Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Kitu gani unaenda kufanya wiki hii ili kujisogeza karibu na malengo yako?

    Kwenye kitabu changu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI, nimeeleza kwamba kadiri unavyokuwa unafanyia malengo yako, yenyewe yanakuwa yanasogea karibu pia. Hivyo, Kuna sehemu mtakutana ambayo ndiyo pointi ya wewe kufikia melengo yako.

    Sasa wiki mpya tayari imeanza, ni kitu gani unaenda kufanya wiki hii ili usogee karibu na malengo yako?

    Hakikisha unafanya kitu. Bila kufanya kitu unaweza kuishia kusema labda Mimi nimerogwa au nimelaaniwa, Ila kumbe siyo.

    Unaweza kusema Mungu hajanibariki, lakini kumbe hajaona juhudi zako ili akubariki. Si unajua Mungu anabariki juhudi eeh!

    Haya Sasa kazi ni kwako. Kwenye mipango yako ya wiki hii, chagua kitu kimoja ambacho utafanya. Kisha komaa nacho mpaka kieleweke. Kila la kheri.

    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Namna ya kufanya usomaji wa vitabu uwe sehemu ya pili ya maisha yako

    Kusoma ni tabia. Na tabia yoyote hujengwa.  Kuna tabia ambazo unazo sasa hivi unazifanya ila hujiulizi mara mbili kama uzifanye au uache. Kwa mfano kila siku unapiga mswaki ila hujiulizi mara mbili kwamba upige au usipige leo utapiga mswaki kesho. Yaani, kupiga mswaki kumeshakuwa tabia yako ya pili.

    Sasa hata kusoma kunapaswa kuwa tabia yako ambayo unafanya bila kujiuliza. Na unaweza kuifanya iwe tabia yako ya pili kama utaamua kila siku kusoma kitu. Yaani, hakikisha ukianza leo kusoma na kesho soma. Na kesho kutwa soma pia. Hivyo ndivyo utajenga tabia ya kusoma kila siku.

    Robin Sharma kwenye kitabu chake cha The 5am Club anasema kwamba tabia ya kweli inajengwa ndani ya siku 66. Yaani siku 22 za mwanzo zinakuwa ni kuanzisha tabia. Siku hizi huanza vizuri kabisa ila huanza kuwa ngumu katikati. Siku 22 zinazofuata huwa ngumu zaidi ila ukizivuka hizi utakuwa umeimarika sana. Siku 22 za mwisho ndio tabia yako inakuwa tayari imejengeka. Kwa  hiyo na wewe kuanzia leo weka mpango wa kusoma kitabu kila siku kwa siku 66 bila kukosa. Itapendeza zaidi kama muda huo wa kusoma utakuwa ni ule ule kila siku.

  • Zama Zimebadilika (Part 1)

    UTANGULIZI

    Dunia tunamoishi sasa imepitia katika nyakati mbali mbali kwa vipindi mbali mbali. Dunia hii imekumbana na vitu mbali mbali ambavyo vimekuwa vikiiweka hii katika vipindi kadha wa kadha ambavyo tunaviita zama. Zama ni nini? Kamusi ya Kiswahili sanifu inazizungumzia zama kama nyakati. Kwa hiyo tungeweza kusema kwamba nyakati sasa zimebadilika badala ya kusema kwamba zama zimebadilika..

    Kwa nini tunasema kwamba zama zimebadilika?

    Zama ni kipindi ambacho matumizi ya kitu fulani yanakuwa juu sana na ndio  yanakuwa yanatawala kwa hali ya juu. Ukiilewa dhana hii tu utaelewa mengi kutoka kwenye kitabu hiki. Dunia yetu imepitia katika vipindi hivi vingi, kuanzia hapo wanadamu walipoanza kuishi kwenye hii dunia mpaka leo. Kila kipindi kimekuwa na kitu fulani ambacho kinaifanya kipindi kile kiwe chenye utofauti mkubwa sana. Mwanzo kabisa dunia ilipitia katika zama za mawe, baadae ikaja kwenye zama za chuma na baada ya hapo ikaja kwenye zama za viwanda lakini pia ikatoka kwenye zama za viwanda na kuhamia katika zama nyingine ambazo ndizo tulizopo sasa hivi. Na zama hizi ambazo tulizopo sasa hivi hazitaendelea kudumu kwa kipindi kirefu sana maana zitabadilika na kutakuwa na ujio wa zama nyingine.

