Hayo ndio mambo matano ambayo tunajifunza kutoka kwa Arnold Schwarzenegger. Kwenye kitabu chetu cha mwezi wa 10 cha timiza ndoto zako tutakkutana na mengi zaidi kutoka kwa mtu huyu na magwiji wengine walio fikia ndoto zao.Hakikisha unajiweka kwenye nafasi ya kupata kitabu hiki mapema sana kuanzia sasa. Utaweza kukipata kwa elfu mbili tu. Pesa hii unalipia kupitia nambari ya simu 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA.Kwa kufanya hivyo utaunganishwa kwenye kundi la THINK BIG FOR AFRICA kwa mwezi mzima. Ambapo utakuwa unapata masomo mengine zaidi. Karibu sana.KWA KUMALIZIA; mambo matano tunayojifunza kutoka kwa1. kuwa na ndoto kubwa ambazo unazifanyia kazi2. usifikiri kwa udogo3. achana na wakatisha tamaa4. kubali kuwekeza muda wa kutosha kabla ya kufikia ndoto zako5. kubali kutokwa jasho na damu kabla ya kufikia kwenye kilele cha mafanikioUmekuwa name,Godius Rweyongeza (songambele)0755848391www.songambeleblog.blogspot.com -
Kubali Kulipa Gharama Ili Uzifikie Ndoto zako
LIPA GHARAMAIli kweza kufikia mafanikio makubwa kwenye kutimiza ndoto zako basi moja ya kitu ambacho utapaswa kufanya ni kulipa gharama. Hii haijalishi kwamba wewe ni ndoto yako ni kuwa baba bora au mama bora, au iwe ni kufikia viwango vya juu katika mchezo fulani. Kwa vyovyote vile gharama bado haitaepukikiNa hapa ninapozungumzia gharama kinachokuja kwenye akili yako basi kinaweza kuwa ni kulipa pesa peke yake. Japo kwa vitu vingi gharama unazopaswa kulipa ni gharama ya pesa ila kwako wewe kuweza kufikia ndoto zako utahitaji kulipa zaidi ya gharama ya pesa. Kuna nyakati utapaswa kulipa gharama za pesa peke yake. Pia kuna nyakati ambapo utapaswa kulipa gharama ya pesa pamoja na vitu vingjne na hizi gharama nyingine ndizo ningependa uzifahamu siku hii ya leo.1. gharama ya muda2. gharama ya kujifunza3. gharama ya kuachamna na baadhi ya vitu. Kuna baadhi ya vitu ambavyo unavipenda sasa hivi. Utahitaji kuachana navyo ili tu uweke muda wako na nguvu zako kwenye kutimiza ndoto zako na malengo yako ya muda mrefu.4.gharama ya kufanya kazi kwa bidii. Kumbuka kwamba kuna kufanya kazi na pia kuna kufanya kazi kwa bidii. Hi ndio kusema kwamba utapaswa kufanya kazi zaidi ya uluvyozoea. Utapaswa kuweka juhudi zaidi ya vile ambavyo umezoea na uta[aswa kufanya kazi masaa mengi zaidi ya ulivyozoea.5. gharama ya kujifunza6. gharama ya pesa yenyewe.Baada ya kuzijua gharama ambazo utapaswa kulipa ili kuweza kufikia ndoto zako hapa una vitu ambavyo utapaswa kuvifahamu katika kutimiza ndoto zako.1.Kila ndoto yako uliyonayo leo hii itatimia ila unapaswa kuwa tayari kulipa gharama2. sehemu pekee ambapo unaweza kunywa na kula kabla ya kulipa gharama ni kwenye mgahawa au hotelini. Ila kwenye maisha na kutimiza ndoto zako basi utapaswa kulipa gharama kwanza kabla kupata kile ambacho unakitaka3. ukiona watu waliofanikiwa kimaisha unapaswa kujua kwamba watu hawa walilipa gharama kuweza kufika hapo walipofika. Na wewe unapaswa kuwa tayari kulipa gharama ili kuweza kufika hapo walipofika au kwenda zaidi ya hapo.4. kadri ndoto yako inavyokuwa kubwa ndivyo unapaswa kulipa gharama kubwa Zaidi.5. lipa gharama mapema. Kuna usemi kwamba muda mzuri wa kupanda mti ulikuwa ni miaka kumi iliyopita ila muda mzuri zaidi wa kupanda miti ni leoo hii. Vivyo hivyo kwenye kutimiza ndoto zako. Muda mzuri wa wewe kutimiza ndoto zako ulikuwa ni miaka kumi