Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Jinsi Ya Kupakua Vitabu Bure Mtandaoni-2

    Kama umekuwa unajiuliza unawezaje kupakua vitabu mtandaoni, leo nimekuja na maelekezo yanayojieleza moja kwa moja kuonesha namna ambavyo unaweza kupakua vitabu mtandaoni.

    Kuna video ya kwanza ambayo ilitangulia hii.
    Kwa hiyo unaweza kutumia video hii ya kwanza au ukatumia video hii ya pili.

    Ila sana sana nashauri utumie hii ambayo nimekushirikisha hapa.

    Kila la kheri.

  • Jinsi Ya Kuanzisha Biashara Bila Mtaji Tanzania

    Utangulizi

    Vijana wengi wamekuwa wakitamani kuanzisha biashara zao ila sasa wamekuwa wanakwama jinsi gani ambavyo wao wenyewe wanaweza kuanzisha hizo biashara bila ya mtaji.  Kila  ninapoongea na vijana nagundua kuwa wapo wengi wenye ndoto kubwa za kufanya makubwa ila kuna ambao kama bado wamefungwa hivi. Na kitu ambacho kimewafunga walio wengi ni kufikiri kuwa bado unahitaji mtaji fedha mkubwa ili kuanzisha biashara.

    Zama Zimebadilika

    Kwenye zama za viwanda mtaji fedha kilikuwa kitu muhimu sana kilichokuwa kinahitajika. Ili kununua vifaa na kila kitu kilichokuwa kinahitajika viwandani, ulipaswa kuwa na fedha nyingi za kukusaidia kufanikisha hilo.

    Ila sasa mabadiliko mengi yanetokea kwenye zama za sasa. Ni kweli bado kuna biashara ambazo bado zinahitaji mtaji fedha mkubwa. Ila pia kuna biashara ambazo zinahitaji mtaji fedha kidogo na nyingine hazihitaji mtaji fedha kabisa.

    Kama huwezi kuanza biashara kwa ukubwa, Anza kwa udogo

    Kwa kawaida watu huwa hatukosi visingizio. Watu wana visingizio kwa nini maisha yao ni mabaya, kwa nini hawajatoboa…
    Kuna watu wana kisingizio mpaka kwa nini hawakuwahi kulala jana usiku, wakati walikuwa wanaangalia tamthiliya, loooh!

    Ngoja nikwambie kitu, visingizio haviwezi kuleta chakula mezani. Unachopaswa kufahamu wewe ni kwamba, pale unapogundua kuwa una ndoto kubwa au lengo kubwa la kufanya biashara,  ila kwa sasa unaona  mtaji fedha hautoshi.

    Fanya hivi, amua kitu kimoja. Amua kwamba ninaenda kufanya hiki kitu hata kama Ni kwa udogo.
    Kama huwezi kufanya kitu kwa ukubwa, amua kukifanya kwa udogo. Huwezi kushindwa vyote.

    Juzi nilikuwa nasoma ujumbe wa Ryan Holiday. Kwenye ujumbe huo akawa anaeleza kwamba alikuwa na ndoto ya kuanzisha duka la vitabu.  Ila alipoingia mtandaoni akaona gharama zilizokuwa zinahitajika kifungua duka la vitabu ni kubwa, akaamua kuwa kwa lengo lake ni kuanzisha duka la vitabu. Bado tu atapaswa kulianzisha Hilo duka. Na kwa kuwa hawezi kuanzisha duka la vitabu kwa ukubwa , anaweza ataanza kwa udogo huohuo alionao. Na atautumia udogo huohuo kuwafyekelea mbali washindani wake.

    Unaona eeh…

    Yaani, kwake hiyo ikawa tayari fursa…

    Na wewe udogo wa mtaji wako ni Fursa.

    Badala ya kufikiri uanzishe biashara itakayoshughulika na kila kitu. Anzisha biashara ambayo utajikita kwenye kitu kimoja au viwili ambavyo vinapendwa sokoni. Kisha pambana….

    Nakumbuka mwaka mmoja wa nyuma hivi nilikuwa naongea na rafiki yangu Edius Katamugora.

    Akawa ananiambia kuna mtu ana duka la vitabu linalouza kitabu kimoja tu…

    Yaani, yeye ukiingia kwenye duka lake unakutana na aina moja ya kitabu. Kama ni KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI, Ni hicho tu. Kama ni JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO ni hicho tu.

