Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Utafanyeje Unapokuwa Na Wazo La Kufanya Biashara Ila Huna Mtaji

    Rafiki yangu, leo nataka niongee na wewe na kwa namna ya kipekee sana. Najua kwamba kuna vijana wengi huko mitaani ambao wana ndoto za kufanya makubwa. Vijana ambao wana ndoto za kuanzisha biashara ila tatizo au kisingizio wanasema,ni kwamba hawana mtaji.

    Je, ni kweli kwamba tatizo lako ni mtaji. Je, ni kweli kwamba hauna mtaji wa kukutosha kuanzisha biasahra?

    Siku ya leo nataka nikupe mfano kidogo tu wa mnyororo wa chakula. Hiki kitu tulijifunza shule ya msingi

    Kwenye mnyororo wa chakula ni kwamba mnyama aliye juu kwenye myororo wa chakula anakula mnyama aliye chini yake.

    Mahindi yanaliwa na panya na panya analiwa na Bundi

    Karoti zinaliwa na Sungura na sungura analiwa na mbwa mwitu na mbwa mwitu wanaliwa na simba

    Sasa nataka kusema nini kwa kuonesha hivi vitu. Nataka nikwambie kwamba, kama una wazo la biashara au la kufanya kitu chochote kile ila huna mtaji, maana yake una NDOTO KUBWA.

    Kitu hiki siyo kibaya maana mara zote nimekuwa nakusisitiza wewe uwe na NDOTO KUBWA kweli.

    Ila sasa unataka uwe Simba wakati hujafikia hivyo viwango Unapokuwa na ndoto kubwa unapaswa kuwa tayari kuanzia chini na kupanda juu. Siyo utake kuanzia juu kwa juu.

    Yaani, ni sawa na kwamba uwe SUNGURA kwenye mnyororo wa chakula halafu eti utake kumla MBWAMWITU.

    Kubali kwamba kwa sasa wewe ni SUNGURA na kula majani. Baadaye ukifikia hatua ya USIMBA utakula hao mbwa mwitu bila tatizo lolote.

    Hiki ni kitu ambacho unapaswa kukipokea, kwa sababu pia vijana wengi hawapendi kuanzia chini. wengi wanapenda kuanzia juu kwa juu. Unakuta kijana ana ndoto ya kuanzisha biashara na anakwambia kwamba yeye anataka kufanya biashara ya mtaji wa milioni 200. Sasa wewe unafanyaje biasahra ya mtaji wa milioni mia mbili wakati hata mtaji wa milioni moja unakushinda kuuendesha vizuri? Unafanyaje?

    Kiukweli kubali kuanzia chini.kisha kubali kukua kidogokidogo, mpaka mwisho.

    KILA LA KHERI

    Umekuwa nami

    Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE CONSULTANCY

    Tuwasiliane kwa 0755848391

    Morogoro-Tz

    NB: Hakikisha kwamba umepata kitabu changu cha NGUVU YA WAZO NA KITABU CHA MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA. Vitabu hivi viwili vitakusaidia sana wewe kuweza kufika mbali kwenye kufanyia kazi wazo lako na hata kupata mtaji wa kuanzia kwenye kufanya biashara. Upo tayari nikutumie vitabu hivi viwili? Upo tayari?

    TUma elfu kumi leo nikutumie ebooks zote mbili. Wahi sasa hivi.

    Tuma kwa 0755848391 jina ni Godius Rweyongeza. Akhsante

  • Mwongozo kwa wapambanaji (Hustlers Guide)

    Leo nataka nitoe mwongozo maalumu kwa mtu yeyote ambaye anapambmana kufikia mafanikio makubwa sana.

