Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Mwandishi ni mwandishi kwa sababu anaandika. Kama Huandiki nina haya ya kusema na wewe

    Mwandishi ni mwandishi kwa sababu anaandika. Kama huandiki, wewe siyo Mwandishi.

    Kwa hiyo, nataka na wewe uanze kuitwa mwandishi tena kuanzia leo, na utaweza hilo kwa kuanza kuandika.


    Kitabu kitakachokusaidia kufanikisha lengo lako ni kitabu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU.

    Gharama ya kitabu hiki ni 20,000/- tu.

    Lipia kwa 0684408755 sasa upate nakala yako.

     

  • Watu wa Kawaida Vs Matajiri

  • KITABU: NGUVU YA KUWEKA MALENGO

    Kitabu cha NGUVU YA KUWEKA MALENGO kinaeleza dhana muhimu unayoihitaji kwa ajili yakufanikisha jambo lolote lile. Ukiona mtu kafanikisha jambo lolote lile kubwa, ujue kwamba nyuma ya lile jambo kulikuwa na malengo ambayo mtu huyo aliweka na akayafanyia kazi.

    Usipokuwa na malengo, ujue kwamba utazunguka huku na kule ila utashindwa kufanikisha jambo lolote lile la maana.

    Kwa kulifahamu hili hapa, nimeamua kukuandalia kitabu. Cha NGUVU YA KUWEKA MALENGO.

    Kwenye kitabu hiki
    Utajifunza jinsi ya kuweka malengo
    Aina ya malengo ambayo watu waliofanikiwa huweka na malengo ambayo wewe unapaswa kuweka
    Hatua za kufuata ili kufanikisha kila lengo unaloweka
    Utavijua vikwanzo vinavyozuia watu kufanikisha malengo yao na ni kwa namna gani unaweza kuvivuka kuhakikisha kwamba umefanikisha malengo yako.

    Utaona mbinu sahihi za kukukutanisha na watu sahihi wa kukusaidia wewe kufanikisha malengo yako.

    Utaona to do list na namna ambavyo unaweza kuitumia to do list kufanya makubwa zaidi
    Looh, kitabu kimeshiba sana, aisee…

    Wacha sasa tufungue kurasa za kitabu hiki na tuanze kuona sura moja baada ya nyingine.

  • The Law Of Attraction Kitabu Kilichoandikwa na Simon Gray

    UTANGULIZI
    1. Mwandishi wakitabu hiki anatujuza kwamba maisha tunao ni nishati yani kila tofali(seli ) mwilini ni nishati kutokana na fomula ya Albert Einstein:
    E=MC2 E= Nishati, M= mwili C = kasi ya mwanga

    Kwa hivyo basi, tunao uwezo mkubwa hapa duniani kiasi kwamba huwa tunazo nguvu zakufanya chochote kile tutachodhamiria kufanya, ubunifu, kuyafanya makubwa yoyote tutakapowaza ili kuipanua na kuigeuza dunia kwa mafanikio makubwa kwa makusudi yetu binadamu.

    2. Matokeo makubwa huwa yaweza kufanyika pale tutageuza fikra zetu kiakili na mwisho wa siku maisha yetu vile itakuwa nzuri mno.

    3. Mhimu zaidi kwanza tunapaswa kuwa na mawazo na mipango mikubwa ya picha au ramani ya maono tunao ya kile tunachopenda au tunachotaragia kutokea kwa uhalisia hapa duniani na kukifanyia kazi.

    4. Ramani hii hapa ya maono yako ya siku za mbeleni, huwa itakutia hamasa kubwa ya kujishangilia , na kuwa msukumo wako wa kufanya kile unachotaka kutokea bila kuacha na maro zote kuwa makini bila kutoka kwenye mstari.

    5. Mwandishi huyu anachosisitiza kwa nguvu sana ni kuyafanya malengo yako kwanzia na lengo moja likamilishe kisha fanya lingine ukitumia upendo, uvumilivu na unyenyekevu wako wote wakati unapotenda kazi yako kuhusu lengo husika.

    Aidha anatukumbusha kwamba dunia nzima inakusubiri na kukusikiliza mpaka pale utayatimiza maono yako!
    Yupo tayari?

    Mwandishi Dr Busingye Warugaba Amos

    Mkurugenzi mku wa WARUGABA AMOS MEDICAL CENTER

    mawasiliano kwa:

    Simu: 256772367793/ 256708470471
    Barua pepe: amosbusingye05@gmail.com
    Tovuti: https://warugabamedicalcenter.com




  • Kanuni ya miezi sita kwenye biashara

    Kuna mambo 55 ya kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara, mambo haya yote yameelezwa kwenye hiki kitabu. Kupata nakala yako, wasiliana na +255 684 408 755
    Hakikisha unajipatia nakala ya kitabu hiki. Tumia namba ya simu +255 684 408 755

    Kuna kanuni ya miezi sita kwenye biashara ambayo wafanyabiashara wengi hawaifahamu.