    Binafsi nimewaona watu wanaouza vitabu vya mwandishi mmoja tu.

    Kwa hiyo Kama mtaji fedha kwako bado ni tatizo, FIKIRI TENA! Kuna njia nyingi ambazo unaweza kuanzisha biashara kwa udogo au hata bila mtaji kabisa.

    Nadhani kinachokukwamisha wewe siyo mtaji
    Maana mitaji unayo ya kutosha. Kinachokukwamisha wewe ni udhubutu.

    Ungana na watu wenye mitaji

    Kuna watu wana mitaji ila hawajui wanaweza kufanya nini. Unaweza kuungana na hawa watu na wenyewe wakakupa fedha. Hata hivyo, kwenye hili unapaswa kuwa umeonesha uaminifu wa hali ya juu. Vijana wengi wa siku hizi siyo waaminifu.

    Nakumbuka mwaka juzi tu, kijana mmoja ambaye binafsi nilikuwa namfahamu vizuri. Alikusanya vijana wengine wanne, hivyo jumla wakawa watano. Wakaja na wazo la kuanzisha kampuni ya kilimo cha mboga. Wakaenda kwa mtu mwenye mtaji fedha Sasa. Wakampanga akapangika…

    Wakakubaliana makubaliano ya kwanza…
    Wakaelekezana kuwa vijana wale watano wangekuwa na umiliki wa asilimia 60 ya kampuni wakati mwekezaji akichukua asilimia 40.

    Mipango ya kulima kitaalamu ikawekwa wazi na kazi ikaanza…

    Kazi ilianza wakati mipango mingine ya kukamilisha kusajili kampuni ikiendelea..

    Yule mwekezaji akatoa milioni saba ya kwanza na kumpa kiongozi wa wale vijana… Mara baada ya kiongozi kupokea hiyo fedha akatokomea kusikojulikana na hiyo fedha. .
    Akawaacha wenzake solemba…

    Mpango ukashindwa kufanyiwa kazi tena…

    Moja ya zao walilopaswa kulima mwaka huo lilikuwa ni nyanya…
    Na ninadhani sote tunakumbuka nyanya ilivyokuwa dili mwanzoni mwa 2020… Ila jamaa alishatokomea

    Ninachotaka kusisitiza hapa ni UAMINIFU. Ukimpata mtu wa kuwekeza fedha kwako, zitumie vizuri fedha zake na kwa uaminifu.

    Ukifanya vitu vidogo, kwa uaminifu vina uwezo wa kukufikisha mbali….

    Tumia Mali kauli


    Unaweza pia kutumia mali kauli kwenye kuanzisha biashara. Ukawa unachukua bidhaa za wafanyabiashara dukani kwao na kuziuza kwa faida kidogo, kisha ukawarejeshea fedha za bidhaa walizokupa.

    Na hapa pia bado unapaswa kuwa mwaminifu.

    Kama wewe siyo mwaminifu, Anza walau leo…

    Kila la kheri..
    Umekuwa nami
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Jinsi Ya kupakua vitabu bure mtandaoni

    Mara kwa Mara nwatu wamekuwa wakiniuliza mi kwa jinsi gani wanaweza kupakua vitabu mtandaoni.

    Wengine huwa wananiomba niwattumie vitabu fulanifulani.

    Binafsi huwa sipendi kumtumia mtu kitabu wakati najua anaweza kukipata mwenyewe. Ni mpaka pale ninapokuwa Nina uhakika kuwa huyu mtu hawezi kukipata kitabu fulani ndio namtumia.

    Kwa leo sasa ningependa wewe ujue namna unavyoweza kupakua vitabu bure mtandaoni.

    Kesho tutakuwa na sehemu ya piili inayoonesha namna ya kupakua vitabu mtandaoni

  • Kitu kimoja kinachounganisha washindi wote

    Kama una ndoto za kuwa mshindi na kufanya makubwa unapaswa kufahamu kitu hiki kimoja ambacho kinaunganisha washindi wote na watu wote ambao wanafanya makubwa.

    Kitu hiki ni kuwa na ndoto kubwa.

    Na siyo ndoto kubwa tu, bali ndoto kubwa ambazo wapo tayari kuzifanyia kazi mpaka zikatimia.