    Kama unapambana kufikia mafanikio makubwa hakikisha kwamba

    1. una malengo na unayafanyia kazi kila siku bila ya kuchoka

    2. unajihusisha na watu sahihi, watu chanya na watu ambao wanaendana na wewe. Watu hasi watakuangusha

    3. unaangalia namna ya kubadili ndoto yako kuwa huduma. Angalia namna ambavyo unaweza kuwasaidia watu kutatua matatizo yao kwa kujenga huduma nzuri kwenye ndoto yako. Kumbuka usemi wa Zig Ziglar unaosema kuwa “unaweza kupata chochote unachotaka kwa kuwaswaidia watu kupata kitu wanachotaka.”

    4. Kila siku piga hatua haka ni hatu ndogo, kuelekea kwenye mafanikio yako.

    5. Usiache kusoma kitabu kila iitwayo leo. Tena anza na hiki hapa chaMAAJABU YA KUSOMA VITABU. kinapatikana bure tu.

    6. Jifunze kutoka kwenye makosa ambayo umewahi kufanya siku za nyuma. Usirudie makosa yaleyale kila mara.

    8. Usitake kujionesha kwamba wewe ni mtu wa aina fulani. Acha vitendo tu vikuoneshe

    9. Fanya mazoezi ya kutosha nyuma ya pazia kabala hujatokea kuonekana mbele ya watu. Yes, fanya mazoezi ya kutosha rafiki yangu.

    10. Fanya mazoezi kiasi kwamba ukionekana mbele ya watu, watu wafikri kuwa wewe kipaji chako cha asili, kumbe nyuma ya pazia wewe unapiga kazi kwa namna ambavyo hakuna mtu anajua.

    Hiki siyo kitu cha ajabu, akina Ronaldo hawa unaowaona wanafanya vizuri uwanjani nyuma ya pazia wanafanya mazoezi ya kufa mtu. Akina Diamond hawa unaowaona wanatoa nyimbo mara kwa mara, nyuma ya pazia wanarekodi nyimbo nyingi kuliko unavyoweza kutazamia. Ila chache unazoziona ni hizo. Wanafanya mazoezi kwelikweli. Na wewe fanya hivyo.

  • Jinsi Ya Kubadili Mwelekeo Wa Kile Umachofanya Bila Kuathiri Matokeo (True Story)

    Leo nimeikumbuka stori ya Sixto Rodriguez. Huyu ni mwanamziki wa kimarekani ambaye mwaka 1967 alirekodi wimbo wake wa kwanza. Na miaka mitatu baadaye ilikuja kurekodi albamu ambayo ilikuwa inajulikana kwa jina la cold fact.

    Mwaka mmoja baadaye alirekodi albamu nyingine ambayo ilikuwa ikijulikana kama coming from reality. Hata hivyo, hizi albamu zake hazikufanya vizuri sana kiasi kwamba ile label yake iliyokuwa imemsajiri iliamua kuachana naye. Kipindi hicho alikuwa katika harakati za kurekodi albamu nyingine na alikuwa tayari amerekodi nyimbo tatu. 

    Kwa hiyo hicho kitu kilimfanya aachane na muziki huku akianza kujishughulisha na kazi nyingine za kawaida nyumbani kwao. Taratibu alipotea kwenye chati ya mziki wa Marekani.

    Ilitokea kwamba kulikuwa na binti ambaye alienda kumwona mchumba wake Afrika kusini. Akawa ameenda na albamu ya Rodriguez AFRKA KUSINI

    Akiwa huko wakawa wanacheza nyimbo za Rodriguez na watu wakaanza kuzikubali. Ghafla albamu yake ilikuwa miongoni mwa albamu zenye  uhitaji mkubwa zaidi Afrika kusini. Hii ilitokana na ukweli kuwa miongoni mwa nyimbo zilizokuwa kwenye albamu ya Rodriguez zilikuwa za kiharakati, halafu kipindi hicho nchi ya Afrika kusini ndio ilikuwa kwenye harakati za ukombozi wa mtu mweusi.

    Hivyo ilibidi shirika moja lianze kuchapa na kusambaza nyimbo  zake kulingana na uhitaji wake. Kutokana na umaarufu wa nyimbo zake watu waliamua kumtafuta mwanamziki huyo ili aweze kuja Afrika kusini kufanya show kwa mashabiki wake wa muziki. Hata hivyo hakuna mtu aliyekuwa anajua habari zake. Baadaye ilikuja kusambaa miongoni mwa watu kwamba mwanamziki huyu alijiua baada ya albamu zake kutofanya vizuri.