    Kwa hiyo, ni muhimu sana kujua kwamba zama za sasa hivi zimebadilika, tena sana. kuwa na taarifa kwamba zama za sasa hivi zimebadilika ni hatua moja kwenda katika mafanikio. Maana kama hata hauna taarifa kwaba zama za sasa hivi zimebadililka basi ni hatua moja kurudi nyuma.

    Kwenye kila zama huwa kuna zana fulani ambayo ndiyo huwa ni msingi mkuu wa uzalishaji. Ndio maana tangu mwanzo nimekwambia ukiilewa maana ya zama, utaelewa mengi kutoka kwenye kitabu hiki.

    Kwa kukumbusha tu ni kwamba “zama ni kipindi ambacho matumizi ya kitu fulani yanakuwa juu sana”.

    Kwenye zama z mawe. Jiwe ndilo lilikuwa msingi mkuu na lilikuwa linahitajika sana. kwa hiyo kwenye hiyo zama, watoto waliozaliwa na kukua walielekezwa namna ya kutafuta mawe mazuri kwa ajili ya kuwinda, kutafuta mizizi, kujilinda dhidi ya maadui, na hata mapango mazuri ya kuishi. Hizo ndizo zilikuwa zama za mawe. Ulichokuwa unahitaji kwenye hii dunia ilikuwa ni kuwa na jiwe sahihi kwa wakati sahihi ili uweze kutoboa maisha.

    Baadaye zama za mawe ziliisha na zama za chuma zikawa zimeingia. Kwenye zama hizi, kitu kikubwa ambacho kilikuwa kinahitajika kwenye hizi zama ilikuwa ni chuma. Aliyekuwa na chuma kwa wakati husika ndiye alikuwa mshindi. Chuma ndicho kilitumika kutafuta chakula, kuwinda, kujilinda na kujikinga dhidi ya maadui.

    Hivyo, watoto waliozaliwa na kukulia kwenye hiki kipindi walipewa ushauri nakuaminishwa kwamba ili utoboe kwenye maisha unapaswa kuwa na chuma. Na huo ndio ulikuwa ukweli.

    Baada ya zama za chuma yalifuata mapinduzi ya viwanda. Hiki nacho kilikuwa  ni kipindi muhimu sana, kwenye zama hizi hapa kiwanda ndiyo ulikuwa msingi mkuu wa uzalishaji na mtu yeyote ambaye alikuwa na kiwanda alikuwa na uwezo wa kufanya vizuri na kutoboa kimaisha. Zama za viwanda zilizalisha makundi mawili ya watu.

    Kundi la kwanza ni la wamiliki wa viwanda. Na kundi la pili ni la waajiriwa kwenye viwanda. Kwa mara ya kwanza watu walianza kuajiriwa na kupewa ujira kwenye zama hizi. Kundi la pili ndilo lilikuwa na watu wengi kulinganisha na kundi la kwanza.

    Hivyo, watoto waliozaliwa kwenye kipindi hiki walielewa vitu viwili. Kwanza ni kwamba ili ufanikiwe ni lazima uwe na kiwanda na pili ni kuwa ili ufanikiwe  unapaswa kuajiriwa kwenye kiwanda. Na huo ndio ulikuwa mwanzo wa usemi maarufu wa soma kwa bidii, ili uje ujiriwe kwenye kampuni itakayokulipa vizuri.

    Pata ebook hii yote kwa elfu 3 tu

  • KUTOKA KWENYE AJIRA MPAKA KUJIAJIRI

    Nakumbuka juzi nilikushirikisha safari ambayo unapaswa kuifuata ili uweze kujiajiri kama umeajiriwa kwa sasa. leo hii naomba kuendelea tena kwa kukushirikisha vitu zaidi kwenye suala zima la ujasiriamali na kujiajiri.  Na leo ninakushirikisha machache niliyopata kutoka kwenye kitabu cha Employee To Entrepreneur

    Moja ya ushauri ambao umekuwa unatolewa kwa watu wengi ni ushauri wa kwamba unapaswa kwenda shuleni, kusoma kwa bidii ili hatimaye uweze kuajiriwa kwenye kampuni au serikalini ambapo utaajiriwa na kulipwa vizuri.