    Bila ya kuwa na ndoto kubwa utakosa msukumo wa kufanya makubwa na hata utashindwa kufika mbali.

    Kuwa na ndoto kuwa na kuwa tayari kulipa gharama ili uifikie.

    Kuwa na ndoto kubwa Kama vile utaishi milele na ifanyie kazi leo, kama vile unakufa kesho.

    Je, wewe ndoto kubwa ya kwako ni ipi?

  • AMRI KUMI ZA MAISHA

    Huwa likitajwa neno Amri mara nyingi huwa linahusishwa na Amri za Mungu ambazo ndizo amri maarufu. Leo nataka nikwambie pia amri za maisha. Hizi amri hizi hakuna mtu yeyote ambaye anakubembeleza kuzifuata au kuzivunja. Ni au unazifuata kwa faida yako au unazivunja kwa hasara yako.

    Kama umewahi kusikia usemi kwamba malipo ni hapahapa duniani. Ukizifuata  amri hizi malipo yake unayapata hapahapa duniani na ukizivunja, unalipwa hapahapa duniani.

    Hizi amri hizi hazina cha kusubiri mpaka moto milele ili kuadhibiwa. Adhabu yake ni papo kwa hapo au baadaye kidogo, lakini adhabu yake haisubirishwi wala zawadi yake siyo ya kusubiri pepo, ni hapahapa duniani.

    AMRI YA KWANZA: UTAVUNA ULICHOPANDA ( Hii pia inatokea kuwa ndio amri kuu kwenye hizi amri za maisha).

    Kulingana na amri hii ni kwamba huwezi kupata kitu, tofauti na vile unavyostahili kupata. Unavuna kile ulichopanda. Huwezi kupanda maharage, baadaye ukaja kuvuna mahindi. Haiwezekani.

    Kulingana na amri hii ni kwamba pale unapokuwa unataka matokeo fulani, basi panda mbegu inayoendana na matokeo unayotaka.

    Kama unataka karanga, panda mbegu ya karanga.
    Kama unataka utajiri panda mbegu ya utajiri. Kama unataka mahusiano mazuri basi panda mbegu yake.
    Unavuna ulichopanda.

    Ikitokea kwamba, ukataka kwenda kinyume na hii amri. Ukweli ni kwamba utaishia kuadhibiwa maana malipo ni hapahapa duniani.

    Ukienda kuvuna mahindi pasipo kupanda maana yake utakuwa umevunja hii amri na mwisho wa siku utapaswa kuadhibiwa kama mwizi.

    Ukitaka utajiri bila kupanda mbegu yake maana yake utakuwa umeenda kinyume na asili na utakuwa fisadi. Na malipo yake ni hapahapa duniani.

    Kama Kuna kitu unapaswa kufahamu ni kwamba mara zote na sehemu zote utavuna ulichopanda.
    Ukitaka matokeo fulani, basi panda mbegu zake.

    AMRI YA PILI: KITU CHOCHOTE KIKIRUSHWA JUU, KITARUDI CHINI

    Hii ni kanuni ya fikizia lakini inatokea kuwa ndiyo kanuni ya asili pia. Si unajua kuwa fizikia ndio tawi kongwe kwenye matawi yote ya masomo. Fikizikia ilikuwepo tangu uumbaji au wakati wa Bing bang.

    Kanuni hii ukiijua utaifurahia sana. Na ubora hakuna mtu anayekulazimiaha wewe kuifuata. Ni au unaifuata wewe kwa faida yako au unaachana nayo kwa hasara yako.

    Ukiivunja amri hii kwa kupanda juu na kujirusha chini, utavunjika. ukiifahamu amri hii maana yake utajua wapi unapaswa kuruka na wapi hupaswi kuruka. ni wapi ujiachie na wapi usijiachie.

    AMRI YA TATU: UTAENDELEA KUKAA KATIKA HALI ULIYONAYO MPAKA PALE NGUVU YA ZIADA ITAKAPOTOKEA

    Hii ni amri nyingine unayopaswa kuijua. Kitu chochote ambacho kimetulia kitaendelea kutulia mpaka itokee nguvu ya ziada ya kukiweka kwenye mwwndo. Na kitu chochote ambacho kipo kwenye mwendo kitaendele kuwa kwenye mwendo mpaka itokee NGUVU YA ZIADA ya kukitoa kwenye mwendo.