    Lakini mwanahabari mmoja hakuamua kuchulia kitu hiki kama kilivyokuwa kinasambazwa na watu. Hivyo aliamua kuanzisha tovuti ambayo lengo lake lilikuwa ni kumtafuta mwanamziki huyu tu. Siku moja mtoto wa Rodriguez akiwa anapita mtandaoni aliona hiyo tovuti ambayo ilikuwa imelenga kumtafuta mwanamziki huyo. Aliandika pale kwenye ile tovuti kwamba Rodriguez ni baba yangu, na ninamaanisha hilo. Akawa ameacha mawasiliano yake. Baadaye alipigiwa simu na mipango ya Rodriguez kwenda Afrika kusini ilifanyika. 

    Habari zilisambaa sana kwamba legendari wa mziki alikuwa hai na alikuwa anakuja Afrika kusini. Watoto wa Rodriguez walikuja na baba yao ila hakuna mtu hata mmoja aliyekuwa anatazamia kukutana na watu wengi kwenye hiyo show. Sio hata Rodriguez mwenyewe.

    Ila cha kushangaza walipofika Afrika kusini walishangaa kukuta watu 5000 na tiketi zilikuwa zimeuzwa zote na kuisha. Rodriguez aliposimama kwenye jukwaa alishangiliwa na watu waliokuwepo kwa dakika 10 mfululizo (10 minutes standing ovation).

    Kumbe umaarufu wake Afriks Kusini ulikuwa ni mkubwa sana kuliko mtu msanii mwingine nchini Marekani. Na alikuwa tayari ameuza nakala za albamu yake kuliko wasanii maarufu wa kipindi hicho kama Bob Dylan na Cat Stevens.

    Nyimbo za Rodriguez zinatupa picha ya jinsi kitu kinaweza kukataliwa nyumbani, lakini kikaja kukubalika ugenini, kisipokubalika leo hii basi kinakuja kukubalika kesho. Lakini ili kiweze kukubaliwa utapaswa kuhakikisha umekifanya na kukimaliza.

    Lakini pia ni funzo kubwa kwamba usikate tamaa mapema. Kuna wakati unapaswa kubadili mwelekeo kwa sababu kule ulipokuwa umeleekeza mwanzoni siyo sehemu sahihi. 

    Naipenda sana hii picha ya mvuvi. Huyu jamaa, baadaye anaweza kukata tamaa, lakini kumbe issue hapa siyo kukata tamaa, issue ni kubadili mwelekeo kidogo tu na mambo mengine yote yakakaa sawa.

    Kwa Rodriguez muziki wake haukubalika nchini mwake. Lakini, kumbe kuna sehemu muziki wake ulikuwa unahitajika. Kazi yako kubwa ni wewe kujua wapi watu wanahitaji kazi zangu.

    Kazi yako ni kusoma mazingira ili ukiweka chambo, samaki wanase.

    Anyway, leo vipi? Angalia hii video yangu hapa youtube kisha usubscribe.

    Mpaka wakati mwingine. Mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE

    0755848391

    Morogoro-Tz

  • Usiishie tu kukaa kwenye kochi na huku ukisema, ONE DAY YES!

    Kwa jinsi hii hata kama una ndoto kubwa hazitaweza kutimia. Kitu kikubwa ni wewe kuchukua hatua ili uweze kufikia malengo na ndoto zako. Hakuna ndoto kubwa inatimia ukiwa umekaa kwenye kochi. Huwa napenda kusema hata watu ambao wanapata lift siyo wale waliokaa nyumbani wakiisubiri, bali wale wanaokupa barabarani wanaendelea na safari.