iliyopita ila muda mzuri izaidi wa wewe kutimiza ndoto zako ni leo hii.6. unaruhhusiwa kuchukua njia za mkato kwenye kutimiza ndoto zako ila fahamu kwamba hazitakufikisha kwenye mafanikio unayotaka na wala hazitakufanya upate mafanikio ya kudumu.7. utapaswa kufanya kazi yako vizuri zaidi kiasi kwamba kama kuna mtu ambaye anafanya kitu kama cha kwako aje kwako kujifunza namna kinavyofanyika. Na wakati yeye anajifunza kwako wewe unakuwa unachukua hatua zaidi kufanya vizuri zaidi..8. ili uweza kufikia ndoto zako utapaswa kutoa pia sadaka. Kwanza ufahamu kwamba kila kitu ambacho umewahi kufikia maishani kuna sadaka ambayo uliitoa. Iwe unaona umetoa sadaka au la! Hakuna kitu cha bure na wala dunia haijawahi kufanya hivyo.Kama kweli umejitoa kuhakikisha kwamba unafanikisha ndoto zako na kufikia viwango vikkubwa maishani mwako basi unapaswa kufahamu gharama ambazo utapaswa kulipa ili kuwea kufika huko uendapo. NAKUKUMBUSHA TU. Kila kitu ambacho unataka leo hii kina gharama yake ambayo utapaswa kulipa. Je, upo tayari kuilipa?Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
TOA USO WAKO FACEBOOK NA UWEKE KWENYE KITABU
“Get your face out of Facebook and get it into the book”
UnknownKama bado hujajiunga na mfumo wetu maalumu wa kutokea makala, bonyeza HAPA
Wiki Chache zilizopita nilikutana na usemi ambao nakubaliana nao kwa asilimia 100. Usemi huu mzuri
“unasema toa uso wako kwenye mtandao wa Facebook na uweke kwenye kitabu”.Kiukweli huu ni usemi ambao haujaremba kitu.
Yaani kama unapenda kutengeneza maisha ya tofauti basi utapaswa kutoa uso wako Facebook na kuuweka kwenye kusoma vitabu kwa muda mwingi.Ni ukweli kwamba Facebook na mitandao mingine inatuunganisha, lakini muda ambao watu wanatumia kwenye mitandao hii ni mwingi zaidi kuliko muda unaotumika kufanya kazi za kujenga. Imefikia hatua kila kitu ambacho mtu anafanya anakimbia kukiweka Facebook. Akiamka asubuhi basi anaweka Facebook
Akipata kifungua kinywa basi anaweka picha Facebook
Akikasirishwa bado na chenyewe anaandika Facebook. Kwa maisha ya sasa hivi unaweza kufuatilia maisha ya mtu Facebook na ukajua kila kitu alichofanya kwa siku nzima.Sasa swali Je, haya yote yanakusaidia nini? Hivi ukiweka Picha kwamba upo hoteli fulani au umekutana na fulani inakuongezea thamani gani mishani mwako? Je, inaingiza pesa? Na Je, usipofanya hivyo utakufa?
Ubovu wa mitandao hii ni kwamba ukiangalia kitu facebook wanakuletea kingine kinachofanana na kile cha awali. Hivyo unajikuta unatumia muda mwingi kwenye ni mtandao huu kuliko muda unaoutumia sehemu nyingine.
Utafiti unaonesha kwamba watu wanaingia Facebook kila baada ya dakika tano mpaka kumi
Sasa umefika wa wewe kutoa uso wako Facebook na kuuweka uso wako kwenye Vitabu.
1. Soma kujiongezea Maarifa na kujitofautisha.
2. Ukisoma kitabu, utaimarisha Afya akili. Na Afya ya akili ambayo itapelekea kwako kuwa na Afya ya mwili na roho.
3. Soma ili kupanua fikra zako na kupata mawazo chanya ya kumujenga.
4. Soma pia kuongeza kumbukumbu na kupunguza kusahau sahau
5. Soma kukutana na watu ambao huwezi kukutana nao. Au ambao hata ukikutana na bado hutapata kila kitu kutoka kwao.
6. Soma ili kuongeza kipato chako😊.
Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Vitu Viwili Kuhusu Ndoto Ambavyo Watu Wa Kawaida Hawana (Kama Utakosa Vitu Hivi, Utaishia Kusikia Mafanikio Kwenye Vyombo Vya Habari).