    Na kwenye maisha ni au upo kwenye mwendo au umeitulia. Ni hivyo tu.

    Kama kuna malengo au ndoto kubwa ulizonazo na unataka kupata matokeo basi ingia kwenye mwendo.
    Wengi kwenye maisha hawapati wanachotaka kwa sababu hawapo kwenye mwendo; muda wote wametulia…

    Mtu anataka kufikia Mambo makubwa maishani, Ila haweki kazi. Kwa amri hii Ni vigumu sana kuyapata hayo matokeo.

    AMRI YA NNE:  TUNZA MUDA
    Vitu vyote vitafanyika kulingana na muda uliopo. Kwa siku tuna saa 24 tu na siyo zaidi ya hapo. Kama unataka kufanya makubwa, tumia vizuri muda wako.

    Usikubali kuibiwa muda wako. Muda ni Mali Kama zilivyo mali nyingine.

    Mtu akija kwako na kubeba runinga, simu yako na samani utasema Ni mwizi kwq sababu amebeba mali zako.

    Lakini mtu akija kwako kukupisha stori unamwacha, unaona Ni mtu mwema. Wakati anakuibia muda.

    Laiti kama kila mtu angejua umuhimu wa muda na kuutumia muda wake kufanya kazi kwa weredi, Nina hakika hii duniani kusingekuwa na malalamishi wala ufanyaji wa maovu.

    AMRI YA TANO: Tunza mawazo yako vizuri

    Wanasaikolojia wamethibitiaha kuwa kwa siku moja tu mtu unakuwa na mawazo 6000 kwa siku.

    Mawazo mengine huwa yanapita kiasi kwamba wewe mwenyewe hatahufahamu Kama yameoupita. Kumbe Sasa kitu kikubwa kwako ni wewe kuhakikisha kwamba unatunza Yale mawazo yako ya muhimu.

    Unapaswa kufanya hivyo ili kutoa nafasi ya mawazo mengine kuendelea kuja.

    Lakini pia ili uweze kuyakumbuka mawazo yako yote hapo baadaye.

    Hivyo kuanzia Sasa, Jenga utaratibu wa kuandika mawazo yako chini.

    AMRI YA SITA: HAKIKISHA UNAJUA UNACHOTAKA
    Kinachofanya watu wasipate wanachotaka ni kwa sababu hawakijui. Na wewe usipojua unachotaka utazunguka huku na kule bila kupata matokeo yoyote Yale ya maana.

    AMRI YA SABA (A): WAFANYIE WATU KILE UNACHOPENDA UFANYIWE
    Kama kuna kitu hupendi kufanyiwa usiwafanyie watu wengine.
    Najua hupendi kuibiwa, kwa hiyo usiibe.
    Najua hupendi kupigwa, kwa hiyo usipige watu.
    Najua hupendi kusemaa vibaya, kwa hiyo usiwaseme watu vibaya.

    AMRI YA SABA (B): WAFANYIE WATU WANACHOPENDA WAFANYIWE

    Kuna wakati unapaswa kuwafanyia watu kulingana na vile wanavyotaka wao.

    Kama mtu ana kiu, mpe maji.
    Kama mtu ana tatizo,  msaidie kulitatua.

    AMRI YA NANE: KAMA UNATAKA KUPOKEA TOA.

    Kutoa ni kitu muhimu sana kwenye maisha. Kama unataka kupokea toa. Na hivi vitu viwili vinaendana sana. Kutoa na kupokea. Yaani, ni kama mzani vile. Unapaswa kujenga utaratibu mzuri wa kutoa, lakini pia unapaswa kuwa na utaratibu wa kupokea.

    Ni muhimu kutoa, ni muhimu pia kupokea.

    Kuna watu ni wabovu kwenye kupokea ndio maana fursa nyingine za kifedha huwa zinawapita.

    Nakumbuka nilijiwekea utaratibu wa kutoa kitu hata kama Ni kidogo kila siku.

    Siku moja nilikutana na mtoto na kuamua kumpa shilingi mia moja kama sehemu ya utoaji wangu. Yule mtoto aliikataa Ile hela kwa kusema kwamba amekatazwa kupokea fedha na wazazi wake. Sikumlazimisha kwa sababu asili pia huwa hailazimishi. Ilikupa wewe kitu ukakikataa, jua wazi kuwa Kuna MTU mwingine ambaye anaenda kunufaika na kile ambacho wewe mwenyewe umekataa.