    Ushauri huu umefanya vizuri hasa kwenye karne ya 20 ambapo nguvu kazi ilikuwa ikihitajika zaidi kwenye viwanda na maeneno mengine. Hata hivyo kwenye zama hizi kuna mabadiliko kidogo.

    Kuna kazi ambazo zilikuwa zikifanywa na watu sasa hivi hazifanywi na watu tena. Lakini bado ushauri wa kwamba unapaswa kwenda shuleni na kusoma kwa bidii ili hapo baadaye uweze kuajiriwa umekuwa ukiendelea kutolewa.

    Japo ujasiriamali unaonenaka ni njia nzuri na ambayo naweza kubadilisha maisha ya watu wengi, ila sasa wengi wanashindwa kuufanya. Na moja ya sababu  kubwa inayowafanya watu washindwe kujihusisha na ujasiriamali ni kwa sababu ili uwe mjasiriamali unahitaji mabadiliko kwenye akili yako.  Ebu fikiria hili. Tangu umezaliwa ulikuwa ukiambiwa kwamba ili uweze kuishi maisha mazuri unapaswa kuwa na kazi ambao itakulipa vizuri. Lakini sasa cha kushangaza ni kwamba unapohitimu chuo unakuta kwamba ajira hamna.

    Kwa wengi ni vigumu sana kubadili akili zao na kujiingiza kwenye ujasirimali na hilo linafutanya tuje kwenye pointi yetu ya kwanza kwa siku ya leo ambayo

    #1. ILI UWE MJASIRIAMALI UNAPASWA KUBADILI FIKRA ZAKO

    Unapaswa kubadili fikra zako ili uweze kujiingiza kwenye ujasiriamali. Watu wengi hawapendi ujasirimali kwa sababu ujasiriamali unahusisha kuanguka na kushindwa. Hakuna mtu ambaye anapenda kushindwa na kuanguka.

    Na watu wanaogopa kushindwa kutokana na fikra zao walizonazo. Linapokuja suala zima la fikra kuna watu wa aina mbili. kuna watu wenye fikra mgando na kuna watu wenye fikra za ukuaji.

    Watu wenye fikra mgando ni wale ambao wanafikiri kwamba haiwezekani kufanyika  kitu chochote kipya. Ndio wale utakaowasikia wakikwambia hakuna jipya chini ya jua au kila kitu kilishagunduliwa.

    Hata hivyo watu wenye fikra za ukuaji wenyewe wanaangalia ni kwa namna gani ambavyo wanaweza kukua zaidi kutoka hapo walipo. Wapo tayari kujifunza na kuchukua hatua. Wakianguka wanaona hilo kama somo ambalo wanaenda kulifanyia kazi kwenye maisha.

    Ujasiriamali unahitaji fikra za ukuaji. Kwa sababu kwenye ujasirimali kuna kuna vitu vingine ambavyo mwanzoni unaweza kuwa unafikiri kwamba ukivifanya mara moja tu vitafanikiwa, ila ukienda kuvifanyia kazi kwenye uhalisia ukakuta kwamba mambo ni tofauti.

    Ndio maana watu wengi huwa wanaanza kufanya vitu vipya lakini baadaye wanaishia njiani. Unajua kwa nini?

    Kwa sababu ujasirimali unahitaji kujitoa kwelikweli. Na unapaswa kuwa tayari kupokea mabadiliko ambayo yanatokea kwenye ulimwengu wa leo.

    #2 JUA KUSUDI LINALOKUFANYA UINGIE KWENYE BIASHARA

    Huwa napenda sana kutolea mfano wa wachezaji wampira wa miguu. Kuna baadhi ya vyakula hawawezi kula hata kama vinapendwa na watu wengi kwa sababu tu wao ni wachezaji wa mpira wa miguu. Wanajua kabisa sili hiki chakula kwa sababu nataka nitimieze kusudi langu ambalo ni hili.

    Usipokuwa na kusudi kwenye biashara unayumbishwa. Wewe pia unapoingia kwenye ujasiriamali unapasaw kuwa na kusudi kubwa ambalo linakusukuma wewe.