Kama Utakosa Vitu Hivi, Utaishia Kusikia Mafanikio Kwenye Vyombo Vya Habari
Mwaka juzi wakati nasoma kitabu cha Who Will Cry When You Die nilikutana na kitu cha kushangaza kidogo ila ikabidi nikifanyie kazi. Mwandishi wa kitabu Robin Sharma alisahuri kwamba unapaswa kuwa na kitabu cha ndoto chenye orodha ya vitu 101 ambavyo utavifanyia kazi kabla ya kufa. Vitu hivi vinaweza kuwa ni ndoto, malengo na mipango yako ya muda mfupi na mrefu. Hiki ni kitu kimoja ambacho kina sehemh mbili
Kwa hiyo mpaka hapo tunaona vitu viwili muhimu vifuatavyo.
1. Unapaswa kuwa kitabu cha ndoto
2. Unapaswa kuwa na orodha ya vitu 101 ambavyo uyavifanyia kazi maishani mwakoKabla hujaishia hapa ngoja tuendelee kidogo!
Ni watu gani ambao ungependa kukutana nao maishani mwako?
Sehemu gani ungependa kutembelea?
Lugha gani ungependa kujifunza?
Je, ungependa kuandika kitabu? Kitahusu nini? Mwaka gani?
Hivi kuna biashara au fursa unayiona kwenye akili yako? Ni ipi?
Gari gani ungependa kumiliki? Linafananaje? Nyumba je?
Je, unapenda kuwa huru kiuchumi? Itakuchukua nini na baada ya mwaka gani?
Afya yako je? Ungependa iweje?
Kama kuna kitu ungependa kufikia kati ya hivyo basi kiandike kwenye KITABU CHAKO CHA NDOTO.
Na hapo nimekupatia maswali ya kuanzia ili kutengeneza orodha ya vitu 101 ambavyo utafanyia kazi. Ni juu yako kuendelea mpaka ufikie 101.
Ngon nikwambie kitu. Mimi mara ya kwanza niliandika vitu 21 tu. Rafiki yangu mmoja akaja akasoma hiyo orodha kisha akacheka. Akaniambia hivi, acha uoga. Andika vitu mpaka ufikie vitu 101. Nikagundua kweli ulikuwa uoga, nikaanza tena.Sasa unajua nini?
Baada ya kuwa umefanya vitu vyote hivyo, kuna hatua saba hapa napenda uzifuate.
1. Orodhesha lengo au ndoto moja kubwa ambalo utafikia maishani.2. Weka sababu tano kwa nini utafikia lengo au ndoto hiyo. Katika nyakati ambazo utakutana na ugumu rudi kwenye KWA NINI zako ili zikupe moto za kusongambele katika kutimiza ndoto yako.
3. Chukua kalamu na karatasi na andika kila kitu ambacho kitahitajika kufikia ndoto hii. Andika kila hatua ambayo unafikiri utapitia kabla ya kufikia ndoto zako.
4. Andika vikwazo vyote ambavyo unafikiri vinaweza kujitokeza na hatua ambazo utachukua.
5. Andika majina ya watu muhimu kwako unayohitaji ili kufikia ndoto zako
6. Tengeneza orodha ya washauri. Hawa ni watu ambao watashiriki katika kukushauri na kufikiri juu ya ndoto zako.
7. Eleza jinsi ya uyakavyojisikia endapo utafikia ndoto hii. Je, utakuwaje kiuchumi, kihisia, kiroho na mwonekano.
Huu ndio mwongozo wako wa kutengeneza orodha ya vitu 101 ambavyo utafikia maishani.
****************🔥kama bado hujapata nakala ya kitabu cha jinsi ya kuibua ubunifu ulio ndani yako, chukua hatua leo. Kitabu kinapatikana kwa shilingi 7,000/- tu.
Tuma pesa kwenda 0755848391 jina Godius Rweyongeza.
Baada ya hapo nitumie ujumbe wenye barua pepe yako ili nikutumie kitabu.Asante sana,
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com -
Vitu vitano vinavyofanya watu waue ndoto zao na hivyo kushindwa kuzifikia
Katika hatua fulani maisha watu huwa na ndoto za kufikia vitu au kuwa aina fulani ya maisha. Ndoto hizi huwa ni nyingi hasa kwa watoto maana huwa wanazisema kwa kujiamini kuliko watu wazima. Ndio maana ukiongea na mtoto mdogo na kumwuliza kwamba unataka kuwa nani basi bila ya shaka na bila kukwama sehemu atakuambia anataka kuwa daktari, nesi, rubani, mwanasheria n.k. wakati anakupa jibu hilo hakwami popote wala haogopi chochote.