    Wakati unasema, ONE DAY YES vitendo vyako pia vioneshe hilo
    #FANYA #onedayyes #inawezekana #songambele #usirudinyuma #hainakufeli #godiusrweyongeza

  • Jinsi Teknolojia Kidogo Inavyoweza Kuleta Mabadiliko Makubwa Kwenye Biashara

    Siyo kwamba mara zote utahitaji kuwa wa kwanza kufanya kitu fulani ili ufanikiwe.

    Ukweli ni kwamba muda mwingine utahitaji ubunifu kidogo. Au utahitaji kuweka teknolojia kidogo tu na kubadili kila kitu.

    Mfano Amazon, ujue wazo lao la kuuza vitabu halikuwaa jipya au hata bidhaa nyingine walizokuja kuuza baadaye.
    Watu walikuwa wananua na kuuza vitabu kabla yao. Kampuni ya WARMART ulikuwa unafanya hiyo biashara.

    Wenyewe walichofanya ilikuwa ni kuongeza teknolojia kidogo tu kwenye kitu kilichokuwepo.

    Waliona kweli watu wanahitaki kusoma vitabu, ngoja niongeze teknolojia kidogo tu niwasaidie watu kupata vitabu mtandaoni.

    Kitu kilichokuwepo kikapewa teknolojia na watu wakakipenda sana.

    Wewe pia huhitaji kuwa wa kwanza ili ufanye makubwa. Kwanza ukiwa wa kwanza kabisa watu wanaweza hata wasinunue bidhaa ZAKO.

    Matatizo ya watu ni yaleyale unachohitaji wewe Ni

    Kuongeza teknolojia kidogo kwenye kitu ambacho watu wamekizoea.
    Watu wamezoea kusoma vitabu, unawawekea mtandaoni. GETVALUE, AMAZON.

    Watu wamezoea kutafuta taarifa, warahisishie upatikanaji. GOOGLE, BING

    Watu wanapenda kuwasiliana wape nAmna ya kuwasiliana. APPLE, SAMSUNG, AMAZON, TECHNO

    Watu wanapenda kuwatumia ndugu zao fedha, Ila sasa utumaji siyo wa kuamininika. Hivyo, watengenezee teknolojia nzuri ya kutuma na kupokea fedha. M-PESA

    Watu wanapenda kuangalia tamthiliya, ongeza teknolojia kidogo, Kisha wape movie za kutosha. NETFLIX.

    Watu wanasafiri, na teksi ni kitu muhimu kwenye usafiri. Wasaidie kupata teksi kwa haraka popote walipo. UBER

    Kwa hiyo nisikilize. Huhitaji hata kuwa wa kwanza kufanya kitu cha kipekee ambacho hakijawahi kifanyika. Angalia Vitu vilivyopo Sasa hivi. Kisha jiulize ni teknolojia gani kidogo naweza kuongeza hapa ikaleta matokeo ya tofauti.

    Na kwenye biashara yako hiyohiyo. Jiulize ni teknolojia gani unaweza kuongeza sasa hivi ikarahisisha upatikanaji wa huduma na kuongeza mauzo?

    Kama ipo, itumie.

  • Hii Ndio Gharama Halisi Ya Kufanikiwa. Upo tayari Kuilipa?

    Unaweza ukawa unajilinganisha na watu wengine na pengine kuona kama unachelewa  kufanikiwa ukilinganisha na wengine.

    Ila sasa usichokijua ni nguvu na juhudi lakini pia miaka ambayo hao watu wamekuwa wakifanya kitu ambacho wanafanya.

    Unawajua imewachukua miaka mingapi kufikia walipofikia?

    Ebu kwa mfano tuseme wewe ni kijana amayependa utangazaji, na  Salim Kikeke ni mtu unayetamani mafanikio yake!  Unajua miaka mingapi amekuwa kwenye industry ya utangazaji? Unajua?

    Ukifuatilia utagundua kuwa amekuwa  akifanya anachofanya kwa miaka mingi.