    Ni kitu gani kinakusukuma kuanzisha biashara. Kama lengo kubwa ni fedha utajikuta kwamba unakwama kwa sababu msukumo wa fedha peke yake hautoshi kukufanya uweze kusonga mbele na kufanya makubwa zaidi.

    Msukumo kama

    Kupata uhuru binafsi

    Uhuru wa kifedha

    Familia

    Kuwasaidia wazazi

    Hii inaweza kuwa ni msukumo mzuri wa kukufanya uzidi kusonga mbele.

    Kwa hiyo ni muhimu kwako kujiuliza hivi ni kweli nina msukumo mzuri kutoka ndani ambao unanisukuma

    #3. KUSANYA MAWAZO MBALIMBALI KISHA TENGENEZA WAZO LAKO

    Najua kuna nia mbalimbali za kupata mawazo ya bisahara, ila kwa leo nataka nikueleze hii njia ambayo unaweza kuitumia kama unataka kutengeneza wazo la kipekee kwenye biashara. Njia hii ni kuangalia vitu ambavyo tayari vipo kisha kujenga kitu kipya na cha tofauti kutokana na hivyo vitu ambavyo vipo.

    Siyo lazima mara zote uje na wazo jipya na la kipekee sana. ila unaweza kutumia vitu ambavyo vipo kwa sasa kujenga wazo jipya na la kipekee

    #4. JARIBU WAZO LAKO KWA WACHACHE WA MWANZO KABLA YA KUWEKEZA FEDHA NYINGI

    Badala ya kuwekeza fedha zako kutengeneza bidhaa na kuileta sokoni. Anza na kuleta bidhaa yako kwa watu wachache wa kwanza, kisha baada ya hapo utawekeza zaidi.

    #5. UTUMIE MUDA WAKO VIZURI

    Kwa siku mtu wa kawaida anasemekana kugusa simu mara 2617. Na mara nyingi sio kwamba kunakuwa na kitu cha maana ambacho mtu huyu anafanya, badala yake unakuwa ni upotezaji wa muda tu mtandaoni kwenye makundi ya whatsap na maeneo mengine.

    Sasa unachopaswa kufanya wewe ni kuhakikisha kwamba unautumia muda wako vizuri. Usitumie muda wako mwingi kwenye mambo ambayo hayana manufaa. Wekeza muda wako na hasa unapouwa kwenye hii safari ya kutoka kwenye ajira kwenda kwenye kuajiriwa.

  • Ushauri Mzuri Ambao Nimewahi Kupokea Maishani Mwangu

    Nakumbuka mwaka 2016 hivi wakati naendelea na masomo yangu ya chuo. Nilikuwa njia panda nikifikiria niache chuo niendelee na biashara na uandishi au nifanyeje?

    Uamuzi wangu ulikuwa kuacha chuo…

    Baadaye katika kuwashirikisha watu wangu wa karibu; mmoja wao aliniambia hivi;

    Godius fanya vyote, endelea na kusoma, andika na fanya biashara. Ukifanikisha vyote vitatu utaonekana shujaa siku za mbeleni utaonekana shujaa mkubwa sana.

    Leo hii sipo hapa kukwambia kwamba mimi ni shujaa kwa sababu nilifanya vyote. Ila tu kukushirikisha yafuatayo:

    1. Kwenye maisha kuna watu ni wabobevu na wana ujuzi na uelewa mpana zaidi yako. Inapotokea ukawa njia panda basi usisite kuwasiliana nao ili wakusaidie kukupa ushauri.

    2. Unapokuwa njia panda huelewi ufanye kitu gani, unapaswa kufikia uamuzi wa kufanya kitu. Kutokufanya uamuzi kabisa ni hatari. Chagua kitu kimoja na ukisimamie hicho.

    3. Kama upo chuoni, usiache chuo. Leo hii nipo nafikiria hivi ningeacha chuo mwaka ule ingekuwaje sasa hivi. Sisemi hivyo labda eti kwa sababu labda nimeajiriwa. Sijaajiriwa na hata cheti changu cha chuo sijawahi kukitoa chuoni! Ila kwa sababu moja tu. Katika kuendelea kusoma nilikuja kujifunza kitu ambacho leo hii nimeamua kukifanyia kazi maisha yangu yote.