    Baada ya kugundua kuwa Hilo, nimeandaa sala yangu binafsi linapokuja suala la fedha, kutoa na kupokea. Na wewe unaweza kuitumia pia. Inasema hivi. Ewe nguvu ya asili, Kama kuna fursa au fedha zinakuja kaa watu na hawapo tayari kuzipokea, tafadhali Sana naomba uziletw kwangu. Nipo tayari kuzitumia na kuzitumia kwa usahihi maishani mwangu.

    Napenda kusisitiza kitu kimoja kikubwa: najua wengi wanaamimi kuwa ni kheri zaidi kutoa kuliko kupokea. Ila ukweli ni kwamba, kwa kanuni za asili zilivyo, ukitoa milango ya wewe kupewa inafunguka pia. Hivyo siyo kheri kutoa tu! Bali ni kheri zaidi kutoa na ni kheri zaidi kupokea. Kama nilivyosema tangu mwanzo, hivi vitu ni Kama mzani, hakuna upande ambao unapaswa kuzidiwa.

    Haupaswi kuwa mpokeaji tu kila mara. Na haupaswi kuwa mtoaji bila kupokea.

    Ili mzani uende sawa unapaswa kutoa na unapaswa kupokea. Kwa hiyo, ni kheri zaidi kutoa na ni kheri zaidi kupokea pia.

    Ila sasa ukitoa, usianze kulazimisha kupewa. Kamwe usifanye hivyo. Na usitegemee kupokea kutoka kwa mtu hiyohiyo ambaye wewe umempa.

    Asili huwa haisahau, ni Kama vile inakutunzia mema yako na baadaye yale mema yako yanakurudia kwa njia nyingine ambayo ni bora zaidi.

    Na wala ukitoa usijigambe.

    Mwembe unatoa maembe lakini haujigambi kuwa umetoa maembe.
    Ng’ombe anatoa maziwa ila haujigambi wala kutamba kuaa katoa maziwa.

    Na wewe ukitoa usije kuanza kusema ooh, unajua, fulani asingekuwa na maisha aliyonayo bila ya mimi. Ooh unajua mimi ndiye nimemsaidia mtu fulani kupata kitu fulani.

    Kibaya zaidi, usije ukaanza kulazimisha mtu akupe, eti kwa sababu wewe umempa au uliwahi kumpa kitu fulani siku za nyuma.

    AMRI YA TISA: SHUKURU

    Jenga utaratibu wa kushukuru. Kuwa mtu mwenye shukrani Mara zote!

    Kuna watu wanashangaza kweli.
    Mtu anaweza kuwa na shida ya fedha, akatokea mtu akamtumia kiasi kidogo kulinganisha na kile alichokuwa anataka, unakuta huyu aliyetumiwa anaanza kulalamika, ooh fedha yenyewe kanitumia kidogo!

    Ndugu yangu, SHUKURU. Kushukuru ni kuomba tena Kama ulivyo methali ya wahenga wetu.

    Mtu akikupa kitu SHUKURU.
    Ukiamka asubuhi SHUKURU,
    Ukimaliza siku yako SHUKURU.
    SHUKURU kwa ajili ya wazazi wako, ndugu zako, watoto wako, mwenza wako, nguvu zako, mali na chochote unachomiliki.

    Una vitu vingi vya kushukuru kuliko kulalamika.

    Kwenye Biblia Yesu alikuwa mfano mzuri kwenye hili. Kila alipotaka kufanya Jambo alishukuru kwanza.

    Ndio maana kwenye Biblia utakutana na maneno kama baba nakushukuru kwa ajili ya…Mara nyingi.

    Alipotaka kuponya mtu alishukuru.
    Alipotaka kulisha watu alishukuru
    Na hata alipokuwa anakufa alishukuru.

    Wewe pia Jenga utaratibu wa kushukuru.

    Ila ngoja kwanza,
    Napenda kushukuru sana kwa kusoma andiko langu la leo. Ubarikiwe sana, endelea kufuatilia mafunzo mengine zaidi hapahapa.

    Kila siku naweka Makala mpya mbili bila kukosa.