    Sasa swali langu kwako, upo tayari kulipa gharama unayotakiwa ili uweze kufikia kule unapotaka! Upo tayari? Upo tayari kukifanya kwa miaka yote kama ambavyo yeye amefanya

    Hapo Sasa ndio ujue kuwa mafanikio makubwa siyo rahisi, yanachukua muda.

    Na hili siyo kukuogopesha bali kukuonesha uhalisia wa kile unachotakiwa kufanya mpaka ufike kule unapotaka.

    Sasa leo nataka uangalie video hii niliyorekodi miaka Kama kumi iliyopita😂😂. Halafu, ukishaiangalia. Subscribe kwenye channel yangu pia.

    Mpaka wakati mwingine, mimini GODIUS RWEYONGEZA
    0755848391
    Morogoro-Tz

    NB: LEO nataka ufanye kitu kimoja tu, uangalie video ya gu yotote YouTube. Kisha usubscribe na kuwashirikisha wengine.

  • Maisha Ni Wajibu Wako

    Kama kila mtu akijenga utaratibu wa kuona maisha Kama wajibu wake tutafika mbali unajua kwa nini? Kwa sababu, ukianza kuona maisha kama wajibu wako utapambana kwa hali na mali kuweka kila Kitu sawa. Hutakuwa tena na muda wa kumlalamikia mtu KUWA Kitu fulani hakijakaa sawa au hakijafanyika.

    Unatumia mitaji hii kupata fedha, ambayo baadaye unaweza kuitumia kufanya kitu Cha maana.

    Napenda sana ule usemi wa Martin Luther King Jr. Anaosema kuwa kama kila mtu akifangia barabara dunia hii itakuwa safi Sana. Yaani, ebu fikiria hivi, kama kila mtu mtaani mwake akifagia mazingira yanayozunguka ya nyumba yake tu. Si mtaa wote utapendeza ndani ya siku moja? Si ndio?.

    Sasa na kwenye hili suala zima la ajira. Kama kila mtu akisema ngoja kwanza nipambane na hali yangu. Nifanye kile kinachoweza tu. Niamini mimi, ndani ya miaka mitano mpaka kumi tuna uwezo wa kutatua tatizo hili la ajira.

    Bado huamini tu? Sikiliza, kama kwa mfano wewe ulisema kwamba kuanzia leo, nitapambana nipate elfu mbili, elfu tatu, nne au tano na kuiweka akiba. Kila siku. Naamimi, kuwa baada ya miaka mitano, akiba yako hii ya elfu 2 kila siku. Itakuwa imekufikisha mbali. Tena siyo mbali kidogo, mbali sana tu.

    Hii ndio Dhana nzima ya kuona maisha Kama wajibu wako. Na siyo wajibu wa MTU mwingine. Siyo wajibu wa mjomba au babu!

    unahusika wewe mwenyewe bila kumtulia mtu lawama au kumtegemea mtu.

    Sikiliza, kuanzia leo hii, Anza kujitegemea.

    Usilalamike wala kumtupia mtu yeyote yule lawama. Kukitokea tukio. Jiulize ninahusikaje hapa kulitatua. Kama lipo nje ya uwezo wako achana nalo. Pambana na kile kilicho ndani ya uwezo wako.

    SOMA ZAIDI: Hivi Ndivyo Unaweza Kufanya Mishale Inayolenga Kukuangamiza Kuwa Baraka

    Kama umependa makala hii, utapenda pia Makala ninazotuma kwa njia ya baruapepe. Jiunge na mfumo wetu wa kupokea Makala kwa njia ya baruapepe kwa kujaza taarifa zako hapa chini

  • Mimi Nakuamini Sana

    Kama kuna mtu namwamini Basi, Ni wewe…
    Naamimi haukati tamaa
    Naamimi hauko tayari kurudi nyuma hata ukikutana na kikwazo
    Na hicho kitu ukiendeleze kila siku.
    Usikate tamaa na wala usirudi nyuma.
    Endelea kupambana.