    Kuna kozi nilikuwa bado sijajifunza kipindi nataka kuacha chuo. Sasa hivi nimefungua kampuni kufanyia kazi kile nilichojifunza kwenye hiyo kozi.

    Rafiki yangu, huo ndio ushauri mzuri ambao nimewahi Kupokea maishani mwangu.

    Wewe unakumbuka ushauri mzuri ambao umewahi kupokea ni upi?

    Tushirikishe hapa chini

    [mailerlite_form form_id=0]

  • Nguvu Ya Kuwa Na Ratiba Na Mambo Matano Ya Kujifunza Kutoka Kwa Benjamin FranklinKila Mara nimekuwa

    Kila mara nimekuwa nikisisitiza juu ya umuhimu wa kuwa na ratiba. Ukiamka asubuhi pangilia siku yako kwa namna ambavyo ungependa iwe. Andika vitu ambavyo utafanya na hata vile ambavyo hutafanya.

    Lakini pia kuna vitu ambavyo vinajirudia kila siku katika ratiba yako. Na hapo ndipo unapaswa kuwa na mfumo fulani ambao unaufuata. Mfumo huu utakuwezesha wewe kuchomeka majukumu ya kazi kwenye ratiba yako ambayo yanajitokeza mara moja.

    Moja ya ratiba ya siku ambayo imekuwa maarufu mtandaoni ni ratiba ya Benjamin Franklin. Bwana Franklin alikuwa na ratiba maalumu aliyokuwa anaifuata kila siku ya maisha yake na pale ambapo kuna majukumu mapya ambayo yangejitokeza basi alikuwa anayaweka humo katikati kwenye ratiba iliyopo

    Ratiba yake ilikuwa hivi:

    Alikuwa anaamka saa 11 asubuhi na kitu cha kwanza alikuwa ananiuliza. Ni kitu gani kizuri ambacho ninaenda kufanya siku ya leo?

    video toka miaka miwili iliyopita nikizingumzia kuhusu kulala na kuamka mapema.

    Baada ya hapo alikuwa anahakikisha amepangilia ratiba yake ya siku hiyo. Baadaye alikuwa anasoma kitabu na kupata kifungua kinywa.

    Ukiangalia vizuri ratiba ya Benjamin Franklin unatoka na vitu vifuatavyo.

    Pili ni kusoma vitabu. Inaonekana wazi kuwa Benjamin Franklin alikuwa msomaji mzuri wa vitabu, kwenye ratiba yake kuna vipengele vya kusoma mara mbili. Na wewe jiwekee utaratibu wa kusoma kila Mara. Kiufupi kusoma kupe kipaumbele kwenye maisha yako sawa na ambavyo unatoa kipaumbele kwenye kula na kuoga.

    ANZA KWA KUSOMA KITABU HIKI CHA BURE

    Tatu kufanya kazi kwa bidii. Hiki Ni kitu kingine muhimu kwenye ratiba ya Franklin. Jamaa anaonekana alikuwa anathamini kazi kazi kwelikweli na alikuwa anafanya kazi kwa bidii. Na hiki linaweza kuthibitishwa kupitia nukuu zake pia;

    Kama uko huru kufanya kazi, basi fanya kazi kwa bidii na kamilisha majukumu ya muhimu.

    kila mtu anaweza kuwa na utajiri, afya njema na busara kupitia kufanya kazi kwa bidii, kujituma na nidhamu

    Benjamin Franklin

    Nne kujitathimini. Kila siku jioni alikuwa anajiuliza ni kitu gani kizuri nimeweza kufanya ndani ya siku ya leo chenye manufaa kwa watu wengine.

    Wewe pia unapaswa kuwa na utaratibu kama huu. Ikifika jioni jiulize ni kitu gani kizuri nimefanya leo? Ni mchango gani nimeweza kuleta kwa jamii yako. Ukigundua kwamba hakuna kitu cha maana umefanya usilale kwanza. Amka walau ufanye kitu kimoja tu kwa siku hiyo.

    Tano, chakula na ulaji. Hiki ni kitu kingine ambacho kinaonekana kilikuwa kinafuatiliwa kwa ukaribu sana na Benjamin Franklin.


    Watalaam wanashauri kuhakikisha kuwa walau upate kifungua kinywa hata kama hutapata mlo wa mchana.