Sasa swali hilo hilo ukimwuliza kijana utashangaa sana. Utasikia mwingine anakwambia kwamba wewe hiyo hapo inakuhusu nini. Au utasikia mwingine anasema kwamba nasubiri kitu fulani kitokee ndio nitajua. Kama ni mwanafunzi basi atakwambia kwamba nasubiri nifaulu mitihani ndio nitajua kinachoendelea. Mwingine atakwambia kwamba nasubiri serikali itangaze ajira ndio nitajua. Hii ndio kusema kwamba mtu huyu sio tu amepoteza ndoto yake bali pia kwa sasa hivi hajui ni wapi anaenda. Lakini mtu huyu huyu miaka ya nykazikidogo ndiye alikuwa na ndoto kubwa ya kuwa raisi, daktari au rubani. Sasa ni nini hiki ambacho huwa kinatokea na kuua ndoto za watu. Leo hii nimekuandalia vitu vitano ambavyo vinasababisha watu kuua ndoto zao. Vitu hivi vinaweza pia kuwa vimechangia kuua ndoto zako ambazo umekuwa nazo maishani mwako, pengine usipokuwa makini vitaua na ndoto zako za sasa hivi.
1. Watu wengine wamekuzuia kuwa na ndoto kubwa
Kuna watu wengi ambao kazi yao ni kuua ndoto za watu. Watu hawa wanaweza kuwa ni watu wa karibu yako. Au wanaweza kuwa wale ambao kwa hakika wanajua ukiweza kuifikia ndoto yako basi kitendo kama hicho kitawafanya wawe watu wa chini. Hivyo wanachofanya ni kukutatisha tamaa na kukuonesha kwamba haiwezekani kabisa kufanya wala kutimiza ndoto kama hiyvo hapo.
Na watu wanaoua ndoto zako wanaweza kuwa ni watu wa karibu yako. Wazazi, ndugu jamaa na marafiki ambao pengine wao walijaribu kufanya kitu wakawa wameanguka au waliwaona watu wengine wakifanya kitu hicho wakawa wameshindwa. Hivyo wanachukua hizo kumbukumbu na kuzileta kwako, kuonesha kwamba na wewe hutaweza, tena watu hawa watakuja na kila aina ya sababu ya kuonesha ni kwa namna gani huwezi, na pengine watakupigia hesabu za kuonesha kwa nini ndoto unayotaka kuifanya haitawezekana.2. watu wengine wanaugulia maumivu ya nyuma au kukatishwa tamaa
Kukata tamaa na maumivu ni uhalisia kati kile ambacho unategemea na ukweli. Kila unayemowna amefikia mafanikio makubwa sana maishani basi ujue kwamba amepitia hali kama hii hapa. Na kuna nyakati maumivu yanaweza kuwa mazito kiasi cha kukufanya wewe upoteze matumaini uliyokuwa nayo. Hata hivyo unapaswa kuchukua somo na maumivu ambayo unakutana nayo kwa wakati husika. Maana siku zote matatizo huwa sio tatizo, bali fursa ya wewe kusonga mbele ya kufanya makubwa zaidi ya hapo.
Usipojifunza kutokana na matatizo basi utakuwa kama paka ambaye akikaa kwenye jiko la moto likamuunguza basi hatakaa tena kwenye jiko hilo hata kama ni la baridi. Siku zote chukua somo kutokana na changamoto ambazo unakutna nazo kasha songambele.
Kamwe usije ukajiambia kwamba sitarudia kufanya kitu hiki baada ya kuwa umeshindwa. Hilo hapo ni kosa kubwa kwa ndoto zako. Ni ukweli kwamba utashindwa mara kwa mara kabla ya kufikia ndoto zako ila usiache kuendelea na safari ya kutimiza ndoto yako. Ndio maana aliyekuwa waziri mkuu wa uingererza Magreth thatcher amewahi kusema, kuna nyakati utapaswa kupigana vita zaidi ya mara moja ili kushinda. Kwa hiyo wewe kila mara chukua somo ujifunze na usonge mbele.3.kuna watu wanatulia na ukawaida
Kuna watu wanaamua tu kutulia na kile walichonacho. Ila cha kufahamu ni kwamba unapoamua kutulia na kile ulichonacho, hata kile ulichokuwa nacho kinaanza kupungua. Ni katika nykati kama hizi hapa utajikuta unaanza kuilalamikia serikali, wazazi au watu ambao wewe utawachaggua kuwalalamikia.