    Kikubwa ujue malengo yako.
    Uyafanyie kazi kila siku hata kama ni kwa udogo

    Unaweza usione matokeo kwa muda mfupi, Ila Hilo kisikukatishe tamaa.

    Maana yajayo yanafurahisha.

    Ni Mimi
    Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE CONSULTANCY.
    Tukutane kesho
    0755848391

    Rafiki yangu, Kama umependa makala hii, utapenda pia mafunzo ninayotoa kwa njia ya baruapepe. Weka taarifa zako hapa chini, ili uwe miongoni mwa watu wanaopokea mafunzo yangu kwa baruapepe.

  • USHAURI: Jinsi Ya Kutunza Fedha Itakayokusaidia Kuanzisha Biashara

    Moja ya eneo muhimu sana kwenye maisha ya kila siku Ni fedha. Upende usipende fedha ni muhimu tena sana.

    Maana hakuna hata siku inapita bila ya wewe kutumia fedha.

    Ukiamka tu asubuhi, ujue kitanda ulichokuwa umelalia ni FEDHA.
    Ukivaa nguo zako, ujue umevaa fedha.
    Ukipata kifungua kunywa, ujue hizo ni fedha pia.
    Ukipanda daladala, hiyo nayo ni nini….

    Sikiliza sasa, fedha ni muhimu sana, kiasi kwamba baada ya hewa ya oksijeni ambayo tunaipata bure, fedha ndio inafuata kwa umuhimu…
    Sijui unanielewa hapo bwashehe….

    Sasa mbali na umuhimu wote huo wa fedha, bado kuna watu wanaifanyia masihala.
    Lakini wengine wanapata changamoto wanapokuwa na fedha.

    Fedha ni chanzo Cha furaha yote

    Na siku ya leo, nataka nitoe Ushauri kwa ndugu yangu na rafiki yangu Isack

    Anasema hivi

    Brother m n kijan delev bajaj nataman san kufug kuku ila kinacho nishind upend w kuifaz hela kutafut mtaj kilanikipat ela kidog matumiz yanaongezeka

    Isack kutoka Mbeya

    Ok vizuri sana ndugu yangu Isack. Kwanza nikupongeze kwa kuwa na ndoto na lengo la kufuga kuku.
    Maisha yanaanza na malengo. Maana vijana wengi wanashindwa kufanya makubwa kwa sababu tu hawana ndoto wala malengo makubwa

    Ili uvuke hiki kizungumkuti unapaswa kuwa na malengo au ndoto kubwa.

    Labda ka ushauri kidogo tu kuhusu ndoto Yako. Usiishie tu kusema natamani kufuga kuku. Bali iweke sawa ndoto yako katika namna ambayo itakusuma zaidi

    Kwa Mfano, ndoto Yako ikiwa ni kuwa mzalishaji na msambazaji nambari moja wa mayai kwa mbeya nzima.
    Au mzalishaji nambari moja wa kuku wa nyama mkoa wa mbeya au hata nyanda za juu Kusini.
    Yaani, kwamba ujenge jina kiasi kwamba yakizungumziwa mayai mkoa wa mbeya, au kuku wa nyama, basi jina Isack ndio liwe la kutajwa masikioni mwao.

    Ni kweli hii ni ndoto kubwa, Ila sasa ubora wake ni kwamba unaweza kuanza kuifanya hata kwa udogo. Lakini pia hii ndoto itakusukuma siyo tu, uanze kufuga kuku. Bali utaenda zaidi ya hapo. Ujue ukiwa na lengo la kufuga kuku, hata baadaye ukijenga bada na kufuga kuku kumi tu, utaona Ni sawa. Ila Unapokuwa unajua mkoa mzima wa mbeya unakutegemea wewe kwa ajili ya mayai, au nyama ya kuku. Hapo utaweka juhudi zaidi.

    Sasa tuongelee upande wa fedha.

    Ili uweze kufanikishaa ndoto yako hiyo, jua wazi kuwa fedha haikwepeki. Utahitaji fedha tu. Na sehemu ya kuanza kupata fedha ni hiyo kazi uliyonayo. Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu, nataka wewe uvunje rekodi ya KUWA dereva wa Bajaji wa kwanza, kutoka kwenye udereva mpaka kujenga ngome kubwa.