    Unaweza pia kupata mafunzo zaidi kwa njia ya email hapa.

    Asante.

    AMRI YA KUMI: KITU CHOCHOTE KISIPOTUMIKA KITAPOTEA

    Hii ni amri nyingine pia ambayo unapaswa kuifahamu. Kiungo cha mwili, kipaji au uwezo wako usipoutumia, jua kuwa uwezo huu unaenda kufifia na itafikia hatua ambapo utapotea. kipaji chako usipokitumia kitapotea. Na hata ukijenga nyumba bila ya kukaa, itaharibika.

    yaani kuna vitu viwili. ni au utumie uwezo wako ili uendelee kuongezeka zaidi na zaidi au usiutumie ili upotee.

    kuna watu huw wanadhani kwamba wakitumia kitu labda kipaji chao kitakwisha. hakuna kitu kama hicho. kadiri unavyotumia uwezo wako, ndivyo unavyoongezeka na kuzidia na wewe unazidi kuwa imara zaidi.

    kadii unavyoandika ndivyo unazidi kubobea zaidi

    kadiri unayotibundivyo unazidi kuwa daktari mbobevu.

    kadiri unavyoimba, ndivyo unazidi kupanua wigo wako na kuwa mwimbaji mzuri zaidi.

    kadiri unavyochora ndivyo unazidi kuwa mchoraji mzuri zaidi.

    ukifuatilia watu wote waliobobea, kazi zao za kwanza hazikuwa kazi bora kabisa. hata Ben Carson ambaye ni daktari maarufu kwenye suala zima la upasuaji, hakubobea siku ya kwanza. ila kadiri alivyokuwa akiendelea kutumia uwezo wake, ndivyo alivyokuwa anazidi kuimarika na kuwa bora zaidi.

    na wewe kama una kipaji. kitumie. nakuhakikishia kuwa utazidi kuimarika na kuwa bora zaidi ya ulivyokuwa mwanzoni.

    hizo hapo ndizo amri za maisha. zifuate kwa manufaa yako, zivunje kwa hasara yako.

    kila la kheri.

    Ni mimi rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE

    Tuwasiliane kwa 0755848391

    kwa mafunzo mengine zaidi kutoka kwangu. usisite kujiunga na jumuiya ya watu wangu wa nguvu wanaopokea mafunzo kwa njia ya barua pepe hapa chini. kila la kheri.



  • Kitu muhimu unachopaswa kufahamu kabla ya kuajiri

    Ukiingia kwenye ujasiriamali ni wazi kuwa itafikia hatua ambapo utahitaji kuajiri.

    Iwe Ni msaidizi wa kazi
    Mtu wa masoko
    Mtu wa mauzo
    Au yeyote yule..

    Kwa vyovyote vile utapaswa kuajiri…

    Sasa kabla ya kuajiri jiulize je, kuna mashine au kitu ambacho kinaweza kufanya hii kazi?

    Kama hiki kitu kitumie kwanza badala ya kuajiri.

    Kama hakuna mashine wala kifaa chochote kinachoweza kufanya hiyo kazi jiulize swali la pili.

    Je, kuna mtu AMBAYE anaweza kufanya kazi hii kwa part time na akalipwa kidogo? Kama yupo mtumie huyo pia…

    Kama hivyo vyote viwili vimeshindikana basi nenda moja kwa moja kwenye kuajiri.

    Kila la kheri.

    [mailerlite_form form_id=0]

  • Hata kama itatokea ukasahau vyote maishani, Ila hakikisha hausahau kufanya hivi vitu

    1. Usisahau kuweka AKIBA. Kwa kila kipato chako unacjopata weka akiba ya asilimia 10.

    2. Usitumie fedha zaidi ya unavyoingiza.

    3. Usifanye vitu kuwaridhisha watu.

    4. Usitegemee chanzo kimoja cha kipato na hasa mshahara.

    5.  Mara zote kuwa na kitabu na soma vitabu.

    6. Hakikisha unakuwa na malengo na unayafanyia kazi.

    7. Ukitaka kuibadili dunia. Anza kufanyia mbele ya nyumba yako. Ukitaka kuibadili dunia tandika kitanda.

    8. Usiangalie runinga na hasa taarifa ya habari.

    9. Usisahau kuwa maisha ni wajibu wako. Ukishinda ni juu yako na ukishindwa ni juu yako.

    10. Mahusiano yako yawe kipaumbele kwako.

    Kwa sasa kutoka hapa mji kasoro bahari; mji kasoro pwani sina la ziada.