Kama kweli kwa sasa unajua kwamba unaishi maisha ya kawaida na umetulia basi amua sasa kuanza kufikiri tofauti. Kumbuka kwamba uwezo wako ni mkubwa na hhivyo unapaswa kuutumia. Ukitulia na kuridhika na hali ya sasa unakuwa umeamua kuuzika uwezo wako kaburini. Tunaweza kusema kwamba unakuwa na sawa na mtu ambaye anachukua meli kubwa ambayo imetenegezwa ili kusafirisha watu na mizigo kwenye maji makubwa ya bahari, sasa meli hii inawekwa kwenye kijito kidogo tu. Huhitaji mtu wa kukwambia kwamba hapo sio mahala pake. Na wewe hivyo hivyo, ukitulia na hali ya sasa unajjikwamisha.
Kuna shida gani katika kutulia na kuridhika?
Hili hapa ndilo linaweza kuwa ni swali lako ambalo unajiuliza. Ngoja ni kwambie kitu. Vitu vilivyotulia ndivyo huja na madhara makubwa. Mbu huzaliana kwa wingi kwenye maji yaliyotulia na kutuama. Hata konokono wanaoeneza magonjwa wanakutwa sehemu kama hizi zilizotulia. Yaani naweza kusema kwamba kila kitu ambacho kinakaa kwa muda mrefu kimetulia kinaoza, hata mdomo ukikaa muda mrefu umetulia unaanza kutoa harufu. Unaona sasa, kumbe ni wakati wako wako wewe kuhakikisha sasa hautulii tu kuridhika na hali ya sasa. Kwa sababu unaweza kufika mbali zaidi ya hapo na unaweza kuwa zaidi ya ulivyo sasa hivi kama utaammua kuzifanyia kazi ndoto yako.4. watu wengine wanakosa ujasiri unaotakiwa ili kuzifikia ndoto zao,
Ni ukweli kwamba ndoto huwa ni kubwa. Lakini pia huwa zinahitaji muda ili kuweza kuzifikia ndoto hizi. Cha ajabu zaidi kuhusu ndoto ni kwamba wewe ndiwe unakuwa unaona kule unapoenda ila wengine hawapaoni. Pia wewe ndiwe unakuwa unajua ni wapi unaenda na kwa nini unaenda huko ila wengine ndio kwanza wanakushangaa. Sasa katika nyakati kama hizi hapa unahitaji ujasiri mkubwa kuendelea kuifanyia kazi ndoto yako kila siku hata kama watu wengine wote watabaki u kukucheka, kukutania na kukutukana. Inahitaji ujasiri mkubwa. Kadri unavyokuwa na ujasiri wa kuiongelea ndoto yako ndivyo unakuwa pia na ujasiri wa kuifanyia kazi na kuifikia.5. kuna watu wanakosa fikra za kuota ndoto kubwa.
Hivi watu huwa wanaanzaje kuwa na ndoto kubwa? Hili ni swali ambalo pia tunapaswa kujiuliza na kulitafutia majibu yake kwa kina. Nakumbuka mvumbuzi Thomas Edison akiwa na umri wa miaka 21 alisema kwamba “ningependa kutumia maisha yangu nikiwa navumbua vitu. Kuna vitu vingi sana vya kufanya na ninaaweza kufa kabla sijafikia hatua kubwa, hivyo nitatumia muda mwingi kuhakikisha kwamba navumbua hivyo vitu”. Kwa hiyo yeye ndoto ya maisha yake ikawa ni kuwa mvumbuzi. Na unaweza kuona hapo kilichofanyika ni kwamba alianza kuwa na fikra juu ya kitu ambacho angekifanya ili kufanya thamani na maisha ya watu kuwa bora zaidi.
Kama kuna kitu kimoja ambacho utapaswa kuhakikisha unakifanyia kazi basi ni kuwa ndoto kubwa ya maisha yako.Rafiki yangu hivi ni vitu ambavyo vinawazuia watu walio wengi kuweza kufikia ndoto za maisha yao. Hivi ni vitu ambavyo vimekuwa vikikuwamisha pia na wewe. Sasa ni wakati wako kuhakikisha kwamba unasonga mbele na kufanya makubwa zaidi. Hakikisha kwamba unakuwa na ndoto na uifanyie kazi
Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Mambo Muhimu Unayopaswa kuyafanya Unapoamka Asubuhii
Moja kati ya vitu ambavyo vimekuwa havielekezwi kwa umakini sana basi ni namna ya kuianza siku yako. Unapoamka asubuhi unakuwa na mambo mengi sana ya kufanya.
Wengi huutumia muda huu kufungulia redio na kusikiliza taarifa ya habari. Hata hivyo hapa napenda nikushirikishe namna sahihi ya kuianza siku yako.Haupaswi kuianza siku yako kama mnyama au ndege. Kuna mambo machache ambayo ukiyafanya yatakunufaisha na kuifanya siku iwe ya kipekee. Hizi ni mbinu pia ambazo wataalamu na watu waliofikia mafanikio makubwa wamekuwa wanatumia.