    Unajua utaendaje. Fuatilia kwa umakini hapa

    Kila siku kwenye kazi yako, jiwekee kiwango ambacho utakuwa unaweka akiba kuanzia leo. Kwa mfano, labda unaweza kuniambia nitaweka akiba ya elfu kumi kila siku. Kwa hiyo, kwenye kazi yako utakayokuwa unafanya utapaswa ujitume kwanza upate pesa uliyokuwa unapata kawaida, lakini pia utapaswa ujisukume uweze kutengeneza fedha ya ziada ya akiba, ambayo ni elfu kumi.

    Najua lengo hili linaweza kuwa kubwa, lakini sasa hakuna jinsi. Kwa sababu kwanza umeshakuwa na ndoto kubwa, wewe pia unapaswa ujitume kiasi cha kutosha, ili hii ndoto yako uweze kuifanikisha. La sivyo, itabaki KUWA ndoto ya Habunwasi.

    Ndoto kubwa zinahitaji kujitoa. NDOTO KUBWA ZINAKUHITAJI ULIPE GHARAMA. Na hii ni gharama mojawapo.

    Kwa hiyo basi, kwa mpango huu maana yake, Kuna wakati utalazimika kuamka mapema sana kwa ajili ya kuanza kazi. Utalazimika kuwasiliana na watu mbalimbali ambao unawajua huwa wanasafiri kutoka eneo moja kwenda jingine, ili uwachukue wewe wakupe fedha.
    Utalazimika kuacha kuangalia mechi hata kama ulikuwa unaipenda ili upige kazi ya kukuingizia kipato.
    Na hata mchepuko wako,…au basi, utajua mwenyewe unafanyaje na mchepuko wako.

    Bwana Isack nataka uanze kufanya hivi vitu kitalaam zaidi. Yaani, usiishie tu kutafuta hela na kuweka akiba chini ya godoro.


    Hapa chini Kuna maeneo matatu ambayo napendekeza uweze kuweka akiba yako.


    Nenda benki kafungue akaunti
    . Kisha weka utaratibu wa kuweka kiwango cha akiba ulichopanga.
    Ubora siku hizi benki zimerahisisha. Unaweza kuweka fedha benki ukiwa hata mtaani kwako. Au pale kijiweni baada tu kumshusha abiria…
    Sijui unanielewa….

    Kuna baadhi ya benki pia zinaruhusu wewe kufungua akaunti kwa mawakala. Hili nalo ni bao kisigino ndugu Isack. Kumbe haulazimiki tena kupanga foleni benki ili ufungue akaunti. UNACHOHITAJI NI KUDANDIA TEKNOLOJIA KIHIVYO.

    Ukishafungua akaunti, hiyo hiyo kadi ya benki hiyo. Unaweza hata kuituma kwa bibi yako kijijini. Maana, kadiri unavyoendelea kuweka akiba najua utashawishika kwenda kuitoa fedha ukiwa na kadi. Ni Bora uitume Kijijini kwenu, au la unaweza kuiharibu kadi kabisa. Siriazi. Ujue hapa ninaongelea Mambo siriazi kwa ajili ya malengo na ndoto zako.

    Ukikaa na hiyo kadi utashawishika kwenda kutoa fedha benki siku ukikutana na changamoto kidogo. Ila kama kadi huioni, itakusaidia usitoe pesa yako kwa haraka.

    Kwa hiyo, unaweza kuiharibu kadi, ukifika wakati wa kutoa fedha benki utaomba kurenew kadi yako.

    Ngoja ninywe maji kwanza, kabla sijaendelea…

    Enhee, sasa bwana Isack, ukiachana na kungua akaunti benki. Unaweza kufungua akaunti UTT.
    UTT, Ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja ulio chini ya serikali ambao unawawezesha watanzania wenye fedha kidogo kuzikusanya kwa pamoja. Ambapo hizo fedha baadaye zinawekezwa kitalaam. Kwa fedha yako unayoweka, baadaye ukija kuitoa, unaitoa na faida.