    Ni kanuni muhimu ambayo kama mfanyabiashara unapaswa kuifahamu. Kutoifahamu kanuni hii kutakuponza sana Kanuni hii inasema kwamba, ukianza kufanya biashara, ndani ya miezi sita ya kuanza biashara kuna watu wengine wataanzisha biashara kama hiyo.

    HII kanuni inafahamika kama kanuni ya copy cat. ikimaanisha kwamba baada ya miezi sita kuna watu watakuwa wanafnaya biashara kama ya kwako uliyoanza kufanya baada ya miezi sita.

    Kuna watu watazalisha bidhaa kama hizo miezi sita baada ya wewe kuwa umeanza kufanya uzalishaji.

    Kwa hiyo hakuna kitu unachofanya kwenye biashara yako ambacho kipo salama ambacho watu hawatakuja kukifanya Sasa unafanyaje kujitofautisha Kitabu hicho hapo👆🏿👆🏿 Ni 20,000/- tu Lipia kwa 0684408755 sasa Nakala laini ni 10,000/- Namba ya malipo ni 0684408755 JINA ni GODIUS RWEYONGEZA

  • Utajiri haudaiwi mahakamani, ila ukifanya hivi utaupata

    Rafiki yangu mpendwa salaam, utajiri ni haki yako ya msingi ambayo unapaswa kupata. Tofauti kubwa ya haki hii na nyingine ni kwamba unapaswa kuipambania.

    Wakati haki nyingine zinadaiwa mahakamani, utajiri haudaiwi mahakamani. Utajiri unakuja kwa kutokwa na jasho, damu na machozi.

  • Malengo yako Yasome Kila Siku

  • Semina ya Juni 2024

  • Umewahi kujiuliza kuwa unaweza kupata wapi muda wa Kuandika Kitabu Chako?

    Umewahi kujiuliza kuwa unaweza kupata wapi muda wa Kuandika Kitabu Chako? Jibu ni rahisi sana. Na jibu Hilo lipo kwenye SoMo la leo. kupata kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU, wasiliana na 0684408755 Jina ni GODIUS RWEYONGEZA karibu sana

  • Dhana ya jeshi la mtu mmoja, je ni dhana halisi au tunahitaji kufikiri nje ya boksi?

    Moja ya dhana ambazo zimekuwepo miongoni mwa watu wengi ni dhana ya JESHI LA MTU MMOJA, kuna watu wamekuwa wanaamini kwamba kwenye shughuli zao ambazo wanafanya basi wao wanasimama kama jeshi la mtu mmoja.

    Wakimaanisha kuwa wao ndiyo kila kitu kwenye shughuli au jambo fulani ambalo wanafanya, sasa ambacho leo hii ningependa tujadili hapa ni kwamba je, dhana ya jeshi la mtu mmoja ni dhana halisi au tunahitaji kufikiri kwa namna nyingine?

    Tukitafakari kidogo kuhusiana na dhana hii ya jeshi la mtu mmoja, tuanze labda kwa kujiuliza. Jeshi ni kitu gani. Kujua hili nimezalimika kuangalia kwenye kamusi ya kiswahili sanifu, ambayo inasema kwamba Jeshi ni jumla ya askari ambao wameajiriwa kwa ajili ya kuilinda nchi. Maana ya pili ya neno Jeshi kutoka kwenye kamusi hii hii inasema kwamba jeshi ni jumla ya watu.

    Tukiangalia maana hizi zote mbili tunagundua mambo yafuatayo.

    Kwanza tunagundua kwamba tunapoongelea JESHI. Tayari tunakuwa hatuongelei mtu mmoja bali kikundi cha watu (jumla ya watu).

    Lakini pia ukifuatilia zaidi kwenye maana hiyo, utagundua kwamba jeshi, siyo tu jumla ya watu, bali watu ambao wanafanya kazi kwa ushirikiano ili kufanikisha lengo au kusudi fulani. Hilo ndilo jeshi.

    Sasa mpaka hapo unafikiri Dhana ya jeshi la mtu mmoja bado ni dhana halisi?

    Tukija kwenye biashara kwa mfano. Kwenye biashara kuna vitu vingi ambavyo vinahitajika kufanyika. Unahitaji ufanye masoko, unapaswa kuuza, unapaswa kutengeneza bidhaa na mengine mengi…

    Inawezekana kwenye biashara yako uko peke yako, ila kiuhalisia siyo kwamba wewe ni jeshi la mtu mmoja. Bado kuna watu ambao unashirikiana nao, wasambazaji, watu wa usafiri, wateja n.k

    Kwa hawa watu wote ambao unashirikiana nao, bado huwezi tu kusema kwamba wewe ni jeshi la mtu mmoja.