    Umekuwa nami,
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Jinsi ya kuandika KITABU kikubwa kwa namna ya kawaida

    Mwaka juzi nilitoa Kitabu CHANGU cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Kwenye Kitabu HIKI nimeeleza hatua kwa hatua jinsi ambavyo unaweza kufikia malengo na ndoto kubwa kwenye maisha.

    Mmoja wa wasomaji wa Kitabu hicho alinipigia simu baada ya kuwa anlmekisona na kuniambia kuwa ana ndoto ya kuandika tamthiliya. Niliongeaa Naye na kumtakia kila la kheri.

    Sasa juzi nilimpigia mwenyewe. Tukaanza kuongea na nikamwuliza mwenendo wa kitabu chake.

    Ndipo aliponiambiabkuwa hajakiandika.

    Hapohapo nikaanza kuweleza mbinu rahisi ya kuandika kitabu bila kutumia nguvu kubwa.

    Nilimwuliza. Kwa siku unachati na kutuma SMS ngapi?

    Nikamwambia Sasa aikiliza. Ni kweli unaposikia kitabu lazima tu uogope. Maana kitabu tu Kama kitabu utakuta kina kurasa 200 au zaidi…

    Sasa ukifikiria Hilo utajikuta unakwama.

    Ebu fikiria kitabu kama kuchati.  Na kila siku uandike ujumbe mfupi tu wenye maneno 100. Ambapo kwa siku ya kawaida wakati unachati kuandika maneno 100 siyo kitu kikubwa Sana. Na hata wewe ukiandika maneno 100 huoni kama issue yoyote ile.

    Sasa kitabu pia kiandike hivyo..

    Kiandike kama unachati vile..

    Ukiandika maneno 100 kila siku kwa mwaka Ni sawa maneno 36,000/-
    Sijui unanielewa?

    Sasa ebu fikiria huyu msomaji wa kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO angekuwa ameazimia kuandika maneno 100 tu kila siku tangu mwaka 2020. Leo hii so agekuwa anakaribia kufikisha maneno elfy sabini?

    Kitabu chenye maneno elfu sabini ni kitabu kikubwa chenye kurasa kuanzia 400 na kuendelea. Huyu jamaa angekuwa tayari anamalizia kuandika kitabu chake

    Na wewe hivyo ndivyo unaweza kuandika kitabu chako.

    Ukweli ni kwamba usipoanza kuandika kitabu chako, miaka miwi kutoka Sasa bado utakuwa unakwama na kusema kuwa Nina ndoto ya kuandika kitabu.

    Amua leo kuwa unaenda kuandika kitabu. Hata ukiandika maneno 50 tu.  Ukifanya hivyo kila siku utajikuta mbali.

    Mimi kutoka hapa mji kasoro bahari, Morogoro sina la ziada.

    Naitwa
    Godius Rweyongeza
    Tukutane baadaye kwenye makala nyingine.

    Makala ya leo imeletwa kwako kqa udhamini mkubwa wa kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 . Kupata kitabu hiki tafadhali lipia 5000 tu kwenda 0755848391 jina Ni GODIUS RWEYONGEZA. Utatumiwa ebook ndani ya dakika 5.

    UKINUNUA KITABU HIKI, UNAWWZESHA MAKALA NYINGINE NZURI NA BORA ZAIDI KUENDELEA KUANDALIWA KAA AJILI YAKO.

  • Kitu kikubwa na muhimu kwenye ujasiriamali siyo kujua kutengeneza bidhaa

    Kitu kikubwa na muhimu kwenye ujasiriamali siyo kujua kutengeneza bidhaa. Siyo kabisa! Ingekuwa hicho ndio kitu kikubwa basi wengi wangekuwa wametoboa.

    Hiyo ni sehemu ndogo tu…

    Juzi tu hapa nilikuwa naongea ndugu mmoja ambaye anakaribia kuhitimu chuo. Kama ilivyo kawaida yangu nilimwuliza una mpango gani na maisha baada ya chuo…!