    Tena badala ya kufungua akaunti benki, Bora ufungue akaunti UTT mfuko wa Umoja. Au wewe unaonaje?

    Huku fedha yako inakaa, Ila siku ukiihitaji, utajaza fomu, na itachukua siku saba tu kuipokea

    Ukiona maelezo ya UTT huyaelewi vizuri hapa, unaweza kuwatwangia jamaa wa UTT wenyewe kwa namba hii 0754800455. Watakupa kizima. Halafu namba yenyewe unapiga bure bila hata kulipia . Yaani, hata kama hauna bando sasa hivi, ukipiga inaita na unaongea nao, labda ukipiga muda ambao siyo wa kazi mzee baba.

    Sijui niendelee…au niishie hapa

    Ngoja niendelee, kwanza…

    Ukiona mizunguko yote hiyo mirefu basi kafungue laini ya simu maalumu kwa ajili ya kuweka akiba tu. Halafu unajua utafanyaje. Ukishafungua hii laini ya simu. Mfuate mtu wako wa karibu, labda mama, baba, mke, rafiki au yeyote unayemwamini. Utamwambia aweke namba ya siri.

    Kwa hiyo, wewe utakuwa na laini, labda tuseme yenye Mpesa. Ila hujui namba ya siri. Utakuwa unaweka akiba kila Mara, Ila siku ukija kutoa fedha, utapaswa kuomba namba ya siri kwa mtu aliyekusaidia kuweka namba ya siri.

    Mtu huyu unapaswa kumshirikish lengo na umwambie asikupe namba ya siri mpaka utakapokuwa umefikisha kiwango fulani Cha pesa.

    ONGEA naye, kuwa mimi nataka niweke akiba ya milioni tatu kwenye hii laini. Tafadhali usiniambie namba ya siri mpaka nitakapokuwa nimeweka kiasi Cha milioni tatu kama akiba.

    Siku nikikuonesha kuwa nimeweka milioni tatu kama akiba. Basi hapo ndipo utapaswa kuniambia namba ya siri.

    Naona maji yangu ya kunywa yameisha, na Mimi naacha kuandika, ngoja nikatafute maji ya kunywa kwanza.

    Halafu sikiliza kwanza
    Hapa nina orodha, ya vitabu vitakavyokusaidia wewe Kufanikisha haya yote niliyoandika leo.

    1. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA
    2. MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE
    3. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO

    Kupata vitabu hivi, wasiliana nami kwa 0755838391.

    Mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE CONSULTANCY
    0755848391
    Morogoro-Tz

    Una swali, maoni au ushauri? Kuna jambo linakutatiza, unataka ushauriwe?

    Basi sikiliza, tuandikie chini


    .
     


    Nenda benki ufungue akaunti.
    Kisha Anza kuweka fedha

    Fungua laini ya simu ya kuweka AKIBA tu

    Thibutu matumizi yako

    Kusanya kiasi Cha kutosha kuanza kuwekeza.

  • MAISHA NI KAMA KUENDESHA BAISKELI..

    Leo nimeukumbuka usemi wa Albert Einstein. Anasema maisha Ni Kama kuendesha baiskeli, ili usianguke unapaswa kuendelea kunyonga.

    Ukiacha tu, unaanguka

    Hivi ndivyo ilivyo hata kwenye maisha ya kutafuta…

    Ili uendelee kusongambele haupaswi kuacha kuweka juhudi, haupaswi kuacha kupiga kazi kwa bidii, kujituma, kufanyia kazi malengo yako kila siku.

    Hivi ndivyo maisha yalivyo.

    Ukikata tamaa, Basi…hutoboi..

    Kama umependa Makala hii, utapenda Makala zaidi nikazotuma kwa njia ya barua pepe… Jaza taarifa zako zote hapa chini

X