    Na ushauri mwingine maarufu ni ule unaosema;

    Pata kifungua kinywa kama mfalme, chakula cha mchana kama mwana wa mfalme na chakula cha jioni kama ombaomba.

    Hayo ndiyo Mambo muhimu ya kujifunza kwa leo kutoka kwa Benjamin Franklin. Naamimi umepata hata kitu kimoja cha kufanyia kazi.

    [mailerlite_form form_id=1]

  • TAARIFA: Masomo Na Uchambuzi Kuhusu Soko La Hisa Kwa Siku 30 Zijazo

    Leo rafiki yangu nina habari njema Sana. Unajua ni habari gani?

    Ewaaa! Ni kuhusu uwekezaji kwenye soko la hisa. Kwa siku 30 zijazo kuanzia tarehe tarehe 1 aprili nitafanya kimoja kati ya vifuatavyo.
    1. nitatoa uchambuzi Kuhusu mwenendo wa soko la hisa
    2. Nitatoa mafunzo kuhusu soko la hisa
    3. Nitajibu maswali yanayoulizwa kuhusu uwekezaji na soko la hisa.

    Kila siku jioni nitakuwa natuma somo fupi Ila lenye funzo kubwa kuhusu soko la hisa. Na masomo haya yatatolewa kwa njia ya barua Pepe tu.

    Hivyo, basi ili kujiunga na masomo haya fanya hivi: Jaza taarifa zako hapa chini ili uweze kuwa unapata mafunzo haya.

    hakikisha umejaza taarifa zako kwa usahihi

    Wakaribishe na wenzako wajiunge.

    Karibu
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

    NB. Nashauri pia kama bado hujapata kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE ukipate leo. Gharama yake ni elfu tano tu.

    Karibu.
    Tuma elfu 5 sasa kwenda 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

  • Kwa nini hufikii ndoto zako

    Umekuwa na ndoto kubwa Ila bado hazifanikiwi? Unajua kwa nini?

    Najua kwa asili sisi ni viumbe wenye ndoto kubwa. Ndio na hili naweza kuliona kwa watoto wadogo. Maana mtoto mdogo haogopi kusema waziwazi kuwa siku moja atakuwa daktari au kuwa siku moja atakuwa rubani. Mtoto akiona ndege anasema ni ya kwangu au ya baba yangu kwa sababu yeye kwa asili ni mtu AMBAYE ana ndoto kubwa. Anafahamu kuwa hakuna kitu chochote kile kinaweza kumzuia kufikia ndoto zake. Anajua kwamba anaweza kuwa anachotaka.

    Wewe pia najua una ndoto kubwa. Unaweza kuwa umezikatia tamaa, ila najua unazo. Si ndio? Walau ndoto ya kuwa fedha nyingi utakuwa nayo.

    Ila tu tofauti na watoto wadogo ambao wao wanatamka waziwazi kuwa wanataka kufikia ndoto fulani, wewe unaogopa kusema ndoto yako mbele ya watu.

    Kwani uongo? Wewe mara ya mwisho kusema mbele ya watu juu ya ndoto yako kubwa ni lini?

    Kama tu unaogopa kuwaambia watu kuwa una mpango wa kujiajiri na kutoka ajirani, unadhani utawaambia hizo ndoto nyingine?

    Kama tu unaogopa kuwaambia kuwa unataka kujiajiri baada ya chuo na hutaki kusikia kabisa habari ya ajira. Unadhani Sasa utadhubutu kuwaambia kuhusu hiyo ndoto nyingine?

    Halafu mimi, niache uchokozi! Kwa nini nakuchokoza hivyo lakini? Hahaha, Ila na wewe ujirekebishe bwana, unaogopa kusema hata ndoto zako! Unazidiwa na mwanao……

    Halafu unategemea uzifikie. Usipozifikia,unaanzaa kusema aliyekupa wewe ndiye kaninyima mimi. Hahaha!

    Sasa ebu tuendelee tuone mambo mengine muhimu yanayokwamisha watu na kuwafanya washindwe kufikia ndoto zao na hasa yanayokukwamisha wewe.