    Hili ni swali ambalo nimewauliza vijana wengi walio chuoni na wale ambao wanaokaribia kuhitimu kila ninapopata nafasi.

    Kijana huyu alinijibu kuwa alipata nafasi ya kujifunza ujasiriamali. Si unajua ujasiriamali siku hizi watu unahusishwa na kutengeneza bidhaa kama vile sabuni, vitenge, viatu vya kimasai…..

    Ukiwa unatengeneza hivyo vitu, wewe ni mjasiriamali. Kama hutengenezi hivyo vitu wewe siyo mjasiriamali. Hii ni maana potofu kweli kuhusu ujasiriamali!!!!!

    Hata hivyo wacha kwanza niendelee kueleza lililonileta hapa. Inshallah, kesho au kesho kutwa nitarudi hapa kueleza mjasiriamali ni nani? Kwa mara ya kwanza nitakupa maana inayojitosheleza kuhusu mjasiriamali!

    Niendelee au nisiendelee….

    Acha tu niendelee hata kama hupendi 😂😂.

    Sasa bwana, nataka nikwambie wewe kuwa ujasiriamali siyo tu kutengeneza hizo bidhaa. Hiyo ni sehemu ndogo sana….

    Muziki mkubwa wa ujasiriamali upo kwenye kuuza bidhaa na brand ya biashara yako.

    Ngoja nikwambie kitu…

    Walau si unamfahamu Bakhresa. Huyu jamaa anauza hata mandazi. Ila haya mandazi yake yanasambaa kila kona ya Tanzania.

    Na wewe mtaani kwako Kuna mama anatengeneza mandazi. Si ndiyo? Tena ninavyojua utamalizia kwa kusema mama yule anapika mandazi matamu kuliko ya Bakhresa!

    Ila sasa usije ukakimbilia kununua mandazi kwa sababu nimeyataja hapa ukaacha kusoma makala hii mpaka mwisho. Nikikugundua…😂😂.

    Sasa unadhani kwa nini maandazi ya mama hayajafika mbali hivyo?

    Hapo issue kubwa ni masoko na kuuza. Na hapo ndipo ulipolala ujasiriamali wenyewe.

    Ujasiriamali siyo tu kutengeneza bidhaa, bali kuziuza pia.

    Usipojua namna bora na nzuri ya kuuza bidhaa hizi, utahangaika kutengeneza bidhaa nzuri ambazo wewe mwenyewe utashindwa kuziuza. Hivyo basi, ukiachana na kujifunza utengenezaji wa bidhaa. Ukiachana na kutengeneza hizo bidhaa…

    Uuzaji wa bidhaa ni kitu muhimu sana na wewe unapaswa kuhakikisha unaufahamu wa ndani wa huu ujuzi.

    Kama unashindwa kuuza bidhaa fanya hivi.

    1. Kaajiriwe sehemu ambapo utafanya mauzo ili ufanye mauzo kwa vitendo.
    2. Kachukue bidhaa ya mwingine na uiuze.
    3. SOMA vitabu vya mauzo na yafanyie kazi yale unayojifunza.

    Kwa leo kutoka hapa Morogoro mji kasoro bahari, sina la ziada.

    Umekuwa nami rafiki yako
    Godius Rweyongeza
    0754848391
    Cheers!

  • Kitu gani unaenda kufanya wiki hii ili kujisogeza karibu na malengo yako?

    Kwenye kitabu changu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI, nimeeleza kwamba kadiri unavyokuwa unafanyia malengo yako, yenyewe yanakuwa yanasogea karibu pia. Hivyo, Kuna sehemu mtakutana ambayo ndiyo pointi ya wewe kufikia melengo yako.

    Sasa wiki mpya tayari imeanza, ni kitu gani unaenda kufanya wiki hii ili usogee karibu na malengo yako?

    Hakikisha unafanya kitu. Bila kufanya kitu unaweza kuishia kusema labda Mimi nimerogwa au nimelaaniwa, Ila kumbe siyo.

    Unaweza kusema Mungu hajanibariki, lakini kumbe hajaona juhudi zako ili akubariki. Si unajua Mungu anabariki juhudi eeh!

    Haya Sasa kazi ni kwako. Kwenye mipango yako ya wiki hii, chagua kitu kimoja ambacho utafanya. Kisha komaa nacho mpaka kieleweke. Kila la kheri.

    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

X