Moja, jisemee maneno chanya
Kuna mtu ambaye ubora wa siku au ubaya wa siku unatokana na kile anachokutana nacho anapoamka. Akiamka akakuta mvua inanyesha basi anatoa tafsiri na kuiita siku hiyo njema au mbaya kulingana na anavyojisikia. Mwingine akisikia mlio wa mnyama fulani basi anatoa tafsiri kuonesha kwamba hiyo ni siku njema au mbaya. Ila nipende kusema kwamba kila siku huwa ni bora. Ubora wa siku hautokani na hali ya hewa. Ubora wa siku unaanzia ndani yako. Anza kujisemea maneno chanya asubuhi unapoamka. Jisemee maneno chanya na maneno ya kukusukuma kufanya makubwa. Jisemee kwamba wewe ni mshindi, umezaliwa kushinda na utaishi kiushindi ndani ya siku hii mpya. Maneno mengine chanya unayoweza kujisemea ni kama……….Pili, Soma malengo yako
Utumie muda huu wa asubuhi kuhakikisha unasoma malengo yako. Jiulize Je, bado ninatembea kwenye nia sahihi kuelekea ninapotaka kufika kimafanikio. Inashauriwa kila siku upate muda wa kupitia malengo yako walau mara mbili. Ila bado unaweza kupitia malengo yako zaidi ya hapo. Na muda mzuri wa wewe kupitia malengo yako ni asubuhi na mapema kabla hujakutana na uhalisia wa dunia.Tatu pangilia ratiba ya siku nzima
Winston Churchill amewahi kunukuliwa akisema kwamba akipewa saa sita za kukata mti atatumia masaa manne kunoa panga na mawili kukata mti. Muda wako wa asubuhi ni mzuri kwako wewe kuanza kunoa panga. Unanoa panga kwa kupangilia nini utafanya. Baada ya hapa utaianza siku yako ukijua haswa ni nini unapaswa kutimiza.Nne, soma kitabu, ianze siku yako kwa kusoma kitu chanya. Soma kitu ambacho kinakuongezea maarifa zaidi. Kumbuka kipato chako kitaongezeka mara dufu kama utaongeza maarifa yako mara tatu zaidi kama anavyotuasa Robin Sharma.
Tano, andika mambo ambayo kamwe hutafanya.
Mbali na kwamba umeshapangilia siku yako kwa kuandika nini utafanya. Andika pia yale ambayo hutafanya hata iweje. -
Kitu cha kufanya pale unapokuwa na ndoto kubwa inayohitaji pesa na wewe hauna pesa.
Mara nyingj unapokiwa unaanza maisha, lazima ndoto zako zitakuwa kubwa. Ni kubwa kiasi kwamba ukimwambia mtu atabaki kushangaa na kukakaa mdomo wazi hadi nzi wakaingia. Bila shaka unekutana na hali hii kama bado utakutana nayo. Wewe unayejua wapi unaenda na kwa nini huwezi kushangaa. Mwingine akisikia ndoto yako atakuuliza pesa utaitoa wapi ya kufanya hayo yote? Kwa haraka unapaswa kumjibu kwambabnitasambaza upendo. Ila kadri tunavyoendelea na Makala hii utaona kweli kusambaza upendo ni kitu muhimu sana. Sasa hapa chini nimekuwekea vitu vya kufanya kama hauna pesa na una mdoto kubwa.