    Kama wewe ungekuwa ni jeshi la mtu mmoja maana yake ni kwamba ungekuwa unafanya kila kitu mwenyewe bila kuhitaji mtu yeyote, na hata wateja ambao wananunua kwako hawapaswi kuwa wanwanunua kwako, badala yake unapaswa wewe kuwa ndiyo mteja wako kwenye biashara yako, ili tuseme kweli wewe NDIYE JESHI LA MTU MMOJA.

    Ili biashara yako ikue, inahitaji watu. tena watu sahihi, kama hauna hawa watu utaishii tu kufanya biashara kama ambavyo watu wengine huwa wanafanya. Kwa namna ya ukawaida.

    Hata kwenye maisha ya kawaida ya kila siku, dhana ya jeshi la mtu mmoja haipo. Haipo kwa sababu wewe haufanyi kila kitu mwenyewe. Dhana ya JESHI LA MTU MMOJA ingekuwa halisi kwenye maisha ya kawaida maana yake ungekuwa unapika chakula chako mwenyewe kwa sufuria ambazo umezitengeneza mwenyewe, unajisafirisha mwenyewe kwa gari ambayo umeitengeneza mwenyewe, unalima chakula chako mwenyewe kwa jembe na trekta ambayo umetengeneza, unapanda mbegu zako mwenyewe ambazo umezitengeneza mwenyewe, unaangalia runinga ambayo umeitengeneza mwenyewe na vipindi ambavyo umeviandaa mwenyewe na kuendelea na kuendelea.

    Kiuhalisia ni kwamba dhana ya jeshi la mtu mmoja kwenye maisha haipo. Maisha ni kushirikiana na watu.

    Upo kwa sababu fulani yupo, na yeye yupo kwa sababu wewe upo.

    Ninavyoandika makala hii nimemkumbuka Harmonize maarufu kama Konde Boy ambaye anajiita jeshi.

    Akimaanisha JESHI LA MTU MMOJA.

    Kwa maoni yako unadhani Harmonize ni jeshi la mtu mmoja?

    Siyo kweli kwamba harmonize ni Jeshi la mmoja. Harmonize ana meneja wake. Harmonize ana producer. Harmonize ana watu wa video. Harmonize anafanya kazi na watu wa redio na vyombo mbalimbali vya habari n.k

    Hajifanyii interview mwenyewe.

    Hasikilizi muziki wake mwenyewe baada ya kuutoa.

    Haendi kwenye show kujitumbuiza mwenyewe…..

    Ni kwa sababu kuna watu.

    Kumbe dhana ya jeshi la mtu mmoja kwenye maisha ya kila siku, haifanyi kazi.

    Kijana mmoja alimwambia baba yake kuwa baada ya hapa ninaenda kuwa naishi mwenyewe na nitakuwa sihitaji msaada wa mtu yeyote.

    Hili jambo lilionekana kuvuta umakini wa baba yake.

    Hivyo alitaka kuhoji na kuuliza zaidi kuwa je, ataanyaje?

    Mtoto aliendelea kujieleza kwa kusema kwamba nitatatoka hapa, nitaita TEKSI ambayo itanipeleka uwanja wa ndege.

    “Enhee” baba yake alionekana kumakinika.

    Mtoto aliendekea kusema kwamba, nikifika uwanja wa ndege nitapanda ndege na kuelekea sehemu ambapo nitaanza kuishi maisha yangu.

    Baba yake alivuta pumzi kidogo kisha akamwambia je, kwa nini unawatumia watu kufanikisha mambo yako. Kwa nini usifanye kila kitu mwenyewe. kwa nini wewe mwenyewe usijipeleke uwanja wa ndege. Kwa nini wewe mwenyewe usiwe rubani wako mwenyewe?

    Mtoto alibisha kidogo na kusema.

    Lakini si nitakuwa nawalipa?

    Ndipo baba yake alimwambia “kuwalipa watu hakukufanyi wewe kuwa jeshi la mtu mmoja”

    Ukweli ni kuwa, kwenye maisha ya kawaida ya kila siku, naam, kwenye maisha ya kila siku, hakuna jeshi la mtu mmoja. Maana unamkuna mmoja na yeye anakukuna, tunakunana.

    Makala hii imeandikwa nami rafiki yako wa ukweli. Godius Rweyongeza

    Hakikisha umepata vitabu vyangu ili kujifunza zaidi. Kupata nakala za vitabu vyangu ni rahisi sana. Wasiliana nami kwa 0684 408 755 sasa. Namba hiyo ipo whatsap na inapatikana kwa meseji na simu za kawaida.

     

X