    Kutokuwa na utaratibu wa kujikumbusha ndoto zako kubwa mara kwa Mara. Bilionea Richard Branson aliwahi kunukuliwa  akisema, mabilionea ni watu wanaojikumbusha ndoto zao mara nyingi kwa siku.
    Huku watu wa kawaida wakiwa hata hawajikunbushi kuhusu ndoto zao.

    Wewe Leo ulipoamka asubuhi umejikunbusha ndoto zako kubwa. Au ndio umefungua Instagram.

    Huwa kuna kichekesho kuwa mtu anaamka asubuhi. AKIWA HAJAJUA HATA KAMA ANA MIGUU YAKE, ILA TAYARI YUPO FACEBOOK NA INSTAGRAM.

    Sasa sijui huyu mtu wa aina hii ni wewe? Halafu unataka ufikie ndoto kubwa? Rafiki yangu EBU FIKIRI TENA.

    KINGINE kinachokuzuia kufikia ndoto zako Ni kukata tamaa mapema.
    Unapoanza kufanyia kazi ndoto zako, unapaswa kujitoa haswa kufanyia kazi ndoto zako. Muda mwingine matokeo unayotaka hayatokei haraka. Yanachukua muda. Ukikata tamaa mapema hivyo utashindwa kufikia ndoto zako zote.

    Hiki kitu kinaweza kukufanya ufanye Mambo meengi Ila mwisho wa siku matokeo yawe ni SIFURI. Kuna wazee wetu unakuta wameupiga mwingi ila hawakupiga hatua kubwa kimaisha. Utakuta mzee anakwambia niliwahi kufanya kazi fulani, nikafanya na kazi fulani, nikaenda eneo fulani n.k.

    Nisikilize mimi: suala siyo kuupiga mwingi. Suala ni je, unaupiga mwingi kwenye kitu gani? Ukiupiga mwingi kwenye kila kitu utajikuta hufiki sehemu yoyote maishani mwako. Ila ukiupiga mwingi kwenye ndoto yako kwa muda mrefu. Kutoboa lazima tu!

    Looo! Kumbe napaswa kuendelea na pointi nyingine halafu mimi nimekazana kuandika kuupiga mwingi. Kama vile kuupiga mwingi Ni pointi ya msingi kwenye makala ya leo.

    Halafu mimi…..

    Umeanzia juu kwenye ndoto yako
    Umewahi kuona hili. Unakuwa na ndoto kubwa kiasi kwamba unaanzia juu sana. Kuanzia juu siyo kitu kibaya. Ila Sasa tatizo ni pale ambapo unakutana na changamoto ambazo wewe mwenyewe unashindwa kuzihimili.

    Muda mwingine ni vizuri kuanzia kidogo, kisha ukaendelea kukua. ila hata ukigundua kwamba ulianzia juu na sasa mambo yamekuwa makubwa, unaweza kuamua kushuka chini kidogo ili uweze

    Mambo mengine yanayokukwamisha wewe kufikia ndoto zako nimewahi kuyaeleza kwenye video hii fupi kwenye channel yangu ya youtube. naomba uiangalie pia maana ina vitu vikubwa na vya msingi sana. Uisahau kuSUBSCRIBE kwenye channel yangu.

    JIUNGE NA MTANDAO HUU

    * indicates required Email Address * First Name Last Name Phone Number

  • Kinachowatofautisha Wanaofikia Ndoto Zao Na Ambao Hawazifikii

    Kitu kimoja kikubwa ambacho kinawatofautisha wanaofikia ndoto zao na ambao hawazifikii ni vitendo.

    Wanaofikia ndoto kubwa ni watu wa vitendo. Siyo watu wa kukaa mtandaoni na kuanza kuzungumzia ndoto zao.

    Bali vitendo vyao ndivyo vinaongea.

    Wewe pia kama unataka kufikia ndoto zako. Tenda zaidi ya unavyoongea.

    Hivyo tu. Anza leo.

  • Ulipata kitabu cha bure?

    Rafiki yangu kwa siku Sasa nimekuwa natoa kitabu cha bure. Itasikitisha sana endapo hutachangamkia hii ofa na kuchukua hiki kitabu.

    Yaani, wewe ushindwe kupata kitabu cha kununua. Ushindwe hata kupata cha bure. Kweli?

    Ebu chukua hatua Sasa hivi….

    Kipate hapa

X