1. Anza kufanya biashara ndogo ndogo
Mara nyingi utakuta kwamba ndoto yako inahitaji pesa ya kutosha. Na wewe unaweza ukawa kabisa hauna pesa au una kiasi kidogo kiasi hata ukianza kwa kiasi hicho hutaweza hata kufikia katikati ya ndoto zako. Katika nyakati kama hizi basi utapaswa kuchagua biashara ndogo ndogo ambazo utatoa thamani kwa watu na kupata hela. Unaweza kufanya hizi kwa muda kisha ukapata hela ya kutosha na ukaamua kuingia moja kwa moja kwenye utimizaji wa ndoto zako kubwa.Anzia chini panda juu
Kuna usemi wa kiingereza unaosema kwamba dream big but start small. Ukimaanisha kwamba kuwa na ndoto kubwa ila kuwa tayari kuanza kidogo. Kuwa tayari kuanza na kile ulicho nacho huku unakikuza zaidi. Yaani unataka chini kuelekea juu. Vitu vidogo huwa vinatoa mambo makubwa ambayo watu hawategemei kabisa. Mbuyu ni mti mkubwa ila mbegu yake ni ndogo. Ukiiona mbegu ya mbuyu huwezi kuona uwezekano wa mbegu hiyo kutoa mti mkubwa. Lakini uwezo wake huwa unajidhirisha kadri muda unavyosogea. Na wewe utaweza kutimiza ndoto zako, ni suala la muda tu.Jitume sana
Utahitaji kuweka nguvu katika kutimiza ndoto yako. Wafanyabiashara wengi na watu waliofikia hatua kubwa kimasisha wanasema wazi kabisa kwamba mwanzo ni mgumu. Na katika kipindi hiki lazima utapaswa kufanya kazi kwa bidii na kujituma kwa bidii kubwa. Kama unakaribisha ukawaida basi utaendelea kuwa wa kawaida ila kama umepanga kufanya vitu vya tofauti lazima uwe tayari kufanya vitu katika namna ya utofauti. Na hivyo kufanya kazi kwa bidii hakuepukiki. Katika kipindi hiki usemi wa Waziri Mkuu wa uingereza Winston Churchill wa damu, kuteseka, machozi na damu ndipo haswa unatumika.Kumbuka ukitoa jasho jingi sana wakati wa mazoezi utatoa damu kidogo wakati wa vita.
Ukitoa jasho jingi wakati wa ujana, utaondoa mateso yatakayokupata wakati wa uzee.Usitarajie tu kwamba ndoto yako itatimia wewe ukiwa umelala kitandani. Katika kitabu chake cha DESTINY mwandishi T. D. JAKES anakazia msumari kwa kusema, usikae tu kwenye sofa na kusema ONE DAY YES! Ndio itakuja siku ambapo utafikia hatua kubwa lakini unapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kufikia huko.
Kubali kuanza kuifanyia kazi ndoto yako leo. Kubali kuifanyia kazi haswa. Anza sasa hivi.
Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391Hakikisha umesubscribe kwenye YouTube Channel Yangu Ya Youtube Kwa Kubonyeza Hapa -
Kitu kibaya zaidi ya kutokuwa na macho ya kuona (utashangaa kusoma kitu hiki cha kipekee).
Hellen Keller (1880-1968) alikuwa mwandishi, mwanasiasa na Mwalimu wa chuo. Kwa miaka hiyo alikuwa ni kipofu wa kwanza kupata shahada ya Chuo kikuu. Siku moja alitoa hotuba moja ambayo iligusa maisha ya watu. Baada ya hotuba hiyo waandishi walikusanyika ili kumuuliza maswali ya hapa na pale. Wakati maswali yanaendelea kuulizwa alijitoleza kijana mmoja ambaye alisafisha koo na kusogea mbele kidogo. Kijana huyu alikuwa ameitafuta nafasi hii kwa muda mrefu na isitoshe alikuwa mchanga kwenye ulimwengu wa habari. Aliuliza, “kitu gani ni kibaya zaidi katika maisha zaidi ya kuwa kipofu”.
Mara ghafla sauti ya miguno zikaanza kusikika. Mtu mmoja kwenye kundi la watu akasikika akisema, swali gani hilo achana nalo usilijibu. Mwingine akasema swali hilo linadhalilisha achana nalo.Lakini hali haikuwa hivyo kwa Hellen Keller. Alionekana kulipenda swali na hivyo aliwaashiria watu watulie ili aweze kujibu hilo swali. Alisema, “kitu kibaya zaidi katika maisha ni kuwa na macho bila ya kuwa na maono/ndoto”.
Akamaliza.Unajua nini? Kuna watu walifikiri kitu kibaya zaidi ya kuona kitakuwa labda ulemavu wa mikono au miguu. Ila alisema maono au ndoto ndio kitu kibaya zaidi.
Swali kama hilo lingeulizwa kwa vijana wa zama hizi basi ungeshangaa. Kuna ambao wangesema kitu kibaya zaidi ni kutokuwa na mtaji wa kuanzisha biashafa, wengine wangesema kitu kibaya zaidi ya kukosa msaada wa serikali, wengine wangesema kitu kibaya zaidi ni kukosa elimu.
Tunachojifunza kwa Hellen Keller ni kwamba maono ni mwongozo wa maisha. Mtu mmoja amewahi kusisitiza kwa kusema kuwa, maono au ndoto sio zile unazoota ukiwa umelala. Bali ni kile kitu ambacho unakiona na kukiendea hata kama umefumba macho. Tena wataalam wanasema ndoto zako zinapaswa kuwa kubwa zaidi kiasi cha kukuogopesa hata wewe. Ndoto kubwa ziyakufanya
1. Upate nguvu ya kusonga mbele hata pale mambo yanapokuwa ni magumu maishani mwako au unapokutana na changamoto2. Zitakufanya upangilie muda wako kwa vipaumbele.
3. Zitakufanya utengeneze konekisheni za maana na kwa wakati.
4. Zitakufanya ubaki ukiwa na motisha ya kufanya makubwa kwa wakati wote.
Je, wewe ndoto zako kubwa ni zipi?
Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Imethibitishwa. Mbinu Za Kitabibu Zinafaa Kutumika Katika Maisha Ya Kawaida Ya Kila Siku
Hongera sana rafiki kwa kuiona siku hii ya leo. Ikiwa ni tarehe 29 AugustUkienda hospitali unaumwa utataja tatizo lako kwa mtaalamu wa Afya. Mtaalamu huyu wa Afya kwa kutumia ubobezi wake atakupima au atakusikiliza tu na kisha kutoa dawa.Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa wataalamu wa afya wa hospitalini ila kwa leo napenda tuyajue haya mawili ambayo yamethibitika kufanya kazi kwenye maisha ya kawaida.
Kinapatikana kwa sh. 10,000/- KWANZA, mtaalam wa Afya atakupa dawa kulingana na ugonjwa wako. Haijalishi unaipenda au huipendi. Haijalishi unampenda yeye au humpendi yeye. Ile dawa unapaswa kuitumia.Sasa kwenye maisha ya kila siku. Imethibitika kwamba ukweli wa jambo fulani ukitolewa. Haijalishi unaupenda au huupendi. Haijalishi unampenda aliyeutoa au hupendi aliyeutoa ukweli unabaki kuwa ukweli tu. Na huna budi kuufuata. Hivyo jitahidi kuanzia leo kuuchukua ukweli na kuufanyia kazi bila kujali umetolewa na mtu aliye juu ya wewe au aliyechini. Ukweli unabaki kuwa ukweli siku zote.Mfano wa ukweli ambao utapaswa kuukubali ni huu hapa.Huwezi kutatua matatizo kwa namna ile ile ya kufikiri iliyosababisha matatizo.Huwezi kuondoka kwenye madeni kama utaendelea na fikra zilezile ulizokuwa nazo wakati wa kukopa. Huu ni ukweli. Na hivyo utapaswa kuchukua hatua za tofauti ili uweze kuondokana na madeni.Kama fikra zako zilikuwa kwamba madeni katika maisha hayaepukiki, basi sasa unapaswa kufahamu kwamba madeni ni utumwa. Ukianza kuyaona madeni kama utumwa ujue kwamba umetokea kuona vitu kwa namna ya tofauti ambayo ulikuwa hujaitumia hapo awali.PILI; Mtaalamu wa afya akishagundua kwamba una ugonjwa fulani atakupa dawa ambazo utazitumia kwa maelekezo yake. Anaweza kukupa maelekezo kwamba utumie hizo dawa mara tatu kwa siku. Au utumie dawa hizo mara mbili kwa siku. Kama kweli upo makini na afya yako basi utafuata maelekezo ya daktari bila kipingamizi ili uweze kupona.Sasa imethibitishwa kwamba kuna dozi unahitaji ili uweze kufanya mambo ya tofauti.1. Dozi ya kusoma vitabu mara tatu kwa siku. Kama kwa siku unaweza kupata muda wa kula mara tatu mfululizo bila kuacha sasa unashindwa nini kusoma vitabu mara tatu mfululizo. Soma vitabu asubuhi, mchana na jioni kama vile umepewa dozi kutoka kwa mtaalamu wa afya.2. Fuata maelekezo mpaka upone. Hakuna daktari anayekwambia tumiatumia hii dozi ukijisikia kupona achana nayo. Sharti ni kwamba dozi lazima iishe. Vivyo hivyo kwako. Ukitaka kupata matokeo ya tofauti sharti lazima ukubali kulipa gharama na kuvumilia mpaka mwisho.Hizo ndizo mbinu za kitabibu zilizothibitishwa kufanya kazi kwenye maisha ya kawaida.KUMBUKA: utapaswa kuupokea ukweli kama ulivyo na kuufanyia kazi, lakini pia utapaswa kufanyia ukweli huo mwanzo mpaka mwisho.Jiunge nami kwenye kundi la THINK BIG FOR AFRICA ili tuambizane ukweli na kuchukua hatua kila siku.Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

